Naomi Simulizi |+1 205 767 8163 |naomisimulizi@gmail.com NILIPOTEA! - SEHEMU YA 37. - Naomi Simulizi

NILIPOTEA! - SEHEMU YA 37.

 


Net akajikaza na kujibu. “Mimi mwenyewe.” Akaendelea.“Nampenda Tunda jamani.” “Hilo tunajua. Wala hatujawahi kulitilia mashaka.” Akajibu mchungaji. “Mimi sijawahi kuoa na wala sijawahi kuona mama akifanya anayoyafanya. Nimejifunza kutokana na makosa.” Net akaendelea. “Sasa hivi hata nana, yupo makini na mama kwa kuwa tumejua kuwa ni mtu hatari. Ila tabia ya kuhakikisha anapanga mipango kwa makini mpaka kufanikiwa, hilo kila mtu anamjua. Anaakili sana yakupanga mambo yake. Popote nitakapokuwa na Tunda, nitaongeza umakini. Nitahakikisha Tunda hana kosa kisheria.” “Utafanyaje?” Mama Penny akauliza kwa haraka.

“Nyumba ya hapa, ipo chini yake. Namaanisha ni ya Tunda. Hata leo akiniacha, nyumba ni yake kwa jina lake kabisa. Sitamtoa Tunda hapa, nikaenda kuishi naye kule bila kibali maalumu. Nitahakikisha nakamilisha kibali cha ‘Permanent resindence’ ili aweze kuishi kule na kuwa na uwezo wa kuwa huku bila shida.”

“Atakuwa akifanya kazi na mimi, sio kuwa namchukua tu hapa ili akawe mama wa nyumbani au kumfungia mahali! Hapana. Ataishi maisha ya uhuru sio kama mfungwa. Akiwa huru kuchagua na kufanya kile anachokipenda. Akiona hapapendi au haridhiki na mazingira ya kule, atakuwa huru kuchagua kile anachokipenda.” Net akaendelea.

“Kujibu swali lako baba Penny. Nakwenda kuishi na bibi. Pale ndio nyumbani kwetu au kwangu. Bibi yangu ni mtu mzima, sina jinsi yakumuacha na kwenda kuishi sehemu nyingine, na hilo nilimwambia Tunda. Bibi au nana kama nilivyozoea kumuita, anajua na anaelewa kuwa nina familia, au alijua nitakuwa na familia. Anapoishi ndipo nitakapokuwa nikiishi. Ndio maana kabla ya ndoa yetu, alitaka kupata muda na Tunda. Walizungumza nini, mimi sijui.”

“Lakini nana alimpenda sana Tunda. Anahistoria nzima ya Tunda, na bado alinitia moyo na kuniambia kama nataka kuwa na maisha yenye amani hapa duniani, basi niwe na Tunda. Akatoa baraka zake zote. Na yeye akiwa kama mmiliki mwenye kampuni ninayofanya kazi kwa sasa, ananiruhusu kuwa na Tunda hapa, huku nikiwa na majukumu mazito ambayo inamlazimu kuajiri mtu wa pili kufanya kazi yangu.”

“Hayo yote anafanya kwa ajili ya Tunda. Nana anampenda Tunda na ndio maana alirudi nchini kumpigania kisheria, kuhakikisha makosa yake yanafutwa. Tukafanikiwa mawili, moja kumbe Bethy alificha ushahidi. Yote hayo nana amefanya kwa pesa zake ikiwa imemgarimu mamilioni ya pesa.” Net akaendelea.

“Tutakuwa pia tukiishi na mdogo wangu, Maya. Lakini Maya pia anampenda sana Tunda, hata Tunda anajua. Tuliishi wote watatu Arusha. Tunda ndiye aliyemfanya Maya arudi shule. Hilo analisema Maya kwa kila mtu, na familia yetu hawasahau hilo. Anamsubiri Tunda kwa hamu sana, na kila wakati anauliza ni lini tutakwenda. Hao watu wawili waliobaki kwenye maisha yangu, ndio wamuhimu, na ndio watakaoishi na Tunda na watoto wangu. Mengine nitajua mbele ya safari.” Kimya.

“Narudia tena. Sijawahi kuoa, wala kuwa na mama wa namna hii. Nikisema nina mipango fulani makini dhidi ya mama yangu, nitakuwa nawafurahisha tu na kuwadanganya. Sasa hivi yupo kimya. Sijui anawaza nini na anamipango gani mingine. Sijui natakiwa kujipanga dhidi ya nini! Ila nimeshajua au tumeelewa kuwa nia yake nikunitenga na Tunda, basi nikuongeza umakini.”

“Sasa hivi hata nikisema nimuache Tunda hapa kwenu, itasaidia nini? Na kwa muda gani? Itakuwa ndoa ya namna gani hiyo?! Tunda amekubali kuambata na mimi, naombeni mtutie moyo. Halafu Canada sio mbali jamani! Milango ya nyumbani kwetu ipo wazi. Muda na wakati wowote, mje kututembelea, na mtushauri.” Kidogo mama Penny akaridhika.

“Eti mama Penny?” Mama Penny akacheka kidogo. “Hapo sawa Net. Naomba muongeze umakini tu. Tafadhali sana. Najua mnapokuwa kwenye mapenzi machanga, mnakubaliana mambo ambayo hamfikirii madhara ya mbeleni. Sisi tumeishi kwenye ndoa, ndio maana mnaona tupo kama tunawabana.” “Binafsi nashukuru, japo unakuwa mkali sana kwangu mama Penny!” Net alilalamika kidogo, wakacheka. “Hata kwangu Net. Sio wewe tu.” Tunda akaingilia.

“Kwa kuwa nawapenda. Sitaki mkapotea, au watu wakamfanya Tunda kama mpira wakuchezea na kuutupa popote. Hapana. Na sijui kwa nini! Moyo wangu umefungamana na Tunda, siwezi kuhema wala kujisaidia.” “Na hilo analolisema mama Penny sio uongo. Tumepoteza washirika wengi sana.”  Akaongeza mchungaji.

“Nimeona, nikataka kuuliza kuna nini!?” Net akaingilia. “Penny huyo! Mimi nikiwaambia naenda kumtoa sadaka, hamuamini. Heri anyamaze tu.” Tunda akacheka na kumwangalia. “Mfunikeni jamani Penny wangu! Pale baridi inampiga.” Tunda akamuita dada. “Naomba mfunike Penny wangu, jamani! Ona alivyojikunja!” “Ujanja wote umemwisha!” Dada yao aliongeza huku akienda kumchukua na kumpeleka kitandani.

“Mtoto huyu jamani! Sijui namfanyaje?” Wote wakacheka wakati anatolewa pale kwenye kochi. “Kwani alifanyaje?” Tunda akauliza. “Ila ujue mwanangu sio muongo.” Baba yake akamteta. “Ni mkweli wakupitiliza Penny jamani! Na hana hofu hata!” Wote wakacheka.

“Nilimuona anamsuta mama Vero pale kanisani!” Tunda aliwafanya waanze kucheka tena. “Na usifikiri ule ndio mwanzo! Hata yule mama kumuona pale tena ni muujiza tu.” “Ila sidhani kama na yeye atarudi tena. Kwa nilivyosimuliwa baada ya ibada ya leo!” Mumewe akaongeza.

“Hawezi kurudi kama wenzake.” Mama Penny akamalizia. “Yote hayo ni Penny?” Tunda akauliza. “Dhambi zao bwana. Waache kumsingizia mwanangu.” Mchungaji akamalizia, kisha akaanza kucheka. “Tena Pendo nitamchapa! Anamwambia Penny anakipilipili kama changu!” Mkewe na kina Tunda wakaanza kucheka tena mpaka machozi.

“Pendo amenishauri nichague mtoto wa kizungu, asiwe na nywele kama za Penny, anakipilipili kama cha dad wake. Sasa sijui nachaguaje na mtoto yupo tumboni!” Tunda aliongea huku akisugua tumbo taratibu kama alivyomuona Net akifanya.

“Nitamtandika tu, ngoja aamke.” Baba yao aliongeza. “Watoto hawa, naona niwagawe tu jamani!” Mama Penny aliongeza huku akifikiria. “Niambie walifanyaje tena?” Tunda akauliza. “Si unajua mambo yako ndio yalijaa mtandaoni?” “Askari wa pale mahabusu, Keko, walikuwa wakinionyesha na kuniambia.”

“Basi, ukawa gumzo. Kila mtu anaongea lake. Lakini ni kama Net akawa hayupo kwenye picha sana. Ni wewe, Gabriel na Bethy. Sasa watu wakawa wanasema Net alikukimbia. Maana si alikuvalisha pete ya uchumba hadharani?” “Nilipokuwa jela, niliona picha zangu mtandaoni za siku Net akinivalisha pete ya uchumba. Nikajiuliza watu walijuaje?” “Itakuwa ni watu wa palepale kanisani tu, ndio walianza kuzisambaza baada ya lile tukio la Gabriel na mkewe.” Mchungaji akajibu.

“Au hata marafiki zangu na washirika wa kanisani kwetu niliokuwa nimewaalika siku ile.” Net akaongeza huku akifikiria. “Labda. Basi, habari ikawa hiyo kwenye mitandao. Tunda! Tunda! Sasa si Penny akawakuta kina mama Vero na wenzie wanaangalia huku wakikusema? Penny akawasikiliza mpaka akaridhika mwenyewe na kichwa chake. Acha aanze kuwasuta. Akawaambia Tunda ni anti yake yeye. Ni kama mama yake wa pili. Anamjua anti Tunda, na wao ni waongo wanamsingizia sababu ya wivu wao. Acha bwana yule mtoto awaseme wale kina mama!”

“Akawaambia mzungu wa anti Tunda alimuoa, wala hajamkimbia. Na yeye amesimamia harusi.” “Mama Penny!” Tunda akashangaa. “Kwani ni madogo? Akawaambia na dad alikuwepo, yeye na Pendo walimwaga maua. Ilikuwa harusi ya kizungu, wamefungia kwenye maua.” Wakaanza kucheka.

“Msicheke! Mtoto yule aliyaongea yote bila kuacha hata neno. Yeye na mdogo wake walivalishwa nguo mpya, wakapanda limozini.” “Yaani Penny!” Tunda alishika kichwa. “Akawasuta hapo na kuwaambia anaenda kuwasemea kwa dad wake, na ibada ikianza atawatangaza kuwa wao ni wasengenyaji. Si wakadhani anadanganya?” “Usiniambie alitangaza!?”  Tunda akashituka sana.

“Wewe si unamjua Penny? Sasa kipindi cha ushuhuda kikaanza. Mchungaji kakaribisha watu kama leo vile. Hatujui kinachoendelea, Penny kanyosha mkono. Baba yake akamkaribisha pale mbele tukijua ni mambo yake ya kawaida. Acha mtoto aongee pale mbele. Niliomba Mungu ashushe unyakua siku ile. Mtoto aliwasema vibaya yule, huku akiwashitakia kwa Mungu kuwa wao wanadhambi kuliko shetani. Akawataja kwa majina yao wote pale mbele. Akieleza baba yake na mama yeke ni mashahidi wa harusi ya anti wake, na wao walisimamia wala mzungu wa anti yake hajamkimbia.” Tunda akatoa macho.

“Jamani Penny nyinyi!” “Akasema yeye anataka watubu.” Tunda akaanza kucheka mpaka machozi. “Sasa baba Penny kwa nini hukumpokonya kipaza sauti?” “Hivi wewe umemsahau Penny!? Mimi mwenyewe nilikuwa kwenye mshtuko. Nilishinda kujua naendelezaje ile ibada! Maana ni kama na sisi alitushitaki. Wachungaji, tunasimamia harusi za vichochoroni! Mambo yalianza kanisani, kwa nini tulimalizia vichochoroni? Halafu na zile kashfa zote, mwanangu anasema sisi tunajua. Alimsikia anti Tunda akitubu mbele ya Mungu na dad wake. Na akasema hiyo ilikuwa mara ya pili. Alishasikia anti wake alienda hata kutubu kwenye kanisa la mzungu wake.” Net alibaki akitingisha kichwa.

