Naomi Simulizi |+1 205 767 8163 |naomisimulizi@gmail.com Nilipotea! - Sehemu ya 4. - Naomi Simulizi

Nilipotea! - Sehemu ya 4.

 

B
aba Tom alizidi kuchanganywa na binti huyo mdogo aliyemfundisha mwenyewe mapenzi. Hapakuwa na kutosheka. Kila wakati alimtaka Tunda, kama aliyekuwa na kiu ya miaka. Kila siku ilikuwa lazima ahadumiwe na Tunda, tena alitaka apewe huduma kwa nafasi. Aliitafuta nafasi hiyo kila siku, kwa amani na kelele, ilimradi tu apate muda na Tunda wake. Siku Tunda awapo kwenye hedhi, nyumba ilikuwa haikaliki. Walijua rangi zote za huyo baba Tom. Kelele, hasira na kugomba hata kusiko na sababu. Wakati mwingine Tunda alikuwa akitumia kigezo hicho kujipumzisha mwili wake. Akimdanganya yupo kwenye siku zake, ilimradi tu asimwingilie.

    Japokuwa alifuatwa na vijana wengi pale shuleni mpaka walimu, Tunda na kuvutia kwake kote, alikataa kata kata. Alijaliwa umbile zuri la wazi kabisa. Kwa kuwa alikuwa na weusi uliokolea, macho na meno yake vilikuwa viking’aa sana.

    Yale macho mama yake aliyokuwa akiyaita ya paka, akimkejeli nayo na kumtukana, Tunda akashangaa ndio ikawa kivutio kwa wanaume. Wengi walimsifia kwa wazi kuwa anamacho mazuri yakuvutia. Baba Tom alishamuonya kabisa kuwa na mahusiano na mwanaume wengine. Alimwambia siku atakayomgundua, atamfukuza pale nyumbani kwake bila hata shilingi. Na atahakikisha anaacha vitu vyote alivyomnunulia pale pale nyumbani kwake na kumrudisha nyumbani kwa baba yake bila kumsamehe. Kwa hiyo akili za Tunda zilikuwa ni jinsi ya kumridhisha baba huyo aliyekuwa akimpa kila kitu. Alianza kumfundisha kuendeshea gari, huku akimuahidi atamnunulia gari zuri sana kama la mama yake.

~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~
Huwa hakuna mapenzi yanayonoga kama mapenzi ya wizi. Kwa kuwa mara zote wawili hao wakutanapo, huonyeshana upande mmoja tu wa maisha yao. Ambao upande huo haukusudii kumuumiza mwenzake kwa kipindi hicho kifupi cha kuibia. Hata mazungumzo yao, yanakuwa yakuonyesha ubaya wa wenza wao ambao hawapo pale na ukienda kwenye ufanyaji mapenzi pia unakuwa wakiustadi sana. Maandalizi yanakuwa makubwa ili kuhakikisha wanaridhishana ipasavyo kuliko kwa wenza wao wa halali.

~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~

    Ndivyo ilivyokuwa kwa Tunda na dad wake. Tunda alifika mwisho wa kidato cha pili hakuwa akielewa chochote juu ya shule anayosoma, isipokuwa uzoefu mkubwa alioupata wa mapenzi. Simu yake aliyokuwa amepewa ilisaidia sana kujifunza yale aliyoona ni muhimu kwake, lakini sio shule. Akawa mtu muhimu sana kwa baba Tom.

    Ukitaka baba Tom aongee humo ndani, au umbadili mudi yake, basi mguse Tunda. Hata kama atashindwa kuingilia ugomvi huo moja kwa moja, basi atalipa kisasi kwa njia nyingine, na atahakikisha Tunda anajua na kuona hilo.

    Taratibu Manda akapoteza usemi kwa mtoto wake, na Tunda naye akalijua hilo kuwa mama yake hana kitu chakumfanya tena, yeye yupo chini ya dad. Jeuri ikaanza, hata mama yake akigomba, akawa hajali tena. Kwanza dad aliingilia huo ugomvi na baadaye atampa pole ya zawadi ndogo ndogo kwa ubaya aliofanyiwa na mama yake. Mbaya wao sasa akawa Manda.

    Baba Tom alimsimulia Tunda matatizo ya mama yake kuwa hana uwezo wa kufanya tendo la ndoa, na hata akijitahidi, hamridhishi kabisa kama yeye Tunda anavyomfanyia. Basi Tunda akajiona yeye ni wa maana kuliko mama yake. Na yeye Tunda akamlalamikia dad wake chuki ya mama yake juu yake. “Sijui ni kwa nini amebeba chuki kubwa hivyo kwangu! Hata nikijitahidi kumpendezesha, ni kama ndio nazidi kuharibu!” Basi dad naye akawa faraja kubwa kwa Tunda, akimwambia asiwe na hofu. Yeye atamtunza kama anavyomtunza mama yake pale ndani. Kwani Manda naye alikuja pale ndani kama yeye Tunda. Akakuta kila kitu. Alimwambia hata miradi anayofanya yote ni pesa yake.

