Naomi Simulizi |+1 205 767 8163 |naomisimulizi@gmail.com Nilipotea! - Sehemu ya 3. - Naomi Simulizi

Nilipotea! - Sehemu ya 3.

                               Baada yakumaliza darasa la saba.

K
wa mshituko wa maisha, na yele anayofanyiwa kila wakati bila mama yake hata kuhisi. Huku akiendelea kutumiwa kwa vile yule baba atakavyo, ndio Tunda alipotea kabisa kwenye ulimwengu wa masomo. Hata ungemkuta sehemu, ungemkuta ametulia kama ameduaa. Mambo aliyokuwa akifanyiwa, au kufanya kwa yule baba, yalianza kuharibu akili yake. Alitamani hata siku moja wafumaniwe, lakini baba Tom alikuwa na akili ya aina yake. Alihakikisha anawapanga vizuri watu wa nyumbani kwake, na kuhakikisha hata Tunda mwenyewe hawi na maumivu. Maisha ya kunywa dawa za maumivu kikawa kitu cha kawaida sana kwa Tunda. Alikuwa akipewa azinywe, kama pipi.

Tunda alifanya vibaya kwenye mitihani yake ya darasa la saba kitu kilichomuudhi sana mama yake. Lakini baba yake wa kambo alimtetea na kumuahidi yeye mwenyewe atamsomesha shule ya kulipia. Hilo lilimpa moyo mama yake na kumshukuru sana mumewe aliyekuwa akijisifu kwa mashoga zake, kuwa ni mume ambaye hana mpango na wanawake wengine ila yeye tu. Na ni kweli, baba Tom alikuwa mtu wakuwahi kurudi nyumbani sana. Asubuhi alitoka na watoto, na jioni alirudi nyumbani moja kwa moja bila kupitia hata baa. Utamkuta nyumbani mbele ya tv akisubiria taarifa ya habari. Hapakuwahi hata kuwa na fununu ya mwanamke wa nje. Mwanaume wakuheshimiwa sana kwenye jamii. Usingemkuta kwenye mambo mabaya. Muungwana kwa majirani na mchapakazi kazini. Alitunza familia yake, na heshima yake iliongezeka hata ukweni kwa kumpokea Tunda na kumtunza bila malalamiko. Misaada kwa wakweze ikaongezeka, hapakuwa na ubaya kwa baba Tom.

Manda alimpenda na kumthamini zaidi mumewe kwa moyo wake wa uvumilivu kwake na heshima aliyomuwekea kwenye jamii. Tokea apate matatizo ya mgongo mara baada ya kujifungua, mahusiano yao ya kimapenzi kama wanandoa, hayakuwa kama zamani. Tendo la ndoa ilikuwa mara chache sana. Lakini mumewe hakuwahi kulalamikia zaidi ya kumfariji akimwambia asiwe na wasiwasi, anaridhishwa na kidogo anachopewa. Hata hivyo alimpongeza kwa kumzalia watoto hao wawili na juhudi zake za kusaka pesa.

Kwa kuwa alikuwepo tu nyumbani akisubiri kwenda kidato cha kwanza, Tunda akageuka kuwa mlezi mkuu wa mdogo wake, Aneti. Alipewa na aliambiwa afuate masharti yote ya malezi. Manda alimfundisha kuanzia kumuogesha huyo mtoto, kumlisha, kumbeba na matunzo yote kwa ujumla. Kazi pekee ya Tunda ikawa mtoto. Na kwa kuwa mama yake alikuwa mkali sana kwake, wakati wote ungemkuta Tunda na huyo mtoto akifanya kazi za huyo mtoto tu, tena kwa makini. Kuanzia asubuhi akimka, mama yake akitoka hapo ndani mpaka usiku huyo mtoto akienda kulala. Msafi muda wote, na wala usingemkuta nje akicheza au akifanya kazi nyingine. Wakati wote yupo ndani na mtoto kama yeye ndio mzazi. Na hapo ndipo baba Tom alipopata sababu ya kumnunulia simu nzuri sana.

