Naomi Simulizi |+1 205 767 8163 |naomisimulizi@gmail.com NILIPOTEA! – sehemu 38. - Naomi Simulizi

NILIPOTEA! – sehemu 38.


B

ila kuongeza neno, Tunda akanyanyuka pale alipokuwa amekaa akatoka kurudi chumbani kwao. Net naye hakuongeza, akamfuata nyuma. Walimuacha baba yake Tunda, ameinama tu. Baada ya muda akampigia simu mama Penny. Alimweleza kila kitu. “Nakuja.” Ndilo lilikuwa jibu la mama Penny.

Mama Penny!

Haukupita muda mrefu sana, saa tatu kamili usiku huo huo, mama Penny alikuwa mlangoni kwa Tunda hapo hotelini. Akagonga, Net akafungua mlango. “Tunda yuko wapi?” “Kitandani.” “Haya naomba mvae twendeni.” “Wapi tena!?” “Kwa mama yake. Asinichezee akili.” “Usiku huu!” Net akashangaa.

“Nakwambia sasa hivi. Najua anapoishi. Asijifanye amechanganyikiwa!” Akaingia ndani mpaka alipokuwa amelala Tunda. “Haya, toka hapo kitandani, kausha machozi, twende.” “Amenitukana!” Tunda aliongea huku akilia. “Ndio nataka nikayasikie matusi yake. Nataka nikamsikie akikutukana wewe na baba yako, mimi nikiwepo. Yeye si mwehu? Sasa twende.” Net alibaki ametoa macho.

“Na wewe unakuja au unabaki?” Mama Penny akamuuliza Net. “Huna lazima ya kwenda.” Akamwambia tu hivyo alipomuona Net anababaika. Kisha akamgeukia Tunda. “Baba yako nimemwambia ajiandae, sasa hivi anakuja, twende.” Tunda akaingia bafuni, akatoka ametulia.

Alimkuta baba yake amekaa hapo kwenye kochi. “Mimi nipo tayari.” Tunda aliongea kwa upole. “Haya beba chupa yako ya uji, twende.” Mama Penny alikuwa amesimama.

Tunda akaanza kucheka. “Hivi sasa hivi unajua inakwenda saa tatu na nusu usiku!” Tunda alimwambia mama Penny huku akichukua chupa ya uji. “Ndio vizuri, tumkute nyumbani kwake.” Net akapokea ile chupa, akachukua na kikombe.

“Sasa naomba mchukue gari yenu. Tukimalizana na mama Tom, mimi huku sirudi.” Tunda akaendelea kucheka. “Muone na huyu naye! Utajifunza lini kujitetea wewe!? Watakuja kukufunga tena kama unaishia kulia!” Tunda akaendelea kucheka taratibu.

“Sasa twendeni.” “Akikataa kutusikiliza?” Tunda akauliza. “Subutu! Atakusikiliza tu. Wewe twende.” Wakatoka hapo wakiendesha magari mawili. Mama Penny na Tunda kwenye gari ya mama Penny, Net na baba yake Tunda kwenye gari ya Tunda. Net alisharudisha gari aliyokuwa amekodisha. Wakaendelea kutumia gari ya Tunda.

Kwa mama Tom!

Mama Penny alimuendesha Tunda, huku Net na baba yake mkwe wakiwafuata kwa nyuma mpaka Kurasini nyumbani kwa mama Tom. “Nisubiri hapa kwenye gari, nitakupigia mje. Sitaki kuwaingiza kwenye matatizo. Tukishindwana naye iwe juu yangu. Nyinyi muondoke kabisa hapa. Kama ni polisi, atakuja kunitoa baba Penny.” Alimtaka Tunda ahamie kwenye gari alilokuwa amekaa Net na baba yake.

“Naomba uwe mwangalifu mama Penny bwana. Mimi sina wakunipikia uji.” Mama Penny akacheka nakuondoka. Hawakuwa wameegesha mbali. Mbele tu ya nyumba.    

Aligonga mara kadhaa, mlango ukafunguliwa. Walimuona akizungumza na mama Tom, kisha akapiga simu kuwaita. Wote watatu wakashuka, na kumfuata. Wakakaribishwa ndani. Uzuri Tunda walipokuwa njiani alimsimulia mama Penny kila kitu. Na mama Penny akampanga Tunda vizuri, mpaka wakafika pale. Wakaingia ndani.

Tunda aliweza kutambua vitu vyake vyote mle ndani. Makochi, tv, kapeti, kabati la vyombo. Asilimia 99 ya vile vitu mle ndani vilikuwa vya Tunda. Hata Net aliweza kuvitambua

“Sasa sisi hatutakaa sana. Tunajua umechoka, hatutachukua muda wako mrefu, ili tukuache upumzike.” Alianza mama Penny. Wazi mama Tom alionekana ameshtuliwa na ule ugeni wa ghafla. “Karibuni.” Alijibu kiuungwana mama Tom, kama sio yeye.

Lakini Tunda alijua huwa anamuogopa sana mama Penny. Yeye huwa anamuweza. Hata baba yake akashangaa uungwana huo wa gafla unatoka wapi!

“Sasa Net na Tunda wanaondoka kesho kutwa. Kabla yakuondoka, nataka, umsikilize Tunda upande wake wa stori. Hatujali kama utaamini au hutaamini. Hiyo ni juu yako wewe, ila binafsi nisingependa kujua. Na ili kuwe na usalama hapa, ficha kile unachokifikiria. Sijui kama unanielewa mama Tom?” Kimya.

“Maana hili zoezi limekuwa likiahirishwa sana. Alianza nalo Net. Akakubaliana na Tunda kuja kukueleza na kukuomba msamaha, japo sikuona sababu ya wewe kuombwa msamaha.” “Alitakiwa..” Mama Tom akataka kumkatisha, lakini mama Penny akamuwahi. “Nikiongea huwa sipendi kuingiliwa mama Tom. Na nilikwambia ficha hisia zako.” Kimya.

“Isingekuwa Tunda, mimi binafsi ningekushitaki. Nakumbuka hili nilishakwambia tokea tupo pale mahabusu ya Keko. Tukatolewa. Na usifikiri iliishia pale! Kuna mtu alinifuata baada ya wewe kuondoka, akasema nikushitaki, lakini nikawahurumia hao wanao wengine. Wewe ni mama mzembe ambaye sijawahi ona! Nyamaza tu umsikilize Tunda, maana ukianza na mimi, utaishia polisi usiku wa leo.” Kimya. Mama Penny akaendelea.

“Net alipokuja na Tunda nyumbani kwako ili kuzungumza na wewe, ndio akakukuta na matatizo. Tunda akakuchukua wewe na wanao. Tena Aneti akiwa mgonjwa. Akawahudumia, na kuwalisha.”

“Hapa ulipo bado unatumia kodi aliyolipa Tunda. Kila ninachokiangalia hapa, ni cha Tunda ambacho nilikupa mimi mwenyewe na vijana wangu ndio walikuhamisha hapa.” Mama Penny akaendelea kibabe.

“Kazi inayokuingizia pesa, inatokana na kampuni ya Tunda. Na mimi na Tunda ndio tumekufundisha hii kazi, na wateja wengine mimi ndio nakupa. Ni jumamosi hii tu iliyopita, umetoka kupamba ukumbi wa mtu niliyekutambulisha kwake. Kwa kifupi tu, upo hapo ulipo sababu ya Tunda.”

“Nikiita vijana wangu nikiwaambia wapakie vitu vya Tunda hapa, wewe na wanao mtalala chini. Na nikienda umbali wakudai hii sehemu, utalala nje na wanao. Maana hata hapa ni mimi na Tunda ndio tuliingia mkataba.” Watu wote kimya.

“Hayo yote nimekukumbusha tu ili kukurudisha ulipotakiwa uwepo kabla ya Tunda hajaja kukuokoa kule kwa ndugu wa mume wako. Kwa hiyo basi, nakusihi sana, unapozungumza naye Tunda, kumbuka nafasi yako na uwe na shukurani. Sijui kama unanielewa mama Tom?” Kimya.

“Unanisikia au unataka nirudie kukukumbusha vile Tunda anavyokusitiri hapa mjini?” “Mimi sio mtoto mdogo mama Penny. Nakusikiliza.” “Basi anza kuishi kama mtu mzima. Acha kujidai umechanganyikiwa!” Mama Tom akamkazia macho mama Penny kama amjibu lakini akashindwa.

“Naamini umenielewa.” Mama Penny akaongeza kwa ukali, kisha akamgeukia Tunda. “Haya Tunda, ongea kile ulichotaka kumwambia mama yako. Leo wote wapo hapa. Wazazi wako wote wawili. Nina uhakika hata baba yako hajui ukweli. Ongea kwa utulivu bila hofu, maana hapa ni kwako hakuna atakayekufanya chochote. Atakayeshindwa kukusikiliza hapa, achukue mabegi yake aondoke. Hii nyumba nitaitafutia mteja, turudishe pesa yetu. Kesho asubuhi, nauza kila kitu mpaka kijiko, uondoke na pesa yako. Tena kwa dola.” Mama Penny akajiweka sawa, huku akimtizama Tunda.

Hatimaye Tunda apata fulsa yakueleza upande wake mchungu kwa wazazi wake.

N

et akamuwekea mkono mgongoni, akampapasa taratibu. Tunda akamwangalia, nakujiweka sawa. “Kwanza mimi nilijua yule bibi aliyenifukuza na kunionya nisiwahi kurudi tena kwao yeye na babu ndio wazazi wangu. Yaani wazazi wa mama Tom ndio nilijua ni wazazi wangu. Na mama Tom ni dada yangu. Shida yangu ilianza pale ndugu wa mama Tom walipotaka mimi niondolewe pale kijijini.” Tunda akaanza kuelezea.

“Mama Tom alinichukua kutoka pale kwa wazazi wake kunipeleka kwa baba, kwa hasira sana. Njia nzima akinipiga kwa makosa haya na yale. Kwa kuwa nilikuwa simulewi. Sikuwa nikijua kiswahili vizuri. Kijijini tulikuwa tukizungumza kilugwa, mpaka darasani. Sasa mama Tom alipokuwa akinipa maelekezo kwenye gari, nikiwa sijawahi hata kupanda gari, alikuwa akinipiga sana.” Tunda akaendelea.

“Alinifikisha kwa baba, akiwa ametoka kunipiga sana nje ya ile nyumba. Kwa kuwa sikuwa najua kufungua mlango. Nikiwa kwenye hofu vilevile, alinivuta mpaka sebuleni kwa mama Chale na baba. Akaniacha hapo, akiniambia baba, ndio baba yangu.”

