Naomi Simulizi |+1 205 767 8163 |naomisimulizi@gmail.com Chozi Langu! - SEHEMU YA 8. - Naomi Simulizi

Chozi Langu! - SEHEMU YA 8.

     Jax aliumia sana. Alibaki pale akiwaza kwa muda na kuondoka. Akili zake zilikuwa zikizunguka ila akakusudia kumuonyesha dada yake yeye sio kama baba yake, na amekusudia kubadilika. Akaamua kwenda nyumbani kwa dada yake. Kwa kuwa ni yeye, mlinzi alimfungulia kwa haraka tu. Akaenda kuegesha gari kabisa na kuingia bila hodi. Dada yake akatoka chumbani. Akamsalimia, Nelly akabaki akimwangalia tu bila kuitika. Jax akaongeza. “Wewe funga tu mlango unapotaka kulala, mimi naingia kulala.” Nelly akabaki ameduaa. Kwamba usiku huo analala hapo kwake! Jax akaingia kwenye chumba chake ambacho hata Tino huwa anakitumia, kimya.

Kesho yake akatoka asubuhi na mapema kwenda nyumbani kwake kujiandaa kwenda kazini. Jioni Nelly akiwa nyumbani kwake anaangalia taarifa ya habari akamuona anaingia na masanduku mawili pamoja na mabegi. Akasalimia, na kupitiliza chumbani kwake. Akatoka nje, akamuona anaingiza tena na suti zake. Nelly kimya akiendelea kuangalia taarifa ya habari. Akapita hapo mara kadhaa na mizigo yake kama anayehamia hapo na mizigo yake. Akatulia chumbani kwake kwa muda, kisha akatoka. “Nilikununulia hii pochi nilipokuwa Uswiz. Najua unapenda hizi rangi.” Nelly akamtizama na kuitizama ile pochi, kimya. “Naenda kuiweka chumbani kwako.” Jax akaondoka pale maana hakujibiwa, ila alimjua Nelly, dada yake, hakujali.

Maisha ya Jax yakaanza hapo nyumbani kwa dada yake. Akarudi kuishi na  dada yake kama zamani. Nelly hakumuuliza. Ila kumuona anatoka asubuhi, na kurudi nyumbani mapema tu akiashiria hana pakwenda. Ila kumjali dada yake kukaongezeka mpaka Nelly akawa anashangaa. Zawadi za hapa na pale hazikukoma. Na akiwepo naye nyumbani mara amtengenezee chai ya jioni au kumtengenezea juisi kisha kumuwekea kabisa na kumsogezea alipokaa. “Hii ina virutubisho vizuri na muhimu mwilini, unahitaji.” Nelly akawa anajiangalizia tu na kunyamaza.

 Maisha yakaendelea kwa ndugu hao wawili. Wanaishi hapo wawili tu bila wenza ila ajira zao ndio zikawa ndoa. Wote kujituma sana kazini. Na ukweli upande huo wa kazi walifanikiwa sana, ila si kwenye mahusiano. Hata wao wenyewe wawili hawakuwa na muda wa pamoja wa kufurahia kama ndugu. Wakiwa hapo kwenye nyumba hiyo kama hawaangalii taarifa ya habari, basi kila mmoja macho kwenye kompyuta akifanya kazi za kiofisi. Siku ikianza, wote barabarani kuwahi kazini. Magari yaliyoegeshwa hapo nje ya nyumba ya Nelly, na jinsi wanavyovaa wakitoka hapo, ndipo utajua wamefanikiwa kifedha, ila mbali na maisha ya kazini, hapakuwa na maisha mengine. Na hakuna aliyejua kinachoendelea kwa mwenzie.

~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~

B

aada ya maharusi hao watarajiwa kutengana na ndoa kushindikana, Jax akiwa kwa dada yake, kwa upande wa Lara yeye maisha ya kaanza na kushika kasi huko kisiwani Zanzibar akiwa hakuna anayejua alipo. Ila akafurahia kuishi asikojulikana kashfa yake. Ile hali ikamsaidia kumuongezea ujasiri na kumtoa majonzi na ikabidi afanye juhudi za makusudi kuchangamka ili kutoa maswali kwake ya moja kwa moja. Akajulikana tu ni binti ambaye hajaolewa wala hana mchumba. Akakazana kutumia dawa alizoandikiwa hospitalini alipokuwa na Jax, zakuongeza damu huku akizingatia milo.

Haikuchukua muda mrefu kwa Lara kurudia hali yake ya zamani ila safari hii sio na tabia za kisichana alizokuwa nazo. Lara alishajiona amekuwa mtu mzima. Utoto uliisha siku anampoteza mtoto wake na Jax. Akarudia uzuri wake, lakini mtulivu. Na kwa kuwa aliowakuta pale kazini ni watu wazima, akakosa wasichana kama kina Suzy wakuzunguka nao kwenye starehe. Akajituliza. Kazini, nyumbani kwake, basi. Hakutaka urafiki wa undani ambao itamlazimu kueleza historia ya nyuma. Akakwepa ushoga.

Baada ya miezi mitatu kupita akiwa kazini siku ya jumamosi, waliingia wanaume wawili. Walionekana ni watu wazima kidogo. Lara aliona wakihudumiwa na mwenzao. Akaendelea na shuguli zake. Kukatokea kutoelewana kidogo na anayewahudumia wakaambiwa wasubiri. Akaitwa Lara. Lara akaenda pale. “Naomba uwasikilize wewe Lara. Naona mimi nikizungumza nao, hawanielewi.” Lara akawasalimia. “Niwasaidie nini?” “Simu na laini yenye namba hizi. Ilikuwa simu yangu, nimeibiwa.” Mmoja akaongea. “Hiyo ni rahisi tu. Naomba tuhamie pale kwenye meza yangu.” Lara akawatoa hapo akijua waliposhindwana na muhudumu wa kwanza.

Walikaa, Lara akaandika ile namba kwenye kompyuta yake likaja jina kamili. Kabla hajamtajia, Lara akamwangalia. “Naomba kitambulisho chako chenye jina kamili kama inavyoonekana wakati ukisajili hii namba.” “Ulisikia pale alipokwambia kuwa ameibiwa mpaka waleti?” Mwenzie akauliza kwa ukali kidogo kama asiyetaka kupotezewa muda zaidi. Lakini akashangaa muomba namba ambaye ndio alikuwa mwenye kelele, amepoa. “Siwezi kujua kama wewe ndio...” Lara akarudi kwenye kompyuta kutaka kusoma jina. “Jeremaya Kembo.” Akawahi huyo muibiwa kabla Lara hajasoma jina lake kwenye hiyo kompyuta na kuongeza. “Lakini wewe unaweza kuniita Jerry.” Lara na mwenzie aliyekuja naye na kujaribu kumtetea, wakamgeukia. Mwenzie akashangaa kidogo.

