Naomi Simulizi |+1 205 767 8163 |naomisimulizi@gmail.com MAPENZI & PESA! - SEHEMU YA 4. - Naomi Simulizi

MAPENZI & PESA! - SEHEMU YA 4.

 Kwa kuwa baba yake na wadogo zake wakiume walimudu ile biashara ya kusambaza mayai na maziwa. Wakati mwingine kuku, Naya akajikuta yupo tu hosteli. Hana anachokifanya isipokuwa kusoma. Baba yake alikuwa akimtumia pesa kiasi cha matumizi. Akawa hana sababu yakulalamika tena. Maisha yakawa shule na hosteli kwenye kelele za Lulu na Malon.


Kila siku kulikuwa na jipya juu ya Lulu na Malon. Na Lulu naye aliyapamba hayo mahusiano, kama kujivunia tu na kufurahia.

Siku hiyo ya alhamisi akiwa ndio anatoka darasani, akapigiwa tena simu na Madamu Vane akimtaka arudi kazini. Naya alifurahi sana. “Lakini bado siku chache tuanze mitihani. Nitafanya weekend hii, halafu nitapumzika. Nikimaliza mitihani nitarudi.” “Utakuwa umenisogeza. Si unajua Lulu naye ameacha? Nasikia amepata mwanaume anayemtunza vizuri. Ameacha bila hata kuniaga! Nimeona tu hafiki, nikimpigia simu, hapokei! Ndio rafiki zake wameniambia amepata mwanaume.” “Hamna shida. Mimi nitajaza nafasi yake.” “Lakini nakutaka na usimamizi Naya. Napenda jinsi ulivyo mwaminifu na unavyojituma. Zungumza na wasichana wa hapo. Waambie ipo kazi. Tuone wangapi watakubali, kisha unijulishe.” “Sawa. Nitazungumza nao, kisha nitakujulisha tumepata wangapi.” Wakaagana huku Naya akiumia na kufurahia.

Alirudi hosteli akaenda chumbani kwa Girls star, akakuta wamenunua tv kubwa, spika nzuri na redio yenye CD, wanashangilia na wapambe wao. “Mambo ya Lulu hayo!” Naya akacheka. “Hongereni. Mtatupunguzia kiwingu kwenye tamthilia.” “Na kweli. Siku hizi tunakula kuku na kuangalia tamthilia vitandani kwetu, tena kwenye flat screen!” Lulu akajisifia. “Haya mama, hongera. Sasa kazi jumamosi, mpo?” “Kwani umerudi kazini!?” Wote wakashangaa. “Nimerudi ndio natafuta watu wakufanya kazi.” “Mimi sitaweza. Jumamosi natoka na Malon.” Lulu akajitoa kwa majivuno. “Haya, na nyinyi kina Hawa, Tuli na Tunu?” “Mama sisi tupo. Tena utuandike wa kwanza. Sisi bado hatujawapata kina Malon.” Naya akaandika majina yao, akatoka. Akawaacha wanashangilia utajiri.

Ni kweli maisha ya Lulu yalibadilika. Alibadili chumba chao. Akaweka thamani za maana. Kazi akawa hafanyi tena. Ikawa ni shule na chumbani akiangalia tv na kufurahia utajiri. Naya yeye akarudi kazini kwa nguvu zote. Jumamosi hiyo alifanya kazi kwa bidii zote. Mitihani ikaanza. Akatulia kabisa shuleni. Wakamaliza mitihani, wakafunga likizo ya mwezi wa sita. Akarudi nyumbani.

~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~

Akawekeza akili kwenye kazi, na tuition. Alikuwa kidato cha 4, hapakuwa na mapumziko mengi. Shule ya ziada iliendelea wakati wenzao wapo mapumzikoni. Na akili zilitulia kwa kuwa hapakuwa na habari za Lulu na Malon. Alikuwa akikutana na wenzake mara kwa mara kujisomea katikati ya juma. Hakukosa. Jumamosi kama kawaida akawa akienda kazini anakoitwa na Madamu Vane. Akichelewa kutoka, anakwenda kulala nyumbani kwa bosi wake, Madamu Vane. Ukaribu ukaongezeka. Naya akawa mtu wa karibu sana na bosi wake, kila mtu akamuheshimu.

Likizo ilikwenda kwa haraka sababu ya shuguli nyingi. Shule, kazi na majukumu ya nyumbani. Naya alikuwa mchapa kazi za mikono haswa. Hakuwa mzuri kwenye mambo ya ndani ya nyumbani kama mtoto wakike. Lakini ukimuweka nje, hata kuwapa kuku chakula tu, hakuwa na shida. Kwanza hakusubiri kutumwa. Kipindi hicho cha likizo, wakawa wameshamjua. Akiamka tu asubuhi, kitu cha kwanza sio kupika hata chai. Ni kwenye banda la kuku. Ataosha vyombo vyote vya kuku. Ataweka maji safi na dawa. Ataweka chakula. Ataokota mayai, ndipo anatoka kwenda kusoma. Kwanza hawakupenda apike. Walisema hajui kupika. Na yeye hakuwa akijisumbua hata kusogea jikoni. Mdogo wao wa mwisho yeye ndio alikuwa akiosha vyombo. Usingemkuta Naya jikoni. Mpaka mama yake alikuwa anasema Mungu alitakiwa amfanye Bale ni Naya, Naya, Bale.

~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~

Alirudi hosteli siku ya jumapili jioni kwa kuwa jumamosi alikuwa na kazi ya usiku. Alirudi kulala nyumbani kwao kwa kuwa alijua lazima siku inayofuata arudi hosteli. Alijiandaa kuweka akili shuleni haswa, kwani ndio ulikuwa muhula wa mwisho.

Shule ikaanza kwa kasi zote. Shuleni, hosteli na kazini. Safari za nyumbani zikawa zimepungua sababu ya ubusy wa kujisomea. Mtoto huyo wa Mwalimu, hakuhitaji kuhimizwa shule. Nyumbani kwao kila mtu alijua umuhimu wa kusoma.

Ulikuwa mwezi wa nane mwishoni. Birthday ya Naya. Hakuwa hata na habari kwa sababu nyumbani kwao hawakuwa wakisherehekea vitu kama hivyo. Kwa hiyo siku za birthday hazikuwa za ajabu. Ni kama siku nyingine zozote tu. Naya alikuwa ndio anatimiza miaka 18. Ilikuwa siku ya jumatato. Alikwenda shule kama kawaida. Akaunganisha kwenda kujisomea na wenzake. Akarudi hosteli kama kwenye saa 12 na nusu jioni.

“Nimechoka, nakaribia kuanguka na usingizi.” “Kula ndio ulale.” Wahija akamjibu akiwa na yeye anarudisha vitu kabatini kwake. Ndio alikuwa anarudi na yeye kutoka chuo. “Mtu kama anampenda mdogo wake si angeenda kumletea tu maji yakuoga!” Wengine wakacheka. “Umeanza Naya!” “Mimi mbona huwa nakuchotea maji, da Wahija? Tena bila kunituma.” “Na kweli. Haya, anza kuvua nguo, naenda sasa hivi. Na usilale.” “Najilaza kitandani kwako.” “Hapana naya bwana! Utaniwekea jasho.” “Da Wahija, hata mimi?” Mara hodi.

“Mnataka nini chumbani kwetu?” Wahija akaongea bila kukaribisha, Lulu akaingia. “Nina mzigo wa Naya.” Lulu alionekana kukosa raha sana usoni. Alipooza kupita kiasi. Naya na Wahija wote wakageuka. Ulikuwa mfuko mkubwa sana wa zawadi. Unakadi nyekundu kubwa iliyoweza kuonekana mpaka nje ya ule mfuko na maua. Wakati anashangaa, Lulu akauweka ule mfuko chini kwa hasira kidogo, akaondoka na kufunga mlango.

“Makubwa! Nani huyo?” Wahija akauliza huku akiokota ule mfuko, akamkabidhi Naya. Akaanza kuufungua na maswali mengi mpaka usoni. Akatoa maua kwanza. Wahija akavuta kadi na kuifungua kwa haraka. “Haaa!”  Wakamsikia Wahija anashangaa kwa sauti. “Inatoka wapi da Wahija?” Naya akauliza huku akifungua kijiboksi kidogo kilichofungwa vizuri. Macho yakamtoka Naya. Ilikuwa cheni nzuri sana, nzito ya dhahabu. Yenye kidani kidogo cha alama ya kopa kilichobeba herufi ya N. Naya akakunja uso na kumpokonya ile kadi Wahija. “Kumbe leo ni birthday yako!?” Wahija akashangaa. Naya akasoma. Haikuwa na maneno mengi zaidi ya kumtakia birthday njema, chini jina la Malon. Naya akamtizama Wahija kwa mshangao.

Wote wakabaki kimya kwa muda. Ndipo na wenzao wakatoka vitandani kwao na kusogelea vile vitu wakitaka kujua. “Vimetoka wapi?” “Eti kwa Malon!” Wahija akajibu. “Sasa kwa nini ampe mwanamke wake alete!?” Mmoja wao akauliza kwa mshangao. “Ndio ushangae na wewe!” “Ndio maana Lulu kaingia hapa amenuna! Atakuwa amemlazimisha yeye ndio alete.” Mwingine akaeleza. “Huyu Malon si mjinga. Atakuwa ameleta hivi vitu na ujumbe wa zaidi ya huo, ndio maana akataka Lulu ndio alete.” “Sasa ni ujumbe gani huo kama sio kutukosanisha na Lulu tu?” “Kwani wewe Lulu alikwambia Malon amemuoa?” Wahija akauliza, Naya akakunja uso.

“Wewe si ulibadilisha namba ya simu? Sasa unajuaje kama kumkubali Lulu ndio ilikuwa njia yakuendelea kuwa karibu na wewe?” Naya akabaki kutoa macho. “Wewe huyajui makubaliano ya Malon na Lulu. Unachujua ni kelele za Lulu akitoka huko kwa Malon.” “Sio kwa Malon, anakuwa anatoka kwenye starehe na mpenzi wake.” Naya akaongeza kwa wivu. “Kama angekuwa mpenzi wake angemtuma akuletee wewe cheni, mwanamke uliyemuacha amekupigia magoti?” “Wala hakupiga magoti! Wamemsingizia Malon.” “Leo ndio unataka kusema wakati sisi tulikuuliza humu ndani ilikuaje, tena kwa kurudia rudia, ukasema hutaki kuongelea! Leo ndio unajidai kusema hakupiga magoti!” Naya akaanza kucheka.

“Tula au Chezo mmoja wao aliongeza chumvi ili kunogesha stori. Malon anipigie mimi magoti wakati watoto wazuri kama kina Lulu wapo! Anataka nini kwangu na wakati wote tulikuwa tunatangaziwa hapa staili alizokuwa akipewa huyo Malon?” “Nakuuliza kama angekuwa anapewa hayo yooote, kwa nini akuletee cheni leo, tena amtume Lulu mwenyewe?” “Bwana mimi sijui! Sasa nitafanyaje da Wahija?” “Asante.” “Akuu! Sitaki kumtafuta yule kaka.” “Ila cheni unataka?” Naya akacheka sana.

“Dhahabu hii da Wahija!” “Tena dhahabu haswa.” “Mimi naiweka bwana. Kwani nimemuomba? Si kaniletea mwenyewe.” Wahija na wenzake wakaanza kucheka. “Naya wewe mtoto mkorofi wa chini chini.” “Kweli da Wahija. Mimi sikumuomba. Kwanza hata nilikuwa sijui kama leo ni birthday yangu. Sijui kaambiwa na nani. Kaniletea cheni...” “Tena yenye jina lako.” Wahija akamkatisha na kumfanya acheke zaidi. “Si umeona mwenyewe da Wahija? Sasa yeye anaitwa Malon. Mwanamke wake Lulu. Nikiwarudishia kidani chenye N, utakuwa utahira.” Wakacheka hapo, lakini Naya alifurahi sana.

~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~

Siku zikaendelea kwenda. Naya akiendelea kutafakari juu ya Malon. Hakika hakuwa amemuelewa, ila alimfurahisha sana. Aliona ni kama amemkumbuka, bado hajamsahau. Ilimgusa sana. Ila taratibu kelele za Lulu zikaanza kupungua. Akawa ametulia sana tofauti na zamani. Week hiyo ikaisha, na ya pili. Lulu akawa ametulia sana.

Naya akawa amepewa tena kazi. Ilikuwa mwezi wa 9 katikati. Madamu Vane alimwambia ni mtu amenunua nyumba hapo jijini. Anafanya house warming. Amealika rafiki zake, anataka wasichana wanne. Akamtaka na Naya awepo. Kama kawaida, hakumsahau Hawa rafiki yake aliyemuunganishia kwenye hiyo kazi. Akamfuata Tula na Tunu chumbani kwao. “Kuna kazi jamani. Safari hii nyumbani kwa mtu. Madamu Vane amesema kuvaa nyeusi, sio lazima kiatu cha juu. Mnataka?” Kimya. Akaona na wenyewe wamepooza. Naya alipoona kimya hakutaka maneno mengi na wao, aliwajua wale wasichana. Akataka kutoka.

“We Naya.” Tula akamwita. “Nini? Naona mmeninyamazia, nikajua hamtaki.” “Na Lulu?” “Nimeambiwa watu wanne. Kwa kuwa siku hizi Lulu hachukui kazi, nimemtafuta Hawa. Ipo nafasi ya watu wawili. Sasa nyinyi chagueni wenyewe, kisha mniambie nani anakwenda. Tena sasa hivi ili nimtumie majina Madamu Vane.” Tula na Tunu wakatizamana. “Tuandike sisi.” “Sawa.” Naya akajibu na kuondoka. 

Jumamosi.

K

wa kuwa Naya alishakuwa kiongozi wao, alijitahidi kuwahi kujiandaa. Wakaita usafiri, akaenda kumfuata Tula na Tunu. Akashangaa kumkuta Lulu pale chumbani, hajatoka kama kawaida yake, Naya hakutaka kumsemesha. “Mpo tayari warembo?” “Mbona sasa wewe umevaa kawaida tu, umetuacha wenzio tumevalia?” Tunu akawa kama analalamika. “Niliwaambia kabisa ni nyumbani kwa watu, Madamu amesema tuvae nyeusi sio lazima viatu vya juu. Nyeusi niliyonayo na niliyoona inafaa nyumbani kwa mtu, tena ufukwenu ndio hii na sendozi. Kama nyinyi mmependeza zaidi, tatizo liko wapi!?” Wakanyamaza.

“Naombeni tuwahini. Mimi sitaweza kuchelewa zaidi.” “Umepanda cheo ndio umesahau kama sisi tulikuwa tukikusubiria?” “Sijasahau hata kidogo. Lakini nimepigiwa simu muda sio mrefu, natakiwa kuwahi kabla ya sherehe kuanza, ili kukabidhiwa vitu. Nyinyi mnaweza kuchelewa kidogo, mimi siwezi. Kwa hiyo basi, anayetaka kuongozana na mimi twende, ambaye bado, aite taksi au uber.” Naya akatoka. Wakamfuata nyuma bila kuchelewa maana walimjua Naya hababaishwi na haogopi mtu.

