Naomi Simulizi |+1 205 767 8163 |naomisimulizi@gmail.com Nilipotea! – Sehemu ya 45. - Naomi Simulizi

Nilipotea! – Sehemu ya 45.

 Msako Unaendelea.

M

paka giza linaanza kuingia, hapakuwa na fununu yeyote ya nani aliyemteka nyara Tunda na wala wapi alipopelekwa mzazi huyo mwenye kidonda kibichi kabisa cha uzazi. Watu wa usalama wenye sare na wasio na sare walimwagwa kila mahali akitafutwa Tunda Cote. Redio kwa television zilitangaza utekwaji nyara wa Tunda, kina Cote wakiomba msaada kwa yeyote hata mwenye fununu tu, ajitokeze na ahadi ya pesa nyingi sana kama zawadi kwa atakayetoa habari za kweli.

Polisi walisubiria sebuleni kwa kina Cote simu ya mtekaji aombe pesa. Lakini mpaka ilipofika saa moja usiku, wakaamini haukuwa utekaji wa pesa. Itakuwa wivu au kisasi. Wengine walisema kama sio wao kina Cote wanahusika, basi muhusika anatafuta tu umaarufu wa kuweza kumteka Cote katikati ya ulinzi mkali.

Lakini watu wengi walimsema vibaya sana Net na mahusiano ya wizi aliyokuwa akiyaendeleza na Vic. Wakamshutumu kwa maneno mabaya sana kwa kusababisha ubaya kwa Tunda. Kuanzia anafuatwa na kutukanwa na Vic mbele ya ulinzi wao! Tena ndani ya nyumba yao! Na baadaye kudanganya ameibiwa akiwa na mlinzi ambaye hata hakujeruhiwa! Ni kama walikabidhiana tu. Shutuma kwa familia hiyo ziliendelea mpaka bibi Cote akaagiza hiyo nyumba izimwe kila tv na redio ili kumfanya aweze kufikiria.

~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~

     Ilipofika saa moja na nusu usiku huo, ndipo Net akakumbuka kesho yake usiku ilikuwa baba yake Tunda na familia ya mama Penny waondoke nchini Tanzania kuja nchini Canada kwa  harusi yao. Hakuwa hata amemwambia Tunda. Alitaka kumfanyia mkewe surprise ili tu kumfurahisha. Alipanga baba yake Tunda ndiye amtoe Tunda kanisani siku ya harusi yao ili tu kuwafurahisha watu hao wawili. Kwani Tunda alitamani tokea mwanzo baba yake angekuwepo hata kwenye ile harusi ya Tanzania, na baba yake vilevile, ila alikuwa jela.

     Net alishashugulikia mpaka Viza yao kama juma moja lililopita. Tiketi zilishakatwa kwa watu hao watano. Baba yake Tunda, mama Penny, Mchungaji mwenyewe, Penny cha maneno na Pendo. Gino alishaambiwa siku hiyo kungekuwa na wageni. Hata menu ya siku hiyo Gino alishaiandaa. Vyakula vya kitanzania kidogo na vigeni kwa wageni wao pia. 

Carter na Emily walishaandaa upande wa pili wa nyumba hiyo ambao hufikia wageni wao wakaribu sana. Hata kina Gabriel na Bethy walishakuwa wakifikia na kulala huko. Kukafanyiwa usafi maalumu kupokea wageni hao kutoka nchini Tanzania, tayari kwa harusi.

 ~~~~~~~~~~~~~~~~~~~

     “Oooh my goodness!” Net akashituka mpaka polisi waliokuwa nao pale ndani na bibi yake, wakamgeukia. Walikuwa polisi watatu pale sebuleni pamoja na mitambo yao iliyokuwa imeunganishwa tayari kupokea simu ya mtekaji, ili kufuatilia sehemu inapopigwa hiyo simu na pengine kutambua sauti ya mtekaji. Lakini mpaka muda huo hapakuwa na simu yeyote ile iliyoingia wala kutoka iliyowatia mashaka maafisa hao wa usalama. Simu zote zilizokuwa zikiingia na kutoka zilikuwa zikisikilizwa na hao maafisa. Na zote walijiridhisha ni zakawaida tu na za watu wakaribu kutoa pole. 

Kwani hata kina Cote wenyewe walikuwa wakichunguzwa na kufuatiliwa kwa kila kitu wanachokifanya. Bado vyombo vya usalama walisema hawana mtu au watu wanaowashuku. Kwa hiyo mpaka hapo, kila mmoja anapaswa kufuatiliwa kwa karibu na wakaombwa kutoa ushirikiano. Mbali na hao maafisa matatu hapo sebuleni waliokuwa na bibi Cote na Net, wengine walikuwa wakizunguka hiyo nyumba nje na ndani, kila sehemu mpaka vyumbani waliombwa waache milango wazi. Mtu asifunge mlango endapo anataka kuwa chumbani. Siku hiyo hakuna aliyefanya kazi. 

Bibi Cote hakumsemesha wala kumtizama machoni Net. Net akajua amekasirika kwa alilotenda. Akaamua kumuacha kwanza mpaka hasira zitulie na ile hekaheka ya polisi kuingia na kutoka pale nyumbani kwao ipungue. Maana simu na redio call zilikuwa zikipigwa mfululizo na afisa hao walikuwa wakipita huku na kule. Mara jikoni, wakati mwingine vyumbani. Yeyote anayenyanyuka kuelekea popote, alifuatwa. Hapakuwa na utulivu hata kidogo. 

Mtoto wa Net na Tunda, Cote, alishaletwa nyumbani tokea mchana wake, kwa ombi maalumu la bibi Cote. Akiangalia usalama wake. Cote alirudishwa nyumbani kwa makubaliano daktari kwenda tena kumuangalia hapo siku inayofuata. Japo mpaka anaruhusiwa hakuonekana na tatizo lolote, lakini aliruhusiwa na nesi maalumu wa watoto. Na Maya naye akawepo hapo kusaidia. 

          “Ni nini?” Mmoja wa polisi akamuuliza Net akijua amesoma kitu juu ya Tunda kwenye simu yake. Bibi yake alimtizama tu na kugeuka pembeni. “Niliwaalika familia ya Tunda. Kesho ndio walikuwa wanaondoka nchini kwao kuja huku kwa harusi. Itabidi.., Itabidi..” Net akaanza kufikiria. “Sitaweza kufikiria kama mama Penny atakuja na kukuta hii hali.” Net akasimama kabisa akiwaza. Kila alipomfikiria mama Penny! Aje akute Tunda ametekwa nyara! “Hapana.” Net akapinga kabisa. 

“Utabiri wake utakuwa umetimia.” Akaumia sana moyoni . Wakamuona amesogea mpaka dirishani, simu mkononi anawaza. “Mungu wangu nisaidie nimpate Tunda. Kama kuna muujiza ninao uhitaji mwaka huu au maishani, naomba hili liwe la pekee.” Net akaomba kwa uchungu, asijue anafanyaje. Hakuruhusiwa kwenda mbali na hapo. Na aliambiwa anafuatiliwa kwa karibu sana na polisi. Net alishakuwa mtuhumiwa wa kwanza. Mengi yalikuwa yakiendelea kwa Net kwa wakati huo. Mambo yalimgeukia kila mahali. 

Mtoto aliyekuwa akimsubiri kwa hamu, alifika kwake akiwa na shutuma kila mahali, akashindwa kumfurahia au hata kuwa karibu na mtoto wake. Hakuna aliyemwamini kuwa anauchungu wakupotelewa na mkewe hata kidogo. Wengi walisema ndiye mla njama, na hilo linalompata kwa wakati huo alishaliona tokea mwanzoni kabisa. Polisi kumfuatilia kwa muda, kisha watakubali kushindwa kwa kukosa ushahidi unaonyesha yeye anahusika moja kwa moja, watafunga kesi na maisha yake kuendelea kama kawaida. Hakuna aliyemuongelesha kwa heri. Bibi yake ndio kabisa. Alijawa uso wa umeniabisha na sikutegemea kutoka kwako. Hakumsemesha hata Maya na Carter. Alibaki kimya tu wasijue anawaza nini. 

Carter amemficha kama Vic alilala nyumbani kwake! Wamemsababishia aibu na kuonekana ni mama anayeshindwa kutawala nyumba yake. Halikuwa jambo dogo hata kidogo. Kwake imemuharibia sana. Kuwa yapo mambo yanaendelea nyumbani kwake, yeye hafahamu. Ni uzembe wa namna gani huo! Kwa hakika walimfunga mdomo huyo bibi. Alibaki ametulia kwenye kiti chake kimya. 

Akijitahidi sana ni kusimama kwenda msalani au kwenda chumba alicholazwa mtoto na kumwangalia. Basi. Anarudi hapo hapo kukaa. Net aliumia sana, lakini hakujua jinsi yakujitetea. Ni bora angemwambia akajua chakufanya mapema hata kabla hajamkaribisha Tunda mbele ya umati mkubwa kiasi kile. Pongezi nyingi alishapokea kutoka kwa watu wakubwa wa nchi mbali mbali. Wakimpongeza kwa kupata mkwe, Tunda, ambaye atampokea madara. Leo anashutuma za kuzuia penzi la kweli la mjukuu wake huyo aliyemnadi kwa nguvu sana! Vic amemshutumu vibaya sana na akatoa uthibitisho wa penzi zito alilofanya na huyo Net. 

Inamaana yeye bibi Cote anatetea haki za wanawake wengine huku akikandamiza wengine! Inamaana ipo hila ndani ya kile alichokuwa akikifanya na kukipigania miaka yote.Vic aliwapiga pabaya sana. Na safari hii na wao wakaonja maumivu ya Vic. Walimpuuza Maya miaka yote akiwaambia juu ya Vic, wakamuona yeye ni teja tu, sasa na wao wamefedheheshwa vibaya sana. 

Bibi huyo naye alichafuliwa vilivyo huko mitandaoni. Na yeye walimlaumu kusababisha kutekwa kwa Tunda. Wengine walisema kama asingekuwa yeye kumzuia Net kuwa na mwanamke anayempenda, yaani Vic, ambaye inamlazimu kumuingiza chumbani kwake kwa siri bibi huyo akiwa hayupo, inamaana mabaya mengi yasingetokea. Alisemwa vibaya sana na wakamkashifu vilivyo. 

~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~

     Kwa upande wa Vic, yeye alisimama na kuzungumza na vyombo vya habari bila shida. Alionekana ni jasiri kama simba. Hata polisi alionekana hakuhusika na kumteka nyara Tunda. Usiku huo ambao Tunda alikuwa hospitalini baada yakujifungua, hata kamera za nyumbani kwao kina Vic zilionyesha Vic alikuwa nyumbani kwao mpaka mida ile Tunda anatekwa nyara. Polisi walikwenda kuangalia. Ni kweli Vic alikuwepo nyumbani kwao. 

Usiku uliopita bibi Cote alipompigia simu mama yake Vic na kumwambia anampa masaa mawili, kabla masaa mawili hayajaisha kweli Vic na wazazi wake walishajisalimisha kituo cha polisi pamoja na mwanasheria wa familia ya kina Vic. Vic akajitetea vizuri tu. Aliwaambia polisi yeye alikwenda kuzungumza na Tunda kwa amani kabisa. Hakujificha. Hata walinzi wa Cote na Carter walikuwepo wakati akiingia nyumbani kwa Cote. Vic alisema yeye hakumgusa, wala kumtukana Tunda. Tunda alianguka yeye mwenyewe, mbele yake wakiwa wamekaa kiti cha mbali kabisa. 

Mwanasheria wa familia hiyo ya kina Vic, akawaambia mpaka hapo Vic sio mtuhumiwa. Yupo tayari kujibu chochote watakachomuuliza. Waliondoka usiku huo huo kurudi nyumbani bila shitaka lolote. Kwani Vic aliwathibitishia maafisa hao wa usalama kuwa, mahusinao yake na Net sio kificho kwa yeyote pale kwa kina Cote. Kila mtu analifahamu hilo. Hakwenda pale kwa kina Cote kama mgeni ila mpenzi wa Net na ndio maana hakuzuiliwa. 

Kulithibitisha hilo ndipo Vic akawaonyesha ule ushahidi wa ile video yake yeye na Net wakifanya mapenzi baada ya Net kuoa, akiwaambia Net alioa  kimakosa huko nchini Tanzania, ndoa yao haitambuliki kwa sheria ya kimataifa. Na kweli. Wale maafisa walipoangalia ile video kwa haraka, wawili hao kwenye video, hawakuonekana kama si wapenzi au kwamba Net ameshurutishwa. Alionekana akitoa ushirikiano mzuri tu kwa kile wanachokifanya. 

Na Vic hakuishia hapo. Akatumia ile video aliyochukua Renee kama ushahidi wake mwingine. Vic akabadilisha. Akawaambia alikwenda pale kwa kina Cote na Renee kama shahidi wake na yeye ndiye aliyemtuma Renee achukue ile video kama ushahidi kuwa hakuna baya atakalotenda kwa Tunda, ila alikwenda kumwambia ukweli. Hapakuwa na sababu ya kumshikilia Vic. Kwa shutuma ipi? Vic akaachiwa huru kabisa. 

Hata bibi Cote hakumfuatilia tena Vic, kwani alijua ni kama kuzuia mvua isiloweshe aridhi. Kumbe Vic huwa anaitwa kwa siri nyumbani kwake! Akaona anyamaze kabisa. Hata Logan alipompigia simu kumwambia kuwa Vic ameruhusiwa, hakujibu hilo. Alisisitiza wafanyakazi wake pia watolewe. Zaidi Carter na Ms Emily. Wakati huo anazungumza na Logan na kutoa amri hiyo, bado Tunda hakuwa ametekwa nyara. Alipotekwa nyara na polisi kwenda nyumbani kwa kina Vic, walimkuta Vic nyumbani kwao ametulia kimya. Walimtaka kituoni, bila kubisha, akapiga simu kwa mwanasheria wao akamweleza kila kitu, akamwambia watakutana kituo cha polisi. Aende nao tu hao polisi. 

Vic akasindikizwa tena kituoni na wazazi wake wote wawili. Na baadaye mwanasheria wao akaongezeka hapo kituoni kuongeza nguvu kwa Vic kisheria. Mpaka hapo Vic kama mpenzi wa Net, hakukutwa na hatia. 