    Akamwahidi kuwa, akimaliza shule ya sekondari, atamfungulia miradi yake na yeye. Atamnunulia gari na kumtafutia kwake ambako watakuwa na uhuru wote. Hata simangwa tena, kwa hiyo avumilie. Kiburi kikapanda kwa Tunda. Hakuona tena tofauti yake na mama yake. Hata alipomtisha kuwa atamrudisha kwa baba yake, hakujali tena. Dad alishamwakikishia yeye hana uwezo huo, pale sio kwake. Ila yeye dad ndio alikuwa na huo uwezo. Maisha yakaendelea.
~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~

    Alitoka kwenye chumba cha mtihani wa kidato cha pili kuingia cha tatu, akijua wazi hakuna chamaana alichoandika. Lakini hakujali. Somo alilochukua la nyongeza na kulitilia maanani ni kifaransa, ndio akawa akijitahidi na kingereza. Alikazana sana kusoma kifaransa na hakuwahi hata kukosa tuition yake. Kwa hiyo alifaulu vizuri, kingereza na kifaransa tu.

    Mitihani ilipoisha akamuomba mama yake aende kumsalimia kwa siku chache bibi yake. Mama yake hakuona tatizo. Kwanza alikuwa likizo yakusubiria matokeo yatoke, aingie kidato cha tatu. Manda aliondoka asubuhi kuelekea kazini, nakumuomba mumewe ampeleke Tunda kituo cha mabasi.

    Siku hiyo baba Tom hakuonekana kazini. Kweli waliingia kituo cha mabasi pale pale Ubongo, moja kwa moja mpaka hotelini pale. Wakachukua chumba humo, wakakaa na dad wake humo ndani, Tunda akimuhudumia. Asubuhi ikaisha, mchana nayo ikaingia. Akaagiza chakula, akataka kiletwe mle mle chumbani. Kikaletwa. Wakala, yeye akasema anataka alale kidogo. Akalala Tunda akiwa anachezea simu yake. Alipoamka, shuguli ya kuagana ikaendelea mpaka jioni ndipo alipomruhusu Tunda kuondoka. Akapanda basi la mwisho kabisa la kwenda kwa bibi yake huko mjini Morogoro, Uluguru na dad akarudi nyumbani. Tunda aliondoka na pesa nyingi sana alizokuwa amepewa na dad wake.
  

Tunda kijijini kwa bibi yake tena.
A
lifika usiku sana, na kumkuta bibi yake akimsubiria. “Mama yako anawasiwasi kweli! Alisema ulitakiwa kuingia hapa mchana.” “Poleni kwa kuwatia wasiwasi. Tuliposhuka kwenda kujisaidia nikaachwa na basi. Ikabidi nisubiri basi jingine, hapa nipo hoi.” “Pole sana.” Bibi yake alimwandalia maji yakuoga, Tunda akaingia kulala mara baada ya kuoga bila kula. “Nimechoka sana bibi. Nitakula kesho.” “Kweli utakuwa umechoka. Umeshinda juani siku nzima! Pole mama.” “Asante bibi.” Nikweli Tunda alikuwa amechoka. Alishugulishwa karibu siku nzima.

    Baba Tom alimwambia Tunda, kwa kuwa anakwenda kijijini na kumuacha pale peke yake, na mama yake hana uwezo wa kumridhisha, basi akataka Tunda amuache vizuri. Ni kweli Tunda alijituma na yule baba alimtumia kama anayejiandaa kuingia mfungoni. Kila alipomwambia Tunda hiyo ndio mara ya mwisho, waagane, aondoke, alipomaliza, alizidi kumbembeleza Tunda wabaki kidogo. Alibadilika kuwa mwema kwa Tunda. Na kwa kuwa Tunda hakutaka awe anamuudhi, basi hakuwa akibisha.

~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~

    Tunda alikuwa amebadilika sana. Bibi yake alibaki akimtizama bila kuchoka. Kila kitu chake kilikuwa kizuri, hata jinsi ya kuongea alibadilika. Mbali na hapo kuna mabadiliko yaliyomfanya bibi yake kuingiwa na wasiwasi asijue ni nini kinaendelea kwa Tunda. “Unapata muda na mama yako?” Bibi yake akamuuliza taratibu. “Hata kidogo. Ana mambo mengi huyo! Hatulii nyumbani. Na kama unavyomjua, hapendi hata kuiona sura yangu. Kwa hiyo tunapishana tu humo ndani.” Bibi yake alitulia kidogo, wakiwa jikoni akipika na Tunda akiandika jumbe kwenye simu yake.

