Naomi Simulizi |+1 205 767 8163 |naomisimulizi@gmail.com Nilipotea! – Sehemu ya 12 . - Naomi Simulizi

Nilipotea! – Sehemu ya 12 .

 

T

unda hakutembea hatua nyingi kutoka kwenye gari ya Kinny, simu yake ikaanza  kuita. Akapokea. “Kesho nina safari ya Dodoma. Naondoka na ndege ya mchana. Ni  safari ya kibiashara. Naomba nisindikize.” Tunda akacheka. Acha kunicheka Fina!” Unataka nikusindikize?” “Tafadhali sana.” “Saa ngapi?” “Naweza kukufuata kwako  mchana wa saa sita.” “Hapana. Tukutane  hapahapa. Tena muda huo ndio nitakuwa  nimemaliza na mimi shuguli zangu.” “Sawa  Fina. Usinidanganye tafadhali. Ujue nakata  tiketi ya watu wawili.” Kinny  akabembeleza. Siwezi kukupa ahadi ya  uongo.” “Basi nitafurahi nikikuona tena. Tunakaa siku ngapi?Akauliza Tunda  huku akitembea kutoka kwenye eneo  hilo la Mlimani city. Siku mbili, ya tatu  tunarudi. Nakutana na jamaa mmoja wa pale  bungeni, kisha tukifanikiwa, tunapumzika siku  moja, inayofuata tunarudi.” Sawa.Tunda  alitamani kuruka juu kwa furaha.  Hakutegemea kumpata Kinny kiurahisi hivyo.

  ~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~

     Alifika kwake ambako hakuna  mtu yeyote aliyejua anapoishi kwa wakati ule. Na  wakati wote alitaka mwisho wa  kusindikizwa iwe Mlimani City. Hata  alipokuwa  na  Sadiki.  Kama hawataachana hotelini, basi atajidai  kuna kitu anahitaji hapo Mlimani city.  Atamzungusha hapo madukani mpaka  Sadiki achoke. Basi hapo ndipo atapata  sababu yakumfukuza. Atamwambia arudi akapumzike kwa mkewe, yeye  atachukua taksii hapohapo baada  yakumaliza manunuzi yake. Basi,  atasubiri  kuhakikisha  Sadiki  ameondoka kabisa pale, ndipo na yeye  ataondoka kabisa pale Mlimani city,  tena kwa kutembea, mpaka nje ndipo  atachukua taksii yakumpeleka kwake. 

Alishushwa na taksii nje ya geti usiku huo,  akaingia na kusalimiana na mlinzi  aliyemkuta siku hiyo nyumbani kwake.  Kampuni hiyo ya ulinzi ilikuwa  ikibadilisha walinzi mara kwa mara ili  mlinzi mmoja asije kufanya njama za  kuiba kwa wateja wao. Akaingia ndani  akiwa amejawa furaha. Moja kwa  moja  kwenye  chumba  chake  chakuvalia, akaanza kujiandaa na  safari ya kwenda kumwingiza Kinny  kwenye mtego awe Sadiki.

Akaanza  kutafuta nguo zakuvaa kwa siku hizo  tatu ambazo watakuwa Dodoma.  Akaweka mbili zaidi kama akiba.  Kuanzia chupi mpaka nguo za kulalia,  alibeba  mitego mitupu. Akawa  anacheka mwenyewe huku akipanga  mahesabu yake. Akaweka na viatu vya  maana vinavyoendana na hizo nguo.  Aliporidhika, ndipo akaenda chumbani  kwake sasa. 

Akiwa chumbani kwake akijiandaa  kulala, akaanza kuwaza jinsi ya  kufanya na ile gia aliyoingilia kwa Kinny, yakumuuzia vinywaji. Tunda hakuwa na mtu yeyote  anayemfahamu ambaye anauza bia. Ule ulikuwa uongo kwa Kinny baada yakubadili  wazo la kuomba kazi pale kwenye  Club ya Kinny. Lakini hakuwa akijua  chochote juu ya bia. Alikuwa akiona tu  bia zikishushwa kwenye baa za Sadiki.  Hakuwa akiuliza wala kutaka kujua  zinapotoka na kwa bei gani! Sasa anamalizaje hilo bila kuharibu  mahusiano! Ndilo likawa swali usiku  huo. “Lazima kutumia akili ya ziada.” Tunda  akawaza  huku  akicheka  na  kujipongeza kuwa na akili ya haraka  yakufikiria.

~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~

  Asubuhi kabla ya safari ya Dodoma,  Tunda  aliamka  akabaki  amejilaza kitandani kwake.  Wazo likamjia, lililomfanya ajipongeze. Akacheka sana akiwa peke  yake. Akaanza kujiandaa sasa na safari  akiwa akili imetulia na anajua kitu chakufanya. Alijitengeneza vizuri  ndipo akatoka kurudi Mlimani city  ambapo walikubaliana na Kinny wakutane hapo. Kabla dereva hajamwingiza  ndani kabisa pale Mlimani City,  akamwambia amsogeze kituo cha  daladala, kisha amsubirie mbele  kidogo. Akafanya hivyo, Tunda akashuka. Vijana waliokuwa wamesimama pale  kituoni wote wakamgeukia. Wakabaki  wamekodoa macho wakimwangalia kadiri alipokuwa akiwasogelea taratibu. Hata  yeye  mwenyewe  Tunda  alijua  amependeza.

“Samahani.” Akamwambia mmoja  wao aliyeonekena amechangamka  kidogo.  Akamuomba  wasogee pembeni ili wazungumze. Kaitwa na  mrembo waliyekuwa wote  wamempokea kwa macho ya uchu  tokea anashushwa kwenye hiyo gari  safi ambayo ilikuwa kama yake kumbe  Uber! Kwa haraka akasogea kama  aliyewazidi wenzake bila swali.   “Nina kazi ndogo tu, nataka unisaidie  kaka yangu. Nitakulipa.”Akaanza  Tunda taratibu. Akatoa miwani yake  ya jua aliyokuwa ameivaa, akaishika  mkononi na kumtizama yule kijana.  Bila shida.Alikubali kwa haraka  sana.

Tunda  akajua ameshamchanganywa kwa muonekano na sauti yake, akajua atafanya chochote atakachomtuma, akamcheka  akilini  mwake.  Akamwambia kitu anachotaka afanye.  Akampa maneno ya kuzungumza  kwenye simu yake. Akamuuliza mara  mbili tatu kama ameelewa huku na  yeye akimuuliza maswali kutaka  uhakika kama ameelewa sawasawa ili  ajibu  kama  alivyomfundisha,  asiharibu. Darasa hilo liliendelea kwa  muda mfupi tu, kijana akaonekana  kuelewa kila alichofundishwa na  Tunda. Alipojiridhisha naye, ndipo  akampigia simu kijana anayehusika na  manunuzi ya vinywaji pale kwenye  club ya Kinny. 

Alipojitambulisha Tunda kuwa ndiye  Fina wa jana yake, yule mfanyakazi  wa Kinny akakumbuka kwa haraka,  kwani  alimwambia  siku  hiyo  angempigia. “Huyu ndio kiongozi wao.  Hebu zungumza naye ili mpange.” Tunda  akamkabidhi simu yule kijana na  kikaratasi cha maswali ya kumuuliza  yule  mfanyakazi  wa  Kinny.  Walishayapitia hayo maswali pamoja, yalikuwa mawili tu. Tunda alikuwa  ameshayaandaa  tokea  nyumbani  kwake. Juu ya bei na usafiri. Naye yule  kijana akachangamka vizuri sana.  Akaweka shoo ya nguvu hapo kwenye  simu akiuliza hayo maswali mawili tu,  lakini utafikiri ni kweli anao huo  mzigo. Kijana wa Kinny mwenyewe  akashindwa biashara.  Kijana wa Tunda alimwambia kwanza  siku wanazotaka wao mzigo upelekwe kwenye hiyo club yao sio siku  zao za kuuza. Wanakuwa busy  kiwandani.