~~~~~~~~~~~~~~~~~~~

Net akaamua asipige simu kwa mama Penny wala kwa baba yake Tunda, ila akawatumia ujumbe mfupi tu. 

Tarehe ya harusi imesogezwa mbele. Hapatakuwa na harusi tena jumamosi hii mpaka tutakapo wataarifu tena. Simu ya Tunda imesumbua, msione kimya. Lakini kila kitu kipo sawa, msiwe na wasiwasi. Nitawataarifu tena siku ya nyinyi kuja. Asante.

Nathaniel Cote.

     Akatuma huo ujumbe kwa mama Penny na baba yake Tunda. Inamaana hiyo safari imekufa kwa hao watu wa Tanzania ambao walikuwa wamebakisha masaa machache tu wapande ndege kwenda kushuhudia huo utajiri mkubwa walio simuliwa na Tunda. Kina Penny walishaaga kila mtu kuwa wanakwenda kwa wazungu na watahudhuria harusi ya kizungu. Mabegi yalishakuwa tayari muda mrefu tu. Wakijiandaa kukaa huko muda mrefu. Zaidi mama Penny ndiye aliyekuwa akisubiriwa kwa hamu kubwa na kila mtu, kwani Tunda alisema ndiye atakayemlea yeye na Cote. 

Kwa hiyo mazingira tulivu na ya kuwafaa mama Penny na familia yake yalishaandaliwa ili kuwafanya watulie pale nchini kumlea Cote na mama yake. Inamaana hata kazi yakupamba huko nchini hakuwa amechukua kwa kuwa alijua hatakuwepo nchini kwa muda mrefu. Tunda alishamuhakikishia kuwa watamlipa kwa kipindi hicho atakachokuwa akimsaidia uzazi. Asiwe na wasiwasi kabisa juu ya pesa. 

Leo safari inafutwa! Tena kwa ujumbe! Japokuwa Net aliwaambia wasiwe na wasiwasi, lakini wote walishaingiwa na wasiwasi. Mama Penny akajaribu kumpigia Tunda simu yake haikuwa hewani. Alipompigia Net, Net hakupokea ila alimrudishia ujumbe kumwambia kuna kitu anafanya kwa wakati huo, hayupo kwenye nafasi yakuzungumza. Atampigia wakati mwingine, lakini akasisitiza wasiwe na wasiwasi. 

Akawafungia kabisa simu zao zisiingie kwenye simu yake na Tunda. Na hakuishia hapo. Akaandikia ubalozi wa Canada usiku huohuo kuwa anafunga kwa muda ukaribisho wa kina mama Penny aliowatumia na kuwaombea Viza, mpaka atakapowataarifu tena. Kwa maana nyingine ni kama Net alikuwa akiwafungia pia kuwa kama kina mama Penny wataamua kusafiri hivyo hivyo, wasiruhusiwe kuingia hapo nchini kwa Viza hiyo ya kuwa wanakwenda kwa kina Cote. Inamaana waanze upya, kivyao kuomba visa nyingine ya kuingia nchini hapo. Hapo Net akajiambia hata kama wataanza kuomba Visa nyingine, mpaka waipate, atakuwa ameshampata Tunda. Akatulia.

Kwa Tunda.

T

unda alitolewa hospitalini  akiwa amechomwa sindano ya usingizi akiwa bado usingizini palepale hospitalini. Alitolewa pale hospitalini wala asijue alipo na anapopelekwa.  Akahamishwa kutoka kwenye gari moja kupelekwa gari ingine, hana taarifa na chochote. Walimpeleka  kwenye nyumba ilikuwa mbali kabisa na hapo mjini. Ipo peke yake porini, wakaenda kumuweka chini kabisa kwenye hiyo nyumba. Basement  ambayo haikuwa   haina hata dirisha. 

Akiwa humo humo ndani wakiwa wamemlaza tu kitandani mwanamke akianza kumuhudumia kama muuguzi kabisa, wanaume wawili wakaanza ujenzi humo ndani kama ambao hawakuwa wamejiandaa na na ujio wa Tunda. Gonga hapa na pale wakizungushia hicho chumba sufu, mbao za juu na pembezoni mwa hizo kuta zote na kufunikia plastiki maalumu, yote hayo ni kwa ajili yakuzuia sauti isitoke nje. Heka heka zikaendelea, Tunda hana habari hata. Alilala kama nusu mfu. Watatu hao waliendelea mpaka usiku ndipo chumba kikakamilika na Tunda akawa amesharudishiwa dripu mwilini na kuwekewa Catheter yakutolea mkojo. 

Usiku  Tunda akafungua macho kwa shida akiwa na usingizi mzito. Akamuona mwanamke wa kizungu aliyevaa nguo za kinesi akimsafisha kidonda. “Mtoto wangu yuko wapi? Naomba niletee kabla sijarudi kulala.” Hakujibiwa. Yule nesi ambaye hata hakuona sura yake vizuri kwa usingizi, akamuongezea dawa ya usingizi. Hapo hapo Tunda akarudi kulala. 

Maya na Harakati za kumsaka Tunda.

M

aya alikuwa akilia na kufikiria mfululizo. Akapata wazo. Akaamua kutoka pale. Ilikuwa bado muda wa yule nesi wa mtoto kuisha na kuondoka pale, akamuomba asiondoke mpaka atakaporudi. Yule dada akakubali kubaki pale akimlea Cote kwani Maya alimwambia atamlipa zaidi kama atachelewa kurudi. Yule nesi akafurahia hilo, akakubali kubaki huku akiomba Mungu Maya achelewe huko anakokwenda ili yeye abaki na huyo mtoto muda mrefu atengeneze pesa zaidi.

Hakutaka wale maafisa wamfuate. Maya aliyezoea kutoroka kwenye hilo jumba, hakupata shida kuwachomoka hao maafisa wote na hakumuaga mtu. Akaondoka kimya kimya. Alipofanikiwa kutoka tu hapo kwenye viwanja vya Cote, akampigia simu Gina. Aliyekuwa amemtumia ile video. Simu yake ikaita muda mrefu sana bila kupokelewa.

Gina ni rafiki wa karibu sana wa Maya. Na ni mmoja wa marafiki waliomfundisha Maya kutumia madawa ya kulevya. Na wakaendelea kutumia naye madawa, Maya akiwa ndiye mnunuzi kwani Gina na yeye alitoka kwenye familia ya kawaida tu. Lakini pia Gina yupo karibu na rafiki mmoja wapo wa Vic. Ava.

Ava na Renee walikuwa marafiki lakini ni kama wafanyakazi wa Vic. Wanafanya chochote wanachoambiwa na Vic, na huwa wanatembea naye popote pale kama watumwa wake. Siku alipomfuata Tunda, Vic alikuwa na Renee, ambaye alimrikodi Vic akizungumza na Tunda. Maya akajua kwa kupitia Ava, Gina ataweza kumsaidia kumpata Renee ambaye atakuwa na habari zote kutoka kwa Vic mwenyewe kwani alikuwa naye tokea mwanzo wanamfuata Tunda.