“Inamaana sisi tulikuwa tukijua yote kabla ya tukio zima la Gabriel na mkewe halijatokea, ila tulificha au kufunika. Sijui kama mnaelewa Tunda?” Mchungaji akauliza. “Mungu wangu Penny wangu!” “Lakini nia yake ilikuwa nzuri, kukutetea. Yeye alisema anti Tunda alishasamehewa na Mungu kwa kuwa alishatubu mbele ya mchungaji na Mungu. Lakini sasa watu walilaumu sana. Wengine walisema tulikutetea ili utuletee mzungu kanisani kwetu.” “Sisi wanafiki.” Mkewe akaongeza.

“Jamani poleni.” “Pole kubwa tu, maana kuanzia hapo watu wakaacha kufika kanisani.” “Wala hawakuchukua muda mama Penny. Jumapili inayofuata, nusu ya kanisa hawakufika.” Mchungaji akamalizia.

“Poleni sana jamani. Poleni na samahanini.” Tunda alifikiria tena kidogo. “Sijui kwa nini, lakini nilijua tu, anguko langu mimi, haliwezi kuwaacha nyinyi salama! Ndio maana sikutaka mjihusishe na sisi.” “Mama Penny asingeweza. Alikuwa kama amechanganyikiwa. Heri ungetoka labda ungemtuliza. Na usifikiri Penny alipoongea vile ndio ikawa basi? Na yeye akaenda kuwaongezea.” “Mama Penny!” Tunda akashangaa sana.“Aii! Mimi ujinga huwa siwezi. Anayetaka kuondoka ataondoka na anaetaka kubaki abaki.” “Kabakiwa na vijana wake tu wanao mpenda.” Mumewe akaongeza wakaanza kucheka. “Yaani mama Penny jamani!” “Na aliwawashia moto kweli kweli.” “Sasa wewe ukasemaje?” Tunda akauliza huku akicheka.

“Ndio nilijua kibarua changu anakiotesha majani! Nikajua washirika wote wataondoka, maana alifanya kuwapa na ushauri kabisa. Asiyeweza kuendana na maono ya pale, yakupokea na kulea wenye dhambi, aondoke wala hatazuiliwa.” “Mama Penny wewe!” Tunda aliendelea kushangaa huku akicheka. Waliendelea kuzungumza hili na lile, Net na Tunda wakaondoka.

~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~

Tunda alikuwa kimya njia nzima. Net alimuona ametulia zaidi ya kawaida yake. Akaamua kumuacha. Walifika hotelini, akapitiliza kuoga, nakurudi kujitupa kitandani moja kwa moja. Bado hakuwa amezungumza kitu. Hofu ya kumkuta mama Cote huko waendako ikaanza kumsumbua. “Nini atanizulia safari hii?” Tunda aliendelea kuwaza. “Akinifunga huko, nani atalea mtoto wangu?” Tunda akaendelea kuwaza, asijue Net anamtizama muda wote. Na lile ombi lakutaka kusumbuliwa kabla ya kulala pia akatupilia mbali. Akabaki amejilaza akiwaza.

Akajigeuza kulia na kushoto akapotelea usingizini bila hata kuzungumza lolote. Alimsikia asubuhi ameamka. Akafungua macho, alimkuta ameshavaa tayari. Alibeba bakuli la ndizi walilopewa jana yake usiku nyumbani kwa mama Penny, akamuona anatoka. Akajua ameenda kupasha moto. Lakini hakurudi kwa muda mrefu tu mpaka Net akaamua kumfuata. Alimkuta amekaa nje, sehemu ya bustani akila. Akamsogelea, lakini alikuwa akikizungusha tu kile chakula.

Net akavuta kiti mbele yake, akakaa. Tunda akashtuka kidogo. “Sikutaka kula pale chumbani, nilijua ningekuamsha.” “Sasa chakula sikitakuwa kimepoa?” “Hata hivyo nimeshiba. Mama Penny alikiweka kingi. Nataka nikajiandae, niende hospitalini.” Net akabaki akimwangalia. Tunda akajirudi. “Ungependa twende wote?” “Huo ndio ulikuwa mpango wetu. Lakini naona umeamka na mipango mingine!” Tunda akainama na kuendelea kukoroga chakula chake.

“Niambie kile ulichoamua Tunda.” “Sijaamua chochote Net. Ila nikwambie ukweli tu, nimeingiwa na hofu. Maisha ya jela sio maisha mtu yeyote angetamani kuishi. Wakati ule ilikuwa afadhali, lakini safari hii nina mtoto! Itakuaje aje anizushie jambo jingine nifungwe? Itakuaje kwa mtoto wangu? Mama yako anaakili sana Net. Sana. Hujui safari hii atakuja na kitu gani! Najua unanipenda, lakini mapenzi peke yake hayawezi kunilinda na mama yako. Tulijaribu, wewe mwenyewe uliona. Niliishia jela.” “Kwa hiyo unataka kusema nini?” Net akauliza akiwa ameshabadilika rangi kabisa.

“Mama yako hawezi kubadilika. Atabakia mama yako daima. Hata ufanye nini. Kama vile alivyokuwa mama yangu. Hata nifanyeje, bado ni mama yangu tu.” “Kwa maana nyingine, wewe unaweza kubadilika?” Tunda akanyamaza. “Ulipoapa ni katika shida na raha utakuwa na mimi, ulimaanisha nini?” “Hapana dalili ya raha Net. Labda mama yako apate kile anachokitaka, kwa mimi kuwa mbali na wewe. Lasivyo mimi nitabakiwa kuwa muhanga daima. Sitaki kurudia kupita nilikopita Net, hasa sasa hivi ambapo nina mtoto atakayekuwa akinitegemea.” Tunda alimuona mishipa ya kichwani ikisimama.

“Hapa nyumbani ndio utakuwa salama?” “Sijui Net! Lakini angalau kwa hapa ni nyumbani na wewe unaweza kuingia na kutoka utakavyo. Unaweza kuja kumuona mtoto wakati wowote utakao, bila shida. Naomba mimi nibaki Net. Acha mimi nibaki tu.” “Na kuhusu sisi?” Net akauliza.

“Naomba uwe huru kuendelea na maisha yako, ukipata mwanamke mwingine…” “Nyamza Tunda. Usimalizie. Tafadhali nyamaza tu.” “Kweli Net.” “No. Unaniumiza tu Tunda. Naomba unyamaze tafadhali.” Net alifikicha macho. Akavuta pumzi kwa nguvu. “Naomba tujiandae twende hospitalini.” Net akasimama na kurudi chumbani kwao, hapakuwa mbali.

Tunda alimuhurumia sana, lakini hakujua chakufanya. Akasimama na kumfuta. Alimkuta bafuni akioga. Akavua nguo zake zote akaingia bafuni alipo. Alimkuta amesimama katikati ya bomba anaangalia ukuta. Tunda akamshika mgongoni taratibu. Akageuka. “Nakupenda Net.” “Sidhani Tunda. Sidhani hata kama ulishawahi kunipenda.” Tunda alishituka sana.

“Unawezaje kusema hivyo Net?!” “Hivi unajua sababu kubwa yakugombana na Gabriel, rafiki niliyekuwa naye tokea mtoto, ilikuwa ni wewe? Ilikuwa ni heri nigombane na Gabriel kuliko kumuona hata amekugusa. Lakini wewe upo tayari kuniona naoa!? Unawezaje hata kunifikiria nipo na mwanamke mwingine na ukawa sawa tu!?” “Kwa sababu nakupenda Net! Sitaki kukuona unateseka.” “Kweli Tunda!?” “Ni heri mimi niumie, kuliko kukuona unateseka Net. Na ninajua kuwa na mimi nikujitesa tu. Ni heri uendelee na maisha yako.”

“Naendeleaje Tunda? Niambie. Naendeleaje? Eti unasema nikuachie mtoto wangu huku, niwe nakuja kumtembelea kama nakwenda kutizama vivutio fulani hivi! Sijui hayo maisha Tunda. Najua kupambana. Na ndoto zangu zote ni mimi kuhangaika kwa ajili yakumtunza mke wangu na watoto.”

 “Jana uliniahidi tutakuwa wote, huwezi kuiachia bahati ya kuwa na mimi. Leo umenishauri nini tena?” Tunda aliishiwa nguvu, akajiegemeza kwenye ukuta. “Nataka kujua ukweli Tunda, unamaanisha ulichoniambia au ni hofu tu?” Tunda akabaki kimya.

“Niambie tu ukweli. Ukweli ni upi unao umaanisha? Ni jana au leo?” “Nimeingiwa na hofu Net.” “Ukweli ni upi Tunda?” “Natamani kama ingekuwa tofauti Net. Natamani tungekutana kwenye mazingira tofauti. Na wazazi tofauti.” “Nisingekuwa ni mimi! Wapo wengi tu huko nje, wenye wazazi tofauti. Lakini Net huyu ndiye aliyezaliwa na Ritha aliyekufunga, Tunda. Sina jinsi yakubadili hilo.” Tunda alilia sana, hakujua ajibu nini. Net akajisuuza, nakutoka.

 ~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~

Alikaa pale bafuni, mwishowe akaamua kuoga tu. Akaoga na kutoka. Alimkuta Net alishavaa. “Itabidi leo tukatafute nguo zako tukitoka hospitalini.” Tunda hakujibu. Alichukua lotion yake akakaa kitandani nakuanza kujipaka taratibu, kimya kimya.

Net alifunga laptop yake akamfuata pale kitandani. “Lete nikusaidie miguuni.” Tunda akanyamaza bila hata kumuangalia. Net akavuta ile chupa ya lotion, akajiwekea mkononi, akaanza kumsugua taratibu miguuni. Kuanzia mapajani mpaka kwenye nyayo. Akamuona anajilaza kwenye mto.

Akamfanyia hivyo kwa muda, akibadili mguu mmoja kwenda mwingine. Akamuona ametulia kabisa, mpaka akahisi analala. Akaona amshitue. “Ni saa nne Tunda. Jikaze twende. Utakuja kulala ukirudi.” Akajitoa pale kitandani, akavaa gauni jingine alilokuwa ameletewa na mama Penny. Lilimuingia bila shida, Net akamsaidia kufunga nyuma, baada yakumbusu mgongoni. Tunda alilisikia lile busu mwili mzima. Akafunga macho na kuvuta pumzi taratibu na kuzishusha.

Net & Tunda hospitalini. Wajua na jinsia ya mtoto.

N

et alishauri waende wakatafute daktari atakayewapa matibabu ya haraka. Hawakwenda mbali sana na pale hotelini walipokuwa. Wakaanzia TMJ hospitali tena. Wakasogea mapokezi, wakamuuliza muhudumu waliyemkuta pale na kumwambia, wanataka kuonana na daktari wa kawaida tu kwanza. Yeyote, hawachagui. Kwa kuwa watu hawakuwa wengi sana na walitaka daktari yeyote, wakaambiwa haitachukua muda mrefu. Net akaandikisha jina la Tunda, wakati Tunda amesimama pembeni yake.

Walipomaliza wakaelekezwa kwenye chumba kidogo ambacho waliambiwa  Tunda atafanyiwa vipimo vya awali kabla ya kuingia kwa daktari. Maelekezo hayo alikuwa akipewa Net. Akamgeukia Tunda nakumshika mkono. “Twende.” Wakaongozana mpaka hapo kwenye hicho chumba. Kwa kuwa hawakumkuta mtu nje, wakaingia moja kwa moja, wakamkuta nesi hapo ndani.

