Naomi Simulizi |+1 205 767 8163 |naomisimulizi@gmail.com Nilipotea! – Sehemu ya 32 - Naomi Simulizi

Nilipotea! – Sehemu ya 32

 

A

kabaki bibi Cote na Net akiwa ameshachanganyikiwa. Maya naye akasogea. “Amesemaje?” Maya akauliza. Kimya. “Net?” Bibi yake naye akamuuliza. Mbali na salamu, na maneno machache sana ya kiswahili ni kweli yule bibi hakujua kiswahili kingi. Net alimtisha tu Tunda kumwambia asimtete bibi yake.

“Amekwambia nini?” Bibi yake akauliza tena kwa msisitizo. “Ameongea mambo mengi mabaya na kunitisha, Nana. Ila amesema nikimuoa Tunda leo, ndio mwisho wa yeye kuitwa Cote, na..” Net akashindwa kujizuia na kuficha ukweli lakini si kwa undani sana.

“Sidhani kama tatizo ni kutokuambiwa mapema. Tatizo ni yeye kutokuwa tayari kushiriki ufamle wake na Tunda.” Bibi yake alijibu hivyo. “Nitafanyaje Nana? Nimeingiwa na hofu.” “Siwezi kukwambia nini chakufanya Net. Yeye ni mama yako, na unaishi maisha yako. Uamuzi ni wako. Nimeishi maisha yangu kwa miaka 80 sasa. Unafikiri najali wapi nitalala usiku wa leo?” Net akavuta pumzi.

          “And for me, I support you 100% Net. Kile utakachoamua, nitakuwa nyuma yako kaka yangu. I love you and I have never doubt your decisions.” Maya akamtia moyo kaka yake.  “Thanks Maya.” Akamgeukia bibi yake. “I love Tunda, Nana.” “Basi muoe.” Bibi yake akampa huo ushauri.

“Itakuaje kuhusu mama?” “Huwezi kutatua matatizo yote sasa hivi hapa tuliposimama na Tunda yupo ndani ya gari akisubiri. Ni aidha uende ukamwambie unaaihirisha harusi mpaka wewe na mama yako mtakapowekana sawa, au mfunge ndoa kisha mtajua kitu chakufanya baada ya hapo. Lakini kama alivyosema Maya, hata mimi sijawahi kutilia mashaka maamuzi yako. Na nitakuwa na wewe katika kila maamuzi utakayochukua. Lakini lazima uamue sasa hivi, kwa sababu Tunda hatakusubiri milele.” Bibi Cote alimaliza kwa maneno hayo, akarudi kukaa sehemu ambayo iliandaliwa sababu ya harusi. Maya akamfuata bibi yake nyuma wakamuacha Net amesimama.

~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~

Net akajua ndio amepewa nafasi ya kuamua mwenyewe. Akamkumbuka Gabriel anavyomsubiria Tunda kwa hamu. Akajua akiahirisha yeye siku hiyo au kushindwa kwake kumuoa Tunda siku hiyo ndio kumfikisha Tunda kwenye ndoa na mwanaume mwingine, hasa Gabriel ambaye ameshakuwa na mahusiano ya karibu sana na Tunda.

 Na asipomuoa Tunda siku hiyo, atamuoa lini? Mama yake amemkataa Tunda kabisa. Si wakumkubali kesho wala kesho kutwa. Hakuna jinsi atakuja kumkubali Tunda. Na ameshampa shutuma za wizi. Kisheria ni kweli japo nyumba ilikuwa yake. Amchague nani, Tunda au mama? Net akabaki akiwaza palepale alipoachwa amesimama.

“Lakini atanifanya nini hata nikimuoa Tunda leo? Nitakuja kumbembeleza wakati mwingine. Nitamuacha hata kwa mwaka mzima, halafu nitamtafuta. Nikishamuoa Tunda, tutahamia nchini Canada, nitarudi kuzungumza na mama wakati mwingine. Hata iweje, hawezi kuja kunishitaki kwa kosa la wizi” Net akafikia maamuzi hayo akijiaminisha kwa umbali aliofika na mama yake. Aliacha mengi maishani kwa ajili ya mama yake. Amemfanyia mengi makubwa. Akajiaminisha hawezi kumtenda vibaya. Watayamaliza tu.

~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~

Aliponyanyua kichwa, akakuta kila mtu anamtizama yeye pale aliposimama. Ilishafika saa 11 kasoro jioni. Mchungaji akamsogelea. “Kila kitu kipo sawa, Net?” “Kila kitu kitakuwa sawa. Naomba tuanze.” “Unauhakika Net? Maana tunaweza kuahirisha ili uweke mambo ya familia sawa.” “Familia ni hii ninayotaka kuianzisha leo, baba Penny. Nisipomuoa Tunda leo kwa hili, najuaje kesho?” Net akauliza, lakini akionekana ametingwa kweli. “Sawa.” Wakarudi pale sehemu waliyokuwa wameandaliwa kufungishiwa harusi, baba Penny akampigia simu mkewe kuwa wanaweza kuingia.

Nyimbo zilizoanza kupigwa, zikaanza kumtuliza Net. Wakaingia hao watoto wa kike wakimwaga maua. Penny alionekana amechangamka sana, akaja mama yake Tunda. Tom alikuwa amesimama na yeye mbele na mchungaji, pamoja na bwana harusi na yule mfungisha ndoa wa serikali. Akaingia Tunda na mama Penny akimsaidia kuweka sawa shela yake. Kulikuwa na wachukua video na wa piga picha. Macho ya bibi Cote yakarudi kwa Net, akamuona anatoa tabasamu baada yakumuona Tunda. Wakamuona anajifuta machozi mara kadhaa. Bibi yake akamuhurumia sana Net. “She loves her so much.” Maya akasikika akisema ni kweli kaka yake anampenda sana Tunda.

Tunda alipofika karibu na ile sehemu yakufungia harusi, Net akashuka pale na kumpokea. Akamshika mkono. Akaubusu. Tunda akacheka. “Nakupenda Tunda.” Alijikuta akiongea Net bila kujizuia au kwa sauti ya chini. Aliongea kwa wazi kabisa.  “Na mimi nakupenda Net.” Naye Tunda ndani ya shela akajibu taratibu na tabasamu usoni. Net akataka kama kumbusu, akajirudi. Watu wakacheka.

Ilikuwa harusi ndogo. Watu wachache na tulivu. Kule kumuona Tunda kulimfanya asahau kila kitu hata kama mama yake alitoka hapo na vitisho, Net hakuwa akikumbuka. Mabusu kwa Tunda hayakuwa yanaisha. “Naona muondoke tu.” Bibi yake alifanya kila mtu acheke. Na kweli. Hawakukaa hapo muda mrefu. Baada ya kukata tu keki, Net akacheza mziki na bibi yake, wakaagana moja kwa moja kwa makubaliano yakuja kuonana tena nchini Canada. Net na Tunda wakaondoka.

 Honeymoon ya Tunda na Net. Kwenye Resort ya nguvu jijini.

H

awakwenda mbali sana kwenye mapumziko yao. Kutoka hapo Salasala ilipokuwa nyumba ya Net, wakaelekea kwenye hiyo Resort ambayo Net alichagua. Tunda alifurahia sana yale madhari. Alikuwa ameandaa nguo za mapumziko ya juma nzima.

