Naomi Simulizi |+1 205 767 8163 |naomisimulizi@gmail.com Nilipotea! – Sehemu ya 47. - Naomi Simulizi

Nilipotea! – Sehemu ya 47.

 Kwa Vic, Maya na Jake.

V

ic alishamlazimisha Maya kusafisha damu za Jake pale sakafuni na  risasi ikimfuata nyuma mpaka akamaliza kusafisha na Vic akaridhika kwamba panafaa kwa Net. Akafanya kama alivyoshauriwa na Malcon. Akamfunga Maya aliyekuwa bado akilia, mdomo, mikono na miguu kwa kutumia tape. Akamfungia chumbani kwa Jake. Yeye akaanza kujitengeneza vizuri ili  Net akija amkute msafi. Akaosha uso palepale jikoni na bastola yake mkononi. Akaachia nywele zake vizuri huku akizitengeneza na vidole. Akatoa lile koti la juu jeusi. Akabakiwa na kiblauzi cha ndani. Akafungua vifungo kadhaa juu. Na kupandisha matiti yake juu kidogo ili kumvutia Net.

~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~

Kule alipotolewa Jake, hakukimbizwa hospitalini. Uzuri risasi ilipita kwenye nyama. Akaambiwa hatakufa. Akafungwa kile kidonda ili kisitoe damu zaidi. Akahamishiwa kwenye gari ya CSIS na kukabidhiwa laptop palepale kwenye gari. “Usipompata Mrs Cote sasa hivi. Tunafungua kicho kidonda na tunakupeleka jela.” Wakajaribu kumtisha. Jake akacheka.

“Haunitishi. Na siogopi. Nitafanya kwa sababu nilimuahidi Maya. Maya ni mpenzi wangu. Nitafanya chochote kwa ajili ya..” Malcom akampiga Jake ngumi ya nguvu na ya kushitukiza mpaka akaanguka. Maafisa waliokuwa karibu naye wakamshika Malcom. Roy akamtoa pale ndani ya gari.

“Tafadhali tulia Malcom. Usitake baada ya hii kesi, tukaanza ya kwako.” “Amefanya mapenzi na Maya!” Malcom akapiga ngumi gari. “Najua, na ninaomba utulie.” “Mshenzi kabisa.” “Naomba utulie na tukajaribu kumtoa Maya kwa nyuma.” “Hapo sawa. Ngoja nikamuulize Jake jinsi...” “Hapana Malcom. Nisubiri mimi ndio nitazungumza na Jake. Sio wewe. Wewe utaharibu. Jake anatakiwa kutulia ili amtafute Mrs Cote. Na kama akipatikanika ujue sifa zote zitakwenda kwako.” “Sifa za kusababisha Maya afanywe mapenzi!?” Malcom akauliza kwa hasira.

“Naomba nisubiri hapa nje. Na usiingie ndani ya hii gari. Hata kama nitachelewa. Nisubiri hapa nje. Sawa Malcom?” “Fine.” “Fine?” Roy akataka uhakika. “Nimesema fine! Unataka kusikia nini tena?” Malcom akagomba. “Sawa Malcom. Lakini nataka kukukumbusha kuwa, ulianza vizuri sana, unataka kuharibu mwishoni, hii ni promotion kubwa sana kwako.” “At her cost!? Wote mmemwangalia wakati akilia huku akifanywa mapenzi! Hivi sivyo nilivyotaka kupanda cheo. Na wewe unajua. Itanisaidi nini kukalia kiti ambacho najua nilimtoa mtu kafara!? Nina tofauti gani na wanaume wengine waliokuwa wakimchezea na kumdanganya?” Malcom akamuuliza kwa machungu.

“Maya amefanya kila kitu kwa hiyari yake. Alituma ujumbe kwa wazi kabisa. Akisema kama aliweza kutumiwa mwili wake kwa ujinga, si zaidi sasa hivi ili kumuokoa Mrs Cote! Ule ujumbe ulikuwa ni wako Malcom. Alikwambia wewe. Tafadhali tulia na uache kujihukumu.” Malcom akaondoka pale bila ya kumjibu tena.

Roy akarudi ndani ya lile gari akamkuta Jake akishugulika haswa. Wakamkonyeza Roy kuwa asimsumbue. “Lazima nimuulize njia yakumtoa Maya pale ndani. Lazivyo Malcom ataingia mle ndani kwa kupitia mlango wa mbele, na ninajua nyinyi wote hamtaki kumuona Malcom anaingia matatizoni.” Akamsogelea bosi wao.

“Wote tunajua jinsi Malcom alivyohangaika na hii kesi. Tafadhali mfikirie.” Roy akambembelezea kwa bosi wake. “Mnataka nini?” “Ajue chumba alichofungiwa Maya kama kina madirisha mangapi na lipi linaweza kufunguka kwa urahisi, ili akamtoe. Nitakuwa naye, nakuahidi tutakuwa makini. Na tutafanya hivyo wakati helicopter inashuka. Kukiwa na kelele ndipo na sisi tutavunja dirisha. Kwa haraka na kwa umakinifu.” “Tafadhali kusitokee makosa kama yale ya Toronto, Roy! Msichanganye mapenzi na kazi.” Akaonya bosi wao. “Mimi nimekwambia nitakuwa naye. Usiwe na wasiwasi.” Bosi wake akamtizama. Akamkumbuka Roy na Malcom. Akasita.

“Hapana Roy. Nyinyi nawafahamu vizuri sana. Muongezeni na Dan.” “Mbona kama hutuamini?” “Ukitaka ruhusa yangu, kamchukueni na Dan nje. Lasivyo hapana. Nyinyi akili zenu  wote wawili zinafanana. Mtanifanya niitwe tena kujieleza kama ile safari niliyowatuma Toronto. Hapana.” “Sawa.” Roy akakubali. Akamsogelea  Jake. Na kweli Jake alionekana ametulia. Alimjibu maswali yote Roy huku akiendelea na kazi kwenye ile laptop.

“Sogeeni niwaonyeshe kitu.” Wote wakamsogelea Jake. “Unaona hili gari?” Akawaonyesha gari lililokuwa likiingia chini ya daraja. “Angalia uzito wake hapa kwenye kompyuta kabla halijaingia chini ya daraja kwenye muda huu. Kisha angalia hapa wakati linatoka.” Wote wakaangaliana na kustaajabu.

“Wakati haya mengine, kabla na baada ya kupita chini ya hii tunel, yote yaliingia kwa uzito huu na kutoka kwa uzito huohuo.” Mpaka yule bosi wa CSIS akacheka nakumpongeza. “Man you are Genius!”  “Sasa subiri tulifuatilie. Lakini..” Jake akaacha kila kitu na kumgeukia Roy. “Unakwenda kumuokoa mpenzi wangu au  niende mwenyewe?” Jake akamuuliza Roy.

Kama anayemwambia Roy kuwa aende haraka lasivyo ataacha hiyo kazi ili akamuokoe Maya, yeye mwenyewe. “Wewe ni mwenda wazimu J..” Bosi wake akamvuta Roy nje kwa haraka kabla hajamtibua Jake. “Usirudi humu ndani Roy. Wewe na Malcom. Nisiwaone tena.” “Fine.” Akajibu kwa jeuri Roy nakupiga ngumi gari, kisha akaondoka pale kwenda kumtafuta Malcom.

Hawakumuita afisa Dan kama walivyoagizwa na bosi wao, wakaenda wao wawili kujaribu kumuokoa Maya. Walizunguka mpaka nyuma ya hiyo nyumba. Wakamuona Vic akizunguka ndani huku akipiga piga ile bastola taratibu kichwani mwake.

“Unafikiri na huyu naye ni mzima?” Roy akamuuliza Malcom kwa kunong’ona. “Wote wawili yeye na Jake ni ma Psycho.  Vichaa waliotakiwa wawe hospitali ya vichaa hatarishi kwa muda mrefu sana, ila pesa ndio imewaacha mtaani wakiangamiza raia wema.” Akajibu Malcom kwa kuumia akisikika kulalamika pia. Mara wakasikia mlio wa helicopter, wakajua ndio iliyombeba Nathaniel Cote. Bosi wao akawaacha maafisa wawili pale ndani ya ile gari na mtu wa CSIS upande wa Kompyuta kusaidiana na Jake, yeye akatoka kwenda kumpokea Net.

~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~

“Anakwenda wapi?” Jake akauliza. “Wewe tuliza akili kwenye kazi.” “Kwani na wewe unatatizo gani!? Si nataka kujua tu.” “Amekwenda kumpokea Nathaniel Cote.” Ikabidi tu amjibu. Jake akashtuka sana. “Unamaanisha The Nathaniel Cote!?” Akauliza Jake kwa mshangao. “Ndiyo! Kwani wewe unawafahamu kina Nathiel Cote wangapi?” Yule mtu wa Kompyuta wa CSIS akamuuliza kama asiyetaka azidi kupoteza muda.

“Ooooh! Vic anampenda sana. Anakuwa kama anamwabudu kuliko hata Mungu. Unajua wakati mwingine ananilipa niwe kama Nathaniel Cote?” Wote wakamwangalia kwa mshangao. “Sidanganyi. Anapokuwa ananiita labda kwenye hoteli nifanye naye mapenzi,  anakuwa anakuja na pafyume kama anayojipulizia Nathaniel Cote na lotion zake. Ananiambia nioge kabisa, halafu ananipaka lotion na pafyume kama zake Mr Cote. Halafu ananifundisha jinsi ya kuwa kama Nathaniel Cote hapo kitandani. Namfanyia kama yeye. Hapo Vic anaweza kucome zaidi hata ya mara 4 kwa muda mfupi sana.” Wakabaki wametoa macho. Jake akafikiria tena.

“Hawa watu wanatumia pafyume za gharama zaidi ya mshahara aliokuwa akipokea mama yangu kwa mwezi! Saa zao na...” “Tafadhali rudisha mawazo kwenye kazi tumpate Mrs Cote.” Afisa mmoja akamrudisha kazini. “Kweli. Kila dakika moja inayokwenda bila kumpata, ujue yupo hatarini.” Akaongea Jake na kuendelea kufuatilia gari ya pili aliyodhani itakuwa imemtoa Tunda pale kwenye tunel.

~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~

Malcom na Roy walishamuomba bosi wao kuwa ile helicopter iendelee kuwepo pale kwa dakika tano zaidi. Zikiisha tu ndipo inaweza kuondoka au kuzima ili wavunje dirisha. Kwa hiyo ilipotua tu, Malcome na Roy wakajua wanadakika tano kwa hiyo lazima kufanya kazi kwa haraka. Malcom akachungulia dirishani, akamuona Maya amefungwa akilia sana. Wakaanza kazi yakufungua hilo dirisha kwa kulivunja kwa tahadhari ili wasimshtue Vic huko ndani.

Bosi wa kina Malcom alitoka hapo akikimbilia ilipokuwa imetua ile helicopter ili kumpokea Net na kumpa chakuzungumza atakapokutana na Vic. Maafisa wengine wakawa wanaongozana na huyo kiongozi wa CSIS,  wakashtuka sana kumuona na bibi Cote. Magari ya polisi na CSIS yalikuwa yakimiminika hapo kama nyuki. Hali ikawa imechafuka na kubadilika kuwa ni ‘hostage situation’. Tena hostage mwenyewe ni binti wa Cote! Vyombo vya habari vilishaanza kujaa hapo kuwa  Miss Cote ameshiliwa na risasi ndani na Vic.