“Niite tu Jerry.” Akaweka msisitizo akimtizama Lara kwa kutulia kabisa kama siye yeye aliyekuwa akigomba mezani kwa mfanyakazi mwezie Lara. Mwenzie akapigiwa simu, ikabidi kupokea na kuondoka. “Ninachotaka kusema ni kuwa, nilazima kuwepo na kitambulisho kinacho...” “Nimeelewa kabisa. Kwanza ni kwa ajili ya usalama wangu mimi mwenyewe na taarifa zilizopo kwenye hiyo simu na laini yangu. Maana mwingine anaweza akawa mwizi tu, akaja hapa nakutaka laini yangu mimi!” Gafla yeye akaonekana ndio anauelewa juu ya hilo kuliko hata Lara mwenyewe, wakati ndio ulikuwa ugomvi wao na muhudumu wa kwanza waliyeshindwana mpaka kuitwa Lara. Akajieleza hapo Lara akimsikiliza. “Uliniambia unaitwa nani tena?” Ikaishia kutaka kujua jina lake. “Lara.” Lara akamtajia jina akicheka, maana alianza na utundu maneno yakumfanya acheke.

Akatoka bosi wake akaonekana kumfahamu sana huyo mteja. Akamtamka kwa heshima sana ‘Mr. Kembo’. Na kumpa mkono kinyenyekevu akamkaribisha ofisini kwake. Akasimama na kuongozana na bosi wao ofisini kwake. Lara akajua ni mtu mzito. Baada ya muda mfupi akaona bosi wake anampigia simu na kumuita ofisini kwake. Lara akaenda kwa haraka. “Nimempa line yake lakini itabidi uongozane naye hotelini kwake ukachukue vitambulisho vyake.” Lara akashangaa. “Si ulisema umeibiwa waleti!?” “Huwa sitembei na hati ya kusafiria. Nacho si ni kitambulisho? Bosi wako amekikubali, au wewe hukitaki?” Lara akababaika kidogo akiwa na maswali kwa nini yeye mwenyewe asiende na kuleta! “Nimekuja na usafiri, hatutachelewa.” Akaweka msisitizo, Lara akamwangalia bosi wake. Akaona anamwangalia. “Sawa.” Wakatoka.

Walipanda kwenye gari nzuri sana mpaka Lara akashangaa. Ni kama alishafahamu matajiri wa hapo mjini. Kembo hakuwa mmoja wao. Akatulia garini na kupotelea mawazoni. Akamuona Jerry anamcheka, akageuka. “Sasa unanicheka nini!?” “Bwana wewe ni muoga! Sasa hapo unaogopa nini?” “Mimi siogopi.” Lara akajibu huku akijaribu kujiweka sawa. Yule aliyekuwa naye ndani akimtetea wakati akiwahudumia alikuwa akiendesha, wao wakakaa nyuma. Lara aliingia hapo garini na kupotelea mawazoni mpaka hapo anamsemesha.

“Umehamia lini huku Zanzibar?” Jerry akamuuliza kwa utulivu tu. “Sina muda mrefu.” Lara akajibu bila kutoa maelezi mengi kisha na yeye akamuuliza. “Kwa nini umeniuliza?” “Nakuona bado ni mgeni. Umeshapata wenyeji?” Lara akasita kujibu. “Unapapenda huku?” “Sio pabaya.” “Umeshatembelea Bwejuu?” Akamuuliza tena akicheka taratibu. “Hapana.” “Umeshapasikia lakini?” “Ndiyo.” Lara akajibu kwa upole. “Ungetamani kwenda siku moja?” Lara akamtizama na kunyamaza. Akageukia pembeni.

“Lara?” Akamuita tena. Lara akamgeukia. “Sijawahi kufikiria.” Lara akajibu. Hapo ikabidi amtizame vizuri. Ni kweli tokea awe na Jax, Lara alikuwa akitazama wanaume wote nakuwaona kama ndugu, kasoro Jax. Hata mtu alipoonyesha nia ya mapenzi, hakuwa akielewa au hata hakutaka kufikiria mwanaume mwingine upande wa mapenzi. Lakini hapo akajua huyo Jerry anarusha ndoano. Jerry alimtizama kwa kutulia na tabasamu la kutongoza. Lara akatoa tabasamu na kugeukia pembeni. Akamfikiria Jerry.

Alionekana ni mtu mzima, sio kijana. Lakini akamgundua sio wakawaida. Pesa inamtindo wakunukia hata ikiwa haipo kwenye mfuko. Mwenye mafanikio na aliyestaarabika haitaji kukwambia. Utaona tu. Lara akagundua pale yupo tajiri na mfanyakazi. “Huwa mnafunga ofisi saa ngapi?” Jerry akamuuliza tena. “Siku za jumamosi ni saa sita na nusu, lakini jumatatu mpaka ijumaa ni saa kumu jioni. Jumapili mapumziko.” “Huwa unakwenda kupumzika wapi?” Akamuuliza tena. Lara akiwa hamwangalii, ameinama akimjibu. “Bado sijaanza kutembea. Nilitaka kuzoea kazi kwanza.” “Sasa umeshazoea?” Lara akatabasamu tu na kunyamaza akiwa ameinama. Kisha akageukia pembeni. Yule dereva kimya.

Lara akashangaa gari inasimami mbele ya Verde hotel. Akashuka Jerry akaenda kumfungulia mlango. “Nilifikiri nakusubiria hapahapa!” Lara akajihami. “Ndani ya gari!?” Akamuuliza. Lara akajitizama. “Upo sawa. Twende. Tukikipata utakihakiki kama jina ni langu na sura ni yangu, kisha tutashuka chini tena kukinakili, ndipo uondoke na nakala yake. Twende.” Lara akashuka kwani safari hii Jerry aliongea kikazi. “Asante.” Akashukuru Lara kiustaarabu baada ya Jerry kumfungulia mlango na kuufunga. Dereva akaondoka. Lara na Jerry wakaingia ndani.

