N |
elly akatua
jijini Dar, Jax akawepo kumpokea dada yake uwanja wa ndege. Wakiwa njiani
kurudi nyumbani akaanza. “Nampenda Lara, Nelly. Nampenda sana.” “Hayo umeyagundua
lini Jax, kama sio unafanya tu fujo?” “Wakati mwingine huwezi kugundua uthamani
wa kitu mpaka ukipoteze na kuna tabia za kupenda kujificha kwenye maisha fulani
uliyozoea. Nimejigundua kilichonirudisha kwa Tula hayakuwa mapenzi ila mazoea.”
Nelly akamwangalia. “Niliishi na Tula kama mke wangu kwa muda mrefu kuliko
Lara. Tula akajaa kwenye maisha yangu kuliko mtu mwingine yeyote yule kiasi ya
kwamba akaacha historia ambayo haikufutwa na Lara kiurahisi. Nikisema kiurahisi
namaanisha Lara sikupita naye mapito niliyopita na Tula nikiwa sina kitu,
tukihangaika sehemu ya kuishi. Lara alinikuta naweza kula kwenye hoteli yeyote
nitakayoamua mimi, hata kwa mkopo. Lakini si Tula. Alikuwepo kipindi ambacho
siwezi hata kukopesheka! Akaandika historia kubwa. Lakini haimaanishi ndiye
aliyekuwa mwanamke sahihi kwangu au ndiye mwanamke aliyeshika moyo wangu!
Hapana. Sijui kama unanielewa?” Jax asijue anazungumza na dada yake zaidi.
“Imenigarimu ndoa na mtoto wangu kugundua hilo. Nahisi na Mungu
alinipitisha hapo makusudi kujua historia niliyoandika na Tula, sio historia ya
mwisho wangu hapa duniani. Bado nina
nafasi kubwa tu na nzuri yakuandika upya historia yangu. Kwa Tula sio mwisho.
Na dada, nitapambana kumuhakikishia Lara yeye ndio nataka kumaliza naye
kuandika historia yangu ya maisha, na Tula alipita tu kama mwalimu. Hilo darasa
nimehitimu, na yeye Lara ndiye mpenzi wangu. Mama wa watoto wangu, mwanamke
pekee nitakayezeeka naye.” Nelly akamtizama mdogo wake na kunyamaza.
Akahisi amefanya haraka kutoka kwa Billy. Ni kweli Anele amepita
kwenye maisha yake, na amekuwa naye kwa muda mrefu, akatoka akiwa amemuumiza.
Hapana jinsi ya kuacha kumtaja. Akatoa simu na kuamua kumtumia ujumbe. ‘Billy, nimefika Dar salama na Jax ndiye amekuja kunipokea.
Uwe na mapumziko mazuri.’ Akautuma huo ujumbe. Baada ya muda mfupi tu
majibu yakarudi. ‘Hata kama ungekuwa umeniumiza kwa
kiasi gani Nelly, mimi nisingekuacha hotelini. Tena peke yako! Kwa hakika
nisingekufanya hivyo.’ Huo ukawa ujumbe aliojibu Billy. Nelly akafunga
macho baada yakusoma. Billy alishaanza kumuingia moyoni.
Nelly akamtizama Jax, akaangalia tena simu yake. Akabaki akifikiria
chakufanya. Akampigia, akapokea bila ya kuchelewa. “Samahani
Billy. Samahani sana.” Jax akashituka sana aliposikia Billy. “Samahani kwa nini?” “Kukuacha.” Pakatulia kwa muda. “Unaondoka lini?” Nelly akauliza. “Kwenda wapi? Maana pale uliponiacha, sijasogea, nipo palepale.”
“Kwamba bado upo kitandani?!” Nelly akanong’ona Jax asisikie kumbe mdogo
wake alikuwa akimsikiliza. “Kwa jinsi ulivyoniacha
Nelly, ulitegemea niweje?” Nelly akamtizama Jax. “Naomba nisimamishe
gari hapa, nikupishe uzungumze.” Bila kusubiri jibu, Jax akaegesha gari pembeni
na kushuka garini kabisa kumpisha dada yake.
“Billy?” “Nipo Nelly.” “Samahani. Samahani sana.” Kimya. “Leo
ndio siku hata kama naogopa helikopta, ingekuwepo ningepanda nirudi kuja
kukuchukua turudi wote Dar.” “Zipo ndege.” “Kwamba nirudi tena!?” “Mimi
ningerudi kwa ajili yako Nelly. Ningerudi bila yakufikiria mara mbili ilimradi
niwe na wewe.” “Billy jamani! Kwa nini?” “Naanza kuamini nakuependa Nelly.
