“Unakumbuka Ibra, Felex na Ney
walifanya kazi kwa karibu sana na mimi?” “Nakumbuka.”
Sabrina akakubali. “Wanajua ni kiasi gani nakupenda Brina.” Sabrina akabaki
amepigwa na butwaa. “Nakupenda Brina.” “Mwenzio
nilijua nimechelewa Jack! Naona mpaka aibu!” “Sio kwangu. Labda kwa
mwingine na labda uwe hunipendi kabisa Brina. Hapo nitashindwa chakufanya.
Lakini kukiwa hata na upendo kidogo tu, naamini hutashindwa kuishi na mimi.”
Sabrina hakuamini. “Unauhakika Jack!?” Akauliza akiwa haamini. “Nakupenda Sabrina.
Nakupenda kwa moyo wangu wote, sina sababu yakudanganya. Ningeshaoa, lakini
kulikuwa kama na tumaini pengine ungekuja kubadili mawazo, ndio maana niliona
nisiharakishe nikusubiri mpaka nione mwisho wake.” “Asante
Jack.” Jack akakaa na yeye.
“Kwa hiyo umekubali nikuoe?” “Ndiyo Jack. Nitafurahi kuwa mkeo. Nakuahidi nitakuwa
muaminifu kwako.” Jack akamvuta
mkono akamvalisha ile pete kwa haraka sana. Sabrina akacheka machozi mpaka kidevuni.
“Kubwa kidogo. Nitaipeleka wapunguze.” “Lakini acha
nivae kidogo Jack.” Jack akacheka. “Umeipenda?” “Sana,
na nimefurahi kupita kiasi Jack, siamini!” Jack akajisogeza karibu,
akambusu kwa mara ya kwanza mdomoni. Kidogo tu, kisha akamwangalia. Akambusu
tena. Akaongeza tena, kisha akaongeza tena na tena ikawa mfululizo, Sabrina
akamkumbatia kwa upendo, ndipo Jack akaanza kunyonya midomo ya Sabrina kwa uchu
kama fisi aliyeona nyama.
“Jack!” Sabrina akajivuta pembeni
kidogo. “Ulisema utanioa?” “Si umesema ‘ndiyo’?” Na yeye Jack akauliza.
“Lini? Baada au kabla ya kujifungua?” Jack akajivuta nyuma na kujiegemeza
kwenye mto. “Wewe ulitaka iwe lini?”
Jack akauliza kama anayefikiria. “Vile unavyotaka wewe Jack.” Sabrina
akajibu kama anayebembeleza. “Kwa hiyo hata nikitaka iwe kabla yakujifungua pia
ni sawa?” “Ningefurahi Jack. Ningefurahi
sana. Sema nafikiria maandalizi. Nimebakisha kama miezi mitano na siku chache
tu ili nijifungue.” “Mbona tumbo lenyewe halipo!” Sabrina akacheka. “Naomba
kuona.” “Kabisa!?” Sabrina akauliza kwa kushangaa kidogo na cheko la aibu
usoni. “Unamaanisha nini ukiuliza ‘Kabisa’?” “Sijui! Labda unataka kuona
hapa kwenye nguo.” “Kwenye nguo ndio sioni. Ndio maana nataka kuona tumbo
lenyewe.” Sabrina akajishauri.
“Tokea nioge asubuhi, halafu nimekuwa
na siku ndefu! Tumetembea sana juani na Emma. Labda nikaoge kwanza.
Utanisubiri?” “Hapa au chumba kile kingine?” Sabrina akacheka taratibu. “Hapa.
Si ni sawa?” “Sawa.” Sabrina akatoka kitandani, akachukua taulo na khanga. “Njoo
kidogo.” Sabrina akarudi pale kitandani na kukaa. Jack akamsogelea na kuanza
mabusu tena. Akambusu mpaka Sabrina akasalimu amri. Akajiachia hapo mikononi
kwa Jack, asikumbuke kuoga tena. Alichofanya Jack ni kuendelea kunyonya hiyo
midomo huku akipitisha mikono chini ya gauni mpaka akafika tumboni. Akaanza
kumpapasa tumbo huku akiendelea kunyonya midomo yake.
Mvumilivu, Kala Mbivu.
S |
abrina
akahisi vidole vikipenya ndani, pembezoni mwa chupi. “Nikaoge kwanza Jack,
nanuka jasho!” Sabrina akanong’ona taratibu. “Siwezi kusubiri tena.” Jack akajibu
huku akimnyonya shingoni na kumbusu. “Nimekuwa na vipingamizi vingi sana juu
yako Brina. Nimesubiri sana, jasho haliwezi kunifanya nikasubiri tena zaidi,
tafadhali Brina.” Sabrina akajipandisha kitandani vizuri. Kwa haraka Jack
akamuweka sawa. Alimbusu kila mahali kama anayebusu alumasi wakati alikuwa
akitembea juani siku hiyo nzima. Kwa hakika alijua ananuka. Lakini Jack
hakujali. Akaendeleza mabusu ya haja, Sabrina akayasikia katika kila mfupa wa
mwili wake. Harufu ya Jack ikamwingia mpaka kwenye fahamu zake, akasikia
kutulia kwa ajabu, akamvutia Jack mwilini kwake, yakaanza mapenzi.
Wawili hao walifahamiana kwa miaka,
lakini siku hiyo wakavuka mipaka. Sabrina alimsikia vile Jack anavyomfurahia,
ujasiri ukaongezeka. Akajawa nguvu ya ajabu, uchovu ukamwisha. Penzi
lililofanywa hapo, kila mmoja alifurahia, wakajitupa kitandani hoi. “Sasa nenda
ukaoge, nije nimuone mwanangu.” Sabrina akacheka kwa furaha. Akavuta khanga
yake kutoka sakafuni, akajifunga na kuelekea bafuni, akamuacha Jack amejilaza
kitandani.
Sabrina anatoka kuoga, akamkuta Jack
amelala, kama aliyetoka kulima siku nzima. Akajua hakuna kuoga tena.