    “Shule nayo vipi?” “Ipo.” “Najua ipo. Naulizia ipo kichwani au ni majengo tu?” Kidogo simu ya Tunda iliita na kutoka nje. Aliongea kwa muda mrefu sana, kisha akarudi ndani. “Alikuwa rafiki yangu. Ameniomba nikamtembele kwao.” “Wapi?” “Maeneo ya Chalinze.” “Wewe rafiki wa Chalinze, umempata wapi?” “Si na yeye ameenda kwa bibi yake huko kusalimia? Ni rafiki yangu kipenzi wa huko shuleni. Tunasoma naye darasa moja na tunafanya naye tuition pamoja. Wazazi wake wanaishi Dar, ila kwa bibi mzaa baba yake ni hapo maeneo ya karibu na Chalinze.” “Umemjibuje sasa?” “Nimemwambia mpaka nizungumze na mama. Naweza kushuka hapo Chalinze wakati narudi Dar.” Bibi yake akanyamaza.

    Nini sasa bibi na wewe!?” “Aaah! Kuwa tu mwangalifu Tunda. Maisha yako mwenyewe unayajua. Leo uko huku, kesho umerudishwa pale. Huna mahali pamaana pakuishi. Elimu ndio mkombozi wako Tunda. Achana na mambo yote kazana na shule mama.” “Usiwe na wasiwasi bibi. Kila kitu kipo sawa.” Bibi yake alinyanyua uso, akamtizama. “Nini sasa bibi jamani!?” Tunda alianza kucheka. “Naona huishi kunitizama!” “Nakuona ulivyobadilika Tunda!” “Kawaida tu bibi, wala usitie hofu.” Tunda alijibu, macho kwenye simu, akaendelea kutuma jumbe zake akamuacha bibi yake akimtizama na huku anapika.

    Baada ya juma moja tu kuisha, Tunda alimuaga bibi yake nakumwambia anarudi nyumbani kwa mama yake. “Mbona mapema?” “Lazima nirudi nianze kujiandaa na shule kabla hazijafungua bibi.” Bibi yake akaona ni jambo jema. Wakaagana, Tunda akaondoka.

~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~

    Alipofika kituo cha mabasi makubwa ya mjini Morogoro, kutokea kijijini kwa bibi yake, alikata tiketi ya kwenda Arusha kumfuata baba Tom, aliyekuwa ameondoka siku tatu zilizokwisha jijini Dar, kuelekea Arusha kikazi.

    Tunda alimkuta akimsubiri kituo cha mabasi jijini Arusha. Alifurahi sana alipomuona Tunda. “Usingenifuata huku, naona mimi mwenyewe ndio ningekufuata huko Tunda. Nilikuwa nakaribia kuchanganyikiwa! Ushanizoesha vibaya mwenzio!” Tunda akacheka kidogo.

    “Tutakaa huku mpaka lini?” “Tusiongelee kuondoka wakati ndio umefika. Acha nikufaidi kwanza. Unazidi kunenepa Tunda!” “Natunzwa vizuri je!”  Alijisifu mbele ya dad wake.

    Wakaelekea hotelini moja kwa moja. Baba Tom alikuwa akitetemeka kwa uchu. “Juma zima Tunda! Hali mbaya.” “Ngoja nikutulize dad wangu. Na hivi na mimi unanijali hivyo, sitaki uteseke.” “Ndio maana nakupenda Tunda mwanangu. Unanihurumia na kunija ja.. ja..” Maneno yakagoma kwani Tunda alishaanza utundu wake.

    Walijifungia hotelini hapo kwa siku tatu. Tunda akiwa amezima kabisa simu yake, akimwambia baba yake, hataki kelele za mama yake. Anataka akili zake ziwepo tu hapo hotelini akimuhudumia yeye. Akafurahia hilo wazo.
Na kwa kuwa Manda hakutaka kuharibu kwa mumewe, akaamua kumfichia siri mwanae, kila alipozungumza na mumewe, alimdanganya kuwa Tunda bado yupo kwa bibi yake kijijini. “Umezungumza naye lakini?” Baba Tom alimuuliza mkewe kwa sauti ya kujali. “Nakwambia kanogewa kwa bibi yake! Kagoma kurudi. Naona ananikwepa.” “Bora uzima wake tu. Na atulie huko huko kijijini. Sio kukaa hapo mjini vijana wakamchezea.” Baba Tom aliweka msisitizo. Tunda alikuwa akicheka tu kila alipokuwa akiwasikiliza wakizungumza kwenye simu.

    Kila Manda alipokuwa akipiga simu kwa mumewe alikuwa na matatizo ya kifamilia. Tunda alikuwa akimsikia akimlalamikia mumewe juu ya msichana wa kazi. Kuwa hatulii nyumbani, anazurula sana mtaani. Wakati mwingine anamuacha Tom kituo cha basi. Haendi kumcukua kwa wakati, na pengine anakuwa amemuaga Manda anaenda kumpokea mtoto. Tom anaishia kuzurula mtaani tu, au kukaa kituoni hapo peke yake.

    Siku nyingine alipiga simu Tunda akiwa amejilaza hapo pembeni ya baba Tom, mama yake akapiga simu akilia na kugomba kuwa alipigiwa simu na majirani Aneti amefungiwa ndani, analia dirishani, dada hayupo. Ikabidi yeye Manda atoke kazini kwa kukimbia, ndipo akamkuta Aneti amelia mpaka amekaukiwa. Basi Tunda akawa akimsikiliza tu mama yake akiwa analalamika hapo kwenye simu, mpaka wakaagana na mumewe.