Wazazi wa Vic nao walishapigiwa simu kuelezwa hiyo hali, na wenyewe wakawa wapo njiani kuletwa kama Net, ikitokea kama Net akishindwa kumtuliza ili wazazi wake wamtulize na kumtoa pale bila kumdhuru mtu.

Net na Vic .

N

et alivuta pumzi mara kadhaa akajiweka sawa, kisha akaenda kugonga mlango. “Ni Net?” “Fungua mlango Vic.” Vic akafungua mlango kwa haraka. “Kwa nini unabastola mkononi?” Net akamuuliza huku akimpita pale mlangoni. “Sio mimi Net.” “Unaongea nini?” Net akamuuliza taratibu tu. “Najua umenikasirikia Net. Lakini wazo la kusambaza ile video linatoka kwa mama yako. Mimi nakupenda Net, nisingeweza kukufanyia hivyo.” “Kama unanipenda ni kwa nini ulinilevya ili kufanya mapenzi na mimi?” Vic akaanza kulia.

“Naomba utulie Vic.” Vic akaendelea kulia. Ikabidi Net ajirudi. “Niangalie Vic na uzungumze na mimi. Kwanza unafanya nini huku mbali na nyumbani?” “Nilimfuata Jake. Gina alisema Maya amekuja huku.” “Sasa Maya yuko wapi?” “Nimemfungia ndani Net. Maya ndiye anayetutenganisha.”“Tulia tuzungumze.” Vic akajifuta machozi kwa haraa. “Si unajua jinsi Maya asivyonipenda?” “Kwa nini unadhani Maya anakuchukia?” “Anataka kuchukua nafasi yangu kwako Net. Tokea yupo mtoto, hataki mimi na wewe tuwe pamoja.” “Ndio maana ulimtafutia Jake?” Hapo Vic akaanza kulia tena.

“Kwa nini mahusiano yetu unataka yaendeshwe na mama yangu?” “Mama yako alisema Tunda ndiye anatutenganisha mimi ndio mke wako sahihi. Natakiwa tu kukukumbusha.” “Kwa kumchukua Tunda!?” “Hapana Net! Mimi sihusiki kabisa. Huko sihusiki. Na mama yako nilimkatalia kabisa. Naomba niamini Net.” Akazidi kulia akimbembeleza Net. “Mpaka sasa hujaniambia chochote Vic, unataka niamini nini?” “Kuwa sio mimi. Ni mama yako ndiye anayefanya kila kitu.” “Amefanya nini?” Net akaendelea kumuuliza huku amesimama akimtizama kwa utulivu tu.

“Nakupenda Net. Lakini unanipuuza!” “Vic! Tulia, acha kuhama hama kwenye mazungumzo. Focus.” “Kwani hunipendi tena, Net? Hata mama yako anajua kama mimi nakustahili. Nini kimekosekana kwangu? Niambie nijitengeneze niwe mke unayemtaka.” “Vic, huna tatizo lolote. Naomba utulie.” “Sasa kwa nini unanipuuza? Siku unamkaribisha Tunda, hukunitaja mimi. Ulimtaja Troy na Lean tu. Mimi ukanisahau! Ndio maana nilichukia Net. Uliniumiza. Lakini nisingerusha ile video. Nilitaka kukukumbusha na mimi nipo. Niambie kama unanipenda Net.” Vic alikuwa akilia sana.

“Nisikilize Vic. Kwanza unajua huwa siwezi kutuliza akili ukiwa unaongea mambo mengi kwa wakati mmoja tena ukiwa unalia. Wewe unataka nikusikilize au niondoke?” “Usiondoke Net.” “Basi tulia tuzungumze vizuri. Nataka utulie kabisa uniambie kila kitu.” Vic akamsogelea. “Nikumbatie kidogo, angalau nitulie, Net. Au umenikasirikia?” “Sikuelewi Vic. Huwa tunazungumza mambo na tunayamaliza. Kwa nini unarusha mambo mtandaoni nikiwa sijui hata ni nini kinaendelea! Na kwa nini umemchukua Tunda?” Bado Net hakuwa hata amemgusa. Amesimama mbele yake, mikono mfukoni. Mrembo huyo analia mbele yake akiwa amejishusha hasa, anabembeleza.

          “Sio mimi Net. Naomba uniamini.” “Futa machozi. Utulie. Uniambie ni nani?” Net akaonekana yeye anamuweza. Alifanya kila alichomuamuru, tena kwa haraka sana. Akatulia kabisa. Ndipo akaanza. “Unakumbuka mwanamke aliyeletwa kumsaidia kazi Tunda akamkataa?” Net akavuta kumbukumbu akamkumbuka yule mwanamke, Tunda akiwa mgeni kabisa. Akamkataa akisema hataki kufuatwa nyuma.

“Nimemkumbuka sura lakini si jina.” “Anaitwa Malinda. Yule alikuwa mtu wa mama yako. Aliwekwa na mdogo wake, ambaye ni mtaalamu sana wa kompyuta. Anajua jinsi ya kuingia kwenye mitandao na kufanya mambo. Hakuwa hata kwenye ile kampuni ya kupata wafanyakazi. Ila alichomekwa pale makusudi na kwa haraka akiwa ametengenezewa CV nzuri na mdogo wake ili afisa mwajiri wenu, akiingia kule kutafuta mfanyakazi wa Tunda wa kumwajiri, amchague yeye kwa haraka kwa kuwa alikuwa na sifa zote alizokuwa ameandikiwa na mdogo wake. Alizoambiwa na mama yako. Ritha alisema kwa sifa hizo, nilazima akipelekwa kwa bibi yako na afisa mwajiri wenu, atamkubali yeye Malinda na kumpa kazi awe karibu na Tunda.” Net alitamani isiwe hivyo, lakini ni mama yake tena! Aliumia sana.

“Naomba uniamini Net mimi sihusiki. Hata aliponipigia simu kuniambia Tunda alimkataa Malinda. Tu..” “Vic, stay focus. Unaruka mambo na unachanganya habari nyingi kwa wakati mmoja rudi nyuma. Na uache kulia, tafadhali.” Vic akajaribu kutulia. “Nimeshakwambia Net. Yule mwanamke ni mtu aliyekuwa ametumwa na mama yako. Alikuja pale makusudi ili awe karibu na Tunda.” “Ili iweje?” “Ndio ilikuwa akishapata kazi, akafanikiwa kuwa karibu na Tunda, ndio ammpe muongozo.” “Ikawaje?” Net akauliza tena.

“Si ndio Tunda akamkataa wakati yule dada alikuwa na shida sana ya pesa kwa wakati ule! Alifukuzwa kazi katikati ya matibabu, akapoteza insurance na akawa haajiriki tena. Ritha alijua yeye angefaa kwa kuwa kwanza alikuwa nesi, pili alikuwa na shida sana na pesa.” Vic akaendelea. “Ritha aliniambia amempata yeye Malinda ni mtu mzuri, atafanya kila tutakachomwambia, kwa kuwa alikuwa na shida sana na mtoto aliyekuwa akimtafuta kwa miaka mingi. Akashindwa kwa njia ya kawaida ya yeye na boyfriend wake, ndipo wakapata tumaini ya Malinda kupata mimba kwa njia yakupandikiziwa mbegu kwenye hiyo kliniki ambayo inataka pesa nyingi na ni kama Malinda amechelewa. Mbegu zake yeye mwenyewe zinaisha sababu ya umri wake. Yupo desparate, anaweza kufanya chochote ili tumlipe, akafanyiwe matibabu. Sasa si ndio Tunda akamkataa mbele yake. Akaumia sana na ni kama Tunda akawa amempokonya mtoto na mwanaume wake alishachoka kusubiri. Alimwambia hiyo ndio mara ya mwisho. Wasipofanikiwa, anamuacha. Ndio wakapanga. Wakapanga..” Akaanza kujipiga piga kichwani kama aliyesahau anatafuta kukumbuka.

    “Vic, Vic. Niangalie.” “Nakupenda Net.” “Najua. Walipanga nini?” “Mbona sasa huniambii tena kama zamani?” “Kwa kuwa mambo yamebadilika Vic. Mimi sasa hivi nimeoa na ni baba. Unataka nikudanganye?” Vic alilia mpaka akakaa chini. Sivyo Net alivyoambiwa na wale maafisa usalama. Aliambiwa amwambie kitu chakumtuliza ili azungumze wajue anachojua. “Ni bora nijiue nife!” Akajiwekea risasi mdomoni. Hapo ndipo akili zikamrudia Net akakumbuka alichoambia.

“Njoo kwanza Vic. Njoo.” Huku akilia Vic akaanza kumsogelea. “Najua unanichukia sasa hivi.” “Sikuchuii Vic. Kwa nini ufikiri hivyo? Sisi bado ni watu wakaribu sana. Unakumbuka siku yetu ya prom?”  Vic akacheka. “Ulipendeza sana Net. Kila mtu alikuwa akinisifia kuwa nimebahatika.” “Hata wewe ulipendeza na ndio maana tulichaguliwa King na queen.” “Unajua ndio nilijua itakuwa hivyohivyo kwenye maisha yetu yote?” Vic akauliza huku akilia.

“Unafikiri tutakuwa tumechelewa?” Net akamuuliza kwa kumbembeleza. “Sijui Net. Mambo yamechanganyika. Nimeingiwa hofu. Jake naye anaonekana anaweza kutoa siri na kunifanya nifungwe.” “Hawana ushahidi, usiogope. Rudisha mawazo hapa kwangu. Acha kufikiria watu wengine.” “Sijawahi kuacha kukufikiri Net.” Vic akajisogeza kwa Net.

“Nakupenda sana Net. Kuliko nafsi yangu. Kuliko wanaume wote duniani.” “Sasa kwa nini hukuniambia mipango yao juu ya Tunda?” “Kwa sababu mimi nilijitoa mapema kidogo. Yule mwanamke Malinda alitaka amteke Tunda siku atakapokwenda kujifungua  kama hivi. Halafu amfungie, ampandikizie mbegu. Tunda ambembee mtoto wake mpaka miezi 9 ndipo amzalishe yeye mwenyewe. Kisha amwachie Tunda, mama yako. Lakini nafikiri hawakujua kama atazaa kwa operation. Kwa hiyo hii ya kuzaa kwa operation imeharibu.” Net alishituka sana kusikia hiyo mipango ya kinyama dhidi ya mkewe iliyokuwepo kwa muda mrefu tu!

“Jana usiku alinipigia simu kunilaumu ni kwa nini nimeharibu mpaka Tunda kufanyiwa operation! Inamaana itabidi kuongeza gharama yakumuweka ndani Tunda. Kumtibu kwanza mpaka kidonda cha operation kipone ndipo wampandikizie mbegu, abebe mtoto mwingine. Akakataa kusubiri mpaka atibiwe pale apone. Akasema eti Ritha amemwambia kina Cote hawawezi kumuacha aendelee kuwa pale, mtamuhamishia sehemu yenye ulinzi mkali. Kwa hiyo bora awahi kumtoa pale. Ndio akasema yeye atamchukua hospitalini akiwa vilivile mgonjwa na kumtibu mwenyewe mpaka apone. Sasa kwa kuwa mimi ndiye niliyesababisha aanguke na kufanyiwa upasuaji, eti mimi ndio nilipie matibabu yake Tunda akiwa nyumbani kwake yeye Malinda, mpaka apone, na ndipo wampandikizie mbegu.” “Tulia kabisa unielezee vizuri. Futa machozi kwanza.” Vic akatulia. Akawa kama amekumbuka kitu.