Akamsafisha na kumfunika, Jack akiwa hana hata habari. Furaha iliyokuwa imemjaa
Sabrina, alitamani apate wakumwambia kuwa amechumbiwa na Jack. Akajipaka
mafuta. Akavaa tisheti ya Jack akakaa kitandani akijiangalia kidoleni na ile
pete, asiamini Jack amekusudia kumuoa na ule ujauzito! Alijawa furaha, hofu ikaanza
kupungua. Akamvuta mkono pale alipokuwa amelala, akaubusu mara kadhaa. “Asante
Jack.” Akanong’ona taratibu. Aibu yakuzunguka mtaani na tumbo ambalo muhusika
hakutaka kuzaa naye, akimtaka atoe huyo mtoto, ikaanza kupungua. “Sijui
atanioa lini huyu!?” Akajiuliza akitamani iwe kabla hajajifungua. Akajilaza
pembeni ya Jack, ukutani. Akaanza kumnusa mpaka na yeye akapitiwa na usingizi.
~~~~~~~~~~~~~~~~~~
Alam
ya kumuamsha Jack kwenda kazini ndio iliyowatoa wote usingizini. Jack akavuta
boxer yake pembeni na kuivaa maana aliamka mtupu, Sabrina alimfunika tu usiku
uliopita, baada ya kumsafisha. “Ngoja
nikakuandalie kifungua kinywa, wakati unajiandaa kwenda kazini.” Sabrina
akataka kutoka kitandani. Akamvuta. “Unisamehe jana nilipitiwa na usingizi.
Nilikuwa nimechoka! Zaidi mawazo. Sikulala vizuri tokea nimeondoka hapa. Wakati
wote nilikuwa nikiamka kutoka usingizini najaribu kukupigia, na kusubiria simu
yako.” “Jamani Jack! Pole. Mwenzio nilijua unafurahia na wenzio! Sikuwa hata na
wazo kama utakuwa ukinikumbuka huku!” Jack akamwangalia kama anayemuuliza
ningewezaje! “Kweli Jack. Nilijua utakuwa busy na marafiki zako, nikaogopa hata
kukosea kupiga, marafiki zako wasijefikiri nakusumbua.” “Basi heri ungenipigia
nikaacha kupokea, kuliko kuacha kunitumia hata ujumbe kutaka kujua ninaendeleje
Brina!” “Naomba unisamehe Jack. Nisamehe bure.” Sabrina akakaa vizuri.
“Nimekuwa
na watu ambao hawajali mawasiliano na mimi Jack. Historia ya nyumbani ni kama
nilivyokusimulia. Tokea naondoka nyumbani nilipokwambia nakwenda kupumzika kwa
dada Sabina, huwezi amini Jack, mpaka nahamia Moshi, muda wote hata wazazi
wangu hawakunipigia simu kutaka kujua ninaendeleaje, wakati nawaona
wanavyofanya tofauti kwa kina Sabina na kaka! Hazipiti siku mbili, lazima wao
wenyewe wawapigie kuwajulia hali lakini sio mimi! Haya, nikawa na Emma, yeye
ndio ilikuwa wakati mwingine ukimpigia anagomba kabisa ni mpaka akupigie yeye
mwenyewe.” “Haiwezekani Brina!” “Kweli Jack. Mpaka nilikuwa naona aibu
kuwaambia watu hivyo. Tena anakuwa mkali kabisa, anasema mpaka akupigie yeye.
Kwa hiyo swala la mawasiliano halipo kwangu. Na ni kama nimeingiwa hofu, naona
kupiga ni kama kumsumbua mtu!” Jack akaumia kwa kiasi fulani.
“Sio
kwangu Brina. Naweza nisipokee kama nipo kwenye simu nyingine, au katikati ya
mazungumzo na mtu. Lakini lazima nitarudisha, au hapo hapo nitapokea na
kukwambia nitakupigia. Mimi napenda mawasiliano sana. Hata kina Ibra wanajua
hilo. Na Tino naye?” Sabrina akacheka kwa kuguna. “Sasa yeye alipitiliza.
Alikuwa akinifuata mpaka chooni kama nitachelewa. Na hakuna nilipokuwa nikienda
bila yeye. Na hapo nafikiri ndipo nilipojichanganya Jack. Nikafikiri ni mapenzi
ya dhati, kumbe ni kwa kuwa alikuwa akinitegemea, aliogopa ningeweza kumkimbia
kabla hajapona kabisa na kuweza kujitegemea mwenyewe.”
“Mambo
yalianza kubadilika tulipokuwa Moshi, tena alipoanza kujitegemea. Akawa ananionyesha
kama si lazima tena. Wakati mwingine alipokuwa yupo gym anafanya mazoezi pale
kwenye Villa, ilikuwa nikimfuata, ananiambia yeye yupo tu sawa, nirudi kwenye
apartment yetu. Yaani kama anayeniambia nisimfuatefuate. Nikaanza kuumia, kwa
kuwa haikuwa hivyo mwanzo. Alishanizoesha kuwa naye kila mahali. Kwa hiyo
naomba nielewe Jack, na hofu pia inachangia.” “Basi sio mimi. Mimi nataka
unisumbue.” Sabrina akacheka na kuinama.
“Naomba
kumuona mtoto.” Sabrina akashangaa kumbe bado anakumbuka. Alishajiambia ile ya
jana kutaka kuona tumbo, ilikuwa janja yakumvua chupi, kumbe nia alikuwa nayo!
Sabrina akajilaza chali. Jack akampandisha ile tisheti mpaka juu kabisa.
Akaanza kumshika tumbo. “Kweli ukiangalia hivi kwa karibu utagundua. Limetuna
hapa chini na gumu kabisa!” Jack akaendelea kuongea huku akimshika kuzunguka tumbo.
“Inauma nikifanya hivi?” “Hapana bwana. Hivyo unanibembeleza.” Wakacheka.
“Anacheza?” Akauliza tena Jack. “Bado mdogo. Sijamsikia hata mara moja.” Akambusu
mara kadhaa, akamsikia midomo inazidi kupanda juu. Sabrina akacheka.
Kilichoendelea Huko Dar.
“Unanitekenya
bwana!” “Nataka tufunge ndoa Brina wangu. Au unasemaje?” Akawa anamchungulia kule
Sabrina alipokuwa amejilaza, yeye tumboni kwake. “Njoo kwanza hapa nikuhoji
vizuri. Mbona imekuwa gafla wakati uliondoka hapa na Pam vizuri?” “Kama
uligundua, Ibra alilazimishia sana ile safari. Kumbe lilikuwa wazo la Pam na
yeye alikuwa na yake, nitakuja kukwambia wakati mwingine, leo tubakiwe na
furaha tu.” Sabrina hakuwa ameelewa. Jack akamuelezea alivyoambia na Ibra, Pam
alipompigia simu na kumuomba awaalike. Sabrina akashangaa sana.