Pili, kuwapelekea vinywaji  kule kwenye club yao sio bure,  akamtajia bei ya usafiri. “Mbona sisi  tunaletewa mpaka hapa bure kabisa?”Sasa hayo si ni magari ya kiwandani Tajiri yangu? Hii biashara ya binafsi, kaka.” Yule kijana  akajibu na kumfurahisha zaidi Tunda.  Akamalizia kwa kumpa bei ya bia  zenyewe sasa. Ilikuwa chini kidogo na  ile bei ya yule kijana wa Kinny  aliyomtajia Tunda jana wakiwa baa. 

Yule  mfanyakazi  wa  Kinny  akashindwa. Naona kama haitatulipa sana.  Itaongeza tu usumbufu.” Tunda akachukua  yeye simu sasa. Na yeye akaongeza  njia ngumu. Au labda mzifuate wenyewe? Tatizo usafiri dada yangu. Hata hivyo bei  waliyotupa haina tofauti kubwa sana na ya hawa wanayotuletea hapa. Kitakachoongezeka  ni usumbufu tu kwetu.” Ni kweli.  Umefikiria vizuri sana. Nitamwambia Kinny  jinsi ulivyo na akili nzuri ya kufikiria. Akacheka kwa heshima, na  kuagana na Tunda

“Mungu anipe nini mimi!” Tunda  akajipongeza baada yakuona mipango  yake imekaa na kwenda sawa. Hakuna  wakumkamata. Akamlipa yule kijana  aliyekutana naye palepale kwenye  kituo nje ya Mlimani city, akamsaidia  kuzungumza na kijana wa Kinny,  aliporidhika malipo, Tunda akarudi  kwenye ile gari, ili imuingize sasa  ndani kumsubiria Kinny. Lengo lake  likawa limetimia. Akacheka nafsini  kwake. Akajipongeza kwa utapeli wake.  “Nani wa kunikamata? Kijana  hanijui, simu kutumia yangu, namba  yakupiga baadaye akanushe niliyomfundisha ayaseme pia hana.  Na jina la aliyezungumza naye  pia hana! Mjini  Shule.” Tunda akazidi kucheka nafsi  kwake akijipongeza. 

~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~

Alingia ndani kabisa Mlimani City,  akatafuta mgahawa mzuri, akakaa  hapo. Hakuwa amepata kifungua  kinywa. Njaa ilishaanza kumsumba. Na  kwa kuwa alikuwa hali chakula usiku  ili asinenepe zaidi, mara nyingi  asubuhi ilikuwa lazima ale vizuri. Saa 11  jioni, ilikuwa mwisho wakuingiza  kitu kizito tumboni kwake. Muhudumu  akamletea kila kitu alichoagiza,  akashukuru nakuanza kula taratibu bila  haraka.  Saa sita kasoro, akaona simu ya Kinny  inaingia. Akacheka na kupokea. “Nimefika Fina.” Tulikubaliana saa sita  kamili.”“Basi hamna tatizo. Nitasubiri  mama. Utanikuta upande huu wa kuingilia.” Akamwelekeza  alipoegesha  gari yake.  Tunda akaelewa. Sawa. Saa sita kamili  nitakuwa nimefika hapo. Sitakuweka.” “Nitashukuru.” Akajua  wazi  ameshamkamata. Akacheka nafsini  mwake, akaendelea kula taratibu bila  haraka. 

Alimsubirisha kwa robo saa ndipo  akatoka. Akamgongea kioo. Alikuwa  ameinamia simu yake. Akatoka kwa  haraka akabaki ameduaa. Tunda akacheka kama kumtoa kwenye ule mshangao. “Daah! Hakika Fina  wewe ni mzuri! Upo nadhifu!” Asante Kinny. Na wewe  Umependeza.”  Akawa muugwana akapokea sifa na kumsifu na yeye. Wakaangaliana na kucheka. Mbona mimi nimekubali  kushindwa!Tunda akazidi kucheka,  akakumbuka hali ya Kinny jana  kwenye gari. Kinny akazunguka  kwenda kumfungulia mlango na  kumpokea mzigo. Akawa anamtizama  wakati anaingia garini.

Hakika Tunda alipendeza na kuwaka  kwenye hilo jua la saa sita. Alivaa  suruali nyeupe, kiatu kirefu cha rangi  ya kijani ambayo inaendana na aina ya  blauzi aliyokuwa amevaa yenye mistari  ya kijani kwa mbali kama vile viatu.  Alishika pochi mbili. Moja kubwa,  nzuri sana kwa kuitizama kwa macho. Ndio iliyokuwa imebeba nguo zake za ziada na vitu vyakutumia safarini na pochi  ndogo ya rangi ya dhahabu isiyong’aa  sana.  Vyote vilionekana vizuri na vya  thamani. Ile suruali kule chini aliikunja  pindo mbili, alikuwa amevaa cheni  nzito ya dhahabu kwenye mguu  mmoja. Sikioni pia alivaa hereni  zakuning’inia kama cheni aliyovaa  mkononi. Nywele alikuwa ameshonea  wiving ya rangi ya gold kidogo  iliyochanganywa na nyeusi. Fupi,  iliyokatwa kote pembeni kasoro katikati. Akaweka miwani ya jua.  Usingechoka kumtizama, na hata kama  unampango  wakumuhonga,  usingethubutu kumpa pesa chache. 

Kinny akatoa gari pale Mlimani city,  kuelekea uwanja wa ndege. “Sasa nani  atakuja kuchukua gari yako?” Huwa  nikiwa nasafiri siku chache hivi, huwa  naliacha tu palepale uwanjani. Naona  inanipunguzia usumbufu. Wengine hatuna madereva. Tunajiendesha  wenyewe.” “Kwa nini usimuombe  mkeo akulete?” Kinny akacheka  kidogo. Mke wangu na watoto  hawaishi hapa nchini. Wapo ughaibuni  huko. Huku tunatafuta tu pesa.” “Safi  sana.Tunda alijibu hivyo tu kwa  ufupi, hakutaka kuendeleza yale  mazungumzo. 

Akazungumzia maswala ya vinywaji,  na ugumu aliokutana nao yule  mfanyakazi wake. “Anaonekana ni  kijana mwenye upeo mzuri wa  kufikiria.” Ndio maana huwa  nampenda na kumuamini na maamuzi  fulani fulani. Anajua kupima mambo.  Maana  ingekuwa  mwingine,  angehadaika na bei, akasahau garama  ya usafiri.”Kinny akaingia kwenye  mstari wa Tunda, hilo akalifurahia  kuwa wamerekebisha hapo, amepona.  Wakazungumza mambo ya kawaida tu,  mpaka wakaondoka jijini Dar kuelekea  Dodoma. 

 

Tunda & Kinny jijini Dodoma.

 “Twende hotelini kwanza, tuvute muda  mpaka saa mbili ndio nakutana na  jamaa.” Kinny alimwambia Tunda  mara walipotua uwanja wa ndege wa jijini Dodoma. Bado ilikuwa mapema tu.  Kijana mwenyewe mdogo tu, lakini  amepewa majukumu yanayomfanya  anaringa kama mtoto wa kike!  Nambembeleza karibia nimlambe!” Tunda akacheka.  Kwani unataka nini?” “Yeye ndiye  anahusika na bajeti ya wa bunge  wakiwepo bungeni. Wanataka  kuanzisha chakula cha mchana kwa  wabunge wote kipindi cha bunge  kikianza mpaka mwisho. Wametangaza  hiyo tenda. Sasa yeye ndiye muhusika  mkuu. Nilitaka nimuombe mimi hiyo  kazi  yakulisha  wabunge.  Na  kutengeneza mazingira mazuri hata ya  kuwafanya wawe wote wanapata  kifungua kinywa hapohapo bungeni  muda wote wa bunge linapokuwa  likiendelea. Sasa upatikanaji wake  ndio shida.” Kinny akaendelea kama anayelalamika.