“Nimekumbuka Net.” “Nini?” “Anavimbe tumboni ambazo ameambiwa zinakuwa kwa kasi. Kwa hiyo kwa kadiri anavyochelewa kushika mimba ndivyo kadiri ambavyo hatakuja kushika tena mimba. Halafu akaambiwa pia hata akishika mimba, kuna hatari ya akija kushika mimba, mtoto anaweza kutoka mapema sababu ya zile vimbe.”

“Sasa kuja kufanya kazi kwenu ingemsaidia mambo mengi. Mshahara ambao bibi yako alisema atamlipa ulikuwa ni mkubwa na alimuahidi angemlipia pesa ya matibabu pia kama mnavyowalipia wafanyakazi wengine na Ritha naye alisema atakuwa anamlipa kwa kila kazi atakayokuwa akimtuma afanye kwa Tunda. Kwa hiyo alikuwa na uhakika wakupata mtoto na kumtunza pia bila shida. Kitendo cha Tunda kumkataa, inamaana amemkosesha mengi.”

          “Sasa eti Ritha na Malinda walitaka mimi nisubiri mpaka Tunda ajifungue! Mimi nikawaambia siwezi kusubiri mpaka ajifungue kwa sababu itaanza kwanza harusi. Si unakumbuka ilikuwa muone kwanza ndipo muende honeymoon, aje ajifungue? Inamaana Ungemuoa Tunda kanisani wakati ndio ulikuwa mpango wetu mimi na wewe Net, tokea watoto.” Vic akaanza kulia upyaa.

“Ilikuwa ni harusi na honeymoon yetu Net. Lakini umeamua kumpa mwanamke mwingine! Unawezaje Net? Tena kwa honeymoon tuliyokuwa tukiisubiria tokea watoto!?” “Hukuniambia kama bado ulikuwa ukisubiria honeymoon Vic!” “Nilikuwa nasubiria kwa hamu Net. Nataka unioe mimi sio mtu mwingine. Na ndio maana ikabidi kumuwahi Tunda na kumwambia ukweli kuwa sisi tunapendana. Asije kuolewa na wewe. Sisi hatukuwahi kuacha kuwa na mahusiano.” Vic akaendelea kulia.

“Ilibidi kuzungumza naye, Net. Japo mama yako yeye ananilaumu kuwa nimeharibu kila kitu. Tunda hakutakiwa kuzungumza naye, ila kummaliza tu.” “Yeye anataka mumuue!?” “Hapana Net. Sio mimi. Ni yeye mama yako peke yake ndiye anayetaka Tunda afe. Na ndio maana wamepingana hata na Malinda.” “Wamepingana nini?” Hasira zilikuwa zimempanda Net, anatetemeka kabisa.

“Malinda anataka mtoto kutoka kwa Tunda. Unajua Malinda anaamini Tunda ana bahati kuliko hata mimi! Eti anasema hata tumbo lake linabahati ndio maana limeweza kubeba mtoto wako wewe Net, anataka na yeye mtoto wake apitie kwa Tunda, lakini mama yako, Ritha anataka Tunda auwawe.” Net akasikia kuishiwa nguvu kabisa.

~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~

Huku kwa kina Malcom, muda huo wanazungumza, walishafanikiwa kufungua lile dirisha. Roy akambemba Malcom, ndiye akapenya na kuingia ndani ya chumba alichokuwa amefungiwa Maya. Alimkuta Maya amefunga macho akilia sana. Mengi yalikuwa yakiendelea kwa Maya. Amefanywa mapenzi ya muda mrefu tu. Tena sio na Andy mpenzi wa zamani. Na Jake, kichaa kabisa! Na hakufanya kwa kifupi. Kwa kirefu haswa akiwa na uhakika wale afisa hata kama hawakuangalia, basi walijua alichokuwa akifanyiwa muda walipozima kamera.

Maya aliendelea kulia taratibu huku amefungwa mdomo na mikoni. Malcom aliingia kwa kunyata, hata Maya hakuwa amejua kama kuna mtu ameingia hapo chumbani. Akamgusa taratibu huku akimfanyia ishara ya kidole kwenye mdomo kuwa asitoe mlio wowote. Maya akatingisha kichwa kukubali huku akilia. Akamfungua mikono na miguu, akamtoa kwa dirishani. Maya alikuwa akilia sana.

Roy akampokea nje ya dirisha na kumuweka chini. Malcom naye akatoka dirishani. Maya alikuwa akitetemeka huku akilia pembeni. Alijivuta mbali kidogo na Roy. Malcom akamsogelea na kumkumbatia. “Pole sana Maya. Pole na samahani.” Maya aliendelea kulia huku akitetemeka. Malcom akamvuta mpaka kifuani kwake akamkumbatia kwa nguvu huku akimbembeleza. “Lazima tuondoke hapa Malcom. Sio salama. Anaweza akachungulia akatukuta bado tumesimama hapahapa. Naomba tuondoke.” Roy akatoa ushauri. Malcom akaafikiana naye. Wakatoka hapo taratibu huku amemkumbatia Maya.

Walipotokeza tu mbele, polisi wakawakimbilia na kumchukua Maya.  Wakamfuata bibi yake kule ndani walipokuwa wakimsikiliza na kumwangalia Net na Vic. Wakamwambia bibi Cote wamefanikiwa kumtoa Maya. Yule bibi aliruka na kutoka pale kwenye gari kumfuata kule walipompeleka Maya kwenye gari ya wagonjwa ili wamwangalie kama amedhuriwa. “Maya! Baby!” Aliita bibi Cote.

Wazazi wa Vic na wenyewe walishafika eneo la tukio. Walikuwa hapo nje wakisubiri kujua kitakachotokea humo ndani kwa mtoto wao.

Alipotolewa Maya, yule kiongozi wa afisa usalama ambaye alikuwa pale akiendesha mambo kwenye eneo la tukio na viongozi wake wengine wakiwa kwenye simu na kompyuta wakifuatilia kila kitu kinachoendelea, akaamuru waizunguke ile nyumba sasa ili kama kuna lolote litakalotokea wamuokoe Net na kumkamata Vic. Mama yake Vic alikuwa akilia sana huku akiwasihi wasimdhuru mtoto wake. “Vic ni mgonjwa jamani! Amesahau tu kunywa dawa na amekuwa na stress nyingi mfululizo. Tafadhali msimdhuru.” Mama yake akasikika akilia.

Jake!

J

ake naye alishafuatilia ile gari mpaka kwenye nyumba ambayo ilikuwa porini kabisa. Peke yake. Afisa wakawa wameshatumwa huko na helicopter ya usalama ikaelekea kwenye ile nyumba hiyo gari ilipoonekana imekwenda hapo. Na pale tu Vic aliposema Malinda ndio anahusika, na ilikuwa akamfungie Tunda kwake, palepale mtaalamu wa kompyuta huko ofisini kwao ili wasimchanganye pale Jake, akaanza kutafuta anapoishi Malinda. Akaonekana aliishi kwenye apartment moja katikati ya mji, lakini alifukuzwa sababu yakushindwa kulipa kodi.

Wakatafuta walipo wazazi wake. Wakaona walifariki na waliacha nyumba. Kuifuatilia hiyo nyumba, ikaonyesha ni palepale alipopaona Jake gari ile aliyokuwa akiifuatilia kuwa imembeba Tunda, imekwenda. Hapo ndipo wakaamini ndipo alipo Tunda. Ila swali likawa je, bado yupo hai! Wakajua watapata jibu tu maana hapakuonyesha kama ile gari iliondoka pale.

Kwa Net & Vic

N

et ilimlazimu kujikaza ili kuendelea kutafuta chochote kutoka kwa Vic, kitakachosaidia kumpata mkewe. Alijua anasikilizwa na wanaona kila kitu. “Sasa nani yupo na Tunda sasa hivi?” Net akamuuliza taratibu tu huku Vic akiendelea kulia. “Weka hiyo bastola chini nikukumbatie Vic. Usilie.” Kwa haraka sana, akatupa ile bastola na kumkimbilia Net. Net akamkumbatia. “Nyamaza.” “Nimefurahi umenishika Net. Hujui ni kiasi gani nilikuwa na hamu na wewe!”

“Tulia uniambie wapi walipompeleka Tunda.” “Sijui Net. Lakini jana tuligombana sana. Mimi nikakataa kumlipa Malinda pesa, nikakata simu. Ila ninauhakika hawapo kwenye maelewano hata na Ritha. Ila nahisi Malinda na kaka yake pamoja na huyo mwanaume wake, ndio wamemchukua Tunda. Wao wanataka kumtumia Tunda sio kumuua kama Ritha. Ila sipajui kwa kina Malinda na wala sikuuliza ni wapi watampeleka wakishamkamata.” Mpaka hapo Vic hakuwa na matumizi tena na watu wa usalama.

Alishaongea yote, hata ambayo hawakutarajia kuyasikia. Alishakiri maovu yake yote mpaka kuua usiku huo. Akataja wahusika wote, na bahati nzuri vikawa vimeendana na uchunguzi wa Jake. Gari lililotoka chini ya daraja aliloona Jake, likafuatiliwa likawa kweli lipo kwenye nyumba ya wazazi wa Malinda. Kwa hiyo wakachukulia aliyosema Vic yote ni kweli.

Akabaki amemkumbatia Net huku amejificha shingoni. Net akaona afisa usalama wale wa CSIS mlangoni wakitaka kuingia. Akawapa ishara kuwa waingie tu, wakaingia kwa nguvu na haraka, wakamkamata Vic. Vic alilia kama amechinjwa akimtaka Net amsaidie. Bila hata kugeuka nyuma, Net akatoka na kupokelewa na kiongozi wa CSIS.

~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~

“Vipi, upo salama?” “Mmefikia wapi juu ya mke wangu?” Net akauliza bila kujibu swali. “Njoo.” Akampeleka alipokuwa Jake, wakawa wanaangalia kwenye kompyuta. Wale maafisa walikuwa wameshazunguka hiyo nyumba, Net akawaona ni kama wanasubiri amri waingine. “Wanasubiri nini!?” Net akauliza kwa kuona wanachelewa kuingia na kumuokoa mke wake. “Wanasubiri amri kutoka makao makuu. Huo uokoaji mzima unaendesha na mtaalamu wa uokoji huko makao makuu.” Ikabidi Net awe mpole.

“Nimefurahi sana kukuona uso kwa uso Mr Cote. Naitwa Jake.” Jake akataka kumpa mkono lakini Net akakunja uso, akamtizama tu kwa sekunde kadhaa, akarudisha macho kwenye kompyuta bila hata kumpa mkono au kumjibu kitu Jake. Wale maafisa waliona, wakajibaraguza tu.

Kule kwenye nyumba kunakosadikiwa amefichwa Tunda, maaskari walikuwa wamejipanga kila mahali, tayari kwa kuvamia hiyo nyumba bila ya aliyendani kutoroka wasimuone. Nyumba hiyo ilikuwa imezungukwa na usalama! Kuanzia polisi mpaka watu wa CSIS. Helicopter ya CSIS ilikuwa inazunguka juu ya hiyo nyumba, huku magari ya polisi na wagonjwa yakiendelea kumiminika hapo.

