Naomi Simulizi |+1 205 767 8163 |naomisimulizi@gmail.com Nilipotea! - SEHEMU YA 8. - Naomi Simulizi

Nilipotea! - SEHEMU YA 8.

  

Maisha ya Tunda Mtaani.

T

unda akiwa pembeni ya kituo hicho cha Mwenge, kwenye moja ya sehemu wanayouza chakula, akisubiria chakula chake kiletwe, akiwa amejiinamia, akasikia wale wahudumu wakisemezana kama walio paniki na kuingiwa na hofu. “Wewe ndio alisema upeleke.” “Hakutaja jina bwana! Alisema mmoja wenu alete.” “Sasa mmoja wenu ni nani kama sio wewe ambaye unashika pesa za mama hapa!” Mwenzie akauliza kwa kumshangaa. “Sasa wewe si ndiye uliyepokea simu!?” “Kwa hiyo!? Tunda akawasikia wakiendelea kubishana.

“Sasa anakuja mzee mwenyewe! Nyinyi endeleeni kubishana hivyo hivyo!” Msichana aliyekuwa akigawa vinywaji na kusafisha meza, alisikika kuingilia mazungumzo ya hao vijana wawili. “Ni nini kigumu huwa hamuelewi nyinyi!” Ilisikika sauti upande wa kuingilia. Ikizungumza kwa ukali kidogo. Tunda akanyanyua kichwa na kumtizama huyo anayegomba na kuogopwa. Maana kulizuka ukimya kwa wale wahudumu wote. Tunda akajua ndiye huyo Mzee. Alisogea mpaka karibu kabisa na pale alipokaa Tunda, akavuta kiti pembeni yake akakaa.

Hakuwa Mzee kama walivyomsema. Ila alikuwa mtu mzima. Kijana mkamilifu tu. Alionekana ni kama anasogelea miaka ya 50, lakini bado hajafika  huko. Akajua huo uzee ni wa pesa. Mmoja wa wale wahuhudumu  akamsogelea. “Samahani sana. Nilikuwa nimletee mama. Lakini tumekuwa na wateja wengi sana. Nisingeweza kumuachia Udi na Sande peke yao. Nilitaka wateja wapungue, ndio nilete.” Tunda akamgeukia kwa kujiiba yule baba aliyekuwa anaombwa msamaha na kupewa maelezo kwa heshima zote, akaonekana kuelewa kidogo. Yule kijana akaendelea kujieleza. Katika mazungumzo yao Tunda akajua mkewe ndio mmiliki wa ile biashara pale, yeye amepita tu kuchukua pesa baada ya wale wafanyakazi wa pale, kushindwa kumpelekea pesa mkewe kwenye biashara yake nyingine.

Tunda akaendelea kusikiliza kwa makini. Akavutiwa na muonekano wa yule baba. Alionekana anajielewa. Jua kali vile, lakini bado alionekana msafi, halafu kwa umri ule kuwa amevaa safi vile mchana huo, akajua ameacha gari tu mahali na pesa ipo. Akavutiwa kumsikiliza zaidi. Akili zake zikahamia hapo kwenye mazungumzo yake na huyo muhudumu wa hapo. Akasikia na yeye anatafuta mtu mwingine atakayeweza kufanya kazi kwenye baa yake ya Sinza. Wazo lilimjia Tunda, aombe kazi. “Lakini akinipa kazi, nitaishi wapi? Sina hata pakulala usiku wa leo!” Tunda akajiuliza mawazoni mwake.

Wazo la pili la harakaharaka likamjia, la kumtongoza yule baba. Aliona anakabidhiwa pesa nyingi tu. “Sasa kama hiyo pesa yote ni ya mkewe, yeye atakuwa akiingiza kiasi gani!” Tunda akawaza na kuzidi kuvutiwa na kuafikiana na  wazo la kumtongoza na si kuomba kazi. Akajifanya kama hakuwa amesikia chochote.  Akamgeukia mara baada ya yule muhudumu kuondoka. “Mbona hunywi kitu chochote?” Tunda akamuuliza kwa sauti ya kujali. Yule baba akamgeukia Tunda kama asiye na ukakika kuwa anamsemesha yeye. Akakutana na macho matulivu ya Tunda yakimtizama kumuashiria anazungumza naye.

“Jua ni kali  sana. Kunywa hata maji, mimi  nitakulipia.” Tunda akaendelea  kuzungumza naye kwa sauti tulivu  ya ukarimu. Akaanza kumvutia.  Akatulia kidogo kama aliyepigwa na butwaa na yale macho ya Tunda.  Tunda akajua tayari. Akamtolea tabasamu kama kumshtua. Yule baba akagutuka kidogo. “Asante binti. Nimetingwa na mambo mengi, nashindwa hata kujifikiria! Nashika hiki, hiki kinaachia. Ukifanikisha hapa, pale panaachia! Unajikuta unahitajika kila mahali!” Akalalamika. “Pole sana. Lakini  afya yako ni muhimu.” Yule baba ikabidi kumtizama Tunda kwa makini.

Kwa haraka ili kumpumbaza zaidi  akaunganisha. “Kunywa kwanza maji, halafu ndio uniambie kinacho kupeleka kasi hivyo!” Tunda aliendelea kuzungumza kwa sauti tulivu yakujali na kumuwekea yale macho yake mama yake aliyokuwa akiyaita ya paka na yamezubaa. Akamuona yule baba anasogeza kiti upande wake, halafu kama aliyejishtukia akakirudisha palepale kilipokuwa amekaa mwanzoni. Tunda akatabasamu na kuinama.  