“Sasa
ikawa ni kama ikatokea bahati. Yule mwanamziki akawa anafika Dar, na ombi la
Pam. Ndipo Ibra akaona amtumie huyo mwanamziki kama kigezo. Wakati tupo njiani
kuelekea Dar, nilimpigia simu kaka kumsalimia.” “Waziri Msindai!?” Jack
akacheka jinsi Sabrina alivyoshangaa. “Nina kaka mmoja tu Brina. Huyo huyo.”
Wakacheka. “Basi, nikamwambia nitakuwa Dar, nakwenda kwa huyo mwanamziki,
nitakuwa na kina Ibra. Akasema na wao watakwenda kwenye tamasha na mkewe, la
huyohuyo mwanamziki, wana VIP tiketi. Nikamwambia kama anaweza kutufanyia mpango
na sisi tukapata tiketi angalau viti karibu na vya mbele kama VIP tutakosa.
Akasema ataulizia, kisha atatujulisha.”
“Sasa
siku ile ya ijumaa nakupigia simu kukutaarifu kuwa tumefika salama, tunajiandaa
kwenda kula, kaka naye akapiga kutuambia amepata tiketi nne tu za VIP, akaniambia
kama nataka anipitishie hotelini au kesho anipe tukikutana nyumbani. Maana
tulikuwa na miahadi wote tukutane kwa wazazi siku ya jumamosi asubuhi. Sasa
mimi namjua kaka, moyo wake wakugawagawa, nikajua anaweza kukutana na mtu,
akampa zile tiketi. Nikamwambia anipitishie tu pale hotelini ijumaa ile ile.
Akakubali.”
“Sasa
alipofika pale si ndio akamkuta Pam. Akaanza kucheka sana. Maana anamjua Phina.”
“Yule mpenzi wako wa chuo?” Jack akacheka. “Huyo huyo, nilimuomba amsaidie
kumuunganisha na marafiki zake wampe kazi Dar. Maana Phina alisema hataki
kutoka nje ya Dar. Sasa kaka akaanza kunitania kuwa, nimeamua ku upgrade.
Kutoka kwa Phina, nikamtafuta mrembo Pam. Hatujakaa sawa, May msichana wa Ibra,
Ibra mwenyewe, Ney na Felix wakaja. Kaka akawatania na wao wakawa wanacheka tu.
Ndio akawaambia kwa nini wanataka kwenda kula mbali wakati kwenye ile hoteli
napo panauzwa chakula! Ney akamwambia tunakimbia bei. Basi kaka akasema tukae
tule, yeye atalipa kwa furaha ya kuletewa shemeji.” Sabrina akamuona anacheka
kwa kusikitika.
“Nilishindwa
kuvumilia Sabrina, palepale mbele ya kila mtu, nikajikuta nimeropoka. Mpaka
baadaye nilimuomba Pam msamaha.” “Uliropoka nini!?” Sabrina akauliza akiwa
hajaelewa. “Nilisema Pam sio mke wangu, ni rafiki tu wa starehe, mke wangu
ananisubiri nyumbani.” “Jack!” “Kweli tena. Sasa kaka akashangaa. Akaniuliza
uhuni nimeanza lini? Kuwa na wanawake wawili! Hapo nikawa nimejichanganya sasa.
Kila mtu ananitizama kuona natoa maelezo gani. Kaka akawa mkali haswa,
akaniambi wazazi wananiamini sana. Na popote nilipo nawakilisha familia nzima,
ya Msindai. Kwa nini naishi maisha kama mnyama? Ndipo nikamuomba tuzungumze
sasa. Ukumbuke hapo nishatibua hali ya hewa, kila mmoja amebaki akiniangalia
mimi.”
“Nikawaambia
Sabrina yupo nyumbani kwangu. Nikawaambia umekubali kuhamia Singida kwa ajili
yangu. Nikawaeleza kuwa nilikufuata Moshi, sasa hivi tunaishi wote. Nikamwambia
kaka, nimekuwa nikikusubiri tokea chuo. Ndio Ney na na Felix wakanisaidia
kumueleza kuwa tokea nipo na Phina, wewe ulikuwepo kwenye moyo wangu hata Phina
anajua hilo.” Sabrina akashangaa sana. Lakini pia akajiuliza kwa nini katika
huo utetezi, Ibra kama rafiki wa karibu wa Jack yeye asimtetee kwa kaka yake!
Lakini akaona anyamaze aendelee kusikiliza kilichoendelea huko jijini.
“Hao
wawili wakamwambia kaka mengi wakimuaminisha, tena yatokea chuoni. Ndipo kaka
akauliza sasa kwa nini awepo Phina na huyo Pam kama wewe ulikuwepo tokea
zamani? Au tamaa! Kaka akidhani nitamaa. Ndio mimi mwenyewe nikamwambia nilikupenda
ukiwa kwenye mahusiano. Kwa hiyo ulinikataa. Na sasa unaishi kwangu sio kama
mpenzi, lakini kama rafiki. Ndio kaka sasa akasema lazima nikwambia tena. Na
safari hii lazima niende umbali mrefu zaidi nikuonyeshe nia ya kuwa na wewe
kwenye maisha, nifunge hilo jambo sio nionekane mahotelini na msichana huyu,
kesho naonekana nimeoa mwingine. Akasema sio sawa kwangu na kwa Pam pia.
Akanikumbusha ndoto nilizonazo, ninapokwenda na nilipo. Akaniambia kosa
nitakalofanya sasa hivi nikiwa sijulikani, watu hawatajali. Lakini siku
nitakapokuwa kiongozi mkubwa, yote hayo yatanifuata, na yatakuwa mwiba mbaya
sana.”
“Huwezi
amini Sabrina, akahakikisha naondoka pale hotelini, narudi kulala nyumbani
kwake baada yakupata muda wa pembeni kuzungumza na Pam.” “Jack!” Sabrina
akashangaa. “Kweli sikudanganyi. Wewe ushasikia skendo yake yule hata moja?”