Tunda alikusudia kupumzika haswa. Alifanya kazi mfululizo kuanzia anatua jijini kutokea jijini Arusha. Miaka miwili bila mapumziko, mfululizo. Kama si kupamba kwenye kumbi basi yupo ofisini kwake au kanisani. Hata hiyo week ya harusi pia alikuwa na kazi mbili. Hakuziacha hizo za katikati ya juma. Alifanya ili kutimiza lengo alilokuwa nalo. Kupata pesa kamili ya kumkamilishia mama yake kodi ya nyumba ili atoke hapo hotelini siku ya jumapili.

Mama Penny alikubali kuendelea kumfundisha kazi mama yake kama alivyomfundisha Tunda mpaka atakapojua na kuendelea na biashara ya Tunda. Alipata nyumba mitaa ya  Kurasini. Tunda alihakikisha anamkabidhi mama yake pesa ya kulipa kodi ya mwaka mzima ili asisumbuke na watoto. Ni kweli Tunda alikuwa amechoka, maana hiyo siku ya alhamisi asubuhi, alikwenda kupamba ukumbi wa kitchen party, akaenda saluni ndipo akaenda kwa baba yake.

~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~

Net aliingiza mizigo yao hapo ndani chumbani. Tunda alikuwa ameshabadilisha nguo aliyokuwa amevaa ya harusi. Chumbani kwa Net, nyumbani kwao Salasala, wakati Net anaagana na Maya na bibi yake. Kwahiyo alifika hapo hotelini na nguo za kawaida tu, sio shela. “Natamani tu kulala.” Tunda aliongea wakati anatoa viatu vyake. Net akamsogelea. “I wanna make love to you Tunda.” Net akamwambia kwa upendo.

“Nataka kukukumbatia, na kufanya mapenzi na wewe mpaka niridhike. Unajua nilikuwa nakusubiria?” Tunda hakuwa akiamini. “Kweli Net!?” Tunda akasimama kwa mshangao, asiamini. “Oooh yeah! Sasa unafikiri ni kwa nini nilikuoa?” Tunda akacheka na kujificha usoni. Akahisi mikono ya Net mwilini mwake.

Midomo akasikia shingoni, akaendelea kumbusu. Akamkumbatia akitegemea mabusu yaendelee wakiwa wamesimama vile vile, akahisi gauni lake likipandishwa taratibu, mwisho akalitoa kabisa. Midomo ikaendelea kumnyonya shingoni mpaka akafika juu ya matiti yaliyokuwepo kwenye sidiria. “Leo napata yakizungu.” Aliwaza Tunda.

Ile mikono ya Net, ikafika kwenye vishikizo vya sidiria alipitisha vidole mara kadhaa huko mgongoni huku midomo yake ikiwa shingoni, masikioni kwa Tunda mpaka akili za Tunda zikatulia pale kwa mumewe, na yeye Net akaridhika kuwa Tunda yupo pale kiakili.

Aliendelea kumpapasa ndipo akamtoa ile sidiria. Tunda aliyezoea kutumikia wanaume, usiku huo ukawa usiku wake, Net hakutaka afanye chochote kwenye mwili wake. Kila Tunda alipotaka kujitoa ili amchezee yeye, alihakikisha anamrudisha kule alipotaka kumfikisha akiwa ametulia. Alimnyanyua mpaka ukutani akamnyanyua kwa mkono mmoja. Alitua kifuani kwa Tunda, mapenzi mapya na mageni kwa Tunda usiku ule yakaanza.

Mapenzi ya kunyanyuliwa, midomo shingoni huku mtoto huyo wakizungu akifanya naye mapenzi! Tunda alishakuwa amechanganyikiwa. Mwili huo ulipapaswa vilivyo, kwa mara ya kwanza Tunda akajisikia pumziko kwenye mikono salama ya Net.

Alimtoa ukutani hapo na kumuweka juu ya meza iliyokuwepo hapo pembeni, Net akaendeleza mchezo kwa muda mrefu, nakuhakikisha mpaka Tunda anaridhika. Waliingia kuoga wakarudi kujilaza kitandani. Kimya kwa muda. Akiendelea kumchezea vinyweleo vya pembeni ya kichwa. Mara kadhaa alimbusu huku akiendelea kumpapasa.

“Asante Net.” Tunda alijikuta akiongea na machozi. “Kwa ajili ya nini?” Akauliza huku akimfuta machozi na kumbusu. “Sikuwahi kufikiria kama unaweza kunitazama, kunishika na kufanya mapenzi na mimi kama hivi, hasa baada…” Net akaanza kumbusu tena. Nakuufanya usiku ule uwe wa tofauti na siku zote Tunda alizokuwa akiwahudumia wanaume wote kitandani.

Tokea alipokuwa akifanya mapenzi na baba Tom bila kondom, akitumiwa mwili wake, akatoka hapo na kuanzisha biashara kama hiyo, lakini akitumia kondom. Akihangaika kuwaridhisha ili kudumu kwenye soko. Usiku huo kwa mara ya kwanza, anafanya mapenzi ya kweli. Kwa hiari, akibembelezwa vilivyo, tena na mumewe! Bila kondom. Huru. Hakuna wakati Net alimgusa, asifike tena kwa furaha. Ulikuwa usiku wa kihistoria kwa Tunda.

Jumamosi ya Fungate!

Waliamshwa na kifungua kinywa kizuri kilichokuwa kimeletwa na muhudumu wa hapo hapo hotelini. “Kwani uliwaambia walete?” Tunda akauliza huku akitupia zabibu nyekundu mdomoni aliyokuwa ameitoa kwenye kijisinia alicholetewa na Net hapo hapo kitandani. “Nililipia huduma ya fungate. Tungeweza kwenda kula chini mgahawani. Lakini nilitaka kutumia muda huu hapa kitandani na wewe. Sikutaka tutoke kabisa, mpaka siku tunayoondoka hapa.” Tunda akacheka na kujifunika mto usoni.

“Unafurahia?” Akauliza Tunda huku akimchungulia pembeni ya ule mto. “Sana.” Akajibu Net na busu la kipanda uso. Tunda akacheka akiashiria kuridhishwa na hilo jibu.

“Net!” Net alikuwa amerudi kwenye kigari kilichokuwa na chakula, akageuka. “Jana umeufanya ni usiku wangu tu. Na mimi leo nataka kukufurahisha.” Net akacheka tu, na kugeuka. Akachukua na yeye chakula chake akasogea pale kitandani. “Chakwanza nataka ujue jana haukuwa usiku wako tu. Na mimi ulikuwa usiku wangu. Mbali yakukufurahia, ujue furaha yangu imekamilika kuona ulifurahia wakati wote.” “Umejuaje kama nilifurahia?” “Huwa najua ninapo danganywa.” Net akajibu na kumbusu tena. Safari hii alimbusu kwa muda kidogo. Akambusu tena na tena.

Hawakujua ni saa ngapi waliweka chakula pembeni, nakujikuta wamezama katika ulimwengu wao. Tunda akigugumia raha aliyokuwa akiipata kutoka kwa Net. Alimkumbatia Tunda huku akifanya naye mapenzi kwa kutulia bila papara. Aliweza kuhisi ile raha anayoipata hata Net mwenyewe. Hata Tunda mwenyewe alijua hadanganywi, ni kweli Net naye anamfurahia.