    Au alimsikia kwenye simu zake nyingine akiwa anataka mumewe amrushie pesa kwa tatizo hili au lile hapo nyumbani. Basi hapo Manda atajieleza kwa hili au lile akitaka atumiwe pesa. Mumewe akimsikiliza tu. “Manda kwa pesa! Utafikiri hafanyi kazi wala hana miradi! Na akitaka pesa, hamalizi kujieleza. Atatumia kila uongo.” Baba Tom aliongea baada ya kukata simu, akiwa anamrushia pesa mkewe.

    “Nilikuwa niondoke kesho, naongeza siku nyingine mbele. Kesho itakuwa siku ya kupumzika tu, nijiandae na kelele zake nikirudi huko nyumbani.” Tunda akaongeza mara baada ya dad wake kurudi kujilaza hapo kwenye mto baada ya kutuma hiyo pesa ambayo Manda alitaka.

     Ndipo akaongeza siku nyingine mbele hapo hotelini. Ilikuwa ni hoteli kubwa sana ya kitalii ambayo baba Tom alikuwa amefikia hapo kwa ajili ya semina ya kitaifa, ya kazini kwao. Wafanyakazi wa ngazi za juu kwenye hilo shirika lao, kutoka nchi zote za Africa, walikutana hapo.

    Tunda alipata mapumziko mazuri, akiletewa vyakula hapo chumbani. Analala kuanzia asubuhi dad wake akienda kwenye mkutano, mpaka jioni anaporudi ndipo wanaungana pamoja. Wakati mwingine aliletewa mtu wa masaji huko huko chumbani mida hiyo ya mchana. Au Tunda alikwenda kupumzika kwenye Sauna. Ilimradi tu, starehe.

    Wakati huo Tunda alishakuwa binti wa miaka 17. Alishamfahamu dad wake vizuri, akamjulia, kwa hiyo alikuwa akimpatia sawia na kuzidi kumpagawisha ipasavyo. Hakuna jinsi ambavyo mtu angemwambia aachane na Tunda akaelewa. Au kusubiria kufikia mwili huo wa Tunda hata kwa siku moja akaelewa. Alikuwa na kiu zilizokuwa haziwezi kumsubiria Tunda zaidi ya masaa 24. Alimtaka Tunda, angalau kila siku. Hata kama kwa kifupi, basi angalau Tunda amtulize kila siku. Na siku anazopata naye muda, alikuwa anakuwa ni kama hajamshika mwaka mzima.

    Usiku huo wakuagana alimsifia sana Tunda na kumwambia ni mzuri katika kila kitu, kuliko mama yake. “Mbona yeye mweupe? Unanidanganya dad!” Tunda alilalamika kwa deko.  “Kwani weupe ndio nini? Huwezi kujifananisha naye hata kidogo.” Tunda alifurahi sana kusikia hivyo. Kuna kitu kipya kikajengeka ndani yake, akajikubali zaidi.

    Alikuwa ametamani kuanza kujichubua ili kuwa mweupe, lakini alijua kwa weusi alio nao, hata msichana wao wa kazi alimwambia labda anywe vidonge vyakubadili rangi sio krimu. Kwa hiyo akawa hajui tena chakufanya ili ajibadilishe rangi yake, japo bado shauku ilikuwepo na kuongezeka kila kukicha akitamani kuwa mweupe.

    Lakini usiku huo dad akawa ameongeza kitu kikubwa sana, baada yakumwaga sifa juu ya rangi yake, ngozi laini na nyororo. Alimjenga na kumtuliza Tunda, yeye asijue. Na alipoongeza kusema yeye ni bora kuliko mama yake mwenye rangi nyeupe,  hapo akawa ndio amemaliza kila kitu. Hapo hapo Tunda akatupilia mbali lile wazo la kujibadilisha rangi. Akajikubali vile alivyo na kutupilia mbali wazo la kutafuta vidonge vya kujibadili rangi. 

Tunda na Mama yake.
S
iku ya tano tokea aondoke kijijini ndipo Tunda akarejea nyumbani. Tena alirudi jijini na ndege, kutokea Arusha. Baba Tom alimsindikiza uwanja wa ndege mida hiyo ya mchana baada ya kuagana hapo hotelini kwa nafasi.

    Alipotua uwanja wa ndege wa Mwalimu Nyerere, akachukua taksii iliyompeleka mpaka nyumbani kwao Kitunda. Ilikuwa mara yake ya kwanza kupanda ndege. Alifurahia sana ule usafiri wa ndege. Na yote hayo baba Tom alimwambia ni kwa vile anavyomjali na kumthamini. Alirudi akiwa amejawa kiburi, huna utakalomwambia Tunda na kumtisha tena.