“Hata mara moja!” Sabrina akaungana naye. “Basi yule yupo kama mtumzima, mama
anasema tokea mdogo alikuwa hivyohivyo. Na huo usemi wake wa popote nilipo
nawakilisha familia nzima, ni wosia wake ambao haachi kunikumbusha. Aliniambia
nimuage Pam vizuri na kwa amani, niondoke naye.” “Sasa Pam hakulia?” Sabrina
akauliza, Jack akacheka.
“Pam!”
Akawa kama anamfikiria. “Yaani palepale akasema hata yeye alijua sitamuoa. Sisi
hatuendani kabisa.” Wote wakacheka. “Hata pale walicheka. Akasema yeye anazijua
akili zake, haziendani na zangu kabisa. Akatuchekesha hapo, lakini akaomba
tusimfukuze pale, akasema yeye Dar hapajui. Kaka akamwambia hatuwezi kumuacha
hapo, atalala, na kesho kwenye tamasha tutaenda kumchukua. Akaniuliza kama
anaruhusiwa kunywa, nikamwambia lakini asizidishe.” Sabrina akacheka sana.
“Yaani Pam!” “Anapokwambia hapendi kumuudhi mtu, basi ndio akili yake ilivyo.
Wakati naondoka na kaka nikamuomba Ibra wasimuache pale peke yake. Maana wote
wanamjua Pam akilewa. Nikawaomba wakiwa wanaondoka, wahakikishe wanamfungia
kabisa chumbani.” “Jack! Kwa nini?” “Wewe si utakaa hapa Singida, utasikia
habari za Pam. Akilewa huwa akili haifanyi kazi kabisa. Anaweza hata kuvua nguo
mbele za watu.” Sabrina akashika mdomo.
“Sikutanii.
Hivi unafikiri kwa nini namkataza kunywa pombe hovyo? Ni kwa ajili hiyo. Na
anapenda bia, kuliko nitakavyokwambia! Ukitaka mpatane, mpe bia. Na mbaya, huwa
hakumbuki anayofanya akiwa amelewa, pombe ikiisha utamuonea huruma. Ila
niliupenda moyo wake. Basi, kesho yake siku ya jumamosi kaka ndio
akanisindikiza kununua hiyo pete akaniambia nije nizungumze na wewe, ukikubali,
ndipo niwaambie wazazi. Basi, tukahangaika kweli kutafuta pete nzuri. Usiione
hivyo hiyo, ni garama haswa. Hivi hapa ananidai, amesema nitamlipa taratibu.
Lakini nimemwambia mwishoni mwa hii week nitamtumia pesa yake. Sasa kwa heshima
yake ndio wakakubali hata kupunguza ukubwa, ilikuwa kubwa zaidi ya hapo.”
Akamuona Sabrina amepotelea mawazoni.
“Nini
tena?” “Anajua kama mimi nina mimba isiyo yako?” Sabrina akauliza kwa unyonge.
“Ilibidi kumwambia Sabrina. Nikasema asije kuhangaika vyote hivyo, halafu akaja
kujua baadaye, akanilaumu.” “Sasa akasemaje?” Jack akacheka kidogo kama
anayefikiria. “Yule mtu amejaliwa hekima Sabrina, mimi mpaka nikashangaa. Yeye
aliniambia hivi, ‘chakuokota, si chakuiba. Mwenye mali, ndio mjinga’.”
Sabrina akashangaa mpaka akakaa. “Jack!” “Kweli tena. Akasema mtoto yeyote
anayezaliwa ndani ya ndoa, ni wawanandoa. Mengine anajua mama. Akanichekesha
kile kipindi cha mambo ya DNA, akasema ambao hawakufikiria walikimbilia kupima
watoto waliokuwepo nao ndani ya ndoa wakilea kama wao, wakavunja ndoa zao,
wakakosa na warithi. Wenye hekima, wakanyamaza na watoto wao. Akaniuliza, mimi
najuaje kama nina kizazi? Nikanyamaza. Akaniambia hata kama Mungu atanijalia
watoto wangu mwenyewe, akaniambia naweza kuja kukuta huyu mtoto ndiye akanifaa
kuliko mtoto wangu mwenyewe. Akaniambia baba hakatai mtoto.” Mpaka Sabrina
akajisikia machozi yakimtoka.
“Alinitia
moyo, mpaka nikajisikia vizuri. Akasema ni baraka wala nisiogope. Mungu atanipa
hekima juu ya hili, ilimradi tu niwe nakupenda kwa dhati. Mengine nisiogope.
Nilijisikia furaha sana Brina. Maana alinipongeza na akaniambia kweli wewe
utakuwa mwanamke ninayekupenda, vinginevyo nisingekuchukua na hali hiyo. Basi,
jumapili tukampitia Pam hotelini, akaturudisha uwanja wa ndege.” Sabrina
akabaki ameinamia magoti. “Kwa hiyo harusi si ipo, mama?” “Ipo Jack. Wala sijivungi. Mungu anipe nini tena? Hata
kesho wewe nioe tu. Sitakuja kupata mtu anayenipenda hivi. Nioe tu Jack. Mimi
nitataka harusi tu. Tena ndogo, wala si kubwa yakutumia mamilioni ya pesa
wakati tuna shida na pesa. Na sitaki mambo ya sendoff wala kichen party.”
Jack akambusu.
“Naomba
nikumbatie kabisa, ili niamini kama kweli nipo mikononi mwako, wewe Jackson.”
Jack akacheka. “Hujui ni kiasi gani najisikia salama na wewe Jack.” “Nakupenda
Brina. Nakupenda sana. Njoo.” Sabrina akaona atajipunja. Akasimama kwa haraka,
akatoa nguo zote Jack akimwangalia kisha akaenda kumkalia Jack akiwa na yeye
hana nguo ya juu ila boxer aliyoivaa asubuhi hiyo alipoamka. “Nikumbatie
kabisa, nipate mwili wako mwilini mwangu.” Jack akacheka asiamini. “Napenda
matiti yako Brina! Unakifua kizuri sana!” “Nikumbatie kwanza nitulie, nitakupa
yote. Nitakunyonyesha huku nikikufurahisha. Ila nataka unikumbatie kwanza.”
Jack aliposikia hivyo, akatoa nguo ya chini kwa haraka, akajirudisha kitandani
na kumpokea Sabrina kwa mikono yote miwili.