Alipiga simu kwa bosi wake, akampa dereva amuelekeze mpaka kwenye hiyo nyumba. Basi wakatulia garini wakati wakipelekwa kazini. Eneo ilipokuwepo hiyo nyumba ilikuwa Kunduchi beach kabisa. Ndogo tu, lakini nzuri sana. Wote wakabaki wanashangaa. “Huyu atakuwa mzungu tu.” Tuli akanong’ona. “Kwa kukuta magari yote haya, inamaana tumechelewa.” Naya akaongeza. Mlinzi akawaruhusu waingie ndani, maana walishushwa nje ya geti. Wakasogea mpaka kwenye nyumba yenyewe wakionyesha kubabaika. Naya akasogelea mlango na kubonyeza kengele. Akaja mtu kufungua na kopo la Heneken mkononi. Mziki wa kawaida tu ulikuwa ukiendelea.

“Tumetumwa kuja kusaidia kazi ya kugawa vinywaji na chakula.” Naya alianza hivyo. “Chezo! Chezo!” Wote wakaangaliana. Wakasikia Chezo anaitika. “Kuna wageni wako hapo mlangoni.” Chezo akafika pale akionekana alikuwa akicheka. “Mmefika wakati muafaka, warembo. Tuli upo mama?” “Nipo Chezo.” Naya akampisha Tuli aliyesalimiwa kwa kutajwa jina. “Karibuni ndani.” Chezo akatangulia. Naya aliweza kutambua baadhi ya sura. Lakini mbali na wale vijana waliokuwa nao kwenye baa ya Masaki, kulikuwa na wazee, watu wazima na kina mama, wote walionekana kwenye wakati mzuri. Wakina Naya walisalimia, nakupitiliza jikoni. Kabla yakuingia jikoni, kulikuwa na friji na Cooler boksi kubwa sana. Waliambiwa humo ndipo vilipo vinywaji. Chezo aliwaambia hawategemei watu wengi sana, lakini walitaka kitu kisiharibike na baada ya hapo, watataka msaada wakukusanya chupa zote na sahani. Wasafishe ndipo kazi yao itakuwa imeisha. Wakapelekwa na jikoni. Wakaonyweshwa kila kitu kilipo. Chezo yeye akaondoka.

Kwa kuwa walikuwa na uzoefu, walijua nini chakufanya. Wakachukua masinia ya vinywaji matupu ili warudi kule walipowageni. Wachukue chupa tupu na kuchukua oda mpya. Mpaka hapo, Hawa hakuwa amefika na Naya alipompigia simu wakati wapo njiani hakuwa akipatikanika. Wasiwasi ulimwingia, lakini baada yakujua kazi yenyewe, wasiwasi ukamtoka. Akawaambia kina Tula wasiwe na wasiwasi, wao watatu watatosha tu. Akatoka Tula na sinia tupu mkononi. Akafuata na Tunu. Wakati Naya anajiandaa kutoka, akageuka, akakuta Malon amemsimamia nyuma yake.

Akashtuka sana. “Malon!” Akajikuta anamwita kwa sauti ya juu kidogo. Malon akacheka tu. “Ume..” Naya akasita. “Karibuni.” Malon akamkaribisha. “Asante. Lakini tumekuja kikazi. Na wewe umealikwa?” Naya akauliza akionekana kupaniki. Malon akacheka huku akitingisha kichwa kukataa. Naya akakunja uso na kuamua kutoka pale. Ngoja mimi nianze kazi.” Akampita Malon pembeni, akaelekea walipo wageni.

Kulijaa vicheko humo ndani.  Kadiri muda ulivyozidi kwenda, ndivyo watu walivyoongezeka na kuzidi kulewa. Kufika saa nne, hapakuwa na mgeni mpya, lakini wengi wao walikuwa wakinywa tu, walishalewa. Naya na wenzake wakaendelea kuwahudumia. Ilipofika saa 5 usiku, Malon akamfuata Naya jikoni. “Njoo.” “Nani, mimi?” Tula akajishika kifuani. “Naya. Njoo uwasalimie baba na mama. Wanataka kuondoka.” Naya akakunja uso. “Malon!” “Njoo bwana. Usiogope.” Hata hakujua kama wazazi wa Malon walikuwa pale. Naya akamsogelea Malon. “Malon!” Naya akamvuta mkono kama arudi wazungumze kwanza. Malon akarudi, akamshika mkono kwa nguvu na kumvutia sebuleni. Kina Tula wakasogea kushuhudia.

“Mama na baba, huyu ndio Naya.” Naya alikuwa akitetemeka. Kila mtu pale sebuleni akanyamaza kimya. “Shikamooni.” Naya akawasalimia kwa heshima na kuwapa mkono. “Chezo alituambia ulikuja Morogoro. Tukajua ungekuja kutusalimia nyumbani, nikaona kimya.” Naya akababaika kidogo. “Nitakuja wakati mwingine.” Akajibu akimtizama Malon. “Basi jogoo wako anakusubiri.” Akaongeza baba yake Malon. “Jogoo za Mzee, za upendeo pendeleo!” Chezo akalalamika, wote wakacheka. “Mgeni siku ya kwanza. Ya pili kuku wa kienyeji. Siku ya tatu maharage.” Akajibu baba yake Malon, wote wakacheka. “Sisi tunaondoka tunarudi Morogoro. Usiku sana sasa hivi. Tushapaona hapa, inatosha. Siku nyingine tukiwa hapa mjini, mtashtukia tupo mlangoni.” Aliongea baba yake Malon, akisimama na mkewe. Naya hakujua hata ajibu nini. Akacheka tu huku akimtizama Malon kwa wasiwasi.

“Ngoja tuwasindikize mama.” Malon akamvuta Naya mkono mpaka mlangoni wakafungua mlango. “Ushalewa nini, mama?” “Sijanywa sana bwana wee!” Akajibu mama yake Malon. “Mbona sasa miguu hainyanyuki?” Malon akaendelea kumuuliza mama yake huku akimwangalia miguu yake. “Uzee. Unataka nikimbie kama wewe?” “Haya mama. Taratibu usijikwae kwenye meza hapo.” “Nilikuwa namwambia asinywe, akaniona nataka kumnyima raha. Haya, taratibu usije vunja meno bure.” Baba yake akaongeza. Malon akamfuata mama yake akamshika mkono.

“Au mlale tu. Eti mama?” “Acha wasiwasi wewe Malo! Nimekwambia mimi mzima. Miguu tu ndio inasumbua.” “Imeanza lini?” “Muda tu. Baba yako amesema tutaenda kumuona dakatri, naona zimebaki ahadi tu.” “Tutaenda bwana. Mambo yamekuwa mengi.” Naya alikuwa amesimama mlongoni akisubiria Malon na mama yake wafike. Wakatoka, akafuata baba yake aliyekuwa akiagana na wageni wengine kwa kupeana mikono, kisha na yeye akatoka. Naya alibaki hajui kama afuate nyuma au arudi jikoni. “Naya!” Akamsikia Malon akimwita. Akatoka kwa haraka.

Akamkuta Side yupo kwenye gari ileile iliyomrudisha Dar, akilia. Akamsogelea. “Habari Side?” “Ooooh! Naya mwenyewe! Kumbe upo mama?” “Nipo, sijakuona ndani.” “Ndio nimefika muda sio mrefu. Kuna kitu nilikuwa nafanya mjini. Ndio nataka niwarudishe wazee nyumbani. Mzima lakini?” Naya akacheka. Akakumbuka vile alivyokuwa akilia siku ile. “Mzima Side. Muwe na safari njema mnaporudi Morogoro.” “Asante sana.” Naya akarudi alipokuwa amesimama Malon. Akamfungia mama yake mlango, akarudi nyuma kidogo. “Taratibu Side.” “Bila shaka.” Side akamjibu Malon, wakaagana, nakuondoka.

Wakabaki Malon na Naya wamesimama pale nje. Naya akacheka kidogo. Malon akashika kile kidani pale shingoni kwa Naya. Alikuwa amevaa ile cheni aliyokuwa amempa Lulu ampelekee siku ya birthday yake. Akakizungusha kidogo huku akitabasamu kama anayefikiria kitu. “Asante kwa zawadi.” Akaona ashukuru. “Nimefurahi sana kuona umeivaa.” Naya akacheka kidogo, na kugeuka akitaka kurudi ndani. “Naya!” Malon akaita. “Abee!” Naya akageuka. “Naomba unisamehe.” Naya akakunja uso. “Kwa nini tena?” Naya akauliza kwa sauti ya chini tu. “Chochote nilichokuudhi.” Naya akainama akifikiria. Kimya.

 “Hata na hicho unachokifikiria sasa hivi pia, naomba unisamehe.” Naya akamwangalia. Akaona machozi yanajaa machoni. Hata yeye hakutegemea. Akajifuta, na kugeuka. Akaondoka kurudi ndani. Baada ya muda kidogo watu wengine wakaaga. Wazazi wa Chezo nao wakaondoka pamoja na marafiki wengine. Wakabaki Malon, Chezo na marafiki zao wengine. Mpaka hapo hawakuwa wakijua nyumba ni ya nani. Wakaendelea kusafisha. Mpaka wanamaliza kusafisha nakurudisha kila kitu sehemu yake, wakawa wamebaki watu wanne hivi. Mpishi alishamaliza, akalipwa na kuondoka.

Naya alipohakikisha kila kitu kipo sehemu yake, wakasogea pale sebuleni. “Tumemaliza. Mnaweza kukagua kabla hatujaondoka.” Naya aliongea akimtizama Chezo. “Patakuwa sawa tu. Si mkae sasa na nyinyi mpumzike.” Tula na Tunu wakakaa kwa haraka. Naya akacheka. “Jamani mimi naomba niwaage. Nitangulie.” “Kwa nini hutaki kukaa, Naya?” Chezo akauliza. Malon alibaki akimwangalia Naya. “Kwanza nimeshaita Uber, atakuwa yupo hapo nje akinisubiri. Pili, nina mambo yakufanya hosteli. Lazima nimalize leo. Nawaachieni hao warembo, muwe na wakati mzuri.” Naya akamaliza kiustarabu, akatoka.

“Naya!”  Akamsikia Malon akimwita, akageuka. “Naweza kukurudisha.” “Naona Uber imeshafika. Asante.” Wakabaki kimya kidogo kisha Naya akawa kama amekumbuka kitu. “Halafu Malon, naomba usiwe unamtuma mpenzi wako aniletee vitu.” Malon akacheka. “Nani amekwambia Lulu ni mpenzi wangu?” Naya akakunja uso na kushangaa. “Malon!” “Nakusikiliza Naya.” “Basi bwana. Mimi naomba usiwe unamtuma mwanamke wako kwangu. Unatuchonganisha na kutufanya tuwe maadui bila sababu.” “Kwani amekufanyia chochote!?” “Hapana. Lakini..” “Ahaa! Nilifikiri amekufanyia fujo au maneno ya kipuuzi, nimpasue kichwa.” Naya akashangaa sana.

“Mimi naomba nikapumzike Malon.” “Sasa nikitaka kukutumia zawadi nifanyaje?” “Naomba usilete zawadi Malon. Tafadhali sana. Nilikwambia pale hosteli tuna miiko tuliyojiwekea.” “Uliniambia, sijasahau na wala hutavunja sharti lolote lile. Na pia sitakuruhusu ufanye hivyo.” Naya akawa bado haelewi. “Mimi nahisi nimechoka Malon. Naenda kulala.” “Naomba namba yako ya simu, Naya.” Naya akageuka na kuondoka bila yakujibu. 

~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~

             Baada ya ile siku Naya alipoenda kuhudumia na kina Tula kwenye ile nyumba ambayo bado Naya hakujua ni ya nani, kukaanza minong’ono mingi tu pale hosteli juu ya Malon kwa Naya. Kina Tula walipotoka siku ile kule Kunduchi alipowaacha Naya wakiwa na kina Chezo, walikuja kueleza mengi ikawa aibu tena kwa Lulu. Kama kawaida ya Naya, alijibu kila mtu hataki kuzungumzia chochote. Yeye pia hajui. Tula alieleza kuwa Naya ametambulishwa mpaka kwa wazazi wa Malon, na ilijulikana kuwa yupo Morogoro na wakamuulizia kwa nini hakufika nyumbani kwa wazazi wa Malon. Tula na Tunu wakatangaza kuwa Naya ndio anatambulika kwenye familia ya kina Malon.

Na Chezo akawa amemwambia Tula ambaye ni kama mwanamke wake kwa wakati huo, kuwa Malon alikuwa karibu na Lulu ili kuwa karibu na Naya. Ndio maana hata siku moja Malon hakuwahi kufika hapo ndani kwao akimfuata Lulu, lakini alikuwa akiingia mpaka ndani kumfuata Naya. Ikawa maneno mengi. Naya alikuwa akijisikilizia tu na kunyamaza. Watu wakageuka kuanza kumcheka Lulu na Girls star. Ikawa aibu tupu. Kuwa walikuwa na maneno mengi kumbe hata Malon mwenyewe hakuwa anamtaka Lulu. Kama aliyekuwa ameonywa, Lulu hakurudisha neno hata moja. Akawa kimya. Baada ya kama juma moja, Lulu akahama kabisa pale hosteli. Maisha ya Naya yakaendelea kama kawaida. 

Majuma mawili mbeleni, siku ya ijumaa, Naya alimka tumbo likimuuma sana. Akashindwa hata kwenda shuleni. Akabaki hosteli amelala siku nzima. Wahija alitoka chuo, akamkuta anahangaika kitandani, akampa dawa, akarudi kulala. Wahija akaamua kusomea hapohapo chumbani ili awe na Naya. Kila mtu alimjua Naya ni mdogo wake Wahija. Na Naya anaweza kumsikiliza Wahija kwa chochote atakachomshauri. Akasikia mlango unagongwa taratibu kisha Tunu akaingia. “Una mgeni wako da Wahija.” “Nani?”  Akauliza Wahija. “Wewe nenda utamuona mwenyewe.” Akajibu Tunu na kuondoka. Wahija akatoka.

Akashangaa kumkuta Malon sebuleni akimsubiria. “Wewe si ndio Malon!” “Ndiyo. Tunaweza kuzungumza?” “Kama nikuhusu Naya, nataka unijibu swali langu kwanza.” Kila mtu alimjua Wahija kwa maneno. Malon akatulia. “Wewe unamtaka Naya au Lulu? Maana unakazi ya kuchanganya akili za hawa watoto, Lulu kakimbia hosteli hapa.” “Kwani wewe Lulu alikwambia yupo kwenye mahusiano na mimi?” Malon akauliza akiwa ametulia tu. “Ndivyo alivyosema.” “Kwa hiyo na mimi nikisema ni raisi wa Marekani utaniamini?” Wahija akanyamaza.