“Niliamini kwa kuwa ni kweli tulifanana. Hata weusi aliokuwa akinitukana nao, ni kweli nilifanana na baba hivyo hivyo. Maisha yangu yakaanza pale kwa baba.” Tunda akaeleza mateso yote aliyokuwa akifanyiwa pale kwa baba yake, bila utetezi.

“Basi, bibi alipokuja kunichukua kutoka hospitalini Dar, akanirudisha tena kijijini. Ndio akaamua kumpigia simu baba Tom, aje. Ndipo akaja na mama Tom, baada ya mazungumzo ya muda mrefu, wakakubali kuondoka na mimi pale kijijini.” Tunda akatulia kidogo.

“Ukweli mama Tom alikuwa akinichukia nakushindwa hata kujizuia. Mpaka yule msichana wa kazi alikuwa akishangaa. Baba Tom alipoona udhaifu huo, mama hanipendi na kunitukana kila mara, yeye ndio akapata mwanya. Weusi aliokuwa akiutukana mama yangu kila wakati na macho haya akisema kama ya paka, akawa anasifia baba Tom. Wakati mwingine mama alikuwa akinipiga mpaka ananiingiza chini ya meza, baba Tom ndio akawa anakuja kunitetea.”

“Ukawa sasa ndio mchezo. Mama akitaka kunipiga, mtetezi wangu ni baba Tom. Nikilia, yeye ndio ananibembeleza kwa kunipakata.” Tunda akatulia kidogo. Akaelezea mengi yaliyokuwa yakiendelea pale ndani bila mama yake kujua au kujali. “Ile tabia yakunibembeleza ikawa mazoea. Wakati wote alinipakata hata mbele ya mama. Lakini tulipokuwa wenyewe, ubembelezwaji ukaanza kubadilika.”

“Akaanza tabia yakunichezea huku akinisifia mwili wangu. Alipoanza kuvuka mipaka, nilimkatalia. Ndipo akanikumbusha nipo pale kwa sababu yeye anataka. Mara nyingi mama alikuwa akinitishia kuwa atanirudisha kwa baba yangu, mkewe aniue kabisa. Lakini baba Tom akawa akinitetea. Kwa hiyo akaniambia nikimkatalia, hatanitetea tena. Atanirudisha kwa baba yangu.” Tunda akaendelea.

“Ile tabia ikaendelea. Akawa ananichukua mpaka chumbani kwake. Siku ambazo mama Tom analala kazini, na mimi ndio zilikuwa siku zangu zakuchezewa usiku kucha mpaka yeye aridhike.”

“Ikitokea mama Tom haingii kazini usiku, na baba Tom anajua, basi ujue mchana huo nikitoka shule, ndio itakuwa nafasi yake. Ataniambia nikaoge, nipande kitandani kwake. Wakati mwingine na nguo, wakati mwingine bila nguo. Atanifanyia hivyo mpaka mida anayojua mkewe anarudi.”

“Siku ambazo namkatalia, anaweza kuzua jambo lolote. Basi atanipiga wee, mpaka achoke na mkewe ataniongezea. Akinilaumu namtia aibu kwa mumewe. Basi. Alipozoea kunichezea, hapo bado nilikuwa mdogo, akaanza kunifundisha jinsi yakumchezea na yeye.  Hapo ndipo ilikuwa mateso kwangu. Hatosheki wala haridhiki. Unalala umechoka na asubuhi anakuja kukuamsha umchezee tena kabla hajakwenda kazini.”

“Nilipojua kumfanyia anachotaka, akaanza mtindo hata wakunifuata shuleni. Anadanganya labda ananipeleka kwa daktari, au sababu alizojua yeye. Atanichukua kwenye gari au hata hotelini kama atajua mama atakuwepo nyumbani usiku au yupo likizo kwa hiyo usiku hawezi kunichezea.”

“Kama ni hotelini, ujue ndio nitakaa naye mpaka muda wakutoka shule, ndipo tunarudi shuleni kumchukua mtoto wao Tom, tunarudi nyumbani.” Baba yake alibaki ameinama akifuta machozi.

“Mama Tom alipokwenda kupumzika kwa bibi kipindi alipojifungua Aneti, ndipo mumewe sasa akaanza kuniingilia. Tulibaki nyumbani mimi, yeye baba Tom, Tom na kijana wa kazi aliyekuwa akilala nje. Jamani baba alikuwa akinitesa yule!” Tunda akaanza kulia. Alikumbuka maumivu aliyokuwa akisababishiwa na yule baba.

“Diclophenac, zile dawa za maumivu makali ilikuwa kama pipi kwangu. Na alipoanza, hakuweza kusubiri hata nipone. Asubuhi na jioni ikawa ndio kazi. Na hapo nilikuwa nikilala chumbani kwake kama mkewe!” Tunda alimfanya mpaka mama Penny aliyejua hiyo historia aanze kulia tena.

“Alipoona navimba, na yeye hawezi kusubiri, akatafuta kama mafuta hivi. Ananipaka, panakufa ganzi, basi ndio ujue utakesha naye mpaka ganzi iishe. Anakupa dawa ya maumivu, ulale, mpaka alfajiri tena. Anaanza. Alifanya vile mpaka nikazoea. Akaacha kunipaka hayo mafuta akawa ananitumia hivi hivi. Nilipokuwa nikimuomba yale mafuta, akawa akinipiga, ananikatalia.” Kila mtu kimya.

Net alikuwa mwekundu kana kwamba ndio anasikia kwa mara ya kwanza wakati alishasimuliwa. Bado alikuwa amemshika mkewe.

“Basi. Aliendelea hivyo mpaka nikazoea kabisa. Akanifundisha mambo mengi yakufanya. Aliporidhika kuwa nimejua, akaanza yeye kunipangia wapi niwepo na kwa wakati wake. Hiyo inategemea na mkewe alipo.”

“Siku nyingine tunatoka kama nakwenda shule, kumbe nakuwa nipo naye hotelini. Kuanzia hiyo asubuhi, mpaka muda wa shule kuisha.” Tunda akajifuta machozi. “Wakati mwingine siku za jumamosi alianzisha tuition hewa. Kwa hiyo nilikuwa naaga nakwenda tuition, kumbe alikuwa akinitanguliza hotelini. Baada ya kama lisaa hivi, anakuja. Hapo utashinda naye hapo hotelini ukimuhudumia mpaka atosheke yeye. Ndipo ananiruhusu nirudi nyumbani, namuacha yeye akilala.” Net aliendelea kumpapasa mgongoni.

“Ukweli nilikuwa nikichoka. Maisha yangu ilikuwa ni yeye tu. Asubuhi, mchana ananifuata mpaka shule, na usiku kama mkewe hayupo au kama mkewe akiwepo, ujue humo njiani nilazima nimridhishe ndipo turudi nyumbani.” “Tom anakuwa wapi?” Mama yake akauliza.

“Unakumbuka nilivyokuwa nikifeli akakwambia ananianzishia tuition za jioni?” Mama yake kimya. “Basi hapakuwa na tuition wala kusoma. Ananitoa shule, ananipeleka hata baharini. Anaegesha gari, naanza kazi yakumuhudumia yeye. Na ukitaka urudi nyumbani salama, ni yeye aseme basi. Usiseme umechoka. Wakati mwingine anaweza kukupiga huko huko halafu anakwambia muanze upya.”

“Siku moja nilikuwa nimechoka. Ilikuwa siku ya jumamosi, akataka twende hotelini kama kawaida. Nikamwambia nimechoka. Aniache siku hiyo nipumzike lasivyo namsemea kwa mama, namwambia ukweli. Akaniwahi, akaenda kunisemea yeye kuwa nimeanza mambo ya wanaume, ndio maana nafeli darasani. Jamani mama Tom alinipiga! Akaja sasa yule baba mwenyewe. Alinitandika na mikanda ya suruali, mpaka leo nina alama.”

“Walipomaliza hapo, sijui kama mama Tom unakumbuka? Ulinifungashia nguo chache, ukanirudisha kwa shangazi yako. Ukasema heri nikaishi huko, kuliko kupoteza pesa yenu na kukutia aibu.” Baba yake Tunda alishindwa hata kunyanyua uso.

“Basi. Nilikaa kule kwa shangazi yake mama Tom, sijui ni kwa majuma mangapi, lakini hata mwezi haukuisha, baba Tom akaja yeye mwenyewe kunichukua. Akamwambia huyo shangazi kuwa amenisamehe, anaona nirudi tu nikaendelee na shule.”

“Nakumbuka siku ile alikuja asubuhi tu, akanitoa milimani kule, akatafuta hoteli palepale Morogoro mjini, tukaenda.” Tunda akaanza kulia tena.

“Akaniambia kuanzia siku hiyo, nisiwahi kumbishia tena. Nimeona kilichonipata. Mama alinipiga, na kule kwa shangazi ni kama walianza kunikasirikia. Walitaka kunifukuza. Akaniambia yeye ndio amebaki kuwa mkombozi wangu. Ili niishi kwake vizuri, basi, lazima na yeye aishi vizuri. Na ili aishi vizuri, ni mimi nimfanyie anayoyataka yeye, mpaka aridhike. Basi, hapo ndio ikawa sina tena usemi juu ya mwili wangu. Alinifanyia kile atakacho yeye, muda na wakati atakao yeye.”

“Mpaka nikavunja ungo. Ndio ikawa afadhali yangu. Nikiwa kwenye siku zangu ndio pumziko, lakini napo ikawa anakuwa kama mbogo. Mkali pale nyumbani, hapakaliki. Jambo kidogo tu, anagomba.” Net akafungua chupa ya maji aliyokuwa amekuja nayo, akampa. “Asante.” Tunda akamshukuru, na kunywa kidogo ndipo akaendelea.

“Akawa akinipa mahela, na kuninunulia nguo. Anapanga wapi niwe na wakati gani ili nimtumikie. Hata kama ni mchana, nimebaki nyumbani, anaweza kuniambia nihakikishe nambembeleza mtoto alale, yeye anakuja, anataka anikute labda uchi, chumbani kwake. Kipindi hicho namlea huyu Aneti.”

“Basi ndio unahangaika kumbembeleza mtoto. Akija akikuta mtoto amelala, ndio ananitumia. Akiridhika ndipo anarudi kazini. Anakuacha hapo na mauchafu yake na maumivu. Akirudi mkewe jioni, hajaridhika na kile alichokwambia umfanyie mwanae, basi unapigwa vibao vya usoni kama paka mwizi huku akikutukana matusi mabaya.”