Ingekuwa mtu mwingine asingeniumiza hivi! Mpaka nimejishangaa! Nimeshindwa
kutoka kitandani sababu ya mwanamke! Mimi sipo hivi Nelly. Ila wewe imekuwa
tofauti. Na samahani kama nimekuumiza. Sikukusudia.”
“Hapana Billy. Nahisi na mimi sijui nimekuaje! Sikutakiwa
kuondoka kwa haraka. Samahani.”
Wakatulia. “Njoo Dar. Mimi mwenyewe nitakuja kukupokea
uwanja wa ndege.” “Halafu?” “Nitakuwa na wewe mpaka tuagane vizuri.”
Billy akabaki akifikiria. “Kama ukiona vipi, basi natafuta
ndege nirudi huko.” “Tulipanga tumalize likizo pamoja, Nelly.” “Lakini sio
hotelini au hatukuwa na makubaliano ya tumalize pamoja.” “Wewe ulitegemea nini!?”
“Sijui Billy. Lakini mimi nilijua unamaanisha tuchukue likizo tarehe na siku
zinazofanana ili twende wote kupanda mlima Kilimanjaro.” “Nelly!” Billy
akashangazwa. “Kweli Billy! Hatukuzungumza hilo.” “Wewe
umetoka kuniambia wewe sio mtoto mdogo. Kweli ulifikiri nataka muda na wewe kwa
kulinganisha tu tarehe?” “Basi narudi Billy. Acha nitafute ndege ya kurudi
jioni.” “Sawa.” Billy akakubali bila shida wala kusita mpaka
akamshangaza tena Nelly.
“Kwamba unataka nirudi kweli?!” “Kumbe hukuwa ukimaanisha?
Nilifikiri ulimaanisha uliposema wewe hutakuwa ukinidanganya!” “Namaanisha Billy.”
“Basi nitakuona baadaye.” “Sawa.” Nelly akabaki akifikiria garini asijue anarudije tena Moshi.
Akamfanyia ishara Jax arudi garini.
Jax akarudi garini kimya. “Nilikuwa na Billson huko Kilimanjaro.” Jax
akamtizama na kunyamaza. “Nimepanda naye mlima.” Kimya. “Nimemuacha kwenye
mazingira ambayo si sawa.” “Ninaye mtu
anayeweza kukupa tiketi ya kurudi leo jioni.” Jax akaongea bila kufikiria wala
kushangazwa na dada yake, alimjua ni mkorofi. Ila Billson! Akabaki akifikiria
na kujiuliza ilikuaje maana mara ya mwisho alimkataa vibaya sana, tena mbele ya
umati! Kibao kiligeuzwa lini! Akabaki akijiuliza Jax huku akiendelea kukanyaga mafura
kumrudisha dada yake nyumbani.
“Billy ni mtu mzuri.” Nelly akajikuta akisifia. Jax akacheka
kimyakimya. “Acha nimpigie nione kama anaweza kukupa nafasi.” Jax akatoa simu
yake kumtafutia dada yake nafasi ya kwenye ndege kurudi tena Kilimanjaro huku
wakielekea nyumbani kwake.
‘Change of plans.’ Ujumbe huo mfupi ukaingia. Ulikuwa ukitoka kwa Billy akimwambia
mipango inabadilika. Nelly akakunja uso. Akatulia kusubiria. Baada ya muda ukaingia
ujumbe wa pili. ‘Usitafute ndege ya huku. Baada ya kama
lisaa hivi, sekretari wangu atakutumia tiketi. Nipe muda mfupi nifanye maandalizi
mazuri ya mapumziko yetu. Lakini andaa hati ya kusafiria na wewe mweyewe. Na
ujue usiku wa leo tutakuwa na wakati mzuri sana.’ Kisha ujumbe wa tatu
ukaingia tena. ‘Kuweka hili wazi, natizamia kwa hamu penzi
la usiku kucha.’ Jax akamuona dada yake anacheka na kutizama nje.
Hakuwahi kumuona akicheka kwa soni vile kama mtoto wa kike! Jax akajua dada
yake amepatikana.
Zikaendelea jumbe nzuri, ikawa kama Billy anamuandaa Nelly kwa usiku
wa penzi alilokuwa akilisubiri kwa hamu. Akimueleza nini atamfanyia kwenye
mwili wake, mpaka Nelly akawa anaona aibu mwenyewe, tena chumbani kwake akijiandaa
kwa hiyo safari. “Haiwezekani Billy! Wewe matiti yangu
umeyaonea wapi!?” Ilibidi Nelly ampigie tu. Billy akapokea akicheka
sana. “Nilijua tu safari hii lazima upige. Niliona unasoma
jumbe zangu, halafu hujibu!” Billy akazidi kucheka. “Acha bwana kucheka Billy! Umeelezea kama yalivyo! Wewe umeyajuaje?