Sabrina
anamkalia miguu akaikutanisha nyuma ya mgongo wa Jack. Jackson alishakuwa
amesimamisha. Akaona hatakaa vizuri. Yeye mwenyewe Sabrina akamlainisha kwanza
Jack kwa midomo yake, alipoona akijiingizia hataumia, ndipo akarudi kumkalia
vizuri akiwa anajipenyezesha taratibu. Jack akataka kuanza. “Tulia bwana Jack
unikumbatie kwanza.” “Hata nisisogee kidogo!” “Hapana bwana. Mimi nimekuweka
sawa ili niweze kukaa vizuri.” “Nitakukumbatia baadaye. Hivyo unavyonibana
huko, siwezi nikakaa tu nikatulia.” “Ningejua nisinge…” “Wewe mwenyewe
umeninyonya sana halafu unanibana! Malizia vyote ulivyoniahidi kwanza. Niwekee
hilo ziwa moja mdomoni, niruhusu nikushike ninakotaka, nitulize kwanza ndio
nitaweza kukumbatia vizuri. Sasa hivi ushanichanganya.” Sabrina akaanza kucheka
taratibu na kurudi shingoni kwake, akaanza kunyonya shingo yake. Alipofika
masikioni na kuweka ulimi hapo, uzalendo ukamshinda Jack akaanza kuhangaika
hajui ashike wapi. Sabrina akajirudisha nyuma taratibu, akamuwekea titi mdomoni
huku akimsaidia na yeye kwa kujinyanyua juu na chini akikata kiuno.
Jack
akasahau kama mwenzie ni mjamzito, akaanza kuvuta matiti kama mtoto mwenye
njaa, Sabrina akatulia tu akijua hakuna jinsi atamwambia apunguze kunyonya
anamuumiza, akaelewa kwa wakati huo. Lakini kwa kuwa alishamgundua hajiwezi
akishikwa masikioni, akaona amfupishie safari. Akamuwekea vidole masikioni
akimchezea, Jack akasalimu amri bila kuchelewa. “Usingenishika tena masikioni
bwana Brina! Umenikatisha!” Jack akalalamika, Sabrina akamcheka. “Ulikuwa ukiniumiza
matiti. Unatumia nguvu nyingi kuyanyonya, mwenzio naumia. Yameanza kujaa.”
“Samahani nimeshindwa kuwa mstaarabu, sitarudi...” “Hapana bwana hata mimi
napenda. Wewe furahia ila taratibu.” Wakacheka. Sabrina akataka kuondoka, Jack
akamuwahi kwa kumvutia chini asinyanyuke. “Usiondoke bwana. Niache nitulie nikiwa
hukohuko ndani. Unajinsi yako unanibana, nasikia raha.” Sabrina akajiweka sawa
akicheka. Jack akaweka mto nyuma yake vizuri, akamkumbatia akiwa ameegemeza
mgongo ukutani, Sabrina amemlalia begani, akimnusa shingoni. Wakatulia kwa muda. Jack akakumbuka kaka yake
anasubiria jibu.
Jack kwa kaka yake.
J |
ack
akachukua simu yake hapohapo na kumpigia kaka yake. “Amesema ‘ndiyo’.” Sabrina akamsikia anaongea bila hata salamu. “Nilijua umekataliwa dogo. Kimya cha jana siku nzima!” Akawasikia
wote wanacheka. “Sikumkuta nyumbani. Alikwenda kanisani
na huyu dogo ninayeishi naye hapa, nilikwenda kuwafuata usiku.” “Hongera sana.
Sasa harusi lini?” Kaka yake
akampongeza na kumuuliza. “Sijui kama itawezekana kaka.
Nilitamani tufunge ndoa kabla hajajifungua. Amebakisha miezi mitano tu!”
Kimya. “Unafikiri haitawezekana?” Jack akauliza
kwa wasiwasi.
“Hakuna kitakachoshindika ikiwepo pesa. Kwani mnataka harusi ya
namna gani?” Kaka yake akamuuliza. “Tunataka harusi ndogo sana. Ndugu tu na marafiki wa karibu.
Brina hataki hata sendoff. Harusi tu. Kwa hiyo ni swala la mahari, na hiyo
harusi.” “Basi wapigie wazazi simu. Wakusikie wewe mwenyewe kuwa unataka kuoa,
kisha mimi nitamfuata baba na mama, tupange. Halafu tutakwambia.” Jack
akafurahi sana na kumshukuru sana kaka yake. “Pongezi
bwana. Angalau unaongeza kitu kwenye maisha, sio unabaki unazagaa mtaani huna
familia!” Wakataniana kidogo, wakaagana, Jack akiwa na tumaini.
~~~~~~~~~~~~~~~~~~
“Huyu
akishika jambo lako, ujue atakamilisha tu. Sasa kazi kwako Brina. Usiniangushe
tena.” “Mimi nipo hapa na wewe Jack.” Jack akacheka. “Namaanisha kwenu. Sisi
kwetu naona ishakuwa mteremko.” “Mbona utanioa tu Jack! Wapende wasipende, mimi
naolewa na wewe.” “Kweli Brina? Wakiweka kipingamizi?” “Acha kunitania Jack!
Kwani wao wanajua sasa hivi nilipo au hata ninachokifanya? Wanikatalie kwa
sababu ipi? Hakika sitajali vipingamizi vyao. Utanioa tu, wala kwa hilo
lisikutie shaka labda wewe mwenyewe ubadili mawazo.” Jack akaanza tena
kumpapasa.
“We
Jack! Utachelewa kazini bwana!” “Hakika leo siendi. Watanisamehe tu.
Nilivyokuwa na hamu na wewe!” Sabrina akacheka sana akifurahia. “Kwa hiyo
tunabaki wote?” “Siku nzima mimi na wewe tu.” Sabrina akasikika akizidi kucheka
kwa furaha wazi alisikika na kicheko cha kutoka moyoni. Wakatoka kwenda kuoga.
Wakapata penzi jingine tena na tena wakilipiziana kuwa nimekufanikishia safari ile,
mimi sijapata kitu, wakicheka na kurudia bila kuchoka kwa uhuru wote wakijua Emma
hayupo, nyumba nzima wako peke yao, hakuna wakuwaingilia.
Sabrina Kwa
Familia Yake.