~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~

 Kwamba kama macho yake ni kivutio! Hilo alilijua baada ya kuanza shule akiwa anaishi kwa mama yake. Akijua kweli yeye ni mbaya wakupitiliza, kama mama yake alivyokuwa akimtukana. Akaja kugundua watu wengine wanapenda macho yake. Hakuacha kusifiwa na wanafunzi wenzake tokea anafika mjini kuwa ana macho mazuri na sauti nzuri. Kadiri alivyokuwa akikua, ndivyo sifa zilivyozidi. Wanafunzi wenzake, wakike na wakiume alisikia wakimjua na kumueleza kama msichana mwenye macho mazuri.

Hiyo ndio ikawa sifa yake na kitu kinachomtambulisha hapo shuleni kwao. Ukisikia jina la Tunda tu likitajwa hapo shuleni kwao, basi sifa ya macho inafuata. Hilo likamshangaza sana Tunda aliyekuwa akijua anamacho mabaya sana. Likamjengea ujasiri. Ndipo sasa akaanza kujifunza kuyalia pozi na kutengeneza sauti yake kuwa ya chini na taratibu. Na kwa kuwa hakuwa akisikilizwa nyumbani na wala hachangii chochote darasani, haikuchukua muda kuifanya sauti yake kuwa atakavyo Tunda.

Na alikuwa akiamua kuyatumia macho hayo na sauti yake ya utulivu, kukulainisha, ilihitajika mwanaumkwelikweli kutoka. Ni moja ya vitu vilivyokuwa vikimchanganya hata baba Tom. Hakuacha kusifia na macho yake. Basi Tunda alianza kutumia kwa makusudi kama silaha yakuchanganya vijana japo hakuwahi kuwakubali kwa kumuhofia baba Tom. Basi kabla hajasimama na mtu kutizama kaumbile kake, Tunda alianza kwa kutumia macho yake na sauti.

Mwalimu aliyekuwa akimfundisha tuition ya Kifaransa ndio alikuwa akimuona jinsi anavyopagawa. Alipogundua kuwa Tunda ni mkimya. Wanaweza kuanza kusoma mwanzo mpaka mwisho na hajachangia chochote, akatengeneza mazingira ya kumfundisha peke yake. Akazungumza na baba yake, ili kumsaidia zaidi. Akamwambia baba Tom kuwa Tunda ni wale wanafunzi wanao hitaji msaada wa karibu, ni ngumu kujifunza na watu wengi. Na kwa kuwa baba Tom alijua Tunda anapenda Kifaransa, ili kumfurahishTunda, akakubali tution ya yeye peke yake na huyo mwalimu tu. Hakuishia hapo. Walipopata hiyo nafasi yakujikuta wawili tu, akaanza kutengeneza mazingira yakumzoea zaidi Tunda.

Wakati mwingine alianzisha mazungumzo nje kabisa na kile anachomfundisha. Tena katikati ya kumfundisha, ili tu azungumze na kumtizama. Tunda aliligundua hilo, na alishavutiwa naye kwani alikuwa kijana zaidi ya baba Tom, mzuri, mcheshi, lakini asingethubutu kumkubali kwa kumuogopa baba Tom, japo  alishakaribia kutaka kumbusu TundaAlishamsogelea mpaka kabisa midomoni, Tunda akasimama kwa haraka akiwa na yeye  ameshashawishika kabisa. Alimuomba msamaha Tunda na  kumsihi asimwambie baba yake ambaye walikuwa wakifahamiana. Tunda akamwambia asijali, hata yeye angependa kuwa naye, lakini mazingira hayakuwa yakiruhusu.

Akiwa kidato hicho hicho cha pili wakajenga urafiki wakaribu sana. Wakisifiana kwa hili au lile, lakini yeye zaidi alisifia macho na sauti ya Tunda na kuishia wakicheka mambo ya kawaida na kumtaka Tunda awe anaongea chochote. Ndipo Tunda alipojenga ujasiri wakutengeneza sentensi za Kifaransa. Japo kwa kukosea, lakini akawa anafurahia na kumrekebisha. Ndio chanzo cha Tunda kufahamu lugha hiyo kwa kiasi. Ni hiyo tution pekee na ya kingereza ambayo hakuruhusu baba Tom aingilie. Hakuwa akikosa hata mara moja ili tu akakutane na huyo mwalimu aliyekuwa  kijana, akimsifia sana macho na sauti yake.  

~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~

     “Unafanya nini hapa?” Akamuuliza Tunda kwa sauti ya chini kidogo. “Hapa napumzika tu. Njaa imeniuma wakati nazunguka na madalali. Natafuta chumba. Kule ninapoishi mwenye nyumba ananisumbua sana na maswala ya mapenzi. Sina raha! Kwanza chumba chenyewe kidogo, halafu kodi yenyewe anapandisha kila kukicha!” Tunda alijilalamisha. “Kumbe unaishi peke yako?” Tunda akacheka kidogo. “Kwa umri huu, natakiwa kuishi na nani?” Yule baba akazidi kuvutiwa. “Kama hutajali tunaweza kwenda kuzungumzia kwenye gari, hapa wafanyakazi wa mke wangu wananitizama.” Tunda akatabasamu na kujaribu kuwaangalia wale wahudumu, kisha akarudisha macho kwake. 

“Kula basi kidogo.” “Acha nichukue basi hata soda, tuondoke zetu.” Tunda akajua tayari ameshamkamata. “Na mimi nasubiria chakula changu.” “Basi utanikuta nikikusubiria upande wa kushoto wa hili banda. Akamuelekeza aina ya gari yake na wapi amkute. “Sawa.” Wakakubaliana. Akachukua soda yake, akawaaga wale wahudumu wa mkewe, akaondoka.