“Mimi nipo hapa kwa ajili ya Naya.” “Na Lulu?” Wahija akauliza. “Mimi sijui umesikia nini juu ya Lulu, nashauri uzungumze naye vizuri, upate ukweli kutoka kwake. Siwezi kujibu maswala ya Lulu. Ila tu, ujue Naya amebadilisha namba ya simu. Kila ninayemuomba namba yake, hana. Naya ni mpenzi wangu. Kila mtu au anajulikana na wanaonifahamu mimi. Mambo mengine mimi sijui. Leo nimeambiwa ni mgonjwa, hakwenda shule. Ni kweli?” Wahija akanyamaza. “Nimekuita wewe sio kwa bahati mbaya Wahija. Naya ni mgonjwa nataka kujua jinsi yakumsaidia.” “Nimempa dawa, amelala.” “Amekula?” “Alikuwa anatapika. Nimemnunulia chips yai, akimka ndio nitampa nione kama vitakaa tumboni. Ila akitapika tena, ndio nilipanga kumpeleka hospitali.” “Naweza kumuona?” Wahija akanyamaza.

“Nakuuliza kama naweza kumuona sio kwa sababu nashindwa kuingia chumbani kwenu. Ni kwa sababu nataka uzungumze na Naya, akubali nimuhudumie kipindi hiki mgonjwa. Nimeambiwa wewe anakusikiliza.” “Sasa unaomba au unataka nikubembelezee kwa Naya?” Malon akacheka na kutingisha kichwa. “Nakuomba uzungumze na Naya. Nampenda Naya na jibu la hapana kwa yeyote hata Naya mwenyewe haliwezi kunifanya niache kumfuata. Nitafanya chochote niwe na Naya. Wewe naomba unisaidie tu. Kwanza hakuna mtu atampenda Naya kama mimi.” Wahija akaanza kucheka.

“Sasa kilichokupelekea kulala na Lulu ni nini?” “Sasa hivi Naya ananihitaji mimi. Naomba hizo kesi ziwe za wakati mwingine. Nitatafuta muda wakuzungumza na wewe, lakini naomba isiwe leo. Nimepata taarifa za ugonjwa wake, nikapanda gari na kuja hapa. Naomba tu nimuone.” “Twende, lakini ujue itakuwa ni juu yako wewe mwenyewe kama hataki kukuo...” “Sasa wewe ndipo ninapotaka unisaidie. Zungumza naye.” Wahija akamtizama Malon, akaongoza njia kurudi chumbani kwao alipokuwepo amelala Naya.

Wakaingia chumbani kwao. “Kitanda chake hicho hapo juu.” Akamuonyeshea alipolala Naya. Malon akasogea nakuanza kumgusa kichwani taratibu. Akamvuta mkono akaushikanisha viganja kwa kupitanisha vidole vyake katikati ya vidole vya Naya. “Malon!” Naya akafungua macho na kushangaa vile Malon amemshika na kumsimamia pembeni ya kitanda. “Vipi?” “Mwenzio naumwa. Tokea asubuhi natapika!” “Pole.” “Asante. Umekuja kufanya nini?” “Chezo ameniambia unaumwa sana, unatapika ndio maana nimekuja.” “Itakuwa ameambiwa na Tula. Alinikuta nje asubuhi wakati nachota maji, natapika.” “Pole sana.” “Asante kwa kuja kuniona.” Malon akatoa tabasamu.

“Umekula?” “Natapika Malon. Sijui kwa nini mwezi huu umekuja hivi! Huwa sipati siku zangu na maumivu hivi.” “Twende ukapumzike.” “Morogoro!?” “Hapana Naya. Siwezi kukupeleka mbali.” Naya akanyamaza. “Twende. Utapumzika.” “Umeniumiza Malon. Umeniumiza sana.” “Nimekuomba msamaha Naya. Naomba nisamehe. Na ujue nimefanya kila kitu kwa kuwa nakupenda. Sikukusudia kukuumiza. Nisamehe. Na hata kama huna mpango wa kukunisamehe sasa hivi, basi naomba twende nikakuuguze nikuache ukiwa mzima. Siwezi kukuacha ukiwa hivi mgonjwa. Utanifanya nihamie hapo juu kitandani kwako.” “Malon!” “Sikutanii Naya. Muulize Wahija.” “Umeongea na dada Wahija!?” “Yeye ndio ameniruhusu niingine nije kukuona.”  Naya akafurahi kusikia na Wahija ameruhusu. Bado alikuwa amejilaza kitandani, Malon akipitisha kidole chake kimoja taratibu kwenye nyusi zake, na kuzunguka nywele.

“Nakupenda Naya.” Naya akacheka taratibu. “Nisamehe siku ile niliondoka kwa hasira.” Malon akacheka na kujilaza kichwa kwenye mbao ya kitanda akimtizama. “Ulikuwa hata ukinikumbuka kweli?” Naya akanyamaza. “Naya?” “Nina mambo mengi Malon.” “Safari hii nimejifunza. Nitakuwa mtoto mzuri.” Naya akacheka taratibu kwa sauti ya ugonjwa na deko juu. “Twende. Nakuahidi mapumziko mazuri. Utarudi ukiwa unajisikia vizuri.”  Naya akakaa. Akashangaa kumbe kila mtu alikuwepo mle chumbani wakiwasikiliza.

Akacheka na kujifunika na mto. “Bwana da Wahija!” “Wewe nenda. Ukipata nafuu ndio urudi.” Naya akacheka. “Nikubebe?” Malon akauliza huku akimtizama. “Sijazidiwa bwana! Kwanza dawa alizonipa da Wahija, zimenisaidia. Sina hata haja ya kwenda.” “Naomba usibadili mawazo Naya. Tafadhali. Nimeendesha muda wote huo nikiwa na wasiwasi na wewe.” Naya akashuka kitandani.

“Labda nioge kwanza Malon.” “Twende utaoga hukohuko.” Naya akasita. “Vipi?” “Njoo nikunong’oneze.” Malon akainama kumpa sikio. “Naweza kuchafua gari.” Naya akanong’ona. “Usijali. Twende.” Akakusanya vitu vichache. Akawaaga pale na kutoka na Malon. Malon akamfungulia mlango wa gari, Naya akatandika khanga ndipo akakaa. “Hatuendi mbali?” “Tunaelekea pale ulipokuja kwenye house warming.” Naya akamtizama kama mwenye swali. “Vipi?” “Kwani na pale ni kwako?” “Huoni na wazazi walikuja? Nilinunua kwenye mnada wa benki. Bei haikuwa mbaya sana.” “Hongera Malon. Unajitahidi.” “Hivyo hivyo.” Wakatulia. Malon akiendelea kuendesha.

“Unajisikiaje?” “Sasa hivi tumbo na kiuno vimetulia kidogo, sio kama asubuhi.” “Unataka kula nini? Lazima tununue. Pale nimeweka walinzi tu. Nikiondoka nafunga.” “Chochote utakachopenda wewe. Mimi nimetapika sana, nahisi nimepoteza hamu ya kula.” “Basi nitakutengenezea uji.” “Asante Malo. Nashukuru kwa kuja kuniona na kunichukua.” Malon akamwangalia na kuguna. “Unaniringia Naya wewe!” “Sikuringii Malon. Najiona nina mambo mengi yakunizidi umri wangu.” “Kwa kuwa unataka kuyabeba mwenyewe. Hutaki tushirikiane.” “Hutabiriki Malon.” “Mimi sitabiriki tena? Leo ningekuwa hapa kama sitabiriki?” “Basi mimi sikuelewi Malon.” “Kwa kuwa hutaki kunielewa Naya. Tunakwenda mbele, na kurudi nyuma.” Naya akanyamaza.

 “Vipi?” “Natamani kuoga tu nilale. Najihisi kuchoka. Sijisikii vizuri Malon.” “Unauhakika ni tumbo tu, hamna malaria au kitu kingine?” “Sijui. Ngoja nijipe siku ya kesho. Nikiendelea hivi, ndio nifikirie kwenda hospitalini.” “Wazo zuri. Basi twende moja kwa moja nyumbani. Wakati unaoga, mimi niwe nakutengenezea uji, ujaribu.” “Na wewe chakula?” “Usijali. Nitajua tu kitu chakufanya ukisha tulia.” “Pole Malon. Nakusumbua eeh?” “Hata kidogo. Ningesumbuka kama ungekuwa unaumwa halafu sipo kukusaidia. Hiyo ingenisumbua.” Ikamgusa sana Naya. Akajifuta machozi. Malon akamuona. “Nakupenda sana Naya. Kuliko nitakavyokwambia. Na sikukusudia kukuudhi siku ile. Nilifanya kutaka kukulinda. Lakini nimejifunza. Nakuahidi sitaingilia tena.” Naya akanyamaza.

Walifika nyumbani kwa Malon, akamsaidia kushuka. Naya alikwenda moja kwa moja bafuni kuoga. Malon alimletea taulo kubwa. Akarudi jikoni kupika. Baada ya kumaliza kuoga, akatoka na kumfuata Malon jikoni. “Vipi?” “Nasikia kutapika Malon. Huo uji sidhani kama utapita.” “Maumivu?” “Nahisi kama dawa zimeanza kuisha. Natamani kulala tu.” “Nikikupa dawa sasa hivi, hutatapika?” “Sasa sijui nifanye nini!?” “Tujaribu dawa. Ukitapika, nakupeleka hospitalini tuombe wakuchome sindano yakuzua kutapika na wakupime vitu vingine.” “Sawa.” Malon akampa dawa. Naya akabaki amejiegemeza pale jikoni. “Twende kitandani ukajilaze. Usipotapika, nakupa uji.” Wakaongozana mpaka chumbani. Kilikuwa chumba kizuri sana. Naya akakipenda ila hali ilikuwa mbaya.

“Au nimpigie simu baba?” “Naya! Acha kupaniki bwana. Tumekubaliana tusubiri. Naomba utulie. Usiogope. Mimi nipo hapa na wewe, ukizidiwa nakupeleka hospitalini.” Naya akanyamaza. “Ni sawa?” “Nikifa je? Naweza kufa bila kumuaga baba yangu. Na nisipomuaga...” “Naya! Naya! Naomba tulia na unyamaze. Huwezi kufa bwana.” “Unajuaje?” “Jilaze hapa kwanza. Halafu niambie kama bado maumivu yanaendelea.” “Yanaendelea.” “Naya! Wewe muoga bwana.” “Sana.” Malon akaanza kucheka asiamini.

“Usicheke.” “Naomba tulia, tuzipe dawa muda wakufanya kazi. Utakuwa sawa. Lala hapa.” Malon akamuwekea mto vizuri akapanda na kumfunika.  Akakaa hapo pembeni yake. “Utaunguza uji.” “Upo sawa. Nimezimia jiko. Jitahidi kutulia.” Naya akafunga macho kwa muda. Mara akamuona anakimbilia chooni. Alitapika vitu vichungu, kuashiria dawa. Alitapika tena na tena. Malon akaona ampeleke tu hospitalini.

Alipofika hospitalini, akafanyiwa vipimo, akakutwa na Malaria. “Mpigie simu baba yangu. Tafadhali Malon. Nitachanganyikiwa asipokuja.” Malon akachukua simu ya Naya, cha kwanza akajipigia yeye na kumpigia simu baba yake Naya. “Naitwa Malon. Nipo hospitalini na Naya. Anaumwa. Amesema nikutaarifu. Lakini usiwe na wasiwasi. Hajazidiwa sana. Alikuwa anatapika. Wamemchoma sindano na kumuwekea dripu ya maji. Ikiisha watamruhusu.” “Nashukuru kwa taarifa. Nakuja.” “Lakini usiwe na wasiwasi Mzee wangu.” “Huyo hana ugonjwa mdogo wala mkubwa. Ukishamsikia anataka niitwe, ujue ndio amefika kipimo chake cha mwisho cha uvumilivu. Hapo atakuwa ameshafikiria kufa na kila kitu. Hawezi kutulia mpaka niwepo hapo. Acha tu nije mwenyewe.” Malon akacheka kidogo. Akajua ndio tabia yake.

 “Sawa. Sasa usiku huu utapata usafiri kweli? Au uje kesho?” “Nitafika tu. Hapawezi kukucha leo kwa amani bila mimi kuwepo hapo. Namjua Naya. Ikifika hatua hiyo ni heri daktari asiwepo, mimi niwepo. Hawezi kutulia tena, na hakuna dawa itafanya kazi tena. Atakwambia amezidiwa tu. Acha tu nije.” Malon akacheka tena. “Wewe mwambie nakuja sasa hivi, ndio atatulia.” “Naweza kukufuata.” “Usiku huu!?” “Hamna shida. Tupo hapa Mwenge.” “Hakuna sababu. Nitafika tu, nashukuru.” Yule Mzee akakata simu.

 Malon akarudi ndani. “Baba amesemaje? Anakuja?” “Anakuja. Ila amesema utulie. Utakuwa tu sawa.” Akatulia kidogo akafunga macho. “Unafikiri atapata usafiri mida hii au labda unipeleke tu nyumbani kwetu.” “Naya! Naomba ulale bwana. Baba atafika. Tafadhali tulia.” “Tunaishi Kiluvya, Malon. Na sasa hivi...” “Naya! Naya! Naomba utulie bwana. Baba yupo njiani anakuja.” “Nipe nizungumze naye.” “Kwa hiyo mimi hunihitaji hapa?” Naya akatulia kidogo. “Eti Naya?” “Nahisi nikuzidiwa. Hamna dawa inafanya kazi, Malon! Naumwa sana. Nimezidiwa sana.” Malon akakumbuka maneno ya baba yake Naya.

“Nisikilize Naya. Najua unaumwa. Wamekupa dawa na wamekuwekea dripu ya maji. Tulia. Ipe muda ifanye kazi. Na ujue baba anakuja. Au unataka mimi niondoke?” “Hapana Malon. Sina maana ya kukufukuza. Samahani. Ila nahisi naweza kufa, halafu nikashindwa kuagana na baba yangu.” “Utakuwa sawa. Haufi leo na baba yupo njiani anakuja” Akavuta pumzi, akarudi kulala.

Baada ya kama lisaa baba yake akafika. Akampigia simu, Malon akatoka kwa haraka. “Tupo hapa nje.” “Nakuja kuwachukua.” Malon akatoka. Akamkuta baba yake, mama yake na wadogo zake wote. Ikabidi asalimie wote na kuwashika mkono. “Hajaanza kulia?” Zayoni akamuuliza Malon huku wanacheka. “Hajakwambia anataka kufa baba akiwepo?” Bale akaongeza na kufanya wacheke taratibu. “Amelala.” Malon akajibu huku akicheka kwa heshima. “Basi huyo hajui maumivu bila baba yake. Na tungechelewa au angekuwa peke yake, angeanzia nyumbani kwanza, ndio baba yake ampeleke hospitali. Na hatapiga simu kukwambia anakuja akiwa anaumwa. Ili usije mwambia mkutane hospitali. Utashtukia yupo mlangoni, analia kama anakaribia kukata roho. Na amkute baba yake. Asipomkuta, huna dawa utakayompa Naya, ikamsaidia.” Mama yake akaongeza wakacheka taratibu.