Au umeambiwa tena!?” “Hapo sasa unanitia wasiwasi. Nani huyo aniambie?” “Huko
unakotoa habari zangu.” “Kwamba ndio yanajulikana hivyo!” “Acha kunipoteza
bwana! Wewe umeeleza matiti yangu kama yalivyo! Mpaka mimi nilivyokuwa nakua
nikajua yamedumaa!” “Na wakati ndio mazuri! Ukoje Nelly?”
“Napenda hivyo yalivyo. Yaani nilibaki nikijipimishia mkono
kama nitaweza kukamata kila moja kwa mkono mmoja.” “Hakika nakukatia simu. Yaani
mimi nipo na wewe nafikiri akili zako zipo vizuri, kumbe zipo kwenye matiti
yangu!” Billy alingua
kicheko kwa sauti ya juu sana. “Mimi nisingekwambia hivyo
Billy!” “Kwa sababu sina matiti ambayo ni kama yalitaka kuanguka hivi, yakagoma
na kutengeneza duara kubwa hapa chini. Yakajaa haswa na kushikiliwa na chuchu...”
Nelly akamkatia simu.
Hapohapo Billy akampigia tena. “Naona simu
imekatika katikati ya...” “Hapana Billy. Nimekukatia.” Billy akazidi
kucheka kwa sauti. “Mimi najiandaa kwa safari Billy. Unanichelewesha.”
“Hutaki kujua niliyaonea wapi?” “Naanza kutotaka.” Billy akazidi kucheka
kwa sauti. “Sema sasa.” “Unakumbuka siku ile ya kwanza kule
Moshi hotelini, mimi ndio nilikuwa wa kwanza
kuoga?” Nelly kimya. “Najua utakuwa umeshanisoma
Nelly. Mimi kazi za mikono sitaki na sifanyi kabisa japo najua. Nilishajiambia hapa
duniani ni mgawanyiko wa kazi. Wengine tunabarikiwa kipato kwa ajira za
maofisini, wengine majumbani. Sasa huwa nikivua vitu vyangu, naachaga hapohapo.
Na hata kitanda changu yupo wa kunitandikia kila siku na mashuka ninayolalia nilazima
yabadilishwe kila siku.” Nelly kimya.
“Usinikimbie sasa.” “Nakusikiliza.” “Sasa siku ile nikajisahau.
Nikadhani nipo peke yangu. Nikavua kila kitu bafuni na kuacha hapohapo
sakafuni. Nilipotoka ndipo nikakumbuka sipo kwangu na nipo na wewe, inabidi
nionyeshe tabia njema ili usinikimbie.” Mpaka Nelly akacheka. Akiwa ameshamuelewa. “Nikakumbuka
ukiwa umeshaingia bafuni, nikasema nikuwahi niokote vitu vyangu ili kukupa
nafasi. Ndipo nilipoingia nikakukuta umeshaingia kwenye shower unaoga.” “Unatabia
mbaya Billy wewe! Kwa hiyo ulinichungulia pale ndani ya shower?” “Sikukuchungulia
ila nilikuona.” “Huna lolote. Ungejuaje kwa undani hivyo?” “Kwani wewe hujawahi
kushangazwa na jambo na kujikuta ukipigwa na butwaa kidogo.” Nelly
akamkatia simu tena.
Baada ya muda ujumbe ukaingia. ‘Siamini kama
leo nitalala na hizo chuchu mdomoni.’ “Haaa!” Nelly akahamaki kwa
sauti. “Huyu Billy anaakili za kitoto jamani! Alale na chuchu mdomoni, yeye
mtoto mchanga!” Nelly akawaza akishanzwa na vile Billy alivyomkamia. Ila
ikamgusa na kumuongezea ujasiri.
Akabaki akimtafakari Billy huku akiendelea kujiandaa. Pakatulia kwa
muda akatuma ujumbe mwingine. ‘Natizamia wakati wetu wa
pamoja Nelly. Na asante kwa kuamua kunifuata.’ Nelly akakaa kabisa na
kuacha kufungasha. Akarudia huo ujumbe na kutafakari kidogo. Anamjua Billy huwa
hajui kumpunja. Anajitoa kwake na kutumia pesa nyingi sana juu yake. Na alimwambia
ni ili amfurahishe tu. Akajisikia kuvutiwa naye zaidi. Akaanza kufikiria
kufanya mapenzi na mwanaume kama Billy! Akajisikia furaha moyoni. Akajikuta akimrudishia
ujumbe. ‘Na mimi Billy. Naamini tutakuwa na wakati
mzuri.’ Hilo likamfurahisha Billy alipopata hayo majibu. Akajua na yeye
ameridhia. Alishamsoma Nelly, maisha yalifanikiwa kufunga hisia za kimapenzi
kabisa. Sasa kuja kupata huo utayari wake, ikamuongezea shauku ya usiku huo.