Maya alipoona Gina hapokei, akaamua kumpigia simu Renee mwenyewe aliyechukua hiyo video. Yeye Renee naye ni binti wa hapo hapo Norfolk. Lakini hakutoka kwenye familia ya kitajiri kama wao. Amekuwa katikati ya Vic na Maya. Anajua visa vyao watoto hao wa matajiri. Hakuna aliyeweza kuwaingilia Vic na Maya. Kina Renee wakawa watizamaji tu.

Aliposhindwa kumpata Renee, akaamua kumpigia tena simu Gina. Ikaita tena na tena mwishoe Gina akapokea. “Nina shida sana yakuzungumza na Renee, tafadhali naomba uzungumze na Ava, amwite Renee nyumbani kwao mimi niende kwa kina Ava nikazungumze na Renee.” “Hilo unajua wazi halitawezekana Maya. Hasa kipindi hiki. Unawajua Ava na Renee. Ni kama wamekula kiapo kwa Vic.” Gina akamkatisha tamaa Maya, akaanza kulia.

“Lazima nimpate Renee leo, Gina. Lasivyo nahisi nitachanganyikiwa. Hapokei simu zangu. Tafadhali nisaidie Gina. Uko wapi?” Maya akamuuliza huku akifuta machozi. “Nipo Club.” “Unaweza kutoka? Tafadhali Gina. Mimi huko ndani siwezi kuingia, zaidi leo.” Gina akakubali kuonana na Maya usiku huo. Maya akaongeza mwendo mpaka club. Akaegesha gari sehemu yakujificha kidogo, akamtumia ujumbe Gina kuwa amefika, akatoka.

Alionekana amekunywa, lakini hajalewa sana. Mchangamfu tu. “Nimetoka kuzungumza na Ava sasa hivi baada ya kuagana na wewe. Nikamuuliza kama anajua Renee alipo, anasema hata yeye hapokei simu zake. Jana alikwenda nyumbani kwa Renee akakuta kumefungwa kabisa. Anahisi pengine anajificha au ametoroka kabisa baada ya siku ile ya tukio lakuanguka Tunda. Hadhani kama yupo Norfolk.” Gina akamwambia Maya.

“Atakuwa amekwenda kujificha wapi?” Maya akaendelea kumuuliza Gina. “Sasa niachie mimi hiyo kazi. Mpaka kesho, nitakuletea jibu zuri. Acha nikazunguke ndani niulize taratibu. Usiwe na wasiwasi.” “Tafadhali Gina, ukisikia chochote hata kama ni usiku vipi, nitafute. Nitahakikisha pesa yote aliyoitangaza Nana kama zawadi, unaipata wewe.” Hapo akamtia morari Gina akarudi ndani club kwa haraka ili kupeleleza zaidi.

Maya akabaki pale kwenye gari akilia. Akawa amegonga mwamba. Hajui tena chakufanya ili kumpata Tunda. Alibaki akilia huku ameinamia usukani. Akasikia kioo cha gari yake kikigongwa. Akanyanyua uso huku amejawa machozi. “Malcom!” Maya akashangaa na kushusha kioo. Malcom ni yule afisa wa CSIS aliyekuwa akimuhoji Maya maswali na Maya akaondoka akiwa amevunjika moyo.

“Unanifuatilia nyuma!?” Maya akamuuliza kwa kumshangaa. “Ndiyo.” Malcom akamjibu bila kumficha. Maya akashangaa sana. Akidhani anatoroka nyumbani kwao kwenye ulinzi ule mkali na kujipongeza amefanikiwa kuwatoka afisa usalama hao, kumbe walimwacha tu na kumfanikisha atoroke ili kumfuatilia nyuma kujua ni wapi anakwenda. Gari yake yenyewe aliyonayo hapo ilishategeshwa vinasa sauti kujua na kusikiliza kila mtu atakayezungumza naye. Kwa hiyo hata mazungunzo yake na Gina walisikilizwa mwanzo mpaka mwisho. Walimtegemea kwa asilimia 80 kuwa atatoroka ndio maana yeye gari yake ilitegeshwa mapema sana bila yeye mwenyewe kujua.

Maya akabaki ameduaa haamini. “Mtu wa karibu yako ametekwa nyara, Maya. Mpaka sasa hatujapata hata mtu mmoja ambaye anahisiwa. Itakuaje waje wakurudie na wewe?” “Angalau nitakuwa na Tunda. Haya maisha hayana maana bila Tunda.” Maya akaendelea kulia. “Tulia kwanza tuzungumze Maya. Naweza kuingia ndani ya gari yako?” Maya akatoa loki za mlango. Malcom akaingia upande wa pili.

“Nisikilize Maya, jitahidi kutulia ili uweze kufikiria. Nimezungu na wewe kwa muda mfupi sana, nimeona uwezo wako mkubwa sana wakufikiria. Sasa kwa akili hizo, zinaweza kutusaidia kumpata Tunda.” Maya akajaribu kutulia.

“Unajua Andy alipo?” Lilikuwa swali lililomshtua sana Maya. “Kwa nini!?” “Unakumbuka uliniambia nini juu ya Vic?” Maya akatulia. “Sisemi kama ndiye aliyemteka nyara Mrs Cote, lakini sio vibaya kuanzia kwake.” Maya akajiweka sawa kutaka kumsikiliza zaidi. “Kwani nyinyi mlivyomuhoji Vic amesema nini?” Maya akauliza. “Siwezi kukwambia kwa undani ila ni kama vile ulivyosema. Vic anajibu la kila swali. Na yupo makini mpaka binafsi ananitia wasiwasi! Ni kama alikuwa akijua ni nini ataulizwa na polisi. Akaandaa mpaka ushahidi wa video na picha wa wapi alikuwa na nini alikuwa akifanya!”

“Nilikwambia Mal, Vic hamtamuweza kwa hoja. Anaandaliwa na mwanasheria wao. Na usifikiri ni hivi hivi tu! Vic alishakuwa au ana mahusiano na yule mwanasheria wao. Hawezi akaruhusu Vic akamatwe.” Malcom akashangaa kidogo. “Kwani yule mwanasheria si anamke na watoto?” “Kumbe! Ilikuwa karibu mkewe amuache sababu ya Vic. Sema yule mwanasheria huwa analipwa pesa nyingi sana na baba yake Vic, hawezi kuacha kazi kwao. Ikabidi mkewe atulie tu. Kwa hiyo Vic anajua ni nini aseme na atengeneze, ili asikamatwe.” “By the way nimependa ulivyoniita Mal.” Malcom akachomekea hilo.

“Bwana Mal! Focus ili tumpate Tunda.” “Huoni umecheka kidogo? Tulia tupange vizuri.” Maya akatulia kidogo kama anayefikiria kitu. “Nikuulize swali Malcom?” “Uliza tu.” “Unaniahidi hutanidanganya?” “Hata kidogo.” Maya akamwangalia kama anayetaka uhakika. “Huniamini?” “Nimeshadanganywa sana mpaka sijui yupi atasema ukweli na yupi ataanza na ukweli na kuishia na uongo!” Maya akaongea kwa kukata tamaa.

“Nakuahidi sitakudanganya kwa chochote, hata kama nitajua kitakuumiza, nitakwambia tu. Na kama ni mambo ya ofisini ambayo siwezi kuzungumza na wewe, pia nitakwambia ukweli. Kwa hiyo usitie mashaka kwangu. Uliza tu.” Maya akamtizama machoni kama anayemsoma. Akaridhika. “Unataka kujua nini?” Malcom akamuuliza taratibu tu.

“Upo hapa kama afisa wa CSIS au kama Malcon uliyeniahidi nikwambie halafu utanisaidia?” “Vyote.” Malcom akajibu. Maya akamtizama, akanyamaza. “Sasa mimi nimehangaika mpaka nimejua alipo Andy.” Malcon akavunja ukimya kwa habari iliyomshitua Maya. Akamgeukia vizuri na mshangao usoni. Akabaki kama bubu mbele ya Malcom.

“Nafikiri tuanze na Andy” Akaendelea Malcom. “Wewe anza naye, mimi huyo mtu sitaki kabisa kumuona.” “Kwa nini?” Maya akanyamaza na kugeukia pembeni. “Bado hisia za mapenzi zinakusumbua?” Malcom akamuuliza taratibu tu. “Nooo! Hata kidogo!” Maya akakataa kabisa. Malcom akabaki akimtizama. “Ni vile ali..” “Kuumiza?” Akamalizia Malcom kwa swali. Maya akanyamaza na kugeukia tena pembeni.

“Kama unamtaka Tunda, nilazima kumtafuta Andy ili tujue anamfahamu vipi Vic. Anauwezo wa kufanya nini? Yeye alikuwa akimlipaje? Maana kwenye akauti ya Vic, hayaonekaniki malipo yoyote ya ajabu yakututia wasiwasi. Sasa tutafute kujua kama kweli anatumia watu kufanya maovu yake, na je huwa anawalipa vipi?” Maya akashangaa sana. “Yaani mmeshamchunguza kwa umbali huo!?” “Bibi yako ameomba msaada wa mtu mkubwa sana CSIS. Na unajua vile bibi yako anavyofahamika na kile anachokifanya. Amesimama kupigania haki za wengi. Kwa mara ya kwanza kwenye maisha yake yote na harakati zake zote, leo ndio analia shida. Amepata mwitikio mkubwa sana.”

“Hiyo kesi inafuatiliwa kuliko nitakavyokueleza hapa. Macho na masikio ya watu wengi wakubwa ndani na nje ya nchi yapo kwenye hii kesi. Kesi ya Mrs Cote imechukua sura ya kitaifa. Kushindwa kupatikanika kwa Mrs Cote ni kudhalilisha usalama mzima wa nchi. Kwa hiyo ni lazima kufanya uchunguzi wa kina. Hakuna kulala, mpaka Mrs Cote arudishwe nyumbani.” Maya akabaki akifikiria.

“Fanya kwa ajili ya Tunda.” “Sasa hivi giza limeshaingia. Inabidi kurudi nyumbani kukaa na mtoto. Kwanza ni umbali gani mpaka huko anakoishi Andy?” Akauliza na kuguna Maya kwa kusikitika. “Nini?” Malcom akamuuliza. “Hata sijui kama jina hilo ni lake kweli!” Maya akaongea kwa mashaka. “Anaitwa Jake Cole.” Maya akatoa macho. “Malcom!” “Sijala Maya. Tokea tunaachana mpaka sasa hata sijapumzika! Kama ungeweza kunisaidia leo nikakutana na Andy au Jake, ingerahisisha sana.” “Mbona inakuwa ni kama wewe ndio unashida? Ni kama unataka nikusaidie kazi yako tena!” Maya akaongea kwa kulalamika.