Wakaingia kwenye chumba alichopumzishwa kwa muda. Baba yake akamsogelea. “Naya!” Akafungua macho. “Naumwa baba. Nimezidiwa sana.” Malon akaona wadogo zake wanakonyezana na mama yao. “Tokea asubuhi natapika baba. Sipati nafuu.” “Mbona hukunipigia?” “Nilijua nitapona. Lakini nahisi nitakufa tu baba.” Malon akashangaa sana. “Huwezi kufa. Nimeambiwa ni malaria. Ukianza dawa, utapona tu mama.” “Umeniangalia joto lakini?” Baba yake akamuwekea mkono kichwani. “Joto kali. Lakini utapona tu. Pole mama yangu mzazi. Pole sana.” “Asante baba.” “Ngoja nikaombe kitambaa hapo mapokezi, nije kukuwekea kichwani, nikukande mpaka joto liishe.” “Afadhali umekuja baba. Labda nitapona.” “Lazima upone.” “Asante.” Naya akasikika ametulia kwa maneno ya baba yake.

“Mama na kina Bale nao wamekuja.” “Usingekuja na kina Bale!” Wadogo zake wakaanza kucheka. “Watanifanya nizidiwe tu hao.” “Nishawaambia wanyamaze.” “Pole Naya.” Bale akamsogelea. “Sitaki.” Naya akajibu. “Pole Naya.” Mdogo wao mdogo naye akajaribu. “Na wewe pia sitaki. Kwanza sijui kwa nini mmekuja!? Wataanza kunichukua video baba.” “Nimewaonya. Hawathubutu.” Baba yake akamtuliza. “Pole Naya, mama. Pole sana.” “Asante mama. Ungepumzika tu, usingesumbuka. Nimepewa dawa, nitapona tu.” Naya akabadilika kwa mama yake. Mpaka Malon akashangaa. “Hamna shida. Tulilala sana mchana. Hata hao walilala sana mchana ndio maana wametaka kuja na wao.” “Msingekuja nao. Kwanza kesho shule.” “Kweli umezidiwa Naya! Kesho jumamosi.” “Achana na mimi.” Bale na mdogo wake wakazidi kucheka. Malon kimya akiwasikiliza na kuwatizama kwa kujiiba.

“Samahani, tumeingia na swala la ugonjwa tu, tukasahau kufahamiana. Sisi ndio wazazi wa Naya. Hao ni kaka zake.” “Nimefurahi kuwafahamu. Mimi naitwa Malon.” Akajitambulisha tu hivyo. “Tunashukuru kwa taarifa za ugonjwa. Maadamu tupo hapa, wewe nenda tu kapumzike. Wakimruhusu huyu, tutarudi naye nyumbani mpaka apone kabisa.” Zile hazikuwa taarifa nzuri kwa Malon. Lakini akajikaza. “Hamna shida. Nitawasubiri tu, ili niwarudishe nyumbani. Najua usiku sana sasa hivi, mtapata shida ya usafiri.” Mpaka mama yake akamgeukia Malon.

“Umesema wewe ni nani tena?” “Mama!” Naya akashtuka. “Kwani nini? Si nataka kumfahamu?” “Amesema anaitwa Malon.” “Oooh! Wewe ni mwenyeji wa wapi mwanangu?” Akaendelea mama yake Naya. “Naishi Morogoro.” Ukimya wa ghafla. “Sasa nini?” Naya akawauliza. Wakaanza kucheka. Hasa wadogo zake. “Baba si nilikwambia mimi? Heri ungekuja tu peke yako.” Naya akalalamika. “Ujue anachojiuliza mama ni kuwa, Malon wa Morogoro amejuaje kama wewe huku Dar unaumwa?” “Umbea tu. Kwani wewe upo kwenye mawazo ya mama? Hayo ndio mawazo yako wewe Bale. Kwanza ondoka.” Bale na mdogo wake wakaanza kucheka. Na Malon akacheka kidogo.

“Labda mimi niulize, mnafahamiana na Malon?” “Mama Naya! Acha bwana mtoto apone!” “Mimi namuuliza Malon, si Naya mgonjwa!” “Baba umeona sasa? Nahisi utakuwa umejifunza. Siku nyingine usije nao hawa.” “Eti Malon?” “Ndiyo mama. Nafahamiana na Naya. Mmoja wa wanafunzi mwenzake anayeishi naye pale hosteli alimuona akitapika. Ndio nikajulishwa. Ikabidi nije.” “Kutokea Morogoro!?” Bale akadakia na kuuliza kwa mshangao nakufanya wote wacheke mpaka Malon mwenyewe. “Usimjibu mwaya Malon. Hao ni wachokozi tu.” Mama yake akacheka kidogo, akatulia. “Nashukuru sana kumleta hospitalini.” Baba Naya akashukuru. “Na kuja kutokea Morogoro, baba. Morogoro mbali!” Akaongeza mama Naya. “Tena kwa malaria tu!” Bale akaongeza kichokozi, wakacheka tena. Naya akamrushia mto aliokuwa amelalia.

“Haya tokeni nje.” Baba yao akawafukuza. “Sasa hapa kosa langu lipi baba? Mimi nimekukumbusha kushukuru na hilo.” “Baba usimsikilize. Watoe nje. Labda mama na wewe ungeenda kukaa nao hapo nje?” Naya akaongea kwa heshima kidogo kwa mama yake. “Basi nitoke na Malon tuzidi kufahamiana.” “Malon amechoka mama. Mwache bwana.” Wakazidi kucheka. “Sijui mkoje bwana! Baba naomba waambie wakasubiri nje mpaka hii ndipu iishe, tuondoke.” Naya huyu, sio yule aliyekuwa amezidiwa mpaka kutaka kufa. Alishapata nafuu kwa baba yake tu kuwepo hapo, usingeweza jua hata ni kwa nini yupo pale. Baba yake akawafukuza. Akatoka mama yao na kaka zake huku wanacheka. Naya akarudi kulala.

Walikaa pale chumbani kimya. Malon na baba yake. Dripu ilipoisha, Naya akiwa usingizini, Malon akatoka kwenda kumwita nesi. Akaja akamtoa. Akampa kikaratasi cha dawa. Malon akapokea na kumwambia baba yake Naya, ataenda kuchukua dawa, na kulipia kabisa, ndipo atakuja kuwachukua awarudishe nyumbani. “Asante Malon.” “Hamna shida. Nitarudi baada ya muda mfupi sana.” Malon akatoka. Maswali mengi yalianza kwa baba yake Naya. Naya alijua, lakini akanyamaza.

Malon alirudi na dawa mkononi. “Nafikiri tunaweza kuondoka.” “Nashukuru sana. Mungu akubariki.” Baba yake Naya akashukuru. “Amina baba. Basi twendeni ili huyu akapumzike. Kuna dawa za kuzuia kutapika wamempa. Wanasema zinaweza kumfanya alale sana, lakini zitamsaidia kutotapika na kuweza kumaliza dozi yake ya malaria.” “Asante.” Naya akashukuru tena. Malon akamsogelea. “Nikubebe au utaweza kutembea?”  Malon akauliza kwa sauti ya chini ili baba yake asisikie. Naya akakataa kwa kutingisha kichwa huku akicheka taratibu. Malon alikuwa amesimama katikati ya baba yake na Naya. Akamsadia kushuka kwenye kitanda. Wakatoka. Wadogo zake walikuwa wamemuinamia mama yao kama wanaangalia kitu kwenye simu moja. Walipowaona wanatoka, wakasimama.

“Vipi?” Mama yake akauliza. “Tunarudi nyumbani. Malon amesema atatusaidia usafiri.” Akajibu baba yake. “Asante.” Mama yake akashukuru, wadogo zake wakaanza kukohoa kishabiki. Naya akawaangalia. “Sijui mnashida gani nyinyi!” Naya akalalamika. “Sasa tumefanyaje? Sisi tumekohoa tu.” “Twende mwaya Malon.” Naya akaongoza njia, wakawa wanamfuta nyuma Naya. Wakafika nje kwenye gari ya Malon. Wakabaki wamezubaa. “Ni nini jamani kama sio kunitia aibu tu!” Naya akalalamikia wadogo zake. “Bwana baba zungumza nao!” “Hii ndio gari yakutoka Morogoro!?” Bale akauliza, wakaanza kucheka. “Hivi kwa nini hawa hawapandi daladala, baba!” “Tusipande SUV!? Hata kidogo. Hata kwa kupakatana, tunapanda tu.” Malon akacheka.

“Nafikiri tutatoshea tu. Kuna viti vya nyuma kabisa.” Malon akafungua gari ili kuinamisha viti, wapande. “Ungewaacha wapakatane tu.” Naya akaongea huku akifungua mlango upande mwingine nyuma lakini akimpisha baba yake akae mbele. Wadogo zake wakacheka na kuingia nyuma kabisa kwa haraka. Malona akarudisha kiti, nakumpisha mama yake Naya akae pale na Naya. Akafunga mlango, Malon akaingia upande wa dereva, akaanza kuondoa gari.

Akaendesha bila kuuliza. Akafika mataa ya Ubungo, akakata kona kulia, kuelekea Kibaha. “Mama! Bale anauliza mbona Malon haulizi njia? Au anapafahamu?” Kila mtu akaanza kucheka tena. Naya akageuka na kumpiga kaka yake. “Sipafahamu nyumbani. Ila Kiluvya tu.” “Ndio kwetu Malon. Kumbe mwenzetu wewe mwenyeji kabisa. Kumbe ni sisi tu ndio tulikuwa hatukufahamu!” Bale akaongeza kiushabiki. “Baba!” Naya akamwita kwa kulalamika. “Naomba waambie wanyamaze bwana! Wananitia aibu.” Baba yake mwenyewe alikuwa akicheka.

Zikaanza stori mpaka walipofika Kiluvya. “Hapa ndio mwisho wangu.” Malon akamgeukia baba yake Naya. “Hata hapa sio mbali na nyumbani. Ndio kituoni. Tunatembea tu.” “Naweza kuwasogeza mpaka nyumbani, kama ni sawa.” “Ni sawa Malon.” Akadakia Bale. Naya akaguna. “Yaani Bale! Malon anaongea na baba. Wewe yamekupataje?” “Baba hakawii kusema tushushwe hapa wakati tunao usafiri wa Moro mpaka nyumbani tena wa bure!” Ilibidi tu baba yao amuelekeze Malon mpaka nyumbani. Malon alifurahia kufika nyumbani kwa kina Naya.

Wakamkaribisha ndani. Ilikuwa nyumba ya kawaida sana. “Karibu baba.” Akakaribishwa na baba yake mpaka sebuleni. “Asante.” Naya naye akaenda kukaa pembeni yake. “Malon umekula?” Bale akamuuliza. “Tena kweli. Hajala. Alikuwa akinipikia uji, ndio nikazidiwa.” Naya aliropoka tu, akashangaa wote kimya. Naya akajishtukia. “Umepika nini Bale?”  Akajirudi kwa haraka. “Kumbe ulikuwa Morogoro!?” “Acha maswali ya ajabu wakati ulimsikia Malon alikwambia amekuja leo. Wewe sema umepika nini, Malon ale akalale.” “Wali, maharage na mboga za majani.” Bale akajibu. “Akuletee? Bale anajua kupika vizuri sana. Utapenda. Usiondoke bila kula. Usiku umeendelea sana. Utaishia kulala bila kula.” Naya akabembeleza. Wengine wakisikiliza.

“Kalete sasa Bale. Unashangaa nini?” Mama yake akamshtua. “Nilitaka kujua kama atapenda mama.” “Wewe nenda kapashe moto, ulete.” “Na Naya amekuwa anatapika sana. Labda ajaribu kula na yeye.” Malon akaongeza. Naya akasimama. “Wewe kaa tu, watakuletea chakula hapo hapo.” Baba yake akamtaka Naya arudi kukaa. Kikaletwa chakula. Wakala. Malon akashukuru, na kuaga. “Tunashukuru kwa kila kitu Malon.” “Asante kushukuru. Ni sawa kuja kumuona tena kesho?” “Kutokea Morogoro!?” Akadakia Bale. Wakacheka. “Hapana. Nitakuwa Kunduchi kwa muda.” “Aaaha! Ndio huko ulikompikia uji Naya?” Bale akauliza tena. “Usimjibu mwaya Malon. Nenda zako.” “Kwani naongea na wewe Naya? Eti Malon?” Malon akacheka. “Ndiyo Bale. Ni nyumbani kwangu pia.” Malon akajibu huku akicheka kidogo. “Kwa hiyo unaishi Moro na hapa?” “Zaidi Morogoro. Sasa hivi nimekuja hapa sababu ya ugonjwa.” “Wa Naya!?” Bale akadakia kwa mshangao mkubwa sana, nakufanya kila mtu acheke. Malon akasimama.

“Karibu tu. Wakati wowote karibu.” Baba yake Naya, akamjibu Malon. Hilo likamfurahisha Malon. “Nashukuru. Basi nitarudi tena kesho. Naamini sitapotea.” “Kama utaona panakuchanganya, ukifika kituoni piga simu, kina Bale watakufuata tu.” “Nashukuru.” Malon akamtizama Naya. Naya akaelewa. “Twende nikusindikize.” Wakatoka.

“Pole na samahani Malon. Najua ulikuja kwa ajili yangu. Ungependa tukae wote.” “Lakini wewe ulitaka baba ndio akuhudumie.” Malon akamalizia, Naya akacheka kwa aibu. “Na wewe kina Bale wameshakuambukiza?” “Umenitoroka Naya!” “Nahisi napaniki nikiwa mgonjwa. Nitabadilika. Wakati mwingine nitakuwa na wewe tu. Nenda kapumzike, tutawasiliana.” “Nije kesho saa ngapi?” “Muda wowote ule.” “Hata asubuhi!” “Hata asubuhi ni sawa.” “Wazazi hawatakuwa na tatizo?” “Hivyo ulivyowaona, ndio wako hivyo hivyo. Na kwakuwa umetaka kufika nyumbani, mama atajua wewe sio muhuni wa mtaani. Atakuheshimu. Mama ndio mkali sana kwangu.” “Afadhali. Nilete nini sasa?” “Huna haja yakuleta kitu. Si unakuja kuona mgonjwa?” Malon akacheka, nakumbusu kidogo tu. “Nenda kalale. Nitakuona kesho.” Wakaagana. 

Naya akarudi ndani. “Malon ni nani?” Mama yake akamuuliza kabla hata hajakaa chini. “Ananipenda sana Malon. Na ananifuatilia kupita kiasi. Alianza muda kidogo, tokea muhula uliopita. Nilikutana naye kwenye kazi zangu. Hajui jibu la hapana. Yupo tayari kusubiri ilimradi tu yeye awepo kwenye maisha yangu. Mimi nilikuwa nimelala hosteli, nikashtukia ananiamsha, ananiambia ameambiwa ninaumwa. Nikamwambia natapika sana. Ndio akanichukua. Majuzi tu, amenunua nyumba Kunduchi. Kama week mbili zilizopita mimi na wenzangu tulikwenda kufanya kazi hapo kwenye sherehe ya uzinduzi. Nikakutana na wazazi wake.”