Wakapanda kwenye lifti, Lara akifuata nyuma. Wakapandisha mpaka gorofa ya pili tu, Jerry akaongoza njia mpaka chumbani kwake. Akafungua mlango kwa kadi, mlango ukafunguka. “Karibu ndani.” “Asante.” Lara akashukuru na kuingia mpaka ndani. Palikuwa pazuri sana. Safi. Kumepangiliwa vizuri. “Unaweza kukaa tu.” Lara akaenda sehemu ya makochi, Jerry akaingia sehemu ambayo Lara aliweza kuona kitanda. Akapotelea hapo, baada ya muda mfupi akarudi na hati ya kusafiria na kumkabidhi. Lara akahisi mikono inaanza kutetemeka. Akafungua ili kuhakiki kama ni yeye, akasoma jina na kumtizama sura. Jerry alikuwa ametulia tu akimwangalia. “Naona sura ya hapa inafanana na wewe.” Lara akaongea taratibu. “Basi kama umeridhika, twende tukakinakili pale mapokezi.” Lara akasimama kwa haraka, na kwa hofu akamrudishia hati yake ya kuzaliwa kama sicho kilichompeleka pale.

Kabla hajatoka, Jerry akamuita. “Lara!” Lara akageuka. “Hukunijibu swali langu.” “Kama nimeshazoea kazi?” Lara akauliza. “Kumbe upo makini?” Lara akacheka kwa hofu kidogo. “Nimeshazoea, lakini niliamua kutulia tu.” Ikawa kama anajitetea. “Leo kuna simu muhimu sana nataka kuzungumza nayo ili kujua kama nitaondoka hapa au leo nina baki. Ndio maana nilipoibiwa simu yangu nilihangaika ili muweze kunirudishia line yangu. Kama mambo yakienda sawa itanilazimu kuondoka na ndege ya mchana, vinginevyo nitakuwepo mpaka jumatatu. Je, kama nitakuwepo ungependa kurudi kwa chakula cha jioni?” “Hapana.” Lara akajibu bila hata kufikiria mara mbili.

Jerry akakunja uso. “Kwamba wewe huli?” “Kwamba sitaki kurudi hapa na kula na wewe.” Lara akajibu bila hofu. “Kwa nini? Au umeshafikiria mbali na ukajua nitakuwa nakutaka kimapenzi?” Jerry akamuuliza kwa kumsuta. “Naomba niwahi kabla hatujafunga ofisi.” Lara akatoka. “Unarudije ofisini?” Jerry akamfuata nyuma. “Nitajua nikishapata hiyo nakala.” Wakajikuta wamesimama kwenye lifti. Akamsikia akicheka tena.

Lara akageuka. “Bwana usiwe unanicheka!” “Kwani una miaka mingapi Lara?” “Sitaki.” Jerry akacheka zaidi. “Sasa unacheka nini!?” “Unavyoogopa! Sasa hapo unakimbia unafikiri nitakubaka?” “Mimi sikujui.” “Kwa hiyo unafikiri na mimi nitakubaka tu nikiwa sikufahamu? Hujui kubakwa pia ni bahati? Kwamba aliyekubaka inamaana amekuamini.” Lara akamwangalia kwa mshangao.

“Kweli Lara! Sasa unafikiri mimi nitakuita hapa, nikiwa nimekuona tu leo, halafu nikutake kimapenzi! Ukiniua kwa magonjwa! Au kwa kuwa nimevutiwa na wewe ndio unafikiri mimi ni malaya wakutupwa! Kila ninakoenda nakusanya wasichana!” “Mimi sijui!” “Sasa si ungekuta nguo za kike chumbani kwangu au mwanamke kabisa! Unafikiri kwa nini nilikukaribisha wewe mpaka chumbani?” “Mimi sijui Jerry.” Lifti ikafunguka Lara akapanda kwa haraka. Jerry naye akaingia.

“Sasa unakimbilia wapi wakati hata hati yenyewe huna Lara!? Utarudisha nini ofisini? Tulia bwana!” Jerry akaenda kusimama mbele yake. “Pumua.” Lara akabaki akimtizama huku anarudi nyuma. Jerry akaanza kucheka tena. “Ujue hapo ndio mwisho. Na hapa kwenye hii lifti kuna kamera. Siwezi kukubaka Lara! Naomba vuta pumzi kwa nguvu, ili kutoa hiyo hofu iliyokuingia.” “Mimi napumua vizuri tu na sina hofu.” “Sio kweli. Mpaka mabega yako yanaonekana upo na tension. Yapo so stiff!” Lara akainama. “Mimi sio mtu mbaya. Naomba tulia. Sitakufanya chochote kwa kuwa na mimi naheshimika sana kwenye jamii. Siwezi kukubali msichana niliyekutana naye tu, akaniharibia heshima. Ni baba na watoto pia. Ukipiga kelele ukisema nimekubaka, hudhani kuwa nitapoteza kila kitu?” Kidogo Lara akafikiria na kutulia. Lifti ikafunguka akatoka.

“Lara?” Jerry akamuita taratibu. “Upo sawa?” “Ndiyo.” Lara akajibu wakiwa wamesimama pembeni ya lifti. “Upo sawa sababu upo hapa au kwa sababu umenielewa?” “Nimekuelewa.” Akajibu taratibu. “Nashukuru. Basi twende tutoe kopi, ili uwahi kazini. Na samahani kama nimevuka mipaka na nikakuudhi.” Jerry akaongea akibembeleza. “Hamna kilichoniudhi.” “Basi twende.” Wakasogea mapokezi. Wakapata huduma ya nakala, akamkabidhi. “Asante.” Lara akashukuru. “Sasa yule dereva si wangu. Huwa namtumia tu nikifika hapa. Ni wa rafiki yangu. Huwa namtumia ninapotaka kutoka tu, nikimaliza shughuli zangu namruhusu. Ni sawa nikikuchukulia taksii itakayokurudisha ofisini?” “Nitashukuru.” Gafla Jerry akawa wakubembeleza, Lara akapoa kabisa.

Wakatoka hapo ndani wakaenda pamoja mpaka nje. Akamtafutia taksii, akasubiri akapanda tena kwa kumfungulia mlango. Ikamgusa Lara. “Nashukuru Jerry. Uwe na wakati mzuri.” “Naomba nijulishe ukifikishwa salama. Au nitakuwa nimezidisha?” “Hapana. Nitakujulisha.” Lara akatoa cheko la aibu na kuinama. “Nimeshalipia, usilipe tena.” “Asante.” Akamfungia, dereva akaondoa gari. Lara akabaki akimfikiria Jerry. Akacheka. Akakumbuka hiyo hali yakujaliwa. Akacheka na kuinama peke yake.