Wakamsalimia, baada ya maswali machache tu, akaanza vipimo. Alipimwa kwanza uzito, akaja pressure na kuangalia sukari yake. “Vipi?” Net akamsogelea nesi aliyekuwa akimpima Tunda. “Sio mbaya sana. Umekula?” Akamuuliza Tunda. “Nimekula.” Tunda akajibu kwa upole. “Umekula nini?” “Ndizi za kupikwa.” “Umekunywa chai?” “Hapana. Kwani vipi?” Tunda akauliza. “Sukari ipo chini. Lakini usiwe na wasiwasi. Jitahidi kula vitu vya sukari au niseme kula vizuri. Hata uzito wako upo chini kwa mimba ya miezi hiyo sita karibu saba kama ulivyoniambia! Sio uzito mzuri. Kwani unatapika?” Yule nesi akamuuliza tena.

“Sasa hivi sitapiki sana. Ni mara chache sana kama harufu ikinikera au kuna vyakula nimegundua nikila ndio natapika.” “Umeanza kliniki?” “Bado.” Tunda akajibu, akamuona yule nesi ameshangaa kidogo. Hakutaka kumpa maelezo mengi. Akanyamaza. “Muhimu kuanza. Na ukifika kwa daktari atawashauri zaidi.” Tunda akashusha mikono ya gauni lake vizuri, akatulia. “Mnaweza kwenda kumsubiria zamu yenu hapo nje, nesi mwingine ataita jina lako.” “Asante.” Tunda na Net wakashukuru kwa pamoja nakutoka.

“Ungependa nikuletee Fanta Orange? Itakusaidia.” “Nitashukuru.” Net akatoka. Tunda akabaki amejiinamia akifikiria. Wakati ameinama akasikia wanawake waliokuwa wamekaa kiti cha nyuma pembeni yake wakimteta. “Ni yeye.” “Hapana bwana. Wanasema Tunda mwenyewe yupo jela.” Tunda alihamisha mawazo kwao. Kutoka kwenye kile alichokuwa akikifikiria, akarudisha mawazo kwao, akabaki ameinama akiwasikiliza.

“Mzungu waliyesema kamuacha si ndie huyu aliyetoka hapa sasa hivi au siye!?” “Sijui shoga! Nilivyosikia, alimkimbia. Ila sasa tujiulize mimi na wewe. Mimba hiyo kaipataje na yeye alikuwa jela!? Hata kama umalaya jamani, umalaya huo umezidi! Mpaka maafande?” Wakacheka taratibu.

“Mjini kuishi kwa akili. Unawapa watakacho na wao wanakupunguzia adhabu.” Wakacheka. “Kwa hiyo kwenye kupunguziwa adhabu ndio huko?” Mwenzie akamuuliza akicheka. “Kumbe! Ndio na mimba tena! Unatoka na mtoto wa afande.” “Tatu mwehu wewe!” “Mjini shule!” Tunda alibaki kimya akiwasikiliza.

“Mzungu wake anarudi. Huyo! Inama kama hutujamuona.” Net akawapita, na kwenda upande wa pili, kiti cha mbele alichokuwa amekaa Tunda. “Nimepata ya baridi.” “Asante. Itanifaa.” Net akakaa nakuanza kumpapasa mgongoni. Tunda akamwangalia baada ya kunywa pafu la kwanza. Macho yakagongana.

“Vipi?” “Asante.” Tunda akashukuru. Ni kweli alimaanisha shukurani yake kutokea moyoni. Angeficha wapi uso wake angetoka na tumbo lisilo na baba? Inamaana kile alichokisikia pale ndio ingekuwa maneno mengine tena ya mtaani.

“Asante hii ni ya soda?” Net akamuuliza kwa kumnong’oneza. “Kwa kunipenda.” Net mwenyewe hakutegemea. Alibaki akimtizama. Tunda akajifuta machozi, akaina. Net akambusu begani. Akamuegemea begani na kumbusu tena. Wakabaki kimya.

“Tunda Cote.” Akasikia jina lake likitajwa hivyo. Akamgeukia Net kama anamshangaa kidogo. Yeye ndiye aliyemuandikisha hilo jina. Akamsaidia kusimama akiwa amembebea pochi yake na ile soda. “Twende.” Wakaongozana mlango waliosika jina lake likitajwa.

Walimkuta daktari amekaa, Net akamvutia kiti cha mbele ya meza hiyo ya daktari. Tunda akakaa. Net alimueleza yule daktari mambo mengi akitaka Tunda apimwe kila kitu na kama inawezekana wajue jinsia  ya mtoto. Aliwaandikia vipimo huku akiwaelekeza sehemu wanayoweza kufanyiwa ultrasound bila kuweka appointment.

Tunda alifanyiwa vipimo vingi, karibu kila kitu kwenye mwili wake. Walizunguka huku na kule, akatolewa damu na kupeleka mkojo wakatoka kusubiria. Baada ya lisaa wakasikia tena wakiitwa kurudi kwa daktari. Wakaambiwa hakukuwa na tatizo lolote, ila tu upungufu wa damu na uzito upo chini sana. Wakaandikiwa dawa, wakatoka kwenda sehemu ya kununua dawa. Net akatoa kile kikaratasi cha dawa, wakakaa nje wakisubiria.

Mama Penny akampigia Net. Wakasalimiana. “Ndio tupo hapa hospitalini. Wamempima karibia kila kitu, hamna ugonjwa wowote ila upungufu wa damu tu.” “Afadhali. Na mimi nimetoka kukutana na mama anayeuza virutubisho vya GNL, ninamzigo wenu hapa. Mkitoka hapo mpitie mchukue. Anatakiwa aanze leo, wala si kesho.” “Sawa. Lakini tuna kituo kimoja kabla ya kuja kwako.” “Sawa.” Wakaagana, na kukata simu.

“Mama Penny huyo!” “Nimemsikia. Ananipenda huyo mama, zaidi ninavyostahili.” Tunda aliongea huku akifikicha mikono yake taratibu. “Unabahati yakupendwa Tunda.” Tunda akamtizama na kuinama akiendelea kufikiria. “Lakini lazima tumlipe. Itakuwa imemgharimu.” Tunda hakujibu akabaki kimya. Walichukua dawa, wakatoka pale wakielekea Moroco, kwenye sehemu waliyoelekezwa ya Ultrasaound.

Jinsia ya mtoto wao.

W

alifika tena pale, Net ndiye aliyeandikisha na kulipia. Haikuwa hospitali au sehemu kubwa. Ila garama aliyosikia wakimtajia Net, ilikuwa juu. Tunda alitulia kimya. Wala mawazo hayakuwa kwenye jinsia ya huyo mtoto. Binafsi hakujali. Alijiambia atakayekuja ndio huyo huyo.

Akashtuliwa na mikono ya Net tumboni kwake. Akamwangalia akakuta na yeye akimwangalia. “Njaa inauma?” “Naona ile soda imenisaidia, japo natamani kula.” “Unataka kula nini?” “Nikikwambia utamwambia mama Penny, halafu ataanza kunisema.” Wakacheka.

“Basi ngoja nikisie.” “Huwezi kupatia.” Net akakunja uso huku akifikiria. “Mkate?” “Mikate ipo mingi. Wa aina gani?” “Acha kunipoteza Tunda. Kwanza niambie nimepatia?” Tunda akacheka. “Maliza jibu.” “Okay. Mkate mkavu kabisa.” “Haiwezekani Net!” Net akacheka sana.

“Usifanye mchezo na mimi.” “Hapana bwana! Au nilikwambia?” “Wakati hutaki kuniongelesha?” “Sio kwamba sitaki, ila sijui niseme nini Net!” “Niambie kuwa umenichagua mimi dhidi ya hofu inayo kukabili. Hilo ndilo natamani kusikia Tunda.” Tunda akabaki kimya.

“Najua unaogopa, na mimi sijui jinsi ya kukutuliza Tunda, kwa kuwa sijui ni nini kinatukabili mbeleni. Ila najua mimi na wewe tutakuwa sawa, mke wangu.” Ile kuitwa mke wangu ilimfariji sana Tunda.

“Huku unakotaka kujificha, wala hutakuwa salama bila mimi. Utamkimbia mama yangu, utakutana na mtu mwingine. Utafanyaje?” Tunda akavuta pumzi. “Tupange kuwa pamoja na kupambana pamoja. Sio kutengana. Ninauhakika hutaki watoto wetu wakue na mzazi mmoja. Sio kitu kizuri. Tutatesa watoto sana.” “Hata mimi nitateseka kuwa mbali na wewe Net.” Net akajisikia vizuri sana.

Akamsogelea karibu na kuanza kumbusu. Kwa Tunda ilikuwa kitu cha ajabu, lakini sio Net. Alimbusu na kumbusu palepale walipokuwa wamekaa mbele ya watu.

“Basi tusitengane. Nahitajika kazini Tunda. Hapa ninapokwambia mambo mengi nakwamisha sababu ya kuwa hapa.” “Pole Net, na ninakushukuru. Najua ingekuwa ngumu bila wewe.” “Na mimi najua. Na ndio maana nipo hapa. Nimemsihi nana anivumilie.”

          “Basi nenda mpaka visa yangu itoke. Usisubirie hapa. Mama Penny yupo na mimi.” Net akainama kama anayefikiria. “Naomba uwe na amani, Net. Kukitokea tatizo lolote, unajua mama Penny nilazima atakupigia.” Wakacheka.

“Kweli Tunda? Unauhakika niwaache?” “Kabisa Net. Tafadhali fanya lile unaloweza kufanya kwa sasa. Hata mwanao atajua dad anamajukumu. Japo atamiss hiyo sauti yako.” Net akarudisha mikono yake tumboni.

“Najisikia uzito!” “Najua. Na ninakuelewa mpenzi wangu. Lakini huku hupotezi. Jua tunakusubiri, na tukipata tu Visa, tutakufuata. Hata mimi naona shida kuishi bila wewe. Naisubiria hiyo Visa kwa hamu sana.” Net akaanza kumbusu tena, mkono tumboni.

“Tunda Cote.” Wakasikia wakiitwa.  Wakasimama kwa haraka. Safari hii wakiwa wanacheka sio kimya kimya. Wakaingia ndani na kuelezwa kitu chakufanya na dada waliyemkuta pale kama muuguzi. Tunda akafuata maelekezo na kupanda kitandani, ndipo mama wa kiasia akaingia. Alikuwa mchangamfu sana. Akamtania kidogo Net, akakaa.

“Ni mtoto wenu wa kwanza?” “Ndiyo.” Wote wakajibu. “Mnataka mtoto gani?”  Akawauliza huku akicheka. “Wakiume.” Net akajibu yeye wa kwanza tena kwa haraka. Tunda akacheka. “Mimi yeyote. Sijali.” Tunda akajibu.

“Yeyote awe wa pili. Lakini wa kwanza awe wakiume, Tunda.” “Wewe shauri yako kujiwekea mipaka. Utakosa raha bure akiwa wakike.” “Hata kidogo. Tena huyo atakuwa kipenzi cha dad. Japo akianza kaka yake sio mbaya.” Yule mama alikuwa akiwasikiliza huku akicheka.

Aliwasimulia stori ya mtoto wake wa kwanza na wa pili, huku akimpaka jelly Tunda, tumboni. Akaanza kumtizama mtoto. Net akasimama.

“Mnamuona anavyocheza?” Yule mama akawauliza. “Atakuwa amesikia hiyo baridi ndio maana ameamka. Dad yake alimbembeleza, akalala tukiwa TMJ.” “Basi ameamka. Tena ananyonya kidole.” Wakacheka huku wakimwangalia mtoto wao.

“Atakuwa na njaa ya mkate mkavu na chai ya rangi.” “Ngoja tumpigie mama Penny.” “Nimekwambia mtoto, Net! Sio mimi.” Wakaendelea kucheka.

“Nani amesema anataka wakike nani wakiume?” Yule mama akawauliza. “Mimi nimesema yeyote, dad amesema anataka wakiume.” Wakamuona anacheka.