    Alimkuta mama yake amekasirika karibu kupasuka. “Ulikuwa wapi?” “Kwa bibi.” “Bibi yako alinipigia simu siku nne zilizopita, kuniambia uliaga unakuja huku.” “Nilienda kwa rafiki yangu.” Mama yake akamnasa kofi. “Utaniumiza mama jamani! Kwani kuna nini?” “Niambie ulikotoka.” “Kwani unategemea jibu gani mbali na hili? Mbona sikuelewi?” Tunda alimuuliza mama yake kwa jeuri. “Unanijibu hivyo mimi!?” “Ulitaka nikujibuje sasa? Wewe si umeuliza swali? Halafu umeanza lini kunifuatilia maisha yangu? Naomba nikapumzike.” Mama yake alishtuka sana.

    “Wewe Tunda!” “Nini? Yameanza lini!? Tokea lini umeanza kunifuatilia hata kujua tu hali yangu? Tumeishi wote hapa miaka yote! Sijawahi kukusikia hata salamu kwangu. Sasa hayo maswali ya leo na kibao juu, vinahusu nini?” Tunda alimuuliza kama anayemsuta, kisha akaondoka na kuingia chumbani kwake bila kusubiri jibu.

    Mama yake akamfuata nyuma. “Nimechoka sana, naomba niache nipumzike. Sitaki kelele.” “Unasemaje Tunda!?” Tunda alitupa mabegi yake chini na kumgeukia mama yake vizuri. “Unataka nini kwangu? Na kwa nini iwe leo!?” Yule mama alitulia kidogo.

    “Nimekuja hapa nipo darasa la nne. Hujawahi kuniuliza hata naendeleaje, leo unaniuliza nimetoka wapi!?” “Bibi yako ameniambia wewe ni mjamzito.” Tunda alishtuka sana, lakini hakutaka kumuonyesha mama yake.

    “Kwa hiyo?” Akamuliza mama yake kwa jeuri. “Nataka kujua kama kweli.” Tunda akacheka kwa dharau. “Wewe si ni nesi?” “Umeingiliwa na nini wewe Tunda!?” “Wewe ndio nikuulize umeingiliwa na nini? Siku zote tupo wote hapa, hata salamu hunipi kama hawa watoto wako wengine. Ukifungua kinywa chako kuniongelesha unanipa maagizo ya nini nikufanyie na matusi juu. Kama hutanitusi juu ya rangi yangu ya mwili basi ni juu ya haya macho yangu yaliyozubaa na kuyaita kama paka. Hujawahi hata kunipa shukurani kwa lolote nililowahi kukufanyia humu ndani zidi ya vitisho vyakunirudisha kwa baba yangu mzazi, wakati unajua niliteseka! Leo unauliza juu ya ujauzito wangu! Nikiwa nimekuja hapa mtoto mdogo sana, wewe unajua bikra yangu ilitoka lini?” Yule mama akanyamaza.

    Kama kitu kikamkaba Tunda kooni, akaanza kulia kwa uchungu sana. “Inawezekana bikra ni kitu kikubwa sana. Basi nikuulize wewe mama uliyenizaa mimi, hivi hata unajua kama nakula humu ndani au la? Unajua kama naenda shule au siendi? Ushawahi hata kushika daftari langu ukaangalia hata kama naandika huko darasani? Unajua ni mara ngapi nimeugua humu ndani nikaishia kuuguzwa na mumeo? Kila ukirudi kutoka kazini unawaita watoto wako, unawasalimia na kuongea nao. Ushawahi kufanya hivyo kwangu zaidi ya kunitukana weusi wangu na macho tu. Kwanza ulinitelekeza. Wala huna haja na mimi. Kwa hiyo naomba uniache.” “Ningekuwa nimekutelekeza ungekuwa hapa?” Mama yake akajikaza na kuuliza na kumpandisha Tunda hasira zaidi.

    “Acha kunifanya mimi mjinga wewe! Nakumbuka kila neno na tendo ulilonifanyia nikiwa mdogo. Nipo hapa kwa ajili ya baba Tom wala sio wewe. Ulienda kuniacha kwa baba yangu, bila hata kunitambulisha. Unajua mateso niliyopitia? Kwanza unakumbuka ulivyoninyanyasa njia nzima wakati unaenda kunitupa kwa baba yangu? Ulinipiga njia nzima, sababu simuhudumii Tom vizuri. Nilikuwa mtoto mdogo kama Tom, lakini uliamua kunitupa mimi huku ukinisimanga na weusi ambao Mungu alinipa wala sikuchagua.”

    Nilihitaji kujaliwa kama hivi unavyomjali Tom na huyu mtoto wako mwingine niliyekulelea bila shukurani. Naomba unipishe nilale.” “Hapa ni kwangu Tunda.” “Wewe umeletwa hapa na baba Tom kama mimi tu nilivyoletwa. Kwa hiyo usinisumbue. Aliyenileta hapa kutoka kijijini wala sio wewe, ni baba Tom. Yeye ndio anauwezo wakunitoa hapa. Ucha kufikiri unaweza kunitisha na vile vitisho vyako vya kitoto.” Tunda aligeuka na kuanza kuvua nguo ili akaoge.