Bibi Cote naye akarudi pale ndani ya ile gari aliyokuwepo Net kufuatilia uokolewaji wa Tunda. Kama yupo na kama watamkuta yupo hai. Kila mtu alikuwa na wasiwasi na hilo. Walipopewa tu amri, walivamia ile nyumba kama nyuki. Wangine walikuwa juu ya dari, wengine walivunja madirisha. Kulikuwa na hekaheka ya namna yake. Net na bibi yake wakitizama.

Kwa kuwa ilikuwa usiku walivaa kofia zilizokuwa na tochi. Zinazowasaidia kuona ndani. Ilikuwa giza. Lakini kiongozi wa kile kikoso kilichovamia pale alikuwa amevaa kitu ambacho makao makuu na pale walipokuwa kina Net, wanauwezo wakuona kinachoendelea. Walikata tamaa walipoonyesha juu ni giza kabisa kama hakuna hata mtu anayeishi humo.

“Hakuna dalili ya kuwa kulikuwa na mtu hapa!” Muongoza kile kikosi cha uokoaji pale kwenye ile nyumba, akaongea kwa sauti baada yakuzunguka kila chumba pale juu. Akawa anawaambia viongozi wake huko makao makuu. Jake na yeye akasikia. “Hapana. Angalieni kwa makini. Hilo gari lilionekana limeishia maeneo hayo. Na nimetafuta, hakuna nyumba nyingine kwenye hilo eneo, ila hapo. Lazima kuna basemant.” Jake akabisha akionekana anauhakika.

Kile kikosi na kiongozi wao wakaambiwa watafute kama kuna mlango wakushuka au kuingilia chini. Wakaanza kusaka mlango. “Hakuna.” Yule muongoza kikosi cha uokoaji akajibu. “Dammit!” Jake akagomba kwa sauti na kugonga meza karibu kupasua zile mashine pale. Wote wakashtuka mpaka afisa mmoja akamshika Jake kwa nguvu. 

“Nimesema Mrs Cote yupo hapo. Najua ninachozungumza. Najua kazi yangu. Mimi sio kichaa.” Jake akaanza kulia. “Mtafuteni hapo. Vuteni hata makochi. Angalieni hata chini ya kapeti. Lazima kuna njia ya kwenda chini.” Akaendelea kuongea kwa sauti huku akilia. Net na bibi Cote wakashangaa sana wakimwangalia yeye Jake.

Ndipo bibi Cote akaomba wafanye tu kama anavyoshauri Jake, wasikate tamaa. Wakaanza kutoa hayo makochi na kapeti kama alivyoshauri Jake, kutafuta kama hata kuna tundu dogo tu, lakini hapakuwa na kitu chini. Hawakukuta kitu chochote hata alama kuwa kulikuwa na mlango ukajengewa, ila vumbi tu kuashiria hakuna hata aliyegusa kusafisha hapo kwa muda mrefu sana. “Hakuna.” Kiongozi akarudisha ripoti ila na wenyewe walikuwa wakiangalia pia. Kila mtu akawa amekata tamaa.

Jake akawa kama amefikiria  na kukumbuka kitu. Akajitoa kwa yule askari aliyekuwa amemshikilia. “Nipe mimi hizo headphone. Nimeshajua jinsi yakufika chini.” Wakampa. Akamwambia yule kiongozi kule kwenye nyumba ya kina Malinda, mlango utakuwa kwenye kabati fulani alilokuwa ameliona mwanzoni Jake wakati wanapita humo ndani. “Sukuma kulia au kushoto. Nyuma ya hilo kabati la vitabu ndio utakuwa mlango wakuelekea chini. Ninauhakika.” Wakawa kama wameshampuuza tena. Jake akajua. “Jamani, ninauhakika. Ukiangalia jinsi lilivyowekwa, utagundua linasogea, na limetoka kusogezwa muda sio mrefu.” Jake akashangaza kila mtu pale. Uzuri, walikuwa akisikilizwa na wakubwa wa CSIS pia ambaye ni rafiki wa bibi Cote. Wakaamuriwa wafanye tena.

Wakasogeza tu kulia na kushoto lile kabati  halikusogea. “Hamna kitu.” Akarudisha jibu tena. “Nilimuahidi Maya nitampata Mrs Cote. Siwezi kumuangusha. Tafadhali niaminini. Hapo ndipo ilipo njia.” Kimya. “Dammit! Tumieni akili.” Akagomba Jake. “Sogezeni hilo kabati. Msipofanya, nakuja mimi mwenyewe kufanya. Siwezi kumuangusha Maya. Tafadhalini nisaidieni. Kama sio kwa ajili yangu basi fanyeni kwa ajili ya Maya.” Bibi Cote na Net wakabaki wanamshangaa, Jake alikuwa akilia sana.

“Hakuna kitu hapa.” Akabisha yule muongoza kikosi cha uokoaji kule huku akitingisha tingisha lile kabati. “Upo mlango hapo. Angalieni chini. Wazi panaonyesha hapo ni pasafi kuliko kwengine. Kwa nini nyinyi hamshangai nyumba nzima ni vumbi kasoro hapo! Inamaana pametoka kusafishwa muda si mrefu kufuta alama za mikwaruzo wa hilo kabati.” Jake akasisitiza huku akilia. Alikuwa akitoa mambo ya kina. Kama mtu anayeangalia vitu kwa makini sana. Hakusikika kama kichaa. Mtu asiye na akili. Akamgusa bibi Cote

 “Mike!” Bibi Cote akaita kwenye headphone. Alijua director huyo, kiongozi wa CSIS atakuwa anaona hicho anachoona yeye na kumsikia Jake hukohuko alipo na viongozi wengine. Mike akaitika. “Tafadhali, naomba wafanye tu kama anavyoshauri Jake. Hakuna chakupoteza. Tafadhali.” Bibi Cote akamsihi kiongozi wao. “Naombeni msogeze hilo kabati. Ninauhakika hapo ndipo upo mlango wa kwenda chini na huko ndipo alipo Mrs Cote. Angalieni hata lilipowekwa hilo kabati. Katikati ya sebule na sehemu yakulia chakula! Na nyinyi fikirieni hata kidogo tu! Hakuna nyumba inaweka kabati la vitabu kwenye sehemu kama hiyo. Inamaana wameliegesha mahusudi. Wanaficha mlango.” Akaendelea kuwaaminisha Jake huku akilia.

Ikabidi director wao awaamuru wafanye kama alivyosema Jake.   Ndipo ikabidi walisogeze hilo kabati kabisa. Wakasaidiana kulisukuma kwa nguvu, wakafanikiwa kulitoa kabisa. Kweli  wakaona mlango mdogo sana upo juu ya sakafu, chini ya lilipokuwa limesimama lile kabati, wakajua ndio wakuelekea chini.  Jake akasikika akishukuru mfululizo kwa sauti ya chini. Wakamtizama, kila mmoja akarudisha macho kwenye kompyuta. Alikuwa amefunga macho. 

Kazi ya kufungua ikaanza maana ni kama ulifungwa sana. Haikuchukua muda. Walitumia vifaa maalumu, wakafanikiwa kuvunja na kufungua. Kila mtu roho mkononi. Kiongozi wao akatangulia kushuka. Ilikuwa ngazi ndefu sana kufika chini. Wakaendelea kushuka na risasi mkononi mpaka chini kabisa.

Karibu na ngazi za mwisho, walikuta mwili wa kijana tu, wakizungu. Alionekana amepigwa risasi. Damu nyingi chini. Wakamshika, wakataarifu kuwa ameshakufa. Kila mtu akaingiwa hofu. Zaidi Net. Wakaendelea kushuka kwa tahadhari huku wakitangaza kwa sauti kuwa ni watu wa usalama wanashuka. Kama kuna mtu huko chini, atulie asirushe risasi. Lakini ikawa kimya.

Pembeni tena wakakuta mwili wa Malinda. Naye alikuwa amelala chini damu kifuani na tumboni. Ikazidi kuwaingia hofu. Wakamgusa. Akataarifu yule kiongozi kuwa yupo hai lakini hana fahamu. Pakawa hakuna tena kitu hapo. Chumba walichofikia kikawa kitupu. Machozi yakaanza kumtoka Net.

Katika kukata tamaa huko, wote kimya, mara akasikika mmoja wa wale maafisa kule akiongea kwa sauti.“Kipo chumba hapa nyuma ya ngazi.”  Kingozi wao ambaye amevaa kamera akageuka kwa haraka na wao kweli wakaona kimlango kidogo tu nyuma ya ngazi zakushukia chini.  Wote wakaelekea huko. Wakafungua mlango kwa tahadhari, wakamkuta Tunda amelala, hana hata habari na dripu ya maji mkononi. Wakamgusa. Wakatangaza kuwa yupo hai.

Net akaanza kulia tena. Safari hii kwa kupaniki kama mtoto mdogo. Wakajaribu kumuamsha, hakuamka. Hapohapo bibi Cote akaita. “Mike?” “Nipo.” “Unaona kinachoendelea?” “Ndiyo.” “Naomba akimbizwe hospitalini sasa hivi kwa kutumia helicopter yenu ili tujue ni nini wameweka mwilini kwake.” “Nipo mbele yako.” Akajibu yule director wa CSIS.

Tunda alichomolewa yale maji. Hapo hapo akawekewa maji yakusafisha sumu mwilini, akapandishwa kwenye helicopter akakimbizwa hospitalini. Umbali wa waliokuwepo hapo kina Cote mpaka alipopelekwa Tunda ni masaa mawili na nusu kwa kuendesha gari ya kawaida. Hakuna jinsi bibi Cote angeondoka hapo kwa gari. Ikabidi waite helicopter yao.

Wakati wakisubiri huo usafiri, wote wakaenda kwa Maya, wakamkuta na Malcom akijaribu kumtuliza. “Yupo kwenye mshituko tu. Tunafikiria kumpeleka hospitalini ili akaangaliwe vizuri zaidi.” Mtu wa huduma ya kwanza alitoa hiyo taarifa kwa kina Cote.  “Haitakuwa hapa. Nitataka sehemu ambayo ninauhakika anakuwa na ulinzi wakueleweka na ambapo mimi mwenyewe nipo.” Akajibu bibi Cote. “Usafiri utafika hapa baada ya dakika 15 tu, tutaondoka. Yupo daktari tayari anayemsubiria. Kwa hiyo nashukuru, ila tutandoka. Hatatibiwa hapa.” Bibi Cote akaweka msisitizo.

Maya alikuwa amekaa nyuma kwenye gari ya wagonjwa, amefunikwa na blangeti, ameinama akilia. “Come little sis.” Net akamvuta na kumkumbatia. “Asante sana Maya. Niangalie nikwambie.” Maya akaendelea kulia. Net akambusu kichwani mara kadhaa. “Leo usiku umemrudishia Cote mama yake. Umenirudishia mke wangu na kusafisha jina langu. Naomba katika hayo tu ujifariji kuwa kujitoa kwako kumetoa matunda mazuri.” Net akaongea naye akiwa amemkumbatia, asijue alichofanywa dada yake kupata hayo matokeo mazuri.