“Sasa ananizungusha, nakaribia  kuchanganyikiwa. Ni hivyo tu wife  naye anasisitiza. Anaona ikienda  vizuri, tukafanikiwa hiyo kazi, anataka  arudi nchini, aifanye yeye mwenyewe  hiyo kazi ya kuwalisha hao  waheshimiwa.” Pole. Pengine safari  hii atakubali.Akaguna Kinny kama asiyesadiki. Pengine na wewe unamuendea  kibabe ndio maana anakuwekea  ngumu.” “Nilitakiwa nifanyaje? “Kuwa kama mtu mwenye shida,  unayemuomba.” Tuna akatoa wazo. Daah! Mimi nahisi  nimefanya kila njia.

Kwa mazungumzo  yake na Kinny kuanzia wanatoka Dar ampaka hapo, Tunda kwa haraka sana alishajua hawezi  kumfanya kuwa Sadiki mwingine.  Wakati  wote  Kinny  amekuwa  akizungumzia familia yake. Mkewe ni  kama ndiye anayeongoza mambo  mengi ya familia hasa pesa. Swali  likawa atanufaikaje naye? Hilo ndio  likawa swali alilokuwa akiliwaza  Tunda tokea yupo kwenye ndege,  Kinny akiongelea mambo yake na  familia yake. 

Wazo likamjia wakiwa kwenye taksii  hiyo ikiwapeleka hotelini. Uzuri Tunda  alikuwa  mkimya.  Ikamsaidia kufikiria vizuri, wakati  Kinny akiendelea kuzungumzia mambo yake na kulalamika, yeye anafikiria.  Akamgeukia Kinny. “Nikikupatia mimi  hiyo kazi, utanilipa kiasi gani?” Kinny akabaki kama ameduaa kidogo.  “Nakuuliza Kinny? Tuna siku ya leo,  kesho na kesho kutwa. Kama  unauhakika umetumia njia zote. Sasa  hivi ongeza uthamani wako.” Kwa  kufanyaje!?Kinny akakaa sawa  wakati anauliza ili kumsikiliza Tunda  aliyekuwa ametulia wakati wote.

Mtu  ambaye sio mzungumzaji, akitaka  kuongea, lazima utataka kumsikiliza  tu.  “Mpigie simu leo, mwambie una mtu  muhimu sana unamiahadi naye leo  jijini. Huwezi kuahirisha kwa kuwa  yupo kwenye zihara hapa nchini na  anaondoka kesho asubuhi sana. Usitoe  maelezo mengi sana. Lakini mwambie  umemtuma leo meneja masoko wako  huku Dodoma ili kukuwakilisha  kwenye miahadi yenu. Mwambie  tunaweza kukutana saa mbili kamili  usiku. Ila kama bado atakuhitaji wewe  mwenyewe, basi mwambie utawahi  ndege ya kwanza inayokuja huku  Dodoma kesho ili mpate hata dakika chache   za mazungumzo. Hivyo tu.  Usiongeze neno wala kupunguza.  Halafu uone kama sijakupatia mimi  hiyo kazi. Labda iwe haipo.” Kinny  akastaajabu sana. 

Yaani mpaka tu hapa, mimi  mwenyewe umeshanifanya nikukubalie  kwenda kukutana naye.Tunda  akacheka. Na walikuwa wamefika  hotelini. Mama umejaliwa lugha ya  ushawishi! Halafu mwenyewe taratibu,  mpaka unamaliza, mtu anataka aseme  ndiyo tu!” Tunda alizidi kucheka huku  wakiingia ndani. Lakini wewe  unaonaje wazo langu?” “Nakwambia  mimi  mwenyewe  ushanishawishi! Kabla yeye hajasema “ndiyo’, mimi  nishasema ndiyo!” Tunda akacheka.  Lakini nakupa siku ya leo tu, kesho  naenda kupambana naye mwenyewe.  Asiniletee mchezo. Sina ninaloongea  na mke wangu ila hili tu!” “Sawa.  Lakini nikikufanikishia, usinisahau . Siwezi.  Nakuhakikishia  kama  ukinipatia hiyo tenda, nakupa pesa  bila maswali Fina. Ni kazi ya pesa  nyingi, ati! Kwanza hata mke wangu  ataniona wa maana.” Tunda akacheka  kidogo na kunyamaza. 

Walipofika ndani, Tunda alikaa  kwenye makochi akamuacha Kinny  aende yeye mwenyewe mapokezi.  Kinny akajiandikisha, akapewa funguo  za chumba. Akarudi kumchukua  Tunda ndipo wakaelekea chumbani.  Walifika hapo hotelini ilishakuwa   jioni. “Njaa inakuuma?” Tunda akamuuliza.  “Nilivyo na hamu uniguse na hiyo  mikono yako laini, chakula kitasubiri  tu.” Tunda alicheka sana. Hutaki  kuoga kwanza?”“Acha bwana Fina! Sasa tumechafuka wapi wakati  tumetoka kwenye ndege na kuja  hapa?“Mimi nilikuonya mtindo wa  kukariri Kinny. Unapitwa na mengi!” Halafu ukisemaga hivyo inakuwa  kweli!Tunda akaanza kucheka.

 Naomba tuanzie hapa kidogo, halafu  ndio tukaoge. Mwenzio hali mbaya.  Nikikuangalia hivyo! Natamani tu  unitulize kwanza. Nina siku...” Tunda  akamziba mdomo taratibu kwa vidole  vyake viwili. Shhhhh!Taratibu  Tunda akamtaka anyamaze. Hutaki  kelele eeh?Kinny akauliza kwa sauti  ya chini ya kunongona. Tunda akacheka huku akitingisha kichwa  kukubali.  Akamsukuma kitandani taratibu.  Akamuwekea mto chini ya kichwa,  kuwa ajiegemeze. Yaani alale chali.  Alipolala akiwa anamtizama, Tunda  akaanza kuvua nguo zake mbele yake  taratibu bila haraka huku akimwangalia na tabasamu usoni. 

“Sasa na mimi si ni vue?” Kinny akauliza huku akibabaika. Shhhh! Tunda akamnyamazisha tena.  Alianza kwa kutoa ile shati ya juu.  Akabakiwa na sidiria juu. Akachomoa  ule mkanda kiunoni akaurushia  kwenye kochi. Akaanza kushusha ile  suruali na tabasamu usoni. Kinny  akavuta pumzi kwa nguvu huku  akitazama  kwa  makini.  Chupi  iliyokuwa imebaki hapo, ikamfanya  Kinny ajiweke sawa, amtizame zaidi.  Juu ya ile chupi kulikuwa na cheni ya  dhahabu iliyowaka zaidi sababu ya  kiuno cheusi cha Tunda. Kinny  akalamba midomo.  Tunda akacheka taratibu.

Akaanza  kushusha ile suruali akiwa bado  hajatoa viatu. “Nikusaidie?” Kinny  akauliza. Tunda akatingisha kichwa  kukataa huku akicheka. Akageuka,  akainama ili kuvua viatu. “Oooh my!” Kinny alisikika taratibu. Tunda  akacheka taratibu. Akatoa viatu,  akatoa na ile suruali. Akarudisha viatu  vyake miguuni taratibu na ile cheni ya  mguu ikabakia palepale. Akaokota ile  suruali. Akaikunguta kidogo kama  anayeitengeneza.  Akaikunja  na  kwenda kuiweka kwenye kochi  lililokuwa na pochi yake, huku akiwa  na chupi tu, na viatu vilivyokuwa  vimemkaa vizuri mguuni. Virefu,  mchongoko mbele.  Kinny alibaki  akiangalia huku akivuta pumzi.