Alifika ofisini mambo yakawa mengi akifunga week. Mpaka saa nane ndio akatoka. Alipofika nyumbani na kutulia, ndipo akamkumbuka Jerry. Lakini akagundua hakuchukua namba yake ofisini. Akajichukia kuona Jerry alikuwa muungwana vile lakini ameshindwa kumjulisha! Akafikiria chakufanya, mwishoe akaona akamtizame tu kama bado yupo pale hotelini.

~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~

Lara akaoga. Mtoto wa kike akajitengeneza kama enzi zake akiwa anatoka. Mwenyewe alijua amependeza. Akarudi hotelini. Akafika mpaka ndani. Akataka kumuulizia pale mapokezi, lakini akajiambia ni heri apitilize tu wasije kumzuia na kama ana msichana, akamfumanie. Akapanda kwenye lifti mpaka gorofa ya pili huku akijiambia endapo atagonga mlango usipofunguliwa, atajua hayupo, na ataondoka. Akaanza kujishitukia akijiuliza kinachompeleka pale ni nini! Akajisuta akiwa amekaribia mpaka mlangoni. Mwishoe akajiambia sio sawa. Aondoke tu. Haraka sana akaondoka bila hata kugonga mlango.

Jerry.

B

aada ya jumamosi nyingine moja kupita, ya pili tokea akutane na Jerry, Lara akiwa amekaa mezani kwake ana kazi, akashitukia Jerry amekaa mbele yake. “Jerry!” “Nahisi kama nilikusoma kwa haraka Lara. Na katika kukusoma kwangu, uongo haikuwa moja ya sifa nilizoziona unazo.” Jerry aliongea akisikika kulalamika. “Sikukudanganya Jerry!” Akatoa simu yake. “Hii ni simu na line niliyonunua hapahapa kwenu. Inaingia simu zote za watu waliowahi kunitafuta, na hakuna aliyenilalamikia kwamba alinitafuta na kunikosa!” “Kwa sababu sikupiga, Jerry.” “Sasa kwa nini uliniahidi kitu ambacho ulijua usingeweza kutimiza?” Lara na Jerry waliendeleza mazungumzo hapo ofisini, Jerry akiwa amekaa kama mteja na akizungumza kwa sauti ya chini tu.

“Siku ile niliporudi hapa, nikakuta nimepewa wateja wengi na bosi alikuwa anawahi kuondoka. Akaniachia ofisi. Nimetoka hapa saa nane, nikiwa nimesahau kuchukua namba yako ofisini kwa bosi. Kumbuka ulihudumiwa na Bosi, na akawa amefunga.” Jerry akageuka kuangalia ofisi ya bosi wake Lara. Lara akajua anachomaanisha. Kwamba mbona yeye anapaona pako wazi! Inamaana kumefungwa mpaka sasa! Akarudisha macho kwa Lara.

 “Siku ile alikuwa amefunga Jerry. Na huwezi amini nilirudi mpaka pale hotelini.” “Lara!” “Sidanganyi Jerry. Nilirudi.” “Niliondoka. Lakini ulishindwa vipi kunipigia hata jana!” “Kumbuka uliniambia wewe ni mtu wa familia. Ningejuaje kama ni sawa kukupigia tu?” Hapo akamuona Jerry ametulia.

“Nimerudi.” “Utakuwepo kwa siku ngapi?” “Inategemea. Sipo kikazi.” Lara akamtizama kidogo na kurudisha macho kwenye kompyuta. Akamtolea kadi na kumuwekea mbele yake. Lara akaivuta na kuisoma. “Nitakupigia. Safari hii naahidi nitapiga.” Akaiweka kwenye pochi yake. “Nitakuwa hotelini nasubiria.” “Unasubiria nini!?” Lara akawa kama hajaelewa. “Nasubiria simu yako au hukuwa ukimaanisha?” “Nitapiga Jerry.” Hapo hapo akamtumia ujumbe na jina lake. ‘Lara’. Akautuma. “Nimekutumia ujumbe. Ujue safari hii namaanisha.” Jerry akatabasamu na kuangalia simu yake.

Akamuona anaandika kitu kwenye simu yake kisha akamwangalia. “Haya. Nimeitunza. Na mimi naruhusiwa kupiga wakati gani?” “Wakati wowote ule.” “Unamaanisha?” “Kabisa Jerry. Naishi peke yangu na sina mtu anayeangalia simu yangu, ni mimi tu.” Hilo likamfurahisha Jerry. “Swali la mwisho kabla sijaondoka.” Lara akamwangalia. “Itachukua muda gani kufikiwa ujumbe wangu?” Lara akawa ameelewa. Akacheka kidogo. “Hakuna mtu mwingine Jerry. Hakuna msururu wa wanaume wenye namba yangu.” “Asante.” Akashangaa anaondoka bila yakuongeza neno. Inamaana ndicho alichomaanisha na amepata jibu alilotarajia. Lara akacheka taratibu.

~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~

Lara alitoka hapo ofisini akampigia mara alipofika tu nyumbani kwake. “Ni mimi Lara.” Lara akajitambulisha. Akamsikia akicheka. “Pole na kazi.” “Asante. Pole na wewe.” “Nilikwambia kama nipo tu mapumzikoni? Sipo kikazi.” “Sasa unafanya nini kwenye hayo mapumziko?” Lara akauliza. “Nakusikiliza wewe.” Lara akacheka akishangaa. “Sikutanii Lara. Hata ukinikaribisha nikutembelee kwako nitakuja tu.” Lara akacheka. “Naishi uswahilini mwenzio. Chumba kimoja na hakuna A/c feni la mezani.” “Kama wewe unaweza kuishi hapo, na mimi nitaweza kuishi tu.” “Hutapaweza. Unataka tukale sehemu? Sijala mchana.” “Hapa wanavyakula vizuri. Karibu.” “Asante.” “Kwa hiyo unakuja?” “Basi nioge kutoa jasho ndipo nije.” “Ujue nakusubiri.” Lara akacheka na kukata simu. Akaanza kujitayarisha.

