Naomi Simulizi |+1 205 767 8163 |naomisimulizi@gmail.com Nilipotea! - Sehemu ya 2. - Naomi Simulizi

Nilipotea! - Sehemu ya 2.

 

U
likuwa ni mzozo wa muda mrefu sana. Bado Tunda alikuwa amesimama pale pale katikati ya sebule, akisikiliza tu. Mwishowe aliitwa dada wa kazi akamchukua Tunda kwenda naye jikoni kula na kwenda kulala.

Maisha ya Tunda nyumbani kwa baba mzazi, Mama wa Kambo.
Maisha yalikuwa magumu sana mle ndani. Tunda alinyanyaswa kupita kiasi. Kwanza alikuja kwenye familia ile, ndoa yenyewe ikiwa haina amani. Baba yake alikuwa mkimya sana na alionekana na yeye anamambo yake yanayoendelea kwenye maisha yake, hasa kazini. Busy. Akitoka asubuhi ni mpaka usiku, na bado alikuwa akisafiri sana kikazi. Kipindi cha bunge ndio ilikuwa kabisa. Anapotea kabisa nyumbani kwa kuwa yeye ndio alikuwa akiandaa bajeti ya wizara. Basi atakuwepo Dodoma kwa siku nyingi tu.

Hata hivyo, mkewe ndiye aliyeonekana na kauli pale nyumbani na ndiye aliyekuwa akiendesha mambo. Alikuwa mbabe, mkali hata kwa mumewe. Msichana wa kazi mwenyewe alikuwa akimuogopa sana. Japokuwa alishaishi nao hapo miezi kadhaa, lakini alimwambia Tunda, bado hajamzoea mama Chale na aliambiwa na majirani, hakuna msichana wa kazi aliyewahi kufikisha mwaka kwenye hiyo nyumba. Ni mkali, na hana jema. Haridhiki kwa chochote anachofanyiwa mle ndani. Lazima akosoe na alimwambia pia ana mkono mwepesi wakupiga. Hata yeye alikuwa akimpiga vibao mara kwa mara kila anapokosea jambo. Ndio Tunda sasa akaishia kwenye mikono ya huyo mama, bila uwepo wa baba yake mle ndani.

 Alikuwa akipigwa kama ngoma. Hawakupishana sana na Chale mdogo wake, lakini kila kosa alilotenda Chale, alilaumiwa yeye na kuathibiwa. Hakuwa akipewa chakula chakutosha. Msichana wa kazi alikuwa akishapika, anamwita mama Chale, yeye ndio anawapakulia kwenye sahani zao, basi. Huruhusiwi kuongeza tena, mpaka mlo mwingine atakao wapakulia.

Tunda alikumbuka chakula cha kawaida sana alichokuwa akipewa na bibi yake, na kumringia kila wakati mpaka ambembeleze sana, ndio ale. Alitamani kurudi kwa bibi yake, lakini akakumbuka alivyotakiwa aondoke, na mama yake alishamwambia hana pakwenda, pale ndio mwisho. Akaona awe mpole aendelee kujifunza tu mpaka aone mwisho wake. Kazi nazo zilikuwa nyingi zaidi ya umri wake. Hapakuwa na tofauti kati yake na huyo msichana wa kazi. Alitumikishwa kama punda, na kipigo kilikuwa kikimfuata mgongoni kila wakati.

Majirani walijaribu kumtetea kwa kumkumbusha mama Chale umri wake, lakini haikusaidia. Mmoja wa majirani alijaribu kumvizia baba yake Tunda akiwa anatoka kazini mida hiyo ya usiku, na kumueleza mateso anayopata mwanae, lakini baba huyo hakujua chakufanya. Kwani hakuwa na muda wakuwepo nyumbani na majukumu ya kazi yalimuhitaji sana.

**********************

Uliisha mwaka wa kwanza, Tunda akamaliza darasa la tatu kwa shida sana. Akaingia darasa la nne. Mambo ni yale yale. Kila alivyojitahidi kufanya kama mama huyo alivyotaka, alizidi kukosea na kupigwa zaidi. Kazi nyingi akamudu kwa umri huo wa miaka 10 akikaribia 11. Tunda alikuwa akichapa kazi bila yakutumwa. Lakini pia bado yule mama hakuridhika. Hata msichana wa kazi alikuwa akimuhurumia kwa kipigo cha mara kwa mara alichokuwa akikipata kila wakati tena bila kosa au kwa makosa ya Chale aliyokuwa akimsingizia Tunda.

**********************
Majirani walipoona vinazidi, ikabisi siku hiyo kumvizia tena baba yake akiwa anatoka kazini, ili angalau wamwambie kinachoendelea kwa kina ndani ya nyumba. “Hivi hata unajua kama alimpiga mpaka akamvunja mkono? Alikaa huyo mtoto siku tatu humo ndani bila hata ya kwenda shule. Msichana wako wa kazi ndio kaja kutuambia mkono wa mwanao unazidi kuvimba, ndio Mama Abuu, akaenda kumchukua na kumpeleka hospitalini wakati mkeo ameenda kwenye biashara zake.” Waliongeza majirani hao na kumstua baba Chale zaidi. Kwani hakuwa akionana na Tunda mara kwa mara. Alikuwa akiondoka akiwa amelala na kurudi akiwa amelala. Na yule mama alifanya juhudi za makusudi wasiwe wanaonana.

Akaongeza kasi mpaka nyumbani. Akaingia anahema. “Tunda yuko wapi?” “Ndio salamu hiyo?” Alijibu mkewe. “Au binadamu humu ndani ni Tunda tu?” “Naomba tusianze ugomvi mama Chale. Nimemuulizia Tunda tu. Ubaya uko wapi?” “Basi ndio ukamchukue ukalale naye huko chumbani, na akupikie na kukufulia huyohuyo Tunda.” Mama Chale akaondoka.

Kesho yake asubuhi baba yake Tunda aliamua kuchelewa kuondoka ili angalau aonane na mwanae. Alikaa sebleni hapo bila hata kupewa chai kwani mkewe alikuwa amenuna tokea usiku uliopita. Alilala akiwa amenuna na aliamka akiwa na kisirani sana, lakini mumewe hakuongea chochote. Alikaa pale mpaka Tunda alipoamka akiwa na POP mkononi.

Alishtuka sana. “Mkono wa kulia!? Huyu mtoto si ndio anatarajia kufanya mitihani ya darasa la nne! Atafanyaje na mkono upo kwenye muhogo? Shule anakwenda kweli?” “Sasa hapa, unamuuliza nani?” “Kwani alifanya nini, mpaka ukampiga kiasi chakumvunja mkono!?” “Aliyekwambia nimempiga nani? Ndivyo alivyokwambia huyo mwanao? Eti wewe? Umeanza uongo? Si ulianguka?” “Acha dhambi Mama Chale! Mungu atakulipa hapa hapa duniani. Huyu mtoto anakosa gani kumpiga kwa kiasi chakumvunja mkono!?” “Unaniletea maneno ya uzushi humu ndani!? Uliona wakati nampiga? Sasa naona hii ndoa umeichoka. Naondoka na mwanangu, ili muendelee kuishi na huyo anayekuletea maneno ya uchonganishi humu ndani.” Mama Chale aliingia ndani kwa hasira, huku akitoa maelekezo kwa msichana wa kazi wajiandae, asimvalishe nguo za shule Chale, amvalishe nguo za kawaida tu, kwani wanaondoka pale ndani, muda ule ule.