Kweli, Tunda akafungiwa chakula chake, akalipia na kuondoka kwa haraka kumfuata yule baba. Kama aliyekuwa anahofia Tunda atamkimbia, alimkuta akimsubiria pembeni tu hata hakufika kwenye  gari. Tunda akacheka moyoni. Wakaongozana mpaka kwenye gari yake.

Walipofika kwenye gari akamuona anababaika hajui aanzie wapi kuomba penzi. Gafla akapoteza dira, hajui pakuanzia. Akabaki akichekacheka na kuumauma maneno hata gari likamshinda kuwasha. Tunda akaamua kumsaidia. “Uliniahidi utaniambia kinachokuchanganya na kukufanya ushindwe kujifikiria wakati wewe bado damu inachemka kabisa.” Tunda akadai kwa kubembeleza. Akacheka kufurahia kusikia damu inachemka. “Naruhusiwa kukutengeneza vizuri?”  Tunda akauliza tena kabla ya kujibiwa swali la kwanza, tena kwa upendo huku akimtizama. 

“Wapi?” Akauliza kwa wasiwasi huku akijiangalia wapi hajakaa sawa. Alikuwa amevaa tisheti ya rangi ya bluu. Akajitazama hakuona tatizo. Akajitizama tena na tena hakuona tatizo. Tunda alipomuona anazidi  kubabaika, akarusha swali la tatu kabla hata hajajibiwa la kwanza na la pili. “Kwani kuna mipaka?” “Hapana, ruksa kabisa. Hamna mipaka.” Gafla yeye akasikika mdogo mbele ya Tunda. Tunda akatabasamu huku akimtizama. “Nitengeneze tu.” Akamsisitizia Tunda akibembeleza.

Tunda akanyoosha mkono wake moja kwa moja kwenye zipu ya suruali yake. Akaanza kumchanganya mpaka akaamua wakatafute chumba kwenye nyumba ya kulala wageni. Tunda alifurahia sana moyoni. Akaondoa gari pale alipokuwa ameegesha nyuma kabisa ya kituo hicho cha Mwenge, karibu kidogo na hosteli za wanachuo njia ya kwenda Sinza. Tunda akaanza kula. “Tunakwenda wapi sasa?” Tunda akauliza kwa utulivu. “Sehemu ambayo hatutasumbuliwa.” Tunda akacheka taratibu, na kumuwekea chips yai kidogo mdomoni. “Wewe ni mkarimu!” Akamsifia Tunda, Tunda akacheka tu. “Lakini usinipe tena. Wewe kula tu. Mimi nilishakula.” “Unauhakika?” “Kabisa. Sawa.” “Nashukuru lakini.” Akamgeukia na tabasamu usoni.

Tunda akaendelea kula huku yeye akiendesha. Alimpeleka kwenye kijihoteli kizuri, kilikuwa kimejificha mitaa ya Mikocheni B. Mwanzoni Tunda alidhania ni nyumba ya mtu. Kwani ilikuwa katikati na makazi ya watu. Lakini ilizungukwa na majumba ya uhakika yenye mageti yao marefu. Hakuona hata mtu akizurula hapo mtaani. Yule baba akaingiza gari yake mpaka ndani kabisa. Akashuka yeye, wakati Tunda akimsubiria ndani ya gari. “Huyu atakuwa mwizi mzoefu!” Tunda akawaza akiwa peke yake pale kwenye gari.  

Baada ya muda akarudi. “Nimeshapata chumba. Twende.” Tunda akakusanya ile mifuko aliyokuwa amewekewa chakula, akashuka. Akafunga gari yake kwa rimoti ya mkononi, akaongoza njia, Tunda akimfuata nyuma. Kwa kuwa alishakula, walipoingia tu

chumbani akameza dawa ya maumivu kwa ajili ya lile bega lililokuwa likimpa maumivu kiasi. Kisha akaingia kazini. Kwa muda mfupi aliokuwepo naye pale kitandani, akijituma kwa juhudi zote kumpa ya ukweli, akihakikisha anamchanganya vyakutosha ili kumfanya asitamani kuondoka pale na atamani kurudi tena. 

“Nitakuona lini tena?” Akamuuliza kama anayemuomba siku ile isiwe mwisho. “Umenichanganya mpaka nimesahau kukuuliza jina!” Tunda akatoa tabasamu la ushindi. “Naitwa Ani.” “Nitakuonaje Ani?” “Wameniibia simu. Tena ni jana tu wakati nazunguka mitaani na madalali nikitafuta chumba!” Tunda akajilalamisha. “Lazima tutafute simu nyingine. Lakini tukiachana hapa, nitakuonaje tena?” Huduma aliyotoka kupewa hapo akazidi kumtamani Tunda na kuona anamuhitaji zaidi.

Tunda akajua ameshamkamata. “Wewe tu.” Tunda akajibu huku akijisogeza tena.  “Mimi nataka nikuone tena Ani. Tafadhali sana.” “Ningekuwa na simu, na sehemu yakueleweka yakuishi, ingekuwa rahisi kupanga mipango yakueleweka. Lakini hata sijui kama nitafukuzwa pale au la! Yule Mzee ananisumbua! Sina raha. Halafu nahisi ni tamaa tu. Anao  wake wawili, na bado ananitaka na mimi! Ananilazimisha niwe mke mdogo.” “Haiwezekani!” “Kweli. Halafu naogopa, wakati mwingine anaweza kuja mpaka pale kwenye nyumba yake akijua wapangaji wengine hawapo. Akinibaka!” Tunda akajilalamisha huku akimchezea yule baba taratibu.