“Mbali na hapo sweetheart, umefungua mambo makubwa na mazito yaliyokuwa yakiendelea bila sisi kujua. Umesaidia vyombo vya usalama kwa asilimia kubwa sana.” “Na umesafisha jina lako pia.” Akaongeza Malcom pale alipokuwa akizungumza bibi Cote. Malcom alijua wazi alitakiwa apishe muda huo wa familia, lakini ni kama aliyegongewa misumari hapo. Mtu wa huduma ya kwanza alishapisha. Malcom akabaki hapo katikati yao. Roy alimkonyeza kuwa apishe, lakini alikuwa amesimama hapo na Net na bibi Cote mbele ya Maya kama yeye ni ndugu wa familia.

Roy akamgusa begani. Akasogea pembeni kidogo kama asiyetaka kusumbuliwa. Roy alimjua jinsi alivyo mbishi. Akasubiri kidogo. “Malcom!” Akamuita tena kwa sauti ya chini kama asiyetaka kusumbua. Hata hakugeuka. “Hey Malcom?” “Leave me alone, Man!” Akagomba Malcom mpaka akafanya Net na bibi Cote wawageukie wao wawili. “Nataka kuzungumza na wewe kidogo.” “Hapana.” “Basi labda nikwambie kuwa unaitwa.” “Come on Roy!” Malcom akalalamika. “Sikutanii. Unaitwa.” Net na bibi yake wakabaki wakiwatizama.

Come on Malcom!” Roy akaweka msisitizo. “Nitarudi Maya.” Malcom akaaga na kuzidi kuwashangaza. “Wewe ni nani?” Akauliza bibi Cote. “Malcom.” “No Man! Wewe sio Malcom, wewe ni afisa wa CSIS.” Akakanusha Roy na kujisogeza karibu. “Sisi, ndio tumekuwa na Maya kuanzia mwanzo na ndio tumemtoa ndani alipokuwa amefungiwa na Vic.” Akaongeza Roy na kuendelea tena. “Sisi ni CSIS.”  Akaongeza Roy.

“Hayo ni maelezo marefu sana kwa wakati huu.” Akabisha Malcom. “Hapana si marefu. Kwa jina tu, haisaidii chochote kama hawajajua ni kwa nini tupo hapa!” Akamgeukia bibi Cote. “Hatukutaka kumuacha Maya hapa peke yake. Tukaona..” “Roy na Malcom, ondokeni hapo haraka.” Akawa anawasogelea kiongozi wao. “Yes Sir.” Wakaitika kwa pamoja na kuondoka kwa haraka bila kubisha. “Hawa ni kina Cote, Malcom! Unapozungumza nao lazima uhakikishe unatoa utambulisho wakueleweka ili wa..” “Mimi sijali. Ninachotaka kuona Maya..” Wakawasikia wakiongea kwa kubishana huku wakiondoka.

Bosi wao akatingisha kichwa. “Samahanini sana kwa hilo.” Kiongozi wao akaomba radhi na kumsogelea Maya. “Unajua Miss Cote leo umefanya kazi kubwa sana ya CSIS? Itabidi kukuajiri ili utusaidie zaidi.” “Jake ndiye aliyempata Tunda?” Maya akauliza huku akilia. “Ndiyo. Bila Jake pengine wote tungekuwa tumekwama mpaka sasa na bila heshima yake kwako, angekata tamaa yakufikiria zaidi. Pengine mpaka sasa Mrs Cote angekuwa amefungiwa chini ya basement. Lakini kwa ajili yako, amefikiria zaidi na zaidi mpaka akafanikiwa ku..”  Akamueleza kwa kifupi. Angalau Maya akajisikia vizuri.

“Ila nasikitika kuwa kwa sasa yupo chini ya ulinzi. Jake anatatizo la akili lakini anauwezo mkubwa sana kwenye mtandao na kufikiria. Lazima apewe matibabu na awe chini ya uangalizi ili asitumie akili yake kudhuru.” Maya akanyamaza na kujirudisha kwa kaka yake. “Hapa tunapozungumza wamekwenda kumkamata mtu anayehusika na kumuuzia Vic aina hizo za madawa. Na Vic mwenyewe yupo chini ya ulinzi. Haya, ile nyumba aliyokuwa amefichwa Mrs Cote bado inafanyiwa uchunguzi ili kujulikana na kukamatwa wahusika wote. Hayo yote ni wewe Miss Cote! Naomba ujipe faraja katika hayo.” Yule afisa akaendelea kumfariji. Net naye akaendelea kumbembeleza dada yake na kumbusu.

“Na mama?” Akauliza Net. “Naye amekwenda kuchukuliwa. Lakini mpaka kupatikane ushahidi wa kutosha ili kumuhusishanisha na tuhuma zote hizo. Hawezi kutuhumiwa kwa maneno tu. Na tokea asubuhi amekuwa akichunguzwa upande wa fedha, simu zake na nyumbani. Hawakumkuta na kitu chochote chakutilia mashaka.” “Ritha anaakili sana. Anatakiwa mtu mwenye uwezo wakufikiri kumzidi yeye. Hivi hivi ataendelea kutusumbua tu.” Akaongeza bibi Cote.

“Yupo kwenye uangalizi wetu wa masaa 24. Msiogope. Na nina uhakika ulinzi kwenu wote utaongezwa mpaka watuhumiwa wote wakamatwe na kesi ifungwe.” Wakasikia mlio wa helicopter. Wakajua usafiri wao umewasili. Kina Cote na maafisa wawili wa CSIS wakaondoka hapo kuelekea hospitalini. Maya alimuegemea bibi yake wakiwa njiani. “Am so proud of you, baby girl.” Bibi Cote alimwambia na kumbusu pale kichwani alipokuwa amemuegemea. Maya akajivuta karibu zaidi na kutulia akijifikiria jinsi anavyojisikia mchafu kuanzia akilini mpaka mwilini.

Uzuri ile helicopter iliwashusha juu kabisa ya gorofa la hapo hospitalini. Ilikuwa hospitali nyingine sio ile ya kwanza. Kwa hiyo hawakusumbuliwa na waandishi wa habari. Bibi Cote hakutaka Tunda arudishwe tena kwenye ile hospitali. Kwanza alishawachukia na kuwaona ni wazembe kupita kiasi.

Daktari kiongozi wa pale alikuwepo hapo juu kuwapokea kina Cote na watu wa usalama. “Vipi Tunda?” Akauliza Net na bibi Cote kwa pamoja mara tu walipoingia kwenye lift yakuwashusha chini. “Aliweza kuamka walipokuwa wakimshusha hapa. Alikuwa akilalamikia kichwa kuwa kizito hawezi hata kusogea.” “Unafikiri watakuwa wamempa dawa ya kumdhuru?” Net akauliza. “Ameshatolewa damu, imepelekwa maabara ili kuchunguzwa. Ila tokea kule, daktari wa CSIS, alishamuwekea maji ya kusafisha damu kama kuna sumu yeyote. Hiyo ilikuwa baada ya kutoa hiyo damu ambayo imekimbizwa maabara. Baada ya muda mfupi sana tutakuwa na majibu yote.” Akajieleza daktari.

Lift ilipofunguka tu, wakakuta na director wa CSIS, Mr Mike Underson akiwasubiria pamoja na viongozi wengine. Bibi Cote akamsogelea. “Asante haiwezi kutosha kufikisha shukurani zangu kwako Mike. Lakini jua nakushukuru sana.” Akampa mkono. Akageukia na wale maafisa wengine. Akawapa mkono kwa kuwashukuru kila mmoja wao.

Hiyo ilikuwa ni saa sita za usiku. Inamaana hao watu tokea Tunda anaibiwa asubuhi mpaka hapo ni kweli hakuna aliyekuwa amepumzika. Net naye akiwa amemkumbatia dada yake, akawasogelea. “Asanteni sana kwa kunisaidia kumrudisha mke wangu na kuweza kumpa Cote mama.” Akawapa mkono kila mmoja. Bado Maya alikuwa amemkumbatia kaka yake kwa mikono yote miwili na kujilaza ubavuni kwake, amejificha nusu uso kama anayechungulia kidogo, kimya.  Huku Net amempitishia mkono mmoja wa kushoto begani akimpapasa taratibu.

Mr Underson au Mike kama alivyozoea kumwita bibi Cote, akamsogelea bibi Cote. “Ulinzi utaongezeka hata kwenu. Kwa kuwa bado hatujawakamata watu wote wahusika,  na Malinda bado yupo chumba cha upasuaji. Hawajui kama atatoka chumba cha upasuaji akiwa hai, na hata akitoka hawajui itachukua muda gani kuja kuzungumza na kutaja wahusika wote.” Mr Mike akaendelea.

“Ile nyumba waliyokuwa wamemficha Mrs Cote ipo kwenye uchunguzi wa kina kuona kama tunaweza hata kupata alama za vidole ili tujue mbali na Malinda na mdogo wake, nani mwengine alikuwepo ili ataje wahusika wote. Ritha amegoma kabisa kukiri chochote.” Bibi Cote akatingisha kichwa kwa masikitiko. “Kwa hiyo mpaka sasa hatujui wahusika wako wapi, wangapi, na kama watafanya jaribio jingine lolote au ndio watakimbia kabisa! Hatujui. Sasa mpaka hapo ni lazima kuongeza umakini kwenu wote. Nitaomba mtoe ushirikiano wenu kwa maafisa watakao pangiwa kwenu.” Akasisitiza Mike kwa bibi Cote.

“Hilo halina shida kabisa.” Akajibu bibi Cote. “Lakini Maya lazima aangaliwe na daktari.” Wote wakamgeukia yule afisa wa CSIS waliyekuwa wamekuja naye kwa helicopter, aliyesema hivyo. “Mimi nipo sawa.” Maya akakataa. “Ni utaratibu ambao lazima daktari aidhinishe kwa karatasi. Ndipo tutajiridhisha kuwa upo sawa. Naamini haitachukua muda mrefu.” Yule afisa akajieleza kwa heshima, maana alikuwa mbele ya kina Cote, na bosi wa mabosi wake wote alikuwepo hapo.

“Yupo sahihi.” Mike kiongozi wao akamtetea. “Ni utaratibu ambao lazima ukamilike. Miss Cote alikuwa kwenye mazingira hatarishi. Alipigwa na kutishiwa. Lazima kujiridhisha kama yeye mwenyewe yupo sawa, ndani na nje ya mwili. Hakuna kilichodhuriwa. Na kutaka kuzungumza naye kujua hata hisia zake kama zipo sawa.” Maya akaanza kulia tena. “Nataka na mimi kumuona Tunda kwanza.” Akaongea huku akilia akimwangalia bibi yake. “Please Mike. Amemuhangaikia sana Tunda. Mwache akamuone kwanza, mimi mwenyewe nitampeleka kuonana na daktari.” “Yeah, nafikiri anaweza kusubiri kidogo.” Akimfikishia ujumbe yule afisa ambaye anahusika na Maya.

Daktari akawaongoza alipokuwa amelazwa Tunda. “Kabla hatujaingia ndani kumuona Mrs Cote.” Daktari akawageukia wote. Wakasimama. “Mrs Cote hana taarifa na chochote kilichotokea. Anaonekana muda wote alikuwa amelala. Naomba tusimpe taarifa nyingi za kushtua kwa wakati mmoja.” “Inamaana hajui kama alitekwa nyara!?” Akauliza bibi Cote kwa mshangao.