Mzee alipoona ndoa yake ipo matatani aliamua kutuliza jazba na kuingia chumbani kumbembeleza mkewe. Baada ya utulivu wa muda mrefu huko chumbani, walitoka wote wakiwa wanacheka. Mzee akaenda kazini na kumuacha tena Tunda mikononi mwa mkewe huyo aliyekuwa mkatili wa kupita kiasi.

Baba Tunda hakutaka tena kusikiliza maneno ya majirani, ila alimwita Tunda kwa siri na kumsihi sana awe mtiifu ili waishi kwa amani mle ndani. Tunda alikuwa amebakisha majuma kadhaa kuanza mitihani yake ya darasa la nne. Baba yake alimpeleka hospitalini kuangalia kama anaweza kutolewa ile POP ili afanye mtihani ya kitaifa na wenzake, lakini aliambiwa muda bado, kwani ndio ana siku 8 tu tokea afungwe huo mkono, na kwa uvunjikaji ule, mifupa haiwezi ikawa imeshajiunga.
Alimshauri mtoto wake awe anakwenda shule vile vile kuliko kuendelea kukaa tu nyumbani. Akamwambia watajua kitu chakufanya mbele ya safari, siku ya mitihani ikifika. Tunda alianza kwenda shule tena na Chale ambaye alikuwa na tabia ya udokozi kupita kiasi na muongo wakupitiliza.

Kilichomtoa Tunda kwa baba mzazi.
Siku hiyo Chale alizidisha. Wakati anaenda shule, akaingia kwenye mkoba wa mama yake akachomoa elfu kumi akaenda nayo shuleni. Hakuna aliyekuwa amemuona wakati amechukua. Waliporudi kutoka shule, walimkuta mama yao akiwasubiri sebleni na mwiko wakusongea ugali. “Leo mtanieleza ni nani amechukua pesa ya watu ya kibati kwenye pochi yangu. Tena mwenye zamu yake anakuja kupitia pesa yake jioni hii. Anataka pesa yake yote.” Akaanza hivyo“Njoo hapa Chale. Niambie mwanagu, ulimuona nani akichukua pesa kwenye pochi ya mama?” Bila kupepesa macho, “Tunda.”  Chale akamtaja. “Ulimuona akichukua eeh?” “Ndiyo mama. Halafu akaenda nayo shule.” Tunda alivutwa na kaunza kuchapwa huku akilazimishwa arudishe hata chenchi.

Tunda hakuwa na jinsi yakujitetea, hakuwa na hiyo pesa na wala hakumuona aliyechukua. Unaleta jeuri!? Leo utanitambua.” Alimvuta mpaka nje nakuendelea kumpiga kama anaua nyoka, kwa hasira zote. Alipigwa kila mahali mpaka alipozimia. Yule mama akamuacha hapo hapo. “Si unajidai umezimia wewe, sasa utalala hapo hapo. Na nisikuone unanyanyuka.” Akaingia ndani kwa hasira, akafunga mlango na kutoa onyo kali sana, mtu asimfungulie mlango aachwe huko huko nje.

Baada ya muda mfupi tu yule mama aliyekuwa akifuata pesa yake ya mchezo wa kibati naye akaingia. Alielezewa ubaya wote wa Tunda, na kuombwa msamaha wa kupewa pungufu ya pesa. “Baba yake akirudi kutoka safari, atailipa hiyo pesa. Nitakupitishia shoga yangu.” “Wala usijali Mama Chale. Nakujua wewe sio tapeli.” Walicheka kidogo pale, kisha akaaga. 

Alipotoka tu pale ndani, msichana wa kazi alimkimbilia na kumkabidhi kikaratasi kwa siri. “Kifiche, tafadhali. Kampe Mama Abuu.”  Yule dada wa kazi alinong’ona, kisha akarudi ndani haraka na kufunga mlango. Yule mama alishangaa kidogo, lakini akaamua kwenda kwa Mama Abuu amfikishie ujumbe wake kama alivyoombwa.

“Mbona wanijia mimi, wakati pesa yako anayo Mama Chale?” Mama Abuu alimpokea kwa maneno. “Hata! Kilichonileta wala si pesa. Nina ujumbe wako.”  Alimkabidhi kile kikaratasi, pale pale akakifungua na kukisoma. ‘Mama Abuu. Tunda amepigwa mpaka akazimia. Ameachwa hapo nje, mama amesema mtu asimfungulie mlango. Nakuomba sana, uje kwa siri hapo nyuma umwangalie. Alikuwa anatoka damu puani.’ Mama Abuu bila yakupoteza muda akatoka akikimbia.

“Wewe vipi?” Akarudi na kumkamkabidhi tena kile kikaratasi, “Mpe baba Abuu hapo ndani. Atajua chakufanya.” Mama Abuu alijibu na kukimbilia nyumbani kwa Mama Chale. Kama alivyoonywa. Alizunguka uwani. Wakati anatoka akiwa amembeba Tunda, alimuona mumewe amesogeza gari. Wakampeleka Tunda hospitalini.
Baba Abuu alirudi nyumbani kwa Mama Chale. “Mumeo yupo?” “Kasafiri. Kwema?” Akauliza mama Chale. “Tunda amelazwa.” “Tunda wa humu ndani!?” “Ndiyo.” “Tunda yuko huko nyuma anacheza.” “Acha kunidanganya Mama Chale. Kila mtu hapa mtaani anajua unyama unaoufanya kwa Tunda. Mke wangu amemuokota huyo mtoto akiwa hana fahamu, tukamkimbiza hospitalini.” “Sasa kama unajua namfanyia unyama, unachotaka hapa nini? Nishakwambia baba yake hayupo.” Baba Abuu alitoka bila kutaka kuzozana zaidi. 

Kesho yake Tunda aliamka akiwa na nafuu kiasi, lakini alikuwa amevimba kila mahali. Mama Abuu ndiye aliyelala naye hospitalini. Mumewe alirudi asubuhi hiyo kuleta kifungua kinywa kwa mkewe na Tunda. “Naomba simu niongee na bibi.” Tunda aliongea kwa shida akilia. “Kumbe una bibi yako?” “Ndiye aliyekuwa akinilea tokea mtoto. Aliniambia nishike namba yake kwa kichwa, nikiwa na shida yeyote nimpigie.” Tunda akawapa namba.