Bado  alikuwa na nguo zake vilevile  akisubiri kuona kitu Tunda atamfanyia.  Tunda  akafungua  pochi  yake,  akachukua kitu ndani ya hiyo pochi,  akarudi na kupanda kitandani vile vile.  “Fina!” Akamwita  taratibu.  Ungeacha nikuvue mimi hiyo chupi.” Kinny aliongea taratibu kwa sauti ya  chini akionekana wazi ameshalemewa.  Tunda akacheka tu, na kumkalia  mapajani. Akanyanyua mkono wa  Kinny na kumshikisha kiunoni kwenye  kiungio cha chupi kama anayemfanya  ailegeze. Kinny akaelewa kwa haraka,  akavuta kwa makini. Chupi yenyewe  ilionekana nzuri yakuvutia, hakutaka  kuharibu. Kimkanda cha pembeni  kikaachia. Tunda akatoa taratibu  huku  akimwangalia.  Alijinyanyua kidogo kumpisha aitoe  kabisa, kisha akaanza kumfanyia fujo  hapo kitandani na nguo zake vile vile,  hakumtoa. 

Tunda alikuwa yupo kazini, anajua  analolifanya  kwa  hatua.  Hakujichanganya na hakujisahau.  Alijua yupo pale ili atumiwe mwili  wake. Na yeye akakusudia kufanya  kazi yake vizuri huku akijikinga.  Alimchanganya Kinny mtoto wa jiji la  maraha Dar, akabakia akiweweseka na  nguo zake, nusu suruali. “Daah!  Tumekubaliana tukae siku ngapi  tena?” Tunda  akacheka  huku  akinyanyuka pale alipokua amemkalia.  Akatoa viatu vyake taratibu bila  haraka, akaelekea bafuni akiwa na ile  cheni ya kiunoni na ya mguuni.

Kinny  akabaki akijipapasa shingoni, sikioni  kule Tunda alikokuwa akipitisha ulimi wake. Mwili ukazidi kumsisimka.  “Sasa, sasa hivi si naruhusiwa kutoa  nguo?”Akauliza Kinny kwa  tahadhari. Huwezi kuoga na nguo. Tunda akajibu akiingia bafuni. Kama  anayekimbizwa, akatoa nguo haraka  huku akizitupa kila mahali akakimbilia  bafuni kumfuata Tunda. Huko nako  Tunda  akamfanyia  vihoja  vya  makusudi. “Kwani Fina wewe huna  mifupa mama!?” Tunda akacheka  sana. Utanifanya nishindwe kazi  bwana! Na bora ningekubali lile wazo  lako la kwanza, la kuanza kuoga. Nilikwambia uache kukariri.Tunda  akamjibu taratibu huku akiendelea  kuoga.

“Kuanzia sasa hivi nitakuwa  mtoto mzuri. Nafuata ushauri.” Tunda  akamwangalia huku akioga. Akamvuta karibu yake, Tunda akampa mgongo  baada yakumuona anataka kumbusu  midomoni.  Akajua  amenogewa.  Akamkumbatia akiwa amesimama  nyuma yake. Akabaki ametulia  mgongoni mwake, amekumbatia kiuno  kilichobeba ile cheni. Aliizungusha  mara kadhaa, akahisi amepotelea  mawazoni. Tunda akatulia tu huku  maji yakiendelea kuwamwagikia.  Walitoka  hapo,  Kinny  akiwa  ameshachanganywa na Tunda, hakuna  aliloambiwa akakataa au kupinga. 

Akampigia simu huyo mtu  ambaye Tunda alitaka akakutane naye  yeye badala yake. Akakubali hiyo saa  mbili kamili wakutane na huyo meneja  masoko wake Kinny. Hapo hapo  Tunda akachukua namba yake ya  simu. “Anaitwa nani?” Tunda  akauliza wakati anaingiza namba yake  ya simu kwenye simu yake.  “Mbawala.” Kinny akajibu. Tunda  akaandika kwenye simu yake.  Akamuona Kinny anasinzia. Lala. “Kweli? Sio ulitaka tukae wote mpaka  uondoke? Maana muda umeisha.” “Usijali. Lala tu. Nitakuletea na  chakula.” “Hapo utakuwa umenisaidia. Asante.Hapo hapo  akafunga macho na kulala. 

Tunda kwa Mbawala.

Tunda alifurahi sana kuua ndege wa  wiwili kwa jiwe moja. Tumaini  lakumfanya Kinny kama Sadiki,  lilishaisha. Hakuacha kumtaja mkewe  katika  kila  jambo.  “Huyu  tutasumbuana naye huyu. Naona  ameshikwa masikio na mkewe. Hana  analolifikiria au kulifanya bila mke  wake! Club yenyewe ya Dar,  ameongezewa mtaji na mkewe. Wote  tunalia shida! Hapana.” Tunda  alishawaza hilo. Kumpata Mbawala  ikawa faraja. Akakusudia huko  akafanye mawili kwa mpigo. Akajawa  hamasa ya namna yake. Akaamua  apendeze haswa. Kuuza kazi ya Kinny  ili aje amlipe, na kumnasa Mbawala. 

Akavaa kigauni cha hawaida tu. Lakini  kifupi na kilichanua chini. Rangi mbili,  Gold/dhahabu isiyowaka ndiyo ilikuwa  juu ambako ilikuwa kama  shumizi, yaani vimikanda na  katikati ya kiuno mistari  niwili iliyomkaba haswa kiuno. Mistari  ya hiyo rangi ya hiyo dhahabu ya juu  na nyeusi. Chini ya kiuno pale kwenye  kile kiungio cha dhahabu na nyeusi,  kuliunganishwa  muundo  wa  mwamvuli, nyeusi tupu iliyojimwaga  haswa mpaka juu yamagoti kidogo.  Kiatu kirefu chakufunika, mchongoko  kilichokuwa kimemkaa vizuri na  kimeendana na pochi ndogo aliyokuwa  ameshika mkononi ya dhahabu.  Kwa hiyo kiatu, pochi na ile gauni kwa  juu, vyote viliendana. Alivaa hereni  zile za mnyororo ndefu mpaka  mabegani na cheni ya mkononi na mguu mmoja. Basi. Tunda akacheka  alipojitizama  kwenye  kioo.  Akajipulizia pafyumu tulivu. Hakuwa  akijipaka rangi usoni mwake sababu ya  rangi yake ya mwili.

Wakati wote  nyusi alizilaza tu na kuweka wanja  kidogo, pengine usingetambua, na  mafuta ya mdomo ya rangi ya  wekundu kwa mbali kama pinki.  Akajizungusha tena kwenye kioo mara  kadhaa, akiweka kichwa kulia na  kushoto. Akacheka. Akatoka taratibu  kama asiyetaka kumuamsha Kinny. 

Akiwa  njiani  akampigia  simu  Mbawala. Ikaita mara tatu ikakatwa.  Akatuma ujumbe. ‘Naitwa Fina,  tunamiahadi ya saa mbili kamili. Nipo njiani.  Sitaki kukupotezea muda wako, nitafika kwa  wakati.’ Akautuma huo ujumbe. ‘Nipo hapa tokea dakika  10 zilizopita.’ Ujumbe  huo ukarudi. Tunda akajua anakwenda kukutana na kiburi. Akacheka,  ‘Hakuna mwanaume jeuri mbele ya  mwanamke’.  Akajiaminisha Tunda.  Hakumjibu. 

Walishafika kwenye huo mgahawa  waliokuwa wamekubaliana. Ile  sehemu tu yenyewe, akajua Kinny anamuheshimu Mbawala kwa kukutana  naye sehemu kama ile. Tunda  akakusudia kufanya ‘entrance’ ya  nguvu. Kuwa kila mtu amwangalie  kuanzia juu mpaka chini wakati  anaingia pale. Atafanya nini! Akaanza  kuwaza wakati anashuka kwenye  taksii. Akatoa simu yake mlio kabisa.  Akaweka ‘silence’. Mgahawa ulikuwa  mtulivu.