“Hana taarifa hata kama yupo hospitali nyingine. Ametaka aletewe mtoto wake ili amnyonyeshe. Hilo tu. Na anaonekana katika hilo hawezi kusubiri. Naomba mjaribu kumtuliza mpaka tujue kwa hakika majibu ya damu yake.” Akasisitiza yule daktari. “Hiyo imeeleweka. Nitawaambia hata maswali isiwe leo. Wampe muda kabisa.” Akaongeza Mike, director wa CSIS. “Ila kesho kwenye saa nne asubuhi, tafadhali naomba atoe ushirikiano ili kusaidia vyombo vya usalama kwa chochote kile.” “Lakini umesikia kuwa hakuwa na taarifa ya kutekwa kwake nyara?” Net akakanusha.

“Mr Cote!” Mike akamgeukia Net vizuri. “Nimuhimu sana yeye mwenyewe kujua na kutuambia kile ambacho anafahamu. Hata kama nikidogo sana. Huwezi kujua kitasaidia vipi usalama wake na wenu. Bado kesi yake haijafungwa. Watuhumiwa hawajakamatwa. Lazima kuweka kikomo katika hili ili kujiridhisha.” Net akamwangalia bibi yake. “Ni sawa mpate kwanza ruhusa kutoka kwa daktari atakaye kuwa akimtibu? Yeye ajiridhishe kwanza kama Tunda yupo tayari kwa kupokea taarifa kama hizo. Tafadhali Mike. Mmefanya pakubwa sana. Tusije tukawa tumemuokoa kutoka kwenye mikono ya watu wabaya, tukampoteza kwa pressure kwenye mikono yenu.” Bibi Cote akaingilia. “Hiyo inaeleweka. Tutawasiliana na uongozi wa hospitali kwanza kabla ya mahojiano.” “Nashukuru.” Hapo wakakubaliana na kuingia.

Walimkuta Tunda amelala. “Mmempa tena dawa za usingizi?” Bibi Cote akauliza. “Hapana. Hizo..” Tunda akafungua macho. “Nana!” Akaita taratibu, wote wakamsogelea. Bibi Cote akamkumbatia. Net na Maya wakabaki hawajui kama bado amewakasirikia au la. “Namtaka mtoto wangu ili nimnyonyeshe. Hakuna anayenisikiliza!” Tunda akalalamika na machozi yakitoka. Net akamsogelea. “Unajisikiaje?” “Nasikia kichwa kizito. Cote yuko wapi?” Tunda akauliza huku akionekana anapata shida kugeuka.

“Nisikilize kwa makini Tunda.” Bibi Cote akamshika mkono na kuubusu. “Cote yupo salama kabisa. Aliruhusiwa kurudi nyumbani.” “Kwa nini walimruhusu bila mimi? Anakula nini huko?” Tunda akaanza kulia tena. “Nitapiga simu, umuone akiwa amelala. Anaendelea vizuri kabisa. Asubuhi sana nitamleta.” “Kwa nini mimi nisiende nyumbani kumfuata? Sitaki kumuona kwa video, Net. Nataka kumnyonyesha na nimshike mwanangu.” “Daktari ameomba usiku wa leo upumzike kabisa. Kesho utakuwa naye. Na atarudi hapa mpaka siku utakayoruhusiwa.” Tunda akafunga macho wakamuona analia.

“Yamebaki masaa machache sana papambazuke. Vumilia kidogo tu.” Bibi Cote akambusu kichwani huku akimsihi. “Namtaka mtoto wangu, Nana. Siwezi kulala bila mtoto wangu.” Tunda akaendelea kunung’unika huku akilia taratibu. “Subiri nikuthibitishie kuwa mtoto yupo sawa Tunda, ili na wewe utulie.” Chumba kilikuwa na watu zaidi ya watano, wakiwepo hao viongozi wa CSIS. Wote walinyamaza. Tunda akaendelea kulia taratibu.

          Net akapiga simu kwa Carter na kuambiwa ampelekee simu huyo nesi aliyeachiwa mtoto nyumbani. Kwa bahati mbaya akamkuta mtoto analia, na Carter alikuwa ameshaweka video. “Kwa nini analia!?” Net akauliza. Bibi yake na Maya wakasogelea ile simu. “Ameamka muda sio mrefu. Nilikuwa nikimbadilisha diaper sasa hivi, kisha nimpe maziwa.” Akajibu yule nesi. “Mnyanyue hapo, mshike kidogo.” Net akaongeza. “Namtaka mtoto wangu Net. Kamlete tu.” Tunda aliendelea kulia taratibu. “Au mimi mwenyewe niende tu.” Tunda akajaribu kukaa ndipo yule daktari ikabidi amsogelee.

“Mrs Cote! Mrs Cote.” Akamuita taratibu. “Unakumbuka umetoka kwenye operation masaa machache tu yamepita? Na unakumbuka ulilalamika kichwa kinauma sana huwezi hata kukinyanyua?” “Sasa hivi naweza.” Tunda akataka kukaa. Akamshika. “Japokuwa mimi si daktari, ila nashauri akachukuliwe huyo mtoto, aletwe hapa karibu na mama yake, ili kuweza kumtibu. Sidhani kama kunakuelewana tena bila huyo mtoto kuwepo hapa. Huo ni ushauri wangu tu, kama mzazi.” Akaongea Mike kwa kujihami.

“Namtaka mtoto wangu, Nana.” Tunda akasisitiza. “Sisi wote tupo hapa halafu mnamuacha na mtu mgeni kabisa hata hajawahi kumsikia! Sio sawa kwa Cote. Atakuwa akitulilia sisi.” Tunda akalalamika. Asijue hekaheka waliyopitia kina Cote mpaka muda huo. “Basi nakwenda kumchukua Tunda. Naomba utulie ili nikirudi na mtoto, kichwa kiwe kimetulia. Sawa?” “Asante Net.” Akashukuru na kurudi kujilaza vizuri. Bibi Cote akambusu tena. Net akaondoka. Maya alikuwa akifuta tu machozi.

“Samahani Nana. Lakini namtaka mtoto wangu. Umemsikia alivyokuwa akilia.” “Naelewa. Baada ya muda mfupi sana atakuwa hapa. Naomba jaribu kufunga macho ulale kidogo.” Tunda akafunga macho. Maya akaanza kumfuta machozi. Tunda akafungua macho wakabaki wakiangaliana. Maya akaanza kulia. “Nisamehe Tunda. Usinikasirikie.” Maya akaongea kwa uchungu. “Unajua ninavyokupenda. Siwezi kukuumiza hata kidogo.” Tunda akafunga macho wakamuona machozi yakimtoka. “Sikukusudia kukuumiza. Najua na wewe unajua.” Maya akaendelea kumbembeleza. Akahisi anamshika mkono. Maya akajilaza hapo kwa Tunda na kuzidi kulia. “Nisamehe.” Maya akaendelea kulia huku amemugemea.

Tunda akapitisha ule mkono ambao hauna dripu akamkumbatia. Asijue umbali aliokwenda huyo Maya, kumfanya awepo hapo. Chumba kizima kimya. Wakatulia kidogo huku Maya amemkumbatia na yeye. Wakatulia kwa muda.

“Niliingiwa na wasiwasi. Unajisikiaje?” Maya akamuongelesha taratibu. “Kichwa tu ndio kipo kama nimebeba kitu. Sijui kwa nini!” Tunda akajibu taratibu. “Kidonda je?” Maya akamuuliza tena. Tunda akafikiria kidogo. “Hakina maumivu sana, mpaka nikohoe. Umemuona Cote?”  Wakacheka. “Ni mzuri kama wewe Maya! Nilikwambia lazima mnafanana.” Maya akacheka tena. “Ana macho yangu.” Akajisifia Maya. “Sio ya Net?” Tunda akamuuliza huku wakicheka. “Hapana. Hafanani na wewe wala Net.” “Maya!” “Kweli Tunda. Muulize Nana.” Kidogo pakatulia hapo ndani ndipo wakaanza kumsalimia na kumpa pole na hongera ndipo Tunda akajua kumbe pale ndani kulikuwa na watu wengi! Hakuwa na wasiwasi wa kwa nini wamjalie vile, akaelewa kwa kuwa ni kina Cote, lazima ni watu wakubwa wamefika hapo kumuona, asijue janga linaloendelea.

 Baada ya muda kidogo wakaaga wale maafisa, bibi Cote akasema anatoka kuwasindikiza. Akamgeukia daktari. Akamkonyeza watoke naye nje. “Kwa nini kichwa chake kinakuwa kizito!?” Akaumuuliza dokta mara tu walipotoka. “Inaonekana aina hizo za dawa walizompa, ni kali sana kwake. Alikuwa akitumia kileo chochote?” “Sidhani hata kama alishawahi kunywa pombe. Ni kama aliniambia hakuwahi kunywa pombe. Sina uhakika sana.” Bibi Cote akamjibu yule dokta.

“Inaweza ikachangia. Na pia majibu ya damu yake, yatatupa jibu ni aina gani ya madawa waliyokuwa wakimpa kumfanya alale kiasi cha kupoteza fahamu kabisa.” “Hakuna jinsi yakuharakisha hayo majibu?” Akauliza bibi Cote. “Tafadhali fuatilia. Sitaki mtoto aje, aanze kilio cha kutaka kumnyonyesha mtoto wake, halafu mimi ndio niwe mtu wakumzuia! Hapana. Nisaidie tujue kama ni sawa kunyonyesha.” Bibi Cote akasisitiza. Yule daktari akaondoka kwenda kuweka msisitizo huko maabara.

Alipoagana na Mike pamoja na maafisa wengine bibi Cote akarudi ndani. Ni kweli safari hii kulikuwa na ulinzi mkali. “Jaribu kulala kidogo Tunda, ili kichwa kitulie.” Bibi Cote alishamsogelea na kumbusu. Tunda akafunga macho. “Tutatoka kidogo, baada ya muda tutarudi.” “Sawa.” Tunda akajibu bila kufungua macho. Hapo hapo akalala, Maya na bibi yake wakatoka.

~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~

Ilikuwa lazima Maya akapimwe ili kujiridhisha kuwa yupo sawa. Bibi yake akamsindikiza. “Tunda amenisamehe.” Bibi yake akamwangalia tu na kunyamaza. Hata yeye katika hilo walimtenda vibaya. “Usinikasirikie Nana! Vic alitutega.” Maya akaanza kulia. “Hapana Maya. Mlipaswa kuniambia. Hata ingekuaje, mlipaswa kuniambia, pengine hiki kilichotokea leo, kisingetokea. Tungejua hila ya Vic mapema sana. Kuwa huwa anatumia dawa kuwalevya na kuwasahaulisha.” Bibi Cote akaendelea kwa ukali kidogo.

“Leo umejiingiza hatarini kwa sababu ya kunyamazia jambo lililoonekana ni kama lakupuuza, kumbe limebeba hila kumbwa sana!” “Nisamehe Nana. Hata wewe ungemuona vile Net alivyoingiwa na hofu siku ile, usingethubutu kusema.” Maya akawa kama anakumbuka. “Aliingiwa na hofu sana. Alishindwa kula siku nzima, akawa kama mgonjwa.” “Ila itamgharimu sana. Atajieleza vipi kwa Tunda akamuelewa?” “Kuwa alilevywa!” Maya akaongea kirahisi tu.

“Kwa nini asimwambie na Tunda amekuwa pale nyumbani kwa miezi miwili sasa? Atamuamini vipi na yeye hakuwepo wakati Vic akikiri kama alimlevya? Vic amemwambia maneno mazito sana ambayo hayaondoki kwa neno ‘Nisamehe’.” Maya akanyamaza akifikiria.