Net alitawala mchezo na siku hiyo karibia yote. Mwishowe Tunda akahisi labda anataka kumpumzisha na shuruba alizokuwa akizipata kuhudumia wanaume. Ni kama alitaka kumuonyesha kwa wakati ule hakuwa kazini, ila kwenye ndoa.

          Usiku wakiwa wamejilaza kwenye sinki la kuogea, Net akiwa mbele ya Tunda, amempa mgongo, Tunda akimchezea nywele zake taratibu, akamuona anageuka. “Tunda!” Akamwita. “Unapenda watoto wangapi?” “Sijafikiria Net. Unakumbuka nilikwambia hata sijui kama nina uwezo wakuzaa?” “Nakumbuka. Lakini kama ikitokea Mungu akakujalia uzazi, ungependa kuwa na watoto wa ngapi?” Tunda akafikiria kidogo. “Nitajua nikishapata wa kwanza na wa pili.” Net akacheka na kumbusu. “Na wewe?” Tunda akamuuliza. “Natamani wasiwe chini ya wawili.” Tunda akacheka huku akifikiria. Net akajiweka sawa, nakuanza kumbusu tena.

“Twende tukaanze kutafuta wa kwanza basi.” Net alimfanya Tunda acheke. “Tusipofanikiwa?” “Ndio itakuwa hatujafanikiwa.” Tunda alibaki akifikiria. “Umeshafikiria kama tukifanikiwa?” Net akauliza. “Nahisi bado ninahofu na hilo Net.” “Naomba utulie kabisa, tumuachie Mungu. Ila naomba tukifanikiwa tukapata mtoto wa kiume, tumwite Cote Junior Cote.” Tunda akashangaa.

“Net! Umeshafikiria mpaka jina!” Net akacheka. “Unaniogopesha bwana!” “Nimekwambia usiogope. Mwembe ni mwembe tu, hata usipozaa maembe ni mwembe.” “Wewe ni mzungu gani unajua Kiswahili hivyo!?” Net alicheka sana.

“Usiogope bwana. Naamini tutakuwa tu sawa. Twende tukamtengeneze Cote.” Tunda akacheka. “Ndio tunafanyaje?” “Nitakufundisha style nzuri.” Tunda akazidi kushangaa. “Net wewe!” Net akazidi kucheka. “Twende mke wa Net!” Tunda alijisikia vizuri sana. Akacheka. “Nimefurahi ulivyoniita hivyo.” “Ndivyo ulivyo.” “Siamini mwenzio kama nimeolewa na mimi!” “Hata mimi siamini kama nimekuoa Tunda. Nilianza kuingiwa na wasiwasi, nikahisi watanzania watanipora hivihivi najiona.” Tunda alicheka sana.

Jumapili.

Mazito & Machungu kwa Net & Tunda.

W

akiwa kwenye usingizi mzito sana, wakasikia mlango wao ukigongwa. Lakini safari hii uligongwa kwa nguvu sio kama jana yake walipokuwa wakiletewa chakula. Wote wakashtuka. Net akatoka kwa haraka. Akavaa rob  nakusogelea mlangoni akiwa na hasira kidogo kwa nini mgongaji amegonga kwa fujo kiasi kile! Akafungua.

“Wewe ni Nethaniel Cote?” Walikuwa wanaume wanne hapo mlangoni wakamshtua sana Net. “Ndiyo.” Net akajibu. “Upo na Tunda?” Tunda aliyekuwa pale kitandani kama alivyozaliwa, akajifunika vizuri huku hofu ikianza kumuingia. Net akajua tayari mambo yameharibika.

“Kuna nini? Kwa nini mnamuulizia mke wangu?” “Kisheria sio mkeo, sababu hukukamilisha taratibu ili kuweza kuoa hapa nchini. Kwa hiyo hata ndoa mliyofunga siku ya ijumaa, haitambuliwi popote kisheria. Ulioa bila kukamilisha taratibu. Pili, wewe na yeye wote mpo chini ya ulinzi kwa tuhuma zakuibia kampuni ya Cote. Mmechukua nyumba ya kampuni uliyokuwa umeajiriwa, wewe kama mfanyakazi, ukammilikisha Tunda bila idhini ya mmiliki mwenyewe ambaye ni mjane Bi Ritha Cote.” Mwili mzima wa Net na Tunda ulikuwa ukitetemeka. Wale watu wakaingia ndani. Bado Tunda alikuwa amekaa kitandani.

          “Mpo chini ya ulinzi. Vaeni, twendeni kituoni.” “Naomba mnichukue mimi. Tunda hausiki. Kama ni nyumba, mimi ndiye nimemuuzia.” Net akajaribu kumtetea. “Tunda anayo makosa yake. Anatumia biashara ya ngono kujiingizia kipato. Ushahidi wa jinsi alivyokuwa akipokea pesa kwa biashara hiyo ya ukahaba, upo. Na wapo watu ambao wapo tayari kutoa ushahidi wao, kuonyesha jinsi Tunda alivyotumia ngono kama biashara. Safari hii tunamkamata hapa sisi wenyewe tukiwa mashahidi. Yupo na wewe hapo, wote mkiwa uchi akiidhinisha kukaa kwako nchini kinyume na taratibu kwa kukupa ndoa ya uongo ili tu, kujinufaisha.” Tunda na Net wakashangaa sana.

“Sio kweli kabisa. Tunda hajawahi kunishawishi kwa lolote na hajanidanganya! Nipo hapa kwa ridhaa yangu mwenyewe. Kama ni makosa ni yangu sio Tunda. Huo ni uongo wa mama kwa sababu anataka kuniadhibu mimi kwa...” Net akataka kuendelea kumtetea Tunda. “Naomba mvae. Mtapata nafasi yakujitetea mbele ya hakimu. Sio hapa. Sisi tuna kazi moja tu, yakuwafikisha chini ya vyombo vya usalama.” Ilimbidi Tunda kuvaa palepale wakiwa wamewasimamiwa. Wakatolewa pale kwenye chumba chao chafungate na pingu mkononi.

          Walikuwa wamekodi chumba cha juu kabisa. Wale askari kanzu walitumia lift kuwashusha mpaka chini. Waliwatoa pale wageni wote waliokuwepo pale eneo la mapokezi na mgahawa wa pale hotelini wakipata kifungua kinywa, walibaki wakiwashangaa wao jinsi wanavyo vutwa tena wakiwa na pingu mkononi. Walitolewa kama wahalifu haswa. Wakivutwa mpaka nje kabisa sehemu yakuegeshea magari, wakaingizwa kwenye gari ya hao askari kanzu. Tunda alikuwa akilia sana. Net alijaribu kumtuliza huku yeye mwenyewe akitetemeka hapo  ndani ya gari.

Ritha Awatenda Bila Huruma!

Mara mlango wa nyuma wa gari walipokuwa wamewekwa, ukafunguliwa. Alikuwa mama Cote. “Naamini mmesomewa mashitaka yenu.” “Umefanya nini mama? Kwa nini unamwadhibu Tunda bila kosa? Naomba unifanyie mimi chochote, umwache mke wangu aondoke zake. Tunda hafahamu chochote juu ya ile nyumba!” “Basi. Aweke saini hapa, kuonyesha ameirudisha ile nyumba kwa jina la kampuni, ili kesho niende ofisi za Aridhi kuzuia hati.” “Sawa.” Net akakubali kwa haraka sana.