“Na hapo nilikuwa nimeshamkataa. Kumbe alishanitambulisha mpaka kwa wazazi wake! Nikiwa nafanya kazi na wenzangu, hata sikua najua kama pale ni kwake, akanifuata jikoni, niende nikasalimie wazazi wake. Nikasita, nikiwa sitaki anitambulishe kwa wazazi wake, nikiwa sijamkubali. Hapo hosteli wanamgombania sababu ya pesa zake. Yeye amenikazania mimi. Mimi nilishamwambia siwezi kuwa kwenye mahusiano sasa hivi nina mambo mengi, hasa shule.” Naya akaendelea huku wazazi wake wakisikiliza na kina Bale.

“Turudi kwenye ufunguzi wa hiyo nyumba. Ndio akanishika mkono mpaka kwa wazazi wake, akawaambia tu huyu ndio Naya. Kumbe wananifahamu. Basi mimi siku ile baada ya kazi iliyonipeleka pale kuisha, nikaondoka zangu, sikutaka hata kukaa. Na hapo nilikuwa nimebadili namba ya simu kwa ajili yake. Sikutaka mawasiliano naye. Akaniomba tena namba mpya. Mimi nikamkatalia. Yaani baba, huyu Malon anakuwa kama amechanganykiwa na mimi! Hata sielewi. Nikiwa nimemkataa na kumpiga marufuku asinitafute tena, na nikafanya juhudi hata yakubadili namba ya simu, eti siku ya birthday yangu akamtuma dada mmoja wa pale pale hosteli aniletee maua, kadi na hii cheni.” Naya akaitoa ile cheni kutoka ndani ya gauni alilokuwa amevaa.

      Mama yake akasogelea. “Si dhahabu hii?” “Dhahabu. Na kidani hiki. Hajui jibu la hapana. Namwambia kwa nini asichukue wasichana wanaomng’ang’ania pale hosteli. Mimi nina malengo makubwa sana mbeleni, anasema yupo tayari kusubiri. Hivi leo alinilazimisha niondoke naye akaniuguze mpaka nipone ndio anirudishe hosteli. Akaniambia nikikataa, yeye anahamia hapo hosteli aniuguze.” Wakacheka.

“Anaonekana ni kijana muungwana.” Baba yake akaongeza. “Mkorofi huyo, ni kwangu tu ndio mtulivu.” “Labda anakupenda kweli.” Mama yake akaongeza huku akiangalia ile cheni. “Hilo sina mashaka nalo. Ananipenda, na hawezi kujisaidia. Namfukuza, namkataa, utashangaa baada ya muda anatokezea tena! Halafu mtoaji sana. Mpaka utamuhurumia.” Wakatulia. “Sasa nifanyaje baba?” “Nenda naye taratibu tu. Utakuja kujua kama ni mwanaume wa kuoa kweli au la.” “Mbona ashasema labda nife au yeye afe! Amesema lazima anioe mimi.” Wakacheka.

“Na usifikiri anatania! King’ang’anizi kupita kiasi.” Wakacheka. “Wewe unampenda?” Baba yake akamuuliza. Wote wakamgeukia. “Maana asije akajaa kwenye maisha yako akakunyima uwezo wakufikiria.” Baba yake akaongeza. “Nafikiri nampenda Malon. Kila nikimfukuza, akiondoka, huwa natamani arudi.”  Wakacheka tu na kuendelea kuzungumza. 

~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~

      Kesho yake mida ya saa nne, Malon akarudi tena nyumbani kwa kina Naya. Akaambiwa Naya amerudi kulala, dawa zinamlevya. “Ameweza kula?” “Amekunywa uji. Na hajatapika tena. Atakuwa sawa tu. Unaweza kurudi tena baadaye.” Mama yake Naya akamjaribu. “Naweza kumsubiria? Kama ni sawa lakini.” Malon akaongea kwa heshima. “Haina shida kabisa. Karibu ndani nikuonyeshe alipo.” Akafurahi sana kukaribisha na mama yake Naya mpaka chumbani kwa Naya. Wakaingia chumbani kwa Naya. Alikuwa amelala hana habari. “Naamini atapona tu. Vipi homa?” “Baba yake alimpima kwenye saa 12 asubuhi, ilikuwa juu. Akampa dawa.” Malon akamuwekea mkono kichwani. Anaonekana hana joto kali.” Mama yake akatoka kuwapisha.

Malon alishinda hapo mpaka usiku. Alikula hapohapo. Hakuchagua wala kujivunga. Kila alichopewa alikula. Na kesho yake pia siku ya jumapili akarudi. Lakini safari hii alirudi na mboga mbalimbali. Nyama ya ng’ombe na samaki wengi. Bale alishinda akikaanga na kuwaweka kwenye friji na wengine kugandishwa. Jumatatu alirudi Morogoro. Hawakumuona siku hiyo nzima. Naya akawa anamalizia dozi yake siku hiyo ya jumatatu. Akawaaga wazazi wake kuwa lazima jumanne, arudi shuleni. Ni kweli alikuwa kwenye kipindi cha mwisho chakumaliza shule. Ilikuwa lazima ajikaze shule iishe. Siku ya jumanne asubuhi Naya alipomaliza kujiandaa, wadogo zake wakiwa wamekwenda shule na mama yake kazini, Malon akarudi.

Baba yake Naya akajua ndio amekuja kumchukua. Wakazungumza kidogo. Baba yake akimsihi apunguze kazi ili atulize mawazo shuleni amalize shule. “Labda umwambie wewe baba. Mimi alinikasirikia kwa muda mrefu sana sababu ya kumpa huo ushauri.” “Wewe ulitaka niache kabisa Malon. Mimi nategemea ile kazi kwa vitu vingi.” “Yule mama nimuelewa Naya. Nimezungumza naye, anaonekana anakupenda na anakuhitaji. Muombe upumzike kazi mpaka umalize mitihani ndipo uendelee na kazi. Nina uhakika ataelewa tu.” “Nitaishije sasa?” “Naya!” Malon akamshangaa. “Basi nitampigia simu nizungumze naye.” “Umeahidi mwenyewe Naya. Tena mbele ya baba. Lazima utekeleze.” “Basi hapo Malon umepata sababu.” “Sio sababu. Tulia umalize mitihani. Kazi zipo na utafanya mapaka mwenyewe uchoke.” “Ni kweli anavyosema Malon. Umebakisha padogo sana. Jikaze umalize vizuri.” Naya akanyamaza. Wakaaga na kuondoka.

“Asante kwa kuniuguza Malon. Nimefurahi.” Malon akacheka. “Lakini umeniumiza kuwa na mahusiano na Lulu.” “Si wewe mwenyewe ulinielekeza kwake?” “Sasa kwa nini umenirudia?” Naya akaanza kulia. “Nakutania Naya. Sikuwa na mahusiano naye. Ilibidi kuwa naye karibu ili niwe karibu na wewe Naya. Ulinikimbia na kubadili namba ya simu! Ulitaka nifanyeje?” “Kunifuata mimi mwenyewe sio kwenda kulala na wanawake ili kunifikia mimi! Umeniumiza Malon. Umeniumiza sana.” “Ila na yeye tokea mwanzo alijua nipo naye ili niwe karibu na wewe. Anajua kama nakupenda.” “Inasaidia nini wakati umeshamvua nguo! Heshima ipo wapi sasa?” “Acha kuzungumzia hayo mambo Naya. Naomba tusirudi nyuma. Nimeomba msamaha. Nakwambia nilikuwa kama nimechanganyikiwa! Natapatapa sijui chakufanya.” Naya akanyamaza.

“Naya?” “Naomba nirudishe hosteli.” “Usianze Naya. Usianze tafadhali. Nichukie, nifanye chochote unachotaka, lakini tuwe wote tu. Umeshajua huwezi kunikwepa tena. Hata ufanyaje, ujue mimi nitakufuata tu.” “Nipe muda wa kukasirika Malon!” “Sio mbali na mimi. Wewe kama umeamua kunikasirikia, uwe na mimi.” “Sasa ndio inakuaje?” “Wewe ambaye hujui kusamehe, ndio utafute hiyo njia Naya. Mimi sijui. Ila ujue mimi nitakufuata popote uendeko.” Naya akamwangalia asiamini.

“Hivi wewe unafikiri ni kwa nini nimenunua nyumba Dar wakati naishi Morogoro?” “Mimi sijui Malon.” “Kwa ajili yako. Ili niwe karibu na wewe.” Naya akamtizama na kunyamaza. “Nakupenda Naya. Mimi siko hivi kwa wanawake. Ni wewe tu.” “Sasa kwa nini hutulii?” “Naya! Nilikuwa na wewe tokea ijumaa. Unataka nifanye nini?” “Usilale na wanawake wengine.” “Ila wewe tu?” Naya akaona hapo pagumu. Akanyamaza. “Naya?” “Mimi nimebakisha muda mfupi nianze mitihani Malon. Nahitaji kutulia shuleni. Nirudishe hosteli.” Malon akamtizama.

“Nini?” “Unaniringia Naya! Na umekusudia kunitesa tu.” “Kwa nini unasema hivyo Malon? Ulitaka nifanye nini? Mimi nimetulia na wewe.” Malon akafurahi sana. “Hata tulipotengana, sijakimbilia kwa wanaume wengine. Au umesikia nina mwanaume?” “Ila Ino alikufuata mpaka hosteli.” Naya akashtuka sana. “Malon!” “Wewe ulifikiri nitatulia tu nisikufuatilie? Nataka kujua kama ahadi uliyonipa unatunza au ndio uliondoka siku ile na kuvunja kila kitu.” “Sasa hao wapelelezi wako wamekwambia nini?” Malon akacheka.

“Kwani wewe mmekubaliana nini na Ino?” “Nilikwambia juu yangu na Ino. Na hakuna kilichobadilika.” “Basi twende nyumbani kidogo, halafu nitakurudisha hosteli. Kuna kitu nataka kukupa.” “Nini?” “Tulia basi Naya wangu.” “Umeniudhi Malon.” “Bado upo na Lulu tu!?” “Sasa je?” “Naya, jifunze kusahau mpenzi wangu. Utahangaika na Lulu bure ambaye sina hata mpango naye. Wewe ndio mke wa Malon, wengine wote wezi tu.” Naya akaguna na kugeukia dirishani.

Malon akacheka. “Nilikuwa na hamu na wewe Naya!” “Hata mimi nilikuwa nakukumbuka, Malon.” Malon akafurahi kusikia hivyo. “Twende mpenzi wangu tukatulie kidogo ndio nikurudishe hosteli.” “Utanikumbatia?” Naya akuliza taratibu. “Sana. Mpaka niridhike.” Naya akacheka. Wakatulia. Naya akajirudisha nyuma, nakupitiwa na usingizi. Alishtuliwa na Malon kuwa wamefika. “Nalala sana!”  “Dawa bado zipo mwilini. Twende nikukumbatie ulale mpaka usingizi uushe, ndipo nikupeleke hosteli.” Naya akacheka kidogo. “Twende.” Akamfungulia mlango, akashuka.

Walielekea moja kwa moja chumbani, Naya akaenda bafuni ndipo akarudi kitandani alipokuwa amejilaza Malon. “Vipi?” “Nipo sawa. Nilikuwa nabadilisha.” Malon akaelewa. Naya akapanda na kujisogeza karibu. “Hizi ni funguo zako za hapa. Muda na wakati wowote unaojisikia unataka kuja kupumzika, unaweza kuja tu. Nitazungumza na walinzi.” Naya akashtuka kidogo. “Malon!” “Ni kwangu Naya. Na sina mtu wakuja kuishi hapa isipokuwa mimi na wewe. Unaweza kuwa unatamani sehemu tulivu, hapa patakufaa. Hakuna atakayekusumbua.” Naya aliipokea ile fungua akabaki akiitizama. “Unafikiria nini tena?” “Sikutegemea. Asante.” “Karibu.” Naya akainama na kuanza kumbusu.

“Nakupenda Naya.” “Najua Malon. Asante.” Akamsogeza karibu akajilaza, akamlalia pembeni. Malon akaanza kumpapasa taratibu. Huku akirudia kumbusu mara kadhaa shavuni. “Malon!” Naya akamwita taratibu tu. Akambusu na kuitika. “Na mimi nakupenda.” Malon akacheka. Akamgeuza upande wake, kutoka vile alivyokuwa amempa mgongo, akaanza kunyonya midomo yake. Shingoni, midomoni. Naya alikuwa akisikia raha ya ajabu. Malon alimchezea kwa muda mrefu, alivuka mipaka mpaka kifuani. Akaishia kwenye matiti hayo ambayo hayakuwahi hata kuonyeshwa mwanaume. Alicheza hapo akiyanyonya na kuyashika taratibu, mwishowe akamuachia taratibu kwa kurudi mdomoni. Maana hali yao wote ilikuwa mbaya na Naya alikuwa bado kwenye siku zake. Wakabaki wanapeana mabusu ya mdomoni. Malon akamfunika shuka, lakini mkono mmoja uligoma kutoka kwenye titi la Naya. Wakabaki wametulia, Naya akapitiwa na usingizi mkono wa Malon kifuani. 

~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~ 

Malon alianzisha jambo mwilini kwa Naya, Naya akabaki akimfikiria. Mitihani ilikuwa karibu na Malon alishamwambia atulize mawazo shuleni. Watapata muda mzuri akimaliza mitihani. Lakini ilikuwa shida kwa Naya. Alikumbuka midomo ya Malon kwenye matiti yake na vile alivyoweza kucheza na chuchu zake. “Utakuja?” Naya akauliza kwa upole. Ilikuwa imeshapita juma moja tokea walipopata muda huo nyumbani kwa Malon, Kunduchi. Wewe unajua ukinihitaji nitakuja Naya. Ila nilitaka utulize mawazo shuleni. Umebakiza muda mfupi mitihani ianze.” Naya akatulia. “Naya?” “Nina hamu na wewe Malon.” “Basi nakuja.” Malon naye akawa kama amechanganyikiwa na Naya. Akiitwa tu, anaweka kila kitu chini, anachukua funguo za gari, safari ya Dar inaanza.

Naya alitoka kwenye kundi la kujisomea, hajaelewa chochote. Akili zilikuwa kwa Malon, amtoe nguo na kumnyonya kama livyomfanyia mara ya mwisho alipokuwa naye. Akarudi hosteli kwenda kuoga na kujiweka tayari kwa ajili ya Malon. Baada ya kama masaa mawili na madakika kadhaa, Malon akawa ameshafika. Kama kawaida akaingia ndani kumfuata. Naya akacheka alipomuona. “Nimefurahi umekuja.” Malon akacheka. “Twende.” Bila kupoteza muda wakatoka. Bila maswali mengi, Malon akakanyaga mafuta mpaka Kunduchi, nyumbani kwake. “Leo nitalala. Na nimebeba madaftari ya kujisomea asubuhi. Usiku nita.. ” Malon akamsogelea, akamkumbatia na kuanza kumbusu.” 