Mama Abuu na mumewe walimpigia simu yule bibi asubuhi ile ile na kumueleza ukatili wote anaopitia mjukuu wake mpaka kufikia hapo, akiwa hospitalini hatizamiki. Ilipofika jioni, yule bibi aliingia jijini. Baba Abuu alikwenda kumpokea kwenye kituo cha mabasi Ubungo na kumpeleka mpaka hospitalini. Aliumia sana kumuona Tunda kwenye hali ile.

Mateso ya kwa baba mzazi, yamrudisha tena, Tunda kijijini kwa bibi & babu yake.
Waliporuhusiwa tu, yule bibi alimchukua Tunda na kurudi naye tena kijijini bila hata kutaka kuzungumza na baba yake mzazi Tunda. Tunda alijawa makovu mengi sana na madonda juu. Alimchukia baba yake kuona yule mtoto alikuwa akiteswa na yeye yupo humo humo ndani ya nyumba! Makovu ya Tunda na madonda, vilimwashiria yule bibi kuwa ndio maisha aliyokuwa akiishi Tunda siku zote. Hakutaka hata kuiona sura ya yule baba. Aliondoka na mjukuu wake kimya kimya bila yakutaka hata ugomvi na mtu.

************************

Akiwa na hasira sana, alimpigia simu mume wake Manda, nakumwita pale kijijini. Na kweli bila kuchelewa siku inayofuata, Manda alifika pale na mumewe. Alishtuka sana kumkuta Tunda pale kijijini tena akiwa na PoP mkononi na madonda juu.  Bibi mtu alieleza mkasa mzima tokea Tunda anazaliwa mpaka kufikia siku hiyo. Alimueleza mumewe Manda, Collin, kwa tahadhari, bila kumuharibia mwanae Manda kwa mumewe.

Nia ilikuwa kwanza kumtambulisha Tunda kwa baba yake wa kambo na kuona kama anaweza kuwafanya wanandoa hao, angalau wawe wanatoa msaada wakueleweka wa kifedha ili kuweza kuwasaidia hapo kijijini wakiwa wanaishi na Tunda. 

Tunda alikuwa amewasimulia bibi yake na babu yake mengi, machungu aliyopitia huko mjini, na kumsihi bibi yake arudi kuishi nao hapo kijijini. Lakini kwa miaka hiyo miwili tokea Tunda anaondoka kijijini mpaka anarudi, uchumi ulikuwa umebadilika sana. Hata wale ndugu waliosema Tunda analemea pale nyumbani kwao na hawawezi kuwatunza wazazi wao vizuri, nakumtoa Tunda pale, ikawa kama ndio wameleta na laana pale. Maisha ya wazazi wao yakawa magumu zaidi, kila mmoja akawa analia shida. Kukumbuka nyumbani ikawa mmoja mmoja sana tena mpaka mama yao apige simu.

Na Manda nae tokea aondoke siku ile baada ya kugombana na kila mtu pale nyumbani kwao, na kumchukua Tunda ni kama alizira kabisa nyumbani kwao. Manda mbinafsi akarudi kwa wazi kabisa. Angalau ndugu zake walilalamikia ugumu wa maisha, lakini sio Manda. Wakati wengine wakilia njaa nchini, nyumbani kwa Manda kulikuwa na neema kubwa tu. Collin mfanyakazi wa kampuni ya kigeni, maisha yake yalikuwa yakiendelea kama kawaida. Safari za nje ya nchi zilikuwa kama kawaida. Lakini Manda hakujaliwa moyo wa kusaidia yeyote yule. Walimjua tokea mtoto na alikuwa ni tatizo la familia. Hakuwa akituma pesa hapo nyumbani, na ikitokea analazimishwa na ndugu zake kuchangia basi alituma nusu ya kiwango walichopangiana ndugu hao au alitoa sababu nyingi zakutoweza kutuma, na ahadi yakutuma wakati mwingine.

Sasa kwa kuwa mama yake alimjua, ndio maana akamtafuta mumewe aombe msaada wakutumiwa pesa kidogo angalau kila mwezi ili ziwasaidie na Tunda pale kijijini. Lakini chakushangaza, Collin, mume wa Manda hakushtuka hata kidogo, akashauri wamchukue Tunda warudi naye kwao. Kwa ahadi yakumlea bila shida. Aliwaacha wazazi wa Manda na Manda mwenyewe mdomo wazi. “Mtoto wa Manda ni wangu. Hatuwezi kumuacha Tunda hapa kijijini wakati shule nzuri zipo mjini. Haitakuwa sawa kwake mwenyewe Tunda. Kwanza nikimwangalia ni kama anatakiwa kurudishwa hospitalini kwa uchunguzi zaidi.” Hizo zikawa habari njema kwa kila mtu na zakujivunia kwa Manda, kasoro kwa Tunda.

***************************

Bado Tunda alitaka aendelee kuishi kwa bibi yake. Hakuona alichopungukiwa pale kijijini. Amani, furaha, kwanza alikuwa nyumbani. Hakuona uzuri wowote wa jiji la Dar. Hapakuwa na kitu cha ajabu kulinganisha na kijijini kwa bibi yake ambako alikuwa huru. Wakati mwingine Tunda alikuwa akilala na bibi na babu yake akifunikwa na kukumbatiwa usiku kucha. Hakuna aliyemkosoa kwa lolote hata rangi yake, isipokuwa huyo mwanamke aliyesikia sio kutambulishwa, nikusikia kuwa ni mama yake mzazi na ndiye anayetakiwa kwenda kuishi naye!

Kwa muda wote huo wa miaka miwili waliokuwa wametengana na mama yake, bado hakuwa amesahau hata kidogo ukatili aliomfanyia njiani wakati anamtoa hapo kijijini. Bado alikuwa na hofu naye. Utampa nini Tunda chakulinganisha na mapenzi aliyokuwa akipewa pale kijijini kwa bibi na babu yake? Hiyo shida na huo umuhimu wa kwenda kwenye shule nzuri mjini, ni upi kwa Tunda aliyekuwa amenyimwa nafasi yakulinganisha!

Alifika mjini akiwa anaongea Kipogolo, lugha aliyokuwa akizungumza tokea anapata ufahamu. Lugha aliyokuta watu wote wanao mzunguka pale kijijini na wanao kuja kutembea pale kwa bibi na babu yake wakizungumza. Hata kuelewa mwalimu alichokuwa akifundisha huko mjini, ilikuwa shida. Halafu akakutana na kila mtu huko mjini anazungumza kiswahili, hakuna anayejua kipogolo hata aombe maji ya kunywa.

Mbali na lugha, akaishia kwa mama Chale. Hakuwahi kupigwa maishani, mpaka alipokutana na huyo mama. Wakati mwingine alikuwa akifinywa sana muda mfupi kabla ya kwenda shule. Anaingia darasani na maumivu. Si maumivu ya mwili tu, hata nafsi ilisha jeruhiwa sana. Hakuna aliyejali ule mshtuko wa Tunda wakujua watu aliokuwa akiwapenda na kumdekeza sio wazazi wake, na yeye ni mzigo unaotakiwa kuondoka pale alipopaita nyumbani. Hakuna aliyejali ule mshtuko.

