Naomi Simulizi |+1 205 767 8163 |naomisimulizi@gmail.com UTANGULIZI JUU YA SIMULIZI YA {Mapenzi & Pesa!} - Naomi Simulizi

UTANGULIZI JUU YA SIMULIZI YA {Mapenzi & Pesa!}

Kwa vijana wote ambao wanatafuta kuingia kwenye mahusiano na ambao wapo kwenye mahusiano. Ni Mungu mwenyewe ndiye aliyeona si vyema kwa mtu kuwa peke yake{Mwanzo 2:18}. {Wawali ni bora kuliko mmoja kwa sababu wana malipo mazuri kwa kazi yao. Kama mmoja akianguka, mwenzake atanwinua. Lakini ni jambo la kuhuzunisha kwa mtu yule aangukaye, naye hana wa kumwinua.{Mhu 4:9}.}

Usijisikie hukumu wala aibu kutafuta mwenza au bahati mbaya unapokuwa kwenye mahusiano yasiyoendana na kile ulichotarajia. Hakuna mahusiano yaliyokamilika, bila hukamilishwa. Hakuna kusubiri kuliko rahisi, lakini ni bora kusubiri ukiwa na Mungu, kuliko haraka ya kujiwahisha, na kujikuta unaangukia kwenye mahusiano mabovu, yasiyo na msingi wa kiMungu na kujikuta ukipambana peke yako kujenga ambako Mungu hakukusudia uwepo.

 Katika Simulizi hii ya kusisimua ya Mapenzi & Pesa, utakutana na mahusiano mengi yaliyochanganywa na pesa, na kuondoa maana halisi ya watu kuwa pamoja. Naya binti aliyezaliwa kwenye familia ya wazazi wote wawili, wenye ndoa takatifu na kulelewa kwenye maadili mazuri ya kanisani, anakua akiwa hana hatia moyoni ila anakuja kupambana na uhalisia wa maisha. Ugumu wa maisha na uhalisia wake pamoja na mapenzi vinamuingiza binti huyu kwenye maisha mengine kabisa na kumbadilisha utu wake kabisa, na kujikuta anakuwa mateka. Mfungwa wa Penzi asijue jinsi yakutoka na kurudia furaha ya awali kabisa, kabla hajajiingiza kwenye mapenzi akiwa mtoto mdogo.

 Anapita kwingi kwa fedheha nyingi mpaka kupoteza kabisa maana ya maisha. Lakini familia ya Magesa, ambao walisimamia ndoa aliyobahatika kuingia Naya, napo akaibua mengi mazito na yakuumiza ndani ya ndoa hiyo, Nanaa Magesa aliyekwisha pitishwa atakapopita Naya, ndiye atakuja kumshika mkono na kutembea naye. Itakuaje?  Yote yapo ndani ya simulizi hii ya kusisimua na kujifunza mengi. 

Usipitwe. Karibu tuwe wote.

CONVERSATION

0 Comments:

Post a Comment