“Bado Net.” “Unataka nini tena mama?” “Msaini karatasi za talaka.” “Haiwezekani mama!” Net akabisha. “Hivi unajua kosa linalokukabili wewe Net? Umeoa kimakosa. Tena ukiwa upo hapa nchini bila kibali.” “Unaongea nini mama!?” “Kampuni ya Cote inaonyesha ilishakufukuza kazi miezi mitatu iliyopita. Kwa hiyo upo hapa nchini zaidi ya siku 90 ukiwa huna kazi.” “Mama!” Net akashangaa sana.

“Mbona barua yako yakufukuzwa kazi ipo kwenye faili ya wafanyakazi wa kampuni ikionyesha ulishafukuzwa kazi! Na ushahidi ninao.” Net hakuwa akiamini. “Ila kwa muda wote huo umekuwa ukijilipa mshahara wewe mwenyewe. Uliiba hundi zangu ukawa unaniibia kila mwezi.” “Kweli mama!?” Net aliumia, akaona machozi yakimtoka bila kujua.

“Unakumbuka mimi kukuandikia hundi ya kukulipa mshahara?” “Si kwa kuwa mimi ndiye niliyekuwa nikilipa wafanyakazi mshahara?” “Kwa hiyo ndio hapo na wewe ukatumia mbinu hizo hizo kuniibia?” Ritha alimgeuka mtoto wake, kama hamfahamu.

Tunda alikuwa akilia sana nakushindwa hata kumwangalia mama Cote. “Wewe ni mwizi, na umesaidiana na huyu malaya kuniibia. Kosa la pili upo hapa nchini zaidi ya muda uliotakiwa kuwepo. Tatu, umedanganya serikali ya Tanzania kwa kutoa vithibitisho vya uongo ili kukufanikisha kufunga ndoa.” “Naomba unifunge mimi muache Tunda. Hana hatia.” Net alijitahidi kumtetea Tenda.

“Kwani hujaambiwa makosa yake huyo malaya?” “Naomba usimwite hivyo. Ni mke wangu. Tafadhali mama.” “Mke wako au tapeli uliyekubali akuibie mchana kweupe?! Una nini wewe unachoshindwa kuelewa? Tunda anakabiliwa na kosa lakufanya biashara ya ngono hapa nchini. Vidhibitisho vipo polisi. Wameprint historia za simu zake zote jinsi alivyokuwa akipokea pesa za biashara zake. Na mashahidi wapo. Makosa mengine ni kama niliyokutajia hapo juu. Kuingia naye njama za kuniibia, ili umpe yeye mali zangu kwa kukufundisha wewe jinsi ya kumuoa ili upate kibali chakuwepo hapa nchini. Kwa hiyo amekurubuni kwa ndoa yeye kama raia ili umpe mali zangu. Usitegemee huyo malaya wako atatoka jela leo wala kesho. Watamfunga mpaka kifo chake.” Tunda aliendelea kulia tu.

“Mkitaka msaini haya makaratasi, ili nifute kesi ila kama hamtaki basi, mtakutana na vyombo vya sheria.” Akataka kuondoka. “Naomba karatasi ya nyumba nisaini.” Net akamuwahi kabla hajafunga mlango. “Kwa hiyo unaenda kufuta kesi?” Net akauliza. “Si ndivyo nilivyokwambia? Okoa muda hawa maaskari wanataka kuondoka na nyinyi.” “Wanifungue sasa! Nitasaini vipi na pingu?” Mama Cote bila hata wasiwasi akaenda kumwita mmoja wa askari, akaja kuwafungua pingu Net na mkewe.

Net akasaini zile karatasi baada yakusoma na kuona hajategwa tena. Akampa na Tunda. “Naomba utulie uweke saini Tunda, haya mambo yaishe. Na samahani nimekuingiza matatizoni.” “Huyo malaya alikuwa kwenye matatizo kabla hata hujamuokota. Asijidai kulia. Weka saini urudishe mali zangu.” Mama Cote aliongea na kufyonza.

Tunda akafuta machozi na kuweka saini. “Bado ya talaka.” “Ni nini mama? Nyumba yangu nimekupa. Tena kwa maandishi kabisa. Endelea na maisha yako niachie mke wangu. Hayakuhusu tena. Umetaka nisikutafute, sitakutafuta. Naomba utuache.” “Sitakubali Tunda akuharibie maisha yako Net. Hata kama sasa hivi utanichukia, nichukie tu. Hii ndoa nitafanya kila niwezalo, ife. Yeye ameshaishi maisha yake yote hapa duniani, anataka amalizie na wewe! Sitakubali. Hata kama itanigarimu mtengane kwa kuishi jela. Potelea mbali.” Net akainama kama anafikiria huku akilia kama mtoto.

“Basi mtakachoamua, mtamwambia hakimu. Mimi nakwenda kupumzika.” “Naomba usibiri kidogo. Naomba muda na Tunda.” “Ili akutapeli kwa maneno yake yenye sumu! Hata kidogo. Nikifunga huu mlango hapa, mjue kujitetea kwenu ni mbele ya hakimu.” “Mama please!” Net akajikuta akibembeleza karibia kupiga magoti kwa hofu. “Sikukusudia kudanganya swala la ndoa. Yule mwanasheria aliniambia amefuatilia kila kitu na kukamilisha. Tunaweza kufunga ndoa.”

“Usinitanie Net. Ujue unazungumza na mimi? Nakujua sana wewe sio mjinga, mtu wakudanganywa kama mtoto mdogo. Ulikusudia kufumbia macho sheria, sasa hivi ndio unajidai hukujua sababu unabanwa! Mimi naondoka. Sina jinsi yakukusaidia tena. Nilikuonya juu ya huyo malaya, ona alipokufikisha!” “Tunda hajanifikisha hapa mama, wewe ndio umenifikisha hapa.” “Unaendeleza kiburi tu, kwa nini unashindwa kujifunza!?” Mama Cote akauliza kwa kushangaa.

“Anawalisha nini huyu Tunda kitu kinachowafanya muwe kama wajinga!? Afadhali mwenzako Meto amefunguka macho na ameamua kumshitaki huyo Tunda.” “Haiwezekani kama umeweza kumshawishi hata na yule mzee mpaka akakubali kuingia kwenye hila zako! Ni nini mama?” “Mungu amemfungua nakumjua Tunda kwa hila. Kuwa ameingia kanisani kumaliza na wakanisani. Waduniani amewamaliza wote, sasa hivi ndio anaharibu kanisa! Sasa hapa kwa Cote ndio aandike maumivu. Na ninakuapia Net, usipo saini hiyo talaka, utayaona maisha ni machungu.” “Mimi naomba nisaini, ili nimuache huru Net.” Kwa mara ya kwanza Tunda akaongea.

          “Nipe mimi hizo karatasi.”  Tunda akasisitiza, Net akazidi kulia. “Sasa kwa kuwa ulishaingia kwenye hiyo ndoa feki, nataka na uandike kabisa. Umeamua kumuacha Net, bila kutaka akupe kitu chochote. Mali ulizomkuta nazo Net, zitabakia ni za Net, na wewe hutaki kitu chochote kutoka kwake.” “Mama! Yaani akili zako ziko kwenye pesa tu?” Mama Cote hakutaka kumjibu Net, akampa zile karatasi Tunda. Akasaini na kuandika kama alivyoambiwa na mama Cote. Akamkabidhi.