“Nimekwambia tokea mwanzo Maya. Nipo hapa kwa kofia mbili. Kwa kile nilichokuahidi kwamba ukijibu maswali yangu nitakusaidia, na pia nikifanikiwa mimi, ujue na wewe utafanikiwa. Kama kweli Vic yupo nyuma ya utekwaji, utampata Mrs Cote. Kama yupo nyuma ya hayo madawa, tutajua ukweli wote. Utathibitisha kwenye kesi zako na lililompata kaka yako. Na kama hayupo, basi utajiridhisha, na mimi nitakamilisha kazi.” Maya akaona ni win win situation. Akakubali.

“Basi ngoja nimpigie simu nesi ambaye yupo na mtoto ili nimuombe kama anaweza kuendelea kukaa na mtoto.” “Wakati ukizungumza naye, mimi nitakusubiri kwenye gari yangu.” Maya akashangaa kidogo. “Hatuendeshi gari hii?” “Hapana. Naomba mimi nikuendeshe.” Wakabaki wakiangaliana. “Please!” Akaweka msisitizo Malcom. “Acha gari yako hapa, nitakurudisha hapahapa.” “Sawa.” Maya akakubali.

Malcom akatoka kwenye gari ya Maya na kurudi garini kwake. Maya akazungumza na yule nesi, akaonekana hana tatizo kabisa lakubaki na huyo mtoto. Hata angeweza kulala. Hilo likamfurahisha Maya. Akafunga gari yake na kuhamia kwenye gari ya kawaida tu ya Malcom. Akaingia na kufunga mkanda. Akatulia. “Uliniuliza ni safari ya muda gani.” “Ni mbali sana?” “Kiasi. Masaa mawili.” Maya akashangaa. “Sasa unajuaje kama tutamkuta nyumbani?” “Kuna gari ya usalama ipo nje ya nyumba yake, wanasema yupo.” Maya akawa hajaelewa.

“Mal! Naomba niambie ukweli. Ni nini kimewashinda nyinyi watu wa usalama kumuhoji Andy mpaka mimi!?” “Ndio maana nasema wewe una akili sana Maya.” Malcom akamsifia na kuendelea. “Kila dakika inayokwenda tukiwa hatujui Mrs Cote alipo, ni mbaya zaidi. Tungeweza kumchukua Jake au Andy kwa nguvu tu na kwenda kumuhoji. Lakini inaweza kuchukua muda mrefu sana kuweza kupata ukweli wote kutoka kwake na sisi muda huo hatuna. Na mbaya zaidi, kwa sasa Andy au Jake, hana chakupoteza. Kiasi chakumtisha nacho ili kuzungumza kwa haraka.” Bado akawa amemchanganya Maya.

“Unamaanisha nini?” “Mara nyingi ili kuweza kutoa siri kwa mtu, tena kwa haraka huwa tunatumia kumtisha ndugu au mambo mabaya aliyofanya zamani. Kwenye rekodi za Jake, hana kosa baya. Na maisha yake ya nyuma hayana doa.” “Ndugu?” Akauliza Maya. “Ndio nataka kukueleza. Jake ni mtoto wa pekee kwa mama yake. Ni kama mama yake alizaa na mume wa mtu, yule mwanaume akamtelekeza. Akalelewa na mama tu, bila ndugu yeyote.” Maya akajiweka vizuri kumjua Andy mpenzi aliyemchanganya zamani.

“Mama yake alipoanza kuugua. Akapoteza kazi. Jake ndio akawa akimuhudumia nakushindwa kusoma au tuseme kufanya kazi. Maisha yakawa magumu na wakapoteza insurance pia. Mama yake akashindwa kupata matibabu. Haya tumeambiwa mchana wa leo na mwanamke aliyekuwa akifanya kazi na mama yake kwenye supermakert. Sasa sisi tukiunganisha tunafikiri hivi, Vic alikutana na Jake kipindi hicho cha shida yake akihangaika kumtunza mama yake bila kazi. Akapenda ule uzuri wake, ndipo akampa hiyo kazi ya kuwa na wewe, iliyokuwa ikimsaidia kumtunza mama yake.” Maya akashangaa sana.

“Maana huyo mwanamke anasema mara kwa mara alikuwa akienda kuwatembelea Jake na mama yake. Walikuwa kwenye shida sana. Na mara nyingine yeye alikuwa akiwasaidia chakula. Lakini mambo yakabadilika gafla. Yule mama akatafutiwa na Jake nesi wakumuuguza, yeye akasema amepata kazi mbali na pale. Na akaanzishiwa matibabu ya hali ya juu.” “Mungu wangu Mal!?” Maya akaanza kulia. 

“Sasa ugumu unakuja hapa, yule mama alifariki. Ni kama walichelewa matibabu kitu kilichomuumiza sana Jake. Sisi tukienda kwa Jake, hatuwezi kumtoa ukweli kirahisi. Ila kwa kuwa wewe umeishi naye, unajua udhaifu wake na ulisema alikupenda, anaweza kufunguka kwako kwa haraka na ikatusaidia kukomboa wakati.” Maya akapotelea mawazoni.

“Nikuulize kitu Maya?” Maya akamgeukia. “Unafikiri utaweza?” Maya akavuta pumzi kwa nguvu. “Kwa kuwa na wewe unanitumia kufikia lengo lako kama wengine tu, niambie kile unachotaka kusikia kutoka kwa Andy au Jake. Nitamfanya aseme.” Maya aliongea kwa unyonge huku ameinama. “Sikutumii Maya!” “Wewe niambie ni nini unataka nikafanye kwa Andy. Nimalize tuachane kwa amani.” “Tafadhali usinifikiri kwa ubaya.” Maya akacheka kwa kuguna.

“Malcom! Haya ni maisha yangu. Na nimeshazoea. Kila anayenisogelea ni kwa sababu anataka kujinufaisha na mimi. Huwa wanakuja kwa njia au sababu tofauti tofauti ila mwisho wao kama si pesa, basi mwili wangu. Sasa kwa kuwa nimeshapanda ndani ya gari yako. Na viongozi wako wamekutumia wewe kijana mwenye sifa kama za Andy tu, wakijua ukitumia wajihi wako nitafanya kile utakacho, acha tumalize hili, ili tuachane kwa  amani na haraka.” Maya aliongea kwa kuumia sana na kujifuta machozi. Akajiegemeza pembeni karibu ya dirisha, akanyamaza. Na Malcom naye akanyamaza na kuendelea kuendesha.

Gina kwa Maya.

S

imu yake ikaanza kuita. Akaitoa kwenye pochi. Alikuwa Gina akaipokea kwa haraka sana akijua anacho cha muhimu chakumwambia na kwa kuwa alimwahidi pesa, akajua atahangaika tu ili kujinufaisha na yeye. “Umempata Renee?” “Nasikia ametokea polisi usiku huu kujisalimisha na kuuliza kama anatafutwa. Ameulizwa maswali machache, akaruhusiwa kwa kuwa ni kama maelezo yake yamefanana kabisa na ya Vic. Hawana hatia. Ila nasikia ameambiwa asikae mbali kama kuna swali ataitwa.” Maya akavuta pumzi kwa nguvu akatulia.

“Maya?” Gina akaita. “Najua hiyo ni kazi ya Vic tu. Itakuwa ameenda kutafutwa Renee na wazazi wake Vic ili aende akazungumze alichoambiwa na kufundishwa na mwanasheria wa wakina Vic.” Maya akawaza kwa sauti. Gina kimya. “Nashukuru Gina.” “Sasa utafanyaje?” “Acha nifikirie. Mpaka baada ya masaa mawili, nitakuwa nimeshapata jibu.” “Haya, kila la kheri. Ila kuwa mwangalifu.” “Gina!” Maya akamwita kabla hajakata simu.

“Nipo bado.” “Nikuulize swali unaniahidi hutanidanganya?” Akamsikia Gina akicheka kilevi kama kawaida yake. “Swali gani?” “Nilipokuwa nikilewa, watu wakinifanyia mambo mabaya, unajua ni nani aliyekuwa akinichukua video na kunipiga picha hata nilipokuwa vyumbani, kwenye gari au vyooni?” Kimya.

“Gina?” Kimya. “Katika hili ujue nitapata tu ukweli Gina. Iwe kutoka kwako au kwa Andy ambaye namfuata sasa hivi. Ila ujue nitajua.” Kimya, lakini alisikia kelele nyuma ya simu ya Gina. Inamaana alikuwa akisikiliza ila akawa kama amekufa ganzi. “Gina?” Maya akaita na kutizama simu yake. Hapo hapo Gina akakata. Malcom akamtizama na kurudisha macho barabarani. Akampigia Gina simu ikawa haipo hewani kabisa.

Maya Kwa Aliyekuwa akimuuzia Dawa.

Malcom akaona anapiga tena simu nyingine. “Umelewa?” Akamsikia Maya akimuuliza mtu wa upande wa pili wa simu. “Kwanza pole kwa matatizo.” “Nina swali dogo tu. Ukinijibu hilo, utakuwa umenisaidia sana.” “Nini?” “Ile cocaine tuliyokuwa tukitumia club, ulikuwa ukinunua wapi?” “Unajua hilo siwezi kukujibu Maya.” “Kwa nini?” “Nikuhatarisha maisha yangu!” “Sawa. Nisaidie swali jingine.” Maya akaendelea. “Cocaine uliyokuwa ukiniuzia mimi ni sawa na uliyokuwa ukiwauzia wengine?” “Yako ilikuwa grade A, wengine ilikuwa ni unga tu wakawaida.” “Unamaanisha nini?” Akauliza Maya huku akimwangalia Malcom.

“Mimi sijui Maya. Ndivyo nilivyokuwa nikipewa huko nilikokuwa nikinunua. Walikuwa wakinipa yako tofauti na wengine. Walisema hiyo inakustahili wewe mwenye pesa, wengine niliambiwa wanapewa unga tu wakawaida sio unga wenyewe sababu ya pesa yao.” Malcon na Maya wakaangaliana.

“Nani alikuwa akikwambia hivyo?” “Maya!” “Nataka kujua na ninakuahidi sitakutaja.” “Nihurumie Maya. Wewe ni wangu, lakini ukumbuke ndio nimetoka tu jela. Na nimetoka kwa kuponea tu! Niliyekuwa nikimuuzia hayo madawa kwenu, ndiye amenitoa. Siwezi kumtaja.” “Basi nashukuru.” Maya akakata simu.

~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~

“Ni nani huyo?” Malcom akauliza. “Nafikiri makubaliano yetu ni kukusaidia kwa Andy tu. Sio mpaka kwa watu waliokuwa wakitumiwa na watu wenye pesa kuuza madawa ya kulevya kwa watoto wa watu wasiokuwa na hatia.” Maya aliongea kwa hasira kidogo kama aliyeumia. “Umenichukia tu bure Maya. Na kwa kuwa nimekwambia ukweli. Ila nilikwambia tokea mwanzo. Sitakudanganya hata kama utaumia.” Maya akanyamaza.