“Ikawa hivyo hivyo. Nikagundua njia ya kusema nipo kwenye siku zangu, ili niwe napumzika. Najikata mahali, napaka damu kwenye pedi, akihakikisha pedi ina damu ujue utaachwa.”

“Hakuwa akijua siku za hatari wala salama. Yeye ilimradi amepata anachotaka. Hakuwa akitaka kondomu kabisa. Mwanzoni akawa anakumbuka kunipa dawa kwenye siku zangu za hatari. Akishamaliza haja zake, akijua ni siku za hatari, basi anakupa dawa ili usishike mimba, au anatoa nje. Mimi sikujua kama nimeshika mimba kwa kuwa alikuwa makini sana.”

“Siku aliponiambia nimfuate Arusha nikiwa nimetoka kwa bibi. Nilikuwa wala sijui kama bibi alinigundua ni mjamzito. Kumbe alikuwa ameshamwambia mama. Nikatoka Morogoro, nikamfuata Arusha, tulikaa nafikiri siku 4 au zaidi, nikimuhudumia tu yeye, wakati yeye yupo kwenye semina iliyokuwa imempeleka kule Arusha.”

“Nikakaa naye mpaka semina ikaisha maana nilikuta inakaribia kuisha. Alipomaliza semina, tukaongeza siku zakukaa kule huku akimdanganya mkewe kuwa muda uliongezwa. Baada ya siku 4 hivi nafikiri, akaniruhusu nirudi. Akanikatia tiketi ya ndege ya asubuhi, yeye akaja na ya mchana.”

“Ndio kwa mara ya kwanza nikashangaa eti mama Tom ananiuliza maswali yanayonihusu mimi! Kumbe mwenzangu alishaambiwa na bibi kuwa mimi ni mjamzito, ndio maana ananiuliza.”

“Japokuwa tulikuwa tukiishi nyumba moja, hakuwa akinisemesha. Akinisemesha ujue ananipa maagizo ya nini nimfanyie mtoto wake Aneti ambaye nilimlea, au kunitukana. Kila mtu alikuwa anajua pale ndani mahusiano yangu na mama Tom. Basi ndio akanichukua siku inayofuata, akanipeleka shule. Akashangaa matokeo yangu. Ni kweli nilikuwa nakuwa mtoto wa mwisho darasani.”

“Akashituka sana mpaka akamshangaza mwalimu. Akamuuliza kwani alikuwa amesafiri? Nani alikuwa akiishi na mimi asijue kilichokuwa kikiendelea kwa muda wote ule! Aliambiwa nilishapewa barua nyingi tu niwe napeleka nyumbani juu ya maendeleao yangu shuleni na vile ninavyolala darasani, lakini zote zilikuwa zikiishia mikononi kwa baba Tom.”

“Akihitajika mzazi shuleni, yeye alikwenda na kuzungumza na walimu. Walimu karibia wote walikuwa wakimlalamikia baba Tom vile ninavyolala darasani. Yeye alijua sababu ya ukweli, akazua ugonjwa.”

“Sijui aliwaambia nilikuwa nikisumbuliwa na ugonjwa gani sijui, yeye baba Tom aliujua na wale walimu wakauelewa. Basi ikawa ni sawa mimi kulala darasani na yeye kuja kunitoa darasani muda na wakati anaotaka, na kunipeleka hotelini na si hospitalini au kumuona daktari wa huo ugonjwa kama alivyokuwa akiaga walimu shuleni.”

“Mama Tom alinitoa hapo shuleni na kunipeleka kwa wafanyakazi wenzake. Wakanichoma sindano ya usingizi, wakanitoa mimba.” Tunda akaanza kulia. “Nilikuja kuzinduka wodini nikiwa na maumivu, na baba pembeni yangu na barua yakufukuzwa kwa mama na ndugu zake rasmi.”

“Baba aliniuguza bila hata maswali. Akawa ndiye wakuniletea uji asubuhi na jioni. Mpaka nilipopona, na yeye akaenda kuniacha nyumbani kwa dada yake. Ambako huko tena ni habari nyingine, ila ndiko Mungu aliponikutanisha na Net.” Tunda akatulia kidogo.

“Kwa hiyo hayo ndiyo niliyotaka uyasikie kwa upande wangu. Sijui utaamini kwa asilimia ngapi, lakini namshukuru Mungu kwa kunipa mama Penny, aliniwezesha kupata hii nafasi angalau na mimi unisikilize na nikuombe msamaha kwa pale nilipokosea kama mtoto.”

“Sijui nilitakiwa kufanya nini, ili isiwe kama ilivyokuwa. Nyinyi wawili wote mlikuwepo kwenye maisha yangu, na mkaacha wenza wenu wakinitesa.” Tunda akazidi kulia zaidi.

“Baba ulijua jinsi mama Chale alivyokuwa akinitesa. Tena kwa kuambiwa na majirani na yule msichana wenu wa kazi. Lakini ulishindwa kunisaidia. Mama wewe ndio sijui hata niseme nini! Nashindwa hata nianzie wapi! Tokea nilipokuwa kwa bibi, ulikuwa ukija kule hutaki hata kunitizama! Umebeba chuki dhidi yangu, natafuta sababu siioni! Huoni shida kunitukana, au kuniumiza kwa wazi kabisa, ukitaka onione ninavyoumia! Chuki imekujaa ndani yako kila kitu ninachokufanyia huoni thamani yake!”

“Nilikulelea mtoto wako Aneti, lakini ulishindwa hata kupokea salamu yangu! Hata kuniuliza tu hujambo, ulishindwa. Japokuwa nilikuwa nikimlea mtoto wako na kutumiwa na mume wako, lakini umeua mtoto wangu bila idhini yangu! Uliniacha hospitalini navuja damu, akaenda kuzunguka kila nyumba kutangaza nimezaa na mume wako.”

“Haya, nilikuja kukusaidia wewe na watoto wako. Dunia ikiwa imekugeuka kabisa. Nimewaweka hotelini kwa pesa yangu! Muulize mama Penny. Nilikuwa nikichukua kazi nakuzifanya kama punda, bila msaada hata shilingi ya Net, ili kukusaidia wewe na watoto wako. Bado hukuridhika.”

“Nimefungwa jela, hukuja hata kunisalimia, umechukua kampuni yangu na mali zangu karibia zote. Sijalalamika wala sikukutafuta kukudai. Nakutafuta, unakataa kupokea simu zangu mpaka nakwambia naondoka, ndipo ukaridhia kunisikiliza! Hata usiulize afya yangu na ulijua nilikuwa nimefungwa, unadai mali zangu zaidi!”

“Unakasirika mimi kumpa baba vitu nilivyotafuta kwa jasho langu! Unanitukana mimi na baba ambaye alikuja kujirudi kwangu bila kutaka kujua ukweli huu niliowaambia wote!” Net akampa tena maji ya kunywa. Kama aliyekuwa akimkumbusha atulie. Akatulia.

“Mpaka kochi ulikokalia sasa hivi hapo ni langu. Bado unakasirika kujua nampa baba simu! Kweli!? Hakuna mtu yeyote mwenye haki yakuniambia nitumie vipi mali zangu. Kwa kuwa nyinyi wote mliniacha nikiteseka mbele ya macho yenu.”

“Narudia, ni afadhali baba, alinihudumia hospitalini na kunisaidia vile alivyoweza yeye, lakini sio wewe. Huna haki kabisa mama Tom. Nimekuja kukwambia haya na kukuaga kwa amani kama baba alivyonishauri. Mungu akikupa neema yakunisamehe pale nilipokukosea, basi, naomba unisamehe.”

“Ila mimi nawatangazia nyinyi wote wawili, nimesamehe yote mabaya mliyonitendea. Nashukuru Mungu kunirudishia japo mzazi mmoja.”

“Ila mama Tom, kuwa makini. Sasa hivi alipo Aneti, hakumbuki diaper za thamani ulizokuwa ukimwaga pesa ukimnunulia nimvalishe. Sijui makopo ya maziwa ya thamini au nyumba aliyokuwa akiishi yenye AC na sisi tukimtumikia.”

“Kumbukumbu atakayokufa nayo huyo Aneti hata akifa akiwa mzee sana, ni kuwa mama yake alimuacha akitendwa vibaya na baba yake. Mimi nilipita alipopita Aneti, sema mwenzangu yeye ulimuuguza gonorea, mimi ulinitoa mimba na kunitelekeza hospitalini.”

“Ila madonda aliyoyaacha baba Tom, mumeo, wewe ukiwepo, ndani ya nyumba hiyohiyo, hayaponi hata kidogo. Si kwa muda wala dawa. Hakuna pole au faraja yakuponya hayo madonda.”

“Mwisho kabisa, nashauri urudi kwa Mungu. Hata kama si kwa ajili yako, basi kwa ajili ya Aneti. Mimi Net alinitafutia mchungaji akaniombea. Nilitokwa na mapepo mengi tu. Lakini baadhi yalisema yalitokana na agano nililokuwa nimeingia na baba Tom au mumeo. Kwa njia gani, mimi sijui. Unakumbuka Net?” Net akatingisha kichwa kukubali.

“Basi ni hayo tu. Mpeleke huyo mtoto akaombewe. Pengine itamsaidia na yeye kwa namna moja au nyingine. Mungu hashindwi. Twendeni.” Tunda akasimama.

Baba yake Tunda naye.

“Naomba kabla yakuondoka, niweke jambo moja sawa. Mbele ya Manda, ili kusitokee kubisha baadaye.”  Baba yake Tunda alimuwahi Tunda kabla yakutoka. “Naomba ukae kidogo Tunda. Maadamu tumepata muda huu, naomba na mimi nikuweke sawa.” Baba yake akajifuta machozi. 

“Nakumbuka kukwambia kwa sehemu Tunda, lakini wakati ule wote hatukuwa kwenye mazingira mazuri yakuelezana jambo, ukaliweka akilini. Wewe kwangu sio mtoto wa bahati mbaya, ila ni mtoto niliyekujua na kukabidhiwa kwa gafla nikiwa kwenye matatizo makubwa sana ya ndoa yangu.” Yule baba akajiweka sawa.