Tunda alitolewa darasa la pili la kijijini, milima ya Ulugulu, ndani kabisa, ambapo hata walimu walipotaka kuelewesha wanafunzi, walitumia lugha hiyo ya Kipogolo. Kuzungumza kiswahili hata kwa wageni wanaokuja kutembea majumbani kwao, walihesabu nikujidai. Tunda alikuwa akikizungumza kilugha kwa ufasaha na ndicho walichokuwa wakikiongea nyumbani na shuleni kila wakati.

Leo anafikishwa mjini kama mtuhumiwa, anaingizwa shule za kiswahili, tena na somo moja la kingereza! Ilikuwa ni bora aendelee kuishi kijijini kwa bibi na babu yake, kwenye viwanja vyake vya nyumbani. Hakuna wakumlazimisha kusoma, akitoka shule, michezo tu. Maswala yakusikia anarudishwa mjini kwenye nyumba nzuri, sijui shule nzuri, hizo hazikuwa habari njema kwa Tunda hata kidogo. Tunda hakuona shida ya nyumba ya bibi na babu yake. Tena alilala akiwa amekumbatiwa. Ukisema chakula kizuri, hakuona shida yeyote ya chakula alichokuwa akipikiwa na bibi yake. Tena alipewa kwa kubembelezwa. Sasa anafuata nini tena mjini!? Tunda alizidi kuwaza huku hofu ikizidi kumsumbua. Alihisi kabisa moyoni ni kama anatolewa sehemu salama sana, na kuhamishiwa matesoni tu. Lakini atafanya nini? Hakupewa nafasi hata yakusikilizwa na kutoa maoni yake. Safari ya mjini ikaanza.

Maisha ya Tunda, nyumbani kwa Mama Mzazi, baba wa Kambo.
Tunda alirudishwa mjini tena, lakini safari hii nyumbani alipoolewa mama yake mzazi na alipokelewa tofauti. Kwa mapenzi mazito ya baba wa kambo. Alirudishwa hospitalini. Akafanyiwa vipimo vyote na ule mkono ukapigwa tena x-ray. Kila ugonjwa kwenye mwili wa Tunda ulitafutiwa tiba na kuuguzwa nyumbani hapo, baba Tom, Collin akiwa mstari wa mbele kutoa ushirikiano. Alipona lakini alishachelewa kufanya mitihani ya darasa la nne na wenzake. Ilimbidi kurudia darasa. Lakini muda huo wakati wenzake wanamalizia mwaka, Tunda akabaki nyumbani akipumzika. Kula, kulala vizuri bila shule.

Kabla mwaka haujaisha, Collin au baba Tom, akaanza kutafuta nafasi ya shule ya Tunda kwenye shule hiyo hiyo aliyokuwa akisoma mtoto wao Tom, aliyekuwa ameanza darasa la kwanza, miaka 7 tu, ili Tunda aje arudie mwaka unaofuata darasa hilo la 4 ambapo angetakiwa kuwa darasa la 5. Mpaka Manda mwenyewe akashangaa moyo na juhudi za mumewe. Shule ya kimataifa, kwa garama zote hizo! Ilikuwa na mitala ya Uingereza. Kwamba mtoto akisoma vizuri, anaweza kwenda kusoma chuo nchi za Ulaya bila shida.

Collin alihangaika mpaka akapata nafasi ya Tunda shuleni hapo. Kwa jeuri Manda akatangaza zile habari nyumbani kwao akijua wazi na ndugu zake watasikia. Kuwa yale waliyotegemea mabaya kumpata kwa mume wake, wameaibika wao. Kuwa mumewe amempokea Tunda na anamsomesha shule za kimataifa ambazo hata wao hawawezi kupeleka huko watoto wao. Zikawa ni habari zakujivunia sana.

Lakini sio kwa Tunda. Tunda huyu hata lugha ya kiswahili kuielewa vizuri, ilimlazimu kujifunza kwa makofi na kufinywa kwa mama yake wa kambo. Wakati wote alikuwa akimlalamikia mumewe kuwa Tunda anaakili nzito. Na ndio maana vibao vya usoni, mgongoni vya mara kwa mara kwa Tunda vilikuwa haviishi kule kwa mama wa kambo. Lugha ilisumbua sana. Kila neno alilokuwa akiambiwa, ilimlazimu kufikiria sana na kutumia akili ili kuelewa na mara nyingi sababu ya hofu, hakuwa akipatia.

Leo unamwambia unampeleka shule ya wanaozungumza Kingereza kitupu! Halafu eti ndio akajifunze masomo ya sayansi, geografia, historia, sijui hesabu kwa lugha ya kingereza! Anaanzia wapi Tunda!? “Sasa sio uende huko ukanitie aibu. Unapoteza muda na pesa ya baba wa watu wakati baba yako alishindwa kukutunza. Umepata bahati hii, ukaitumie vizuri. Ukiniletea ujinga hapa kwa watu, nakutoa hayo macho yako kama ya paka na ninakurudisha kwa Mjaluo mwenzio ukiwa kipofu. Lione lilivyozubaa. Kama lijipaka jizi! Unanisikia lakini?” Huo ndio ulikuwa husia kwa Tunda kutoka kwa mama yake, siku chache kabla hajaanza hiyo shule.
***************************
Hakuna aliyekumbuka kuwa Tunda huyu ndiye Tunda yule yule aliyekuwa ameanza elimu yake kwenye shule za kawaida za kijijini, akahamishiwa kwa baba yake, akageuzwa mtumwa. Miaka miwili aliyokuwa akisoma akiwa kwa baba yake ilikuwa ni kama hakuwa akisoma sababu ya mateso makali na shuguli nyingi huku akipambana na lugha ya kiswahili. Hapo alipokuwa, bado alikuwa kwenye mshtuko. Kutoka kwenye malezi mazuri, akidekezwa kwa bibi yake aliyejua ni mama, sasa yupo mjini kwa mama yake.

Ila hapa kwa mama mzazi na baba wa kambo ni pazuri. Nyumba ya kisasa zaidi ya kote alikowahi kuishi. Maisha ya kisasa. Halafu kwa asili, Manda alikuwa msafi sana na mpenda vitu vizuri. Hiyo nyumba ilikuwa safi. Vitu vichache, lakini vya thamani sana, tena vimepangiliwa vizuri. Vyakula vingi, vizuri tena vilivyopikwa vizuri. Msichana wa kazi wa Manda, alikuwa akijua kupika sana. Ukila, lazima utoe shukurani ya kweli. Mavazi yao, kuanzia Manda na wanae, yalikuwa ya thamani. Kila Collin alipokuwa akisafiri, Manda hakuacha kumuagiza nguo kutoka nchi mbali mbali alizokuwa akienda, na hapo ndipo Tunda naye akaingia kwenye mavazi mazuri. Akabadilishwa muonekano, akawa Tunda aliyeoshwa na kuvalishwa vizuri.