“Mbona simu yenyewe ya garama hivyo!?” Manda alimlalamikia mumewe. “Huoni anavyomtunza mtoto vizuri? Anastahili hiyo simu.” “Basi ngoja nibadilishane naye. Nimpe yangu.” “Hapana bwana. Mwachie mtoto. Tunda anastahili hii simu. Ametulia sana. Muda wote yupo na mtoto. Aneti ni safi wakati wote. Afya yake nzuri. Ameokoa garama kubwa ambayo tungemlipa mtu wa kumuhudumia Aneti, na pengine tusingepata huduma nzuri kama Tunda anayompa mtoto. Hiyo simu itakuwa njia moja wapo yakumtia moyo na kumuonyesha tunathamini anachokifanya.” Manda hakuwa na jinsi. Mnunuaji alikuwa ni mumewe. Na mumewe huwa akipanga kitu na kukisimamia, huwa sio mtu wakubadilika. Ikabidi awe mpole tu. Tunda akaitwa na kukabidhiwa ile simu huku akipongezwa.

Hiyo ndio ikawa njia nzuri sana ya mawasiliano kati ya baba Tom na Tunda. Ratiba haikubadilika sana. Kipindi hicho cha mwanzoni aliporudi kazini, Manda alikuwa akiingia asubuhi kazini na kuwahi kutoka kwenda kunyonyesha. Lakini kwa kuwa alikuwa nesi na msafi sana, alijua jinsi yakutunza maziwa yake. Alikamua na kuyaweka kwenye friji vizuri. Akamfundisha Tunda jinsi ya kupasha moto na kumpa mtoto. Yeye akawa anatoka asubuhi, nakurudi jioni au usiku. Akitoka kazini, anapitia kwenye miradi yake ambayo ilisimama kwa miezi michache nyuma, alipofikisha miezi 8 ya ujauzito na mgongo kuanza kusumbua, daktari alimshauri apunguze shuguli, kwa hiyo akaacha ufugaji. Aliuza kuku wote. Kuanzia wa mayai na nyama. Akawa anakwenda kazini tu na kurudi, bila hata biashara mpaka alipokwenda kujifungua. Aliporudi sasa, ndipo akafufua miradi yote kwa nguvu zote, na kumuacha Tunda kama mlezi wa katoto hako kachanga.

Tom yeye aliendelea kwenda shule kama kawaida. Kutoka asubuhi na baba yake, anashushwa shuleni, baba yake anakwenda kazini mpaka jioni anapokwenda kumchukua. Dada wa kazi, kazi zake zile zile. Hajihusishi na mtoto. Akimaliza shuguli zake asubuhi wenye nyumba wakiondoka, anaingia mtaani mpaka mida ya jioni, anarudi kupika chakula cha usiku na kumsubiria Tom arudi kutoka shule ampe chakula na kumuhimiza kuoga, na kumuhudumia mama mwenye nyuma wake usiku anaporudi. Alikuwa na uhuru wote sio kama Tunda aliyekuwa akilea, hawezi kutoka kwenda popote sababu ya mtoto. Labda siku za jumapili, Manda akiwepo nyumbani, ndipo Tunda alikwenda kutengeneza nywele, sio katikati ya week. Na hiyo ndio ikawa nafuu ya baba Tom.

Mawasiliano kati ya mkewe na Tunda yakawa ya kila wakati. Wakati wote baba Tom alitaka kujua mkewe yupo wapi na anafanya nini. Simu za mara kwa mara kwa mkewe akimjulia hali yake hazikuisha. Manda alikuwa akifurahia sana ile hali yakujaliwa, asijue nia ya mumewe akitaka kujua alipo, ili akapate muda na Tunda nyumbani. Kila alipojua mkewe yupo kazini muda wa mchana au kwenye miradi yake, yeye alirudi nyumbani kwa kisingizio cha kumuona mtoto au kupeleka mahitaji ya mtoto nyumbani. Na hapo pia akajikuta anapata muda mfupi, lakini mzuri na Tunda. Ili akimbizane vizuri na muda na asichelewe kote kote. Hapo nyumbani na kazini, alikuwa akimtumia ujumbe Tunda, aandae mazingira mazuri ili akifika amkute huru. Kama aanze kumbembeleza mtoto mpaka alale, na yeye awe ameoga vizuri, awe tayari tayari akimngojea. Na akikaribia nyumbani, atampigia tena simu, amkute chumbani kwake, na ahakikishe mtoto amelala kitandani kwake.