Chuoni Mzumbe.

N

aya akacheka peke yake akiwa bado amekaa hapo chuoni akikumbukia mwanzo wake na Malon. Akajishika midomo yake. Akainama akiwa peke yake na tabasamu. “Malon anajua..”  Akiwa mawazoni akashtukia busu la kichwani. Akashtuka sana. Kugeuka alikuwa Malon. “Malon!” Akasimama. Malon akamvuta karibu na kumbusu. “Vipi? Mbona umekaa hapa peke yako?” “Tulikuwa mapumzikoni. Watu wanakula, tuingie kipindi cha mwisho. Mbona upo hapa?” “Nimekukumbuka, nikaona nije kukuona.” Naya akamwangalia na kucheka.

“Nini sasa? Nimemaliza shuguli zangu mapema, nikaona nije tu. Nimekuletea chakula na zawadi. Ipo kwenye gari.” “Sasa umejuaje kama nipo hapa?” “Nimeuliza, nikaambiwa walikuona umekaa hapa. Unawaza nini?” Naya akafikiria kidogo. “Nini?” “Nilikuwa nakumbuka tulivyaanzana Malon. Ulikuwa ukinipenda karibu kuchanganyikiwa na mimi.” “Bado nakupenda Naya.” Naya akacheka kwa kuguna.

“Mtu angeniambia kipindi kile kama unaweza au ungekuja kunipiga, au ukaendelea kuwa na wanawake wengine!” “Kwa nini husahau Naya? Nimeomba msamaha mara nyingi tu.” “Msamaha hauondoi kumbukumbu Malon. Na unayoyafanya ni matukio yakurudia. Utalala na huyu, nikijua, unaomba msamaha, unatulia au labda unaendelea kwa siri, mpaka najua tena.” Malon akanyamaza.

“Ulinionyesha upendo wa ajabu sana Malon! Sikuwahi kufikiri kama mwanadamu anaweza kumpenda mwanadamu mwenzake kwa kiasi kile. Na tulikuwa na wakati mzuri sana. Ulinifanya nikatulia, na ninakiri wewe ndio uliyenifanya nifaulu kidato cha sita kwa kiasi hiki japo ulishaanza kuniumiza, ila ulinifanya nitulie Malon. Mbaya sana ni unakuwa ukinisaliti katikati ya wakati mzuri. Tunakuwa tumetulia, kuna amani na utulivu, ndipo unapoanza mambo ya ajabu. Najiuliza kuna kuwa na nini? Au ni nini kinakupelekea kuanza kulala na wanawake wengine? Unakuwa hutosheki au inakuwa ni nini! Najiuliza na kuumia sana.” “Nimekuahidi haitatokea tena.” Naya akamwangalia kwa kumsuta.

“Mbona huniamini?” “Kwa kuwa hii sio mara yako ya kwanza Malon! Huwa unashindwa kusimamia hiyo ahadi yako. Upo jasiri kwenye kila kitu, lakini dhaifu sana linapofika swala la wanawake.” “Naya! Umeanza kunitukana, wakati mimi nimekuja hapa kwa upendo tu. Leo ni alhamisi. Najua kesho nakuja kukuchukua hapa, turudi nyumbani. Lakini nipo hapa kukuona tu. Nimeacha kila kitu kwa ajili ya kukuona tu!” “Sijawahi kuwa na shaka na upendo wako kwangu Malon. Hata mara moja. Kweli unanipenda. Lakini huthamini tulichonacho. Sasa sijui ni kwa kuwa nimekuhakikishia sana uwepo wangu!?” Kimya Malon hakujibu.

“Ila Malon, sitavumilia hivi daima. Safari hii ukiamua kumvulia nguo mwanamke mwingine, ujue ndio umeachana na mimi kabisa. Na sitabadili mawazo. Tafadhali naomba jihadhari. Nitakuacha nikiwa nakupenda Malon, lakini sitakuwa na jinsi mpenzi wangu.” Malon akavuta pumzi kwa nguvu, akanza kuondoka. Naya akamfuata nyuma mpaka kwenye gari.

Kweli alikuwa ameleta vyakula. Alikuta na soda mbili. Inamaana alitaka wale pamoja. “Umekula?” Naya akamuuliza baada yakumuona amerudi kwenye gari ametulia kimya kitini. “Hapana Naya. Nilitaka tule wote. Lakini umenijaza tumbo na maneno!” “Nataka ujihadhari Malon. Unajua nakupenda sana mpenzi wangu.” “Lakini unanitisha sana Naya!” “Sikutishi. Nakwambia ukweli na ninatamani uwe umenielewa na usirudie. Kwa kuwa utakaporudia, utakuwa umeniambia wazi kuwa umechagua kuendelea na maisha yako au tabia zako, sio mimi. Namuomba Mungu mchana na usiku unichague mimi Malon.” “Nimekuchagua wewe Naya. Naomba uniamini. Huoni tumekuwa na wakati mzuri?” “Ni kweli tumekuwa na wakati mzuri sana. Hata mimi nimefurahi na ninakushukuru. Asante.” Malon akabaki akimwangalia.

“Nakupenda Malon.” “Najua sana Naya. Na asante.” Malon akavuta mfuko. “Zawadi yako ipo humo ndani.” Naya akacheka nakupokea. “Asante.” Alikuwa amesimama dirishani, upande ule wa dereva alipokuwa amekaa Malon. Akamshika Maloni sikioni, akaanza kumbusu taratibu. Wanachuo wengine walikuwa wakipita, wanawaona. Lakini Naya hakujali.

Tokea ajirudi, Malon alimpa mapenzi ya kweli Naya mpaka mwenyewe Naya alikuwa akishangaa. Kwa kuwa Malon alikuwa akifahamika hapo mjini Morogoro, kila mtu akajua mwanaume aliyekuwa akimshusha Naya hapo chuoni alikuwa Malon. Zamani alikuwa akiishia kwenye gari, Naya anashuka. Safari hii akawa anashuka yeye na kumfungulia mlango, na kumuaga na busu juu. Siku za kumchukua Naya zikawa hazitabiriki. Inategemea na Malon au Naya. Naya akikataa kuondoka akiwa na mitihani, basi Malon ataleta chakula muda wowote. Watakaa kwenye gari, watakula pamoja, nakuondoka kumuacha Naya. Iwe mchana au usiku, hata kama Naya hataondoka naye lakini atakuja kumtembelea. 

~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~

     Mwaka wa kwanza wa chuo cha Mzumbe kwa Naya ukaisha kwa amani na utulivu. Malon akiwa ametulia. Hapakusikika hata fununua kuwa alitoka nje ya mahusiano tena, japo na hapo chuoni alishafahamika sana. Fujo za mabinti wa hapo napo hazikutofautiana sana na kule hosteli alikokuwa Naya akisoma sekondari, ila hapa chuoni kukawa na usiri mkubwa. Naya akashindwa kujua ni yupi ameshafunuliwa na Malon, akazidi kujitenga nao.

 Kwa kuwa walishaanza kuishi pamoja kama mke na mume tokea Naya yupo kidato cha tano na sita, hata kipindi cha likizo, Naya alikuwa nyumbani kwa Malon. Wazazi wa Malon, ndugu na jamaa wa karibu na Malon wote walijua mahusiano hayo kwa undani huo, isipokuwa wazazi wa Naya hawakujua kama Naya anaishi na Malon kama mke, ila kujua yapo mahusiano kati yao na akimaliza chuo wataoana. Naya aliaminika sana nyumbani kwao kwa uwezo wakuzaliwa na kuishi katikati ya jiji na kuweza kuepuka vishawishi hata alipokuwa nyumbani hajaanza maisha ya hosteli. Kama hayupo nyumbani akibishana na Bale, basi ujue wapo na huyohuyo Bale kanisani wakifundishwa kwaya na Ino pamoja na vijana wengine.

Hakuwa na tamaa ya wanaume wala hakuwa akisumbua nyumbani kwao kwa tabia za uhuni. Kipenzi cha baba na akaaminika sana kuwa anajitunza. Na kilichomvutia hata baba Naya, ni kule kwa Malon kuongeza msisitizo kwenye elimu ya Naya. Akimtaka akazane na shule si kazi tu. Na kweli Malon alimpenda Naya na kumtunza vilivyo. Hapakuwa na shaka juu ya mapenzi ya Malon kwa Naya. Linapofika swala la Naya, kila kitu huwa kinasubiri kwanza.

Maisha ya wapi wanaishi ilikuwa ikitegemeana na ratiba za Naya na Malon. Kama Naya yupo likizo, basi atakuwa ni wa Malon kabisaa. Alipo  Malon ndipo atakuwepo Naya. Alishaacha kazi kwa Madamu Vane muda mrefu tu. Lakini akabakiwa na kisingizio cha kazi ili kudanganya wazazi wake anakazi awapo likizo ili awe na Malon bila shida. Akadanganya pia kwa wazazi wake kuwa nyumba ya Malon ya Kunduchi ameachiwa yeye ili aitumie itakapo mlazimu, atokapo kazini usiku sana. Kwa usalama wake asiwe akisafiri usiku atokapo kazini kwenye kazi za Madamu Vane kurudi nyumbani kwao Kiluvya ambako ni mbali sana na mjini. Hilo nalo likaongeza sifa na kujali kwa Malon, nyumbani kwa kina Naya. Kwamba anamlinda Naya vizuri. Wazazi wake wakijua kuwa ameachiwa nyumba na Malon anayeishi na kufanya kazi Morogoro, amempa funguo za nyumba hiyo na kumuwekea ulinzi, aishi bure kwa usalama wake Naya asiwe anazunguka usiku akitokea kazini, kumbe huyo Malon alishaanza kula faida za ndoa tokea Naya ni mtoto wa sekondari.

Naya akiona amekaa sana kwa Malon, atashtukiwa nyumbani, ndipo atarudi kwa wazazi kulala hata siku mbili au tatu, kisha anarudi tena kwa Malon. Chuo kikifunguliwa, wakidhani anaishi chuoni, kumbe nyumbani kwa Malon, Morogoro au kweli siku chache chuoni tena endapo wanamitihani, au wamegombana tena. Wazazi wake hawakujua linaloendelea walibaki kumpongeza Naya kwa kuweza kumudu ratiba za kazi na shule.

~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~

Safari za Brazili na Dubai zilikuwa za kawaida sana kwa Naya na Malon. Kukaa mtaani kwa muda mrefu kwa Malon baada ya kukataa shule, kukamsaidia kujua mengi. Alifanikiwa kununua kibali cha kimataifa cha ufanya biashara. Alikuwa akinunua sukari kwa bei ya chini sana nchini Brazili na kuuzia nchi kama Dubai na nchi nyingine ambazo hazikuwa na masharti magumu. Kwa hiyo kila Naya anapokuwa likizo, na Malon akiwa na safari, basi atakwenda na Naya.

Maisha ya Naya yakaendelea kubadilika siku hadi siku, utu wake wa ndani ulivyokuwa ukibadilishwa kwa kasi kama huo utajiri wa nje aliovalishwa na Malon. Wazazi wake wasijue kinachoendelea, wakidhani ni binti mdogo, kumbe alishajiingiza kwenye maisha ya haso za ndoa muda mrefu tu. Naya mtoto wa kanisani aliyetulia, mwadilifu, akajiingiza kwa Malon mtoto wa mtaani haswa aliyeshindikana hata kwa wazazi wake. Ngono kwake ilikuwa ni starehe kama starehe nyingine yeyote ile akijiburudisha tu. Ila Naya akiamini ni jambo la heshima sana. Linatakiwa kuwa la watu wawili tu waliokubaliana. Akafungwa ndani ya penzi zito la Malon na pesa yake ambayo ni kweli ilimsaidia Naya. Maisha ya aina hiyo  yakaendelea. 

Malon na Ndoto Za Naya. 

K

atika safari hizo za nje ya nchi Naya akapata wazo la kuweka kwenye matendo kipaji chake cha ubunifu. Maswala ya ubunifu wa mavazi kitu anachopenda na kukijulia sana. Aliona vile chuoni alivyopata wafuasi wengi wakijaribu kumuiga kwa kila anachovaa. Kila wakati wakimsubiria ashushwe garini au atoke chumbani kwao, aonekane amevaa nini siku hiyo na kuwa gumzo siku nzima wakimthaminisha na wengine kujaribu kwenda kutafuta aina hiyohiyo ya vitu vya Naya. Hicho kikamuongezea ujasiri. Akataka kubuni na kuuanza kujitangaza yeye kama Naya, na kuwauzia watu. Binti huyo mwanafunzi wa masoko, akajua biashara matangazo. Ili kujulikana na kufikia wengi ni lazima kufanya maonyesho ya mavazi.

Akamshirikisha Malon, kwa kuwa ni kitu anachokipenda Naya, Malon akakubali bila shida tena kwa haraka sana. Na kwa kuwa pesa ya Malon ilikuwepo utekelezaji wake hata Malon hakuona kama utasumbua, pesa ipo ni kutendea kazi tu. Na kwa kuwa Malon alikuwa akifahamika sana hapo mjini Mororgoro, Naya naye akafahamika kwa haraka sana hapo Morogoro kama mwanamke wa Malon. Kwa hiyo haikuwa shida kuzungumza na yeyote anayemtaka. Na jijini Dar napo ikawa rahisi. Kazi aliyokuwa akifanya tokea kidato cha nne, ilimkutanisha na wengi. Kwa hiyo akajua haitakuwa shida kufikia ndoto zake.

Akafikiria kitu mashuhuri nchini Tanzania ambacho hakitagharimu wengi na kila mwanamke wa kitanzania anatumia. Tajiri kwa msikini. Wazo likamjia kuwa ni khanga. Akawekeza muda wakutosha kwenye kuandaa hilo. Akaanza kwa michoro. Akichora mitindo mbali mbali. Huku akiwa tayari na picha ya warembo atakao watafuta wakipita jukwaa siku ya tamasha lake. Nini anataka wageni wake waone na kufurahia! Hiyo ikamuongezea hamasa na ari kwa kuwa alishaona mwisho tokea mwanzo.

Wakati akiendelea kuchora, huku anaandaa mipango ya idadi ya warembo atakao hitaji siku hiyo. Kuanzia wembamba sana, umbo la kati na wanene kiasi mpaka wanene kabisa. Ikaanza kazi ya kuwatafuta na kuandaa mitindo aliyobuni yeye mwenyewe. Kokote alipokuwa hata mapumzikoni na Malon, basi utamkuta akiwa peke yake akichora na kuweka mipango yake. Katika hilo Malon akazidi kumpenda na kumuheshimu sana Naya.