Mida ya saa kumi akawa anagonga mlangoni kwa Jerry. Safari hii ilikuwa gorofa ya tatu. Jerry akamfungulia na tabasamu kubwa. Alikuwa mtu mzima, lakini alionekana anajipenda sana. Msafi kwa kumtizama, hata mwili wake alionekana ana utunza vizuri. Hakuwa mnene kabisa. Akampisha mlangoni. “Nimekuletea zawadi kutoka safari. Lakini sijui kama utapenda!” Lara akakunja uso. “Mimi!?” “Nipo hapa na wewe Lara. Sizungumzi na mtu mwingine.” Lara akacheka.

Jerry akaelekea ndani. Akamtolea mfuko. “Najua wewe ni mrefu futi.” Akamtajia. “Niliangalia mkono wako nikakisia. Nafikiri sijakosea.” Lara akashangaa sana. “Na harufu niliyoipata siku ile kutoka kwako, naamini kwa aina hii ya parfume sijaenda mbali.” Lara akamwangalia na kufungua mfuko akiwa bado na mshangao.

Akakuta pafyumu na saa nzuri sana ya mkononi. Akamwangalia tena. “Hivi vitu ni vya thamani sana Jerry. Kwa nini umeninunulia mimi!?” “Nafikiri nimevutiwa sana na wewe, Lara. Ndio maana nimerudi ili kukwambia. Halafu kama utakubali, tuanzishe mahusiano.” Jerry alikwenda moja kwa moja kwenye pointi mpaka Lara akabaki anamshangaa.

“Samahani Lara. Mimi nimuwazi sana. Halafu siishi hapa Zanzibar. Kusema nitachukua mambo taratibu nijivute ndio baadaye sana nikwambie. Nikija hapa nakuja sababu za kibiashara tu. Na pia sio kijana na sitarudi kuwa mtoto. Sina muda wakupoteza. Nikishajua nataka kitu, kuwa situlii mpaka nikitafute na kukipata.” Lara akabaki anamwangalia nakushindwa ajibu nini.

Jerry akakaa pembeni yake. “Lara?” “Uliniambia unafamilia Jerry! Mimi naingilia wapi!? Sitaki kuwa mvunja ndoa.” “Usiwe na wasiwasi. Hutavunja ndoa yangu na wala hutaingilia chochote kwenye ndoa yangu.” Lara akawa hajaelewa. “Ndio itakuaje!?” “Nina watoto wawili wakubwa tu. Ni mapacha, wapo wakiishi na mke wangu kwenye mji unaitwa Virginia. Mke wangu na watoto wanaishi huko. Na ni vijana wakubwa tu, wanaingia chuo mwaka huu mwishoni.” Lara akajiweka sawa.

“Nilikuwa na mahusiano mengine. Lakini yale nilikuwa na mke wa mtu. Tuka...” “Jamani Jerry wewe ni muwazi kupitiliza bwana!” Jerry akaanza kucheka. “Nivumilie nimalize. Pagumu panakaribia kuisha.” Lara akamtizama. “Basi napunguza ukali wa maelezo.” “Hapana. Lakini sijawahi kukutana na mtu kama wewe!” Jerry akacheka. “Basi nimalizie kwa kusema niliachana naye. Amerudi kwa mumewe, wakaamua kuongeza mtoto mwingine. Imeshapita miezi nane sasa tokea tuachane.” “Sasa amepata mtoto?” “Sidhani. Maana mara ya mwisho nilimuona akiwa hana tumbo na hiyo ni miezi mitatu iliyopita.” Lara akashangaa. “Sasa hukumuuliza?” “Sikuona sababu kwakweli. Kwa kuwa hainihusu tena.” Lara akamtizama.

“Na sina UKIMWI.” Akaongeza na kuzidi kumshangaza Lara. “Ila tunaweza kwenda kupima tena tukiwa pamoja ili ujiridhishe na mimi. Ila mimi nimeridhika na wewe. Kwanza nimevutiwa na kila kitu chako. Nakutaka Lara. Na mimi huwa sio mzuri wa jibu la hapana. Nitakung’ang’ania mpaka unikubali.” “Kwa hiyo mbali na mimi, unawasichana wengine wangapi?” “Kwa kuniona hapa, ujue ni wewe peke yako mbali na mke wangu. Kingine, mimi sio mtu wa wanawake wengi. Kwa hiyo usiwe na wasiwasi. Mtakuwa wawili tu, na mke wangu. Ila ningependa kujua kama unakuwa na mahusiano mengine. Mimi ni muoga sana wa magonjwa. Na sitaki kumuu mke wangu tukaacha watoto wetu.” Lara akahisi ni kama anasikiliza hadithi. Akaweka ule mfuko chini.

Jerry akacheka na kusimama. “Nikuagizie chakula gani? Nataka tule hapahapa chumbani tufahamiane zaidi.” “Hapana Jerry. Mimi sipo tayari kueleza chochote kinachonihusu.” “Kwa nini!?” “Kwa sababu ya nyuma ni machungu matupu. Na ndio maana nilikimbilia huku na nimebaki bila rafiki kwa kuwa sitaki kuzungumzia maisha yangu ya nyuma.” Jerry akafikiria kidogo. “Mara ya mwisho kupima UKIMWI ilikuwa lini na umejamiana mara ya mwisho lini?” Lara akamtizama na kutingisha kichwa. “Naomba na hilo lisiwe siri Lara. Mengine ni sawa.” “Naomba twende hospitalini tukapime upate majibu yako, tafadhali. Lakini si kukueleza maisha yangu ya nyuma.” “Wazo zuri.” Kama utani, Lara akashangaa anachukua waleti na kutorudi pale. “Twende.” Lara akacheka kama haamini wakatoka.

“Unafikiri mimi nakutania? Nipo hapa kwa ajili yako Lara. Sipo kikazi. Nimerudi juzi kutoka kwa familia yangu. Japo nilipeleka mzigo wa biashara kule, nimerudi ndio nikakufuata. Nilikuwa nakifikiria hicho kiumbo chako kila wakati!” Lara akacheka mpaka akainama. “Bwana Jerry!” “Nakwambia ukweli. Sidanganyi. Unafikiri ingekuwa mtu mwingine angenitoa hapa kwenda kupima UKIMWI kama sio kwamba nakutaka kwa hali na mali!” “Bwana Jerry!” Jerry akazidi kumcheka Lara aliyekuwa amejificha uso wakiwa wamesimama kwenye lifti. Akampitishia mikono kiunoni na kumvuta karibu. Lara akajisogeza karibu mpaka mwilini mwake. Jerry akamkumbatia vizuri. Akashangaa Lara anatulia hapo. Kimya. Akahisi analia. Akamchungulia pale kifuani, akagundua analia.