    Manda alikuwa kwenye mshtuko, hakuwahi kumsikia Tunda akiongea vile. Kwanza hawakuwahi kuwa na mazungumzo ya namna yeyote ile, tena marefu, halafu Tunda akajibu. Alibaki ameduwaa kwa muda, kisha akaondoka. Tunda aliingia bafuni kuoga, akatoka na kujitupa kitandani akapitiwa na usingizi.

    Aliamshwa na kelele za Tom akimfurahia baba yake. Aliangalia saa ya ukutani, ilishakuwa saa tatu usiku. Alijigeuza na kulala tena. Baada ya muda tena alimsikia mama yake akiongea na mumewe huku akilia sana. Tunda hakutaka hata kujisumbua. Alijiweka vizuri na kupitiwa na usingizi tena.

~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~

    Asubuhi sana alikuja kuamshwa tena. “Tunaenda wote hospitalini.” Tunda alikaa. “Huwezi kunishtukiza. Lazima nikaoge.” “Nakusubiri. Lazima tuondoke wote.” Tunda alicheka kwa dharau na kuelekea bafuni.  Alitoka akamkuta mama yake amekaa kitandani kwake ameshika simu yake. “Naomba password ya simu yako?” “Hee! Kwa nini?” Tunda akamuuliza kwa mshangao huku anamcheka mama yake kwa kejeli. “Usinitanie Tunda!” “Tumeanza lini mimi na wewe kutaniana? Acha simu yangu.” Tunda akaenda kumpokonya. Manda naye akapokonya, wakavutana, ile simu ikaanguka na kupasuka kioo.

    “Umefurahi sasa?” Tunda akamuuliza mama yake kwa hasira. “Kwanza tulikupa sisi hiyo simu.” “Hukuwahi kunipa kitu hata kimoja. Hiyo simu alinipa baba Tom, tena ukiwa unamkataza. Ukataka uichukue wewe. Unafikiri sikuwa nakusikia?” Tunda akamuuliza mama yake na kuendelea. “Nakuomba unipishe nivae kwa uhuru.” Manda akatoka.

Tunda alivaa vizuri. Akajitengeneza ndipo akatoka. “Twende.” “Siwezi kuondoka na njaa. Mpaka nile.” Tunda alijibu huku akielekea jikoni. Akajitengenezea kifungua kinywa chake. Msichana wa kazi akicheka taratibu, lakini asiamini kama ni Tunda kweli, kwa mama yake!

    Baba Tom alishaondoka tokea alfajiri sana, kuwahi kazini. Hapo ndani alikuwa amebaki Tom, Tunda, shule zilikuwa zimefungwa. Wapo likizo ya mwezi wa kumi na mbili. Mama yao, Aneti na msichana wa kazi, ndio waliokuwepo hapo.

    Bila haraka, akajiwekea kifungua kinywa mezani, akaanza kula huku akijaribu kuwasha simu yake. “Huyo anayekupa hicho kiburi!” Manda akaongea wakati anamsogelea pale mezani. “Ni wewe mwenyewe, wala usimtafute mchawi wako.” Tunda alimjibu huku akiendelea kula. “Usinicheleweshe Tunda.” Tunda akamtizama huku anaendelea kutafuna taratibu. Manda akaamua kuondoka tu pale. 

Manda Shuleni kwa Tunda.
T
unda alipomaliza kufanya mambo yake bila haraka, ndipo wakaondoka hapo nyumbani. Siku hiyo walitumia gari ya mama yake. Kimya, hakuna anayemuongelesha mwenzake hapo garini. Tunda macho kwenye simu, Manda akiendesha. Manda akaamua kupitia shuleni kwa kina Tunda kwanza. Huko ndiko alichanganyikiwa kabisa baada yakuonyeshwa matokeo yote ya mwanae kuanzia kidato cha kwanza mpaka hapo anaposubiri kuingia kidato cha tatu. Tunda alikuwa akifanya vibaya sana darasani. Kuna mitihani mingine alikuwa anapata 2 au 1 ya 100. Sawa na sifuri.

    Akamgeukia Tunda aliyekuwa akisikiliza bila hata kushtuka na alikuwa akichezea simu yake. Manda alikuwa kwenye mshtuko ulioonekana usoni. Utafikiri ametua kwenye ulimwengu mwingine kabisa. “Kwani nyinyi hamuishi pamoja? Maana matokeo yake yalikuwa yakitumwa nyumbani kila mara.” Mwalimu wa taaluma akauliza baada ya kumuona Manda anakaribia kuchanganyikiwa. Tunda alicheka kwa sauti. “Swali la msingi sana hilo mwalimu. Umesikia hilo swali mama au nikuite mama Tom?” Tunda aliuliza huku anacheka. Manda kimya.