“Au ulitaka nikudanganye ili kukufurahisha?” Maya akamwangalia na kunyamaza. “Maya?” “Nitazungumza na Andy, Malcom. Usiwe na wasiwasi. Mimi ni mtu wakusimamia maneno yangu.” “Hata mimi ninasimamia maneno yangu, na si tapeli. Sikutumii. Nakuhakikishia Maya, hata sasa hivi ukikataa kwenda kwa Andy, ukaona nakutumia vibaya. Sitakulaumu. Nitakurudisha na nitakuacha kwa amani kabisa.”

“Hapana. Twende tu. Sina ninachokwepa kwa sasa. Ni mimi Maya. Hakuna geni litanitokea kutoka kwa yeyote likawa la ajabu na waliyonifanyia wengine. Na kama nilitumiwa kwa mabaya, naweza kutumiwa na kwa mazuri. Twende tu, tumalize hili.” Malcom akamwangalia. “Lakini bado ahadi yangu ipo palepale.” Maya akamwangalia na kunyamaza. “Nitakusaidia mpaka kujua ukweli. Na nitahangaika mpaka kumpata Mrs Cote.” Maya akanyamaza bila kujibu kama aliyemuhesabu kuwa ni walewale tu, huna tofauti.

Malcom akaendesha mpaka kituo cha mafuta, akasimama. “Maya?” Akamuita, Maya akamwangalia. “Nimekuahidi sitakudanganya hata kama ukweli utakuuma. Nitakwambia ukweli ulivyo. Nataka kujua, tunakwenda kwa Jake ukiwa na mtazamo kuwa nakutumia?” Maya akanyamaza nakuanza kulia. “Niambie tu ukweli. Kama ndivyo hivyo unavyofikiri, nakurudisha sasa hivi. Mimi nitatafuta jinsi ya kupata ukweli kutoka kwa Jake na nitakuwa sawa tu. Lakini sitaki kuendelea kukuumiza. Mimi sio Andy au Jake, na ninakuahidi sitakuwa hivyo.” Malcom akabembeleza. Maya akajifuta machozi.

“Samahani kama umejisikia ni kama nakutumia tu.” “It’s okay Malcom.” “Hapana. Sio sawa. Nataka uwe huru kufanya kile unachojisikia moyoni. Na bado nakuahidi nitahangaika kivyangu ili kukusaidia na wewe. Na nitafanya kila niwezalo kumpata Mrs Cote.” “Kwani wewe ndio umepewa hilo jukumu?” Maya akauliza huku akijifuta machozi. “Ili kurahisisha kazi na wakati, tumegawana. Kwa hiyo mimi sio kiongozi na sipo peke yangu. Katika hili nafikiri wamenichagua kwa kuwa wameniona nikijana mwenzako.” “Kwa hiyo kumbe nilipatia?” Akamuuliza Malcom.

“Ndio maana natamani kukusikia mawazo yako Maya. Unaakili nzuri ya kufikiria. Usinikasirikie bwana!” “Watu wamekuwa wakinitumia sana Malcom.” “Nafahamu sana tu. Ila mimi nakuahidi sitakutumia vibaya, tena bila wewe kujua.” Maya akatulia kama aliyeridhika. “Ni sawa?” Malcom akauliza kwa upendo. Maya akatingisha kichwa kukubali, na tabasamu lililosindikizwa na machozi. Ungependa kumtizama mtoto huyo mwenye asili ya kitanzania na uzungu. Alijaliwa usichana wa kitoto, akitulia, hachoshi kumwangalia. Tunda alipenda kumwangalia wakati wote na kucheka.

Malcom akarudisha tabasamu na kuondoa gari kuelekea kwa Jake/Andy. Mpenzi wa zamani wa Maya. Angalau wakaanza kucheka, Malcom akamfundisha jinsi ya kumwingia Andy na kuhakikisha anajibu maswali yote. “Jitahidi kuweka au kuficha hisia zako mbali.” Maya akafikiria kidogo. “Nikwambie kitu Mal?” “Nakusikiliza.” “Unaponiambia niweke hisia zangu mbali kwa Andy, nataka nikwambie ukweli juu ya Andy.” Maya akaanza.

“Katika wanaume wote ambao umewahi kusikia nimekuwa nao na kuniona nao mitandaoni, hakuna aliyeonyesha mapenzi ya kweli kwangu kama Andy.” Maya akamuelezea mahusiano yake yeye na Andy kuanzia mwanzo mpaka mwisho. “Hudhani ni kwa kuwa kwanza alikuwa kazini. Alikuwa na shida sana na pesa. Ikabidi afanye kazi yake kwa bidiii. Na ndipo inakuja kitu cha pili. Alipatia kazi yake kwa kuwa alianza na wewe akiwa anakujua vizuri?” Malcom akamuuliza.

“Upo sahihi kabisa. Lakini Andy alikuja kunipenda kwa dhati, mpaka mimi mwenyewe nilijua napendwa! Mimi nikidanganywa huwa najua. Unafikiri ni kwa nini Gina amenizimia simu?” “Kwa kuwa anajua akikudanganya utajua?” Maya akacheka. “Unaakili Malcom!” “Kama wewe.” Wakacheka. “Mwanzo wa Andy na mwisho wake ulikuwa wa tofauti kabisa. Tuliachana na Andy nikiwa nampenda.” “Najua wewe ulitolewa jela na mwanasheria wenu, Logan. Ulijua ni nani alimtoa Andy?” Maya akashangaa sana.

“Kwa hiyo wewe Malcom unanifahamu kwa asilimia ngapi?” “90.” Akajibu Malcom bila kusita. Maya akacheka kidogo kama anayefikiria. “Ngoja nikwambie ukweli Malcom. Nilipofungwa jela kabla yakutaka familia yangu wajue, nilipata muda mrefu bila madawa, kwa hiyo sikuwa nikilewa, nikaweza kufikiria. Nikajiuliza kuanzia mwanzo mpaka pale tulipokuwa tumeishia na Andy, nikajua kuwa ile ni kazi ya Vic tu.” Maya akatulia kidogo. Kisha akaendelea. 

“Niliumia sana Malcom. Nilimchukia vibaya sana Andy. Kwa kuwa tokea tunaanzana sikujificha kwake. Nilimwambia ukweli nia yangu yakutaka kubadilika na kuacha maisha mabaya niliyoishi nyuma. Nilimwambia nimeacha marafiki wote, natulia na yeye tu. Ni kweli Andy alionyesha kunipokea kwa mikono miwili, kumbe ili alipwe! Iliniuma sana.”

Maya akaendelea. “Nilijitetea. Na logan akanitetea. Kuwa tulipokuwa club mimi na Andy kuna mtu alituwekea madawa. Mimi nikashinda kesi. Sasa sikutaka hata kumtafuta au kujua aliishia wapi. Kwanza nilikwenda rehab. Nilipokonywa simu na kufungiwa mawasiliano yote. Nilikuwa nikitoka rehab nakwenda mahakamani. Halafu ndio kipindi hicho tulikuwa tumefiwa na Papa. Papa yangu mimi alikuwa kama baba yangu. Kwa hiyo nilikuwa na wakati mgumu, ya kwangu tu yalikuwa yamenilemea. Sikuwa na nguvu yakumfuatilia tena Andy, kwanza sikutaka hata anisogelee tena.” “Pole Maya.” Maya akanyamaza.

“Kwa hiyo sasa hivi nani ndio amebahatika?” Malcom akamchokoza baada yakumuona amekosa raha. Maya akamwangalia na kunyamaza. “Maya?” “Mambo yamebadilika Malcom. Kwangu mimi mwenyewe na watu wanao nizunguka.” “Kivipi?” Maya akafikiria. “Kabla sijaangukia kwa Andy, ni kweli nilikusudia kubadili maisha yangu. Nilitamani kutulia. Ndio nikaharibu tena. Na hiyo haikuwa mara ya kwanza. Nafikiri na wewe unajua.” Malcon akatabasamu ishara ya kuwa anajua.

“Sasa kwa kuharibu kote huko. Kutangaza nitatulia, na bado nikaendelea kuharibu tena na tena. Unafikiri mwanaume gani wa maana. Aliyetulia. Mwenye akili zake. Sio tapeli kama kina Andy na wengine niliokuwa nao, atakubali kuwa na mtu kama mimi!?” Maya akauliza na kuendelea. “Sina sifa nzuri popote na siaminiki, Malcom. Kwa kujibu swali lako. Nimebaki mimi peke yangu na ndio Mungu akanipa Tunda.” Maya akaanza kulia.

“Tunda ananipenda sana Malcom. Isingekuwa upendo wa Tunda kwangu, usiku huu nisingekuwa njiani nikihangaika. Natafuta nini! Ni vile sitaki kumpoteza.” “Usilie nikwambie kitu.” Maya akajifuta machozi. “Cha kwanza, nina imani kuwa tutampata Mrs Cote. Cha pili, mwanaume anayekupenda kwa dhati, atakupokea hivyohivyo ulivyo na historia yako ilivyo. Na atakupenda na kukulinda.” Maya akamwangalia.

“Huamini kwa kuwa hajaja Mr. Right. Akija, utakumbuka haya maneno yangu. Atakupenda mpaka utafurahia na kusahau hao matapeli wote waliokuwa wakikupendea pesa, na kuona fahari kuonekanika mitandaoni na wewe.” Maya akanyamaza. “Kaa mkao wakumpokea. Atakuja tu.” “Wewe umeoa Malcom?” “Nilioa, tukapata mtoto mmoja wa kiume, lakini tuliachana na mke wangu.” Maya akakunja uso na kumwangalia Malcom vizuri.

“Unaonekana wewe ni mdogo sana Malcom! Umeoa lini na kuacha lini? Au uliingia kwenye ndoa kujaribisha, ulipoona mambo magumu ukakimbia?” Malcom alimtizama kwa tabasamu ambalo Maya akajua sio la furaha, akarudisha macho barabarani. Hakujibu. Maya akamuona amepotelea mawazoni. Akajua kuna linalomsibu. Na yeye akanyamaza.

Kwa mara nyingine tena Maya kwa Andy.

M

alcom alimfikisha mpaka nje kabisa ya nyumba ya Jake. “Unataka niingie mwenyewe!?” Maya akauliza kwa kushangaa kidogo. “Nafikiri itakuwa vizuri akuone peke yako kwanza. Mimi nipo hapa nje. Ukinihitaji nitakuja.” Maya akafikiria kidogo. “Naomba tu tuongozane.” “Maya!” “Namfahamu Andy. Hatakuwa na neno. Twende.” “Hawezi kuwa huru kuzungumza na wewe kama mimi nitakuwepo.” “Sasa wewe utasikiaje mazungumzo yetu?” Malcon akatulia kidogo.