“Basi dad ameshinda.” Net aliruka akishangilia. “Subiri kwanza Net. Unauhakika wa asilimia ngapi?” Tunda akauliza. “Asilimia 97” Akajibu kwa uhakika na kuzidi kumfurahisha Net.

“Mungu wangu ni wa ajabu! Usifanye mchezo.” Net akajisifia, Tunda akaguna. “Mnajina lake tayari?” “Nakwambia kabla mimba haijatungwa, alishapewa jina kamili huyu mtoto.” Tunda akajibu. Wakacheka.

Walipotoka tu, Net akampigia simu bibi yake na Maya. Alikuwa na furaha, aliongea na bibi yake karibu njia nzima, akifurahia. Wakampongeza Tunda na kumuuliza lini anakwenda. “Nataka huyo mtoto azaliwe kwenye hospitali aliyozaliwa babu yake na baba yake.” Bibi Cote alisikika. “Ndio ukazane kuomba Mungu ili Visa itoke mapema.” Net aliingilia, Tunda akacheka tu.

“Hakuna jinsi yakulipia ili iwahi kutoka?” Akauliza bibi Cote. “Labda uende ofisi za uhamiaji ukawaombe, uwaambie ni muhimu Tunda awepo hapo mwezi huu.” Net alikuwa akimchokoza tu bibi yake, lakini bibi yake akachukua hilo wazo.

“Kesho nitakwenda.” “Nana! Nakutania bwana.” “Unajuaje kama haitasaidia kuharakisha visa yao?” Net na Tunda wakaangaliana. “Kweli utakwenda Nana!?” “Oooh yeah! Why not? Nitamwambia Logan apige simu ubalozini sasa hivi. Ili aulizie kama nahitaji kuweka appointment kwao au ofisi za uhamiaji.” Hata bibi Cote alisikika amehamasika. “Asante Nana! That’s why I love you so much.” “I know son. Talk to you tomorrow.” Wakakata, Net akapiga yowe. 

“Tunaondoka wote Tunda.” “Unajuaje?” “Namfahamu Nana. Akikusudia jambo! Nakwambia kesho watakupigia simu ukachukue visa. Huwa hajui jibu la ‘hapana’. Na akisema atafanya kitu, ujue atafanya tu. Subiri uone.” Tunda akacheka na kubaki akifikiria.

“Tunda huyu anaenda kuzaa kwa wazungu!!” Tunda hakuwa akiamini. Akacheka. “Unacheka nini?” “Siamini!” Net akajua na yeye amehamasika. 

Tonight, we gonna make love alllll night!” Tunda alicheka sana kumsikia Net akisema watafanya mapenzi usiku kuchwa. “Net! Kwa nini sasa!?” “Kumsherehekea Cote.” Tunda aliendelea kucheka.

Siku hiyo ilijaa furaha kwa Net, alikuwa hawezi kutulia. Kila mtu aliambiwa Cote atazaliwa. Walikwenda kula. Wakaenda kununua nguo za Tunda, ndipo wakaenda kwa mama Penny.

          Alishampigia simu mama Penny na kumpa taarifa za ujio wa Cote. Tunda alikuwa akicheka tu. Walikaa hapo nyumbani kwa mama Penny wakiongea na kucheka mpaka usiku wa saa mbili, wakaondoka na virutubisho vya Tunda. Wakarudi hotelini.

~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~

Ulikuwa usiku uliojaa furaha kwa Net, Tunda alibaki akimwangalia tu. Kwake si kumpata tu mtoto wa kiume, bali hata kwa Tunda kukubali kwenda naye. Tunda hakuwa akielewa umuhimu wake. Ni kwa nini anamng’ania kwa kiasi kile! Kwa lipi? Tunda alijifikiria na kujiangalia mara kadhaa na kushindwa kuelewa.

Kwa uzuri aliokuwa nao Net, uwezo wa kifedha anaojua kwa sehemu anao, angeweza kuoa mtu yeyote yule, hata mtu wa kwao, akapumzika. Kwa nini yeye? Tunda aliendelea kuwaza huku akimtizama Net.

Ukweli hakujua kucheza nyimbo za kiswahili japo alielewa maneno, kwa hiyo alimfanya Tunda acheke katika kila mziki wa nyimbo za kiswahili aliokuwa akicheza. Alicheza vibaya bila hata kufuata mlio wa mziki. Ilikuwa fujo lakini ilimradi alicheza.

“Sasa furaha hiyo ni ya Cote au ni nini Net?” “Nimepata uhakika wa kustaafu mapema.” Akaendelea kucheza, Tunda akakunja uso. “Bwana tulia unieleweshe?” Net akambusu, na kukaa pembeni yake.

“Nilikwambia nina biashara ambayo familia tunarisishana. Kutoka kwa mababu na mababu. Sasa imefika kwangu, ndio mimi.” “Kwani angezaliwa wa kike si angeendeleza tu?” “Si kwa jina la Cote. Akiwa wakiume, jina litabakia la Cote, daima.” “Net!?” Tunda akamshangaa mumewe.

“Wewe sasa hivi si unaitwa Tunda Cote?” “Kwani lazima kubadilisha? Si angeweza kubakia kuitwa Cote tu!?” “Sisi tumekuzwa traditional. Huku mnasema kama watu wa zamani. Bado kuna mambo tunashikilia na kuyaamini, japo yanaonekana yamepitwa na wakati.” Tunda akabaki akimshangaa.

“Basi kazi ipo!” “Usiogope. Ni mambo ya kawaida sana. Utayaelewa na kuyazoea tu.” Net akambusu. “Mimi naenda kuoga nilale Net. Upunguze fujo.” Tunda akasimama, Net akacheka.

“Sasa na lile ombi langu?” “Lipi tena Net?” Net akasimama nakumfuata pale alipokuwa akivua nguo, akaanza kumpandisha kigauni alichovaa taratibu huku akimbusu mgongoni.

“Net! Mimi na tumbo hili mapenzi ya usiku kuchwa siyawezi bwana! Umeambiwa na daktari nipumzike.” “Basi twende wote kuoga. Unipe ‘agaist the wall’, kidogo tu, tumfurahie mtoto.”  “Wakati hapo ushaanza kunichokoza!” Net alicheka sana.

Akamgeuza taratibu akaanza kumbusu midomo yake taratibu. Alishakuwa amemtoa gauni lake, mikono ikitembea kwenye mwili wa Tunda. Alishuka mpaka kifuani huku akimbusu shingoni na masikioni. “Asante.” Tunda alimsikia akinong’ona masikioni. “Asante ya kuamua kuwa na mimi daima.” Tunda akacheka. Akahisi mikono ya Net kiunoni akimpapasa juu chini, juu chini taratibu huku akimbusu.

Akashuka kifuani kwenye matiti. Tunda alianza kuchezesha miguu. Mikono ya Net ilitua sehemu ambayo Tunda mwenyewe alijilaza pale sakafuni. Net akavuta mto, akamuwekea chini ya kichwa. Alimchezea mpaka aliporidhika kuwa anaweza kuingia bila kumuumiza mkewe. Alimnyanyua miguu, hata hakutumia muda mrefu pale chini, Tunda akamaliza.

Image result for sex position for pregnant women

Net alimwongoza bafuni, akamgeuza ukutani, akapata ‘against the wall’. Staili aliyoipenda sana kuitumia wawapo bafuni. Aliweza kuitumia hiyo staili akiifurahia yeye mwenyewe huku akimchezea Tunda mwili wake vilivyo, atakapo.

          Mikono yake ilikuwa huru kupita mbele kwenye matiti, uke wake, na alifika kwenye hips zake pia. Alicheza na huo mwili, akihakikisha akili za Tunda zinabaki naye pale bafuni na yeye. Mara kadhaa alimbusu katikati ya mgongo ili kumsisimua zaidi. Na kwa kuwa Tunda alikuwa akisimama tu, hakuwa akichoka kwa haraka, kwa hiyo Net alikuwa akitumia muda wake atakavyo, mpaka afanikishe kwa wote.

Walitoka hapo bafuni, akamsaidia kumkausha, wakajikuta wote wanataka tena. Ila hawakuliongelea hilo. Wakati amekaa kwenye kochi wote wakiwa wametulia, Tunda akilipaka tumbo lake mafuta maalumu kupunguza kupasuka au alama za michirizi inayosababishwa na kupanuka kwa tumbo hilo kwa ujauzito, akaanza kujutia kumwambia Net anataka kuwahi kulala. Ni kama usingizi ulipaa kwa mchezo wa bafuni.

Alijisugua taratibu kuzunguka tumbo zima. Pembeni, chini, juu, taratibu tu huku akifikiria. Akamuona Net amepiga magoti mbele yake, akiwa ametoa taulo alilokuwa amejifunga tokea bafuni. Tunda akacheka taratibu. Alijua kinachofuata. Ni mtindo alioupenda sana Tunda. Kwani hakuwa akitumia nguvu yeyote ila kufurahia tu. Net alipenda kumfanyia hivyo zaidi alipotoka kifungoni. Ili tu kumfurahisha mkewe akiwa hatumii nguvu yeyote.

Akamvuta kiuno mbele taratibu huku akinyonya ulimi wake kwa kuufurahia bila papara akiwa yeye Net amepiga magoti mbele yake, katikati ya mapaja ya Tunda. Atakapoinama hapo Net, hatatoka mpaka mkewe awe ameridhika. Atampa ‘non penetration’ mpaka afike kileleni akiwa amejilaza nyuma, ameegemea kochi akimpa uhuru wote Net. Na yeye alijua mikono ipite wapi na midomo ili tu kumfurahisha mkewe. 

Na alipomfanikishia tu hapo akamfikisha kileleni, akamtaka kwa ‘Edge of the coach’. Akamnyanyua nakumvuta kabisa mbele mwisho wa kochi, hapo napo Net akaingia taratibu huku mikono ipo mwilini kwa Tunda. Zaidi kwenye matiti. Akaendelea mpaka na yeye akamaliza hiyo safari. Hilo nalo likamfurahisha hapo kwenye kochi, kwa kuwa hakutumia nguvu nyingi ila kufurahia akiwa ametulia Net ndiye alishugulika.
third-trimester-pregnant-sex-positions-edge-of-bed

“Mara ya mwisho Net.” Net alicheka sana. “Nilijua umechoka!” “Acha bwana!” Akamtoa hapo kwenye kochi akamuweka kitandani. “Hata mimi sijaridhika. Tupate ‘Spoon au kijiko’.”  “Ila uninyonye maziwa mpaka niridhike.” Net akamlaza kama ubavu huku kifua amekiweka chali mbele yake. Akajinyanyua na kuanza kunyonya matiti yake taratibu kisha akaingia. Miguu yao ikiwa imepishana chini. 

Taratibu huku Tunda akinung’unika taratibu na vidole vya Net vikiongeza ladha ya tendo zima kwa kutekenya kinembe chake. Tunda hakuchukua muda, akakamilisha hiyo safari, ndipo akamuinamisha ili kupata, ‘rear entry.’ Hapo Net alikuwa akiingia taratibu akiwa amemuinamisha mkewe, amemshikilia kwa upendo. Aliingia na kutoka kwa hisia zote, taratibu kuhakikisha hamuumizi ili asimtoe kwenye furaha aliyompatia muda mfupi uliopita.

Ulikuwa usiku wa namna yake kwa wote wawili. Hawakukesha, lakini walilala wote wakiwa wameridhika. Furaha ndiyo iliyowapoteza kwenye ulimwingu huu na kuwapeleka kwenye ulimwengu wa usingizi.

Viza ya Tunda

I

lishakuwa saa 9 za mchana nchini Canada, wakati simu ya Net ikiita nchini Tanzania saa moja asubuhi. Net akashtuka kutoka usingizini, akaimbilia pale alipokuwa ameiacha mezani ili asimuamshe Tunda. Ile shtuka ya pale kitandani, hata kabla hajafikia hiyo simu yenyewe, Tunda alishituka akakaa.