I |
lipofika mchana,
Sabrina akaamua kumtafuta kwanza Sabina. Alikuwa amejilaza miguuuni kwa Jack,
akimchezea maziwa. “Wewe mtoto umepotelea wapi? Maana
ulikuwa ukitafutwa na Lela karibu kuchanganyikiwa.” “Sitaki kusikia habari za
kina Lela kabisa. Nishamalizana nao hao. Ila kwa sasa nipo Singida na sitaki
uwaambie. Sitaki kufuatwa nyuma. Nilichokupigia ni kukutaarifu kuwa naolewa.”
Kimya kama aliyepatwa na mshituko. “Unanisikiliza?”
Sabrina akauliza. “Nipo, nawafikiria wazazi wako
watakachosema. Habari wanayotaka kusikia kutoka kwako ni shule. Angalau
ungerudi na habari ya kusema ulipata kazi, ukarudi shule, hapo mtaelewana. Wewe
una diploma hata maisha yako hayaeleweki unakimbilia ndoa! Una...” “Samahani
Sabina. Samahani sana dada yangu.” Sabrina akamkatisha kwa hasira na
kukaa kabisa, mkono wa Jack ukatolewa kwenye ziwa alilokuwa akichezea.
“Wewe unajua sasa hivi nipo wapi na ninafanya nini? Unajua naolewa
na nani? Unajua nipo kwenye hali gani?” “Si wewe mwenyewe umejificha!” “Hata
wakati nipo hapo Dar na nyumbani, ulikuwa ukinitafuta mimi kama mdogo wako
kunisaidia au hata kunijulia hali wakati ulijua nipo kwenye shida?” “Sasa
ulitaka nifanye nini?” Sabina akauliza kwa ukali. “Sasa kama hujui chakufanya kwenye maisha yangu, nisikilize
mimi ninayejua chakufanya. Wewe umesoma, ndio mtoto mzuri hapo nyumbani ridhika
hivyo. Nimekupigia kwa heshima tu nikijua wewe ni dada yangu nikidhani
utafurahia pamoja na mimi! Lakini..” “Wewe Sabrina, mimi nakwambia wazazi wako
watakachosema.” “Sijali.” Sabrina akajibu kwa ukali Jack akimsikiliza.
“Hapa sijapiga simu kuomba ushauri. Naomba hata na wewe uelewe. Na
ukiweza naomba umwambie na baba na mama, angalau kwa mara ya kwanza kwenye
maisha yangu, wanyamaze wasiniambie vile wanavyojisikia juu yangu. Washaongea
sana na kunitukana kwa kurudia rudia. Waambie sijasahau, nakumbuka. Ninachotaka
nikuwapa heshima kama wazazi. Wakwe wanataka kuja kutoa mahari. Kama wapo
tayari kupokea mahari yangu mimi kama mtoto wao, nitashukuru. Wakikataa, basi. Waambie
lakini mimi naolewa baada ya miezi miwili kuanzia sasa.”
Sabina kimya.
“Sijui kama unanisikiliza?” “Nakusikiliza Sabrina. Lakini mimi sio
kwamba sijakufurahia.” “Basi kama umenifurahia, naomba usimame na mimi katika
hili. Angalau mara moja tu kwenye maisha yangu. Hili ni muhimu sana kwangu.
Linaweza lisilete maana kwenu, lakini kwangu linamaana sana. Sasa kwa nini
nimekupigia wewe kwanza simu?” “Umekuwa mkali Sabrina!” “Nimechoka dada.
Nimechoka kudharauliwa na kunyanyaswa kwa maneno machungu. Inakuwa kila mtu
anajua ni nini
nahitajika kufanya! Nini natakiwa kufikiri na ni nini natakiwa kujisikia
isipokuwa mimi mwenyewe! Nahisi ninahaki na mimi yakupendwa na kuthaminiwa kama
wanadamu wengine. Sasa nimepata mtu wangu, mnataka tena kuniwekea vikwazo!
Hapana jamani.” Sabrina akawa mkali haswa.
“Ulitaka mimi nifanye nini?” Akamsikia
Sabina ametulia. “Kwa kuwa wewe huwa wanakuheshimu
sana. Wanakupenda na lolote ukizungumza huwa wanakuelewa, naomba nisaidie kuwafikishia
huu ujumbe kwanza kuwa naolewa. Ili mimi mwenyewe baadaye nitakapowapigia simu kuwataarifu
waweze kuelewa nini nazungumzia. Maana kwao mimi nakuwa kama nazungumza nao
kichina, huwa hawanielewagi. Kwanza hawajawahi kuwa tayari kunisikiliza, wakati
wote wanataka niwe nawasikiliza tu wao. Ndio maana nimekupigia wewe simu,
uwaambie ambacho ningeweza kuwaambia mwenyewe, lakini najua kwa hakika
hawataelewa kwa kuwa huwa hawanielewagi.” Sabrina akaendelea.
“Kwa hiyo da Sabina, naomba ujue hili na uwataarifu kuwa, NAOLEWA.”
“Nimeelewa Sabrina! Na mimi nitampigia baba simu kumwambia, nimsikie.” “Sawa.
Lakini waambie nitasikitika kuwakosa kwenye harusi yangu kama watakataa, lakini
mimi naolewa.” Akamsikia Sabina anacheka. “Sasa unacheka nini?” “Ungeanza ukali huo tokea zamani, wangekuheshimu.”
Ikabidi Sabrina acheke tu.
Wakataniana
kidogo. “Sasa hii ndio namba yangu mpya, ukitaka
kuwasiliana na mimi juu ya hili, unaweza kunipigia.” “Sasa mbona hata shemeji
mwenyewe hujaniambia jina?” Sabrina akaanza kucheka. “Unataka kumsalimia?” “Kumbe yupo hapo!?” “Ndiyo! Kwani
vipi?” “Mama wewe umekuwa mkali! Mimi nimeuliza tu! Naomba nimsalimie shemeji.”
Sabrina akamgeukia Jack aliyekuwa akimpapasa taratibu mgongoni baada ya mkono
kutoka ziwani. “Sabina anataka kukusalimia.” “Hamna shida.” Jack akapokea simu.