Japokuwa mama alikuwa mkali sana, lakini baba wa kambo alionyesha upendo mkubwa sana, lakini bado lugha ni changamoto. Tunda anayeingizwa darasa la 4 kwenye shule ya kingereza, ni Tunda mwenye elimu ya darasa la pili, kwa lugha ya Kipogolo, aliyopata kijijini, kwenye kusafisha darasa na kufagia uwanja kwanza kabla masomo hayajaanza.
*************************
Shule hiyo yakuingia kukiwa kumeshasafishwa, mazingira mazuri, na kila kitu kisafi, ikawa ni shida kubwa sana kwa Tunda. Kwanza hakuwa na uwezo wowote darasani. Elimu yake ya kijijini, darasa la 2, kwa waingereza hao, ilikuwa hamna kitu. Zaidi yakujua kuumba herufi vizuri, hakuna alichojua au kuweza kuelewa darasani. Upole ukaongezeka zaidi.

Hapakuwa hata na mtu wakumuomba maji yakunywa kwa kiswahili pale shuleni. Kwanza watoto wengi pale ni wale watoto wanaotokea kwenye familia za kigeni waliokuja na wazazi wao nchini Tanzania kikazi. Walisoma na watoto wa mataifa mbali mbali. Nyumbani kwa mama yake, lugha inayozungumzwa kila wakati ni kiswahili kitupu na kila mtu busy na shuguli zake, ila Tom alizungumza lugha ya kingereza wakati wote na baba yake. Sasa Tunda anaanzia wapi! Lakini hakuna aliyelikumbuka hilo. Tunda akawa mkimya wakati wote. Si shuleni, si nyumbani. Huwezi kumkuta Tunda anazungumza.
*****************************
Maisha yake yalijaa mashaka, wasiwasi na machungu ya namna yake, ambayo hakuwa na mtu wakuzungumza naye. Msichana wa kazi wa mle ndani alikuwa muhuni wakupindukia. Kila wazazi hao wanapotoka kama hataingiza wanaume mle ndani, basi aliwafuata huko huko waliko. Akifanya mambo yake akimaliza, ndipo anarudi nyumbani. Anafanya kazi zake kwa haraka ili amalize, mama mwenye nyumba akirudi, akute kila kitu kipo sawa. Hakuwa na muda na Tunda hata kidogo isipokuwa maisha yake tu. Na alijua kupangilia mambo yake, usingekuta akiingia matatizoni na mama mwenye nyumba wake. Isipokuwa vitu vidogo vidogo tu kama mwanadamu.

Kwa upande wa mama yake naye ndio hakuwa na ukaribu kabisa na Tunda. Kwanza alimchukia sana, kitu kilichokuwa kikimshangaza hata Tunda mwenyewe. Alibeba chuki ya ajabu sana kwake. Kila neno lililokuwa likimtoka mdomoni mwake kwenda kwa Tunda lilikuwa ni kumkejeli rangi yake, ambayo hakuwahi kuona tatizo la rangi hiyo mpaka alipoanza kutusiwa na mama yake mzazi. Macho ndio kabisa. Asitokee akamtizama, na mama yake akamuona au macho yakagongana, basi ataambiwa macho yake ni kama ya paka. Na vitisho vingi kila wakati anapomgombesha, hasa kumtishia kumrudisha kwa baba yake mzazi, sio kijijini tena, kitu kilichomuogopesha zaidi Tunda. Na ndipo hapo na baba yake wa kambo alipogundua udhaifu huo, akatumia upweke na hofu ya Tunda vizuri sana.
Mwanzo wa Collin kwa Tunda.
Collin alishamsoma Tunda na mazingira yanayo mzunguka. Kwanza alishajua hakuna mtu mwenye muda naye kabisa. Sio mle ndani tu, ila kwenye maisha yake kwa ujumla. Alishajua hakuna anapotakiwa kuishi, pale kwake ndio amefika. Na mama yake alimuhakikishia kwa wazi kabisa, pale nyumbani kwake kwa wakati huo, ndio tumaini lake la mwisho, na Collin akamuona ameingiwa hofu ya kufukuzwa. Akawa na yeye ndio amepata fimbo kubwa yakumchapia Tunda.

 Lile tusi la mara kwa mara la macho ya Tunda kama paka, lilimfanya Collin kuanza kutizama hayo macho ya Tunda, na kumshangaza. Kwake hakuona hivyo, yalikuwa yakimvutia mpaka kuamsha hisia zake. Ni kweli alikuwa na macho yaliyozubaa, na muundo wa kama paka. Meupe sana, labda kutokana na weusi uliokolea mwilini mwake. Kwa Collin, aliyapenda sana macho ya Tunda. Wakati mwingine alikuwa akizubaishwa na hayo macho anayoyatukana mama yake.

Kwa kula vizuri, vaa vizuri, kadiri siku zilivyosogea mle ndani, ule mwili wa Tunda ulichukua sura ya tofauti. Kalikuwa kabinti kenye viungo vilivyoanza kukomaa. Kila kitu ungeweza kukiona kizuri mwilini mwake. Hata ule weusi, ukachukua namna yake. Tunda alikuwa mweusi haswa, lakini kuishi kwenye nyumba inayopulizwa upepo mzuri kila wakati, kula vizuri, hafanyi kazi, mafuta mazuri. Gari upepo msafi. Shuleni kwenyewe mazingira mazuri. Mpaka darasani ndani, ni hewa safi. Jua halimpigi Tunda, ungependa kuangalia rangi yake. Jicho la Collin, likaanza kumtizama kama kivutio, sio mtoto tena.

Collin akaanza kujisogeza yeye kwa Tunda na kujifanya ndio kimbilio na sehemu pekee salama ambayo Tunda anaweza kwenda. Kumjulia hali kila wakati, akitaka kujua anajisikiaje, amekula, yupo sawa, ikawa ni kawaida ya baba Tom kwa Tunda. Alikuwa mbabe kwa asili. Na alitaka wote wanaoishi mle ndani watambue yeye ndio mwenye nyumba. Alikuwa na kanuni zake alizokuwa amejiwekea kwenye maisha, na alitaka zifuatwe hivyo. Akisema mchana taa zizimwe, basi ifanyike hivyo. Akikuta taa za nje zinawaka mchana, hata Manda kama yupo nyumbani ataupata moto wake. Ataeleza jinsi inavyomgarimu hili na lile, tena kwa sauti ya ukali.