“Net bwana! Tulisema tuwe tunazima simu.” “Pole, pole.” Net alinong’ona. “Sasa unanong’ona nini wakati umeshaniamsha!?” Net akacheka na kupokea. Namba ilikuwa ngeni kwake.  “Nethaniel Cote!” Akaanza Net. “Tunataka kuzungumza na Tunda.” Ilisikika sauti ya mwanamke aliyezungumza kwa lugha ya kigeni. Net aliweza kugundua lafudhi ya nyumbani kwao. Akacheka huku akimsogelea Tunda. “Just a minute.” Akajibu Net.

“Ongea nao Tunda.” “Mimi!?” Tunda akashangaa kwa woga. “Itakuwa ubalozi wa Canada. Ongea, usiogope.” Tunda akachukua simu. “Tunda Cote.” Tunda alianza hivyo kama Net na kumfurahisha sana Net. “See!” “Shhhh!” Tunda akamnyamazisha Net huku akicheka.

Alisikia wakimuuliza Tunda maswali kadhaa, naye akijibu akisikika ametulia. Mwishowe akaambiwa akachukue Visa. Tunda hakuamini. Akashukuru na kukata simu. “Mungu wangu Net! Wamenipa Viza.” “Huyo ni Nana tu! Nilijua tu atafuatilia.” Net alifurahi sana.

Akachukua simu kutoka kwa Tunda, na kumpigia simu bibi yake bila kupoteza muda. Akapokea huku akicheka. “Nilijua tu utanipigia.” “Asante Nana. You are the best!” “Sijasikia Net. Umesemaje?” Net akaanza kucheka. “Usinifanye nirudie bwana! Najua umenisikia.” Wakataniana na bibi yake hapo.

“Sasa juhudi zangu zote, ni Tunda afike huku mapema. Aonane na daktari wa wakina mama. Tufanye vipimo vya uhakika.” “Tunataka twende honeymoon kwanza, Nana!” “Hapana Net. Hospitalini kwanza. Wakiona kila kitu kipo sawa, mtakuwa huru kwenda popote.” Bibi Cote akaweka msisitizo.

 “Tunda na mtoto walikuwa kifungoni kwa miezi sita! Hatujui kwa hakika mtoto ana hali gani. Hatuwezi kuzembea halafu tuje kusema, ‘tungejua’. Sitakubali uzembe wowote utokee, Net. Lazima kujiridhisha kuwa Tunda yupo salama na anauwezo wa kumbeba huyo mtoto mpaka mwisho, na Cote mwenyewe azaliwe salama.” Kwa ile furaha ya kuondoka na mkewe, Net alikubali kila kitu.

Tunda naye akapata nafasi ya kushukuru. Akamuuliza maswali waliyomuuliza watu wa ubalozi, Tunda akawa anamwambia maswali na vile alivyojibu. “Lakini maswali mengine nilikuwa sina majibu yake, niliwajibu sifahamu.” “Swali gani?” Akauliza bibi Cote.

“Kama mji ambao nategemea kuishi. Sikuwa na jibu.” Akamsikia akicheka. “Nilishawaambia utakuwa hufahamu mambo mengi, lakini niliwaambia Net atakuwa na wewe safarini.” Wakazungumza tena kidogo. Tena kwa urahisi tu, bibi yule akimuhakikishia hata asingewajibu chochote zaidi ya kutaja jina lake pia wangempa hiyo Viza. Wakacheka kidogo na kuagana.

Tunda akabaki akijiuliza familia hiyo ni familia gani inayoweza kuamuru mambo kama hayo na kutokea! “Huyu Net ni nani haswa!? Anatoka kwenye ukoo wa namna gani!?” Tunda akajiuliza. Safari hii akimtizama Net kwa jicho la pili.

Ni jana yake tu Net ndipo alipomwambia bibi yake labda aende ubalozini. Tena kwa utani. Kesho yake anapigiwa simu na kufanyiwa usahili na ubalozi wa Canada akiwa kitandani kwake! “Mmmh!” Tunda akaguna mawazoni.

~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~

Net ndiye aliyekuwa na hati ya kusafiria ya Tunda. Walitoka hapo. Wakaenda kulipia na kupeleka hiyo hati kwenye ofisi za ubalozi wa Canada, wakaambiwa wafuate baada ya siku mbili. Wakaacha hapo hiyo hati, wao wakaondoka. Hapo hapo Tunda akampigia simu mama Penny nakumuelezea kila kitu.

Gafla hofu wote iliwaisha, ikawa ni furaha tupu. “Tutakuja kuwaaga vizuri nyumbani. Acha nikuage kwa sasa, ili nimpigie simu baba, nimuage.” “Utakuwa umefanya vizuri. Kwani mnaondoka lini?” Mama Penny akauliza. “Sijui Net. Lakini bibi yake ametaka iwe mapema, ili nikaonane na daktari wa wakina mama.” “Nakwambia umeukata Tunda! Unaenda kuzalia uzunguni!” Tunda alicheka sana.

“Mimi mwenyewe siamini dada yangu! Hilo swali nilishajiuliza. Kama utani!” “Hongera mdogo wangu. Hongera sana.” “Ninafuraha yakupita kiasi mama Penny.” “Nakusikia.” “Tutaongea zaidi baadaye. Acha nimtafute baba. Natamani aje huku anione kabla sijaondoka.” “Muombe.” “Eti eeh?” Tunda akaona ni wazo zuri.

“Kabisa. Baba yako ni mtu mzuri sana Tunda. Ni hivyo nahofia kusafiri kwako, ningekushauri umfuate huko alipo ukamuage. Upo dhaifu sana kwa kusafiri safari ya Kigoma. Ni muhimu muonane kabla hamjaondoka. Mwambie ungetamani kwenda lakini daktari amekushauri mapumziko, unamuomba yeye ndio aje?” Mama penny akampa hilo wazo. “Nashukuru. Basi ngoja nimpigie.” Wakaagana.

“Nataka kumpigia simu baba.” Akamgeukia Net. “Nimesikia. Mwambia tutamtumia tiketi ya ndege ili aje huku muagane.” “Kwani ulitaka tuondoke lini?” “Kwa kuwa tumeshapata uhakika wa Viza, naomba tusisubiri Tunda. Tuondoke tu niwahi kazini kidogo. Niweke mambo sawa wakati daktari akishugulikia mambo yako na mtoto, kisha ndipo twende mapumzikoni.” “Ndio lini sasa?”

“Tukipata hiyo Visa asubuhi, tuondoke na ndege ya usiku wake. Nitawapigia simu, niwaambie watukatie tiketi yakuondoka hapa usiku ili kusiwe na kuchelewa ndege.” Tunda akakunja uso. “Nani Tena?” “Yupo mtu ofisini ambaye anashugulikia safari zetu. Usiwe na wasiwasi. Wewe jua kesho kutwa tunaondoka.” Tunda akatulia kidogo akifikiria hili na lile juu ya maisha hayo mapya anayokaribia kuanza kuyaishi. Kidogo akawa kama haamini kama ni yeye.

~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~

Akaamua kumpigia simu baba yake. Iliita mara moja tu, akapokea. “Ni mimi baba.” “Hospitalini wamekwambiaje?” “Kila kitu kipo sawa. Nimejua jinsia ya mtoto wangu.” “Wetu Tunda! Mbona hivyo?” Net akaingilia. Akamsikia baba yake akicheka.

Net akampokonya simu, “Mtoto ni wakiume. Anaitwa Cote Junior Cote au CJ Cote the 4th. Shikamoo.” Akarudisha simu kwa Tunda. “Nakwambia Net amefurahi huyo! Kila saa anacheka.” “Namsikia! Naona na majina yote kwa kirefu na kifupi pia anayo huyo mtoto!” Baba yake akajibu. Tunda akacheka na kuongeza. “Alikuwa nayo hayo majina hata kabla mimba yake haijatungwa!”

“Hongereni sana. Nawaombea mtoto akue vizuri na wewe uwe na afya njema.” “Asante baba. Lakini tunaondoka. Tunaenda kuishi na Net. Canada.”  Kimya. “Baba!” Tunda akaangalia simu yake. “Nipo mama. Nakusikiliza.” “Nilitaka tuonane kabla sijaondoka. Angalau nikuone. Net amesema atakukatia tiketi ya ndege uje hata kesho, maana tunaweza kuondoka kesho kutwa usiku.” “Napanda ndege mama!?” Tunda akacheka.

“Nitafurahi kukuona kabla sijaondoka baba.” “Sawa. Tena kwa ndege ndio itakuwa rahisi. Nitawahi kuja kuwaona kabla hamjaondoka.” Wakazungumza wakipeana mipango ya hapa na pale, wakaagana.

~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~

“Mbona sasa ni kama umekosa raha?” “Sio mimi. Baba anaonekana kukosa raha. Hakufurahia kusikia ninataka kuondoka.” “Nisikilize Tunda. Watu wote wanaokuzunguka bado wanakumbuka kilichokupata, hasa akiwa aliyesababisha ni mama yangu mimi.”

“Kitendo chakuondoka hapa nchini, mama akiwa hajulikani alipo, kila mtu anakuhofia ni kama unaenda kuyafuata matatizo.” Tunda akainama akifikiria. “Natamani kukuahidi mambo mengi ili tu kukufariji, lakini naomba unipe nafasi nyingine. Sitaki kukwambia mengi, lakini naomba uniamini hata mimi nimeongeza umakini. Sijui kinachotukabili mbeleni, ila naamini kile alichoniambia hata bibi yangu na kile ninachojisikia. Maisha yangu hapa duniani, nitayafurahia nikiwa na wewe.” Tunda akamwangalia.

“Naomba wewe utulize mawazo. Tupokee siku moja hadi nyingine kwa shukurani bila hofu ili tusiishi maisha yasiyo na maana. Naamini tukishikamana, kila kitu kitakwenda vizuri. Sawa?” Tunda akatingisha kichwa kukubali.

“Naomba unijibu Tunda.” “Sawa.” “Mbona huongezi neno?” “Kwa kuwa naogopa Net! Sijui ni nini kitanikabili huko ugenini! Nimekubali kukufuata, kwa kuwa tu najua siwezi kuwa na furaha mbali na wewe.”Tunda akajiweka sawa kuweka msisitizo.

“Tafadhali usije kusahau hilo. Nakufuata wewe. Usije ukafika huko, ukapata watoto, ukanisahau mimi.” “Siwezi Tunda. Sitaki watoto bila wewe.” “Basi naomba hilo usije ukalisahau tafadhali. Nikumbuke kila wakati na kwa kila utakalofanya. Jua Tunda yupo na wewe kwa kuwa nakuhitaji wewe. Naomba nikose kila kitu, ila niwe na wewe. Siku nitakayokukosa, ujue ndio umenimaliza Net.” “Mungu atanisaidia Tunda. Nakuahidi siwezi kukuacha.” Tunda akavuta pumzi kwa nguvu, nakujiweka sawa pale kitini akageukia dirishani.

Gafla ile furaha waliyokuwa wameamka nayo asubuhi, ikapotea kwa simu moja tu aliyozungumza na baba yake. Na yeye akamtia hofu kama ya mama Penny na mumewe. Akabaki akiwaza lakini alishaamua atayavulia maji nguo.

Baada ya ya miaka Mingi, Tunda & Baba yake Uraiani .

Yohana alimuacha binti yake hospitalini akiwa mgonjwa, akafungwa. Tunda akamuacha baba yake akiwa mgonjwa gerezani, akisubiri atoke, na yeye akafungwa.

Baada ya miaka mingi tokea wawe pamoja uraini. Tena wakikutanishwa na matatizo tu. Sasa hivi wote wakiwa huru, hatimaye maisha yanawapa fulsa nyingine ya kukutana, lakini kwa ajili ya kuagana tena. Siku inayofuata baada ya kuzungumza na baba yake kwenye simu, nakupanga hiyo safari, Net alimsindikiza mkewe uwanja wa ndege kumpokea baba yake.