Nelly Mikononi kwa Billy.
N |
elly
alitua kwenye uwanja wa kimataifa wa Robert Gabriel Mugabe, mjini Harare, Zimbabwe
usiku huo, akakuta Billy akimsubiria. Wote wakacheka. “Nimefurahi umenifuata,
Nelly.” Nelly akagundua hilo amelirudia tena. Inamaana amemaanisha. “Sasa kama
ulitaka nibaki kwa nini hukuniambia nibaki?” “Hapana. Nilitaka na mimi
kuchaguliwa. Safari hii na mimi nilitaka kuchaguliwa.” Nelly akacheka. Hata
kabla hajampokea mizigo yake, palepale nje ya uwanja wa ndege, akamvuta pembeni
ya kigari cha mizigo alichokua akakisukuma, akamkumbatia Nelly vizuri na kuanza
kupata mabusu. Akambusu kwa kituo kabisa ndipo akamuachia.
“Karibu, Harare Zimbabwe. Ndio kwetu.”
Ndipo akachukua sasa kigari kilichokuwa na mizigo yake, aliyorudi nayo. Giza
lilikuwa limeshaingia. “Kwa nini imekua hapa?” “Tokea Anele anitende vibaya, nilipachukia
sana.” Akajishitukia kwa haraka akaingiwa na hofu mpaka Nelly akamuona. Ni kama
aliropoka tena. “Samahani kwa kumleta tena..” “Hapana Billy. Tafadhli kuwa tu
na amani. Nataka na mimi niwe mtu wako unayeweza kumwambia chochote
kinachokusumbua.” Hilo lilimgusa sana Billy. Mpaka akasimama kabisa.
“Kweli Nelly?” “Kabisa. Sasa
usipozungumza na mimi, utazungumza na nani! Tafadhali kuwa tu huru.” “Nashukuru.
Hilo limenifurahisha zaidi na nitakavyokwambia! Ni kweli huwa nazungumza na
mama karibu kila siku, pamoja na binti yangu, lakini kuna mambo siwezi
kuzungumza kwao. Sijui kama unanielewa? Najikuta mpekwe!” “Samahani mwanzoni
niliondoka kwa haraka, Billy. Lakini mimi sio dhaifu kiasi cha kutishwa na Anele
ambaye mlishaachana! Kuwa huru kabisa.” “Afadhali. Sasa tokea Anele anitende vibaya,
sijawahi kurudi tena kwenye hii nchi. Nafikiri labda nilikuja kikazi tu, basi. Ila
napakwepa sana. Sasa kwa kuwa ni nyumbani kwa wazazi, kwamba nilazima siku moja
ningetakiwa kurudi, kama nyumbani, lakini nikawa sina huo ujasiri. Sasa kwa
wewe kukubali kunifuata, nikaona angalau tuwepo hapa pamoja, nitengeneze historia
mpya, nyingine, mbali na ya uchungu niliyobaki nayo.”
Nelly akamuhurumia. Akagundua bado Billy yupo na maumivu yakutendwa. “Umekula?”
“Tutakula chumbani. Nimeandaa usiku mzuri sana. Kila kitu kitatufuata tulipo.
Nimefurahi sana umerudi.” Bill akarudia tena. Nelly akamwangalia. “Na mimi
nataka kupendwa Nelly. Na mapungufu yangu yote, bado nataka kupendwa. Nastahili
jamani!” “Kweli unastahili Billy. Wewe ni mtu mzuri, mwema, na ndio maana
nimerudi. Na samahani kwa kuondoka vile. Nahisi ni wivu tu.” “Huna haja
yakumuonea wivu Anele. Hatawahi kurudi kwenye maisha yangu tena. Ila sikatai
kama ameacha historia kubwa na ameniumiza. Lakini hata nijikute naye uchi,
hakika sitamgusa.” Nelly akacheka. Dereva akaendelea kukanyaga mafuta kurudi
hotelini.
~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~
Walipofika tu mlangoni, wakaangaliana, Billy akaanza tena kumbusu
wakiwa hata hawajaingia ndani. Muhudumu wa hiyo hoteli aliyekuwa amewabebea
mizigo yao alifungua mlango wa chumbani kwao akiwa na mizigo yao wote wawili,
akawaacha hapo nje wakiendeleza kiss za haja. Billy alikuwa amemvutia
Nelly pembeni akaweza kuegemea pembeni ya ukuta hapo karibu ya mlango, na yeye
akawa kama amejiegemeza kwake akiendeleza kiss kwa kutulia tu. Baada ya
muda yule muhudumu akatoka na kueleza kila kitu kipo tayari ndani, amekwisha
panga. Alijieleza akiangalia pembeni kwani bado walikuwa wakiendelea
kubadilishana ndimi kama wanandoa wachanga waliokuwa wamesubiriana kwa muda
mrefu, ndio siku hiyo yametimia. Akataka kuondoka kwa kuwa hakuwa amejibiwa na
Billy ndiye aliyekuwa amempa mgongo. Alipofika mbali kidogo, Billy akamuita ili
kumpa tip. Pesa ya kumshukuru kuwabebea mizigo yao mpaka ndani. Akamuacha
Nelly akishika midomo yake na cheko la taratibu.