Akaanza kuongea kama  anayezungumza na mtu kwenye simu  wakati anakaribia mlangoni kwa sauti  yake tulivu isiyo ya fujo ila yakusikika  kiasi. “No. I hope it wont take long.” Tunda alisikika akizungumza na mtu  kwenye simu akimwakikishia kuwa hiko kikao anachokwenda kufanya, hakitachukua muda mrefu huku akiingia taratibu  kwa sauti yake tulivu. Noo! Akacheka Tunda taratibu, simu sikioni. I promise. Bye for now. Tunda akaahidi huko kwenye simu kisha akabonyeza simu yake kama aliyekata.  Akawa amesimama katikati ya ule  mgahawa.

“Sorry!” Akajifanya muungwana, akaomba msamaha wa usumbufu, kinyenyekevu kwa watu aliowakuta pale ndani ya ule mgahawa waliokuwa wametulia yeye akizungumza na simu wakati akiingia. Akawa  kama amekumbuka kitu, akarudi  nyuma mpaka pale alipompita mtu  wakupokea wateja.  Naitwa Fina, nina miahadi na  Mbawala.”Akanongona. Akaona mtu  anamfuata kwa haraka. Ni mimi. Wote yeye na muhudumu wakageuka. “Ni  mimi  ndiye  Mbawala.”  Akajitambulisha kwa haraka kama aliyekwisha kubabaika tayari.

 Hapakuwa na watu  wengi humo ndani na Tunda  alishamuhisi kwani alikuwa amekaa  peke yake kwenye meza, ila tu, alitaka  ageuke wamuone na nyuma.  Kwa jinsi alivyokuwa amependeza,  hakutaka kufika na kukaa tu. Alitaka  kila mtu amuone. Alivyomtulivu  usoni, usingejua hila ya Tunda  kichwani mwake. Hakika alikuwa  amependeza. Kuanzia kichwa mpaka  unyayo  yupo  safi.  Kingereza chenyewe alichokuwa akikiongea kwa pozi kwenye simu kilikuwa kimetulia, hakusikika kuunga maneno kwa shida. Kigauni kile  kilifika sehemu ambazo ungependa  kuangalia zaidi. Mguu mweusi, laini  kwa kuutazama kwa macho, mrefu,  ulionyooka, umetulia kwenye kiatu  hicho cha juu kizuri. Akaning’iniza  cheni nene. Mtaratibu usoni, na tabasamu lenye kuonyesha meno  machache meupe pee na macho hayo,  hakika utatamani asikae. Huwezi  kulaumu usumbufu aliosababisha  wakati anaingia. Utachukia akikaa tena  akafichwa na mtu mbele yake. 

Naitwa “Fina.” Tunda  akamsogelea  Mbawala na kujitambulisha taratibu huku akimpa  mkono ulionyoka tena uliokaza si mlegevu. Kuashiria yupo  kikazi. Mbawala akaupokea mkono  huku amekodoa macho usoni. Naitwa  Mbawala.” Nimefurahi kukufahamu.  Nashukuru kwa muda wako. Nakuahidi  sitakuchukulia muda wako mwingi. Karibu mezani. Nilikuwa nimekaa  pale.Akanyoosha mkono huku  akitangulia kuonyesha njia. Tunda  akamfuata.

Karibu.Tunda akakaa  alipoonyeshwa, mbele yake. “Acha tuagize hata vinywaji.” Tunda  akamtizama kama  anayemshangaa  kidogo. Kama huna haraka lakini. Akajihami. “Niliambiwa wewe ni mtu unayethamini sana muda wako. Akacheka kwa kujisuta kidogo. “Sio  hata weekend bwana! Leo siku ya  mapumziko. Naomba tuzungumze  wakati tunakula. Sijala siku nzima.  Naona hata macho yanaanza kuona  yasiyokuwepo.” Tunda akatulia tu akimsikiliza.  Unakunywa nini?” “Maji tafadhali. Mbawala akamshangaa kidogo. Maji  tu!?” Maji yananitosha. Asante. Tunda  akajibu  na  tabasamu.  Muhudumu akaja, Mbawala akasisitiza  kuwa lazima wote wale. Akamuagizia  na  yeye  Tunda,  muhudumu  akaondoka.

“Unaishi hapahapa Dodoma?”  Mbawala akaanzisha mazungumzo. “Hapana. Nimekuja huku kwa ajili yako. Wewe mtu mkubwa  sana, bwana! Naona kukupata  inakuwa garama kweli!” Mbawala  akacheka sana. Wanao kwambia hayo,  wanakuwa wananitafuta mida mibaya.  Ila mimi napatikanika sana tu.” “Basi  afadhali  nimekupata  siku  ya  mapumziko. Naamini na mimi utanipa  sikio lako.Wakacheka kidogo.  Naona safari za Dar zitaanza kuwa  nyingi.Tunda akacheka kwa utulivu na kuuliza. “Kwani zilikuwa chache? Na fujo zile,  najitahidi sana kuzipunguza.” Kama  mahitaji yote ukiyapata Dodoma, huna  haja ya kufuata kelele za Dar. Huku ni  patulivu.” “Ndio tatizo hilo. Patulivu, lakini bado sijapata vitu nadhifu.” Tunda akacheka na kuinama kidogo.

“Ndio tatizo pekee kwangu kwenye huu mji mkuu.” Fungua milango  tukusogezee huduma huku.  Mkikaribisha wawekezaji, mtapata  huduma zote. Tatizo lenu mnabania. Mbawala akacheka sana. Inategemea  na mwekezaji. Wengine viburi, hawana  lugha ya biashara.” Naelewa. Pole. Ndio majukumu hayo.” “Ukubwa  unakuja na majukumu, sio? “Unakuwa jalala haswa!Mbawala akaafiki. Naomba Mungu  na mimi nipate nafasi kabla hilo jalala  halijajaa na kufukiwa.” Usijali.  Tutatengeneza mazingira mazuri ili na wewe upate nafasi yako.Tunda  akacheka taratibu huku akimtizama.  Alishamuona amelainika. 

Chakula kikaletwa, Tunda akakila kwa  kukidonoa donoa akiwa anatumia kisu  na uma. Huyo kuku akamgeuza kulia  na kushoto na uma wake huku  akimsikiliza Mbawala akijigamba kwa  hili na lile. Aliweka mdomoni vipande vidogo sana vya nyama, na kutafuna  taratibu tena kwa muda mrefu.  Mbawala alimaliza chakula chake,  Tunda hakuwa hata amefika robo. Akaweka kisu na uma chini.  “Ndio tayari hivyo!?” Inatosha.  Imeshakuwa usiku. Sipendi kulala na  vyakula vingi tumboni.”“Ndio maana  una mwili mzuri Fina.Tunda  akacheka taratibu na kushukuru kwa sifa huku akisogeza ile sahani  pembeni. Asante. 

“Sasa maswala ya kikazi yakiisha, ndio basi tena?” Tunda akatabasamu. “Inategemea tunaachana vipi.” Tunda  akamjibu na macho yaliyomfanya Mbawala atulie kidogo. Naomba  nikukaribishe kwangu.” Safari hii  nipo kikazi. Safari za matembezi hizo tuzipange baada ya leo.” “Fina  unamasharti?” “Hataa. Kawaida tu. Hatuwezi  kuchanganya mambo Mbawala! Hili hatujamaliza, tunarukia  mengine!?” “Nimekukaribisha tu  kwangu.” Nimekusikia. Nikifika  halafu  nikagoma  kuondoka? Mbawala akacheka sana.

Hiyo  itakuwa rehema.Tunda akacheka  kidogo.  Naomba nikuache. Nina miahadi  mingine kabla ya saa tatu na nusu  usiku huu.” “Nahisi kama mimi muda  wangu umepunjwa!” Ni kutokana na  nilivyoambiwa juu yako. Kuwa huwa  hupendi kupotezewa muda, nikaweka miahadi ya haraka. Tena nikiwa najua  wala hutataka kunisikiliza.” Hapana  bwana! Wamekutisha tu. Sasa itabidi  mniandalie menu yenu. Mniambie  mtaweza kuwalisha nini. Nijue bei zenu. Kisha tujue kuanzia hapo.” Naomba nikuombe kitu Mbawala. Najua ni nje ya kazi. Ila naomba  msaada wako.” “Nini tena? Mbawala akauliza. 