Msafi na nadhifu kama walio juana na Manda. Wakati wote utamkuta Collin au baba Tom ni msafi na ananukia vizuri na alitaka vitu viwe vipo sehemu yake kila wakati. Asikute vitu vinazagaa, popote. Mshika dini wa kweli. Kila jumapili lazima nyumba nzima muende kanisani tena bila kuchelewa.
Aliheshimika kwa nidhamu ya maisha aliyokuwa ikionekana kwa nje. Japokuwa alikuwa ni kijana aliyefanikiwa kimaisha, lakini alionekana ametulia. Hanywi pombe hata kugusa. Huwezi kukuta pombe nyumbani kwake. Hakuwahi kusikika au hata kuhisiwa kuwa na mwanamke wa nje. Hilo Manda hakuwahi kutilia shaka hata kidogo. Kwanza alivyo mkali na mtu wa maadili, ni ngumu msichana kumsogelea kirahisi. Mwanaume wa familia. Utamkuta nyumbani kwake muda mwingi wala si baa au mtaani. Alikuwa mume wa uhakika ila ukali na ubabe ndio lilikuwa tatizo ambalo hata Manda alikuwa akiliona na kumnyima raha. Alitaka kuheshimiwa na kutambulika kuwa yeye ndio anayewaweka vizuri mjini. Jambo dogo, atagomba kwa kila mtu, lakini sio kwa Tunda. Alionyesha upendeleo wa makusudi kwa Tunda akisema yeye ni mtoto, na mgeni mle ndani anatakiwa asaidiwe.
Zawadi za hapa na pale tena kwa wazi hata mbele ya Manda, hazikuisha kwa Tunda. Mara nyingi kama Collin anakwenda safari, Manda alikuwa akiagiza vitu vyake yeye na mtoto wao Tom tu. Lakini Collin alianza kuongeza zawadi  kwa Tunda pia. Na akileta, atasema hadharani, “Japokuwa mama yako hakunituma nikuletee hivi vitu, lakini mimi mwenyewe nimeona nikununulie.” Basi hapo Tunda atapewa zawadi zake nzuri tu na za thamani mbele ya watu bila hata kificho.

Wakati mwingine alitoka nao, Tunda na Tom tu, kwenda kuwanunulia icecream, wakati mwingine kuwapeleka kula chips kuku, juisi, popcon, chochote kile huku akiwa mwema sana kwa Tunda na kumtaka Tunda ajisikie vizuri na huru kwake. Yeye ndio akawa mtetezi wake. Kila mama yake anapokuwa akimfokea kwa jambo lolote lile, kama hatamkingia kifua kumtetea, basi atambembeleza na kumtuliza kwa upendo kama sio yeye Collin, mkorofi.

Tena alikuwa akijitangazia mamlaka kwa Tunda. Kuwa yeye ndio amekabidhiwa Tunda kutokea kijijini. Tunda ni jukumu lake na aliahidi kutokea kijijini kwa wazazi kuwa atamtunza vizuri. Wakati mwingine kwa utani akiwa yupo sawa na wakati mwingine kwa hasira akimwambia Manda kila akitaka amwache Tunda, kwa kusema atazungumza naye yeye mwenyewe endapo atamkuta akimgombesha. Basi hapo anaweza kumtoa Tunda tu akiaga kuwa anakwenda kuzungumza naye nje ya pale, kwa utulivu. Atatoka na Tunda, na kweli atakwenda kuzungumza naye kwa upendo sana akimbembeleza na kumtaka akiwa na shida yeyote ile, awe akimwambia yeye wala sio mama yake. Ukaribu ukaongezeka. Tunda naye akawa ameanza kumzoea yeye zaidi nakumuona kimbilio. Kidogo utulivu kwa Tunda ukaongezeka. Akimtoa nje pale nyumbani, atamfanya acheke, wazungumze hili au lile. Japokuwa Tunda hakuwa akiongea sana, basi watakaa tu sehemu tulivu. Kama atakuwa na Tom, atawapeleka sehemu kucheza. Atawaacha wao wawili wacheze, yeye atakaa sehemu akiwangalia wanacheza, akili zimezama kwa Tunda. Na pengine kucheza nao wote.

Siku ambazo hatakwenda kazini, kama ni weekend, atatoka nao na kuwapeleka sehemu mbali mbali. Baharini, kwenye michezo, ilimradi tu kuwafurahisha na kumfanya Tunda afurahi na kuzoea jiji.
Atamtaka amsimulie maisha ya kwa baba yake mzazi. Ugumu gani alipambana nao. Nini alikosa. Basi hapo ahadi na utekelezaji wa kweli utatolewa kwa Tunda. Atamuahidi hili na lile. “Sitaruhusu ulale njaa Tunda. Tena hata pale nyumbani wakipika kitu usichopenda, uwe unaniambia, nitakutoa kwenda kukununulia chakula kingine, chochote utakachopenda. Sawa? Usiache kuniambia.” Hapo Collin anakuwa mpole na mnyenyekevu kweli. Usingejua kama ni yeye. Utulivu kwa Tunda ukaongezeka.

Akaanza tabia yakukaribisha watoto chumbani kwake ili wakae kitandani waangalie tv hapo wakati akifanya shuguli zake. Basi hapo anaweza kuanza kwa kuwapakata wote wawili, mwishoe atamshusha Tom kwa kisingizio kuwa hatulii, na kubaki amempakata Tunda, binti wa miaka 12! Japokuwa Tunda hakuwa mtoto wakupakata, lakini baba Tom alipenda kumpaka au kujiweka karibu naye kila wawapo kitandani hapo. Atamtekenya na kumshika hivi na vile, Tunda akichekelea upendo wa ‘dady’. Hakuna aliyeshangaa. “Wewe muendekeze huyo!” Ndio usemi wa mama yake akiona mumewe anamtetea Tunda.

Kwa upande mwingine Manda alishukuru kwa ule ukaribu, akafurahia jinsi mumewe alivyompokea Tunda, japo alimficha na kumdanganya. Collin hakuwahi kulalamikia hilo. Alimuonyesha kuelewa kabisa. Kwa hiyo alipoona ule upendo kwa Tunda, kwake Manda ikawa afadhali. Nyumba ikabaki kuwa na amani, na yeye anaendelea kunufaika kivyake. Akawa anawaacha tu. Hata akiwakuta Tunda na Tom wamelala hapo kitandani na baba yao, au hata wakiwa wamepitiwa na usingizi, hakuwa na neno na wala hakuwatizama kwa jicho la pili. Baba yao alishawatetea na kumwambia Manda ni afadhali wawe pale wakiangalia tv na yeye akiwepo ili kuhakikisha hawaangalii mambo mabaya na hawaendi kucheza hovyo kwa majirani. Hilo likapita bila kikwazo. Kukutwa Tunda kitandani kwa wazazi hao ikawa sio jambo la ajabu kwa yeyote. Collin alishalitengenezea mazingira mazuri tu.