Wakati akimlipa yule muhudumu,
Nelly akaingia ndani. Kwa hakika alishangazwa na hicho chumba. Billy akaingia
na kumdaka kiunoni akiwa bado anashangaa. “Subiri kwanza Billy!” Nelly alikuwa
amekanyaga maua hapo sakafuni. Yalimwagwa kuanzia mlangoni, yakatengenezwa njia
kuelekea chumbani na mpaka bafuni. Na kila sehemu Nelly alipoyafuata, yalikuwa
yamemwagwa kwa unadhifu sana. “Waw!” Nelly akahamaki asiamini ndio chumba atakachokuwepo
kwenye mapumziko yake na Billy.
Akageuka nyuma, akakuta Billy akimwangalia. “Sijawahi ingia chumba
kizuri hivi!” Hilo likamfurahisha Billy. Kwa hakika kulipangiliwa, Nelly akajua na hapo
atakua ameacha pesa ndefu tu. Alilipia classic romatic suite. Sekretari wake
ndiye aliyemsaidia maandalizi yote hayo yeye akiwa bado KIA, uwanja wa ndege wa
Kilimbanjaro akisubiri ndege yake iondoke wakakutane na Nelly, Harare. Aliendelea
kuwasiliana naye akimpa maelekezo ya aina ya chumba anachotaka akikute. Na kweli
waliitendea haki pesa yake. Hoteli yenyewe ilikuwa nzuri sana ya kimataima. Ipo
sehemu nzuri na hata chumba chenyewe, Billy alitaka kiwe sehemu ambayo hapatakuwa
na kelele.
“Nakushukuru Billy. Najua na wewe utapumzika, lakini mimi nilihitaji
haya mapumziko. Mwenzio huwa sichukui likizo.” “Haiwezekani Nelly! Miaka yote?”
“Niende wapi au nifanye nini nyumbani Billy? Sina familia kwamba niende likizo.
Sina starehe yeyote ila kazi tu.” “Kama ndio hivyo basi ni afadhali tumepata
hiki chumba. Huu upande hutasikia kelele za watu, itakusaidia kupumzika.” Nelly
mwenyewe akamsogelea na kuanzisha busu yeye mwenyewe. Billy akacheka kwa furaha
kuona Nelly ameanzisha. Akajua amefurahia ndio anashukuru. Akamuona anazidi kumng’ang’ania.
“Ooohooo!” Billy akasikika. Wakati Nelly akimvua shati. “Tonight, Am in troubleee!”
Nelly alicheka vile Billy alivyosema usiku huo yupo matatizoni. Lakini aliendelea
kumtoa nguo za juu taratibu huku akimbusu kule alipotoa zile nguo. Walikuja
kujikuta kitandani hamna mwenye nguo ila wote wakiwa tayari kuyachukua
mahusiano yao kwenye ukurasa mwingine.
“Unauhakika? Maana baada ya hapa hakuna kurudi tena nyuma, Nelly.”
Billy aliongea akiwa amemlalia Nelly juu yake, matiti yake chini ya kifua cha
Billy, na mkono mmoja upo kwenye hips ya Nelly kwa chini amemkata kwa nguvu. “Unamaanisha
nini!?” “Sitafuti mwanamke wa kulala naye usiku wa leo tu! Wapo wengi. Nakutaka
wewe kwenye maisha yangu.” “Hunifahamu Billy!” “Basi hiki tunachotaka kufanya,
naomba kisubiri.” “Billy!” “Sio na wewe Nelly. Wewe si kwa kupunguza haja za
siku moja halafu basi. Nakutaka kwenye maisha yangu. Nimechoka kuwa peke yangu
Nelly! Nataka uwe wangu. Ni nini unachoogopa bwana? Mimi sio mtoto mdogo. Kama
ingekuwa ni mapenzi tu, tungeyafanya siku nyingi sana. Ndio maana nilisubiri
mpaka nione umbali unaoweza kwenda na mimi.” “Sasa umeridhika?” “Nisingefika
umbali huo kwenye mwili wako!” Nelly akacheka kwa aibu na kujifunika.
Maana ni kweli Billy alimfanyia mengi kwenye mwili wake ambayo
hakuwahi kufanyiwa kabla. Mpaka Nelly aliyeanza na mwili ukionekana stiff
kwa tension, yaani uliokakamaa kwa wasiwasi, ukatulizwa kabisa hapo
kitandani. Billy alimfanyia yote kama alivyoahidi tena bila papara. Hapo Nelly
alikuwa tayari tu ammalizie.