Walikuwa wamemchukulia chumba palepale hotelini. Yule mzee alishtuka sana kumuona Tunda. “Unakula kweli!?” Akamuuliza Tunda. “Hapa nina nafuu baba. Muulize Net. Nilitoka nikiwa nimechoka zaidi ya hivi.” “Mmmh! Umebaki tumbo tu! Huyo mtoto utambebaje kwa hali hiyo!?” “Najitahidi kula, baba. Pole na safari.” “Asante. Nimepanda ndege, wala sijachoka.” Tunda akacheka. Net naye akasogea akamsalimia.

“Mbona mzigo ni wa samaki tu?” “Sina kingine.” “Si utakuwa huku mpaka niondoke?” “Ndiyo.” Tunda hakuwa ameelewa, lakini akaona hilo alinyamazie. “Twende kwenye gari. Umekula?” “Hapana.” Baba yake akamjibu huku akimwangalia kama ambaye haridhishwi kabisa na afya ya mwanae. “Nitakuwa sawa baba. Usiwe na wasiwasi. Huu mwili utarudi tu. Ndio nimetoka jela hata mwezi sijamaliza!”

“Na huo ndio wasiwasi wangu. Unakwenda ugenini huko, unaanza vyakula vyakigeni. Hujui kama utapenda au la! Mwili wenyewe hamna! Mpaka uzoee, unatakiwa ujifungue. Utaweza kweli?” Tunda kimya huku wakielekea kwenye gari.

Gafla wakamuona anakimbilia pembeni nakuanza kutapika. Net akamsogelea. “Vipi?” Alitapika mpaka akakaa chini. “Vipi!?” Baba yake naye akamuuliza. “Nahisi ni hao samaki. Harufu imenichefua.” Wote wakaangalia lile boksi lililofungwa vizuri la samaki.

“Unataka tuwatupe?” Baba yake akamuuliza. “Tumpelekee mama Penny. Atafurahi sana. Kwanza anakupikia chakula. Anataka nikupitishe kwake ukale kwanza.” Tunda alimaliza kuongea vile huku akijaribu kusimama. Net akamsaidia.

“Pole. Bado tu kutapika?” “Sio kila siku na kuna harufu na harufu huwa zinanikera. Naomba nyinyi mtangulie na gari mimi nitawafuata na taksii.” Net akatoa macho. “Kweli Net. Nitatapika njia nzima. Naomba niwafuate kwa nyuma. Mkifika mwambie mama Penny awafungie kwenye friji mpaka nitakapoondoka.”

“Siwezi kukuacha hapa Tunda!” “Huniachi Net! Nawafuata na taksii. Wewe mpeleke baba.” Tunda akageuza palepale akielekea sehemu zilipo taksii, akawaacha Net na baba yake wakishangaa.

 ~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~

“Hili wazo lakumchukua Tunda akiwa na hali hii, linatoka kwake au kwako?” Lilikuwa swali la kwanza alilolirusha baba yake Tunda mara baada yakuingia kwenye gari. Net alitulia kidogo akifikiria jibu sahihi kwa huyo mzee kijana. Alikuwa mkimya kama mwanae Tunda. Na walifanana, hapakuwa na swali.

Net alisafisha koo mara kadhaa, akajiweka sawa huku akiendelea kutafuta njia yakumtoa kwenye sehemu zakuegeshea magari pale uwanja wa ndege. Walisogea mpaka sehemu yakulipia, akalipia bila kujibu swali.

Waliona taksii iliyombeba Tunda mbele yao. Net akamtizama baba yake Tunda baada yakupokea risiti ya pesa aliyolipia yakuegeshea gari pale uwanja wa ndege. Akavuta pumzi mara kadhaa huku akifikiria.

“Tunda ni mke wangu.” Alianza kujieleza Net. “Maisha yangu yapo Canada. Siwezi kumuacha hapa yeye na mtoto. Lazima niwe naye karibu.” “Unajua mama yako alipo?” Swali lililofuata lilimfanya Net abaki kimya nakushindwa kujibu. Hapakuwa na maongezi yeyote humo ndani ya gari lao. Net akanyamaza, na baba yake Tunda akanyamaza.

Walipofika mataa ya Buguruni kutokea Tazara, yule mzee akamgeukia Net. “Watu wanajua ipo jela. Lakini hawajui kinachoendelea humo ndani. Hata kama wakijua, ni kwa kusimuliwa, lakini sio kuishi. Aliyeishi gerezani ana habari tofauti na aliyeishi mahabusu. Huwa havilingani.” Akaendelea taratibu tu.

“Ni maisha ambayo kama una roho ya kawaida kama Mungu alivyokusudia kwa mwanadamu yeyote awe na aina hiyo ya roho ya kibinadamu, basi, usingependa mtu yeyote yule aishi huko. Na wengi wakitoka humo, huwa hawatamani kuja kurudi tena gerezani.” Akamaliza baba yake Tunda, na yeye akanyamaza.

Walifika kwa mama Penny, akawaambia Tunda yupo chooni akitapika. Bila kujibu, Net akaelekea kwa haraka ilikokuwa ikitokea sauti ya kutapika kwa Tunda huko chooni. Baba yake alikwenda kukaa sebuleni bila hata salamu ya kueleweka. Maana sauti ya Tunda ilisikika nyumba nzima.

Baada ya muda yeye na Net wakatoka chooni. “Wakati nyinyi mnakula, naona mimi nikajilaze hapo kwenye kitanda cha Penny. Nasikia mbavu zinauma!” “Utataka kula nini ukimka?”  Mama Penny akamuuliza. “Labda uji. Chakula kabisa, naona hakitapita.” “Basi uji ukiiva, nitakuja kukuamsha.” Mama Penny akarudi jikoni.

“Baba, nakwenda kupumzika kidogo. Nikiamka, tutapata muda wa kuzungumza kidogo.” “Sawa.” Baba yake akajibu, kisha akabaki kimya bila yakuongeza neno. Net akamsindikiza chumbani.

“Pole.” Tunda akacheka. “Muone sura yake. Umepooza!” “Nilikuwa sijawahi kukuona unavyopata shida!” Tunda akacheka huku akijiweka sawa pale kitandani kwa Penny. “Acha nilale kidogo.” “Pole.” Net akarudia tena. Tunda akajua ameingiwa hofu.

“Nitakuwa sawa tu. Wewe nenda kale.” “Nataka kukaa hapa na wewe.” “We Net! Acha woga bwana! Nenda kale. Mimi nipo sawa.” “Unauhakika?” “Kabisa. Mimi nitakuja huko sebuleni muda si mrefu.” Akambusu nakutoka.

Baada ya kama lisaa, Tunda akaamka. Alimkuta Net amekaa pembeni ya kitanda ameinamia simu yake. “Net!” “Unajisikiaje?” “Njaa. Sasa hivi natamani kunywa uji.” “Mama Penny alishapika, ila nilimuomba akuache upumzike kidogo.” “Afadhali. Baba yuko wapi?” “Yupo hapo sebuleni. Twende.” Wakatoka.

“Vipi?” “Sasa hivi nasikia njaa. Umekula?” “Mama Penny ametulisha hapa, nasinzia kwa shibe.” Akacheka na kwenda kukaa pembeni ya baba yake. “Jitahidi kula.” “Nikipata kitu ninachokipenda, huwa nakula sana tu. Hata leo asubuhi nilikula vizuri.” Baba yake akabaki kimya. “Nitakuwa sawa baba.” Alimwangalia akanyamaza.

“Vipi biashara?” Tunda akaendelea kumuhoji taratibu. “Mwanzo mgumu. Ndio mara ya kwanza naanza biashara. Kuna kukosea kwingi, lakini naamini baada ya muda mambo yatakaa sawa. Nitakuwa mzoefu. Halafu pia ndio kama naanza maisha. Kwa hiyo bado.” “Utafanikiwa baba.” “Naamini hivyo.” Tunda na baba yake walikuwa wakizungumza taratibu  wakiwa wamekaa peke yao hapo sebuleni.

Net akatoka jikoni na bakuli la uji. “Huu uji unanukia vizuri, itabidi tubebe. Asante mama Penny.” “Afadhali kama umeupenda. Nakuja sasa hivi, nawaandalia kina Penny chakula, ili wakitoka shule, wale.” Tunda akaanza kucheka.

“Unacheka nini?” Mama Penny akamuuliza akiwa jikoni. “Penny wangu anaendeleaje? Ameacha maneno?” Akamsikia mama Penny akicheka, kisha akawafuata pale sebuleni.

“Kafanya nini tena!?” Tunda aliuliza huku akiendelea kucheka. Alimjua Penny kwa vituko. “Mbona alitukomesha!” “Nini tena?” Tunda akauliza huku akinywa uji. “Siku ile ya jumapili mlimuacha hapa kalala, akaamshwa jioni, akaoga akarudi kukaa palepale. Kimya. Basi sisi tukamshukuru Mungu, somo limeeleweka. Sasa shuguli ilitupata usiku. Hatukulala.” “Kwa nini tena?” “Ndoto!” Tunda na Net wakaanza kucheka.

“Jamani Penny alilia yule mtoto! Mbona nyumba nzima tuliamka! Eti anaota watu wanamla nyama, wengine wanamnyonya damu. Haya, mimi na baba yake tukamuhamishia chumbani kwetu, ikaanza kazi yakubembeleza.” Mama Penny akaguna.

“Na kubembelezwa huko ni amepakatwa na baba yake. Anamlilia baba yake anamwambia yeye alifikiri anampenda, lakini kumbe anataka kwenda kumtoa sadaka! Hapo analia kwelikweli! Anamwambia eti ingekuwa yeye asingemtoa baba yake sadaka.” Walizidi kucheka, mpaka Tunda akaweka bakuli la uji chini.

“Basi, ndio ikabidi baba yake amwambie ukweli kuwa tulikuwa tunamuogopesha tu, hata iweje, hawezi kumgawa. Mtoto alifurahi huyo!” Wakazidi kucheka. “Karudia hali yake ileile! Tena sasa hivi usemi wake ni baba yake amemwambia anampenda sana, hata iweje, hamtoi sadaka. Na dad wake anampenda kwa kuwa anaongea ukweli. Anamtangazia kila mtu eti hata umpe dad wake mamilioni ya pesa za kimarekani, hakuuzii Penny wake.” Tunda na Net walizidi kucheka.

“Basi imekuwa shida! Huna utakalomwambia akanyamaza. Anakuja sasa hivi. Utapata habari za tokea anatoka hapo getini asubuhi mpaka anarudi hapa.” Mama Penny akarudi jikoni akawaacha wakicheka.  

~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~

Wakiwa njiani Tunda akamgeukia baba yake. “Tumekuchukulia chumba pale tunapoishi kwa sasa.” “Asante.” “Sasa utavaa nini?” Akatulia. “Ulisahau nguo?” Tunda akauliza tena. “Nilipotoka jela, nilikuta mama Chale amegawa na kuuza nguo zangu zote na viatu. Nikajinunulia baadhi tu, ambazo zimegeuka za kazi huko nilipo. Kwa kuwa sina pakwenda isipokuwa kazini tu. Zisingefaa kuja nazo huku.” Alijibu huyo mzee taratibu tu.

          “Basi twende tupitie madukani ununue.” “Twende mpaka huko hotelini, nitawaacha mimi nitoke nikajinunulie.” “Kwa nini? Nataka muda na wewe baba.” Tunda alimgeukia baba yake. “Naona umedhoofu sana. Unahitaji kupumzika, Tunda.” “Mimi nipo sawa baba. Twende tu. Nitapumzika usiku.” Wakatoka hapo na kuelekea madukani.