“Kwani unataka watu wangapi?” Malon akamuuliza. “Kwa kuwa ndio ninaanza, nataka wasichana 12 tu. Niwafundishe mwenyewe, ndipo niwaweke jukwani. Sitaki wajuaji sana kama kina Tula. Watanisumbua. Nataka wasichana wakawaida ambao wataweza kunisikiliza na kuelewa kwa haraka, lakini pia sitaki washamba sana.” Malon akacheka. “Na kwa kuanzia, kila mmoja nataka apite na mavazi yasiyopungua matano.” “Tofauti!?” Malon akashangaa sana. “Mbona nimeshafikisha mitindo 53 tofauti! Nitafika tu mavazi 60. Naanzia Dar, nitafanya na Morogoro. Mwitikio ukiwa mkubwa, nitafanya na mikoa mingine. Baadaye nataka nifungue sehemu yangu ya kushonea. Watu ambao watatengeneza nguo nitakazobuni mimi mwenyewe, na ziuzwe kwa jina langu.” Malon akakaa sawa na yeye akiwa amesha hamasika.

“Vyote vinaweza kuanza pamoja Naya. Tena wakati unafanya hayo maonyesho, unawaelekeza watu kwa mafundi wako.” “Kweli Malon!?” “Kabisa. Hakuna kupoteza kwenye kuwekeza. Kwani kinachohitajika ni nini? Si eneo tu?” Malon akauliza kama kitu kidogo sana. Naya akaanza kuona ndoto zinaweza kutimia mapema zaidi ya alivyotarajia. “Unakumbuka tulivyokuwa China tulienda kutembelea wale mafundi wanaotengeneza nguo? Ukauliza wanafanyaje? Wakakwambia wanapokea vipimo kama hivyo kwa njia ya mitandao tu. Mtu anachagua nguo online. Anatuma vipimo au anachagua vipimo vyake hapo mtandaoni na pesa, anatengenezewa na kutumiwa. Au kubuni zaidi jinsi yakuwahudmia kirahisi. Hakuna kupoteza kwenye kuwekeza. Tufikirie kufungua sehemu ambayo tutaweka mashine za kisasa za kushonea na kuajiri mafundi. Tunafanya hayo maonyesho ya mavazi ili kujitangaza kwa wengi, na kuhakikisha kila anayetaka vazi fulani analipata kwa haraka, tena kutoka kwa mafundi wako. Na kwa kuwa unakipaji cha mitindo kizuri na chatofauti, kwa muda mfupi sana utakuwa mbali mno.” Naya akafurahia hilo wazo, maana na Malon mwenyewe alijiunganisha na hilo wazo kumuashiria atasimama naye.

“Sasa eneo?” “Kwa kuwa wewe utengenezaji wako nguo utakuwa tofauti. Tutafute eneo kubwa. Hata shamba tu. Tujenge hapo lijengo likubwa tu kama godauni. Tuweke mashine za kisasa kama nilivyokwambia na tutafute watu.” Naya akaona faida ya kutoka na mtu kama Malon. Mwenye pesa na akili yakuwekeza. “Basi ngoja nimuombe baba atutafutie eneo hata maeneo ya mbele ya Kibaha. Tutapata kwa bei nzuri.” “Sawa tu.” Malon akakubali bila shida. Kwa kuwa alishaishi na Naya, akaujua moyo wake na tabia zake. Na alijua kwa hakika atamuoa tu, akajua hapotezi atakapowekeza kwake. Hakufikiria hata mara mbili. Kwanza akafurahia kupata mwanamke kama Naya.

Naya akampigia simu baba yake wakiwa nchini Dubai, akamueleza mipango yake na mawazo ya Malon. Baba yake akampongeza sana na kumuahidi kutoka muda huo kwenda kusaka eneo. Na kweli, kabla ya kurudi nchini, baba yake Naya akawa amepata eneo zuri tu, maeneo ya Picha ya ndege, karibu tu na Kibaha. Alipokutana na mwenye hilo eneo na kumpa bei, akampigia simu Naya kumjulisha. Malon aliposikia bei, akakubali na kuzungumza na mwenye kiwanja kuwa atakwenda kumuona watakaporudi nchini.

Baada ya siku 4 mbeleni, Malon na Naya waliporudi nchini, wakaelekea Picha ya ndege kuonana na muuza lile eneo. Walifuata taratibu zote za manunuzi. Bila kupoteza muda, Malon na Naya wakaanza kufuatilia hati ya lile eneo. Ikawa chini ya jina la Malon na Naya. Akili za Naya, zikahamia kwenye ujenzi wa lile eneo huku akiendelea kutunza mitindo yake aliyokuwa akibuni yeye mwenyewe. 

~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~ 

Sasa ili asipoteze wateja au umaarufu mjini kwa kuwa alishaacha kazi za waitress kwa Madamu Vane, Naya akafikiria kufanya kitu cha kumjengea jina mjini na kumsogeza karibu na watu. Akapanga kila mwisho wa mwezi, kukutanisha watu mbali mbali kwa lengo tofauti tofauti. Akafikiria wakati mwingine akutanishe wanawake tu, akitaka kuwafanyia maonyesho ya vipodozi mbali mbali atakavyokuwa anavitoa Dudai na nchi nyingine atakayokuwa akipata kwa bei nzuri na kuja kuwauzia nchini. Au Perfume za kike na kiume. Hapo akapanga kuwe na kula na kunywa na kuwatafutia wageni wake viburudisho mbali mbali. Auze bidhaa mbali mbali. Viatu, pochi na kadhalika. Na hakutaka kuwe na watu wengi. Malengo ni kwa watu wachache na wenye pesa. hilo nalo likafanikiwa, Malon akiwa nyuma yake kumuunga mkono.

Naya alikuwa mtoto mdogo lakini mwenye akili iliyomshangaza mpaka Malon akajua hata akifilisika kwenye biashara zake, basi anaye mwanamke wakumuinua. Hapakuwa na swali kama ni watu waliokusudiwa kuwa pamoja au wanaofaa kuwa pamoja. Walikuwa wakiendana kwenye mawazo ya kibishara na kuungana mkono. Na huo mpango Malon akaukubali bila shida. Naya akaanza kufanyia kazi mawazo yake. Akaanza kufanya tafrija ndogo ndogo mjini. Akisaidiwa kutafuta kumbi kwa bei nafuu na Madamu Vane. Basi atapatengeneza na kualika watu aliowakusudia kwa wakati huo, anauza vitu. Warembo wote aliokwisha fanya nao kazi na marafiki wa marafiki zao Naya akawatafuta. Basi na kwa kuwa alijua ni nini warembo wa mjini wanataka, na wanawake wenye pesa, Naya akawa akiingiza bidhaa hadimu. Hana duka. Analeta vitu. Anauza kwenye tafrija anazokuwa akiandaa. Anamaliza na kubuni kingine na shule ikiendelea na ujenzi kupamba moto.

 Mahusiano yake na Malon yakawa yameongezeka, kutoka kuwa tu wapenzi, mpaka kuwa wawekezaji wa pamoja. Kila faida aliyokuwa akipata ya ziada, alijitahidi kukumbuka kwao, hasa baba yake. Hakufanya kitu bila kumshirikisha baba yake aliyekuwa anajiona ni kama alijizaa pale kwa Naya. Akili ya kufikiria na kuchukua hatua. 

~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~

Alimnunulia baba yake gari nzuri tu kutoka kwa mtu aliyekuwa akiuza kwa bei nzuri pia, aina ya pickup. Ikawa msaada sana kwenye biashara ya baba yake. Kubebea mayai na maziwa kusambaza mjini. Pesa ya Malon, wazo kutoka kwa Naya. Wadogo zake pia aliwashirikisha kwenye mambo anayofanya. Naya na familia yake wakaanza kuinuka kiuchumi. Hakuna kukopa hovyo tena. Naya alijua nini kinahitajika kwao, basi hakuacha kumsaidia baba yake.

 Malon na Naya wakazidi kupanuka na kujulikana kwa bishara. Morogoro sababu ya Malon, watu walijazana kwenye matamasha yao. Dar sababu ya Naya. Ungependa uwaone pamoja. Walijua kuvaa. Walijua kuungana mkono kwenye mambo yao. Akisimama Naya, ujue Malon na Chezo wapo nyuma yake. Mwili wa Malon, ulivutia kutizama alichoweka. Na Naya alijua kujipangilia haswa. Mtoto huyo aliyekuwa akiimba kwaya kanisani na kwenye matamasha ya dini, hakupata shida kusimama mbele ya watu na kunadi bidhaa zake. Akajibeba kimwanamtindo haswa, ukichanganya na akili na ubunifu aliojaliwa na Mungu, sura na umbile lake, lazima ufurahie kuwa kwenye kila tamasha wanaloandaa.

Shule nayo ilikuwa ikiendelea, huku maisha ya nje yakiendelea. Na kwa kuwa alikuwa na mama mwalimu wa shule ya msingi, Naya alikuwa akitamani kulia. Utafikiri mwalimu anayemsimamia mwanafunzi na kiboko. Neno shule, lilikuwa kila wakati mpaka Naya alikuwa hataki kumpigia simu mama yake mara kwa mara. “Fanya mambo yako weee, lakini uniletee cheti hapa nyumbani. Wajukuu wanaweza kusubiri mpaka shule iishe. Lakini wakitokea hapo njiani, niletee nilee mwenyewe, shule hiyo iishe Naya.” Alimkera kwa hayo maneno kila anapomuona Naya. Hata kama akimpa habari njema kuwa amefanikiwa kwenye tamasha fulani, au jengo lao linaendelea vizuri kwenye ujenzi, basi mama yake lazima atamalizia kuwa anataka cheti kizuri nyumbani. Basi Naya hakuwa na mapumziko. Akiwa shule, basi akili zinakuwa shule. Na anapokuwa nyumbani, kwenye mambo yake anakumbushwa na shule. Akawa busy kupita kiasi.

Wakati anamaliza mwaka wa pili, Malon naye akawa amemaliza ule ujenzi huko Picha ya Ndege. Lilikuwa tu kama godown, lenye ofisi 4, mlemle ndani. Zilitenganisha na mbao chini, vioo juu. Ofisi ya Meneja ambaye ndio Naya. Malon naye akajiwekea ofisi yake yeye mwenyewe Malon. Ofisi ya masoko. Ofisi hiyo ya mtu wa masoko aliifanya kubwa kidogo. Kukawekwa meza tatu. Alimwambia Naya, wanahitaji mtu ambaye atakuwa akitafuta wateja, mtu wa kupokea kazi kutoka nje na ndani ya nchi, na mtu ambaye atakuwa akiandaa hizo oda kutokana na tarehe alizopokea, na kupeleka kwa watendaji pamoja na ofisi ya wafanyakazi wa stoo. Napo kwenye hiyo ofisi palikuwa pakubwa tu kwa ajili ya mtu wa kutoa oda ya malighafi. Kumwambia Naya na Malon ni nini chakununua na usafirishaji wa nguo za watu na kupokea kutoka kwa mafundi.

Naya alifurahia kila kitu kwenye lile eneo. Walirudi China tena kwenye kiwanda wanachotaka kuwaiga. Wakatumia muda hapo kujua ni vipi wanafanya na aina gani za mashine. Malon akanunua vitu kama vile walivyoona kwenye hicho kiwanda. Wakati huo nchini Tanzania mama yake Naya akiendelea kutafuta mafundi wazuri ambao bado hawajawa maarufu sana. Tena alitafuta wale mafundi wa kawaida tu wanaoshona nje ya nyumba zao. Akazungumza nao. Naya alitaka wawe 10 tu kwa kuanzia. Ili aweze kuzungumza nao na kuwafundisha ni nini anataka kutoka kwao.

Waliporudi nchini, walikuwa wameshazungumza na Malon juu ya malipo kwa hao mafundi. Badala ya kulipwa kwa nguo, Malon na Naya, wakawaahidi mshahara kabisa na marupurupu kama chakula cha mchana kitakachokuwa kikipikwa hapo hapo kazini, tena bure. Wote hao mafundi wakakubali bila shida. Kutoka kuganga njaa na kushonea watu nguo moja mwezi mzima, pale walipewa mashine za kisasa, mazingira mazuri na wakawa wengi. Wakagawana kazi kutokana na ujuzi. Kiwanda kikafunguliwa rasmi.

Mpaka Naya anarudi chuoni kumaliza mwaka wa mwisho, kiwanda chake kilikuwa kimeanza. Walikisajili kwa majina yao. Malon na Naya. Naya ndiye aliyekuwa mtoa mitindo yote aliyokuwa amebuni. Kazi yakutengeneza na marekebisho ili kitokee kitu anachokitaka yeye mwenyewe Naya, ikaanza. Hakutumia vitu vya gharama sana ili kuweza kufikia watu wengi. Alitumia khanga, vitenge, na vitambaa tu vya kawaida alivyoweza kuvipata kwa bei nafuu. Lakini alibuni mitindo mizuri sana. 

Mwaka wa tatu na Wa Mwisho Chuoni

C

huo kikafungua, mwaka wa tatu akienda kumaliza, mambo yakiwa mengi mno. Naya akawa na majukumu mengi kupita kiasi. Shule ambayo ndio ilikuwa salamu ya mama yake, hicho kiwanda, Malon mpenzi wake, na tamasha alilokuwa akiliandaa, na kuendelea kujitangaza jijini Dar kwa mavazi. Maonyesho ya kwanza alikusudia kufanya kwa watu aliokuwa akiwafahamu kwanza na marafiki zao. Alikuwa akiwapigia simu, kuwakaribisha yeye mwenyewe rasmi, na kuomba wakaribishe wengine. Idadi ya tamasha la kwanza hakutaka iwe kubwa. Ilikuwa na kiingilio kwani aliandaa na viburudisho vingine. Naya na Malon wakawa busy kupita kiasi, wakiwasiliana huku na kule kuhakikisha jambo lolote haliharibiki.

Malon aliwekeza pesa na nguvu. Alimsaidia Naya na kuamini kile anachokifanya mpaka Naya na wazazi wake walikuwa wakimshangaa Malon. Lile wazo la Naya, alilipokea na kulifanyia kazi kama lake! Sehemu nyingi na mambo mengi alifanya Malon, ili Naya atulie shuleni kwa kiasi fulani, japo kuna mambo mengine yalimuhitaji Naya mwenyewe.

Nidhamu ya shule ikaongezeka ili asije kufeli hata somo moja na kumlazimu kurudia. Kwa hiyo kila alipopata mwanya, popote alipo, akili alirudisha shuleni, kusoma. Hakuwa na masaa mengi ya kulala kama wengine, ila kufanya kazi, shule na kuandaa hilo tamasha alilotaka lifanyike kipindi cha likizo. Hakujulikana analala wapi. Kama ni chuoni au kwa Malon hapo hapo Morogoro au Dar.