“Aisee hapo ni pakukimbia kabisa.” “Ndio nilikuwa nafikiria labda nirudi tu kwa bibi kijijini.” “Hapana. Yule baba akashtuka sana. “Sasa niambie nafanyaje hapa mjini? Hata simu tu ya mawasiliano sina!” Tunda akakaa akiwa uchi kabisa. “Mbona simu sio tatizo kabisa!  Naweza kwenda kukuchukulia hata sasa hivi! Na kwakuwa hapa panaonekana ni patulivu, unaweza ukapumzika tu hapa kwa siku chache mpaka tutakapopata chumba kizuri utakachopenda. Huwezi jua ni kwa nini tumekutana leo! Tafadhali usiondoke kwa haraka. Tutafikiria pamoja chakufanya.” Kweli? Maana usije ondoka hapa ndio ukawa umeniacha mimi moja kwa moja!” “Sithubutu. Mimi nakuhofia wewe. Usije nikimbia Ani, utakuwa umenionjesha tu halafu..” Tunda akamkalia tena yule baba akiwa amejilaza pale kwenye kitanda ameegemea mto, akamuona anababaika tena. Akashindwa hata kutoa neno linaloeleweka.  

Tunda alikuwa akimcheka sana moyoni jinsi alivyokuwa anaweweseka, alihisi lazima ni mshamba au hakuwahi kukutana na wakumpagawisha kwa kiasi kile. “Ila hapa amewezaje kupata chumba kwa urahisi hivi au tu amepajuaje!? Maana hapa jinsi  

Palivyojificha! Huwezi kukamatwa wizi labda mtu awe anakufuatilia.” Tunda aliendelea kuwaza wakati akimzungusha kwa mara nyingine tena pale kitandani kwa hili na lile muda huo wa mchana, jua kali nje na ilikuwa siku ya kazi. Tunda aliporidhika kuwa amemuweka sawa na lazima atarudi tu, ndipo alipomuachia. Alimuachia pesa nyingi sana, huku akimbembeleza asimtoroke.  

“Tafadhali nikukute Ani.” “Sasa niende wapi na wakati nimekwambia hali ya ninapoishi!? Nasubiri tufikirie kwa pamoja kitu chakufanya. Wawili ni wawili tu.” “Hapo umenena. Na mimi huko ninapokwenda, nitaanza kukuulizia sehemu. Lakini nataka iwe sehemu tulivu ili tusiwe tunasumbuliwa.” “Na sasa sio unitafutie sehemu za mbali, halafu unaniacha nyumbani peke yangu, unashindwa kuja kunitembelea!” Hilo likazidi  

kumchanganya yule baba. “Yaani nitamiliki mimi mwenyewe! Akauma meno huku akimtizama Tunda asiamini kama ndio hana mpango wakumuwekea mipaka! Kwamba na yeye anataka kuwa naye! Akazidi kuona amebahatika siku hiyo kumpata Tunda.  

“Siwezi kukuacha peke yako Ani.” Tunda akacheka kwa deko.  “Twende ukaoge ndio utoke. Usitoke hivyo.” “Yaani unanisindikiza!?” Hakuamini. “Sasa nani anakusugua huko bafuni. Nataka nikuoshe vizuri, sio ufike mbele za watu unanuka.” Akazidi kumchanganya. Tunda akatoka hapo akielekea bafuni, bila hata shuka. Akamsikia anaruka pale kitandani anamfuata kwa haraka. Baada ya fujo zakutosha za Tunda za huko bafuni nako, Tunda akamfukuza.

“Ulisema unatakiwa kwenye baa yako ya Sinza. Nenda kazini, mimi utanikuta nakusubiria.” Akachekacheka kama mjinga mbele ya Tunda.” “Naamini nikirudi  tutapata muda mzuri zaidi.” “Uwahi sasa! Sitaki kukuingiza kwenye matatizo huko nyumbani.” Hilo nalo akalifurahia kuwa anajali na kuheshimu maisha yake. Wakatoka hapo bafuni, akaanza kumfuta maji mgongoji huku wamekaa kitandani. “Ningekuwa na mafuta yangu hapa, ningekupaka. Lakini sina.” “Basi itakuongezea pesa zaidi ukanunue. Lakini yangu usinunue yenye harufu kali.” Tunda akacheka na kumbusu mgongoni. “Siwezi bebi. Sitaki kukuingiza matatizoni.” Gafla anaitwa bebi! Hilo nalo akapenda.  

~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~

Alimuacha Tunda pale chumbani  yeye akatoka kwa kufukuzwa na Tunda. Alishataka kuahirisha, abaki naye, Tunda akamkatalia. Alibaki pale kwenye kile chumba kizuri, kisafi, akifurahia kutengeneza pesa ya haraka haraka kwa kiasi kile. Maana yule baba alijitutumua na kumuachia pesa karibia yote aliyopewa pale kwenye ile biashara ya mkewe, Mwenge. Tunda  alizihesabu zile pesa huku akicheka. “Na simu amesema ataniletea!” Tunda akawaza huku akizirusha zile pesa juu. Zikasambaa chumba chote na pale kitandani. Akaendelea kucheka huku akigaragara na zile pesa pale kitandani. “Nimelala masikini, nikiteswa na kipigo juu, nimeamka tajiri kilaini!” Tunda hakuamini.

Akaamua ile ndio iwe biashara yake. Na akakusudia yule baba ndio  atakuwa mteja wake wa kwanza. Angalau amtumie hapo mwanzo, wakati akijipanga zaidi. “Nitambana huyu, mpaka asijielewe. Atamwaga pesa hapa bila kujijua.” Tunda aliendelea kumpigia mahesabu. Na kwa kuwa alionekana nimtoaji, akajua mambo yake yamekuwa sawa.  

~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~

     Wazo la kujitengeneza likamjia. Tunda mpenda mwili wake. Baba Tom alishamzoeza saluni na kujipendezesha. Akaona asilale. Atoke pale. Akakusanya pesa yake yote mpaka chini ya uvungu.  Akapiga simu mapokezi kwa kutumia simu ya mezani, kuomba aitiwe taksii. Taksii ilipofika, muhudumu akampigia simu kumtaarifu. Akatoka na kurudi Mwenge. Kitu chakwanza akatafuta saluni ili wamtengeneze nywele ambazo ilishapita miaka miwili, hazijatengenezwa vizuri kitaalamu zaidi ya Nyange kumsuka twende kilioni tena usiku wakiwa wamechoka wanataka kulala. Na alishakaa hospitalini muda mrefuSiku hiyo aliyoporuhusiwa, asubuhi hiyo, akiwa hospitalini kabla yakutoka, alioga na kuzichana kama kawaida, na kuzifunga upande mmoja tu. Kwa hakika alihitaji huduma nzuri ya kitaalamu.

 Dada aliyemkuta pale saluni alikuwa mcheshi sana. Tunda akaomba amtengeneze vizuri na kumwitia mtu  wakumtengeneza kucha akiwa  anamuhudumia. Bila kuchelewa kijana wa kucha akaingia hapo. Baada ya kuoshwa vizuri nywele zake ambazo hazikuwa na dawa, wakati anatengenezwa kichwani, yule kijana wa kucha akaanza kumuosha miguu. Kazi mbili kwa wakati mmoja zikaanza. Urembo wa nywele na kucha. Alimshonea wiving fupi. Akaikata kwa mtindo uliompendeza sana Tunda. Nakufanya uso wake wa mchongoko kuonekana vyema zaidi. Usingeweza kumtambua Tunda huyu na yule aliyekuwa amelazwa hospitalini  masaa machache yaliyopita au yule aliyekuwa mtumwa nyumbani kwa shangazi yake.

Kijana wa kucha naye akawa amemtengeneza vizuri kucha za miguuni, akambandika kucha nzuri kwenye vidole vya mikononi. Tunda alitoka hapo akiwa wa tofauti sana. Akaingia sasa madukani, akiwa nadhifu. Akajinunulia mafuta mazuri,{Lotion} yakunukia, kisha akamnunulia na yule baba mafuta ya maji ya kawaida tu. Akahakikisha pia yanafaa kwa masaji. Akajinunulia chupi nzuri za kisichana, nguo chache za kulalia,  nzuri na za kuvutia. Akaingia kwenye maduka ya nguo. Akajinunulia vigauni kadhaa. Kisha Akamnunulia mke wa yule baba chocolate nzuri zenye muundo wa kopa. Akacheka kwanza yeye mwenyewe. Akatoka hapo akajinunulia vitu vidogo vidogo vya kujitengeneza. Aliporidhika na vitu alivyohitaji, akachukua tena taksii akarudi pale kwenye ile nyumba ya kulala wageni, na kujitupa kitandani mpaka usiku wa saa mbili aliposikia tena mlango unagongwa. 

~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~

Tunda alikuwa amepumzika vya kutosha kuifanya kazi yake vizuri. Akasimama kufungua mlango. Akabaki ameduaa akimshangaa Tunda. “Nimepotea mlango nini!?” Tunda akacheka na  kurudi ndani na yeye akafuata nyuma na mifuko, Tunda alijua mmoja wapo unachakula maana harufu ya kuku wa kuchoma ilienea chumba kizima. “Nimekuletea na chakula.” “Asante na karibu ukae.” Akakaa akionekana wazi bado anamshangaa Tunda. Tunda akacheka taratibu akimtizama. “Mbona umebadilika gafla hivyo!?” “Nimependeza au nimetisha?” Tunda akamuuliza na tabasamu usoni, akijua wazi amependeza. 

“Umependeza sana. Unazidi kunichanganya Ani!” Kabla hajatoa alicholeta Tunda akamuwahi yeye. “Nilikuwa najua utawahi ili tupate muda hata wa masaji! Ona mafuta haya nimekununulia. Mazuri na hayana harufu.” Tunda akayatoa kwenye moja ya mfuko, akamnukisha huku anamkalia na kupitisha kucha zake taratibu mapajani mwake. “Ndio inakuaje?” “Ningekufanyia, lakini masharti yake unatakiwa upumzike baada ya masaji. Sasa nikianza sasa hivi,  utachelewa nyumbani.” “Hamna neno.” “Hapana bebi. Sitaki uwe unachelewa nyumbani kwa mkeo. Kwanza nimemnunulia zawadi.” Yule baba akahisi hajaelewa. Tunda akasimama, akarudi na mfuko mkononi.

“Unamaanisha ni zawadi ya mama Amini?” “Kumbe mtoto wako mkubwa anaitwa Amini?” Tunda akauliza huku anarudi kumkalia. “Ndiyo.” “Kwa hiyo na wewe nikuite baba Amini?” “Hapana.” Akakataa kwa haraka. “Wewe endelea kuniita hivyo hivyo.” Tunda akamcheka  moyoni. Akajua amefurahia kuitwa Bebi. “Ni nini umemnunulia?” Tunda akatoa. “Kijizawadi chake yeye. Sio tena ukifika unampa mbele ya kina Amini, halafu waishie kumuomba!” Akacheka. “Sijawahi kumnunulia...” Akasita.  “Ndio unaanza sasa.” “Akiniuliza yameanza lini?” “Wewe mwambie katika pitapita zako ukaona hizi chocolate, unataka ale mkiwa peke yenu, chumbani kwenu.” Akacheka kama anayemtafakari mkewe. 

“Nini sasa?” “Sijui, lakini ngoja nikamjaribu.” “Hakuna mtu anakataa zawadi na kila kitu kina mwanzo.” Akabaki akicheka kwa wasiwasi kama anayesita. “Vipi?” “Sijawahi. Lakini acha  nikajaribu. Nashukuru sana kwa kunifikiria. Kweli una moyo mzuri.” “Basi ndio uwahi. Sio ufike huko umkute amekasirika kwa kuchelewa, ushindwe hata kumkabidhi zawadi yake.”  Anajua kama nipo kwenye baa zetu. Huwa nachelewa kurudi nyumbani. Anaelewa.” “Na mchana huwa unafanya nini?” Tunda akamuuliza taratibu. “Nina baa nyingine kule Ilala pia. Ile ipo busy kuanzia asubuhi wanauza kifungua kinywa, chakula cha mchana na usiku ndio zaidi. Na pia napatengeneza vizuri kuwe na night club. Mziki pia. Sasa kwa kuwa ni katikati ya makazi ya watu wengine, huo ukumbi wa mziki, nautengeneza upya kwa kuweka sound proof. Ili sauti zisitoke nje. Sasa lazima niwepo kusimamia.”

“Pole.Utakuwunachoka!” “Nimeshazoea.” “Basi kesho katikati ya kazi uje nikufanyie masaji. Itakusaidia mwili kujisikia vizuri, na sisi tupate muda wetu.” “Nashukuru kunifikiria Ani. Kwa hiyo sasa hivi niondoke?” “Naomba nikuage. Sitakuchelewesha.” Akajifanya yeye ndio anamuomba penzi, tena kwa kumbembeleza kumbe anatamani aondoke, apumzike. “Nitashukuru Ani. Na kesho nitajitahidi kuhangaikia sehemu yetu nzuri. Nimeshaanza kuzungumza na watu. Naamini tutafanikiwa tu.” Bila kujibu au kuonyesha ni habari njema sana, akamparamia baba wa watu. Akambadilishia mara mbili tatu akamuacha hajielewi hapo kitandanakihema, yeye akaenda bafuni.   

Wakati anarudi, amejifunga taulo  safi la hapohapo hotelini jeupe, refu, akamwambia asogeze hiyo mifuko aliyokuwa amekuja nayo. Alikuwa amemnunulia simu, Samsung Galaxy mpyaaa iliyokuwa ndio imetoka. Tunda mwenyewe akashangaa kwa  muda huo mfupi aliwezaje kupata simu nzuri vile. Alitegemea simu ya kawaida sana. Akaipokea, asiamini. “Nitaenda kulipia chumba mimi mwenyewe. Ili wasikusumbue.” “Nakushukuru bebi. Uzidi kubarikiwa na uongezewe.” “Na wewe pia Ani. Nimependa moyo wako.” Tunda akacheka taratibu huku akiangalia ile simu yake. Akamvuta mkono wake wakulia, nakuubusu.

“Asante.” Tunda akashukuru tena na sauti yake ya chini na macho yake ya upole. “Karibu. Ukiwa na shida yeyote. Namaanisha yeyote ile, tafadhali usisite kuniambia Ani. Kukimbilia kwa bibi iwe wazo la mwisho kabisa. Jua nipo kwa ajili yako.” Hata  masaa 24 hayakuwa yameisha, baba anajitia kitanzi kwa binti ambaye hata jina amedanganywa!  Walizungumza kidogo, akaaga akiwa amekumbuka zawadi ya mkewe. Akaishika mkononi. Tunda akacheka. “Nitakuona kesho Ani, asante kwa zawadi.” Karibu na uwe na usiku mwema. Naamini kesho na mimi utanipa muda mrefu kidogo. Tukae hata masaa mawili!” Tunda akajilalamisha kwa deko. 

“Kabisa. Kesho nitakuwa hapa. Naamini nitakuja na habari njema.” “Hata kama hutafanikiwa mambo ya sehemu yangu ya kuishi, usisite kuja kuniona tafadhali.” “Lazima nitarudi Ani, usiwe na wasiwasi. Tunda akampa busu la shavuni. “Haya nenda, usije kuchelewa zaidi nyumbani.” “Sawa. Lakini siwezi kukuacha hivi hivi.” Akawa amesahau kabisa kama alimuachia pesa mchana. Akatoa tena waleti. “Si uliniachia mchana!” Akajifanya kama hataki. “Pesa yenyewe umenunulia mpaka zawadi! Sitaki upate shida.” Tunda akapokea na cheko. Mzee akatoka na kumuacha Tunda kwenye chumba kizuri,  akipulizwa na kipupwe, AC, na pesa mkononi.   

~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~

Tunda alibaki mle chumbani  akicheka peke yake. Kumbe ndio  rahisi hivi! Hii ndiyo ajira yangu. Nitaenda kuongeza kondomu tu.” Tunda aliendelea kucheka akijipongeza. Akawasha simu aliyokuwa ameletewa, huku bado haamini macho yake. Kutoka hospitalini na kufikia kwenye maisha ambayo hakutegemea! Kula ugali kwa maziwa mgando/mtindi kwa takribani miaka miwili mfululizo akiwa kwa shangazi yake. Akahamia chakula cha hospitalini! Usiku huo kuku wa kuchoma anamsubiria yeye hapo chumbani! Kwake aliona ni muujiza. 