“Halow!” Akaanza Jack. “Halow,
naitwa Sabina. Dada yake Sabrina. Sijui kama amekutambulisha kama kuna dada au
imekuwa harakahara hata hufahamu ndugu!” Jack akacheka kidogo, akielewa
anachomaanisha. Hao ndugu aliwafahamu kwa kuwasikia kwa muda mrefu sana. “Nakufahamu kwa zaidi ya miaka mitatu sasa, sema
hatukubahatika kukutana tu, lakini nawafahamu ndugu wote wa Sabrina. Kuanzia
wewe Sabina dada mkubwa, Seba ambaye yupo katikati yako na Sabrina, halafu
wadogo zenu wa mwisho wa kiume. Sethi na Simon.” Sabina akashangaa sana.
“Haiwezekani! Kumbe mnafahamiana kwa muda mrefu hivyo!
Ndio unaitwa nani!?” Sabina akaonekana kushangaa sana. “Jackson.” “Hamna jina la pili?” Jack akacheka kidogo.
“Jackson Msindai.” Pakazuka ukimya. Jack naye
akanyamaza akijua ameshituka kusikia Msindai.
“Unamaanisha Msindai! Msindai! Msindai waziri!?” “Hapana. Mimi ni Msindai
Jackson.” Jack akajibu akicheka taratibu
kiungwana. “Nimeelewa. Lakini Namaanisha kwani
hamfahamiani na waziri Msindai?” “Yeye ni kaka mkubwa, mimi ndio wa mwisho
kwenye familia.” “Acha masihara! Kwahiyo Sabrina anaolewa na Msindai au
sijaelewa vizuri?” “Mimi Jackson ndiye namuoa Sabrina.” Sabina akaanza
kucheka, wazi alisikika kubabaika.
“Ndio maana mnajeuri yakufanya harusi ya haraka! Mama yako si ndio
alikuwa waziri wa afya awamu ya Mkapa?” Jackson akacheka
kiuungwana tu na kukubali. “Ndiyo. Nikurudishe kwa
Sabrina?” “Subiri nishangae kidogo bwana! Kwani mnaharaka ya kwenda wapi
jamani! Mimi nataka kukufahamu zaidi. Au kuna tatizo?” “Hamna shida. Karibu.”
Jack akakubali. “Kwa hiyo mmefahamiana na Sabrina kwa
miaka mingapi?” “Mitano sasa. Hatujakukurupuka tu. Namuoa mtu ninayemfahamu
vizuri sana.” Jack akajibu kwa uhakika mpaka Sabrina akamgeukia.
“Kwa hiyo muda wote huo mlikuwa kwenye mahusiano na Sabrina?” “Nililo
nauhakika nalo, ni mapenzi yangu kwake kwa muda wote huo. Maana tulipokuwa
chuoni nilimuomba mahusiano, akanikataa. Lakini bado nilikuwa na matumaini.
Aliondoka na kuniacha chuoni, lakini tukaendela na mawasiliano. Kwa hiyo
nimekuwa nikimsubiri anikubali ili tu nimuoe yeye Sabrina. Kwa kuwa kwa hakika
nilijua moyoni, Sabrina ndiye mke wangu. Ukiniuliza kivipi, mimi mwenyewe
sikuwa nikijua, lakini kwa miaka yote nilikuwa nikisubiri mke wangu, ambaye ni
Sabrina. Kwa hiyo kwa mara nyingine
tena, jana ndipo nimemuomba aje awe mke wangu, kwa mara ya kwanza amekubali na ndio
maana sitaki tena kusubiri. Nataka nimalize kabisa, nijue natulia, Sabrina akiwa
mke wangu mimi.” Mpaka Sabina ikamgusa.
“Kweli simfahamu Sabrina! Au niseme yupo sahihi. Tumekuwa kama
tumemtelekeza. Amekuwa kwenye maisha yetu, lakini sisi tumeshindwa kuwa kwenye
maisha yake!” Kimya. Jack hakutaka hata kuongeza
hapo. “Haya Jack. Nimefurahi kukufahamu zaidi ya jina.
Angalau tumeongea kidogo nimeelewa sio kwamba Sabrina amekurupuka tu. Anaolewa
na mtu anayemfahamu na kumpenda. Kwa hiyo hata nikizungumza na wazazi, nakuwa
na kitu chakuongea zaidi.” “Nitashukuru ukiturahisishia, na kukuona kwenye
harusi yetu.” “Oooh lazima. Najua huko
nitakutana na wakubwa wa hii nchi.” Ikamuumiza kidogo Jack kuona lengo
si kuja kujumuika na mdogo wake ila kukutana na watu wengine! “Na Sabrina atakuwepo kama mlengwa mkuu na sababu yakutukutanisha
wote.” Jack akaongeza taratibu tu na kumfanya Sabrina ajisikie vizuri. Sabina
akacheka. “Kweli naona unampenda Sabrina! Nawatakia
kila la kheri. Nitawataarifu kile wazazi watazungumza.” “Asante sana.” Jack akashukuru na kukata simu.
Sabina Kwa
Wazazi.
S |
abina akabaki
ameshikilia simu, haamini! Ikabidi kuanza kutafuta habari za familia kiyo ya Msindai
kwa haraka mpaka akazipata kwa kina. Ndipo akampigia baba yake simu baada ya
kumpata kaka mkubwa, yaani anayemfata huyo Sabina ndio Sabrina. “Upo na mama?” “Yupo karibu. Kwani vipi?” Baba yake
akauliza. “Naomba mkae karibu muweke simu kwenye spika,
hapa nipo na Seba kwenye line pia.” Wakashituka. “Kwema?” Baba yake akauliza kwa wasiwasi. “Ushaweka
kwenye spika, mama anasikia?” Sabina akauliza. “Nipo.
Kwema?” Akauliza mama yao. “Kwanza shikamooni?”
Na Seba naye kaka yake Sabrina akasalimia. Wazazi wakaitika. “Kuna nini!?” “Mnawafahamu kina Msindai?” Akauliza
Sabina. “Yule ambaye mama alikuwa waziri wa afya? Baba
daktari wa watoto wa muda mrefu sana alikuwa pale hospitali ya taifa Muhimbili?
Nafikiri amefungua hospitali yake sasa hivi yule mzee, au sijui!” Baba yao
akawa kama anajaribu kuwatambua. “Au unamzungumzia huyu
wa sasahivi?” Akauliza Seba.