Mpaka inafika katikati ya mwaka wake wa mwisho wa shule, mambo hayakuwa mabaya. Hakuwa akifaulu sana, lakini alikuwa na uhakika hatafeli somo hata moja. Alipomaliza tu mitihani yake ya muhula wa kwanza, Malon akaenda kumchukua, safari ya Dar kumalizia maandalizi ya tamasha, ikaanza. Kuhakikisha nguo alizobuni zipo sawa, na wavaaji pia wapo sawa, na pia kuhakikisha anawanoa vilivyo ili waweze kuzitendea haki jukwaani. Hapakuwa na mapumziko mpaka aliporidhika kila kitu kipo sawa. 

Siku ya Tamasha La Mavazi Ya Naya.

S

iku ya tamasha yenyewe kila mtu aliyemfahamu Malon alinunu tiketi akawepo ukumbini, Ubungo Plaza, Dar. Chezo naye alikuwa akihangaika tu kama Malon, akihakikisha hilo tamasha lenyewe linafanikiwa. Kuanzia usalama wa wageni wao, ukaaji pale ukumbini ambapo walipapamba vizuri na kuweka jukwaa zuri tu la kutembelea hao wavaa mavazi aliyobuni Naya. Kulikuwa na vinywaji vingi tu kwa wageni wao.

Muda wote huo Naya na mafundi wake walikuwa kwenye vyumba vya nyuma wakiwasaidia wavaaji wao kuvaa na kuhakikisha nguo hizo zinawakaa vizuri. Malon alikuwa ukumbini na wageni waalikwa pamoja na Chezo. Malon akamtuma Chezo ampelekee Naya maji ya kunywa. “Hajala kitu tokea asubuhi. Naomba mpelekee haya maji na soda.” Chezo akachukua na kurudi alipokuwepo Naya.

Katika wasichana wote waliokuwepo pale kambini, Naya alitokea kumpenda Loi, binti aliyetokea Morogoro. Alikuwa na umbile la kati tu. Zuri lililopendeza kila nguo. Na uzuri wa Loi alikuwa mwepesi. Wakati wa mazoezi, kila Naya alipokuwa akimvalisha nguo ya aina fulani, kwenye kundi fulani, alimtaka yeye ndio awe anapita wa kwanza kisha kurudi kwa haraka kuvaa vazi aina jingine, apite na kundi jingine labda la kundi la mavazi ya ofisini kama wametoka kwenye vazi la kanisani au ufukweni. Na Loi alifanya hivyo kwa haraka sana, bila kuchelewa, kitu kilichokuwa kikimfurahisha sana Naya, na kumfanya Naya kumsifia mbele za wenzake walipokuwa wakifanya mazoezi huko kwenye hoteli waliyokuwa wamekodishiwa na kufanya kambi ya siku tatu kabla ya siku hiyo ya tamasha. Kwenye kila zoezi, Naya alimsifia Loi akiwa hana hila kabisa ila kutambua kipaji chake.

Asidi Haachi Asili.

W

akiwa kwenye pilikapilika ya kuvaa na kutengenezwa, Naya akawasikia wakilalamikia uchache wa aina hizo za pini wanazotumia kwa warembo hao na wanazihitaji sana. Akakumbuka alikuwa nazo kwenye gari aina hizo za pini alinunua zamani akabaki akizunguka nazo tu kwenye gari. Akatoka pale kwenye kile chumba walichokuwepo wale warembo kufuata hizo pini garini. Alirudi kimya kimya bila wengine kujua na kumkabidhi mmoja wa wapambaji kisha akarudi kufanya kazi kwenye nguo ya Loi, ambaye ndio alitakiwa kuwa wa kwanza atakayeongoza kundi la kwanza la mavazi ya weekend kwa wadada. Akiwa ameinama anamtengeneza yule msichana, na Chezo naye akawa ameingia na vinywaji vyake wote wakasikia minong’ono kwa nyuma.

Japo ukumbini kulikuwa na mziki ukiendelea, ila waliweza kusikia. “Na angejua kama Loi ni mke mwenzie, wala asingehangaika naye hivyo!” “Hawezi kujua. Malon ni mshenzi. Anacheza karata zake kwa akili. Alitaka mimi ndio nimpendekeze Loi kwa Naya, ili Naya mwenyewe ampigie simu. Na kweli, Naya akakubali na kumpigia Loi. Wote wanamfanyia kazi yeye Malon, bila wao kujua.” Mwingine akaongeza. “Lakini nasikia hii shuguli ni ya huyu dada!” “Sio yake Naya. Na yeye mfanyakazi wa kulipwa tu kama sie. Sie Loi katuambia. Anasema Malon amemwambia ameona huyu Naya anaakili ya mitindo, ndio akampa hii kazi. Kwani nyinyi hamumjui Malon jinsi alivyo mshenzi kwa wanawake? Anajua kut..” Chezo akakimbilia kule walipokuwepo wale wasichana wakinong’ona kwenye chumba cha pembeni, hakikuwa na mlango.

Wote wakashtuka kwa sababu walikuwa kama wapo nusu uchi. “Kwa nini hugongi Chezo, wewe!?”  Wengi walikuwa wakimfahamu Chezo kwa kuwa walitokea Morogoro na wale wageni pia walimfahamu kabisa kwa kuwa kwa siku tatu ambazo Naya aliwakusanya kwenye hoteli, na kuwaleta hapo ukumbini kwa mazoezi, Chezo na Malon wakisaidiana na Naya, walikuwa karibu nao sana. “Toka bwana.” “Nilitaka kuwaomba tu, habari zenu za umbea, msubiri mtakaporudi hotelini au Morogoro. Hapa tunataka mfanye kazi tuliyowaitia. Kama mnaona hamuwezi, ondokeni.” “Hapana Chezo.” Naya akaingilia.

“Malon amemwaga pesa nyingi sana kwenye hii shuguli. Kwanza naombeni wote mje hapa.” Naya akawaita. Wote wakasogea. “Naombeni tusikilizane. Kama nilivyowaambia mwanzo. Malon amemwaga pesa nyingi sana kwenye hii shuguli. Wote sisi tutanufaika kwa namna moja au nyingine. Na ninaamini katika juhudi tulizoweka kwenye hii shuguli nzima, tutafanikiwa tu. Sasa, sidhani kama kuna hata mmoja wetu hapa anataka leo ndio iwe mwisho.” Wote wakatulia. Naya akawaangalia mmoja hadi mwingine.

Ukweli wote waliingiwa na hofu, wakijua Naya amewasikia na Malon ni mvuta bangi. “Eti jamani?” Naya akaliza akiwa ametulia tu. “Hapana.” Wote wakajibu. “Basi. Ili kufanya tamasha hili liendelee, na tufanye mengine zaidi, nilazima tuweke akili zetu hapa. Kwanza kuhakikisha tunafanikiwa kuwauzia huduma nzuri wateja wetu, na kuhakikisha pesa ya bosi wetu Malon, inarudi.” Naya aliongea hiyo sentensi kwa tabasamu. Lakini Chezo alijua wazi ameshabadilika.

“Na niwaombe radhi kama nimeonyesha upendeleo kwa Loi. Mnisamehe. Labda kwa kuwa amekuwa kwenye kila kitu. Naona na kutambua juhudi mnayoweka nyinyi wote hapa. Sina nia yakuonyesha huyu anafaa na huyu hafai. Wote mpo hapa kwa kuwa nimewaamini na ninajua mnaweza. Hata kama utaonyesha vazi moja tu nililokupangia, ujue ni kwa kuwa nimekuamini kama unaweza kuwakilisha mawazo yangu kwenye hilo vazi. Hakuna vazi hata moja nililobuni ambalo si la thamani. Yote imenilazimu kukaa chini, kuchukua muda mrefu kufikiria na kuchora, ndipo kushonwa mpaka kufika mwilini mwako. Hapakuwa na vazi lisilo la thamani na hakuna asiye na thamani kati yenu. Kwa hiyo naomba tuendelee na kama tulivyozungumza, naomba mjiamini.”

“Mmevaa vitu vya thamani sana. Lakini kama utavaa hilo vazi, halafu wewe mwenyewe ukawaonyesha wateja wetu upo duni, inamaana aina hiyo ya vazi ndio halitauzika sokoni. Naomba kila mmoja wenu, ajiamini, na kila mmoja wenu ajue yupo hapa kwa sababu najua mtaweza kuuza bidhaa zote tena kwa bei ya juu. Sijui kama mmenielewa?” “Sisi tumeelewa Naya. Na tunaomba msamaha. Hatukutak..” “Wala msijali. Naomba turudi kwenye kujiandaa.” Naya akamaliza hapo na kurudi kumtengeneza Loi.

Chezo alibaki ameduaa hapo kwa dakika kadhaa, akaamua atoke. Naya hakumuongelesha kabisa Chezo, kwani alijua kama kweli Loi ni mwanamke wa Malon, na yeye lazima anajua ila amemficha. Aliumia sana kuona anazidi kujidhalilisha. Kusikia kuwa Malon anatangaza kama ile ni biashara yake, na Naya ni mfanyakazi tu, iliondoa nguvu kubwa sana moyoni mwa Naya. Ile morali ikaisha kabisa. Akatamani ingekuwa sio siku yenyewe ya tamasha hata angeahirisha. Lakini hata wazazi wake walishakuwa ukumbini wakisubiria kwa hamu hilo tamasha lianze. Aliwekeza nguvu nyingi sana. Ndoto na mawazo yake yalishafika kwenye uhalisia, tayari kuonyesha kwa walimwengu! Naya akaamua kujikaza tu, ili ile ndoto yake itimie. Akajiambia afanye kwa ajili yake mwenyewe.

~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~ 

C

hezo alitoka pale akaamua atoke kabisa pale ukumbini. Akaenda kusimama nje ya ule ukumbi lakini ndani ya lile lile jengo, akasimama akiwa ameegemea ukuta. Na yeye akawa kama amepigwa na butwaa. Malon akawa amemuona kwa mbali akitoka, akamfuata kwa haraka. “Wewe vipi? Shuguli inakaribia kuanza.” Kimya, Malon akashangaa na kushindwa kumuelewa jinsi alivyobadilika. “Vipi Chezo, mbona hivyo kaka!?” Chezo akaguna na kubaki akitingisha kichwa. “Nini tena?” Malon akazidi kuuliza asimuelewe Chezo.

“Hivi shida ni nini Malon?” “Kwa nini tena!?” Malon akawa bado hajaelewa. “Hivi unakuwa zile hamu za kuku ambazo huwezi kuvumilia, au unakuwa unataka kuvua tu wanawake nguo?” “Chezo!” Malon akatoa macho. “Tafadhali niambie Malon. Kinachokufanya unahangaika wakati unaye Naya, ni nini ndugu yangu!?” Hapo Malon akanyamaza kidogo. “Eti Malon?” Kimya. “Kwa nini unamtesa na kumdhalilisha Naya kwa kiasi hicho Malon!? Wewe mwenyewe uliniambia hakuna mwanamke anayekukata kiu kama Naya. Sasa kwa nini unapita kufunua funua wanawake wengine? Mbaya zaidi, unawaleta mpaka karibu na Naya! Shida ni nini kaka!? Ni nini unataka?” Chezo alikuwa akiongea kwa kuumia sana.

“Kinachoniuma na kushindwa kuelewa, sijui unakuwa unazungumza nao wakati wamekuvulia nguo! Unaongea mambo ya ndani ambayo sijui kama ni kweli au sio kweli!” “Nimeongea nini!?” Malon akauliza hilo. “Mimi sijui Malon ndugu yangu. Lakini mimi nishakuona na wanawake wote unaolala nao, hutapata mwanamke kama Naya. Kwanza anakupenda kwa dhati. Ashakufumania mara nyingi tu, lakini yule mtoto amebaki mwaminifu kwako, sisi wote ni mashahidi. Pili, Naya ametulia kaka. Mbegu hizo mjini hadimu. Ametulia, hana papara. Tatu mzuri. Mzuri kwa kila kitu ambacho ungekitafuta kwa hao wanawake zako. Ana uzuri wakumfanya mwanaume yeyote akatuliza macho kwake tu. Cha  nne na mwisho, yule mtoto anaakili kaka. Hutakufa njaa ukiwa naye. Hata ukifilisika, unauhakika atakulishia watoto na wewe atakulisha. Sasa mimi najiuliza mpaka naogopa Malon, unachotaka ni nini kaka!? Mbona hufikii mwisho wala hukinahiwi? Unataka kuvua chupi ngapi ndio utosheke? Hakuna mwanaume mwenye akili yake, akakubali kumdhalilisha mwanamke kama Naya, Malon! Ninauhakika hakuna. Nimekaa na wewe, na Naya, nawajua nyinyi wote.” Malon kimya.  

 Chezo akataka kuondoka akarudi. “Kweli Malon!? Unaacha mwanamke kama Naya anadhalilishwa na hawa watoto wajaa vumbi tu! Tumewaosha vizuri, siku tatu tunawalisha na wanafundishwa kutembea na Naya! Wachafu, wananuka mikojo na jasho hawa, unaenda kuwafunua na kurudi kwa Naya! Wanamsema Naya na mwenyewe yupo! Mimi naomba nikuache mwenyewe kaka, ila ujue tu, hata mapenzi, huwa yana expiring date. Huwa yanafika mwisho na kufa. Kama sio mtu mwenyewe kufa, basi mapenzi yenyewe. Na kila mwanadamu, anamipaka yake. Usicheze na hisia za Naya, kaka. Ukaona unakosa, anasamehe mnaendelea. Itafika mwisho, na ninavyokujua wewe, hutakuwa salama Malon.” Chezo akaanza kuondoka.

“Sasa unakwenda wapi Chezo?” “Mimi siwezi kukaa hapa Malon. Binafsi nimevurugukiwa akilini, nitaharibu shuguli nzima kama nikibaki hapa. Acha mimi nirudi Morogoro kaka. Mimi sijajalia kama wewe, Malon. Sina uwezo wakucheza karata zote kwa wakati mmoja. Siwezi. Hapa natetemeka hata sijui nafikaje Moro. Ila najua lazima niondoke hapa. Siwezi. Sasa najifikiria kama mimi niliyeyasikia tu na sio Naya, nipo hivi, je Naya mwenyewe!?” Malon na Chezo wakatizamana kwa muda, Chezo akatingisha kichwa kwa masikitiko na kuondoka. Alibadilika, hata Malon alimuona amefika mwisho, hakuwahi kumbadilikia hivyo.

Malon akabaki ameduaa asijue ni nini kimetokea na asijue dhambi ipi imejulikana, tena kwa umbali gani!  Kwa kuwa kipindi cha mwisho wakati Naya yupo chuo anajiandaa na mitihani, Malon alikuwa huru mtaani. Kwa kipindi hicho cha maandalizi ya mitihani na mitihani yenyewe, Naya alirudi kabisa kuishi chuoni. Hakujihusisha na chochote cha nje ya shule yake. Malon ndiye aliyekuwa akifuatilia na kumpa maendeleo. Labda ndio kipindi hicho!? Hata Naya naye aliendelea kujiuliza wakati akiendelea kuwavalisha warembo wake, asiamini katika kumsihi kote kule Malon, amerudia tena! 

~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~

CONVERSATION

1 Comments: