Naomi Simulizi |+1 205 767 8163 |naomisimulizi@gmail.com Jinsi Ya Kupunguza Uzito kwa Kutumia Kinywaji cha Tangawizi. - Naomi Simulizi

Jinsi Ya Kupunguza Uzito kwa Kutumia Kinywaji cha Tangawizi.

Vipo vinywaji vingi sana vyenye sifa za kupunguza uzito au kukata mafuta mwilini. Lakini kama nilivyoonyesha kwenye nakala yangu nyingine juu ya 
Nguvu ya Tangawizi mwilini”,  leo nitakupa siri ya kutumia Tangawizi Kupunguza Uzito.

Mahitaji.
*Maji
*Tangawizi
* Limao {Ukipenda}

Uandaaji.

Chemsha Maji yako, kisha ongeza Tangawizi ambayo utakuwa umetwanga. Acha ichemke kwa muda, kisha uitoe jikoni. Waweza kuinywa kama chai, bado ikiwa ya moto bila ya kuongeza Sukari. Na kuweka maji ya Limao kiasi, kama utapenda. 

Hakikisha unaweka Tangawizi ya kutosha. Ladha ya Tangawizi isikike kwenye Maji.

Wakati Gani wa Kuinywa?
*Usiku Wakati wa Kwenda kulala :- Kwa kuwa Tangawizi inasaidia kusaga chakula mwilini huku ikiyeyusha mafuta, ni vyema kinywaji hicho kukinywa wakati unakwenda kulala, ili isikufanye ukasikia njaa, na kushawishika kula tena. Cha msingi ni kulala ukiwa unauhakika wa chakula ulichokula kwa siku nzima, kitasagwa na kutolewa uchafu wote ambao hautahitajika mwilini. Na

*Asubuhi kabla ya Kifungua kinywa :- Soma faida ya Tangawizi kwenye nakala yangu iliyopita. {Je, Wajua Nguvu Ya Tangawizi?}

CONVERSATION

0 Comments:

Post a Comment