Najua sasa hivi umechoka. Naomba  nipe muda mfupi kesho. Nikufuate  popote, ili tuiandae hiyo menu pamoja  ambayo unafikiria wangependa. Na  bei  ambayo Mbawala ataikubali.” Mbawala akacheka sana. “Fina unaniibia bwana!” “Nisaidie  tafadhali. Angalau nipate tu mwanga.  Lakini kama unaona ni kuvuka  mipaka, basi. Tusichanganye mambo.” Tunda akatingisha kibiriti.  “Hapana. Hata kidogo. Hamna shida.  Kwani unafikiri itachukua muda  mrefu!” Ehe!” “Sio kitu kirefu hata  kidogo. Hata mimi mwenyewe naweza  nikaandika na kukutumia.” “Kweli  Mbawala!? Sitaki nikuchoshe kwa  kukuongezea jukumu zito.Tunda  aliongea kwa kubembeleza kama  anayemuhurumia tena.

“Hata kidogo.  Ni nafasi nzuri, ningependa na nyinyi  mnufaike.  Tena  ikikaa  vizuri,  tutaipitisha  kwa  haraka  tu.” Nakushukuru sana Mbawala. Hata  sijui nikulipe nini?” “Niahidi kurudi  huku kunitembelea.Tunda akacheka  sana.  Au  ombi  zito?” Hapana.  Linawezekana  kabisa.  Umekuwa  msaada mkubwa kwangu. Naomba  tupange, naweza kukukaribisha Dar, au mimi nikarudi kukutembelea. Lakini  naomba  niwe  nimekukamilishia jukumu ulilonipa kwanza.” Tunda  akamuwekea ngumu kiustarabu. Kwamba ni mpaka amkamilishie haja yake. “Hilo  mbona ni kama limesha kwisha Fina!  Nakutengenezea  kila  kitu,  na  kukuwekea mpaka bei. Kitakachobakia  ni kuweka tu kwenye karatasi yenye  logo yenu na muhuri, basi. Na kama  mtabadilisha, iwe kidogo.” Basi  itabidi kuja kusherehekea hukuhuku. Naomba na mimi niwepo kwenye hiyo  sherehe.Tunda akacheka tena.  Wewe ndio muhusika mkubwa.  Utakosaje tena?” “Basi acha nikaanze  kazi. Naamini weekend ijayo utakuwa  mgeni wangu.” Wema hauozi. Akisisitiza, afanye upande wake,  atapewa tu penzi. Wakacheka na kuagana Tunda akiwa amempa mawasiliano ya barua pepe ya Kinny. Kwamba akimaliza atume  huko.

~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~

 Alimwambia dereva taksii ampitishe  sehemu yenye nyama choma nzuri,  akanunua na kurudi nayo hotelini.  Kinny bado alikuwa amelala. Tunda  akamuamsha. “Kula kwanza ndio urudi kulala.” Nilikuwa na uchovu na ukame wa muda mrefu!Tunda  akacheka. Kweli. Sijapata muda  kama huu kwa muda mrefu. Kwanza  nilitoa akili kabisa kwenye mapenzi.  Nilikuwa nakimbizana na biashara,  bila kupumzika huku wife naye akipiga  kelele kila siku!” Pole. Kaa ule  kwanza halafu nikupe habari njema. Kinny akakaa kwa haraka.

“Haiwezekani! Usiniambie yule mpuuzi  amekukubalia!” Hajaishia hapo. Na  amesema..Tunda akamuelezea kila  kitu kinachomuhusu yeye kasoro kuja  kukutana wao wawili tena. Mpuuzi  sana yule. Au una kimzizi wewe Fina! Tunda alicheka sana. “Ungejua jinsi nilivyosumbuka naye  huyu  mjinga,  usingeamini.  Nimeshafanya safari kama hizi zaidi  ya mara mbili! Nakuja, ananiambia  hataweza kuniona, yupo busy.  Nikimpigia simu, ananijibu kwa ujumbe kuwa atanitafuta. Ujue hapo ni  mpaka nimtafute tena na anaweza  asipokee au akapokea na kuniambia  tuonane siku ambayo ukifika hapa  anakwambia amepata safari ya kikazi  yupo nje ya Dodoma.” Tunda akazidi  kucheka. 

“Kweli Fina. Nimefurahi sana.” Sasa  sio ufurahi, unisahau!” “Sithubutu.  Umeniokoa na kelele za mke  wangu kuliko nitakavyokwambia!  Tukikamilisha  tu,  nakulipa, na yeye nampigia. Nahisi  atakusanya watoto kesho yake arudi.  Kashachoka kuishi huko.Tunda  akanyamaza, hakuchangia.  Hapo  Kinny akajishtukia kidogo. Akajirudi. 

~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~

          Kesho yake asubuhi, Kinny  alipoangalia barua pepe ambayo Tunda alimpa  Mbawala atume hapo,  akakuta ameshatuma. Akamuamsha  Tunda akiwa haamini. “Huyu mjinga  ametuma bwana! Ona.” Tunda akakaa huku akivuta shuka asibakie mtupu.  Umemchanganya mpaka ameweka na  bei mbili mbili, kama jinga!  Ameandika hapa, isizidi hii ya pili.  Angalau iwe katikati. Bwana kaka huyu umemchanganya Fina! Naona  hata ukimuomba gari yake, huyu  atakupa tu.” Wakacheka.

Kinny akairekebisha haraka huku Tunda  akiwa amejilaza tu hapo kitandani  akihesabu pesa atakayomchomoa  Kinny.  Inabidi uende mapokezi ukaiprinti  umpelekee.” “Mimi tena! Hapana  Fina. Naweza nikaharibu mama.  Tafadhali mrudishie wewe mwenyewe.  Asije akaona hii sura yangu,  akagairi.” Tunda akacheka. Basi  kaiprinti  halafu  mimi  nitampelekea. Kinny akambusu nakutoka hapo akikimbia. 

Bahati yake mbaya, nzuri kwa Tunda  akasahau simu yake. Tunda akakaa  kwa haraka akaingia moja kwa moja kwenye phonebook yake ili kuiba namba  za simu za watu. Alijua mtu kama  Kinny, mtoto wa jiji, ameishi nje ya  nchi, lazima anao watu wenye pesa.  Akaanza kuperuzi taratibu akisoma  majina ya watu kwa makini. Yale ya  watu wakubwa aliyoyasikia mtaani,  alichukua namba zao. Moja kwa moja  akawa anahamishia kwenye simu yake.  Aliporidhika, akaweka simu ya Kinny  pembeni na kumpigia simu Mbawala. 

“Naomba nikushukuru kwa kuwa  mwaminifu, Mbawala. Asante.” Hiyo sauti  tu yenyewe, akafurahia. Karibu  mrembo. Unarudi lini Dar?” “Leo jioni. Hatuonani?” “Lazima nikuage Mbawala.  Siwezi kuondoka kimya kimya. “Nitashukuru. Na leo nipo tu nyumbani.” “Ulitaka nije mpaka kwako!?Tunda  akashangaa kidogo. Hamna neno.  Karibu. Naishi peke yangu na ni mazingira  matulivu. Niambie nini unapenda,  nikutayarishie ukifika ukute kipo tayari. Tunda akacheka huku akifikiria. 

“Niambie chochote Fina, nitapika.” Mimi sio  mchaguzi Mbawala. Nakula kila kitu. Ni  surprise. Mbawala akacheka kama  aliyeridhaka. Hapo umenipa uhuru. Basi  karibu.” “Nije saa ngapi?” “Muda wowote  hata sasa hivi.Tunda akacheka taratibu kama anayefikiria kisha akafikia muafaka. “Basi naomba iwe mida ya saa tano ili  angalau saa saba niweze kuondoka. Nijiandae kurudi Dar.” Naona kama unanipa muda  mfupi! Mbawala akalalamika kidogo. 