Billy akawa kama ameshitushwa na kitu. “Subiri kwanza Nelly! Wewe
ulifikiri ndio nafanyia wanawake wote niliyokufanyia wewe hapa!?” Nelly
akatingisha kichwa kukubali. “No way! Haiwezekani kabisa! Wewe unaniona
kwa wasiwasi nini!? Au unafikiri kwa kuwa nimekung’ang’ania hivyo unafikiri ni
kwa kila mwanamke?” “Mimi sijui bwana Billy! Wewe fanya mapenzi na mimi sasahivi.
Unanikata stimu.” Billy alicheka sana. “Usiniambie umenogewa hivyo!” “Sana. Kumbe
ndio vitamu hivyo!” Billy akarudia romance kidogo akijua ni kweli ameshamtoa
kwenye hali ya utayari aliyokuwa nayo kabla ya swali lake alilopenyeza hapo
katikati. Akamfanyia tena kidogo, akatoa midomo chini, akairudisha kwenye chuchu
kisha akamwangalia. “Kwa hiyo hakuna kurudi nyuma?” “Sasa hivi naweza kukuapia
chochote kile. Wewe endelea tu, nitakuwa chochote unachotaka.” Billy alicheka
sana na kuendelea.
Ukweli Nelly alifurahia mapenzi ya Billy. “Utaalamu huu wa mapenzi ni
wa kila siku au leo tu kunivutia?” “Tuna siku tano hapa. Kwa nini usivumilie
ukajionea mwenyewe?” “Ninachojaribu kukwambia ni, usipunguze hiyo nguvu ya
mvuto ila kuongeza.” Billy alicheka sana. “Hakika nimependa Billy. Upo vizuri
halafu umetulia, huna hekaheka nyingi, una nguvu na stamina. Napenda unavyonishika
kwa nguvu, na ukiingia hakika nakusikia vizuri sana bila maumivu! Halafu nimependa
vile ulivyonimwagia...” Nelly akawa kama anajaribu kuvuta kumbukumbu hapo
kitandani baada ya mapenzi marefu matulivu waliyomaliza.
“Ile ya baridi au vuguvugu?” Billy akajaribu kumsaidia kumkumbusha kwa
swali akicheka. “Labda unimwagie tena, halafu usiharakishe kuilamba ukinyonya
ndio nitajua kama napenda ya baridi zaidi au vuguvugu.” Billy alicheka mpaka
akapaliwa. “Pole.” Nelly akatoka kitandani kwa haraka kumletea maji ya kunywa
akiwa uchi kabisa akichikilia matiti yake. “Kunywa maji.” Billy akanywa mpaka akatulia, ila akagundua
kuna vipande vya barafu ndani. Nelly akamuona anacheka. “Nini sasa?” “Ulivyonisimamia
hivyo uchi, nishapata wazo la wapi pakumalizia hizi barafu zangu kwenye hii
glasi.” Nelly alifurahia na kujitupa kitandani akisema. “Enjoy your ice cubes.”
Billy alizidi kucheka vile Nelly alivyokuwa akimkaribisha bila kusita huku
akijiweka sawa hapo kitandani, chini ameweka taulo mbili ili kitanda kisilowe,
miguu wazi ili Billy aweke chochote huko.
Alipenda sana jinsi alivyokuwa akimmwagia mwilini mwake vitu tofauti tofauti kuanzia katikati ya matiti, anaweka michirizi kiasi mpaka kitovuni, kisha kushuka chini akiweka nyingi juu ya kinena ili ichirizike kiasi chini kabisa. Na mapajani kidogo kisha kuanza kuila hivyohivyo. Jinsi alivyopitisha ulimi juu ya huo mwili wa Nelly, kwengine alilamba na kwingine kunyonya. Nelly alijikuta akitoa milio tofautitofauti. Kwengine ikawa akicheka sana, kama anayemtekenya, kwengine migugumo ya haja. Na Billy alijaliwa utaalamu wa mikono pia. Hakuna alikopita na kumuacha Nelly salama, na kumtaka tena na tena, mpaka aibu ikamuisha akabaki akidai, kitu kilichomuongezea ujasiri Billy mwenyewe akijua anafanya kitu kinachopendwa. Hapakuwa na kutoka tena. Chakula kiliwafuata hapohapo chumbani. Wakamaliza uchovu wa kupandisha mlima, na likizo hapohapo hotelini.