“Manda hakutaka kabisa nifahamu kama ana mtoto wangu. Kwa sababu zake binafsi. Ila namjua tabia yake yakupenda kutumia watu. Huwa hajali unaonekana vipi au ukoje linapokuja kwenye swala la pesa, na ndio maana nafikiri, ukampitisha Tunda huko alipopita mpaka leo.”

“Hee! Kwa nini gafla mimi ndiye naonekana mbaya?” “Subiri kwanza Manda? Wewe kilichokushinda kuniambia una mimba yangu, si kwa kuwa ulitaka kumbambikizia Mosi mimba ili akuoe? Si kweli?” Kimya.

“Mimi nakujua sana Manda. Na ninahisi chuki yako na kisa cha kumtukana mwanangu ni kule kuzaliwa mweusi na hayo macho, akazaliwa anafanana na mimi asilimia 100, ukaishia kuachwa na Mosi.” Akaendelea.

“Wakati unamalizia masomo yako pale chuo cha Muhimbili, kwa maswala ya uuguzi, rafiki yako aliniambia mahusiano uliyokuwa nayo na rafiki yangu Mosi, na ukawatangazia pale chuoni, mimi hunipendi, unachukua pesa yangu tu, lakini Mosi atakuja kukuoa. Ulisema unanionea kinyaa mimi, isipokuwa pesa yangu.” Kimya.

“Baada ya kusikia hayo, tena kutoka kwa rafiki yako, nikaamua kukaa mbali na wewe kabisa. Wewe mwenyewe ukanitafuta. Ukaja mpaka nyumbani kwangu. Kwa kuwa nilijua nia yako ilikuwa pesa tu, nikakukaribisha siku ile sebuleni, sikutaka hata uingie chumbani kwangu.”

“Unakumbuka ukaomba mpaka kulala kwangu na tulikuwa hatujaonana zaidi ya mwezi? Nikakwambia ukweli wote niliojua juu yako, ukapinga.” Baba yake Tunda akaendelea.

“Ulimpigia simu rafiki yako palepale kwangu mkaanza kusutana. Nilikwambia kama ni kweli haupo na Mosi, umpigie simu mimi nikiwepo, na ajue upo kwangu. Ukanizungusha wee, mpaka nilipokwambia kama hutazungumza na Mosi, uondoke usiku uleule. Ndipo ukampigia simu Mosi, ukamwambia umeamua kurudi kwangu.”

“Siku ile ukalala kwangu, ukaamka na shida ya pesa. Ukasema kama hutamaliza ada, hutafanya mtihani wako wa mwisho. Nilikupa ada yote, ukaondoka kwangu. Sikukuona tena.”

“Baada ya miezi mitatu mkiwa mmeshamaliza chuo, nikamtafuta rafiki yako tena kukuulizia. Nikamwambia uliondoka kwangu ukisema utakuwa busy sana na mitihani, utanitafuta ukimaliza mitihani. Lakini sikukusikia tena. Ndipo nikaambiwa unaishi kwa Mosi.” Baba yake Tunda akajicheka kidogo.

“Nilivyokuwa nakuamini, nikambishia. Nikamwambia haiwezekani kwani wewe ulimkataa Mosi mbele yangu. Yule dada akanicheka sana. Akasema siku ile usiku ulinitafuta sababu ya pesa. Hukuwa na nia hata yakulala na mimi, ila nilipokufukuza, ndipo ukatafuta njia yakunirudisha kwenye mitego yako, ili nikupe pesa.”

“Na uliyempigia simu siku ile usiku hakuwa Mosi, ila rafiki yenu daktari alikuwa mwaka wa kwanza pale Muhimbili. Yeye ndiye uliyempigia simu, kwa kuwa hakuwa akikuelewa unachozungumza usiku ule ukimwita Mosi na kujidai unarudiana na Yohana, ulipokata tu simu, na yeye ndio akampigia Agi, kumuuliza Mosi ni nani na Yohana ni nani?”

“Ndipo wakaunganisha habari, wakagundua usiku huo upo kwangu kunichomoa tena pesa. Agi akanihakikishia upo kwa Mosi na ni mjamzito. Sikutaka mambo mengi. Nikakuacha kabisa.” Akaendelea.

“Sijui ulizaa mtoto aliyemfungua macho Mosi, sikuuliza kwa kuwa mimi na Mosi tuliacha mawasiliano kabisa baada yakujua anaishi na wewe, msichana aliyekufahamu kupitia mimi, tena kwa kumtambulisha kuwa ni mwanamke wangu. Mosi alihamishwa mkoani, wewe sikukuona wala kukusikia tena mpaka siku mbili kabla hujaniletea mwanangu.”

“Ukaniambia kama hivi Tunda alivyosema unamtukania weusi wake. Ukasema kwa kifupi tu, nijiandae, unaniletea Jaluo mwenzangu. Nikiwa sijakuelewa wala hukutaka nikuulize jambo, ulinikatia simu, ndipo ukaja kunitupia mwanangu ndani ya nyumba yangu, katikati ya ndoa iliyokuwa na matatizo makubwa sana.”

“Ukaondoka na kuacha moto ukiwaka, si kwangu tu, na kwa Tunda pia. Naomba ukanushe chochote nilichokusingizia Manda.” Kimya. Baba yake Tunda mtaratibu, ongea yake kama anayejihami kwa ugomvi.

“Chuki yako kwa Tunda haikuanzia kwa Tunda, ni kwangu. Sasa Tunda akaharibu zaidi alipozaliwa anafanana na mimi. Alikuwa ni kama amekupokonya tonge mdomoni, kwa kuwa ulitaka sana kuolewa na Mosi.”

“Nilisikia mpaka nyumbani kwenu ulimtambulisha, na alishalipa mahari ilikuwa bado harusi tu. Tunda akawa kosa ambalo ulishindwa kulisamehe wala kuliona, ukaamua kwenda kumtupa kwa mama yako.” Baba yake Tunda akanyamaza kidogo kama anayefikiria. Wote wakamtizama.

“Mungu anisamehe sana, lakini nakuhisi vibaya sana Manda.” “Juu ya nini?” Mama Tom akauliza kwa jeuri. “Kwa kuwa wewe ni mshenzi, mpenda pesa sana. Ulikuwa ukinufaika kwa yule baba watoto wako, NAHISI, ulijua unyama anaomfanyia mwanangu, lakini ukaamua unyamaze ili uendelee kujijenga, lakini Mungu amekupiga kofi, akavunja pale ulipojenga kwa kumwaga damu ya mwanangu.” “Wala mimi sikujua. Mbona nilimtoa mimba?” Manda alijitetea bila hofu.

“Ulivyo mbinafsi wewe! Nina uhakika, ulihakikisha yule baba hana mtoto mwingine wa nje, isipokuwa wako tu, ili mtu mwingine yeyote asinufaike na mali zake.” “Huo ni uzushi Yohana, na usitafute kujisafisha hapa. Hata wewe ulishindwa kumlea mtoto wako nilipokupa nafasi hiyo.”

 “Mimi nilishindwa. Wala sikatai na nilishamuomba msamaha Tunda. Lakini  je, mbona baba Tom alipotaka kumtafuta Tunda ili amsaidie baada yakumtoa mtoto wake, ulimtisha?” Mama Tom akashtuka sana, na Tunda pia. Akamwangalia mama yake na baba yake.

“Unafikiri sifahamu hilo? Hivi unajua mumeo nilifungwa naye gereza moja? Unajua kama nilitaka kumlipiza kisasi jela, ndio kuna afande akanionya kuwa nisikubali kosa la mumeo likanifanya nifie jela! Unajua hilo?” Kimya.

“Huwezi kujua kwa kuwa wewe ni mnyama, huwezi kutamfuta mtu asiye na manufaa kwako.” “Amenibakia mtoto wangu, bado nikamtembelee jela!?” “Mbona alipomfanyia ubaya Tunda, na yeye alikiri kuwa alikwambia kuwa alimbaka Tunda, mbona ulikubali kuendelea kuishi naye huku ukimtisha kuwa akimtafuta tu tena Tunda, utamshitaki?” Akamuuliza kwa kumsuta. Kimya.

“Swala la kubakwa kwa Tunda na mumeo wala leo sio mara yako ya kwanza kulisikia. Mumeo alishakiri. Kana kwamba haitoshi ndani ya nyumba hiyo hiyo mliyokuwa mkiishi alimbaka msichana wako wa kazi, mbona ukalifumbua macho na hilo? Ukawalipa wazazi wa yule msichana, mkaendelea na maisha yenu wala usimfukuze mumeo au kumfunga! Ukaendelea kula pesa yake bila shida.”

“Ilikuja kukuuma alipobakwa Aneti! Napo hapo pia anasema anahisi ni kwa kuwa alikuzunguka.” “Ni muongo yule mwanaume. Shetani mkubwa. Amekwambia nini na uongo wake?” Manda akawa na yeye amekasirika.

“Naombeni mnivumilie jamani. Mnipe muda kidogo, nimwambie ukweli Manda, labda kwa mara ya kwanza maishani atakuja kufunguka macho na kuwa mwanadamu wa kawaida. Tunda mama, nivumilie kidogo. Tutaondoka sasa hivi.” Tunda akatingisha kichwa kukubali.

“Asante. Jiegemeze kidogo hapo kwenye kochi.” “Mimi nipo sawa baba. Wewe endelea tu.” Tunda akajibu kwa utulivu akitaka kusikia yaliyojiri baada ya kutolewa mimba na kufikiri ametelekezwa hata na baba Tom.

“Habari za mume wako za tabia zake za kubaka zilienea pale gerezani. Mungu alivyomwema, nikaja kujua ni mume wako wewe, na ndiye aliyempa mimba Tunda. Nikawasimulia watu wangu wa karibu, maana nilishakuwa mwenyeji pale, wakasema tumfanyizie vibaya sana. Kwa kuwa nilikuwa na machungu, nikakubali bila kujua Tunda yupo wapi kwa wakati huo. Nilimuacha amepigwa, amevimba, yupo hospitalini hana msaada.” Akaendelea kila mtu akimsikiliza.

“Tukamkamata lijamaa lako likiwa bafuni linaoga. Yule baba alilia kama mtoto mdogo maana jamaa walishaanza kumkata na wembe. Akieleza kila kitu juu ya Tunda. Na akasema alikulaumu sana kuua kiumbe kisicho na hatia. Yule mtoto hakuchagua atungwe mimba wapi. Anasema ukawa ugomvi mkubwa sana, ndipo akaamua kumtafuta Tunda.”