Huu ni mfupi kwa kuwa umeingiliana na  kazi. Nilikuruhusu unitafute baada ya  kukamilisha hili.” Hapo sawa. Nitafanya  juhudi zote ili weekend ijayo uwepo huku  tena. Tunda akacheka akiashiria kukubalina naye. Baada ya  kumuelekeza nyumbani kwake wakaagana  kwa makubaliano akishindwa kufika, basi ampe dereva taksii  simu, atamuelekeza.  Tunda akajitayarisha vizuri.

Aliporudi  Kinny akamtaka kimapenzi kabla  hajaondoka,  Tunda  akamwambia  anamuwahi Mbawala ili awahi kurudi,  warudi Dar kama alivyobadilisha.  “Naona  leo  tubaki  hapa  tukisherehekea.” Tunda akacheka  huku akimalizia kujiandaa. Ila sio ndio ukatumie siku nzima na Mbawala,  urudi hapa usiku. Wakati mimi ndio  nimekuleta huku.” Ile kauli ilimuuma  sana Tunda. Akamgeukia kama  aliyeishiwa nguvu kabisa.  Kwa  nini  usimpelekee  wewe  mwenyewe tu?” Tunda akakaa kabisa  kama aliyeishiwa nguvu. Nakutania  Fina. Naomba usikasirike tafadhali.  Nimetania tu.” “Hapana. Sio hasira.  Lakini naona kwa kuwa nimeshafanya  kazi kubwa na amekubali. Naona sio  mbaya ukamalizana naye mwenyewe.” Tunda aliongea kinyonge huku akivua  viatu. 

Naomba nisamehe Fina! Nimeropoka  tu. Nahisi nimefurahia kupita kiasi  kazi kubwa uliyofanya. Nimejisahau  naongea na nani. Nishazoea kuropoka  kwa wale walevi wangu. Tafadhali naomba unisamehe.” Tunda hakujibu, akavaa tena viatu vyake, akachukua ile  bahasha akatoka bila kujibu kitu.

 

Nyumbani Kwa Mbawala.

Mbawala alikuwa amejenga nyumba hapo jijini Dodoma. Tunda alipofika nyumbani  kwa Mbawala, akajua ni kwanini  alitaka aende nyumbani kwake. Kama  kujionyesha tu. Kijana huyo mdogo,  alijenga nyumba nzuri sana hapo jijini.  Ilikuwa na ramani nzuri, pazuri na  kweli palikuwa patulivu. “Karibu sana  Fina.”Akaenda kumpokea nje ya geti  baada ya kumpigia simu kumtaarifu taksii imesimama kwenye hilo geti  jekundu kama alivyoelekeza. Mbawala  alimfungulia mlango. Tunda akashuka.  “Asante. Kweli hapa nipatulivu.” Tunda akasifia. Nilikwambia mimi. Wakacheka wakati wanaingia ndani. 

Palikuwa pananukia vizuri. “Ni nini  hicho umepika kinanukia kuanzia  mlangoni?” Twende ukaone. Nimetengeneza  brunch. Tunda  akacheka taratibu huku akisogelea lilipo jiko. Ukutani akakumbana na  picha zilizomfanya atulie aangalie.  “Kumbe waziri Mbawala ni baba  yako!?” Mbawala akacheka.  Huoni tulivyofanana hivyo vichwa? Sasa hivi ndio nikiwaangalia pamoja,  mnafanana naye. Ila naona rangi ya  mama.” “Ewaa. Rangi ya mama.” Tunda akatizama picha nyingine, hapo  ukutani. Kulikuwa na picha amevaa joho halafu akaonekana mwanaume mtumzima mwenye asili ya kizungu na yeye amevaa Joho la tofauti alikuwa akimkabidhi yeye cheti.

 Naona  umehitimu uzunguni!Mbawala akacheka sana.  “Mimi na dada yangu huyu kwenye hii  picha na wazazi, wote tulisomea nje ya nchi. Lakini wote tulirudi nyumbani.  Hapo ilikuwa mahafali ya shahada ya pili.” Hongera sana. Nani sasa mkubwa? Taffy ndiye mkubwa. Tupo wawili  tu.” “Safi sana.Akasifia kidogo  ndipo akaelekea jikoni. Akawa sasa  ameelewa siri ya kiburi na mafanikio  hayo ya huyo Mbawala aliye naye  hapo. 

Alipoingia jikoni akakuta amekaanga  viazi alivyokata pande nne, pamoja na  vitunguu, hoho za rangi tatu. Kijani,  njano na nyekundu. Zote zimekatwa  kwa muundo wa pembe nne tena  kubwa kulingana kidogo na vile viazi.  Vilitoa harufu kama kulikuwa na  kitunguu  swaumu.  Pembeni  kulikaangwa mayai yaliyokuwa na  Cheese katikati. Na firigisi zilizokuwa  zimekaangwa vizuri, na kuwekwa kwenye bakuli zuri pamoja na nyama  za kuku zakukaanga. 

“Mpaka nimepatwa njaa!” Mbawala akalifurahia hilo. Basi chukua sahani,  tuanze kula. Hata mimi bado sijapata  kifungua kinywa.Wakakaa hapo hapo  mezani wakila na kuzungumza.  Vikajaa  vicheko  huku  Tunda  akiendelea kumsoma taratibu kumjua  ni mtu wa namna gani.  Hata walipomaliza kula, walikaa tu  hapo hapo jikoni wakizungumza.  Mbawala ndiye alikuwa mzungumzaji  mkubwa, Tunda akimsikiliza na  kumrushia maswali machache tu  kumuonyesha yupo naye kwenye yale  mazungumzo  huku  kichwani  akimpigia mahesabu. Akaamua siku  hiyo hatampa kitu, mpaka siku  atakayomlipia yeye mwenyewe tiketi  ya kurudi Dodoma. 

Akamkabidhi zile karatasi za Kinny.  Akamuuliza  lini  ategemee  kuidhinishwa. Mbawala akamwambia  atajitahidi kuzungumza na mwenzake,  ili aweke saini ya pili. Napo hapo  akajinadi kuwa yeye ndio mwenye  kauli ya mwisho, akaongea hili na lile.  Ilimradi aonekane wa muhimu kwa  Tunda aliyekuwa akimpigia mahesabu  ni kiasi gani cha pesa atakacho  mchomoa siku akirudi. Tunda alibaki  kimya akimsikiliza tu.

Mwishoe  akaangalia muda kwenye simu yake,  na kumtumia ujumbe dereva taksii  kumtaka arudi pale kumchukua.  “Nashukuru sana kwa brunch.  Naomba niondoke ili niwahi ndege.” “Umeniahidi kurudi.” “Si tulisema weekend ijayo?” “Unafikiri utaweza  kuja?Mbawala akauliza kwa kubembeleza  kidogo.  Kisha  akaendelea. “Nitakutumia tiketi na  mimi mwenyewe nitakupokea uwanja  wa ndege.” Tunda akatoa tabasamu  huku  akisimama.  Nitakuona  jumamosi Mbawala. Nakushukuru  sana.” “Nilidhani unakuja ijumaa  usiku, uondoke jumapili usiku!Tunda  akatulia kidogo kama anayefikiria. 

Naomba nikujibu siku ya jumatato.  Kuna dili ya pesa nyingi ijumaa usiku.  Nitaangalia kama atakubali tusogeze  juma  lijalo.” Daah!  Sitaki  nikuharibie bwana. Lakini ningependa  tupate hata siku mbili Fina. Naweza  hata kufidia hio pesa kama itabidi ili  tu nikupate kwa siku mbili.” Tunda  akacheka kidogo na kumsadiki. Maana  katika mazungumzo yake ya kujinadi,  alionyesha hana majukumu kabisa.  Pesa yake ni yake. Baba waziri, mama ana NGO yake mwenyewe tena nje ya  nchi, wamezaliwa wawili tu. Dada Taffy  naye msomi! Lazima pesa ipo. 