“Malcom?” “Tutakuwa tukisikiliza kila kitu.” Maya akaingiwa hofu. “Inamaana na viongozi wako?” “Ndiyo.” Maya akabaki akimtizama. “Usiogope.” Malcom akajaribu kumtuliza. “Inamaana hata haya mazungumzo hapa ndani ya gari walikuwa wakiyasikiliza!?” “Hapana. Nyumbani kwake ndio kumetegesha tokea mchana. Alitoka, wakapata nafasi ya kuingia. Wametegesha kamera na spika.” Maya akazidi kuogopa.

“Mtamfunga tena?” “Inategemea.” “Sitaki mumfunge. Waambie viongozi wako kama watamfunga mimi sitakwenda kuzungumza naye.” “Siwezi kufanya hivyo Maya.” “Basi nirudishe kwenye gari yangu.” Maya akagoma na kumshangaza Malcom. “Kweli Malcom. Japokuwa amenitenda vibaya, mimi siwezi kumlipa kwa kumkamatisha kwenu. Nirudishe kwenye gari yangu. Sitazungumza na Andy.” “Kwa hiyo unataka aje atumiwe kuja kumwangamiza binti mwingine kama alivyofanya kwako wewe?” Hapo Maya akafikiria.

“Na kama kweli Vic yupo nyuma ya hilo au kweli anatumia madawa kutenda watu vibaya, huoni utakuwa umemtoa mwangani? Utasafisha jina lako na la kaka yako ambaye sasa hivi anakashifa mbaya tu mtandaoni na pia, utaweka kikomo kwa binti wengine wasifanyiwe kama wewe na kaka yako. Halafu huwezi jua anaweza kusaidia vipi kupatikanika kwa Mrs Cote. Chochote kutoka kwa yeyote, tunahitaji ili kuweza kumpata Mrs Cote akiwa salama.” Hicho kikamuingia Maya.

“Unafahamu kifaransa?” Maya akamuuliza. “Nafahamu.” Maya akakunja uso. “Sikutegemea jibu la ndiyo!” “Kumbuka kazi ninayofanya Maya. Inanilazimu kujua lugha pia. Kwa nini umeniuliza?” “Nataka ukinisikia nikizungumza neno la kifaransa, ujue nazungumza na wewe. Kwa hiyo naomba kuwa makini ili nisidhurike. Hatujui Andy yule niliyekuwa naye kama ndiye huyu Jake wa sasa na hatujui ameapishwa vipi na Vic.” “Hilo ni wazo zuri sana.” Malcom akamsifia kama kawaida yake.

“Unaona ile gari pale?” Maya akachungulia nje. Ilikuwa mbali kidogo na ilipokuwepo nyumba ya Andy. “Basi ile ni gari ya CSIS. Imejaa mitambo ya sauti na video nzuri tu. Na kuna watu wazuri tu wa usalama ndani ya ile gari na hili eneo lote, hata wale wanaopita pale na wale waliokaa pale kama wahuni tu. Ni watu wa usalama.” Maya akashangaa sana. Akamwangalia Andy, “Inamaana nilikuwa nikisubiriwa mimi!?” Akauliza Maya. “Ndiyo.” Malcom akajibu nakuendelea.

“Kwa ufupi nataka kukuhakikishia kuwa, hili eneo limezungukwa na maafisa wa CSIS. Na kwa kuwa wewe ni Cote, akili na macho ya wakubwa wote wa CSIS yapo hapa tulipo sasa hivi, na ndani ya hiyo nyumba alipo Jake ili kuhakikisha hakuna linaloharibika hata kidogo. Usiogope. Tutaona na kusikia kila kitu. Ukijisikia tu upo hatarini, niite.”  Akamuona anashuka bila hata kuaga. Malcon akaondoa gari pale karibu na nyumba ya Andy.

Maya & Andy.

M

aya akasogea mpaka mlangoni. Akavuta pumzi mara  kadhaa. Wakamuona anasugua viganja. Akavuta tena pumzi. Akafunga macho kwa muda ndipo akaweza kugonga mlango. Jake akafungua. Alishituka mpaka Maya akamuona usoni. Wakabaki wakitizamana kwa muda. “Maya!” “Umenisahau?” Maya akamuuliza. “Sikutegemea kukuona hapa hasa baada ya yote yanayoendelea kwenye familia yenu!” Maya akabadilika na kuweka sura ya huzuni. “Unakumbuka wakati ule nilipokuwa nipo kwenye matatizo nilikuwa nikikukimbilia wewe Andy?” Maya akaanza kwa sura ya majonzi.

“Ingia ndani. Ingia.” Akamshika mkono na kumvutia ndani. Akafunga mlango. Maya hakutaka hata amguse. “Tunda hakuwa wifi yangu tu Andy, alikuwa rafiki wa pekee ambaye sijawahi kumpata.” “Pole sana Maya. Nilikusikia kwenye tv, siku ya kumkaribisha nchini. Pole sana.” “Sijui nitafanyaje Andy! Polisi wameshindwa kumpata. Wamejaribu kufuatilia gari iliyomtorosha, watekaji wake wanaonekana wanaakili sana. Wamepotelea chini ya daraja.” Maya akaanza kulia.

“Njoo nikwambie kitu. Usilie.” “Nini?” Maya akauliza. “Nimekumiss Maya. Njoo angalau tukae hapa nikushike tu. Nitakwambia kitu.” “Kwa hiyo huwezi kuniambia mpaka unishike?” “Maya! Wewe huna hamu na mimi?” “Wewe ulikuwa wapi siku zote hizo usinitafute mpaka mimi nikufuate?” Maya akamuuliza.

“Hayo ni masharti niliyokuwa nimepewa na mwanasheria wenu. Logan?” “Logan! Alikwambia nini!?” Maya akauliza kwa kushangaa sana. “Atanitetea mimi na wewe kama nitamuahidi kama sitarudi tena kwenye maisha yako. Na akaniahidi nikirudi tu, atahakikisha anatafuta ushahidi wakutosha kuwa mimi ndiye nahusika kwenye kukulevya na kukufanyia mabaya.” “Sasa ulikuwa na wasiwasi gani wakati mimi na wewe wote tulikuwa tukilevya.” Jake akanyamaza.

Maya akamsogelea. “Usiniambie kama wewe ndiye uliyekuwa ukinilevya Andy!” “Nooo. Sio mimi kabisa Maya. Kumbuka mimi ndiye niliyekuwa nikikukataza usinywe hata pombe.” “Sasa kwa nini siku ile tuliamka tukiwa hatujitambui tulifikaje kitandani wakati tulikula tu Piza na juisi? Ukanidanganya kuwa na wewe hujui ni nini kilitokea. Halafu tukaja kukuta video na picha za siku ile mitandaoni? Ulinidanganya, kumbe ulinilevya Andy!”

“No no nooo Maya. Sio mimi na Mungu wangu ni shahidi. Sio mimi. Mimi nilikukataza na unakumbuka nilikasirika mpaka nikakugombesha ni kwa nini ulikuja kuinywa tena ile juisi wakati nilikukataza?” “Kwa nini ulinikataza kama hukujua kama inakileo? Na kama wewe hukuweka, nani aliweka?” Andy kimya. “Unajua nini Andy, umenidanganya vyakutosha. Hukuwahi kunipenda na wewe umekuwa ukinitumia kama wengine. Naondoka.” “Hapana Maya. Naomba usiondoke.” Andy akakimbilia mlangoni.

“Nina mengi ya kukwambia ila akili haijatulia. Nipo kama nimechanganyikiwa.” “Ndio utulie uniambie ukweli.” “Siwezi kutulia mpaka unitulize Maya. Wewe unajua kunituliza.” Maya akashangaa sana. “Umechanganyikiwa Andy! Wewe ni mwenda wazimu. Yaani kwa tuhuma zote hizi ambazo umeshindwa kujieleza hata moja! Bado unaniomba penzi!?” “Nina hali mbaya na wewe ndio utaweza kuniweka sawa.” Akamsogelea.

“Nisikilize Maya. Ukiniweka sawa, nakuhakikishia nitaweza kukusaidia hata kumpata Mrs Cote.” Maya akashangaa na kuanza kutetemeka. Ila akajaribu kutulia. “Huwezi kunifanyia hivyo Andy. Umeniumiza sana. Angalau tuweke mambo sawa, ndipo turudi kwenye mapenzi. Huwezi kunitaka kimapenzi wakati umenivuruga.” “Sio mimi. Hata mimi nimevurugwa Maya. Walikutoa kwangu nikiwa nakuhitaji. Hata mimi nimevurugwa.” “Nani?” Maya akamuuliza.

“Maya! Nisaidie tafadhali. Huwezi jua ni kiasi gani nakuhitaji. Siwezi kukubaka, lakini ujue unao uwezo mkubwa sana wakunifanya nitulie ili nifanye kazi. Tokea niliposikia Mrs Cote ametoroshwa, nilijua naweza kumsaka kutumia ile komputa pale. Iangalie ipo wazi, lakini nashindwa kufanya kazi.” “Kwa nini?” Maya akauliza kwa kumshangaa sana. “Kusikia jina lako tena kwenye mitandao, nikakuona ukilia, ukiomba msaada. Nikakimbilia kompyuta nikijua naweza kukusaidia kumpata Tunda, ili usilie. Lakini pia kukaniharibu akili kabisa. Nikakumbuka wakati ule tukiliwazana kila mmoja wetu akiwa kwenye matatizo. Nikaingiwa tena na hamu ya ajabu. Siwezi kufanya chochote.” Maya alimshangaa akabaki ametoa macho.

“Wewe niache nikuguse kule nitakapo, ndipo nitaweza kufanya kazi. Unakumbuka vile nilivyokuwa nikitulia wakati nipo na wewe?” Maya akabaki anamtizama. “Mapenzi niliyokuwa nikifanya na wewe, yalikuwa yakinituliza sana. Vic amekuwa akinilipa niwe namfanyia mapenzi kama yale tuliyokuwa tukifanya na wewe, lakini bado sijawahi kuridhika kama nilivyokuwa nikifanya na wewe. Niruhusu nikuguse akili itulie nitakwambia kila kitu.” Machozi yalianza kumtoka Maya.

Akajua ni kweli Vic anahusika. Akakumbuka Malcom alimwambia ajitahidi kutawala hisia zake. “Usilie Maya.” “Yaani ulikuwa na mimi pamoja na Vic?” “Nooo. Sio wakati ule ule. Nilipotoka jela ndipo Vic akanifuata tena. Akaniomba nifanye mapenzi na yeye hata kwa malipo kama nilivyokuwa nikifanya na wewe.” “Vic aliona wapi sisi tukifanya mapenzi?” Jake akajishika kichwani kwa mikono yote miwili, akageuka na kuondoka pale. Ikabidi Maya ajitulize ili aweze kumtuliza na yeye azungumze.