Kwa Jax
J |
ax alikusudia kwelikweli
kumrudisha Lara kwenye maisha yake. Wakati dada yake anafaidi na Billy, na yeye
akaendelea kutengeneza yake ambayo hayakuwa hata na tumaini. Safari za Dodoma nyumbani
kwa kina Lara zikaendelea bila kuchoka mpaka na wao wakamzoea. Anafika
jumamosi, anaondoka jumapili bila ya kumuona Lara. Japokuwa alishakatazwa
kurudi hapo, wakamuonyesha wazi hatakiwi, lakini Jax hakukoma kufika hapo. Akafanya
hivyo mfululizo mpaka wakaanza kuandaa chakula kizuri kwa ajili yake siku za
jumamosi wakijua lazima usiku atakuwepo hapo. Alipofululiza weekend tatu
mbeleni mpaka mzee Chiwanga akaanza kumuhurumia. Kila akifika hapo hataacha
kuomba msamaha. Akitubu kwa kuwafedhehesha.
Mzee Chiwanga mwenyewe akamwambia inatosha. “Hii imeshatokea,
nafikiri Mungu aliruhusu kila mmoja wetu apokee funzo lake. Basi. Maisha
yaendelee. Huna haja yakuendelea kuomba msamaha.” Hapo Jax akafurahi sana,
akapiga tena magoti kama mtoto wa kike na kushukuru. Akafurahia angalau moyo wa
Mzee Chiwanga umeanza kufunguka kwake.
Akaendelea kwenda hapo japo hakuwa akimuona Lara ila akaanza kuona
mabadiliko. Akaona wanaanza kujirudi mmoja baada ya mwingine. Akifika,
hawakimbii tena sebuleni. Wanakaa naye. Na yeye hakuacha kuleta zawadi hapo.
Akaweka urafiki na Lucas. Akimuuliza maswali ya hapa na pale akitaka kujua
shule ikoje na mambo mengine. Siku anazofika hapo mapema, anaweza hata kutoka naye
nje na kucheza naye mpira. Watamsikia akicheka nje na Lucas pamoja na marafiki
zake Lucas. Akawa mwenyeji. Bado hawakuwa wameonana na Lara.
~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~
Alipoona anapokelewa vizuri nyumbani kwa kina Lara, akabadili
utaratibu. Akawa akitoka tu kazini siku ya ijumaa, basi safari ya Dodoma
inaanza. Anafika ijumaa usiku, anakaa hapo Dodoma siku ya jumamosi, jumapili jioni
anaondoka. Akaendelea kuja hapo mpaka mtaani nao wakaanza kumzoea. Anaonekana
mtaani siku za jumamosi akiwa anazunguka na Lucas kama asiye na shuguli za
maana. Akajiunga kwenye kucheza mpira wa miguu na vijana hao wadogo wa hapo
mtaani, rafiki za Lucas na Lucas mwenyewe aliyependa mpira kuliko nafsi yake. Mama
yake alishasema juu ya kushinda kwake mpirani mpaka akachoka. Tangia mtoto
mdogo, Lucas alipenda mpira, ndio shule ilifuata, tena kidogo sana. Ila hata
shuleni, alitumia muda wake kucheka mpira wa miguu.
Kwa hiyo hizo siku za jumamosi, utamkuta Jax uwanjani na Lucas pamoja
na vijana hao akicheza mpira mpaka giza linaingia ndipo wanarudi hapo nyumbani
na Lucas wakiwa wanatokwa jasho wakicheka. Atasubiri chakula. Akila ndipo
anarudi hotelini. Alishamletea Lucas raba nzuri sana za kuchezea mpira na nguo
za michezo. Huna utakalomwambia tena Lucas juu ya Jax akaelewa. Sifa zake
zilikuwa zikiimbwa na Lucas kila siku mpaka Jax aje kurudi tena hapo. Wakawa
marafiki kweli na mpaka vijana wanaocheza mpira hapo mtaani na Lucas,
wakamfahamu Jax na kumzoea. Ikawa jambo la kawaida kwao kugongwa na kuuliziwa
Jax kana kwamba anaishi hapo. Akawa kama mtoto wa hapo mtaani.
~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~
“Nashauri uzungumze naye, mama
yangu. Huyu mtu inamgarimu sana kuja hapa kukufuata. Anakuwa ni kama anaishi
huku!” Mwishoe huruma ikamzidia mzee Chiwanga. Akajaribu kumshawishi binti
yake. “Anaonekana anajutia kosa, na amekusudia kujirudi na kwa vitendo. Nilishamsemesha
vibaya sana. Sikutegemea kama angeendelea kuja hapa! Kila mtu mpaka mama yako
amekuwa akimkatisha tamaa, lakini hajaacha kuja. Mara aje na ndege, mara awe
anaendesha! Kila ijumaa yupo huku Dodoma kwa ajili yako mama, mpe hata dakika
tano tu, mzungumze.” “Mimi sina kitu chakuzungumza naye baba. Nilishamwambia
simtaki tena, sina kitu kingine chakumpa. Kwa nini anang’ang’ania!” Lara
akalalamika. Baba yake akaamua kumuacha.