“Nashukuru. Lakini miahadi yenyewe  ni zaidi ya pesa ya siku moja.” Tunda  akazungusha kiuungwana kidogo. Kwa hiyo akikataa tusogeze miahadi  yetu, nitakujulisha ili tupange wakati  mwingine.” “Yaani tusogeze siku!?  Heri hiyo siku moja kuliko kukosa  kabisa.” Wakasikia kengele ya getini.  Wakajua ni dereva taksi.  Naona  amefika.  Tutawasiliana  Mbawala. Asante sana.” “Na mimi  nimefurahi umefika kwangu. Naamini  tutapata muda mzuri ukija.“Naamini  hivyo.” Tunda akambusu shavuni,  akataka kutoka. Mbawala akamvuta  mkono, Tunda akageuka. Naomba  nilipie garama za kuja na kuondoka hapa kwangu.” Tunda akacheka. 

Huna sababu yakufanya hivyo Mbawala!” Wewe ni mgeni wangu  Fina. Nilikualika mimi, sitaki safari yangu ikugharimu bwana.Tunda  akacheka sana.  Unanilipiza nini? “Jana ulinifundisha tabia nzuri. Ukimwita  mtu kwenye kikao, ni kwa garama  zako.” “Sikumaanisha unilipe  bwana.Tunda akakataa kiustarabu  kumbe anashida na kila shilingi  inayokuja mbele yake. “Naomba  unisubiri. Nilijiandaa.” Mbawala  akaondoka pale na kurudi na habasha.  Tunda akacheka huku akiipokea.  Asante.Akamtizama na macho  yake, Mbawala akatoa tabasamu la  kunogewa. Tunda akatoka huku  akicheka taratibu.   

Alipofika tu kwenye taksii akaanza  kuhesabu zile pesa huku akicheka  mwenyewe.  Hakuamini.  “Hapa  sijamvua nguo, nikimvua nguo atanipa kiasi gani!?” Tunda akawaza  huku dereva taksii akiendesha kimya  kimya. Akamuomba wapitie sehemu  mbili  tatu,  ndipo  akamuomba  amrudishe hotelini. 

 Kwa Kinny tena!

Tunda alirudi hotelini akamkuta Kinny anamsubiri  akiwa amejawa wasiwasi. “Bado  umenikasirikia Fina?” Hapana  Kinny. Ila ningependa tuheshimiane.  Mimi sio mtoto mdogo. Najua kitu gani  nafanya.” Nilikosa Fina. Nisamehe  mama. Tafadhali naomba yaishe. Yameisha. Na nimerudi na habari njema zaidi.Akamsimulia  walipofikia na Mbawala, hilo akaona  limemfurahisha zaidi. “Na mimi  nimekuandalia bahasha yako. Hii ni  kwa sasa. Ile tenda ikipita, nitakutafuta.” Asante Kinny. Nashukuru.Tunda akapokea na kuweka kwenye begi lake lakini akionekana amebadilika kabisa usoni.  Ile furaha iliyokuwepo tokea wanafika,  iliisha kabisa.

“Umenichukia Fina?” Hapana.” “Usinichukie tafadhali.  Naona kama tunaweza kufanya  mengi.Tunda akacheka taratibu na kukaa  mbele yake akimtizama, kisha akatulia  kama anayefikiria kidogo, Kinny  akajua ameharibu kwa hakika. Fina  huyu sio Fina waliyekuwa naye jana  na asubuhi hiyo kabla hajaropoka.  “Nafikiri mahusiano yetu yabaki ya  kikazi tu Kinny.” Tunda akaanza taratibu tu na kuendelea. “Nimefurahi tumeweza  kupata muda wa pamoja, na tenda  yako naona ataipitisha bila shida.  Sidhani kama Mbawala ni mtu  kigeugeu. Kwa kumsikiliza tu,  anaonekana anasimamia anachosema. Naamini atakutafuta akupe majibu  mazuri.” Mbona kama unaniaga  Fina?Tunda akacheka kinyonge  kidogo.

Nilipitia kukata tiketi yangu ya ndege, naondoka muda mfupi sana  kuanzia sasa kurudi Dar. Naamini  tutaonana tena wakati mwingine.” Kinny akajirudisha kitandani kama  aliyeishiwa nguvu kabisa.  Tunda  akachukua  vitu  vyake,  akambusu shavuni, akatoka. Kinny  alipogeuka pembeni akakuta bahasha.  Akafungua ndani kwa haraka. Akakuta  pesa  na  kikaratasi  kidogo  kimeandikwa, “Ni pesa ya nauli  uliyonigaramia kunileta huku Dodoma.  Asante.” Kinny akaumia sana. Akahisi  Tunda/Fina  amemuona  ni  mnyanyasaji. Akaogopa hata kumpigia  simu. Akarusha ile bahasha mbali,  ikagonga mlango na pesa zote  zikamwagika chini sakafuni.   

~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~

Tunda aliondoka jijini Dododma akiwa  amemuacha Kinny kitandani. Akiwa  kwenye ndege akaanza kujifikiria.  Akajichukia kidogo. Akaona Kinny  amemdharau kupita kiasi. Lakini  akajiambia hayo ni maisha, na lazima  yaendelee tu. “Kwanza tusingeenda  popote na Kinny! Mkewe amemjaa  sana kichwani mwake.” Akawaza. Tunda  hakutaka kuja kurudi chini. Nani  anafuata baada ya Kinny kushindwa  kuziba pengo la Sadiki? Jibu likawa  Mbawala.  “Mbawala anaonekana anayo pesa  na nimtoaji. Sijamfanyia chochote, amenihonga na kunipa dili kubwa  hivi!” Akawaza Tunda. Na anapenda  sifa, ndio maana  amekazania jina la baba yake ili watu  wajue kama ni mtoto wa waziri.” Akaendelea kukumbuka mazungumzo  yake akijisifia nchi walizokwenda  pamoja kama familia. Dada yake  ananyadhifa hii, mama yake ana hili.  Ilimradi tu kujigamba kwa Tunda.  Tunda akacheka. “Zitamtoka huyu,  mpaka achanganyikiwe.”Akajiambia  Tunda akiwa kwenye ndege. 

  ~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~

Juma hilo Tunda alilichukulia  taratibu akijua akitengeneza  kwa Mbawala, basi tenda ya  Kinny itapita, Kinny atamlipa pesa  zaidi. Bado hongo atakayomchomoa  Mbawala  mwenyewe.  Akaona  ajipumzishe lakini bado akawa na  wasiwasi. “Kweli Mbawala atamudu  kuniweka mjini?” Akajiuliza Tunda.  Huyu ni kijana. Akianza kunihonga  mfululizo, atataka kunimiliki.  Mwishowe atataka nihamie Dodoma.  Kitafuata kutotumia kondomu.  Mwisho mtoto kama sio kuniua kwa  maradhi.” Hapo Tunda akastuka na  kukaa.   

“No way. Hakuna kumtafuta Sadiki  mwingine. Si mzee wala kijana.  Atarudia maombi yaleyale kama  Sadiki.  Kumzalia  mtoto  wa  kuunganisha undugu au ndoa kuwa  mke wa pili.” Tunda akafyonza na  kukusudia kutotafuta mwanaume wa  kumganda. Aliyapenda hayo maisha  yake matulivu ya kurudi nyumbani kwake peke yake na kulala bila fujo baada ya  mahangaiko ya maisha. “Wote  wataniweka  mjini.  Wasijidai  wajanja.”

  ~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~

Tunda mikakati mizito ili Maisha mazuri na matulivu yaendelee jijini. Atafanya nini? Usikose Muendelezo kujua makubwa na mazito ya Tunda kwa wanaume wenye nazo kuanzia kichwani na shahada zao mpaka mifukoni mwao.


CONVERSATION

0 Comments:

Post a Comment