Kwa kuwa msichana wa kazi na yeye alikuwa mzurulaji, na kama endapo akimkuta hapo nyumbani, basi anaweza kumtuma kitu cha mtoto ambacho anajua wazi hawezi kukipata kwenye maduka ya hapo mtaani. Na atamwambia ahakikishe anakipata. Basi msichana wa kazi atatoka hapo na furaha zote akijua anakwenda kuzurula, na kumuachia Tunda. Na wala baba Tom hakuhitaji muda mwingi sana na Tunda pale chumbani. Kwa kuwa alikuwa akimkuta Tunda yupo tayari akimsubiria, kwa hiyo alifanya naye mapenzi haraka haraka nakutoka kurudi kazini. Na kama akishindwa mida hiyo ya mchana akiwa na kazi nyingi ofisini kwake, au labda Manda akiwepo usiku nyumbani, basi atarudi jioni na kisingizio chochote cha maana sana. Atamchukua Tunda akidai anakwenda kununua mahitaji ya mtoto huyo mchanga ambayo labda Tunda alimuagiza hajaelewa au ya Tunda mwenyewe. Na huko njiani alihakikisha anatimiza haja zake kabla hajamrudisha Tunda nyumbani.

Zawadi za hapa na pale kwa Tunda hazikukoma. Iwe ni mchana anaporudi nyumbani au jioni. Hakuacha kumletea vitu vizuri kumfurahisha Tunda. Chochote alichotaka Tunda, aliletewa. Tunda hakuwahi kutoa siri hiyo kwa mtu yeyote. Na baba Tom alijitahidi sana kuwa makini ili mkewe asiwahi hata kuhisi. Mara zote alimpigia simu Tunda sio ujumbe ili isijetokea hizo jumbe zinakamatwa. Maisha ya amani na utulivu yakaendelea ndani ya ile nyumba. Baba Tom akipata anachotaka, bila shida na bila matatizo, kwa kuwa baada ya muda Tunda akazoea na kuelewa kufanya mapenzi na baba huyo. Maumivu yaliisha kabisa, basi alifanya jukumu hilo kwa wepesi bila shida. Amani na vitisho kutoka kwa baba huyo vikakoma. Tunda akawa binti anayependwa na kusifiwa kila mahali. Akamuanzishia kumpa na pesa zake za matumizi mbele ya mama yake. Manda hakuona tatizo. Alimwambia zitamsaidia kwenye matumizi yake madogo madogo. Lakini hizo pesa alizokuwa akipewa mbele ya mama yake ilikuwa gelesha tu. Wakiwa peke yao, alimpa Tunda pesa zakutosha hata Tunda mwenyewe hakuwa akijua azifanyie nini zaidi ya kumtuma dada wa kazi, wajinunulie chips, kuku na kula  hapo ndani kama chakula chao cha mchana, wazazi hao wanapokuwa kazini.

Kwa kuwa pesa ilikuwepo, akaanza kubadili hata aina ya nywele anazotengenezwa. Kila ijumaa anapewa pesa nzuri tu ya kubadilisha nywele na kutengeneza kucha. Jumapili ndio ikawa siku yake ya mapumziko. Anaenda kutengenezwa nywele nzuri, na kutengeneza kucha za mikono na miguu. Mavazi mengi aliletewa na baba Tom kama anavyomnunulia Tom na mkewe. Akaanza na  yeye kuletewa pafyume, mafuta na lotion nzuri za kueleweka kama mama yake. Tunda aliyekuwa amechukua na maumbile ya kwao, urefu, akaanza kujazia vizuri na kupendeza. Chips, kuku na yai kwa kila siku, huwa haziongopi kwa yeyote. Lazima unenepe tu. Tunda akawa binti, na ndio kipindi hicho hicho cha likizo ya darasa la saba ndipo alipovunja ungo. Akaanza kuonekana binti aliyekomaa vizuri. Ni kweli alikuwa mweusi asiye na swali. Lakini kwa kuwa alikuwa akitunzwa vizuri, mtoto wa kukaa ndani kwenye geti. Hana shida. Chips yai na kuku kila siku. Fanta yake kila wakati. Zawadi za hapa na pale. Sifa kila akimridhisha baba huyo, hapakuwa na sababu ya Tunda kutonawili. Akawa na ngozi yakuteleza, inang’aa na vile alivyojazia na kutengeneza umbo la kike, ungependa kumtizama tu.