~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~
Ijumaa inayofuata, Jax hakutokea. Jumamosi nayo kimya. Hakutokea
asubuhi kama walivyozoea kumuona. Lara akaanza kuhangaika. Wazazi wake wakatoka
kwenda kwenye biashara yao wakamuacha hapo anasafisha kwa mkono mmoja akipanga.
Ilipofika saa 9 mchana wakamuona amewafuata pale dukani, amepoa. Akakaa hapo
hakuna aliyemuuliza. Ilipofika saa 12, akauliza. “Kwani umemwambia Lily apike
nini usiku?” Akamuuliza mama yake. “Vipi? Kuna kitu unataka kipikwe?” Akatulia
mama yake akiendelea na kazi zake hapo dukani. “Labda kuongeza kidogo. Jax
anapenda sana mboga za majani.” Mama yake akasikia kucheka moyoni. “Anatengeneza
chapati na maharage. Nitampigia nimwambie aongezee mboga za majani.” “Labda
nimpelekee na samaki.” “Sawa mama.” Kumbe Mzee Chiwanga alikuwa akisikiliza tu.
Lara akaondoka.
Siku hiyo ya jumamosi mpaka wanakwenda kulala saa nne usiku Jax akawa
hajafika hapo na chakula aliachiwa. Jumapili nayo asubuhi hakutokea. Wakaenda
kanisani na kurudi hapo mchana. Wakapika, wakala, Jax hakutokea. Ilipofika
usiku wakamuona Lara amejikunja kwenye kochi ameegemeza kichwa kama mnyonge
anaangalia tv hata hazungumzi tena. Ameshikilia mkono wake.
“Mkono vipi mama? Umeanza maumivu?” Lara akamwangalia baba yake na
kurudisha macho kwenye mkono. “Wala hauumi. Nafikiri umeshapona. Week hii
tukatoe, baba. Nahisi muda umeshapita!” “Tutaenda wakaangalie. Tuone.” Baba
yake akataka atoke kwenye yale majonzi. Lara akahamia kwenye kochi alilokuwa
amekaa baba yake, akamsogezea mkono uliofungwa PoP.
Familia nzima walikuwepo hapo. “Halafu ujue ni mimi peke yangu humu
ndani ndio sijaandika hapa!” Lara akacheka kidogo. “Nitaenda kutoa ukiwa
hujaandika chochote!” “Acha leo niandike. Lucas niletee kalamu.” Wote wakacheka
nakutaka kujua baba yao ataandika nini maana walishamshawishi sana, bila
mafanikio. Akaletewa kalamu. “Nitafutie sehemu nzuri.” Lara akawa anacheka huku
akitafuta. “Huku juu ndio wengi hawajaandika.” “Ewaa!” Kila mtu akasogea pale
kwenye kochi walilokuwa wamekaa Lara na baba yao. “Mtanitingisha sasa! Si
msubiri kwanza niandike ndio msome?” Wakasogea pembeni wakicheka, wakisubiria
kwa hamu.
‘Vipingamizi visiwahi kukusimamisha maishani. Unapokumbana
na ukuta ukikusimamia njiani, usiogope wala usikwame. Jifunze jinsi ya
kuupanda, au kupita katikati yake au kufikia lengo lako na wenyewe ukiwepo.’ Wakamuona Lara anafuta machozi,
wakajua baba yao amemaliza. “Nisome na mimi, Lara.” Lucas mleta kalamu akawahi
na wengine wakasoma. Mama yake naye akasoma na kunyamaza. Lara akajirudisha
nyuma kwenye kochi akatulia. Hiyo siku nayo ikapita bila Jax kuonekana.
~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~
Mambo yanaendelea. Usikose Muendelezo
kujua kitakachoendelea kwa Penzi zito la watu wazima hao wenye pesa.
Je, Tamu mpaka mwisho?
Je, Jax amekata tamaa na kuamini hatampata tena
Lara?
Si kwamba aliishiwa. Ni maisha mazuri
aliyoishi na Lara ndio aliyataka tena na kufanya amrudie. Lakini bado Jax yupo
zaidi ya vizuri. Jax bado anakazi nzuri, mvuto, na yupo jijini ambako angeweza
kupata yeyote na kumuoa. Hilo ndilo lilianza kumuumiza Lara kila masaa yakizidi
kuyoyoma na Jax kutoonekana tena hapo kwao. Akamkumbuka Tula ambaye hajui kumzira Jax. Kwa
yeyote na popote, hana haya yakusema shida yake ni Jax. Wasiwasi ukazidi
kumuingia Lara. Amemringia Jax zaidi ya kawaida.
Je, nini kitaendelea?
Usikose muendelezo....
0 Comments:
Post a Comment