“Utamfanya nini mama?”  Baada ya muda Maya akauliza. “Nitahakikisha anapata kinacho mstahili. Kwa kuwa nilimfuata Tanzania na kumuonya. Kuja kumfuata huku Tunda, na kupanga mauaji yake kwa siri, hilo ni kosa ambalo sitamsamehe. Hata akitumia akili vipi, safari hii nitahakikisha anapata kinacho mstahili. Acha wewe utibiwe na Tunda atoke hapa.” “Utafanyaje?” Maya akauliza.

“Nguvu ile ile niliyotumia kumtafuta Tunda na kufanya wakubwa wote wa nchi waweke akili zao kwenye kumsaka Tunda, ndivyo nitakavyo hakikisha ninatumia nguvu hiyohiyo mpaka kumtia Ritha nguvuni. Yeye na wote wanaohusika.” Akaapa bibi Cote. Maya akafurahia sana. Alimjua bibi yake huwa haropoki. Kwa hiyo mama yake lazima akamatwe.

Kwa Mara ya kwanza Net na familia yake yote.

N

et aliingia na mtoto wao, Tunda akiwa amelala kabisa. Kwa kuwa walimwambia wametoka kumpa dawa za maumivu ya kichwa, hakutaka kumuamsha. Mtoto akatengenezewa kitanda palepale ndani ya kile chumba. Akalazwa akiwa alishapewa maziwa ya kopo tu. Ameshiba. Net alisimama pale akiwaangalia Tunda na Cote jinsi walivyolala, baada ya kuachwa peke yao, asiamini vile hata mipango iliyopangwa kwa umakini sana na pesa nyingi jinsi inavyoweza kubadilika na kuvurugika kabisa. Kufumba na kufumbua kutoka kwenye maisha yaliyojaa heshima sana na kusifiwa, Net anajikuta yu uchi mitandaoni akifanya mapenzi nje ya ndoa ya mwanamke waliyetoka kuvishana sifa mbele ya umati!

Net akamwangalia vile Tunda alivyolala. “Sidhani kama Tunda atakuja kunielewa?” Akawaza Net. Akamgeukia mtoto wake. Cote alikuwa amelala na yeye. Akakumbuka jinsi walivyokuwa wakimsubiria huyo mtoto kwa hamu. Alivyokuwa akitangazwa mitandaoni na kwenye vyombo vya habari akitabiriwa makubwa na mazito kama ujio wa Mkombozi kutoka mbinguni. Leo amefika hakuna hata anayemzungumzia ila kashfa yake yeye baba mtu, akifanya ngono na mwanamke ambaye si mama yake!

Net aliweka mikono kichwani na kuvuta pumzi. Yalikuwa masaa machache hata hayakuzidi 50, lakini yalibadilisha na kutingisha maisha yake vilivyo. Mpaka hapo hakuwa akijua kama ndoa ipo au la! Tunda ataamua nini juu ya ndoa yao. Hakujua kama usiku ule alichukuliwa video ndio maana akaamua kunyamazia swala la kulala na Vic. Alijua wale walioona Vic akiamka pale kwao. Carter na Maya, ambao alishawaaminisha hakuna lililotokea huko chumbani, watanyamaza wasiseme kwa mtu. Kwa hiyo hakutaka mtu mwingine ajue, asijue kama Vic aliondoka na ushahidi mzito. Anakanusha vipi aliyosema Vic, kama alishindwa kueleza kisa chenyewe kabla!

Net akaenda kukaa kwenye kochi pembeni ya kitanda cha Tunda na kilipowekwa kitanda cha mtoto wao. Lile kochi lilikuwa na uwezo wa kugeuka kitanda, na alijua wazi mashuka na mto wa ziada vipo hapohapo kwenye kabati la pembeni, lakini alishindwa hata kulala. Akakumbuka maelezo ya Vic kuhusu ushiriki wa mama yake. Akainama huku ameshika kichwa, Net hakujua kama hatari ilikuja mpaka ndani ya nyumba yake wakati anamzungushia mkewe ulinzi anaolipia kwa pesa nyingi sana nje. Hasira juu ya mama yake ikawaka tena ndani yake. Akajiambia nilazima kuweka kikomo kati yake, familia yake na mama yake.

Wakaingia Maya na bibi yake kwa kunyata. “Vipi Maya?” Net akauliza. “Kila kitu kipo sawa.” Akajibu Maya na kumsogelea. “Pole Net. Naamini kila kitu kitakuwa sawa.” “Sijui Maya. Sidhani.” Maya akaenda kukaa pembeni ya kaka yake. Bibi Cote akamsogelea Tunda. Akambusu kichwani. Kisha akamsogelea Cote. Akamfunika vizuri. Akabaki amesimama na kumtizama yule mtoto bila kuongeza neno. Wakakaa kimya kwa muda. 

Maya akambusu kaka yake shavuni. “Nakupenda Net.” “Na mimi nakupenda na ninakushukuru kwa kunipigania mimi na Tunda. Sitasahau hilo.” Maya akambusu na kumkumbatia.

Walikuwa wakinong’ona. “Nikwambie kitu?” Maya akamuuliza huku akimnong’oneza. Net akamgeukia mdogo wake. “Sasa hivi unaweza ukaona ulimwengu mzima umekugeukia wewe. Umeingiwa hofu. Kila mtu hakuelewi umewezaje kufanya hivyo. Hata watu wako wa karibu watakuwa hawakuelewi. Kila kitu kinakuwa kimegeuka. Zaidi maisha na mipango. Lakini unajua nini?” Net akajifuta machozi huku akimsikiliza Maya.

“Kumbuka. It always gets better. Be strong, because things will get better. It may be stormy right now, but it never rains forever. Haitanyesha daima. Yoote yatapita na kukupa sura mpya ya maisha. Hutakuwa sawa, lakini nakuhakikishia haya yote yamekupata ili kukufanya uwe bora zaidi.” Net akamuegemea Maya. “Lini umekuwa na hekima hivi!?” Net akamuuliza na kumbusu Maya. Wakacheka huku wakilia. Bibi yao kimya. Macho kwa Cote. “Asante Maya.” “Karibu. Sasa acha mimi nimrudishe Nana akapumzike. Kama kwetu imekuwa ngumu hivi, najua Nana zaidi.” Maya akambusu na kusimama.

Net akabaki amekaa ameinama. Aliogopa hata kumtizama bibi yake. Wawili hao hawakuzungumza tokea Net akiri ni kweli alilala na Vic pale nyumbani kwao, tena akiwa ameoa! Bibi Cote akatoka bila hata kumsemesha Net. Na Net naye hakutaka hata kumsemesha. Akaona anyamaze na kumuacha kwanza. Pengine akienda kulala, kesho yake atakuwa sawa. Maya akambusu tena kichwani vilevile alivyokuwa ameinama pale kwenye kochi. Akatoka na yeye.

Akaanza kusinzia. Akaona ajiegemeze kwenye kochi. Baada ya kama masaa mawili mbele akiwa amepotelea usingizini akasikia Cote akilalamika kwenye kitanda. Akaamka kwa haraka ili Tunda asiamke. Akamtoa kitandani. Cote akazidi kulia, Tunda akaamka. “Mlete nimnyonyeshe.” “Nisubiri nakuja sasa hivi.” Net akatoka kwa haraka na yule mtoto akilia. Akaenda kutafuta wauguzi. Akamuacha Tunda haelewi.

Akakimbilia mapokezi. “Majibu ya mke wangu yakoje? Anataka kunyonyesha.” “Daktari alikuja kuzungumza na wewe akakuta mmelala. Lakini kila kitu kipo sawa. Amesema anaweza tu kunyonyesh..” Kabla hajamaliza, Net akarudi haraka chumbani kwa mkewe.

“Kuna nini, kwa nini unakimbia na mwanangu?” “Nilienda kuzungumza na daktari kama unaweza kunyonyesha.” Tunda akakunja uso akampokea mtoto wake. Akamuona anatabasamu mara alipoona sura ya mtoto wake. Akambusu mtoto wake zaidi ya mara moja. Nesi akaingia na kitu cha kumsafishia. “Lazima kukusafisha kabla hujanyonyesha.” Tunda akakubali.

Net akamchukua mtoto tena. Akaanza kumbembeleza wakati mama yake akishugulikiwa. Yule nesi akamsafisha Tunda vizuri kifuani. Akambadilisha na nguo. Akanyanyua kitanda vizuri, akarudishiwa mtoto wake. Akamuweka kwenye ziwa, Cote akaanza kuvuta. Yule nesi akacheka jinsi Cote alivyonyamaza gafla na kudaka nyonyo ya mama yake. “Labda alikuwa na njaa.” “Labda.” Tunda akajibu taratibu huku akimtizama. Nesi aliondoka na kuwaacha.

Net bado alikuwa amesimama. Tunda macho na yeye kwa mtoto akimpapasa taratibu huku akimwangalia. “Unajisikiaje?” Net akauliza, lakini Tunda hakujibu wala kumtizama. “Nakupenda Tunda. Nakupenda sana mke wangu.” Net akasikika kwa sauti iliyojaa hofu. “Hata kama sasa hivi haileti maana tena, lakini nataka ujue. Na sitaacha kukwambia hivyo.” Tunda akajifuta machozi. “Ukiwa na Cote, usipokuwa na Cote, nakupenda wewe Tunda. Na nilikuchagua wewe kabla hata Cote hajaja kwenye maisha yetu. Naomba usije kulisahau hilo.” Tunda kimya. Net akaenda kukaa kwenye kochi.

Tunda akanyonyesha mpaka akasikia tena maziwa yanasisimka, akajua yanaanza kutoka. “Naona yanaanza kutoka!” Akaongea Tunda taratibu akisikika kuhamasika. Akajiangalia ziwa jingine akaona yanaanza kuchuruzika. Akaanza kucheka huku akilia. Net akasimama. “Kwani yalikuwa hayatoki!?” Net akauliza. Tunda akatingisha kichwa kukataa huku anamwangalia mtoto wake wala sio Net. Akaendelea kujifuta machozi.

Cote alianza kusinzia, Tunda akajitahidi kumwamsha ili anyonye asilale na njaa. Akamuhamishia kwenye ziwa jingine. “Unafikiri hajashiba?” Net akauliza. “Naona nyonyo linamliwaza tu ndio maana analala. Lakini maziwa sio mengi. Nahisi kesho yataanza kutoka mengi.” Tunda akajibu taratibu macho kwa mtoto wake. “Siamini kama na mimi nimeshika mtoto wangu mwenyewe!” “Hongera Tunda.” Tunda akanyamaza hakuitia pongezi ya Net. Net akabaki amesimama akimtizama na kutamani aongeze neno jingine, ila akaona atulie.

Baada ya nusu saa nesi akarudi. “Bado ananyonya tu!” “Angekuwa amemaliza, ila mimi ndio namwamsha kila wakati nataka aendelee kuvuta, ashibe vizuri.” Wakacheka taratibu. “Nahisi atakuwa hajashiba! Maziwa hayakuwa yakitoka mengi.” “Hata hivyo na yeye tumbo lake bado ni dogo. Kile kinachotoka, kinamtosha kabisa. Usiwe na wasiwasi.” “Unafikiri hivyo?” Tunda akauliza taratibu akiwa na wasiwasi. “Najua hivyo. Kwa sasa tumbo lake ni dogo sana. Linapanuka kutokana na anavyokua. Kwa hiyo hata akipata kidogo tu, inatosha.” “Ataweza kulala muda mrefu kwa chakula kidogo hivyo!?” Yule nesi akatabasamu.