Sekondari!
A
kaanza kidato chake cha kwanza katika shule nzuri yakulipia ya sekondari, akiwa sio tu amefeli darasa la saba, ila hajui lolote lile ila kuumba herufi vizuri na kuongea kingereza kizuri kana kwamba ametokea Britain. Lakini pesa ya baba Tom iliongea. Tunda akapata nafasi huko kwenye hiyo shule bila kusumbuka au mtihani.
 Ratiba za shule zikaanza tena kwa Tunda ambaye amebadilika, sio mtoto tena. Akili na mwili vilishakomazwa. Kila kitu cha Tunda mwilini mwake kilikuwa kizuri na cha thamani. Kuanzia nguo za ndani alizokuwa akiletewa kila mara tena nzuri na za kisichana, mpaka nguo zake za nje. Baba Tom zawadi yake kubwa ya mara kwa mara kwa binti huyo ilikuwa chupi, nguo nzuri za kulalia na mataulo yale mazuri na ya thamani kwa Tunda. Lakini zaidi chupi alizokuwa akimletea za kila namna. Ilikuwa ni zawadi aliyopendelea kwa kuwa haikuwa ikionekana kwa urahisi kila avaapo, kwa hiyo hata maswali kwa mama yake hayakuwepo. Hiyo ndio ikawa ni zawadi aliyozoezwa na baba huyo. Alizijua kwa majina ya madizaina. Akiwa na umri huo mdogo, Tunda alishajua madizaina mbali mbali na alikuwa akivaa nguo zao, akijua mtengenezaji ni nani na yupi anatengeneza nzuri. Kuanzia nguo, mafuta na pafyumu alijua watengenezaji wake. Ukweli alijitahidi sana kumtunza Tunda, na alihakikisha Tunda anajua anamuhangaikia. Hakuacha kumwambia ili kuzidi kumleta karibu na kumtawala. Zaidi kifikira. Akamfanya Tunda kuwa mateka wake kweli kweli.

~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~

Sasa shule zilipoanza, ilibidi kubuni njia nyingi tofauti tofauti za kukutana nje ya pale nyumbani. Baba Tom akaja na hoja nyingine ya nguvu. Ili kumsaidia kimasomo, baba huyo alimwambia mkewe Manda, lazima Tunda awe na masomo ya jioni ya ziada. Akamwambia yeye mwenyewe atamtafutia mwalimu, baada ya kutoka shule, atampeleka kwa huyo mwalimu, atarudi ofisini kwake, na kumsubiria mpaka amalize kufundishwa, ili akamchukue na kumrudisha nyumbani. Wazo likazidi kuvutia zaidi. Manda akakubali bila shida. Kwanza mumewe alionyesha kumchunga sana Tunda. Alikuwa akimwambia Manda hataki vijana wa mjini wamchezee binti yao, anataka Tunda atulie. Na kwa kuwa tamaa kwa Tunda iliongezeka, ni kweli alimchunga Tunda. Hakutaka Tunda awasiliane na mwanaume yeyote yule. Manda alikuwa akimuona jinsi mumewe anavyomuhoji mambo ya msingi kama binti yake na kumkaripia akimtaka atulie. Alikuwa akimwambia Tunda mbele ya mama yake, tena kwa kurudia rudia, kuliko kuwa na tamaa huko nje, ni heri awaambie wao wazazi, chochote anachotaka, watampa, ilimradi tu atulie asiwe na mambo ya wanaume. Manda naye alikuwa akiweka msisitizo kila akimsikia mumewe akizungumza na Tunda, akitaka amsikilize kwa makini baba yake. Tom akaanza kutumia basi la shule kwa usafiri wa jioni kurudishwa nyumbani. Ratiba za masomo ya ziada kwa Tunda siku za shule zikashika kasi. Hapakuwa na masomo ya ziada ila mapenzi matupu.