“Haya, na pete zote ulizovalishwa na Net, naziomba hapa.” Mama Cote akanyoosha mkono kwa Tunda. “Haiwezekani mama. Hizi pete za ndoa ni jasho langu. Nimetengeneza kwa pesa nyingi sana na hiyo pete ya uchumba ni ya bibi! Naomba muachie mke wangu avae.” “Ni nini usichoelewa Net? Unataka kuzidi kunipandisha hasira? Bado unamwita huyu malaya ni mke wako! Nipe hizo pete Tunda kabla sijakukata hicho kidole.” Tunda akavua zile pete na kumkabidhi Mama Cote. Akaziweka kwenye pochi yake, akatoka na kumwita askari.

Yule askari akafika pale. “Huyo mwanamke nishamalizana naye. Mnaweza kuendelea naye.” “Hapana mama. Umeahidi Tunda akisaini ndio anakuwa huru.” “Hayo ni juu yake yeye na sheria za Tanzania. Ataenda kujitetea juu ya biashara ya ngono aliyokuwa akifanya. Huko sihusiki. Nahusika na kumdhibiti kwenye himaya yangu.” Bila hata kupoteza muda, wakamvuta Tunda kumtoa pale kwenye gari.

Net alimsukuma mama yake kwa nguvu pale mlangoni alipokuwa amemsimamia, akataka kwenda kwa Tunda huku akipiga kelele, askari mwingine alimkamata Net, Tunda akaingizwa kwenye gari nyingine huku akilia, wakaondoka.

  Kwa Net!

Baada ya Tunda kuondolewa pale, Ritha akamgeukia mwanae. “Sasa hapa nchini huwezi kukaa hata lisaa.” Mama Cote akiwa na askari wawili, akamwambia Net. “Unamakosa ambayo ukifikishwa kituoni, hutakaa utoke leo wala kesho. Kwa usalama wako tu, heri uondoke. Watu wa uhamiaji wameanza kukusaka tokea ijumaa. Ni vile jumamosi na jumapili hawafanyi kazi. Lakini kesho ujue nilazima utakamatwa. Gabriel naye amekushitaki kwa makosa yake. Yaani kwa kifupi, hapo ulipo Net, ni mhamiaji haramu. Na mbaya zaidi, unaonekana ulikuwa hapa nchini ukiwa huna kazi ila wizi tu.” Net alikuwa akilia huku ameweka mikono kichwani asiamini.

Mama Cote alihakikisha anamtisha Net vilivyo. Akamtajia tena makosa mengi sana huku akimsingizia kwa kazi ambazo alikuwa akimtuma yeye mwenyewe. Na ushahidi alimwambia anao. Net alikuwa anashindwa hata kujitetea. Alijuta kumpeleka Tunda kanisani kutubu. Alijuta kumkutanisha na mama yake. Alibaki akimuomba Mungu msamaha bila yakumjibu kitu mama yake. “Mungu wangu naomba unisamehe! Tunda nisamehe. Mungu wangu nisamehe! Tunda nisamehe!” Net alisikika akiomboleza bila kuchoka wala kumjibu mama yake.

“Nimekukatia tiketi ya ndege ya Emirates. Hawa polisi watakufikisha uwanja wa ndege na kuhakikisha unaondoka hapa nchini mchana huu wa leo. Ukithubutu kuwatoroka kwa namna yeyote ile ukidhani bibi yako atakuja kukutoa kesho yake, ujue utaangukia mikononi kwa Gabriel. Anahasira na wewe yakupitiliza kwa kumsaliti. Umemuoa mwanamke wake akiwa ameshakuonya. Kwa kifupi na yeye anakusaka kama alumuasi.” Mama Cote akaendelea.

“Tangia siku ya ijumaa aliposikia unamuoa Tunda, alianza kupita humo kwenye mahoteli akikusaka. Mimi mwenyewe wamekubali kunipa namba ya chumba ulichopo ni kwa kuwa nimeonyesha kitambulisho kuwa ni mama yako, na hawa ni polisi. Ndipo nikajua kama upo chumba gani. Sasa ni aidha uondoke sasa hivi, au akukamate Gabriel uliyemsaliti kwa kumuoa mwanamke wake, au ukamatwe na serikali ya Tanzania, ufungwe jela na kujiharibia kabisa.”

“Na ujue kwa kuwa ni wewe Nathaniel Cote, kesi yako itanguruma ulimwengu mzima. Habari zitafikishwa mpaka Canada, hakuna atakayekuamini tena kwa makosa uliyojiingiza kijinga hapa nchini. Na ujue wazi, hata hizo mali ulizotakiwa kukabidhiwa na bibi yako hutaweza kumiliki tena kwa kuwa unaweza kujikuta unaishia jela. Na utaua jina la Cote kote ulimwenguni. Hata kule alikokuwa akipita bibi yako, hataweza tena.” Net aliendelea kulia tu.

“Tiketi na hati yako yakusafikiria hiyo hapo.” Akamrushia pale alipokuwa amesimama. “Uamuzi ni wako. Kwenda au kubaki, ukawe mali ya wanaume wenzako huko jela. Na hayo macho na hiyo rangi, nakuhakikishia hutakaa jela ya hapa hata siku mbili bila kulawitiwa, na utatoka na UKIMWI. Wewe wapelekee hiyo sura nzuri ya kizungu hao wanaume wa jela wenye njaa za miaka na miaka za wanawake, halafu uone kama hujanikumbuka zaidi.” Mama Cote akaondoka bila hata kugeuka nyuma.

Na wale askari hawakusubiri Net aamue. Walimfunga pingu. Wakaokota ile hati yake yakusafiria na tiketi, wakamwingiza Net kwenye gari mpaka uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu JK Nyerere, Dar. Aliingizwa kwenye ndege kama mfungwa, wakahakikisha ndege inaondoka, ndipo wale askari nao wakaondoka. Nao walilipwa ili kukamilisha hilo.

Kwa mama Cote.

Wakati mama Cote akifanya hayo yote, Bethy hakuwa mbali. Alikuwa ndani ya gari yake akisubiria aone mwisho wake ili kuhakikisha mama Cote hamdanganyi. Ugomvi wa Bethy na mama Cote ni kutowatenganisha Net na Tunda. Bethy alisema wafanye chochote kile, lakini Tunda asije akawa huru kurudi kwa Gabriel. Ndipo mama Cote akatumia akili ya haraka kumtuliza kuwa, atamtenganisha Tunda na Net, na hawatakaa wakaonana daima.

Wasiwasi ulimwingia mama Cote pale alipoitwa na Net, siku ya harusi ya Tunda na Net. Mtu mwenye akili ya haraka na ambaye atamuelewa kwa haraka akamfikiria nakumpata Bethy. Lakini akakumbuka Bethy nia yake ilikuwa nikutaka Tunda na Net wawe pamoja. Inamaana mama Cote hatashinda. Akamfikiria Gabriel. Akajua wote wawili yeye na mkewe watamfaa kwa namna yake.

Akawapigia simu mara tu alipotoka kuzungumza na Net pale nyumbani kwake siku ya ijumaa, ya harusi. Aliwaambia kinachoendelea, ila akawasihi wasubiri mpaka kesho yake ambapo bibi Cote anaondoka nchini na ulinzi wote uliokuwa ukimsubiria, ndipo watekeleze. Ila kwa wakati ule, wakutane na washauriane nini chakufanya.