“Andy?” Maya akamsogelea na kumvuta taratibu. “Niambie ni wapi Vic alituona tukiwa tukifanya mapenzi. Lasivyo naondoka na sitafanya mapenzi na wewe tena.” “Naomba usiondoke Maya. Kama kukusikia na kukuona kwenye tv kumenichanganya hivi, je kukuona na kukugusa kabisa! Naweza kujiua kama ukiondoka na kuniacha hivi.” Maya akashangaa sana. “Wewe ni mgonjwa wa akili na upo kwenye matibabu?” “Zamani!” Maya alishituka akatamani kukaa chini.

“Andy! Kwa nini hukuniambia kama unaugonjwa wa akili?” “Kwa kuwa nilipona kabisa. Na nilipokupata wewe ndio ikawa zaidi. Nisaidie Maya.” Maya akajua anaongea na kichaa hapo. Na kimeshatibuka. Akajua hatima ya Tunda ipo juu yake. “Nahisi hali yangu imerudia Maya. Nilitaka kumtafuta Mrs Cote lakini nimeshindwa. Mimi ni mjuzi sana wa kompyuta. Tena bila kusoma. Nina kipaji hicho tokea mtoto sema mama alishindwa kuniendeleza sababu ya uwezo.”

“Hicho walichofanya hao waliomteka nyara, ni kitu cha kijinga sana. Nilikigundua mchana. Lakini nikashindwa kabisa kufikiria. Nisaidie Maya.” Akashangaa anaanza kulia. “Nikupeleke hospitalini?” Maya akamuuliza huku akianza kumuogopa. “Hapana. Fanya mapenzi na mimi kama wakati ule. Ninauhakika akili itatulia. Nitaweza kufikiria na kufanya kazi vizuri tu. Nitaweza kufuatilia lile gari la pili lililombeba Mrs Cote. Lakini sasa hivi siwezi tena. Nisaidie Maya. Mrs Cote yupo matatizoni na ni lazima nimsaidie.” Akawa kama amechanganyikiwa kabisa. Analia utafikiri yeye ndio Net akitaka kumsaidia Tunda.

Akapiga magoti mbele ya Maya akilia huku amemshika Maya magoti. “Ninauwezo mkubwa sana Maya. Nitakuonyesha. Nina uwezo wa kuingia kwenye mitandao ya usalama wote wa hii nchi. Hata CSIS, nikafanya ninachotaka na nikatoka bila hata mtaalamu wao kuhisi kama niliingia. Namaanisha bila kukamatwa.” Maya akashituka sana. Akajua wamemsikia. “Usilie. Tulia kwanza. Simama.” Akamuwahi ili asiendelee kuongea. Akasimama na kujifuta machozi.

“Utaniambia na maswala ya Vic?” “Nina uhakika nitakumbuka kila kitu. Na nitakusaidia kukwambia ni wapi alikuwa akipata madawa ya kukufanya ulewe na kesho yake usikumbuke kitu ulichofanya siku iliyopita.” Maya akashangaa zaidi. “Na nitakusindikiza mpaka kwa aliyekuwa akimuuzia. Alishawahi kunituma kwake nikachukue dawa kwa ajili yako. Unakumbuka ile video nyingine walirusha, walituchukua tukiwa hotelini? Nilikupeleka siku ya birthday yangu? Tukalala huko kama siku mbili hivi? Sijui kama unakumbuka?” Maya kabaki kimya.

“Unasahauje Maya? Ile video mpaka ukashangaa walitupataje vizuri kwa kiasi kile halafu ukashangaa walijuaje tulipo wakati tulikuwa nje ya mji, na hukuwa umemuaga mtu yeyote! Bado hukumbuki tu kama mimi!?” “Nakumbuka Andy!” Maya akaongea kwa uchungu sana. “Basi ujue ile hoteli alitutafutia Vic na ile video ilitoka vizuri vile ni kwa sababu safari ile Vic alitafuta wachukua video wataalamu. Aliandaa kila kitu siku moja hata kabla ya sisi kufika kule. Ndio maana ikabidi anitume mimi kwenda kwa huyo mtu wake kununua hizo dawa kulekule Norfolk kwenye mji wenu. Ni dawa maalumu anazotumia kwako.”

          “Na kwa kuwa siku ile alitaka video ndefu na nzuri, alitafuta wataalamu kabisa wa kutuchukua video. Chumba kilikuwa na wataalamu watupu siku ile. Wakifanya kazi ya kuchukua ile video yetu tu. Vic alisimamia yeye mwenyewe, alisema hataki kitu kiharibike. Sema nimewasahau majina yao. Ukinisaidia, nitawakumbuka wote. Nashangaa mimi huwa sina tabia yakusahau vitu! Kwa nini sasa hivi sikumbuki vizuri?” Akajishika kichwa na kuanza kulia.

“Fix me, Maya! Wewe huwa unajua kunifanya nitulie. Lazima nirudishe kumbukumbu. Siwezi kusahau vitu nilivyokuwa nikivijua. Please Maya!” Maya akaanza kutokwa tena na machozi. Alijisikia uchungu sana. Inamaana inabidi kufanya mapenzi na huyo kichaa ili kumpata Tunda na kusafisha jina lake na kaka yake! “Naomba hii usichukue video tafadhali. Itabidi tu kufanya kama anavyotaka ili aweza kusaidia. Na kama niliweza kutumika kwa ujinga, kwa hili sina budi kufanya. Ila usichukue video tafadhali.” Maya aliongea kwa kifaransa akimfikishia ujumbe Malcom. Lakini akashangaa Andy ameelewa yeye. “Mimi siye niliyekuwa nikichukua Video kwa ajili ya kukutumia Maya. Ni Vic. Vic ndiye aliyefanya kwa ujinga. Mimi nafanya kwa mapenzi ya kweli kwa kuwa nakupenda.” Andy akajibu kwa kingereza vizuri tu kama vile Maya alikuwa akimuongelesha yeye. Maya akashituka sana akajua amekamatwa au hajaelewa.

“Inamaana unaelewa lugha ya kifaransa?” Ikabidi amuulize. “Yeah! Kwani sikukwambia? Nilizaliwa Ufaransa. Mama yangu alikwenda kule kusoma, akapewa mimba na mume wa mtu. Wakakubaliana wafanye siri. Nilipofikisha miaka 10, siri ikajulikana. Mke wa yule baba akataka kunidhuru mimi ili nisichukue mali zao. Ikabidi mama atoroke. Lakini hiyo sio muhimu. Fix me, Maya.” Maya alikuwa akimshangaa Andy, akashindwa kuelewa alikuwaje naye kwenye mahusiano mpaka kumfikiria ndoa akiwa hamjui kwa kiasi hicho!

“Kwa hiyo ulikuwa ukitumia jina hilohilo Andy?” “Nooo. Andy sio jina langu. Hilo amenipa Vic. Jina langu ni Jake. Na tukiwa tunafanya mapenzi sasa hivi, niite Jake sio Andy. Andy ni jina la Vic.” Machozi yakaanza  kumtoka tena Maya. Andy hakwepeki, anataka penzi. “Naomba usilie mbele yangu Maya. Utazidi kunichanganya na kunifanya nizidi kuchanganyikiwa nakushindwa kumpata Mrs Cote. Unajua kila dakika inayozidi kupotea ndivyo anavyozidi kuwa matatizoni?” Jake akazidi kusisitiza bila mapenzi, hawezi kusaidia.

“Unakumbuka ulikuwa ukipenda kunifanyia nini?” Maya akamuuliza kwa uchungu sana. Akamuona Andy anacheka cheka. “Naruhusiwa kuanza?” Akauliza Jake kwa heshima sana akiwa mbele ya Maya. “Lakini unaniahidi utanisaidia Andy?” “Hapana. Niite Jake. Jake ndio jina langu.” “Sawa Jake. Unauhakika baada ya hapa utanisaidia.” “Nimekuhakikishia Maya. Ninauhakika baada ya mapenzi na wewe nitakumbuka kabisa.”

“Unajua Vic alikuwa akinilipa nikamfanyie mapenzi kama niliyokuwa nikifanya na wewe, lakini yeye alikuwa akifurahia mimi sikuwa nikifurahia?” “Uliniambia Jake.” “Unafikiri ni kwa nini?” “Wewe niambie.” Akamuona anatabasamu huku aking’ata meno.  “Kwa sababu Vic sio Maya, na hatakaa akawa Maya. Upo na ladha ya tofauti.” Jake akaanza kumsifia kwa undani kabisa. Jinsi alivyokuwa akifanya naye mapenzi. Maya hakuwa akijua kama watu wa usalama wanawasikiliza au walishafunga kila kitu baada ya kuongea na Malcom kwa kifaransa.

“Unataka tukafanyie wapi?” Maya akaona amkatishe. Maana alikuwa akiongea mambo mazito mno. Akaangalia pale walipo. Ni kweli paliendana na Jake mwenyewe wala siye Andy aliyekuwa amekutanishwa na Vic. Ilikuwa nyumba ya kawaida sana hata thamani yake ilikuwa ya kawaida mno. “Unakumbuka tulikuwa tukianzia popote? Nikiwa na wewe Maya, sihitaji kitanda kuridhika. Au wewe unahitaji kitanda?” Akawa ameanza kumvua nguo Maya.

“Nafikiri chumbani ni pazuri zaidi. Halafu tukimaliza, tutakuja kufanya kazi hapa.” “Asante kwa kunisaidia Maya. Unajua ukinisaidia mimi, nitaweza kumsaidia Mrs Cote. Unajua na yeye anafanyiwa kama alichofanyiwa mama yangu akiwa nchini Ufaransa?” Akaanza Jake huku akiendelea kumtoa Maya nguo. Maya alitulia tu huku akitetemeka na machozi. Alijua historia yake inajirudia. Kufanywa mapenzi mbele ya kamera. Ila safari hii mbele ya macho ya usalama wa taifa.

“Walimteka nyara mama. Wakampa masharti aondoke nchini kwao. Asirudi tena na wala asije kusema kama mimi ni mtoto wa yule baba lasivyo wataniua mimi. Mama alipokubali ndipo wakamuachia. Ndipo tukatoroka kuja huku kama kujificha. Mrs Cote hana tofauti na mama yangu. Lazima nimsaidie.” Gafla yeye ndio akaonekana anauchungu na Tunda kuliko yeyote.