Baba huyo akawa anapata nafasi yakutosha na Tunda kila siku jioni. Ofisini wakazoea kuwa Tunda akitoka shule mara nyingine huwa anakwenda ofisini kwa baba yake kujisomea. Baba Tom, mtu wakuheshimiwa kazini, alikuwa na wadhifa mkubwa tu kazini kwake, na alikuwa na ofisi yake na sekretari wake pia. Ilipokuwa ikifika saa 10 jioni, wafanyakazi wengine wakiondoka pale ofisini, basi ilikuwa kazi ya Tunda sasa kuingia kazini kumuhudumia baba huyo aliyekuwa dad. Watakaa ofisini hapo na dad wake, mapazia yameshushwa, mlango umefungwa mpaka aridhike ndipo wanarudi nyumbani.

Tuition zikachanganya na kukolea. Ikaongezeka na siku za jumamosi pia. Baba Tom akaongeza ratiba nyingine ya Tunda ya kutoka pale nyumbani siku za jumamosi saa nne asubuhi kwa ajili ya kwenda tuition. Lakini lengo kubwa ni kumtoa Tunda pale nyumbani na kupata naye muda. Siku nyingine za jumamosi, walitoka nje kidogo ya mji. Baba Toma alijitahidi katika hilo kuwa makini pia. Walitoka mida tofauti. Wakati mwingine alianza kutoka yeye saa mbili asubuhi, kisha baada ya masaa mawili mbeleni, anafuata Tunda. Hakuna siku waliyochelewa kurudi. Tena wakati mwingine, Tunda alifika nyumbani lisaa limoja kabla ya baba Tom kurudi nyumbani. Baba Tom atapiga simu nyumbani au kwa mkewe kuulizia mahitaji ya hapo nyumbani. Basi, Tunda atarudi na madaftari, baba Tom atarudi na mahitaji ya nyumbani.

Ki ukweli, kwa upande wa baba Tom, masomo haikuwa kipaumbele kabisa kwa Tunda. Hata walipokuwa wawili na Tunda, hakumuhimiza kabisa mambo ya shule. Kwanza hata hawakuzungumzia masomo. Yalikuwa mapenzi na kumtaka afikirie juu ya maisha yao kana kwamba ni mkewe. Alitaka binti huyo kuwa mbunifu kwa wanachokifanya ili kila wanapokuwa amuongezee furaha. Wakati mwingine wanapokutana huko, anaanza kwa kumuonyesha picha za ngono, na kumtaka Tunda ajifunze na wajaribu. Basi na yeye akawa mtu wa shukurani sana kwa Tunda. Alimsifia kwa kila anachomfanyia. Ilimradi tu, kumfanya Tunda aendelee kuwa chini ya hemaya yake.

Matokeo mabaya ya hapo sekondari nayo hayakukawia. Tunda ambaye ni kama hakusoma shule ya msingi, au ni kama aliyeishia darasa la pili la kijijini kwa bibi yake, akazidi kufeli zaidi na zaidi. Hakuna aliyejua hayo, kwa kuwa baba Tom ndiye aliyekuwa akifuatilia mambo ya shuleni, na ripoti zote alikuwa akipokea yeye mwenyewe kama mlipa ada. Hata alipokuwa akiitwa shuleni, kwa ajili ya masomo ya Tunda, alijuwa kupooza walimu. Ili kupunguza makali shuleni, akazua na ugonjwa. Akawataarifu shuleni kuwa Tunda anamatatizo kiafya, alizaliwa akiwa na matatizo. Hata uelewa wake sio kama watoto wengine. Akaomba wamvumilie tu, kwa kuwa ni mtoto wa kike, basi, wasaidiane kumsukuma tu, amalize hata hicho kidato cha nne. Hilo likaeleweka, basi akaongeza na siku za kumtoa Tunda katikati ya masomo ili kumpeleka kwa daktari kwa huo ugonjwa ambao hata Tunda mwenyewe hakuwa akiweza kutamka jina la huo ugonjwa.