“Mumeo alipoonekana hospitali ya Muhimbili, wafanyakazi wenzako wakakupigia simu, ukamfuata, maana muda wakuona wagonjwa ulikuwa bado na yeye alikuwa anapita mawodini kumuulizia Tunda.”

“Ukamtishia kumfungulia kesi ya kumbaka mtoto wake, na ukamuhakikishia utashinda kesi na yeye atafungwa kifungo cha maisha, akae mbali na Tunda. Yule baba akasema Tunda amefikisha miaka 18, anaweza kabisa kuolewa, na yeye anataka kumuoa Tunda.” Tunda akashangaa sana.

“Hapo ndipo ukamwitia askari. Akachukuliwa mpaka kituo cha polisi, akasema yeye hakuwa amembaka Tunda, Tunda anamiaka 18, aitwe yeye mwenyewe Tunda, aeleze. Ndipo ukamwambia utatengeneza kesi kuwa alikuwa ukimbaka Tunda kabla ya miaka 18. Yule baba akiwa hajui kama ilikuwa kitisho au la, akakubali kukaa mbali na Tunda, ndipo ukafuta kesi.”

          “Anasema lakini akashanga japokuwa alikubali, na akarudi nyumbani ukawa kama mwehu, ukapita kila nyumba, kuchafua jina la Tunda! Hapakutokea tena maelewano kati yenu, ndipo akambaka yule mtoto wenu wa kazi. Ukamwambia utamsamehe kama ile nyumba ya pale na Goba, ataiandika jina lako, na awe anakupa pesa kila mwezi zakutuma kwa wale wazazi wa yule binti ili kuwanyamazisha.” Kila mtu akamgeukia mama Tom kwa kumshangaa.

“Yule jamaa alikiri mbele yetu kuwa anatatizo kubwa sana linapokuja swala la ngono. Anasema akili inakuwa kama inamruka, anakuwa kama amepagawa halafu baadaye ndio kama anarudia hali yake ya kawaida. Na akakiri kabisa, akiwa kwenye ile hali, hawezi kuwaza wala kufikiria. Anakuwa kama amepagawa, mpaka aridhike. Ndio akili inarudi.”

“Ni kweli kabisa baba. Mimi mpaka nilimwambia labda anakuwa anapagawa mapepo. Maana anakuwa kama mwehu. Hatulii, anakuwa kama mtu anayetaka kufa kwa njaa wakati unakuta labda hapo ulikesha naye usiku uliopita. Na hawezi kusubiri! Na akikushika anakuwa kama mnyama, hana huruma.” Tunda akamkatiza baba yake, akakumbuka ile hali ya baba Tom mpaka machozi yalianza kumtoka tena. “Pole sana mama.” Baba yake akamuhurumia.

“Lakini aliongeza jambo jingine, kwa upande wa pesa na akili za kazini, walimtegemea. Anasema alijua wazi, akikupa mali zake utamshitaki tu. Akakukubalia masharti yako yote uliyompa. Lakini akakupa hati za nyumba zote, feki.” Manda akashtuka sana.

“Alisema mali zake zoote, aliandika majina ya ndugu zake. Tena kwa taarifa yako tu, mumeo alitumia akili ya haraka ili usije kushinda mahakamani kama mke wake uliyeishi naye kwa muda mrefu na mtu uliye zaa naye.”

“Akaamua kuandika kwa mkono wake kuwa amewauzia hao ndugu zake mali zake alizozitengenezea makaratasi mazuri tu, tena ya kihalali. Akaonyesha alishawauzia miaka 4 iliyopita, hata kabla ya wewe kumfunga jela baada ya kugundua alichokuwa akimfanyia Aneti.” Wote walimuona jinsi Manda alivyoshtuka.

“Anasema kwa maandishi, aliandika pale mlipokuwa mkiishi, Kitunda, mlipewa hifadhi na ndugu yake baada ya kuishiwa na kumuuzia pale ili apate pesa. Upo Manda?” Akamuuliza kwa kumkejeli.

“Eneo na mali zote za Goba ulikokuwa ukifanya miradi yako, pia ameandika ni mali za dada yake alizokuwa amemuuzia. Tena anasema alishaandaa karatasi zenye saini yake, ya kupokea malipo yote ya mauzo ya mali zake zote.”

“Amekiri, na alisema alikukomoa makusudi kwa kuua mtoto wake akijua nia yako ni mali. Alisema inawezekana yeye ana pepo la ngono, ila wewe unapepo la chuma ulete. Linapofika swala la pesa, na wewe huwezi kujisaidia. Unatoa yeyote kafara.” Baba Chale akamtizama kwa kumsuta.

“Kwa hiyo habari ndio hiyo. Poteza pesa, fanya lolote kwa huyo mwanasheria wako, ujue hutakaa ukashinda kesi. Huna mali. Wewe ni mshenzi Manda, na Mungu anakulipiza hapahapa duniani. Kalia makochi haya ya mwanangu. Na lalia kitanda chake, ili iwe hukumu yako. Kila kitu utakachokiona humu ndani, ukumbuke damu uliyomwaga ya mtoto wa Tunda, na Tunda mwenyewe.”

“Kila pesa utakayoingiza kwa kutumia kampuni ya Tunda, ikawe chungu kama uchungu aliokuwa akiupata mwanangu wakati akibakwa na mumeo.” Akamgeukia mama Penny.

“Mama Penny, wala huna haja yakumpokonya hivi vitu. Mwache atumie machozi na jasho la mwanangu. Vitampalia mpaka vimtokee puani. Wewe si ni mshenzi Manda? Basi utakumbuka ubaya wako wote uliofanya na kuufurahia hapa duniani. Labda Mungu aingilie kati, akusaidie. Hata hapa utapaona pachungu. Si unaishi kwa kodi ya Tunda wewe, jasho litakutoka wakati feni la Tunda linakupuliza.”

“Dua za kuku hizo Yohana! Hazinipati ng’o! Kwa taarifa yako napata tenda mpaka nazikataa. Napamba vizuri, kila mtu anasifia. Nina pesa. Hamnibabaishi kwa lolote.” “Sio wewe umetoka kuomba simu na gari kwa Tunda, ulipokataliwa ukaanza kumtusi mwanangu?” “Sina shida.” “Sawa. Twendeni.” Akasimama baba Chale au baba yake Tunda, akafungua mlango akatoka. Wengine wakamfuata nyuma.

Mama Penny aliingia kwenye gari yake, akarudi kwake, Net ambaye alikuwa dereva, akaondoa gari kurudi hotelini akiwa na Tunda na baba yake Tunda.

Tunda ahama nchi.

M

ama Penny na familia yake walikuwepo uwanja wa ndege kumuaga Tunda na mumewe. Baba yake pia alikuwepo. Ulikuwa ni utengano ambao kila mmoja alikuwa na hisia tofauti tofauti juu ya Tunda kuondoka. Wakati mwingine walimfurahia, wakati mwingine waliingiwa hofu wasijue kinachomkabili ng’ambo ya pili ya dunia.

Walikatiwa tiketi first class. Tunda alikaa dirishani. Net alihakikisha anavaa nguo ambazo hazitamsumbua baridi, akamuombea na blangeti hapo kwenye ndege, akamfunika.

“Nashukuru kurudi na mimi Tunda. Angalau akili zitatulia, nitaweza kufanya kazi nikiwa nimetulia. Nikijua upo nyumbani unanisubiri.” Tunda alitoa tabasamu lililojaa maswali mengi, akijiambia muda ndio utajibu maswali yote.

Ndege ilianza kuviacha viwanja vya ndege vya Mwalimu nyerere, Net akaushika mkono wake, na kuubusu. Tunda alivuta pumzi kwa nguvu akajiweka sawa.

“Asante Net. Nakushukuru mpenzi wangu.” “Karibu. Naamini tutakuwa sawa.” “Hata mimi naomba Mungu iwe hivyo.” Wakatulia, safari ikaanza wakiwa wametulia. Hofu kidogo kwa Tunda.

Ndege ilipotulia angani, akaweza kulala Net akiwa amekilaza kiti chake mbavu zisimuume. Aliamka baada ya masaa matatu, Net akiwa amelala. Akatoa mkoba wake, akaanza kusoma barua alizokuwa akiandikiwa na Net kipindi yupo jela.

Zilikuwa barua na kadi tofauti tofauti nzuri. Nyingine za kuomba msamaha na nyingine zakumwambia ni kiasi gani anampenda na kumuomba atoke angalau amuone.

Tunda akaanza kutokwa na machozi na kujutia kutosoma faraja kubwa aliyokuwa amefumbia macho. Habari za kufutiwa kesi mbili alizosababisha Net mwenyewe zilikuwemo kwenye moja za barua hizo. Kuwa alirudi kuishi nchini Canada na anafika hapo nchini kwa ajili yake, pia alimwandikia.

Net alifungua macho akabaki akimtizama anavyosoma. Mara nyingine alimuona akitulia kama akifikiria. Analia na kugeukia dirishani, kisha anaendelea kusoma. Net alipomuona anamgeukia akafunga macho haraka, akajidai amelala.

Akahisi anamnyanyua mkono na kuubusu. Akamcheka moyoni. Akajigeuza kumgeukia vizuri, huku akijidai amelala. Akajua anamwangalia. Aliposikia mlio mdogo wa karatasi, akajua anaendelea kusoma. Akatulia kabisa kama kumpa nafasi mpaka amalize.

Safari ilikuwa tulivu, Net alijitahidi kwa kadiri ya uwezo wake kumsaidia ili asichoke au kuumwa mbavu. Kumgeuza na kumuwekea mto huku na kule, ilimradi tu asichoke. Alitaka walale Dubai, lakini Tunda alimwambia yupo sawa tu, waendelee. Hilo pia alilifurahia Net, ili tu awahi kazini.

Tunda atua nchini Canada.

W

alifika nchini Canada, ilikuwa baridi ndio inaanza.  Sio kali kwa wenyeji lakini si kwa Tunda. Mwezi huo wa 9, kwa Tunda alihisi baridi kali sana. “Pole na safari.” Tunda akacheka. “Na wewe Net. Hujachoka?” “Nimeanza kuzoea. Nimefanya hizo safari miezi sita mfululizo kama rubani!” “Pole mpenzi wangu.” Net akacheka tu akijua amepata ukweli wote kwenye zile barua. Akajua kilichokuwa kikiendelea wakati yupo jela, mwenzake akienda kumtembelea na kukataa kumuona. Akajua ile pole ni ya mengi.