Jerry akamvuta pembeni. Akamkumbatia vizuri na kumbusu. “Naruhusiwa kuuliza?” Lara akatingisha kichwa kukataa. “Okay. Basi tutasimama hapa mpaka utulie. Au unataka turudi ndani?” “Twende hospitalini. Mimi nipo sawa.” Lara akajaribu kujifuta machozi. “Hiyo ni kazi yangu.” Akamfuta machozi kama mtoto, mpaka Lara akacheka. “Ujue mimi mkubwa!” “Sio ukiwa na mimi. Ukiwa na mimi wewe ni babe wangu.” Lara akajisikia vizuri. Akacheka kwa kudeka.

Walikwenda hospitalini. Wote wakatolewa damu. Wakakaa hapo wakisubiri. “Ukikutwa umeathirika, nitasikitika!” Ilimbudi tu Lara acheke. “Kwa nini?” “Ninakutamani sana. Sitaki maradhi yatutenganishe.” Lara akamwangalia na kushindwa kuongea. Akaishia kucheka. “Mimi sina maradhi Jerry. Sijajaamiana nafikiri zaidi ya mwaka sasa.” Jerry akatoa macho. “Hivyo ulivyo wewe!” “Nikoje?” “Mrembo hivyo, hujapata wakukuganda kama mimi!?” “Sikutaka tu.” Lara akajibu na kuinama. Jerry akajua kuna stori nzito hapo. “Basi nakushukuru kwa kunipa mimi nafasi.” “Nani amekwambia kama nimekukubali?” Jerry akacheka sana. 

“Unacheka kwa sauti bwana Jerry, mpaka watu wanatugeukia sisi!” “Mwenzio sina chakujificha. Sasa niambie nafanyaje ili nikupate Lara? Ila nataka kukwambia utakayoyapata ukinikubali. Furaha. Kila ukiwa na mimi utakuwa na wakati mzuri. Huo ni uhakika. Hata ukitaka usifanye kazi ila kutumia tu, ni juu yako.” Lara akashangaa sana. “Sikutanii. Wewe ukitaka uwe na mimi kila wakati, ruksa. Kasoro kwa familia yangu tu. Lakini kwengine hamna shida. Halafu ujue nitakujali, sitakuumiza. Mimi ndivyo nilivyo. Acha nijisifie. Nimejaliwa kupenda na kujali hasa nikipata mwanamke anayetaka kupendwa. Mengine utajionea. Utashangaa wewe ndio unaning’ang’ania. Nipe usiku wa leo tu, uone kama kesho utataka kuondoka.” “Nani amekwambia usiku wa leo nitalala na wewe!?” “Basi naanza kukuomba Lara. Naomba usiku wa leo usiniache peke yangu. Nimekuja kote huku kwa ajili yako, kweli utaniacha peke yangu!?” Lara akainama akiwa ameshalainika.

“Lara?” “Mimi sikufahamu Jerry!” “Nakuruhusu uniulize chochote unachotaka na nakuahidi sitakudanganya, ili tu unifahamu hivyo unavyotaka.” Lara akamwangalia na kuinama tena. Akamshika shingo na kumwinua. Palepale hospitalini akaanza kumbusu. Lara akanogewa na hilo busu. Jerry alijua kubusu! Lara akajisogeza karibu akiwa ameshikwa vizuri, wamekaa tu wala hawajakumbatiana. Akaendelea kumbusu mpaka akamuona amelainika palepale. Akamuachia. Lara akajishitukia na kuinama. Akamvuta mkono. Akaubusu na kuukumbatia. Wakatulia. Akamuona anamuegemea begani kama mtoto mkiwa anayehitaji mapenzi. Jerry akamzungushia mikono na kumkumbatia vizuri.

 Swala la Jerry na watoto.

Walitoka hapo na kurudi hotelini wote wakionekana hawana maambukizi yeyote kwamba afya zao ni nzuri. Waliagiza chakula chumbani. Wakati wanakula Jerry akaanza. “Unahisi nina miaka mingapi?” Lara akamwangalia. “Kisia tu.” “Mwishoni mwa 40.” Lara akajibu, Jerry akacheka. “Nina miaka 55. Nilichelewa kuoa na kuzaa sababu ya kutafuta pesa. Na sikutaka watoto wengi. Mmoja tu, ndio maana mke wangu akahangaika kuzaa mapacha. Kwamba mara moja. Tunalea mara moja, halafu basi.” Mpaka hapo Lara akajua anachotaka kumwambia. Akapoa.

“Nilikwambia mimi nimuwazi Lara. Nataka tukubaliane mapema na unielewe ili kusijekuwa na kutokuelewana au kuumizana. Sitaki uje uumie. Sio kutoka kwangu. Nina malengo ya pesa tu kwa sasa na nipo busy mno. Sina muda wakulea. Na mimi kwangu mtoto sio kitu kidogo. Hao watoto wanaolelewa na mama yao, wananigarimu sana. Muda na pesa, kwa sababu sitaki wakue bila mimi au wahisi sikuwa na malengo wakati wanazaliwa. Inanilazimu niwepo kwenye maisha yao kila wanaponihitaji. Katika uzima na ugonjwa. Najitahidi kuwepo kila wakati wanaponihitaji kitu kinachonifanya niahirishe shuguli zangu nyingi. Ninachotaka kusema ni kuwa..” “Hutaki kuzaa na mimi.” Lara akamalizia.

“Ukiiweka hivyo inakuwa chungu kidogo. Ila ni kwamba sina muda na sitaki kuongeza mtoto mwingine hata kwa mke wangu. Na yeye kuna wakati alijaribu sana kunishawishi tuongeze mtoto, lakini ilibidi kumuweka wazi. Kuwa hataongeza na mimi. Mimi ni baba wa wawatoto wawili, basi. Sina nafasi ya watoto wengine. Kwa yeyote yule.” Jerry akaweka msisitizo, kidogo ikamuumiza Lara.

Jerry akaendelea. “Hata hao mapacha ilikuwa shuguli sana kukubali. Nilitaka mtoto mmoja tu.” Lara akabaki ameinama. Akamkumbuka Jax na mtoto waliyempoteza. Akakumbuka alivyokuwa tayari kuzaa na Jax aliyesema asingekuwa na shida na kuzaa naye. Jerry amekuwa muwazi tokea mwanzo. Lara akawa anajiuliza kama aondoke au la. Moyo ulishatibuka.