          Akawa amemaliza kumtoa nguo Maya. “Oooh Maya! Maya wangu. Vic hawezi kujifananisha na wewe hata kidogo!” Akambeba hapo Maya, mpaka chumbani alipotaka Maya. Alimsikia akigugumia kama aliyepata nafuu. Alifanya mapenzi na Maya akiwa ametulia wala sio kichaa. Alihangaika na huo mwili wa Maya, kama aliyekuwa akijitibu kiukweli. Kila alipomaliza, aliendelea huku akimwambia Maya, hiyo ni mara ya mwisho. Jake alifanya mapenzi na Maya huku akimshukuru na kumsifia, mpaka akaridhika yeye.

“Mbona unalia Maya!?” “Kwa sababu ya furaha Jake. Nilikuwa na hamu na wewe.” Jake akambusu. “Umeridhika sasa?” Akamuuliza kwa upendo. “Nitakuomba tumalizie tena baadaye. Sasa hivi tumtafute kwanza Mrs Cote.” “Upo sahihi Maya. Wasije kumuua.” Maya akajitahidi sana kutulia ili kuweza kutimiza lengo, sadaka yote aliyotoa isiwe bure, kwani machozi yalikuwa yakiendelea kumtoka kama mvua.

“Unafikiri Vic anahusika katika kumteka Tunda?” “Sijui Maya. Lakini Vic anaweza kufanya chochote. Twende kwenye kompyuta.” Na kweli Jake akawa ametulia mpaka akamshangaza Maya. Hapo akaamini ni kweli ni kichaa. Maya akatoka hapo chumbani kwenda kutafuta nguo zake kule zilipokuwa zimeachwa.

Akaziokota huku akilia sana. Mikono imeshilia matiti yake. Alipotaka tu kuvaa Jake akatoka. “Naomba usivae Maya. Si umesema tutarudia?” “Nasikia baridi Jake. Acha nivae.” “Oooh pole. Basi nikusaidie kuvaa.” “Naomba nitumie choo kwanza. Nitarudi baada ya muda mfupi.” Akamsindikiza mpaka chooni. Akaingia humo ndani na kuanza kulia sana. Alilia Maya, mpaka akahisi Jake atamsikia. Akaogopa asije akaharibu tena. Akaosha uso tena na tena ndipo akatoka.

Alitoka na kumkuta Jake ameshavaa na ametulia mbele ya kompyuta akionekana amezama kwenye kile anachokifanya. Akamwambia Maya na yeye avute kiti akae pembeni yake amuonyeshe jinsi ya kumtafuta Tunda.

Vic mbele ya Maya & Jake.

W

akati ndio Maya anatulia tu ili aone anachokifanya Jake kwenye kompyuta, wakashangaa mlango wa nyuma unafunguliwa kwa nguvu. Alikuwa Vic. Amevaa nguo nyeusi juu mpaka chini na kofia. Nywele zake za Blond amezificha ndani ya kofia kabisa kama asiyetaka mtu amtambue. Akawatolea bastola yenye kiwambo cha sauti. Maya akashituka sana. “Unafanya nini hapa Vic?” “Hilo swali muulize Jake, au wewe bado unamfahamu kwa jina nililompa mimi la Andy?” Vic akamuuliza Maya kwa kumkejeli.

“Niangalie mimi Vic. Naomba usimdhuru Maya.” Jake akataka kusimama. “Hatua moja mbele, nakupiga bastola Jake. Sikutanii. Rudi kukaa.” “Basi hiyo bastola nielekezee mimi sio Maya.” Jake akamsihi. “Kwa nini? Hilo umeligundua lini? Mbona ulikubali pesa yangu na kumfanyia kila nilichokutuma? Leo ni kipi kimegeuka?” Vic aliongea kwa ujasiri akionekana amekasirika sana. “Kwa nini ulinifanyia hivyo Vic?” Maya akauliza huku akitetemeka. “Wewe ni mshenzi Maya. Ulianza vita na mimi ukifikiri utashinda! Mimi nina pesa na watu. Marafiki zako wote uliodhani ni marafiki zako, ndio wabaya kuliko mimi.” “Wewe ni muongo Vic.” Maya akabisha. “Sasa unafikiri nimejuaje kama upo hapa kama sio rafiki yako kuniambia?” “Gina!” Maya akashangaa sana.

“Wewe ni mjinga Maya. Miaka yote hiyo ndio leo unaniuliza! Sasa hapa leo sio wewe wala Jake mtakaotoka wazima. Hili jambo ni lazima nilimalize leo. Umenisababishia mateso mengi. Wewe ndio umesababisha Net azae na mwanamke mwingine.” “Wewe ni mgonjwa wa akili Vic. Ni kipi kinachokufanya ufikiri kuwa wewe ni mke wa Net!?” “Hata mama yenu ananikubali kuwa mimi ndiye mke sahihi wa Net. Sio Malaya Tunda.” Moyo wa Maya ukapasuka.

“Ndivyo anavyokudanganya mama? Na kwa taarifa yako tu, mama anamtumia yeyote yule kumuangamiza Tunda. Wewe si wa kwanza na wala hutakuwa wa mwisho.” Akamrushia Maya urembo alioukuta pembeni ya meza. Jake akadaka kwa haraka kabla haujamfikia Maya.

“Ameniambia mimi ni wa tofauti. Net ni mtoto wake anamfahamu. Hakuna mwanamke atakaye mfaa Net kama sio mimi. Unafikiri ni kwa nini nilikwenda kulala na Net?” “Ulimlevya na ndio ukalala naye.” Maya akamkanusha. “Ni kwa sababu hata yeye alikuwa na hisia na mimi ndio maana japokuwa alikuwa amelewa lakini aliweza kufanya mapenzi na mimi. Na kwa taarifa yako, ilikuwa zaidi ya lisaa.” Maya akaona atampoteza na asipate kotekote. Kwake na Jake.

“Wewe na mama wote ni wendawazimu. Haitakaa ikatokea Net akawa na wewe Vic. Usikubali mama akakupotezea muda.” “Sasa kwa ile video niliyosambaza mimi na ile ya Renee, mama yako amesema ile hakuna mtu anaweza kumuamini tena kama kuna mapenzi kwa Tunda ila Net ananipenda mimi. Wewe ninakuaa hapahapa, na Tunda hatakaa akaonekanika hata kama mkihangaika mpaka kuleta FBI wa Marekani.” Maya akatumia akili ya haraka.

“Popote ulipomficha Tunda, tutampata.” “Nani amekwambia mimi nimemficha Tunda? Sina huo muda. Mimi nipo hapa kwa ajili yako Maya. Umesababisha machungu mengi sana wewe. Hivi unajua umenisababisha kuua usiku huu?” Maya akaanza kutetemeka. “Nani amekwambia uanze kuchimbua mambo yaliyokuwa yamezikwa? Nani amekwambia uanze kutafuta watu ambao hakuna hata mtu aliyejua kama wapo?” “Kama nani? Mimi sijamtafuta mtu yeyote zaidi ya Tunda.” Maya akajikaza na kujitetea.

“Acha uongo Maya. Unazidi kuniudhi.” Akataka kumsogelea ili ampige, Jake akamzuia. “Hukutoka kumpigia simu Gina sasa hivi na kuuliza ni nani aliyekuwa akikuchukua video?” Vic akauliza kwa ukali. Maya kimya. “Hujapiga simu kwa mtu aliyekuwa akikuuzia unga wewe?” Maya akazidi kuingiwa hofu asijue nani ameshauwa kwa kupiga kwake simu. “Nisikilize Vic. Hapa bado hujaua mtu yeyote yule. Unaweza kuondoka hapa na mtu asijue hata kama ulikuwepo hapa. Na mimi na Jake hatutasema.” Jake akatingisha kichwa kukubaliana na alichosema Maya.

“Unafikiri mimi ni mjinga! Kwa yote uliyojua hapa. Na ujinga huo anaotaka kukwambia Jake sasa hivi, ni kipi kitakachokufanya usinipeleke polisi wewe usiyenipenda kwa kiasi hicho?” “Jake hajaniambia chochote.” “Mimi si mjinga. Tokea muda nilipopigiwa simu kuwa unakuja kwa Jake, mpaka sasa hivi, mlikuwa mkifanya nini kama sio Jake kukiri kuwa mimi ndiye niliyemwajiri akurudishe kwenye ulevi?” Vic mwenyewe akakiri na bastola mkononi.

“Nakuhakikishia hajaniambia kitu. Mimi nilimfuata kwa ajili ya mapenzi. Nilikuwa nina hamu naye.” Maya alikosa chakujitetea, akaishia kujifunga zaidi. “Kwa hiyo mmefanya mapenzi!?” Vic alishituka sana, akauliza kwa sauti ya juu sana mpaka Maya akazidi kutetemeka. “Tulia kwanza Vic.” “Umenisaliti Jake. Mimi ndiye mwanamke ulitakiwa kulala naye, sio huyo.” Akaenda kumgonga Jake na bastola kichwani mpaka akampasua.

“Acha Vic. Unamuumiza.” Akampiga teke Maya. Maya akaanguka. “Naomba msiingie kwanza.” Akaongea Maya kwa kifaransa akimfikishia ujumbe Malcom. Maana alijua kwa ile fujo, polisi lazima waingie. Hofu ilikuwa imemuingia Maya, akajua yupo hapo na wagonjwa wawili wa akili, lakini ilikuwa lazima ampate Tunda kwa garama yeyote ile. Alishatoa mwili wake kwa kufanyiwa mapenzi kwa muda mrefu tu. Maya akagoma kuyafanya yaishe bila kufanikisha hata kimoja juu ya Tunda.

Kwa kesi yake na kaka yake ni kama ilishakamilika. Wakapata ushahidi wakutosha na Vic alishakiri kila kitu na akasema ameua. Akajua Vic hatakuwa tena tatizo maishani. Ameshajikamatisha kwenye vyombo vya usalama. Swali likabaki kama sio yeye aliyemchukua Tunda, nani amemchukua Tunda. Maya akakusudia mtoe huo kweli Vic. Kufa na kupona mpaka kieleweke.

 Bado Jake alikuwa akivuja damu kichwani. “Usimguse Jake. Tafadhali Vic. Mimi sikujua kama ni mwanaume wako ndio maana leo nilimfuata kimapenzi. Nakuahidi...” “Mmefanya mapenzi kwa muda gani? Sitaki unidanganye Jake?” Vic na yeye akaanza kulia kama aliyesalitiwa haswa. Maya akazidi kushangaa.

~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~

Mambo yanazidi kupamba moto, Ritha amerudi pichani. Amefanikiwa kutengeneza jeshi jingine dhidi ya Tunda. Safari hii huko ugenini amekwenda umbali gani? Kama Vic amekiri hajamchukua Tunda, nani anaye Tunda? Endelea kufuatilia...

CONVERSATION

0 Comments:

Post a Comment