    “Naomba tusipoteze muda hapa, ukitegemea kuvuna kitu ambacho hakijawahi kupandwa na wala hukujaribu kumwagilizia. Kwanza nashangaa. Wewe si unaniita mimi mjinga kama baba yangu? Sasa unachoshtuka hapa nini? Acha usanii.” Tunda akasimama na kutoka nje.
Mama yake akamkimbilia. “Lazima twende hospitali Tunda.” “Kufanya nini?” “Nataka nikakupime, ili nijue kama wewe ni mjamzito.” “Ili ufanyaje?” “Nataka kukupa nafasi ya pili ya maisha Tunda.” Tunda alishangaa sana.

    “Ujue mimi sio mjinga sana kama unavyonidhania? Unipe nafasi ya pili, nani alishanipa ya kwanza!? Ni heri ungeniacha tokea mwanzo kule kijijini na bibi, ukaongeza kutuma pesa kama kina mjomba walivyokwambia, kuliko hivi ulivyoharibu maisha yangu. Mmenileta mjini, mkaninyanyasa kama niliyepanga kuzaliwa na nyinyi, zaidi wewe. Unaninyanyasa kadiri uwezavyo na kuacha nikilelewa na mwanaume ambaye sio baba yangu! Hivi hata unajua ni lini nilivunja ungo?” Manda kimya.

    “Nauliza tu. Au hata unajua nani anayeninunulia pedi ninapoingia kwenye siku zangu?” Kimya. “Naomba usinipotezee muda, nirudishe nyumbani.” “Mimba ya nani?” “Mwanaume.” “Najua ni ya mwanaume Tunda. Nataka jina lake.” Tunda akazidi kumshangaa mama yake na kuumia zaidi.
“Yaani hilo ndilo swali pekee na la muhimu unaloona unafaa kuniuliza sasa hivi tokea unanizaa!?” Tunda akamuuliza kwa mshangao, kisha akaingia garini.
Tunda na mama yake Hospitalini.
    Mama yake hakumrudisha nyumbani. Aliendesha mpaka kazini kwake. Akamwambia lazima ashuke hapo. Tunda akashuka. Wakaelekea ndani ambako mama yake anafanya kazi. Mama yake akamuacha amekaa ndani ya kiofisi kidogo, yeye akaingia kwenye chumba kingine na kaunza kuzungumza na manesi wenzake. Tunda aliinama na kuendelea kuchezea simu yake bila kuwajali. Alijua wanamsema yeye.

    Baada ya muda mrefu sana, aliitwa kwenye chumba na kuombwa mkono. Hakumbishia baba mtu mzima aliyehisi ni dokta. “Naomba usibiri hapa hapa.” Yule daktari aliongea na sura ya kijeshi.

     Baada ya muda yule daktari alirudi na majibu, akakaa kiti cha mbele, kwenye meza ya mbele alipokaa Tunda. “Unajua kama wewe ni mjamzito?” Tunda alinyanyua uso wake na kumtizama yule daktari bila kujibu kitu. “Hivi unajua kama unayaharibu maisha yako? Unakubali kudanganywa sasa hivi wakati unamaisha mazuri sana mbeleni!? Unataka kuacha shule sasa hivi ili uzae! Ushafikiria maisha yako lakini? Hivyo ulivyo na katoto kachanga!” Tunda alibaki akimtizama yule dokta huku akipandisha hasira. Yule daktari alizungumza kwa muda mrefu akimlaumu Tunda, kwa maneno aliyoambiwa na mama yake. Tunda alibaki akimtizama tu mpaka na yeye akanyamaza.

    “Umemaliza dokta?” Tunda akauliza kwa ukali kidogo. Kimya. “Nakuuliza tu.” “Nil..” “Nini? Unanijua mimi? Au unanijua kwa kile ulichoambiwa na mwanamke aliyenitambulisha kwako kama mimi ni mtoto wake? Nafahamu wazi utakuwa ukiwafahamu watoto wake wawili. Tom na Aneti. Wewe jiulize tu, kama mimi ni mtoto wake, na wewe ni mfanyakazi mwenzake aliyenileta kwako sasa hivi, mbona hujawahi kuniona kabla wakati na mimi ni binadamu huwa naumwa kama yeye au watoto wake wengine ambao huwa anawaleta hapa hospitalini! Kwa nini iwe leo?” Kimya. “Acha kuongea kwenye maisha ya mtu usiyemjua. Umemuuliza hata kama anajua ni lini nilivunja ungo? Anajua hata kama nina..” Tunda akatulia kidogo. “Unajua nini? Unanipotezea muda wangu. Acheni kuhukumu msiyo yajua.” Tunda alisimama na kutaka kutoka. Wakaingia wauguzi wengine wanne mle ndani na kumchoma sindano kwa nguvu, Tunda akiwa na mshangao ni nini kimemtokea, akapotelea usingizini.