Tena uzuri wa ajira hii,  hawahitaji kujua nimesomea nini, wala hamna maswali magumu. Nikuongeza ujuzi kitandani ili wakionja tu wachanganyikiwe na  kumwaga mipesa yao kama huyu.”  Tunda aliendelea kujisemea huku akicheka peke yake kama aliyeokota dhahabu. Aliendelea kujiwekea mikakati mingi huku akiangalia mapesa aliyoyapata kwa siku moja. “Kwa elimu niliyo nayo, hakuna mwajiri anayeweza kunilipa pesa kama hii. Huu utundu wa kitandani  nilionao ndio ajira yangu tosha.” Tunda aliendelea kuwaza.

Lakini katikati ya mipango yake akawa kama amegutushwa na wazo. “Nikiruhusu huyu baba Imani sijui Amini, anitafutie nyumba, atataka kuhamia hapo na kunimiliki mimi kama mkewe. Na akishanifanya mimi mke wake, hawezi kuendelea kunihonga pesa yote hii. Atanizoea. Sitaki mazoea kama ya baba Tom. Sitaki kuja kuumizwa.” Hasira zikampanda Tunda na kumbadili moyo kabisa.  

“Kwanza akishanizoea, hatakubali kondomu. Atajidai mimi mkewe, ataishia kunipa mimba, halafu aje aniache nikiteseka.” Tunda akazidi kuwaza huku akiumia. “Lakini hata kizazi chenyewe kipo!” Hapo akakumbushwa jinsi alivyotolewa mimba kikatili. Akawaza hili na lile, akaanza kufikiria tena jinsi ya kuishi na baba Amini kwa akili ili aendelee kunufaika na pesa yake ila si kwa kujifunga kwake kabisa kama nyumba ndogo au mkewe. “Hakuna kuzoea mwanaume. Hakuna mabusu ya mdomoni. Mwiko.” Tunda akaendelea kuwaza usiku huo na kujiwekea mikakati ya kudumu ya maisha.  

~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~

Aliamka asubuhi akiwa ameshapanga maneno ya ukweli na uhakika kumuaminisha baba Amini akija pale. Akatoka hapo mida ya saa tatu kurudi kituo cha daladala za Mwenge. Akaanza kuulizia wapi atapata madalali. Akazunguka huku na kule, akaelekezwa kwa vijana kadhaa, akawapigia simu. Lengo la Tunda ni kupata sehemu ya kawaida, lakini tulivu na inayofikika mchana na usiku. Hakutaka sehemu ya vichochoroni ambako ikimlazimu kurudi nyumbani usiku, awe na hofu ya usalama wake.

    Kama kawaida ya madalali. Wakaanza kumtembeza. Alizunguka  mpaka akachoka. Simu za baba Amani akimuuliza alipo kila baada ya dakika kadhaa zikaanza. “Haya ndiyo ambayo sitayaruhusu. Sitaki kumilikiwa kama alivyonimiliki baba Tom. Leo mwisho.” Tunda aliwaza, mwishowe akaamua kurudi hotelini alikokuwa akisubiriwa.  

Alishakuwa amekasirika. Aliachana na dalali kwa makubaliano watafutane tena kesho yake. “Chukua hata taksii, fanya haraka urudi.” Hayo ndio yalikuwa maagizo ya mwisho yaliyomkera zaidi Tunda. Alikuwa amekasirika karibu kupasuka. Alifungua mlango bila hodi. “Mimi sio mke wako. Acha kuniamrisha kama mtoto mdogo.” Aliingia na kuanza kugomba. “Huwezi kuniita unapojisikia wewe. Hunijui na sikujui. Acha kujipa amri juu yangu. Au kwa kuwa umenipa hii simu?” Tunda akairusha kitandani. “Au kwa kuwa pia nimekushirikisha shida zangu zote mpaka sehemu ninapoishi, ndio unajichukulia mamlaka ya kunitawala wakati..” “Tulia kwanza Ani. Tulia kwanza.” “Hapana. Huwezi kunifanyia hivyo. Usinichunge mimi kama mtoto mdogo.” Tunda akazidi kugomba.

“Unajua  nilipokuwa lakini?” “Samahani. Nahisi nilipaniki. Nikajua umenikimbia.” Akajishusha. “Nina kimbia vipi wakati vitu vyangu umevikuta humu ndani na tumeachana kwa makubaliano ya kutafuta sehemu ya kuishi?” “Mimi sikujua kama na wewe unahangaikia, Ani! Nilitaka wewe upumzike. Mimi ndio nihangaikie.” Hapana. Nimebadili mawazo. Unaonekana wewe utanisumbua sana. Sitaki.” Tunda akaanza kukusanya vitu vyake kama anayetaka kuondoka.

 “Nikupaniki Ani! Naomba yaishe bwana.” Akaanza kumfuata nyuma akimbembeleza. “Nilikuja na habari njema, sasa nilipokukosa hapa nikajua umenikimbia.” “Kwa hiyo huniamini?” “Tumekutana jana tu Ani! Tafadhali nipe nafasi nyingine. Na mimi najifunza.” “Mbona sasa huombi msamaha?” Tunda akamuuliza kwa ukali kidogo. Akaanza kucheka. “Njoo kwanza hapa. Nimekuja na msamaha mkubwa.” Tunda akabaki amesimama akimwangalia. 

“Njoo basi Ani! Acha hasira.” “Omba  kwanza msamaha, lasivyo naondoka.” “Hata magoti napiga.” Tunda akashangaa kweli anapiga magoti. “Nisamehe Ani wangu.” “Acha kuwa kama mtoto anayelilia nyonyo bwana! Mpaka madalali walikuwa wakinishangaa, wakahisi nimeacha mtoto mchanga nyumbani!” “Nilipaniki. Nilikuwa nimejiandaa kuja kukukuta hapa. Jana ulinipa wakati mzuri sana. Halafu...” Tunda alibaki akimtizama kwa kumsuta mpaka akashindwa kumalizia alichotaka kusema, akacheka. “Njoo basi Ani, mama. Hasira haziishi!” Akarudi kukaa.