Taratibu akaanza kuvuka mipaka wawapo kitandani hapo endapo Tom akipitiwa na usingizi, au anamtuma akacheze mpira na wenzake nje ili apate sababu yakubaki na Tunda pale chumbani peke yao. Basi atamtaka kuangalia makovu ya Tunda. Haanzii mbali. Anaweza kuanza mkononi. Atamtaka apandishe nguo ili atizame makovu aliyosababishiwa na mama yake wa kambo, huko mgongoni. Basi atamshika kwa upole huku akimpa pole na kumuuliza taratibu hili au lile, huku Tunda amempa mgongo.

“Ulikuwa ukimuonyesha baba?” “Baba alikuwa na kazi nyingi. Hakuwa akikaa nyumbani muda mrefu.” “Pole sana Tunda. Hapa sitaruhusu mtu akakupiga hivyo. Uliyopitia huko yanatosha. Nataka hapa upumzike kabisa. Umesikia?” Basi hapo atampapasa huo mgongo taratibu tu.
Siku zikasogea, akipapasa makovu ya mgongoni na mkononi, akaona asogee na makovu ya mbele. Siku hiyo akiwa amemtoa Tom chumbani kwa hasira kuwa anaruka ruka hatulii kama Tunda, akaruke nje, akabaki na Tunda tu. “Hakuna siku aliyokuchapa mpaka ukapasuka kabisa?” Tunda akatingisha kichwa kukataa. “Ilikuwa kuvilia damu tu, na kama ni vidonda, basi ni vya kawaida.” Tunda alijibu kwa unyonge.

“Pole sana Tunda. Huyo mama alikuwa katili sana. Hebu tuone tena.” Tunda akanyanyua tena kiblauzi kwa nyuma. Safari hii akafuatisha kovu la fimbo la ubavuni mpaka mbele. Akacheka taratibu, Tunda akashangaa kidogo, akamtizama maana wote walikuwa wakiangalia kovu ubavuni. Baba Tom alishafika mbele, akiwa nyuma yake. “Nini!?” “Umekuwa Tunda, hebu muonyeshe dad maziwa.” Tunda akajifunika kwa haraka, na kucheka. Akakataa kwa kupandisha mabega huku akiendelea kucheka nakujisogeza mbali kidogo. Collin akapotezea kama utani. Akamvuta na kuanza kumtekenya huku akilalamika kuwa Tunda anamnyima  dad kuona.

Ukaendelea utani wa Tunda anamnyima dad kuona jinsi alivyokuwa, huku wakicheka. Mwishoe akaweka msisitizo kwa kumkamata na kumbembeleza sana, mpaka Tunda akamuonyesha. “Yameanza kuuma?” Tunda alitingisha kichwa kwa aibu huku anacheka. Collin akaanza kupitisha mkono taratibu. “Dady!” Tunda akashangaa. “Kwani nakuumiza?” Tunda akakataa kwa kutingisha kichwa. “Sitakuumiza, naangalia tu kama inauma. Na hivi?” Tunda akatingisha kichwa kukataa. Basi hapo Collin akaendelea kumshika taratibu huku akimuuliza maswali na Tunda naye anamwangalia anavyomgusa akisikilizia kama kuna maumivu ili amjulishe ni vipi inauma. Lakini mpaka hapo, hakuwa amepata maumivu yeyote. “Itabidi kuanza kutafuta nguo za juu ili kuficha hizi chuchu watu wasizione kwa nje ya nguo.” Akashika chuchu zake, Tunda akacheka na kujifunika.

Huo ndio ukaanza kuwa mtindo wake, kuulizia kama maziwa ya Tunda yanauma na yanaendeleaje? Basi atamtekenya hapo kitandani mpaka afanikiwe kumfunua na kujidai kumwambia atulie aangalie kitu kwenye vimaziwa vyake. Basi Tunda atatulia akijua dad anaangalia kitu. Baba huyo atapitisha mikono hapo juu ya vimatiti hivyo, Tunda akiwa hajui kama anachezewa.

Akaona ananogewa. Akazidisha mtindo wa kumpakata kila anapokuwa nao hapo kitandani akimwambia Tunda atulie angaalie tv, wakati mikono ikipita taratibu kwenye mwili wa Tunda huku akimwambia baadaye atampeleka kumnunulia hiki au kile kwa kuwa yeye ni mtoto mzuri, mtulivu, sio kama Tom, ambaye hatulii pale kitandani.

Ukweli Tunda hakuwa mtoto mdogo hivyo wala mjinga wa kiasi hicho kama alivyoonekana. Wakati huo tayari alikuwa ameshafikisha miaka 13, darasa la tano ambapo alitakiwa awe darasa la sita, ila alirudia tu. Kaumbile kakijaluo kalishaanza kuonekana bayana kwake. Matiti madogo ya duara yalikuwa yakionekana katika kila nguo anayovaa na alishatengeneza umbile la chini pana zaidi kuashiria kukaribia kupevuka. Zaidi hips na matako. Tunda alikuwa na urefu wa baba yake. Kama ungekutana na shangazi zake, ndipo ungejua wapi Tunda amerithi maumbile yake. Hata Manda mwenyewe, alikuwa na umbile zuri tu kama mwanamke yeyote yule. Kwa hiyo Tunda alishaanza kujitengeneza kama mtoto wa kike mwenye maumbile ya kike mazuri. Hakuonekana tena kama alizaliwa njiti, katoto kalikomuogopesha hata mama yake alipomzaa.

Na ulaji ule wa chips, makuku ya KFC aliyokuwa akipekewa kula na baba Tom mara kwa mara, icecream za hapa na pale, Tunda alishaanza kujazia vyakutosha. Kwa hiyo ni kweli alishakuwa na maziwa yakushika endapo hutamtizama kwa jicho la mtoto wakumzaa. Ila hakuwa ni binti wa kumpakata hata kidogo. Kwanza kalikuwa karefu. Lakini si kwa Collin baba yake Tom.
Mchezo huo ukaendelea, Tunda akaanza kumkwepa. Kila akiwaita wakaangalie tv chumbani Tunda alianza kusema anamsaidia kazi dada jikoni. Alipogundua anamkwepa, akaanza ukali na kwake pia, kitu ambacho hakikuzoeleka hapo nyumbani kwake, nakumfanya Manda azidi kuwa mkali na kwa Tunda bila kutaka kujua undani.

Hakutaka tena Tunda amuharibie ndoa yake. Tunda huyu huyu ndiye aliyempokonya ndoa ya kwanza ya mwanaume aliyempenda sana, kwa kuzaliwa mweusi kupitiliza mpaka Mosi akamkimbia. Leo tena aje amtoe kwa Collin, kwenye neema! Manda hakutaka kumpa huo mwanya tena. Akawa mkali sana kwa Tunda. Kila kosa analolisema Collin, hata lakumsingizia Tunda, basi mama yake naye atakuwa nyuma yake kuwa mkali zaidi kwa Tunda. Collin alipokosa sababu ya msingi, akaanza kufuatila shule ya Tunda ili tu kuwa na sababu nzito. Basi ikawa ni kugomba juu ya matokea ya Tunda darasani.