Bila kuchelewa wakafika kila mmoja kwa wakati aliopangiwa na Ritha, lakini hakutaka wawe wote watatu pamoja. Kila mmoja alikutana na Ritha akiwa na lake kichwani. Gabriel akiwa na hasira yakusalitiwa, Bethy akiwa na furaha ya ndoa ya Net na Tunda.

Ili kumuweka sawa Bethy akamueleza kwa kumrubuni Bethy kuwa Net hawezi akawa amemuoa kihalali Tunda. Akamueleza utaratibu wa sheria za Tanzania, kuolewa na mgeni. Maana na yeye aliolewa na baba yake Net. Anajua mambo yote. Akamuhakikishia hata yeye hayupo salama, kwani endapo ndoa hiyo ikitenguliwa tu, basi akamuhakikishia Bethy kuwa, Tunda atarudi kwa mumewe.

Na akamwambia tena, hata kama ndoa yao haitatenguliwa, basi, kwa kuwa Tunda ni malaya sana, kitendo cha kuolewa na rafiki ya mumewe, ni kama kumkaribisha fisi dukani. Lazima atamzunguka tu na kuishia kuwa na mahusniano na wote wawili. Gabriel na Net. Hapo Bethy akakubali kwenda kikaoni kupanga mikakati mipya. Maana mwanzoni alikataa hata kukutana na mama Cote. Alimwambia mama Cote ni kama kazi yake yeye imeisha. Ameshamtoa Tunda kwa mumewe anaolewa na Net.

Kwa Gabriel, akaweka mikakati rahisi tu. Kwa kuwa ni kama wao wawili malengo yao yanafanana. Kuwatenganisha kabisa Net na Tunda. Kikao chao wao wawili kikaenda vizuri wakiongea lugha moja, lakini akimficha mwisho wa Tunda. Wakaweka mikakati ya mwanzoni pamoja. Gabriel akitaka watengane, ndipo apate nafasi yakujirudi kwa Tunda, aombe msamaha, warudiane.

 Mama yake akajua kabisa atakuwa amemtumia mwanasheria wa kampuni kumfanikishia mambo yake ya ndoa, kwa kuwa aliona ule ukaribu ulioanza ghafla kati ya Net na yule mwanasheria. Akampigia simu yeye moja kwa moja na kumuuliza maswali ya kumtega, bila kujua akijua anamsaidia mama yake Net, yule mwanasheria akamwelekeza kirahisi tu kwa yule mwanasheria mwingine aliyemuelekeza Net, kwake. Alimpa na namba za zimu za yule mwanasheri.

Sasa kwa kuwa mama Cote alijua sheria ya Tanzania kwa maswala ya ndoa, akaanza kumbana yule mwanasheria kwa maswali magumu, mpaka akakiri kuwa alimtapeli tu Net. Hakuwa amepeleka vitu vyote vilivyokuwa vikihitajika kwenye ofisi husika. Hapo wote wakafurahi sana. Wakawa wamemkamata Net. Sasa ili kuwatenganisha, ndio wakapanga kumsingizia makosa mengi ili akiondoka nchini, asiweze hata kurudi tena. Hapo wakafikia sehemu nzuri, kila mmoja na furaha.

Ndipo sasa siku ya jumamosi asubuhi wakiwa wamejawa furaha ya kupata habari zote, wakakutana sasa wote watatu. Swali likaja kutoka kwa Bethy, sasa Net akishaondoka, Tunda je? Kwa upande wa Gabriel alishaonya kabisa kuwa Tunda aachwe, wasifikirie hata kumdhuru. Mkewe alipinga wazo la kuondolewa Net nchini, na kuachwa Tunda bila ndoa. Ugomvi ukaanza hapo. Gabriel na mkewe. Mwishowe mama Cote akamshika mkono Bethy, akamwambia aende naye chooni, akatulie ndipo warudi kuzungumza akiwa ametulia.

Mama cote kama kawaida yake akatumia akili za haraka. Wakiwa kulekule chooni akamuweka sawa Bethy. “Mimi sio mjinga Bethy. Tatizo lako unaruhusu hasira zikutawale na kushindwa kufikiria.” Mama Cote akiwa na Bethy chooni akaendelea. “Tukiwa na Gabriel, muonyeshe huna shida na Tunda. Lakini mimi na wewe tutajua jinsi yakumuangamiza Tunda.” “Tutafanyaje?” Kidogo Bethy akawa ameingia kwenye mstari. Akasikika akiuliza akiwa ameanza kutulia.

“Hayo ndio maneno! Sio matusi na fujo. Haya mambo yanahitaji kufanyika kwa akili. Katika kila hatua tunamuhitaji Gab ili kutufanikishia. Gabriel anapendwa sana na polisi kwa ukaribu aliojitengenezea na hicho chombo cha usalama. Mwache atusaidie. Tukifika mwisho tutaendelea wenyewe. Jifanye mjinga.” Mama Cote aliongea na tabasamu lakumtuliza.

“Hapo sawa, sio vinginevyo. Ndio tunafanyaje sasa?” “Nikumpachika makosa ambayo hawezi kutoka jela leo wala kesho.” “Makosa gani?” Bethy akahoji tena. “Kwanza wewe unajua umalaya aliokuwa akifanya Tunda tunaweza kumshitaki kama ni biashara ya ngono ambayo kwa sheria ya Tanzania ni kosa?” Bethy akacheka na kugonga. “Unaakili wewe!” Bethy akamsifia asijue hata yeye anachezewa. 

“Ndio maana nakwambia tulia tupange.” “Haya, nipe mambo. Lakini hilo kosa, si anaweza kutolewa hata kwa dhamana?” “Kwani tunampa kosa moja? Tunamshitaki kwa kosa la kununua ile nyumba. Tunamshitaki kwa wizi pia. Kuwa alitumia rushwa ya ngono, kumshawishi mfanyakazi wangu kumpa moja ya nyumba ya kampuni kwa ahadi nyingine yakumpa uraia hapa nchini kwa kumtengenezea makaratasi ya uongo. Amemrubuni Net.” Bethy alicheka sana. “Nimekukubali mama Cote!” “Mjini shule. Kula kwa akili. Lasivyo tusingekuwa hapa?” Wakagonga.

“Gabriel yeye atatusaidia kumtoa Net hapa nchini, wakati sisi tunamfunga Tunda. Akija kutoka huko na wewe umetulia na mumeo.” Wakagonga tena. “Sasa kwa furaha hii, sithubutu kurudi kwa Gab. Atanishtukia. Wewe nenda kanichukulie funguo zangu za gari na pochi. Mwambie Bethy amekasirika sana, ameamua kuondoka.” “Umeona jinsi ukitulia ulivyo na akili?” Wakabadilishana mawazo wakapanga mambo yao. Mama Cote akafanya kama walivyopanga. Akaenda kumchukulia pochi na funguo zake za gari, Bethy akaondoka na kumuacha mama Cote na Gabriel.

Walibaki wawili hao wakipanga jinsi yakumtoa Net nchini. Na kwa kuwa Gabriel alikuwa mtu wakuonekana akisaidia watu huko kwenye vyombo vya habari, ashajenga vituo vya polisi zaidi ya vitano nchini ili kuimarisha ulinzi mpaka vijiji vilivyokuwa na uhitaji huo. Alikuwa mtu wakutoa misaada mbali mbali kwenye vituo vya polisi. Basi alifahamika na kuheshimika sana. Ritha alijua Gabriel atamfaa kumtoa mtoto wake pale nchini.