“Wewe niambie habari njema zenyewe kwanza. Maana kama ni sehemu ya kuishi, sitaki tena. Najitafutia kwangu, tutakuwa tukikutana unapokuwa tayari. Sitaki usumbufu.” “Umekasirika Ani. Acha hasira, njoo. Njoo nikwambie kitu kizuri. Njoo mama.” Tunda akasogea.  “Njoo ukae hapa basi! Akimuonyeshea miguuni kwake. “Ongea kwanza. Mimi nanuka jasho, mpaka nikaoge. Umenikimbizkimbiza!” “Mimi sijali kama unanuka jasho. Njoo.” Tunda akaenda kumkalia. “Nina habari njema zaidi ya sehemu ya kuishi. Unaona lile begi pale?” Tunda akageuka. Akaangalia“Kuna nini mle ndani?” “Pesa tupu.” Tunda akamwangalia kama asiyemuelewa. 

“Umekuja na baraka Tunda! Unaonekana unanyota kali sana. Na kuna mtu alishanitabiria kuwa kuna kitu kizuri kinanijia kwenye maisha yangu.  Akaniambia kikija hicho kitu, mambo yangu yataanza kufunguka.” Tunda akapandisha nyusi moja juu kama anayemshangaa. Na kukunja mikono kifuani. “Sasa hapa kitu kizuri ni mimi au hizo pesa!?” “Ni wewe Ani. Yaani nyota yako na yangu imeendana.” Tunda akabaki amekunja uso.  

“Kwanza mimi naitwa Sadiki.” “Mtoto wako anaitwa Amini! Majina ya wapi hayo!?” Sadiki akacheka. “Najifungua kwako Ani, ili ujue sisi tumekusudiwa kuwa pamoja.” “Sitaki kuolewa mke wa pili mimi?” Tunda akasimama. “Kwanza sitaki kuolewa kabisa.” “Nakwambia ni zaidi ya hapo Ani.” Na yeye akasimama. Sadiki alionekana amechangamka  kweli kweli. “Mbona umehamasika hivyo! Kama unafikiri begi la pesa ndio litanihadaisha na kunifungia ndani kama mkeo, jua HAPANA.” Tunda akaendelea kumuwekea ngumu.

“Nakwambia utakuwa zaidi ya  mke.” Tunda akakunja uso. “Tatizo hutaki kutulia Ani! Maisha yetu hayatakuwa kama zamani. Na wewe hivyohivyo. Yaliyotabiriwa yametimia baada ya kukutana na wewe. Tulia, acha hasira, nikupe habari nzima la hilo begi na maendeleo yetu kuanzia hapa. Najua na wewe utafurahi tu.”  Akamsogelea tena.

“Kwanza nusu ya zile pesa pale zitakuwa zetu. Mimi na wewe. Utakuwa huru kufanya kile unachotaka, sitakuuliza swali juu ya matatumizi wala huhitaji kunipa mahesabu yake.” Tunda akaanza kulainika. “Na nusu yake?” Tunda akamuuliza. “Mama Amini anajua juu ya hizo pesa. Lazima azione. Halafu mimi na wewe tutaanza kuingiza mapesa.” Sadiki akawa anaeleza kwa kuhamasika haswa. Tunda haelewi. “Watu si  wanalia pesa ngumu kuiweka mfukoni?” Sadiki akauliza kwa kicheko. “Basi sisi tutashamiri. Tutaingiza mamilioni ya  pesa tukiwa hapa hapa Tanzania. Lakini tukiwa mimi na wewe. Kama utakubali lakini!” Bado Tunda  alikuwa amesimama, hajaelewa.  

Sadiki akasogelea ule mkoba.  Akatoa pesa baadhi akaziweka mezani. “Hizi ni zako na zangu tu. Kwa matumizi yako tu. Huna haja ya kuhangaika tena.” Tunda akabaki kimya. "Nakusikiliza Ani. Niambie kile unachotaka sasa hivi, nifanye. Utulie.Nishakuomba msamaha mpaka wa magoti! Niambie nini unataka Ani. Ili tuanze kuneemeka kwenye jangwa.” Sadiki aliendelea kuongea kwa kuhamasika. Tunda akabaki ameduaa kwenye pesa alizomilikishwa gafla! 

~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~

Kufunga na kufungua Tunda anamilikishwa mapesa. Sadiki anampa ahadi kubwa ya  

Neema katikati ya wenye shida na shidani. Tena si ahadi tu, amemkabidhkabisa pesa isiyo na maswali. Amemwambia yeye atakuwa zaidi ya mke!  

Ø  Ni nini anamaanisha?

Ø  Ni nini hicho cha tofauti watafanya pamoja na Sadiki ambaye anaonekana ameshafanikiwa kimaisha. Ana mke ambaye naye ni  mfanyabiashara mzuri tu, na tayari wana biashara zinazoonekana kufanya vizuri tu!  Tunda anaingiaje kwenye picha akiwa na  huo mtaji alioambiwa ni wa NYOTA nzuri tu?  

Ø  Yepi atafanya na Sadiki?

Ø  Je, ni kweli ni Neema?  

Tunda ameingia mtaani. Atapita kwingi, atafanya mengi ili kuweza kuyamudumu maisha.  

 

Endelea kufuatilia sehemu ya 9.  

CONVERSATION

0 Comments:

Post a Comment