Tunda alishangaa hayo mapokezi. Ni kama Net aliandaa kila kitu. Maya na bibi yake walikuwepo uwanjani hapo na nguo nzito zaidi kwa Tunda ambaye alikuwa mgeni kwa baridi. Maya akamsadia kumvalisha zile nguo. Kuanzia usoni mpaka buti nyepesi za manyoya. Walimfurahia sana Tunda, mpaka Tunda aliweza kuona usoni mwao, akafarijika na hofu ikaanza kupungua.

Gari kubwa ilikuwa ikiwasubiria nje, na yenyewe ilikuwa imewashwa upande wa joto na dereva alikuwa ndani akiwasubiri. Ilikuwa gari ya thamani sana iliyomtoa macho Tunda. Kulikuwa na dereva mwingine na gari ambayo ilikuwa ikichukua mizigo ya kina Tunda.

Alichokifanya Net alipofika pale uwanjani alitoa maagizo juu ya mizigo yao kwa yule dereva wakati yeye akikumbatiana na bibi yake na Maya. Akamuachia jukumu yule dereva. Alipopata mabegi, akamuonyesha Net, akakubali kama niyenyewe. Yalikuwa na majina ya Cote.

Aliyachukua yale mabegi bila hata kuambiwa, akaondoka nayo wakati Maya akimvalisha Tunda koti zito la baridi, skafu, buti hizo za baridi, kofia, gloves, ilimradi kumsitiri na baridi.

Hakujua kilichoendelea kwenye mizigo yao, ila akaona anaelekezwa kwenye gari ingine. Alifurahia ile hali ya joto aliyoikuta mle ndani ya gari. Akajikuta anaanza kusinzia wakati Net akiongea na kucheka na bibi yake pamoja na Maya viti vya nyuma.

Aliweza kumsikia mumewe akitoa habari za safari. Alitaka Tunda ndio akae kiti cha mbele ili aweze kumlazia kiti kidogo. Mbavu zilikuwa zikimuuma.

“Hakupata shida sana. Ila mbavu ndio zilikuwa zikumuuma.” “Anakula vizuri? Mwili wake umeisha sana!” Alimsikia bibi Cote akiongeza hilo swali. “Anavitu ambavyo anapenda. Akivipata hivyo, anakula bila shida.” “Natumaini na huku atapata vitu anavyopenda ili ale. Hivyo alivyo hawezi kubeba mtoto wa miezi 9. Amedhoofu sana.” Yule bibi alimuona wakati anamkumbatia pale uwanja wa ndege na wakati Maya akimvalisha.

“Atakuwa sawa. Naamini akipumzika kwa mwezi mmoja mbele, asiugue, atarudisha nguvu.” Net akaongeza. “Tutumaini hivyo. Akipumzika leo na kesho, kesho kutwa tutampeleka kwa dakatri. Aanze kliniki lakini nilimwambia amfanyie vipimo yeye na mtoto. Ili tuwe na uhakika kuwa wapo salama.”

“Asante Nana. Ndio maana nakupenda.” Akamsikia mlio wa busu. Wakacheka. Yeye kimya. Alikuwa amejilaza huku macho yapo nje ya dirisha yakifunga na kufungua kwa usingizi. Ni kweli alisikia vichomi. Ilikuwa safari ya masaa 18. Alikuwa amechoka.

~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~

Macho yalimtoka alipooona wanaingia ndani ya geti. Ikabidi afungue macho vizuri. “Utafikiri jumba la kifalme!” Tunda akashangaa sana. Bustani iliyokuwa imetokea getini ilikwenda mpaka kwenye hilo jumba. Ilionekana ni kama ya miaka mingi, kama jumba la maonyesho au kihistoria.

Wasiwasi ukamwingia Tunda. Dereva akasimamisha mbele kabisa ya hilo jumba. Net akaenda kumfungulia mlango. “Vipi?” “Natamani tu kulala.” “Basi ndio itakuwa kitu cha pili.” “Cha kwanza ni nini!?” Tunda akauliza huku akishuka garini. Baridi kali ikaanza kumpiga.

“Kula, ndio ukalale. Karibu nyumbani.” Tunda akanyanyua macho kutizama. Ilikuwa usiku. “Pazuri!” Akasifia. “Hii ni nyumba ya zamani sana. Hata baba yangu alizaliwa hapa.” Tunda akamtizama Net, Net akacheka.

“Kwa hiyo na wewe umezaliwa hapa?” “Na Maya pia.” Tunda akacheka huku akitingisha kichwa. “Kazi ipo!” Alikuwa amemshika mkono wakipandisha ngazi zilizojengwa hapo kwa mtindo wake, wakielekea ndani.

“Karibu sana Tunda.” Aliongea Maya kwa lugha ya Kiswahili nakumfanya Tunda acheke na kugeuka kidogo. “Hujasahau tu kiswahili!?” “Nakumbuka vitu vyamuhimu.” Bibi Cote naye alikuwa ameshashuka kwenye gari, akamkaribisha Tunda.

Alipofika katikati ya hizo ngazi na kugeuka nyuma kumtizama bibi Cote na Maya waliokuwa wakimuongelesha kwa kumkaribisha, Tunda akabaki ameduaa vile ule uwanja na mataa yake vilivyo. Akazungusha macho kidogo kule macho yake yalipoweza kuona kwenye mwanga wa taa zilizozunguka bustani mpaka getini. Akaona aingie tu ndani asitie aibu hapo nje.

Alipoingia ndani ndipo alipostaajabu zaidi. Jumba lilikuwa kubwa, na vitu vilivyojaza humo ndani vilionekana ni vya thamani sana, lakini vyote vilionekana ni vya zamani.

Kulikuwa na picha mbalimbali kubwa kwenye ukuta. Kusafi na wafanyakazi aliowakuta hapo, wawili. Mfungua mlango alikuwa babu mtu mzima zaidi ya bibi Cote. Alikuwa kwenye sare. Suti na gloves nyeupe. Mwanamke aliyemtambua kama maid, naye alikuwa kwenye sare. “Hapa kazi itakuwepo!” Akajiambia Tunda, kisha akamtizama Net.

Akamuona anamcheka. “Sasa unacheka nini na wewe Net!?” “Kesho nitakuonyesha video niliyokuchukua. Ni umeshangaa, mpaka raha.” Net akazidi kucheka. “Naomba uifute Net, bwana!” “Lazima tuiweke ukumbusho.” Tunda akacheka. “Sasa kwa nini hukuniambia kama tunakuja kwenye jumba la kifalme?” Mpaka Net akacheka kwa sauti.

Bibi Cote akawageukia. “Kuna nini?” Akamuuliza Net. “Naona amechoka tu. Atakuwa sawa.” Net alijibu huku akimcheka Tunda. “Sasa hapa ili nisiendelee kutia aibu zaidi, nipeleke chumbani kwanza. Nataka nijisaidie halafu nijilaze kidogo. Mbavu zote zinauma!” Wakaongozana.

Tunda aliendelea kushangaa korido nzima wakiwa wanaelekea huko chumbani kwa Net. Kila kitu kilipangiliwa kwa ustadi wa hali ya juu. Upande mmoja wa hizo kuta, aliweza kuona picha kubwa sana zilizopangwa kwa mpangilio. Baba ya babu yake Net, akaja babu yake, baba yake kisha picha kubwa ya Net. Na zote ni nusu, wakiwa wamekaa na mavazi nadhifu sana. Picha kubwa na fremu za chuma kizito cha dhahabu.

Akaendelea kumfuata Net kwa nyuma. Akamuona anafungua lango kubwa. Tunda akavuta pumzi. “Hiki chumba nilikilalia tokea siku ya kwanza naingia humu ndani.” Net aliongea wakati anampisha mlangoni aingie. Mlango wenyewe ulionekana wa zamani halafu wathamani.

Kuingia humo ndani upande mmoja wa ukuta ulikuwa na picha za Net tokea ana siku ya kwanza mpaka ya harusi yake na Tunda. Zilipangiliwa vizuri. Tunda akaduaa. Hakuwa hata akijua kama kulikuwa na picha za harusi! Kilikuwa ni chumba kikubwa sana, kizuri. Jinsi kilivyokuwa kikubwa hicho chumba ni kama nyumba ya mtu. Akabaki ameduaa, asielewe ni nini Net amempendea yeye!

Akarudisha macho nyuma. Alipita picha iliyomshangaza. Net alikuwa ameinama akimvalisha ile cheni ya mguuni. Akamgeukia Net. “Kwani siku ile pale hotelini, kulikuwa na mpiga picha!?” “Nilimwambia asisumbue, ndio maana hukumuona. Ila nilimleta kutoka huku sio mtu wa kule.” Tunda akakunja uso, na kurudisha macho ukutani. Ilitengenezwa vizuri sana. Kuanzia picha yenyewe mpaka ilivyoundwa pale ukutani.

Akagundua Net yule wa Tanzania, siye huyu wa nchini Canada hata kidogo. Taratibu akaanza kuelewa ni nini Mama Cote alikuwa akimaanisha. Huo utajiri aliokuwa akiongelea. Akameza mate. “Utajikojolea Tunda! Twende chooni.” Tunda akacheka na kumfuata Net nyuma. Kuingia tu chooni, akasimama katikati ya kile chumba, akaanza kuangaza macho.

“Usingizi wote umeisha! Kesho nitakuwa na kazi yakupiga picha nimtumie mama Penny, dada yangu. Tushangae wote.” Net alicheka sana. “Unafikiri Net?” “Naelewa Tunda. Hata mimi najua kama ni pazuri. Bibi anatumia pesa nyingi sana kupatunza hapa. Kila kitu hapa kina historia yake. Hakuna aliyewahi kufika hapa, akatosheka. Kwa hiyo hata mimi naelewa. Sikushangai.” “Afadhali.” Tunda alielekea chooni, akatoka. Alimkuta Net akimsubiria nje.

“Naomba ukajaribu kula ndio ulale.” “Nimechoka Net, kuja kuanza kula vyakula ambavyo sivielewi naweza kuanza kutapika, nikaishia kushindwa kulala. Acha nisijitibue kwa usiku huu, nilale.” “Kabla hujakaa, naomba twende ukaangalie. Nana na Maya wanatusubiria. Twende.” Akiwa amechoka, akajivuta taratibu akimfuata Net nyuma huku akitupia tena macho kulia na kushoto.

Kwanza alisimama alipofika sehemu ya kulia chakula. Akabaki amepigwa na butwaa. Bibi Cote na Maya walikuwa wamekaa mezani wakiwasubiria. “Wametupa recipe ya hiki chakula, wamesema huwa unapenda kukila. Na aina ya uji. Chef amejaribu kupika, naamini utapenda.” Bibi Cote akavunja ukimya.