“Naomba usifikirie mbali wakati nipo hapa na wewe. Niulize chochote Lara. Tafadhali usikate tamaa na kuniona mimi ni mbaya. Nina uhakika haukuwa na mpango wa kuzaa na yeyote yule. Na ninauhakika unampango wa kuwa na familia nzuri, na mimi nina familia yangu. Huoni kama nimekuwa mtu mzuri kwako, sijakudanganya?” “Labda sijaelewa, niulize. Unachotaka kutoka kwangu ni nini?” Lara akauliza taratibu tu.

“Kampani yako. Nakuhitaji kwenye maisha yangu. Mimi na wewe tu. Na nimefurahi kujua kwa sasa huna mtu. Kwa hiyo tutakuwa huru kuwa popote tutakapokubaliana kuwa bila kuongeza jukumu jingine la watoto. Utakapokuwa tayari kuanzisha familia yako, uniambie tu, tutazungumza na kukubaliana.” Lara akavuta pumzi kwa nguvu na kuzishusha. “Sio ngumu Lara. Nakuahidi wakati mzuri. Nakuhakikishia. Labda ushindwe mwenyewe. Huna haja yakuishi huku. Labda upende. Wanachokulipa hapo, naweza kukupa kwa mwaka mzima. Ukaweka benki na kuendelea kuwa na mimi tu. Hata ukitaka kufanya hiyo ndio kazi yako, sina shida.” Lara akakunja uso.

“Labda niweke hivi, wanakulipa mshahara kiasi gani, kwa mwezi?” Lara akainama. “Niambie tu, usione aibu.” Lara akamtajia. “Sasa hiyo zidisha kwa mwaka, mara tatu, nitakupa uweke benki kwa kuwa na mimi tu. Ukichoka kukaa tu, ukataka kazi, tutatafuta.” Jerry aliongea kirahisi mpaka akamshangaza Lara. “Na kwa kuwa mimi nina akili ya biashara, ningekushauri ufungue kitu chako ujiajiri.” Lara akahisi ni kama anamdanganya. Ila kwa nini! Jerry amekwenda mpaka kutoa damu! Akanyanyua uso akaona anamwangalia.

“Kwa nini ufanye hivyo!?” Lara akamuuliza. “Labda ungeuliza hivi, kwa nini nafanya hivyo kwako wewe. Si ndio swali lako?” Lara akabaki akimwangalia kama anayetaka kumsoma. “Lara?” “Mimi naona unazidi kunichanganya Jerry!” Jerry akaanza kucheka. “Usichanganyikiwe, wewe niulize tu. Na nimekusaidia kuweka swali vizuri. Sasa ni hivi Lara. Kwa nini wewe, ni kwa sababu nimevutiwa na wewe. Sitafuti mke wa kuoa wala kuzaa watoto. Hicho kipengele nimefunga. Ninachotaka ni msichana mdogo, mzuri wa sura na umbile. Sasa vyote wewe unavyo ndio nilipokuona, nikakutizama mpaka vidole vya mikono, nikajua ndio kitu nataka.” Lara alichoka mpaka akabaki ameduaa. Jerry akazidi kucheka.

“Yaani wewe nimeshakupigia mahesabu yote ndio maana nikarudi. Maana nilikuwa nakufikiria zile siku nitakazokuwa nikiamka pembeni yako!” Lara akanyanyuka na chakula chake. Jerry akazidi kucheka. “Unaweza kujiuliza kwa ninavyozunguka kote huko sijaona wasichana wengine?” Lara akasimama na kumgeukia. “Nawaona lakini unakuta wanavimapungufu fulani fulani. Halafu wamejaa mpaka wanakera! Hawapo kama hivyo wewe, mtulivu na unaunyenyekevu fulani hivi. Hujikubuu! Sio lishangingi. Upo kitoto kitoto, unaweza kujaa mkononi. Halafu mzuri. Mpaka midomo yako mitamu! Pale hospitalini nilikuwa natamani nisiku..” Lara akaondoka. Jerry akazidi kucheka. “Sasa mbona unakimbia sifa zako! Lara?” Lara akaenda chooni na chakula chake. Akamsikia akizidi kucheka kule alipomuacha, yeye akaendelea kula huko chooni.

Mwishoe akamfuata. “Sasa kwa nini unakula huku chooni?” “Nakukimbia Jerry.” Jerry alicheka mpaka akakaa chini kabisa. “Njoo ukae hapa ule. Mimi nitanyamaza.” Lara akaenda kukaa pale pembeni yake. Lakini chini hapohapo chooni wakiwa wamekaa sakafuni kabisa. Akaanza kula tena, kimya. Akala mpaka akamaliza bila Jerry kuzungumza kitu.

Lara akamwangalia. “Sasa unafanya nini hapo?” “Nilikuahidi kuwa kimya ili umalize kula. Na sitaki kukuacha peke yako, wewe ni mgeni wangu.” “Asante kwa chakula.” “Umetosheka?” “Kabisa. Twende na wewe ukale.” “Mimi imeshatosha. Nimekwambia miaka yangu. Nipo hivi nilivyo mpaka ukadhani ni mdogo kihivyo ni kwa kutoa mlo wa usiku. Ndio maana unaniona hivi.” “Kweli una mwili mzuri!” “Na mazoezi. Chakula kwangu ni kwa ajili yangu sio mimi kwa chakula. Si hata kitabu cha Mungu kimeandika?” Lara akamtizama na kunyamaza.

“Umeamua nini?” “Juu yako?” Lara akamuuliza. Jerry akacheka. “Juu yetu sio yangu mimi. Huhitaji muda mzuri na mtulivu?” “Nataka.” “Sasa kwa nini unajifikiria wakati mimi nakuahidi wakati mzuri na ahadi nzuri kiasi hiki! Hutakaa ukapata mwanaume kama mimi Lara. Mkweli na mwenye pesa!” Lara akacheka. “Unafanya biashara gani?” “Una muda kiasi gani wakunisikiliza juu ya biashara zangu?” Lara akacheka na kusimama kwenda kuosha mkono, Jerry akasimama na yeye.