“Lazima ujue kila akijisaidia atataka abadilishwe. Atalia. Amezaliwa bado hajui mchana na usiku. Bado anaji adjust na hali ya hewa na mazingira, atalia. Ndio maana atakuwa akiamka kila baada yamuda mfupi. Lakini si kwa kuwa anatatizo kubwa. Hapana. Anajizoeza mazingira mapya.” “Oooh!” Tunda akaitika na kumwangalia mtoto wake.

“Ila hivyo unavyopenda kunyonyesha imetugusa wauguzi wote hapa. Kila mtu anakusifia. Kina mama wengi siku hizi au huku hawapendi kunyonyesha. Ukiendelea hivyo itamsaidia sana yeye. Maziwa hayo ya mwanzo yanavirutubisho muhimu kwa mtoto. Nakupongeza.” Tunda akacheka wala asielewe inakuaje usitake kumnyonyesha mtoto uliyemzaa mwenyewe! Jinsi yeye alivyokuwa na hamu yakunyonyesha, kwanza alihisi Cote ni mvivu, hamtendei haki.

Akampima pressure. “Vipi, ikoje?” Akauliza Net. “Sio mbaya. Kesho watamtoa catheter ili ajaribu kutembea.” “Nakuoga. Natamani kuoga maji mengi. Nahisi nitajisikia vizuri zaidi.” Tunda akaongeza. “Basi nitamwambia dokta. Akija kukuona mtazungumza.” “Asante sana.” Yule nesi akatoka na kuwaacha wote macho kwa mtoto.

“Nilitamani Cote aje akute kuna amani kati yetu!” Net akajiongelesha. Tunda hata hakujibu. “Naomba nikupokee.” Tunda kimya. “Unatakiwa kupumzika Tunda. Mweke chini upumzike.” Kimya. Akamuona anaweka mto vizuri, akamuweka mtoto wake kifuani, akajilaza akiwa amemkumbatia mtoto wake. Akafunga macho. Net akaenda kumbusu kwenye kipanda uso. Akabaki anamwangalia. Tunda hakufungua macho, lakini machozi yakaanza kutoka. Net akaweka uso wake pembeni ya shavu lake. Akabaki amesimama lakini amejificha uso hapo kwenye shavu la Tunda. Alipolala, akamtoa mtoto taratibu na kwenda kumlaza. Angalau na Net naye akarudi kulala mpaka pakapambazuka.

 Asubuhi baada ya kutekwa.

 Saa moja asubuhi nesi tena akaja na daktari. Wakampima Tunda. Kila kitu kikaonekana kipo sawa. Wakamtoa catheter na kumruhusu kwenda kuoga.Alitoka kuoga, Maya na bibi yake walikuwa pale wameleta supu. Baada ya salamu, Tunda akiwa amepoa, sio kama zamani. Kila bibi Cote alipomuuliza kama anamaumivu mahali, alimwambia yupo sawa. “Mbona kama kuna kitu unataka kuniambia lakini unasita?” Bibi Cote akamuuliza. Tunda akafikiria kidogo. Akamwambia ni kweli kuna kitu anataka kuwaambia.

“Ni nini?” Bibi Cote akamuuliza tu taratibu. “Daktari alipita alfajiri. Amenipima na majibu ya maabara yote yanaonekana nipo mzima kabisa.” Akatulia kidogo. Akainama. Na kujifuta machozi. Wote kimya. Maya, Net na bibi yao walikuwa hapo. Wote wasiwasi wakitaka kujua nini kinafuata. “Ni nini Tunda?”  Bibi Cote akauliza tena. “Nilitaka kurudi nyumbani Tanzania.” Tunda akaongea huku akilia. Kimya kilizuka cha gafla. Kama waliopigwa na ganzi.

“Naomba nirudi nyumbani tu.” Net akainama na kushika magoti kama aliyepatwa na kizunguzungu cha gafla. Maya akaanza kulia taratibu. “Nikuulize kitu Tunda?” Bibi Cote akamuuliza taratibu. “Unafikiri kama isingekuwa Vic, au kabla ya kisa cha Vic, ungeondoka?” Tunda akanyamaza. “Niambie ukweli Tunda.” “Naomba nikujibu hilo wakati mwingine nikisharudi nyumbani na kupumzika. Ila naomba niwatoe wasiwasi. Sihitaji chochote kutoka kwenu, zaidi ya nauli tu. Sitadai chochote na wala sihitaji chochote.” “Unamaanisha unaachana na Net!?” Bibi Cote akauliza kwa mshangao sana.

“Nilikuja huku kwa ajili ya Net, Nana. Nahitaji muda wakujijenga upya. Kisha nitawatafuta. Nahitaji kusafisha akili zangu pengine kujipanga upya na kumpa nafasi Net yakufikiria. Ni kweli nilitoka jela nikiwa mjamzito. Asingeweza kuondoka bila kujua hatima ya mtoto wake. Lakini nafikiri Net anahaki ya kuwa na furaha Nana!" Tunda akaendelea taratibu tu huku akijifuta machozi.

“Naomba niwahakikishie kwangu hamtampoteza Cote. Mpo huru kuja kumuona muda na wakati wowote, na kama mkitaka niwe namleta, nitamleta muda na wakati wowote ule.” “Na mimi Tunda?” Maya akauliza huku akilia. “Na taasisi niliyokuachia? Unafikiri mimi nina akili kama za Vic? Unafikiri mimi nilikurupuka? Wale wanawake na watoto wao wanakuhitaji Tunda. Ile taasisi ni yako. Ukirudi Tanzania utaendeshaje ikiwa huku?” Tunda akazidi kulia sana. “Nilipokuchagua si kwa sababu yakuambiwa na Net. Ni kwa kuwa najua unastahili. Usikubali Vic akakukimbiza!” Bibi Cote akasogea karibu.

“Nilikwambia nini? Kila maamuzi unayofanya usifanye kwa hisia. Kwa sasa hisia zako zimeumizwa. Utafanya maamuzi kutokana na hisia zilizoumia. Wakati wote, unaposema nakwenda nyumbani iwe ni pale nilipo mimi. Unanielewa Tunda?” Bibi Cote akaweka msisitizo. “Ile nyumba ni kubwa sana. Tutarudi wote nyumbani. Utapata sehemu yako nzuri na yakutosha kupumzika na kulea mtoto wako vizuri na kwa utulivu. Mwachie uhuru wake Net. Akafanye kile anachokitaka na yeyote. Hata mimi sijali tena. Mwache achague yeyote anayemtaka. Hata mimi nimejiapia sitahangaika naye tena.” Net akajua ule ujumbe alikuwa akipewa yeye si Tunda.

“Usiwahi kufikiria kuondoka Tunda. Unamajukumu mengi sana mbali na kuwa mke wa Net. Na nilikwambia, kuanzia sasa, kila maamuzi unayochukua, fanya ukimfikiria mjukuu na watoto wa Cote. Unanielewa?” Tunda akatingisha kichwa kukubali huku akifuta machozi. Akafurahi kuona bibi Cote yupo upande wake. “Niambie tu. Nitawaambia wakuhamishie kila kitu chako kutoka kwenye kile chumba cha Net, uwe na kwako palepale ndani. Lakini si kurudi Tanzania. Sawa?” Tunda akatingisha tena kichwa kukubali.

“Naomba usimwamini Vic, Tunda. Kwanza ni mgonjwa wa akili.” Tunda hakuwa ameelewa akajua ni msemo tu. Maya akajua. “No Tunda. Namaanisha ni mgonjwa kabisa wa akili. Unakumbuka habari za Andy?” Tunda akatingisha kichwa kukubali. “Sasa kumbe Andy ni Jake. Jana ndio nimegundua kila kitu.” “Jana!?” Tunda akawa hajaelewa. “Kuna kitu tunataka kukwambia lakini naomba usishtuke.” Bibi Cote akaingilia.

Net akamuwekea supu akiwa mwekundu usoni kama aliyekuwa akikaribia kulia. Akamvutia kijimeza cha wagonjwa kirefu cha kitandani. “Asante.” Akashukuru na kuanza kunywa. “Umependa?” Net akauliza. “Ni nzuri.” “Gino amekutengenezea.” Tunda akanywa tena.

“Nana ulitaka kuniambia nini chakunitahadharisha nisiogope?” “Labda nikuulize wewe unajua umejifungua lini?” Tunda akakunja uso kama anayefikiria. “Jana jioni au usiku nilipoanguka nyumbani na kupoteza fahamu! Daktari ndivyo alivyoniambia alipopita janaaa...” Akatulia kidogo.

“Hapana. Jana usiku ndio mlikuwepo hapa, nikaomba mkaniletee mtoto wangu.” Akasita na kuweka bakuli chini. “Nahisi kama nimechanganyikiwa. Kwani mbona kama nina usiku miwili ila asubuhi moja ambayo ndio hii! Maana..”  Akatulia. “Alfajiri ile ingine waliniletea mtoto wangu nikamnyonyesha. Alikuwa hospitalin... Halafu hii ya leo..” Akatulia. “Mbona nahisi kuchanganyikiwa! Au nilipoteza fahamu?”  Akawaangalia kwa zamu. Net akamtizama bibi yake, akajua ndio anamwachia yeye.

“Nataka unisikilize kwa makini sana na usiogope.” Tunda akaanza kuingiwa na wasiwasi. “Unakumbuka nilikuahidi nini uliponiambia juu ya Ritha na watu kama Vic?” “Uliniambia nisiogope kwa kuwa wewe umesema nitakuwa salama na hawawezi kunigusa, na wakinigusa watapambana na wewe. Kitu kama hicho.” Tunda akajaribu kukumbuka huku akiwa na wasiwasi kidogo. “Sasa walijaribu.” Tunda akakunja uso.

“Jana asubuhi tulipokuja sisi. Mimi na Maya, tulimkuta Net akikusubiri.” Wakamuelezea mwanzo mpaka hapo walipokuwa. Tunda alibaki ametoa macho na machozi. “Nitafanyaje na Ritha, Nana? Hawezi kutulia mpaka ahakikishe ameniangamiza kabisa. Sina ninapoweza kumkwepa!” “Huhitaji kufanya chochote. Nakuahidi mwisho wake umefika Tunda. Naomba usiogope.” “Naachaje kuogopa Net? Kila ninapokwenda anajitahidi kutengeneza au kugeuza na kutafuta watu wa karibu yangu ili waniangamize. Mwisho wa hii ni nini?”

 ~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~

Ritha bado amebaki amesimama. Na huko tena nchini Canada ametengeneza jeshi la kizungu. Wote wamempisha mtaani, maisha yake yakiendelea. Aliopanga nao mipango wao wamegonga mwamba, lakini si Ritha mwenyewe.

-       Vic mtoto wa milionea wa nchi amemudu kumfikisha jela, kama mke wa Gabriel.

-       Malinda yu mahututi huku mdogo wake fundi mitambo/kompyuta amekwenda kulazwa chumba cha maiti kama Gabriel na mama yake.

 Tunda naye anataka kukimbia nchi ampishe tena kama alivyofanikiwa kumpisha nchini Tanzania na kumuweka jela.

Nini hatima ya kichwa nzuri kwa mipngo, Ritha?

Endelea kufuatilia.....

 

 

CONVERSATION

0 Comments:

Post a Comment