          Meza ilikuwa imeandaliwa, kama hotelini! Hicho chumba chenyewe tu na aina ya viti pamoja na meza yenyewe, vilimtoa macho Tunda. Aliyekuwa akihudumia pale alikuwa kijana wa kizungu, mrefu, mzuri na amevaa sare maalumu, akionyesha kweli yupo kazini.

Net akamvutia kiti. Tunda akakaa. “Asanteni sana.” Tunda alishukuru kwa lugha yao. Na wote mle ndani walikuwa weupe kasoro Tunda tu.

Alicheka alipoona ndizi za kupikwa Canada. Akamwangalia Net. “Nilimuomba mama Penny aniandikie kila kitu na vipimo vyake, nikamtumia Maya, Maya akampa chef, sasa onja kama amepatia.” “Asante Maya.” Maya akacheka na kubaki wakisubiria aonje ili wajue kama atapenda.

“Tunatamani ule vizuri Tunda. Umekonda sana!” “Nitakuwa sawa. Niliugua sana. Karibu kipindi cha miezi mitano nyuma, sikuwa nakula vizuri. Magonjwa yalikuwa yakipokezana. UTI haikuwa ikiisha. Hata first trimister ya mimba, haikuwa rahisi. Naamini nitakuwa sawa tu.”

“Tutakwenda kwa daktari kuangalia afya yako na ya mtoto. Wakupe na kinga zakukufanya usiugue tena ili urudishe nguvu na mwili. Uweze kubeba mtoto vizuri.” Aliongeza bibi Cote. “Nitashukuru.”

Net alimuwekea chakula kwenye sahani. “Jaribu.” Tunda akajisogezea karibu. Akaweka mdomoni. Wakamuona anacheka. “Nikizuri.” Tunda akasifia. “Asanteni.” Akashukuru akiwatizama wote, maana ni kama wote walitulia wakimsubiria wajue kama atapenda kile chakula.

Alimsikia Net akivuta pumzi kwa nguvu. “Hey Gino! Thanks Man. She likes it.” Net aliongea kwa sauti, akasikia mtu upande wa pili akicheka. “You’re the best, Gino.” Maya akaongeza kutoa sifa wakimshukuru huyo Gino. Tunda hakuwa ameelewa Gino ni nani, lakini akahisi ndiye mpishi. Alicheka tu taratibu akaendelea kula.

Bibi Cote alikuwa kimya akitabasamu na bakuli dogo tu, Tunda alijua ni supu. Kwa aina ya kijiko alichokuwa akitumia na bakuli kama kikombe. Akaamua atulie na sahani yake ya ndizi.

Mara yule kijana aliyekuwa akipanga chakula pale mezani akarudi pale kutoka chumba cha pili, ambapo alijua ndio itakuwa jikoni. “You are welcome guys.” Akajua ndio Gino.

“Ni nini nilitakiwa kuongeza au kupunguza?” Akamuuliza Tunda kwa heshima sana. Wote wakamtizama Tunda. “Mwambie ili kesho akupikie vizuri zaidi.” Akaongeza Maya. “Nakiona kipo sahihi kabisa. Nimependa, asante Gino.” “Karibu sana.” Hapo Gino alijibu kwa Kiswahili sio kingereza tena, nakufanya meza nzima wacheke.

Hata hivyo alisikika na lafudhi tofauti na bibi Cote au hata Maya. Tunda akajua sio mtu wa pale. Aliongea kingereza chenye lafudhi nzito kidogo.

“You did your homework good, Gino!” “With Maya’s help too.” Gino akamjibu Net huku akicheka baada yakusifiwa na Net. Wakacheka. “Nakushukuru sana. Utayafanya maisha ya Tunda kuwa rahisi. Na samahani kukufanya kukaa kazini mpaka muda huu.” “Chochote kwa ajili yako, Net.” Gino akajibu kwa heshima sana. Net akatabasamu.

“Nafikiri unaweza kwenda tu kupumzika. Tutamalizia sisi wenyewe hapa mezani, kesho utakuja kuendelea pale tulipobakisha.” Net aliendelea kuzungumza na Gino kwa lugha ya Kingereza. “Una uhakika?” “Kabisa. Sasa hivi ni usiku sana, najua na wewe ungependa kwenda kupumzika. Lakini kabla yakuondoka, naomba nikutambulishe kwa mke wangu. Najua yeye ndio mtakuwa naye hapa kwa muda mrefu.” Tunda akanyanyua uso kumtizama Net, natabasamu usoni.

“Kwa hiyo huyu ndiye mama Cote mwenyewe?” “Haswaa!” Net alijibu kwa kujivuna kidogo. “Kweli ni unique kama ulivyokuwa ukituambia. Na ni mzuri.” “Asante Gino.” Wakati wote Gino alizungumza huku mikono ameikutanisha mbele kwa heshima zote.

“Karibu sana Tunda.” Gino akaongea tena kwa Kiswahili chakuunganisha kidogo. Tunda akacheka, “Asante Gino. Nitakufundisha mapishi mengi ya Kitanzania.” Akajibu kwa kingereza ila ‘Asante’ kwa kiswahili. “Na lugha pia.” Gino akaongeza, wakacheka tena kidogo. “Bila shaka.” Akajibu Tunda. Gino akaondoka baada yakuwaletea baadhi ya vitu pale mezani. Kama matunda, juisi na maziwa kwa bibi Cote. Akaaga na kuondoka.

Tunda alikula vizuri, lakini akakataa kunywa juisi. Akamwambia Net atashindwa kulala kama atakunywa juisi au maji. Atakuwa akiamka kwenda chooni usiku wote.

“Kesho tutakwenda kazini. Kama tutaondoka mkiwa bado mmelala, basi mjue atakuja msaidizi wa Tunda, ambaye atakuwa akikusaidia mambo ya mtoto pia. Nilimwambia aanze kazi mapema kidogo, ili mzoeane kabla ya mtoto kuja. Na mtu wa kukufanyia masaji.” Tunda akatoa macho vizuri na kumgeukia Net. Net akacheka.

“Asante Nana. Ndio maana nakupenda! Nitakuja kazini mchana, baada yakumuonyesha mazingira Tunda.” “Hakuna shida. Wewe pumzika tu.” “Sawa, lakini nitakuja ofisini mchana.” “Sawa.” Bibi Cote akajibu. Net akaenda kumbusu pale alipokuwa amekaa, akambusu na Maya. Wakaondoka kurudi chumbani.

 

Net & Tunda!

T

unda akamvuta Net kwenye kochi mara baada yakuingia chumbani kwao. “Kwanza hembu njoo ukae hapa mimi niulize maswali.” Net akaanza kucheka. “Ujue wewe Net ni mbaya sana?” “Nini tena?” “Kwa nini hukuniambia kama haya ndio maisha ya huku kwenu!?” Net alizidi kucheka.

“Unaishi kwenye jumba la maonyesho! Mnampishi anayewapikia, tena maalumu! Mnakaa mezani kama wafalme, mnahudumiwa! Vyakula vinasindikizwa sijui na nini! Mnaanza na supu, sijui mnakula nini na nini, mlo mmoja!” “Ni full course dinner, Tunda.”  Net alimsaidia huku akicheka sana.

“Ewaah! Hiyo hiyo. Sasa hiyo ni leo tu kwa kuwa mimi nilikuwepo au siku zote?” Net alitingisha kichwa kukataa huku akicheka sana. “Basi kazi ipo! Haya, mnajifunika vitambaa vinavyoendana na…” “Ni napkins.” Net akaongeza akicheka sana.

“Bwana mimi leo jasho limenitoka! Sasa ulaji ule na utaratibu wake itakuwa kila siku!?” Net alicheka mpaka akainama. “Net hujanitendea haki bwana! Ungeniambia mapema.”  “Nisikilize Tunda. Acha nikwambie ukweli. Hapa nchini, au haya maeneo, ukiuliza matajiri wa hapa, hutakosa kusikia jina la Cote. Tunafahamika sana. Bibi na babu, wametafuta mali na wakafanikiwa sana. Wamewekeza kwenye hii aridhi, kwa kiwango kikubwa sana.”

“Kwa kifupi tu, yale yote aliyokwambia mama kwa sehemu, japo kwa wakati ule sikutaka kwenda kwa undani, ni kweli. Pesa ipo. Nilikuja kuishi Tanzania moja ya lengo kubwa ni kutafuta mwanamke atakayenipenda kwa vile nilivyo mimi, wala si jina au mali.” Tunda akaanza kuishiwa utani.

“Wengi wa wanawake hapa, nikisema wengi, namaanisha wapo wengi sana. Wanampenda Nathaniel Cote kwa sababu ya mali. Na mbaya zaidi, hakuna mapenzi ya kweli. Wakiingia kwenye ndoa kwa muda mfupi tu watataka talaka ili muachane, wanufaike na mali ambazo wananufaika kwa ndoa waliyoingia kwa muda mfupi sana.”

“Walihangaika sana kwa babu. Kwa kuwa babu alibahatika mwanamke mzuri, yaani Nana, hawakuwahi kutengana. Upendo ukawa siri ya mafanikio yao. Hakuna sehemu ungewatengenisha, kuanzia nyumbani mpaka kazini. Nana alimkuta papa akifanya kazi na baba yake kwenye ile kampuni, akatulia, akafanya nao kazi, mpaka wote wamefariki wakamuacha Nana.”

“Unakumbuka nilikwambia habari za Chloe?” Tunda akatingisha kichwa. “Chloe alinikubali kwa haraka sana. Nikataka kujua kwa hakika kama kweli anampenda Net au utajiri. Nilimpa maisha mazuri sana hapa nchini. Sasa nilipomuomba kama anaweza kuongozana na mimi Tanzania. Nilipata jibu langu pale aliposema yupo radhi anisubirie hapa nchini, kuliko kuhama naye nakumpeleka nchi masikini kama Tanzania.”

“Aliniomba nimuoe, halafu nimuache hapa nyumbani, yeye atanisubiri tu. Nikajua moja kwa moja anachotaka nikuishi humu ndani. Ndipo nikamwambia babu, Chloe sio Tunda.” “Sasa wewe ulijuaje kama mimi ndio mkeo wakati ulinikuta kwenye mazingira ya ajabu tokea mwanzo!?” Ikabidi Tunda kuuliza.