Akamfuata pale kwenye sinki nyuma yake akaanza kumbusu shingoni. Huku akimpapasa taratibu. Lara akajikausha mikono Jerry akiendelea kumbusu na kumnusa shingoni. Lara akacheka. “Unanitekenya!” Akamsikia akicheka kidogo na mikono ilishaingia ndani ya gauni kupitia chini akinyanyua gauni taratibu mpaka mikono ikafika kiunoni na kurudi kwenye makalio huku midomo yake ikiwa shingoni kwa nyuma mpaka pembeni akimbusu. Raha aliyokuwa akiisikia Lara, alitamani kugeuka lakini Jerry alikuwa amesimama nyuma yake akiendelea kumpapasa kwa shauku, hakutaka kumtoa hapo. Akahisi anamtoa nguo ya ndani huku mikono ikimzunguka kama aliyekuwa akimuona kwa mikono na hisia. Jerry alikuwa amefunga macho.

“Lara.” Akamsikia akimuita taratibu. Lara akatulia tu. Akamtoa nguo zote akiwa vile vile amesimama nyuma yake, kisha akamnyanyua na kumuweka juu ya sinki. “Nilijua tu siwezi kukosea. Upo vilevile kama nilivyokudhania.” Jerry alikuwa akimwangalia pale alipomuweka. “God! you are beautiful Lara!” Akamsifia kwa kumaanisha. Lara akacheka na kujificha uso. Akamsikia akimbusu tumboni kwenye kitovu huku akipandisha juu taratibu mpaka midomoni. Yeye bado alikuwa ana nguo zote.

Alimtoa hapo na kwenda kumlaza kitandani. Lara mwenyewe alijua Jerry anamfurahia hatua kwa hatua. Ila aligundua amependa hips zake. Wakati mwingi kwenye mapenzi alikuwa akimalizia mchezo akiwa amezikamata kwa nguvu huku akivuta hisia. Alipokuwa anampakata huku mapenzi yakiendelea, midomo haikutoka kwenye matiti na mikono kwenye hips zake ndipo alipokuwa akimaliza na kumuona amefurahia zaidi. Na anapokuwa amemuinamisha, basi lazima atazishikilia hizo hips za Lara kwa nguvu ndipo anamsikia mpaka akigugumia. Lara alijua ameupenda mwili wake na kuufurahia, kitu kilichomuongezea ujasiri na yeye akatulia kufurahia mapenzi hayo yenye ahadi ya utajiri tu.

Na kweli alipata usiku mzuri. Jerry alijua anachokifanya na hakuwa mwenye papara. Alifanya naye mapenzi hatua kwa hatua. Mpaka wanamalizia penzi la asubuhi kabla hawajatoka kitandani, Lara mwenyewe hakutaka kuondoka hapo.

“Jumapili huwa unafanya nini?” Jerry akamuuliza wakiwa bado wapo  kitandani. “Napumzika, nafua na kufanya usafi kwenye chumba changu. Ulitaka niondoke sasa hivi?” Jerry akamgeukia vizuri. “Kwa haya unayonipa hapa, nishaanza kufikiria maisha bila wewe.” Lara akajifunika mto na kumfinya. Jerry akacheka. “Upo kama nilivyokutarajia, ila na zaidi. Mpaka naona shida kukuacha.” “Bwana Jerry!” Akamsikia akicheka. Lara akatoka kwenye mto. “Tuondoke wote basi.” “Twende wapi?” “Tukaishi wote Dar.” Lara akawa kama hamuelewi.

“Halafu kuja huku utakuwa ukinisindikiza kwenye biashara zangu. Nakuahidi hutapata shida na sitasubiri uniombe kitu. Nimejaliwa kujali.” “Wewe ni mtu wa namna gani!?” Jerry akacheka sana na kumvutia juu ya mwili wake, Lara akawa amemlalia. “Bora nijisifie mwenyewe maana hakuna atakayeweza kukueleza habari zangu vizuri isipokuwa mimi mwenyewe. Nitakupenda Lara, mpaka mwenyewe utashindwa kuniacha.” Lara alicheka sana mpaka akajificha shingoni kwake. Jerry akaanza kumpapasa. “Unanifurahia?” Lara akakubali kwa kutingisha kichwa. “Sasa kwa nini unasita kuchukua hatua nyingine? Au kwa kuwa sijaanza kwa kukudanganya?” Lara akacheka na kutaka kutoka hapo mwilini, Jerry akamvuta. Lara akamwangalia. “Una midomo mitamu, Lara! Nibusu tena.” Lara akachangamkia penzi la mara ya pili asubuhi hiyo.

~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~

Mpaka siku ya jumatatu Lara alishindwa kuondoka hapo. Alichofanya ni kumtumia ujumbe bosi wake kumwambia anaumwa. Jerry alikuwa akicheka tu. “Na kesho utamwambiaje?” “Utakuwa umeondoka Jerry, na kuniacha niendelee na shuguli zangu.” Jerry akazidi kucheka. “Mimi nina mpango wakuendelea kupata raha mpaka jioni ndipo niondoke hapa. Usinifukuze na kunipunja kwa kushindwa kuamua kwako. Mimi nimeamua ni wewe. Raha unayonipa, nimeamua kuipokea wala sijivungi. Kwanza kazi yenyewe wanakulipa mshahara mdogo! Sijui kwa nini unaing’ang’ania!” “Ukija kunikimbia nitaishije?” “Ndio maana nakwambia nakulipa mshahara wako wa miaka mitatu kabisa. Halafu unakuwa na kazi yakustarehe tu.” “Hivi wewe unamaanisha kweli!?” Akatoka na kuelekea kwenye mkoba wake.

Akamuona anatoa kitabu cha hundi, akaandika na kumkabidhi. “Ukienda kuweka hii kwenye akaunti yako, inakuwa pesa.” “Jerry!” “Watu wanafanya kazi na kupata pesa, halafu hawajui kutumia pesa zao kuwapa raha. Mimi nina pesa, wewe unacho ninachokitaka. Sasa kwa nini unashangaa! Nakutaka Lara.” Ikawa kama utani. Lara akakubali. Akaanzia benki. Akaweka ile hundi. Alipoona pesa imeingia kwenye akaunti yake, akaenda kuandika barua ya kuacha kazi, kisha akarudi hotelini kwa Jerry. Jerry akapiga simu kuongeza tiketi ya pili yakurudi jijini siku inayofuata. Kuwa wako wawili.

~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~

Kipi kitaendelea, usikose muendelezo...

CONVERSATION

0 Comments:

Post a Comment