“Hilo halina shida mama Cote. Ila naomba kukuonya juu ya Tunda. Mwanao alinisababisha nikamuacha Tunda akiwa kwenye shida, wakati mimi alikuwa akinisaidia sana. Huwezi kujua ni shida kiasi gani ninapitia kwenye ndoa yangu. Kwa mabaya yeyote yale mtakayomsema nayo Tunda, kwangu alikuwa mwema sana. Net ndiye aliyenidanganya nikamtelekeza mwanamke aliyenipenda na kunithamini kwa dhati. Sitakubali tena chochote kibaya kimpate Tunda. Kwa gharama yeyote ile, na kwa yeyote yule, lakini sio Tunda. Naomba hapo tuwekane sawa kabla hatujaendelea.” Gabriel alionekana wazi katika hilo hana ubiya na mtu.

“Mimi nakuelewa Gabriel. Najua maumivu yakusalitiwa. Tusaidiane kutengeneza kisa kizuri chakumuondoa Net hapa nchini. Zungumza na polisi watakao tusaidia kumtoa hapa bila jina lake kuingizwa kwenye vyombo vya sheria. Najua ni ujinga tu, nataka kumfundisha lakini sio kuyaharibu maisha yake kabisa.” Hapo Ritha akawa upande mmoja na Gabriel.

 

“Hilo usitie shaka. Nitazungumza na mkuu wa kituo cha Kawe. Atatupa polisi. Watamtoa Net huko aliko, na nitawaambia wahakikishe wanampandisha ndege. Kazi ibakie kwako. Mtengenezee kesi vizuri, ajue hatakiwi kurudi tena hapa nchini. Na mimi ningependa kuwa na copy ya kila kosa utakalo mtengenezea, ili kuhakikisha tupo sawa na hakuna kugeukana.” Mama Cote akashtuka.

“Lini umeanza kunitilia mashaka Gabriel? Usiwe na wasiwasi.” Mama Cote alizungumza akicheka kama kutaka kumzuga Gabriel. “Mimi sina wasiwasi. Ila nataka Net ndio awe na wasiwasi ili asirudi tena hapa nchini kwetu. Wapo wanawake wengi tu huko kwao, kwa nini aje kuchukua wake zetu huku? Ila kama wewe hutaweza, niachie mimi hiyo kazi nimtengeneze vizuri, nimshikishe adabu.”

“Naona tugawane tu majukumu. Wewe zungumza na  mkuu wa kituo cha polisi kirafiki, mimi nitaandaa vitu vyote na wewe nitakupa.” “Hapo sawa. Jioni tukutane tena hapa ukiwa umekamilisha kila kitu. Na mimi nitakuja na jibu la uhakika.” Bila kusubiri jibu, Gabriel akasimama na kuondoka akamuacha mama Cote pagumu.

Wote watatu walikutana hiyo hiyo siku ya jumamosi jioni. Wakawekana sawa. Wakaonyeshana hili na lile. Gabriel akawapa mwendelezo wa kile walichozungumza na mkuu wa kituo cha polisi. “Ameahidi kutupa askari wa nne bila shida. Tupo naye karibu sana. Nimemueleza hatari ya kumuweka Net hapa nchini kwetu. Akataka tumfungulie mashitaka kabisa. Ahukumiwe hapahapa nchini au hata akirudishwa nchini kwao, arudi na pingu.” Mama Cote akashtuka sana, akajikaza kusikiliza mpaka mwisho.

“Lakini nikamweleza mahusiano tuliyo nayo na wewe mama yake, akanielewa. Lakini ametoa agizo kuwa ifikapo jumatatu, Net asiwepo hapa nchini lasivyo wao watamkamata na kumshitaki.” Hapo mama Cote akameza mate.

Wakaendelea kuzungumza na kupanga, Gabriel akiwa hajui mpango kando wakufungwa kwa Tunda kwa tuhuma nzito. Zile zile alizomshitakia Net kwa mkuu wa kituo cha Kawe, kumbe ndizo hizo hizo mama Cote na Bethy wamezibadili tu jina na kusema Tunda ndiye amezifanya kwa kutumia rushwa ya ngono.

Hiyo Jumapili Sasa.

Ndio hiyo siku ya jumapili sasa wakafanikisha kukamatwa wote. Wale polisi walimtaarifu Gabriel aliyewalipa pesa pembeni, wamjulishe pindi Net atakapopanda ndege. Walimpigia simu Gabriel na kumtaarifu kuwa ndege ya Net, imeshaondoka kwenye viwanja vya mwalimu Nyerere, Dar-es-salaam. Na yeye akampigia simu mama Cote akiwa na furaha sana. Asijue mama Cote alikuwa na Bethy kwenye hoteli ileile wakijipongeza kumtoa Tunda kwenye maisha yao.

Jumapili hiyo ikawa na taarifa alizokuwa akizisubiri kwa hamu Gabriel. Kuondoka kwa Net nchini. Tena baada yakusaini talaka. “Ameniachia Tunda wangu. Sasa tupo huru. Kilichobaki nikurudi kwa  Tunda, nakumuomba msamaha. Maisha yetu yaendelee. Talaka ya Bethy naanza kuishugulikia kwa haraka sana.” Aliwaza Gabriel na tabasamu usoni.

Kwa Tunda!

T

unda alifikishwa kituo cha polisi cha Kawe ilikuwa tayari ni saa tano asubuhi ya siku hiyo ya jumapili. Alifunguliwa kesi ya makosa matatu makubwa, na aliambiwa hawezi kutolewa kwa dhamana mpaka hukumu yake itoke. Gafla ikawa kama anakosa la jinahi! Hata hivyo alijua hakuna anayejua alipo kwa wakati ule. Nani atamtolea dhamana! Akabaki akilia tu asiamini kama fungate limebadilika kuwa kifungo.

                 Aliachana na Net nje ya hoteli. Hakujua Net alipopelekwa na wala Net hakujua alipopelekwa Tunda. Aliondoka nchini akilia bila chochote mkononi ila hati yake yakusafiria tu. Na kama walimfanyia makusudi, asiwasiliane na yeyote yule mpaka anaondoka nchini. Walimbana, hawakumpa hata nafasi ya peke yake akapiga simu. Mtoto huyo wa kiume wakizungu, aliondoka nchini akilia kama mtoto mdogo aliyekatwa kidole akiwa na hati yakusafiria tu, na tiketi yake ya ndege.

Tunda alilala usiku huo, siku ya jumatatu yeye na mahabusu wengine wakahamishiwa gereza la Keko. Tunda hakuwa akiamini. Wakati waliohudhuria kwenye harusi yao wakidhani wapo wakifurahia fungate, kumbe maharusi hao ambao ndoa yao ilidumu kwa masaa 42 tu, walikuwa kwenye shida isiyoweza kusimulika. Na mbaya zaidi, makosa yote ni kweli Tunda alihusika moja kwa moja au kuhusishwa na Net.