 “Kwanza wewe nilikupenda tu. Yaani nilikuta moyo wangu umefungamanisha na wewe, siwezi kujisaidia.” Tunda akacheka kidogo. “Ombi kubwa na hata bibi nilimuomba azungumze na mama, tena kwa kumtisha, ni asikwambie ukweli wote juu yangu. Lakini akawa ni kama anashindwa akihisi ni kama unajua kwa kupitia mimi mwenyewe au Gabriel.”

“Ndio maana akawa anahangaika akihisi unanipendea pesa. Lakini nilimuhakikishia kuwa hunifahamu kwa undani na nikiwa na wewe huwa hatuzungumzii mali kabisa. Nikamuhakikishia mama kuwa wewe hunipendei pesa, na wala hutaki pesa yangu. Nikamwambia nilishajaribu mara kadhaa kutaka kukusaidia, lakini ulikuwa ukikataa.” Tunda akazidi kushangaa kila alipofikiria kumbe alikuwa akisomwa na Net!

“Hukufanya vizuri Net!” “Hapana Tunda. Ninahaki yakupendwa mimi kama Net. Sikuchagua kuzaliwa na kina Cote. Sikutaka hili jina, lininyime furaha maishani. Ndoa ni ngumu Tunda, hasa hapa nchini kwetu na watu wa asili ya huku. Wengi wanaendeshwa na hisia. Wanandoa wengi wanaoana sababu ya mali. Nyumba hazina amani sababu ya mali.”

“Hilo babu amekuwa nalo makini kuanzia kwa baba yangu mpaka kwangu. Alitufundisha hivyo kwa makini, ndio maana hawabagui rangi. Ilimradi ukisema anafaa, hawana neno. Watakuheshimu kwa heshima ileile wangemuheshimu mwanamke mweupe ambaye angeolewa hapa.” “Unajuaje? Kwani wewe ulishawahi kuoa kabla?” Tunda akauliza.

“Baba amemuoa mwanamke wa Tanzania. Mama alipendwa na kutumikiwa humu ndani, mpaka alipoamua kuondoka yeye mwenyewe. Sikuwahi hata kumsikia akilalamika kuwa anafanyiwa ubaguzi. Katika yote hilo hajawahi kulisema hata mara moja.”

“Ila mimi namuogopa bibi yenu bwana! Anaonekana yupo serious sana akizungumza na watu wengine mbali na wewe na Maya, sura inakuwa ya kazi tu!” Net akacheka. “Akiwa na wewe na Maya, utafikiri sio yeye! Mtu wa tofauti kabisa! Sura na sauti inakuwa ya tofauti kama mama anayelea watoto wadogo wakati ni nyinyi wakubwa wazima!” “Utamzoea tu. Na yeye atakuzoea. Mpe muda.” Tunda akajivuta nyuma akiwaza huku akiangaza macho kwenye hicho chumba kimoja tu, cha Net. Akawa kama kuna habari imepita kichwani mwake kwa gafla.

Akamwangalia Net, na kukunja uso. “Sasa ingekuaje kama ningekataa kuja huku?” “Kwanza siku ile pale hotelini uliniogopesha sana Tunda! Kwa sababu nilishampigia simu Nana nikamwambia umekubali kuja na mimi. Swala la kuwa unanipenda, hilo halikuwa na swali tena. Ulishanionyesha unanipenda na umenichagua mimi. Ndio maana sikukukatia tamaa hata ulipokuwa jela. Nilishamwambia Nana, wewe ndiye mwanamke utakayeishi na mimi humu ndani na kunizika.” Hilo likamgusa Tunda, akatabasamu.

Net akaendelea. “Wasiwasi ukamwingia kama utaweza kusamehe ubaya uliofanyiwa na mama yangu! Maana alijua kuwa mama Penny na mumewe walinilaumu sana na wao ndio wako karibu sana na wewe.” Tunda akakunja uso akiwa hajaelewa.

“Mama Penny alikulaumu!?” “Oooh vibaya sana! Walinibana kwa shutuma za kweli tupu. Ni kama walinifukuza nyumbani kwao kwa hasira siku ile. Maana kabla ya harusi, yaani siku ile ya harusi, mama alipokuja na kuondoka kwa hasira, unajua baba Penny alinisihi niahirishe harusi mpaka nikaweke mambo ya familia yangu sawa?” “Sikujua!” Tunda hakuwa akijua lolote hata kama mama Cote alishamfuata mwanae pale kwake siku ile ya harusi.

“Basi siku ile ilikuwa mbaya, nusu harusi isifungwe. Anyways, nikakataa ushauri wa baba Penny wa kuahirisha harusi. Ndoa ikafungwa ndipo sasa ukaishia jela! Mama Penny na mumewe walinichukia sana. Mpaka nikashindwa kumtafuta baba yako, nikajua na yeye itakuwa hivyo hivyo.” “Pole sana Net. Mimi sikuwa najua yote hayo!” Tunda akajikuta akimuhurumia.

“Sasa huo moyo wako wakunihurumia nakujali ninachokisikia, ndio kitu kilikuwa kikifanya nione siku haziendi nirudi Tanzania kuja kukuona jela, na kukaa pale bila kukata tamaa, nikijua labda unaweza kuja kutoka, ukaniangalia. Lakini wapi.!” Tunda akacheka.

“Usicheke Tunda. Was not Funny!” “Si ulishasamehe lakini na ukasema umejilipiza?” Net akacheka, akakumbuka usiku aliofanya naye mapenzi, yeye akaridhika bila kumridhisha Tunda, akamwambia amejilipiza.

“Sasa nikaja kukutana na baba yako pale gerezani, hana hata lawama, amejawa tu shukurani. Wewe ndio ukawa hata hujui ni kwa nini najilaumu. Nikasema asante Mungu wangu kwa mke. Halafu ukatoka mjamzito! Nilijiambia kufa na kupona, damu ya Cote haipotei bure. Ukanipotea kama week mbili. Nikakaribia kuchanganyikiwa. Na ile hali yako ilivyokuwa baada yakutoka jela, nikawa namwambia mama Penny labda utakuwa umezidiwa ukafia sehemu.” Tunda akazidi kucheka.

“Lakini niliwatumia ujumbe wewe na mama Penny kuwa naumwa, nimepewa dawa. Tena wewe nilifanya vile makusudi ili nisije kunywa zile dawa kali, mwanao akatoka, ukasema nimemuua. Nikajiambia nikwambie mapema!” “Ulituma ujumbe na kuzima simu! Acha nizidi kuchanganyikiwa nikawa kama mwehu namsumbua mama Penny kila wakati. Mara baada ya majuma mawili, mama Penny akanipigia, akaniambia umempigia, unataka akupe kazi. Lakini umeahidi utanitafuta. Nilikesha nasubiri simu yako, Tunda.” “Pole!”

“Usiku sana kama saa 7 hivi, uvumilivu ukanishinda. Nikampigia tena mama Penny. Ndio akaniambia huwa ukiahidi kitu lazima utafanya. Akaniambia pengine unaweza ukawa umeishiwa muda wa maongezi kwenye simu. Lakini akanifariji na kuniambia lazima utatokezea pale ukumbini, nikufuate pale. Usipotokea, hapo hata yeye atapatwa na wasiwasi.”

“Ndio nikakupata pale, nikaja kukugundua sio kwamba ulikuwa umenikasirikia, ila ulihitaji muda wakupumzika. Mbali na mimi na mama yangu.” Tunda akacheka sana.

“Maana nilijiambia hata kama tutarudiana, na mama Cote akaamua kunisingizia kitu kingine, anirudishe jela, basi angalau niwe nimelala kitanda kizuri, nimepumzika. Kuliko anikamate tena kwa haraka, nikiwa nimechoka vile! Nikajiambia ningefia jela siku ya kwanza naingizwa huko. Ehee, Endelea.” Tunda alitaka Net aendelee.

“Basi, ndio nikakupanga, nikaona kumbe hukuwa hata na chuki na mimi, ukakubali kila nilichokwambia. Ndio nikampigia simu Nana nikamwambia narudi na Tunda. Akafurahi, sasa nikashangaa baadaye unanigeuka!” “Mama Penny na mumewe waliniogopesha bwana!”

“Ndio utake kunikimbia!?” “Si hapa nipo na wewe?” “Mmh! Lakini ulinikataa kwanza!” “Ni hofu tu Net. Siwezi kupata mtu anayenithamani kama wewe. Mimi mwenyewe nilikuwa kama wewe. Natafuta mtu atakayenipenda mimi kama Tunda na matatizo yangu yote.” “Basi umempata.” Net akaanza kumbusu.

“Uishie hapo hapo Net. Mwenzio nimechoka, mbavu zinauma, nataka nioge, nilale.” “Hivyo hivyo ukiwa umejilaza, mimi napata starehe yangu. Sikusumbui. Nipe ‘Kijiko’.”  “Lakini ujue utanisafisha na kunifunika. Mimi sijigusi.” Tunda akatoa sharti akijua atashindwa.

“Na hivi nililala kwenye ndege, hata hapa nitakubeba mpaka bafuni. Nikuogeshe na kukuweka kitandani.” “Kwani mimi sikujui janja yako? Ukifika bafuni utataka nikupoze kwa kunibeba!” Net akaanza kucheka.  “Tunda kwa kuhesabu mambo ya nyuma!” “Wewe twende tukaoge, halafu upate kijiko, moja tu yakunikaribisha nyumbani. Uchovu ukiisha, kazi itakuwa moja.” Net akamnyanyua kutoka pale kwenye kochi, akakimbia naye bafuni. Mapenzi yalianzia bafuni, wala hawakuweza kusubiri mpaka kitandani.

Tunda akapata penzi la kwanza ndani ya jumba hilo, kwenye chumba hicho cha thamani. Kwa yale tu mandhari, kila alipoguswa kwa penzi, haraka sana aliridhika na kumaliza kwa kufurahia. Akachangamkia mchezo kwa raha zote.

~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~

Je, Tunda ndio ameyapatia maisha huko nchi ya ugenini tena uzunguni, kwenye utajiri? Kweli wenyeji wamempokea vizuri sana.

Je, vita yake ndio imeisha? Ritha atakubali kusikia Tunda yupo mjengoni akitumikiwa halafu yeye ameuza kila kitu anaishi kwenye apartment ndogo tu? Usiache kufuatilia kujua mvujisha siri kwenye vyombo vya udaku huko nchini Canada. Endelea kufuatilia.

CONVERSATION

0 Comments:

Post a Comment