Baada ya kupata nguo zake, na Tunda kuridhika, ndipo wakarudi hotelini. Ilishakuwa jioni, kila mmoja wao alisema ameshiba, ila Tunda alisema atakunywa uji wake akisikia njaa tena. Kwa hiyo hawakuona sababu ya kwenda kula tena kwa kuwa Tunda alikuwa na chakula chake, ikawa inatosha.

Baba yake alipoingia chumbani kwake na Tunda pamoja na Net wakaingia chumbani kwao. Tunda alioga kwa haraka bila Net, akamwambia anataka kwenda kuzungumza na baba yake kabla hajalala. Net akaridhia.

Alifika kwenye chumba alichokuwepo baba yake, akagonga. Baba yake akafungua akionekana na yeye ameoga na kuvaa t-shert moja wapo aliyomnunulia Tunda.  Nyeupe. Tunda akacheka wakati anaingia. “Umependeza.” “Nakushukuru.” Tunda akaenda kukaa.

“Biashara yako na wewe inaendaje?”  Akamuuliza Tunda. “Mama aliichukua.” Baba yake akakunja uso. “Kivipi tena!?” “Kabla ya kwenda jela, nilimtambulisha kwenye ile biashara. Nikamwambia kwa sababu alifukuzwa kazi, anaweza kuwa akiifanya ile biashara ya kupamba. Basi nikaanza kwenda naye kazini, lakini sikufanya naye muda mrefu ndio nikakamatwa nikiwa nimemuonyesha ofisi na kumtambulisha pale kama mama yangu. Kwa hiyo nilipofungwa, yeye ndio akawa mmiliki badala yangu.”

“Mama Penny anasema alibadili jina la kampuni yangu ikawa kwa jina lake. Akatafuta mpangaji pale kwenye ofisi yangu nilipokodisha, nasikia walimlipa pesa, akahamisha ofisi. Sijamsikia kwa muda wote nilipokuwa jela, na mpaka nimetoka. Anavyo vyombo vyote na mapambo yote.” Baba yake akainama.

“Ndio maana umeamua kuondoka hapa nchini?” Baada ya muda baba yake akauliza. “Sio kwa sababu hiyo baba. Tokea mwanzo nilitaka kumuachia kwa kuwa tulipanga baada ya kufunga ndoa mimi na Net, niondoke naye, tukaishi pamoja Canada.”

“Wala huna haja yakumtetea mama yako. Namfahamu vizuri sana zaidi ya unavyomfahamu wewe. Linapokuja swala la pesa, huwa hana undugu.” “Simtetei baba. Nakumbuka hata wewe nilikwambia wakati ule kuwa nitaondoka na Net. Labda umesahau kwa kuwa ni kipindi kile ulipokuwa mgonjwa kule gerezani.” “Nakumbuka sana tu.” Baba yake akajibu.

“Nampenda Net, baba. Hakuna mtu ataweza kunipenda, kuniheshimu na kunijali kama Net, baba yangu. Kwa sifa zote mbaya nilizonazo, bado ananing’ang’ania!” Baba yake akamtizama.

“Halafu kumbuka makuzi yangu. Nimekuwa kwa kutangatanga. Mara leo niishi kwako. Kesho nihamishiwe kwa mama! Na kote mambo hayakuniendea vizuri mpaka kuishia jela. Sitaki mtoto wangu aje awe mtu wa kutanga tanga. Nimejiambia japokuwa naogopa kwenda, lakini kwa ajili ya mwanangu, heri niitumie hii nafasi yakuwa na baba yake. Mtoto wangu apate familia yakueleweka, kitu nilichokosa mimi.” Tunda akaendelea kujitetea kwa baba yake, taratibu tu. Baba yake kimya akimsikiliza.

“Hata hivyo kwa sasa sina jinsi baba. Nina mtoto wake. Mimi sina kazi wala uwezo wakulea huyu mtoto, namtegemea yeye ambaye ana kazi huko Canada.” “Na mama yake?” Baba yake akamuuliza.

“Ni wapi nitakapoishi nitakuwa salama, baba? Nilikuwa hapa nchini, nyumbani kwetu, na bado yule mama alinikamata na kuniweka jela. Wapi najificha nitakapokuwa salama? Ni aidha nijifiche niishi kwa shida, au nikaishi na Net kwa furaha hata kama itakuwa ya muda mfupi.”

“Umezingatia afya yako lakini? Kwa nini usisubiri mpaka ujifungue, upate nguvu, ndipo mfuate? Itakuaje ufike huko halafu mazingira yakawa mabaya? Ukakutana na watu watakao kunyanyasa?”

“Net hawezi kuruhusu mtu aninyanyase na yeye akiwepo. Halafu kama nikiona mambo sio mazuri, nitarudi baba. Sidhani kama watakuwa wakinifungia. Tutakuwa tukiwasiliana. Ukiona kimya hata kwa siku tatu tu, naomba uchukue hatua.” “Labda hivyo. Nakuhofia Tunda!”

“Naomba katika hili uniunge mkono baba yangu. Namuhitaji Net sasa hivi kuliko       zamani. Nahisi nitachanganyikiwa akiondoka na kuniacha hapa. Ananipenda na kunithamaini jinsi nilivyo.” Baba yake akavuta pumzi kwa nguvu na kujivuta nyuma, akaegemea kochi. 

“Utakuja kuniona?” Baba yake akacheka. “Ndege yenyewe ndio nimepanda leo!” Tunda akacheka. “Hata passport sina!” “Naomba uanze kushugulikia baba. Siwezi kuwa huko ugenini peke yangu wakati wote.”

“Kwani hurudi tena?” “Sidhani kama itakuwa kwa haraka. Kumbuka nitakuwa na mtoto. Net hawezi kukubali nianze kumzungusha mtoto huku na kule akiwa mdogo. Nilikuwa nikimsikia akimwambia mchungaji kurudi huku ni mpaka angalau mtoto akifikisha miaka 3 ndio tunaweza kurudi kutembea kama hapatakuwa na dharula.” Baba yake akatulia.

“Mbona hujibu baba?” “Huko mbali Tunda. Mambo yangu hayajakaa vizuri. Nimekuwa kama nina mkosi, sijui! Ile pesa niliyolipwa, ni kama imepotea yote.” Tunda akashtuka sana, akamgeukia vizuri baba yake.

“Kuna mtu aliniambia tufanye naye biashara hiyo ya dagaa. Akaniambia itatulipa kama tukifanya sisi wenyewe. Yaani tusimamie sisi wenyewe. Ikiwezekana twende hata sisi wenyewe ziwani. Akashauri tununue ngalawa ya kisasa na vifaa vingi vya uvuvi, tena vya kisasa. Sasa nikamwamini kwa kuwa ni mtu wa nyumbani, tumekua pamoja kabisa. Halafu yeye ni kama alikuwa anauzoefu wa hiyo biashara. Kwa kuwa alishafanya hiyo biashara zamani. Au niseme alikuwa na hiyo biashara zamani akakwama. Nilipomuuliza kwa nini aliacha, akasema kilichomkwamisha ni pesa, mtaji ulikuwa mdogo, hakuwa na mtaji mzuri.” Baba yake akajicheka.

“Ikawaje?” Tunda akauliza. “Ndio nikampa pesa yote aliyotaka ili akanunue hivyo vifaa ili tuanze hiyo biashara. Baada ya siku tatu akarudi akaniambia ametapeliwa pesa yote. Labda nimpe pesa nyingine. Akaniapia safari hiyo atakuwa mwangalifu. Na ujue mwanzoni nilikuwa nimempa pesa nyingi tu. Basi, kwa kumuamini nikampa tena pesa yote niliyokuwa nimebakiwa nayo.”

“Mbaya zaidi, nilimkabidhi bila kuandikishana wala shahidi. Kwa hiyo akawa anayo pesa yangu yote. Akaondoka. Kukawa kimya. Baada ya mwezi na siku kadhaa, naambiwa na watu ameanza au amerudia biashara ileile, ila safari hii kwa hali ya juu.”

“Hivi hapa tunavyozungumza, ameshaanza kuleta dagaa mpaka huku Dar. Kwa kifupi, amefanikiwa vizuri sana kwa pesa yangu yote.” Tunda aliumia sana. Akajichukia kuona anafanana na baba yake mpaka tabia za kuamini watu hovyo.

“Pole baba.” “Nahisi nina udhaifu ambao natakiwa kuufanyia kazi. Na kazini ilikuwa hivyo hivyo. Nimeamini watu mpaka wakanitia matatizoni. Isingekuwa wewe, mpaka sasa hivi ningekuwa jela kwa kosa lakusingiziwa.”

“Hapa nimeanza biashara ingine kwa kuuza kwa hasara gari aliyokuwa amenipa Net. Nilijaribu kuifanya taksii kulekule Kigoma, nikaona sipati faida, inakuwa inanifilisi tu.” Tunda hakutaka kuendeleza yale mazungumzo. Nitakuachia pesa ya kushugulikia hati ya kusafiria baba. Naomba utengeneze hati, uwe nayo tu. Siku nikikuhitaji uje, kusiwe na vipingamizi.” Kimya.

“Au hutaki kuja kuona mjukuu?” Baba yake akacheka. “Wewe ndiye mtoto wa pekee niliyenaye kwa sasa. Ukinihitaji nitakuja. Kwanza ni Canada, halafu napanda ndege!” Wakaanza kucheka. “Uzazi mzuri.” Tunda alizidi kucheka.

“Nani alijua mtoto wa ujanani angenifaa hivi!” Tunda alimwangalia nakuzidi kucheka. “Baba!” “Kweli mama. Unanipa tumaini, ni vile hujui tu. Huko nimewaaga kwa kishindo kweli! Maana wananiona mchovu mchovu. Kama nisiye na maana. Sasa nikawaambia mwanangu Tunda ananiita Dar, tena nakwenda kwa ndege.” Tunda alizidi kucheka.

“Sasa subiri safari ya Canada.” “Baba jamani!” Wakazidi kucheka. “Tena binti yangu kaolewa na mzungu! Ni hivyo sina picha.” “Hii simu nakuachia baba yangu. Net anasema huko hizi simu huwa hazifanyi kazi sijui, au sitahitaji. Kwa hiyo hii moja mpya nakuachia wewe.”

“Niliinunua siku chache kabla sijakamatwa, na hii ya zamani namwachia mama Penny. Sijui atafanyaje nayo mwenyewe. Ila namwachia.” “Si unaona mambo hayo! Sasa uniachie na picha humo humo ndani.” Tunda alizidi kucheka.

“Uzazi mzuri!” “Hongera baba yangu.” “Na unipe hongera kweli! Maana ni wewe tu ndio tumefanana. Wale wengine wamechukua kwa mama yao. Kwa hiyo nimeponea kwa mtoto wa ujanani.” Tunda alikuwa akimwangalia baba yake huku akicheka.

“Ila ujitahidi Tunda. Mwili umeisha huo. Kazana kula na kupumzika.” “Nitafanya hivyo. Nitakuwa sawa baba, usiwe na wasiwasi.” “Wenyeji wako wanajua kama unakwenda?” “Wanafuraha hao! Mpaka wananishangaza. Wanamsubiria mtoto kwa hamu! Yule bibi kabla ya kulala, anapiga simu, anauliza habari za mtoto. Kama amecheza, kama baba yake amezungumza naye. Haya mara aombe Net aweke simu tumboni amsalimie. Yaani ni fujo ambazo mimi sijawahi ona.” Hapo baba yake akapata faraja.

“Mdogo wake Net, anaitwa Maya, ndio anasema ameshaanza kununua nguo. Naye kutwa ananipigia kutaka kujua ninaendeleaje. Hivi tulikuwa tumepanga na Net twende tukamalizie fungate ndio twende Canada, lakini bibi yake ameomba twende kwanza tukaangaliwe afya. Mimi na mtoto. Daktari akiona nipo sawa, ndio twende kokote ninakotaka.” Baba yake akacheka kwa furaha, akaonekana ameridhika.