Kwenye mashitaka au kosa alilotuhumiwa la nyumba. Yeye alifanya akiambiwa kila kitu kipo sawa kisheria, aweke tu saini. Sasa anakataa vipi wakati aliweka saini kwenye karatasi zilizoonyesha amenunua nyumba kutoka kampuni ya Cote, wakati mwenye kampuni amekataa kuwa hajamuuzia! Net alishaanza kushugulikia hati ya nyumba ziwe kwa jina la Tunda. Fomu zote zipo tayari ofisi za  wizara ya Aridhi, yeye Tunda akiwa ameweka saini na majina yake yote yalikuwa yakionekana kwenye hati hiyo!

Mbaya zaidi hakuwa na habari kamili juu ya maswala ya hiyo nyumba wala hati. Ni mambo aliyokuwa akifanya Net mwenyewe na mwanasheria. Yeye alikuwa ni muweka saini na mtoa taarifa zake kamili. Kama jina na mwaka wake wa kuzaliwa. Na sehemu ya kuweka saini aliletewa hizo fomu na kuweka saini bila hata kusoma, akimwamini mpenzi wake. Hakujua chochote. Ila alipokea milioni 3 taslimu na kuandika hundi yenye jina lake kamili, kutoka kwenye akaunti yake, Tunda akilipa kampuni ya Cote, kuonyesha yeye Tunda ndiye amenunua hiyo nyumba kwa milioni tatu tu. Wapi kunakouzwa nyumba kwa milioni tatu kama sio alitoa na rushwa ya ngono!

Kwenye kosa la maswala ya vyeti vya ndoa, hapo Tunda hawezi kukana pia. Picha zake na saini kwenye kuomba kufungishwa ndoa na serikali vipo kwa yule mwanasheria. Mama Cote alishamuogopesha na kumpanga yule mwanasheria vizuri, mpaka akakubali kumgeuzia Tunda makosa yote. Kuwa yeye Tunda ndiye aliyetumia uraia wake kuolewa na mtu ambaye asiye raia, kwa kumdanganya kuwa ameweka kila kitu sawa ili aolewe.

Tunda aliendelea kuwaza nakushindwa hata kuwatafuta kina mama Penny kuogopa kuwaingiza na wao matatizoni. Hakujua ni umbali gani Ritha na Bethy wako tayari kwenda kumuangamiza yeye na yeyote aliye karibu naye.

“Nikimtafuta mama Penny, anahasira sana. Anaweza kuwavaa wale kina mama. Akaishia kubambikiziwa makosa na yeye.” Tunda akaendelea kuwaza akiwa mahabusu. “Wakimkamata mama Penny, ndio mama naye atakuwa amekwama. Hatakuwa na chakufanya. Tom na Aneti watageuka kuwa watoto wa mtaani kama sio kufungiwa na mama yao na kushindwa kwenda hata shule.” Tunda akaendelea kujiwekea vikwazo vizito wakati akifikiria nani wakumpigia simu ili kumtaarifu kuwa amekamatwa.

“Mwishoe nitajikuta nakwamisha kila mtu mpaka huduma ya baba Penny.” Tunda akaendelea kuona ugumu. “Net inawezekana na yeye amefungwa au amerudi nchini kwao! Mama Penny na mumewe wakikamatwa, na baba naye atakuwa hana mtetezi.” Hapo Tunda akaona atulie kabisa hata mama Penny hakutaka ajue mpaka ajue hatima yake yeye mwenyewe.

~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~

Ikawa mchana, ikawa usiku siku ya kwanza. Ikawa jumatatu, ikawa jumapili, juma la kwanza. Kimya. Hakuna aliyemsikia Tunda wala Net. Kwa kina mchungaji hawakuwa na wasiwasi na wala hawakutaka kuwapigia simu kuwasumbua wanandoa hao wachanga, wakaona wawape muda, mpaka wawatafute wenyewe. Maisha yakaendelea.

Kwa Net!

N

et alitua nchini Canada akiwa na hali mbaya. Kwanza aliondoka akiwa amevaa tu t-sheti na jinsi. Hakuwa hata na sweta au simu. Mbali na tiketi na ile hati aliyopewa yakusafiria na mama yake, hakuwa na simu wala pesa. Barafu ilikuwa ikimwagika nchini hapo pale Net alipotuwa uwanja wa ndege ya Halifax Stanfield katika mji wa Nova Scotia karibu kabisa na anapoishi bibi yake na Maya. Au nyumbani kwao nchini hapo.

Net alipata panic attack, vichomi kama aliyebanwa na pumu. Akiwa kwenye kuhangaika ili kutafuta taksii impeleke nyumbani kwao, kusini mwa Halifax kwenye mtaa wa Beaufort, nje ya uwanja wa ndege kwenye baridi kali, akaanguka na kupoteza fahamu. Gari ya wagonjwa ilimchukua mara moja na kukimbizwa hospitalini huku wakijaribu kupandisha joto la mwili wake lililokuwa limeshuka sana.

          Kwa bahati mbaya sana pale alipoanguka, aliangusha na hati yake yakusafiria mbayo ilikuwa na jina lake kamili na anuani ya nyumbani kwao. Walimpokea hospitalini hata hawafahamu jina lake na yeye alikuwa hana fahamu. Siku tatu zikawa zinaisha bila ndugu yeyote wa Net kumtafuta na yeye bado alikuwa na hali mbaya.

Kwa matatizo ya kubanwa mapafu, Net akaanza kutumia mashine za kupumulia na alishapata pneumonia. Alisafiri kwa masaa yote hayo zadi ya 15 kutoka Tanzania mpaka Canada, bila sweta wala shati zito. Aliingia baridi yakupitiliza. Ni kama alikuwa kwenye friji kwa masaa hayo yote.

~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~

Kwa hakika Tunda yu matatizoni. Tena matatizo makubwa sana. Anajitoa vipi? Nani wakumtetea? Baba yake yupo gereza la Segerea, yeye yupo mahabusu Keko.

Je, mama Penny na mumewe watakubali kujiingiza doa kwa Tunda mwenye shutuma nzito na za kweli za uchangudoa au umalaya kama anavyomwita mama Cote? Tena waliyekutana hata miaka mitano haijafika, na wao wanakanisa la watu wanao wachunga na kuwaongoza?

Wanajibu vipi shutuma nzito za wao kama wachungaji kushiriki ndoa ya serikali, tena kama vifichoni? Walikuwa na haraka gani waliyoshindwa kuwashawishi kondoo hao kusubiri kutangazwa kwa ndoa hiyo mara tatu tu ndipo waoane? Nini walichoficha na kushirikiana na muhalifu huyo Tunda, kutomshauri kufuata taratibu nyingine kama wanazowahubiria washirika wengine, kanisani!

Usikose kifuatilia kitakachoendelea kwa Tunda huko mahabusu na Net mahututi hospitalini, nchini kwao, Canada!

Ø  Nini kitatokea kwa Gabriel baada ya juhudi zake zote kugonga mwamba, na kujua amegeukwa na mama Cote/Ritha?

Ø  Pumziko alilokuwa akihangaikia Bethy, atalipata?

Ø  Mali alizohangaikia kuzilinda Ritha, kwa kiasi kikubwa hicho mpaka kufikia kutumia siri za nyumbani mwa Mungu, na kutengeneza jeshi kubwa kinyume na Tunda, kumfanikishia mipango yake aliyopanga kwa akili kiasi hicho, atafaidi kwa amani na utulivu?

Ø  Bibi Cote atafanya nini?

Ø  Nani wakulaumiwa?

Mengi mazito na yakusisimua yatafichuliwa Part 5. Usikose....

CONVERSATION

0 Comments:

Post a Comment