Collin alikuwa akiongea kwa ukali mbele ya Manda na Tunda kuwa Tunda anacheza tu darasani, anachezea pesa yake na nafasi ya thamani sana maishani. Ni heri nafasi hiyo yakuishi hapo nyumbani kwake na kusoma hiyo shule, angeweza kumpa hata mmoja wa ndugu zake kuliko huyo Tunda ambae hathamini. Hilo likamshtua na kumuogopesha sana Manda. Ikawa lawama tupu.
Manda akaona Tunda anamtia aibu. Neno la kurudishwa kwa baba yake likawa linatoka kwa Manda na Collin, kutishiwa Tunda kila wakati na kipigo kutoka kwa mama yake kikaanza mbele ya Collin kumuonyesha Collin na yeye anaungana na anachosema yeye. Na Collin akaacha kumtetea, akamuacha awe anapigwa mbele yake na mdogo wake Tom.

Madaftari ya Tunda yakaanza kupitiwa kila siku na maswali. Akishindwa kujibu au akionekana ameshindwa kuelewa chochote kile, kwenye somo lolote, basi kipigo kilifuata huku akitukanwa kama yeye ni mjinga sana, mzembe, anacheza tu na hana shukurani.
Hakuishia hapo, wakati mwingine ungemsikia akipigwa na mama yake chumbani akimuuliza kama amrudishe kwa baba yake. Atamfinya na kumwambia anamtia aibu nakutaka kumuharibia amani ya nyumbani kwake. Basi Tunda atapigwa huko chumbani bila utetezi.

Alipoona katika hilo nalo amefaulu akamwambia mkewe, mama yake Tunda kuwa yeye sasa ndio ataanza kusimamia shule ya Tunda kwa karibu sana. Lazima Tunda awe anasoma alipo yeye ili ahakikishe hachezi anasoma kweli. “Siwezi nikawa namwaga mapesa yangu bure wakati mtoto mwenyewe anacheza tu au mnampa shuguli nyingi za jikoni! Lazima kuhakikisha anakazana na masomo. Msichana wa kazi yupo na kijana. Tunda hatakiwi awe anashinda jikoni mara baada ya shule. Lazima atulize akili shuleni.” Hilo nalo likamuingia mama yake. Akamwambia dada wa kazi asiwe anamtuma sana Tunda, amuache ajisomee. Akamsisitiza Tunda kusoma sana na kila akiwa anasoma ahakikishe baba yake anamuona. Asimtie aibu.

Tunda akawa hapewi tena kazi zozote mle ndani. Akaambiwa yeye jukumu lake ni shule na kujisomea tu hapo nyumbani. Na kwa kuwa mama yake alikuwa nesi, basi uingiaji wake wa kazini ulikuwa wa shift. Kama anaingia kazini asubuhi, basi atatoka mchana. Na akitoka mchana kazini, Manda msichana asiyependa umasikini, alijua kujishugulisha. Alikuwa na miradi ambayo alifunguliwa na mumewe. Basi kama hayupo kazini, ujue atakwenda kwenye biashara zake. Na endapo ataingia kazini muda wa mchana, anatoka usiku. Basi asubuhi ndio huanzia kwenye miradi yake kwanza.

Na inakua zaidi anapoingia kazini usiku mpaka asubuhi. Atashinda kwenye miradi yake mpaka jioni, atarudi tu kuoga na kubadili nguo kisha kwenda kazini mpaka asubuhi anaporudi nyumbani, na watoto wanakuwa wameshaenda shule. Kwa ukweli Manda alikuwa mchapakazi na mtafutaji. Ndio sifa kubwa Collin aliyokuwa akimpendea Manda. Alijituma kama mwanamke wakichaga haswa. Sio mvivu na mzuri pia kwenye mambo ya biashara. Amechangamka na mbunifu.

Basi kutokana na hayo yote, mumewe alipata uhuru wote juu ya Tunda. Muda ulikuwa mwingi na mzuri tu wakufanya atakacho kwa Tunda. Kwanza yeye ndio alikuwa dereva wao. Anawapeleka asubuhi, na kila anapotoka kazini, anawapitia watoto shule, na kurudi nao nyumbani. Watakula na kuoga. Tom aliruhusiwa kwenda kucheza nje, lakini Tunda aliambiwa aingie chumbani kwa baba yake na madaftari yake ili ajisomee. Basi hapo huyo baba alipata uhuru wote. Atamtaka Tunda ajisomee kitandani kwake. Na kama mama yake akiingia shift ya kazini usiku, hapo ndio aghueni kabisa. 
********************************
    Collin hakuanza tu na kumwingilia Tunda. Alianzia mbali sana, tena taratibu na kwa umakini. Aliandaa mazingira kwa watu wa hapo nyumbani ili mtu yeyote yule asiwahi kumshuku, na mwilini mwa Tunda pia. Alihakikisha anaanza taratibu sana kwenye mwili wa mtoto huyo na kumjenga kwenye fikra kuwa dad ndio mwenye amri juu ya mwili huo. Alikuwa akimwita chumbani kwake, akijua ameshaoga, na ni msafi. Atamwambia apande kitandani, ajilaze kifudi fudi yaani kwa tumbo kama anayesoma. Madaftari mbele, na atulie. Basi hapo Collin atakaa nyuma yake nakuanza kupitisha mikono kuanzia mapajani mpaka anapotaka yeye. Tunda hakutakiwa afanye chochote, pengine kufuata maelekezo tu.
    Basi hapo atamchezea nakumgeuza hapo kitandani kwa uhuru wote mpaka aridhike ndipo atamruhusu Tunda kutoka hapo chumbani kwake. Iwe kwenda kula chakula cha usiku au kwenda kulala, huku akimuonya asimwambie mtu yeyote, na hiyo ndio njia yakumfurahisha dad wake. Alimwambia dad akifurahi na yeye atafurahi. Na kweli, amani na utulivu vikarejea. Dad amepata anachokitaka.
******************************
Tunda alianza kuwaza lipi lilikuwa bora, maisha yake kwa mama wa kambo akiwepo baba mzazi au kwa baba wa kambo akiwepo mama mzazi! Kwa umri mdogo aliokuwa nao, alishapokonywa uhuru wake kamili. Sio ki fikra tu, sasa na mwili wake pia. Hakuwa na chakuzungumza tena, alikuwa mali kamili ya baba wa kambo. Hana amri tena juu ya huo mwili, ila baba wa kambo kufanya kile atakacho kwa kumuacha aishi hapo nyumbani kwake.
    Endelea kuwa na Tunda kwenye safari yake ya maisha yaliyobadilika gafla. Baba wa kambo naye atampitisha kwenye Mengi. Na Mengi atafanya kwenye nyumba hiyo na maisha yake ya baadaye.

Usikose Sehemu ya 3.

CONVERSATION

0 Comments:

Post a Comment