    Hakujua kilichoendelea wala ni wapi alipelekwa baada ya kupoteza fahamu. Lakini akiwa amelevywa na ile sindano yenye dawa, alisema aliyempa mimba bila hata yeye mwenyewe kujua. Mama yake aliumia sana. Haikuwa nia ya Tunda kumtaja baba Tom. Alitaka asimtaje kabisa, ila aje amwambie mwenyewe baba Tom kama ameshika mimba, ili waendelee na mipango yao kama alivyokuwa amekwisha kumuahidi.  Maana kila alipokuwa akimuomba mapenzi siku za hatari za kushika mimba, na Tunda akimsihi amsubirie mpaka amalize ndipo waendelee, baba Tom alilazimishia. Alisema hizo ndio siku na yeye anazipenda. Joto la Tunda linakuwa juu zaidi. Hawezi kusubiri wala kutumia kondomu.

Alishampa mpango mzima wa nini chakufanya endapo atashika mimba. Alimuhakikishia kumtunza vizuri sana wala hatamtupa kama ikitokea mambo yanajulikana au kuharibika. Alimwambia atamtoa pale kwenye kelele ya mama yake. Atamtafutia sehemu nzuri ya kuishi, na gari nzuri zaidi ya mama yake. Atamfungulia biashara yeyote anayotaka yeye Tunda. Na mapenzi yao yataendelee kama kawaida tena kwa uhuru wote. 


Mkasa mzito kwa Tunda.
T
unda alishtuka kutoka usingizini na kujikuta wodini na maumivu makali sana ya tumbo. Tunda alianza kuhangaika pale kitandani, akagundua anatokwa na damu nyingi sana kama bomba. Wakati bado taarifa haijafika vizuri kichwani, nesi akamsogelea na kumkabidhi barua. Akiwa kwenye mshangao, akaifungua. Ilikuwa karatasi ya wazi tu. Haikuwa hata kwenye bahasha.

‘Nimarufuku kukanyaga nyumbani kwangu tena, shetani wewe. Na kama baba Tom ndio alikuwa akikudanganya ulipokuwa naye kitandani, basi ujue hataki kukuona tena. Usiwahi kurudi tena hapa nyumbani kwangu. Ndio ujue mimi ndiye niliyekuleta hapa duniani na ndiye mwenye ndoa takatifu ya kanisani, wewe ni mchezewaji tu. Na kwa taarifa yako, namsamehe mume wangu, tunaendelea na maisha yetu kama kawaida. Na bibi yako amejua uchafu wako wote, hataki kukuona tena kule kijijini. Ukitoka hapo hospitalini, tafuta pakwenda, usikanyage tena nyumbani kwangu. Wewe si mwanamke kama mimi, sasa tafuta kwako. Nimemtoa huyo mtoto, mume wangu hataki kuzaa na wewe. Ndio ujue wewe ulikuwa upepo mchafu, umeshapita kwenye maisha yetu. Sitaki kukuona tena wala usinitafute mimi au wazazi wangu. Iwe mwisho na mwiko.’

Tunda alibaki akiitazama ile karatasi, asiamini kinachomtokea. Maumivu yalikuwa makali, na hapakuwa na dalili yakupewa hata dawa ya maumivu. Ni kama wauguzi wote walijua kinachoendelea, wakawa wakimpita wakiwa wanahudumia wengine. Kila alipojaribu kugeuka, alishindwa. Tumbo lilikuwa likimuuma sana. Alijua wazi amelowesha hata shuka la chini kwa damu iliyokuwa ikimtoka, lakini hakujua chakufanya. Akabaki akilia pale kwa uchungu bila msaada.

~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~

Tunda yupo hospitalini peke yake, akiugulia maumivu yakutolewa mimba. Manda ametangaza kumsamehe mumewe, wanaendelea na maisha yao kama kawaida. Tunda ndio kwanza binti wa miaka 17. Anakwenda wapi wakati hata kijijini kwa bibi na babu yake amefukuzwa.
Kwa baba yake alitolewa akiwa amezimia. Hajamuona baba yake mzazi tokea yupo darasa la 4.
Hana alijualo kwenye maisha isipokuwa mapenzi aliyoanza tokea mtoto mdogo sana.
Kwenye jamii, Tunda ni msaliti, Mtoto ambaye hana haya na muharibifu awezaye kulala na baba yake! Ajuaye ukweli ni yeye na baba Tom tu.
Lakini lazima maisha yaendelee.
  v Je, ni nani wakumsaidia tena Tunda?
Kwa majibizano ya mwisho kati yake na mama yake, Tunda si mbakwaji hata kidogo. Alikuwa jeuri zaidi ya mama yake alivyomfahamu. Pengine hormones za mimba, au pengine alijibu sababu ya machungu aliyokuwa akipitia na mama yake akiwepo au pengine ahadi alizokwisha pewa na baba Tom ndizo zilipandisha kiburi na hasira zilizompelekea kumjibu mbovu mama yake! Hakuna ajuae kilichojaza moyo wa Tunda, isipokuwa yeye mwenyewe Tunda aliyepita huko. 

  v Ni mapito gani atayapitia kwa doa alilojiingizia kwenye jamii, kushika mimba ya baba yake wa kambo?

  v Nini atafanya Tunda?

Endelea sehemu ya 5.

CONVERSATION

0 Comments:

Post a Comment