“Utamuaga mama yako?” “Hapana. Nimeamua kumuacha kabisa. Hajawahi kunipenda na wala sidhani kama anampango wakuja kunipenda. Sijamtafuta tena.” Tunda akafikiria kidogo.

“Unajua hata hivyo ni mimi ndiye niliyemtafuta kumuomba msamaha, ndipo nikamkuta kwenye matatizo? Wala hakuniomba msaada, mimi mwenyewe ndiye niliyemtoa pale yeye na watoto. Nilimkuta kwenye hali mbaya sana. Mtoto wake mdogo wa kike alikuwa akibakwa na baba yake, akawa amemuambukiza gonorea. Alikuwa akiumwa, mama yake hana pesa, wanafungiwa tu, wakati mama anaenda kukopa pesa mtaani.”

“Ndio nikawahamishia hotelini kwa muda mpaka walipopata sehemu yakuishi huko Kurasini. Nilichofanya nikumlipia kodi, na kumpa vitu vyangu vya ndani ili aanze maisha, nakumtafutia mwanasheria.”

“Sikumbuki hata kukaa chini na mimi kuzungumza. Ila alichoniambia au kuniuliza mara ya kwanza kuniona ni kutaka kujua kama mumewe alikuwa akinibaka kama mwanae yule mdogo. Sikutaka kumjibu kwa haraka kwa kuwa niliona ni kama anayo majibu mbele yake.” “Ungemjibu tu ili ajue.” Tunda akavuta pumzi kwa nguvu.

“Alishambaka msichana wa kazi karibu kumuua, baba. Mtoto wake ndio aliambukizwa mpaka gonjwa la zinaa! Na Tom ananiambia pia alikuwa na mahusiano na msichana mwingine wa kazi ambaye mama yake alimfukuza. Sasa kwangu alitegemea ilikuaje?”

“Kama angetaka kuniamini, ataniamini tu, kama ni mtu ambaye hana imani na mimi, hata ningemwambia nini, asingeniamini. Hata hivyo nilimkuta yupo kama amechanganyikiwa. Alikuwa kama mwehu kwa matatizo.”

“Nisikilize Tunda. Huwezi kuanza jambo ukaishia katikati. Kabla yakuondoka, lazima uhakikishe unakaa naye chini, unamueleza upande wako wa stori.” “Baba!” Tunda akashangaa kwa kusikitika sana. Hakutaka kumtafuta tena mama yake. “Kabisa. Na mimi nitakupeleka. Aamini, asiamini, hiyo iwe juu yake mwenyewe. Lakini lazima kuhakikisha anasikia kutoka kwako.”

“Upande wa ndugu zake wote wanajua wewe ndio ulikuwa mbaya, wakati wao wawili au tuseme sisi ndio tuliyaharibu maisha yako. Mpigie simu usiku huuhuu, mwambie kesho asubuhi unahitaji kwenda kuzungumza naye.” Tunda aliumia sana. Hakutaka kuonana na mama yake tena.

“Atazidi kuniumiza tu baba. Mama amehakikisha kwa maneno na vitendo, naelewa kuwa hanipendi na wala hanitaki kwenye maisha yake. Sikutaka kuonana naye tena au hata kuzungumza naye akazidi kuniumiza.”

“Unafikiri mimi simfahamu Mandi? Namjua vizuri kuliko unavyomfahamu wewe. Hukuchagua uzaliwe na sisi. Imetokea. Mandi ni mama yako hata ufanye nini. Lazima umalize ulichoanza, ndipo utakuwa na amani. Huna haja yakumwambia utakapokuwepo au utakapokuwa ukiishi.” “Kwanza hata sijui kama anashida yakutaka kujua.” Tunda aliongea kwa hasira.

“Basi mpigie. Mwambie kesho asubuhi unataka kuzungumza naye. Utamfuata popote alipo.” Tunda akajifuta machozi huku akijifikiria jinsi hata yakuzungumza na mama yake!

Tunda na Mama yake!

T

unda akachukua moja ya simu yake, akampigia mama yake. Ikaita mara kadhaa, ikakatwa. Walifanya hivyo mara tatu. “Hapokei!” “Anayo namba yako?” “Hii hapa anayo. Ndio nilikuwa nikiitumia sana zamani.” “Basi anakuonea haya kwa aliyokufanyia, na hataki kukupa vitu vyako. Kamuite Net.” Tunda akasimama, nakutoka.

Baada ya muda akarudi na Net. “Nataka kabla hamjaondoka, Tunda aachane na mama yake kwa amani. Aliniambia alikwenda kumuomba msamaha, lakini hamkukuta mazingira mazuri.” “Lakini ni kama ameshajua ukweli wote. Mtoto wake mdogo amepitishwa alikopita Tunda.” Net akajibu.

“Hivyo ndivyo unavyofikiria wewe, ukidhani na yeye angetakiwa kujua hivyo, lakini hatujui kwenye moyo wake. Mama yake hajasikia ukweli kutoka kwa Tunda mwenyewe. Unajuaje labda anadhani kuwa Tunda ndiye aliyemwanzishia hiyo tabia. Akapenda mahusiano na watoto wadogo?” Hapo wote wakanyamaza.

“Kila mtu anaufahamu wake. Na inategemea ni vipi mtu anamwamini mtu mwingine. Unayempenda ndiye utamuwazia vizuri. Sasa ninachoomba ni umpigie simu mama yake, umwamb...” “Sasa asipopokea kama alivyofanya kwangu?” Tunda akamkatisha baba yake. “Amtumie ujumbe, mwambie mnaondoka hapa nchini, mnataka kwenda kumuaga kesho asubuhi. Namjua Mandi. Atawapigia yeye mwenyewe. Tena sasa hivi.” Hapo wakakubaliana.

Net akampigia mara ya kwanza na ya pili. Simu zake yeye hazikukatwa, ila ziliita tu mpaka mwisho. Ndipo Tunda akatuma ujumbe kama alivyoambiwa na baba yake. ‘Shikamoo mama. Mimi ni Tunda. Nilitaka kuja kukuaga wewe na kina Tom. Nilitoka gerezani, tunahamia kuishi Canada kwa kina Net.’ Tunda akamuonyesha baba yake ule ujumbe, baba yake akaridhia, ndipo akautuma.

Mama Tom Amtapikia vilivyo Tunda.

Wakabaki wakisubiria. Wote kimya wakimwangalia baba yake Tunda aliyesema atapiga. Zilipita dakika 6 tu, mama yake akapiga kwenye simu ya Tunda mwenyewe wala sio Net. “Tom alikuwa akichezea simu yangu. Yeye ndio alikuwa anakata hizo simu zenu. Hujambo?” Tunda akamtizama baba yake, akamuona anacheka huku akitingisha kichwa.

“Sijambo. Naweza kuja kukuaga kesho?” “Nitafurahi sana. Tena Tom anashida na simu. Ndio vizuri ukija umuachie hiyo simu yako. Kama ukumbusho. Si unakumbuka alivyokuwa anaipenda?” Tunda aliumia sana.

“Nimeshampa baba.” “Si baba yako umpe ile nyingine? Yeye mtu mzima bwana, anaweza kujitafutia simu yake mwenyewe.” “lle nyingine yenye namba ya Tigo, ilipotea, najua ile nyingine Tom hataipenda, nitaiacha kwa mama Penny.” Tunda akajaribu kujieleza taratibu.

“Sasa kwa nini hiyo usimpe baba yako halafu hii ndio umpe Tom?! Vijana ndio wana mambo mengi au matumizi mengi na simu kuliko wazee. Mbali na kupiga na kupokea, hamna matumizi mengine.” Net na baba yake pia walikuwa wakisikiliza. “Unafikiri kesho muda gani mzuri tunaweza kuja kukuona?”  Tunda akaona arudi kwenye alilompigia simu.

“Ningekuwa na gari, ningesema tuje kukuaga. Lakini hatuna gari. Si unakumbuka gari yangu walichukua ndugu wa baba Tom?” “Nakumbuka. Pole.” “Ndio hivyo. Lakini naona tupo vizuri kwenye kesi yangu. Nitashinda tu.” Tunda akabaki kimya.

“Au utuachie gari yako tutumie kwa muda mpaka nitakaporudishiwa gari yangu.” Tunda akachoka kabisa. “Namuachia baba. Atatusindikiza uwanja wa ndege, kisha atabaki nayo.” Hapo Tunda akawa ameamsha kilichopo ndani ya mama yake.

“Kwa hiyo kila kitu unamwachia baba yako, aliyeshindwa kukulea!?” Akaanza Manda. “Alikuacha ukipigwa na mkewe kama mbwa, mimi nikakuchukua nikakuleta nyumbani kwangu. Leo unashindwa kunipa chochote, unamwachia mpuuzi huyo gari, simu na kila kitu chako!?” Tunda alishindwa hata kujibu, alibaki akitokwa na machozi.

“Sasa hiyo kesho ulitaka kuniona ili iweje?” “Kukuaga na kupata muda wakukupa upande wangu wa stori juu ya baba Tom.” Tunda aliongea kwa shida. Hasira zilishampanda. Alibaki akitetemeka midomo. “Ulitaka kusema nini ambacho ni chatofauti? Sasa hivi amefungwa, na wala hatakaa akatoka jela kukanusha utakachokisema.” “Ungenisikiliza kwanza mama!” Tunda akazidi kuumia.

“Kuwa na wewe alikuwa akikubaka!? Na kwamba hata ile safari uliyokuwa umetoka kwa bibi yako ukasema unaenda kwa rafiki yako kumbe umejifungia hotelini na mume wangu, ukarudi nyumbani nikakutoa mimba, nayo alikubaka kule Arusha ulikokuwa umemfuata?” Tunda kimya.

“Wewe ndiye uliyemzoesha michezo ya watoto. Ukamlemaza mume wangu, akaishia kutaka watoto tu. Umesababisha mateso kwa familia yangu. Umesababisha ulemavu kwa yule binti aliyekuwa msichana wangu wa kazi. Ukampa tatizo lakudumu mwanangu mdogo. Ukamuacha yeye akimtumikia baba yake, wakati wewe unaendelea na kina baba wengine.”

“Leo nakuomba msaada, mshenzi wewe, unaniambia unamwachia baba yako, mpuuzi huyo ambaye hakuna mwanadamu anaweza kuishi naye!” Manda alicharuka haswa, akapata jukwaa.

“Na Mungu ameshaanza kukulipa kwa ubaya uliotendea familia yangu. Hatakuacha Tunda. Na wewe atakutafutia msaidizi kwenye ndoa yako.” Simu ikakatwa.

~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~

Wanasema, ‘dua la kuku, halimpati mwewe’. Manda si mwewe kwa Tunda. Mama mzazi!

     Akiwa bado na hofu ya kuhamia nchini Canada, mama yake anaongeza jambo jingine. Shutuma nzito, zinazoendana na Ukweli. Na Laana juu! Tunda anaondokaje? Kweli ameanza kulipwa?

 

     Ritha amekimbia nchi. Hakuna ajuaye alipo. Vita yake imeisha? Tena Tunda akionekana kama bado amemshinda. Amemfukuzisha nchi, amechukua familia yake. Net na Maya wapo upande wa Tunda. Na sasa yupo huru. Mipango yakumfuata alipo kimbilia ndio imepamba moto. Viza ya kwenda nchini Canada, Tunda ameipata kiurahisiii! Nini hatima ya safari yake?

 

     Yepi mengine yanamkabili Tunda?

     Kama litatokea jambo jingine, je, safari hii Net ataweza kumlinda?

     Ipi hatima ya Tunda na mama yake?

     Nani aliyekuwa akivujisha picha, siri na mambo yaliyokuwa yakiendelea Tanzania upande wa familia hiyo ya Cote, Tunda & familia ya Gabriel, kwenye mitandao ya nchini Canada? Mwisho wake nini? Anamkomoa nani?

Usikose Muendelezo...

CONVERSATION

0 Comments:

Post a Comment