Manda hakuwa na taarifa zozote juu ya maendeleo ya Tunda. Alibaki akihangaika na mambo yake  na watoto wake. Tunda aliyekuwa akimlelea mtoto, hakuwepo tena nyumbani. Msichana wake wa kazi ndio hakuzoea majukumu. Akaanza kuachiwa jukumu la mtoto kwa ahadi ya kuongezewa mshahara! Hakufurahia wala kuzoea. Yule msichana alikuwa mtu wa kuzurula mtaani na kwa wanaume zake. Kushinda nyumbani akibembeleza mtoto kama Tunda, ikawa ngumu. Akaanza kumsumbua sana Manda. Mara mtoto apate maradhi haya au yale kwa uchafu. Zaidi UTI ugonjwa unaonyesha mtoto hakuwa akisafishwa vizuri au akiachwa na kinyesi muda mrefu. Aneti akapungua na kubadilika kiafya kwa kukosa matunzo mazuri. Maradhi ya hapa na pale yakaanza kumlazimu Manda kubaki nyumbani akilea wakati biashara zake nazo zinamsumbua.

Haya, Tom naye ikawa shida nyingine kwa Manda. Muda wa kwenda kumpokea Tom kituo cha basi akitoka shule, ukawa mgumu kwa msicha huyo wa kazi. Tom akawa anashushwa na basi hilo la shule, lakini hamna mtu wa kumpokea, dada yupo kwa wanaume akiwa ametoka nyumbani masaa, anadai kwenda dukani. Hilo nalo likawa aghueni kwa Tom. Asipopokelewa kituoni ili arudishe nyumbani, na yeye anaingia mtaani kucheza mpira na marafiki zake, mpaka majirani wamvushe barabara wamrudishe nyumbani, au Manda mwenyewe akiona muda umepita, Tom hajarudi na msichana wa kazi hajarudi kutoka huko dukani, inabidi ambebe na Aneti, aingie mtaani akamsake mtoto wake. Ikawa ni shuguli nzito kwa Manda na hao watoto wake wawili, pamoja ni miradi yake pia. Hakuna jinsi ungemwambia amfuatilie na Tunda naye, akaweza.

 Kwanza hakuona sababu na haikuwa desturi yake kumfuatilia Tunda. Hawakuwahi kuwa na mahusiano ya kaaribu, halafu akaona mumewe anammudu huyo Tunda. Alikuwepo nyumbani wakati wote, na akitoka hapo basi mumewe alijua alipo na siku za shule alihakikisha anarudi naye nyumbani, hampi mwanya wa kuwa karibu na wanaume. Na vile alivyomuona mumewe anakuwa mkali kwa Tunda, ndio akaachana kabisa na Tunda, akili zikawa kwa hao watoto wake wawili tu na miradi yake.
Tunda na mumewe wakawa na maisha yao tofauti ndani ya nyumba hiyo iliyokuwa imejaa kelele za Manda na wanae, akihangaishana na wasichana wake wa kazi na miradi. Yale maisha Tunda akawa ameshayazoea kabisa. Baba Tom hataki Tunda apewe kazi kabisa, ili atulie na shule, kumbe mapenzi.Ukitaka ugomvi na baba Tom, ni amkute Tunda anakazi humo ndani. Tunda akawa ni wa kula, kulala na kujifunza jinsi ya kumfurahisha baba Tom, basi. Akawa hodari kweli kweli kwenye mapenzi kuliko shuleni.
~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~

Tunda kwa mama mzazi, mikononi kwa baba wa kambo akiwa ameshakuwa mzoefu na faraja yake asiyoweza kuishi bila hiyo. Nini kitaendelea kati ya mchezo huo unaochezwa kwa makini sana na baba Tom? Tunda alishatamani hata wafumaniwe, lakini kabla ya kutenda, alizipanga karata zake vizuri sana. Manda hajawahi hata kuhisi, na Tunda ameshakuwa mzoefu haswa.
Huwa wanasema, ‘Za mwizi ni arubaini’.
v Je, ni nani atakamwatwa na mfupa?
v Nani atakuwa muhanga wa mchezo wa baba Tom?
v  Ni yeye mwenyewe baba Tom, au ni Tunda, au ni Manda?
v Ni nani ataathirika zaidi?

CONVERSATION

0 Comments:

Post a Comment