“Ewaa! Naona wote mnawajua. Yule aliyekuwa waziri wa afya awamu ya
Mkapa, ni mama na huyu waziri wa sasa hivi ndiye mtoto wake wakwanza. Anao watoto
wa nne. Imebidi kuanza kutafuta habari zao.” “Kwa nini?”
Akauliza mama mtu. “Subiri kwanza mama. Sasa mtoto wao
mkubwa au wa kwanza ndio huyo waziri, wanafuata wakike wawili, mmoja anayemfuata
huyo waziri huyo dada mkubwa wa kike yeye yupo Usalama wa taifa pale, ndio
nasikia ndio mkubwa wao pale. Halafu anayemfuata tena huyo wakike wa pili
nasikia ni daktari pia wa watoto, anafanya hapohapo Muhimbili na kwenye
hospitali ya familia. Halafu wanaye mtoto wa mwisho au mdogo wao anaitwa
Jackson, yeye anafanya wizara ya fedha, kama muhasibu Singida mjini.” “Ni
familia iliyoendelea sana!” Akasifia baba yake.
“Wewe mbona unawafahamu sana hivyo!? Kuna nini?”
Mama yake akazidi kudodosa. “Imebidi kutafuta habari
zao kwa haraka. Maana Sabrina kanipigia simu muda si mrefu akiwa na huyo
Jackson. Wanafunga ndoa ndani ya miezi miwili kuanzia sasa, tarehe wamesema watatujulisha.”
Pakazuka ukimya wa hali ya juu. “Sasa huo mshangao mimi
ikabidi kumuhoji sana huyo Jackson Msindai.” “Umezungumza naye huyo mtoto wa
Msindai!?” Akauliza baba mtu kwa mshangao sana.
“Ndiyo. Sasa si ndio maana ikabidi kuanza kutafuta habari za hiyo
familia vizuri ili kujua kama ni kweli au utapeli tu. Ndio nikaambiwa ni kweli
hiyo familia kijana wao wa mwisho yupo Singida, anaitwa Jackson.” “Makubwa!”
Mama mtu akahamaki. “Wala si madogo. Nikamuuliza huyo
Jack juu yake na Sabrina. Akasema walikutana chuoni. Akamtongoza Sabrina,
Sabrina akamkataa. Lakini baadaye wakarudi kwenye mahusiano yakawaida. Anasema
Sabrina yeye alimwacha chuoni, lakini wakaendelea kuwasiliana. Anatufahamu sisi
wote mpaka kwa majina yetu! Tena kwa muda mrefu tu. Anasema lakini yeye alijua
Sabrina ndiye mke wake, akawa anaendelea kumsubiri. Jana, siku ya jumapili
anasema akamjaribisha tena kumuomba safari hii sio tu mahusiano, ni kumtaka aje
awe mkewe. Anasema kwa mara ya kwanza Sabrina amemkubali. Hivi amemvalisha pete
ya uchumba. Na amesema hasubiri tena. Alichokuwa akisubiri ni Sabrina kukubali.
Maadamu Sabrina ameshamkubali, wanaoana kwa haraka sana.” “Hawana sababu yakusubiri, si pesa ipo!” Akaongeza
Seba. Wazazi kimya wapo kwenye kutoamini.
“Alichosema Sabrina, anachoomba kutoka kwenu ni mpokee mahari yake.
Mseme lini mtakuwa tayari, waje hao kina Msindai kutoa mahari. Mimi nikamwambia
mnaweza kukataa kwa sababu mnataka...” “Hee! Wewe Sabina vipi?”
Mama yake akashangaa sana kwa kuhamaki. “Subiri kwanza
mama. Maana ni juzi tu ulikuwa ukimlalamikia Sabrina na maisha yake mabovu
ukitaka arudi shule angalau asomee ualimu. Ndio nikamwambia labda mnaweza
kukataa. Hapo nilikuwa sijajua kama anaolewa na kina Msindai.” Wote
wakacheka sana.
“Kumbe! Nyinyi mngekubali alete mchovu kama yeye!?”
Wote wakazidi kucheka. “Lakini bwana Sabrina
amebadilika! Sio yule mnayemfahamu nyinyi. Amenijibu kwa wazi kabisa, yeye
hajapiga wala hatawapigia kuomba ruhusa. Nikututaarifu tu. Kwa heshima anataka
asipite kipengele cha mahari. Lakini amesema, sisi tuwepo, tusiwepo. Tukubali,
tukatae, yeye anaolewa. Tena kwa ukali kabisa kama asiyejali tena.” “Makubwa! Sasa na sisi atatupigia lini simu atuambie au ndio
ametukasirikia kwa kuwa hatumpigii simu kama tunavyokupigia wewe?” Sabina
alishawaambia malalamiko ya Sabrina. Wakayapuuza. Lakini sasa hivi mambo
yamebadilika. Sabrina anaolewa na kina Msindai.
“Maana sisi ni wazazi. Hata kama tulikosea, bado anatakiwa atupigie
sisi simu atuambie yeye mwenyewe.” Akaongea
kwa kulalamika baba yao. “Amesema atawapigia, lakini
alisema anataka mimi ambaye mnanielewa kwa haraka na mnanisikiliza ndio nianze
kwanza.” Pakazuka ukimya. “Sasa mnasemaje?”
“Ndio atupigie yeye mwenyewe.” Akaanza kibabe baba yao. “Yeye atupigie sisi simu, atutaarifu mwenyewe. Hiyo ndio
heshima” “Sawa baba, lakini nataka tu kuwatahadharisha. Sabrina anao mtazamo
wake juu yenu. Anajua nini mtazungumza na anajua huwa hamumsikilizi na hamjali
anachojisikia.” Sabina akaanza taratibu tu.
“Nilizungumza naye alipokuja hapa kwangu, na leo nimemsikiliza
kwenye mazungumzo yake. Tabia yakumkosoa na kumsema vibaya hata mbele yakina Simon,
ambao anaona ni wadogo sana kwake, inamuuma sana. Anajua wazi kuwa huwa hatumfuatilizi,
nyinyi kama wazazi mnamdharau na bado anao ule usemi uliokuwa ukimwambia mama.”
“Usemi gani? Kama sio ananitafutia tu sababu!” Akakana
mama yao bila hata kujua ni usemi gani yeye kama mama aliokuwa akiusema na
kumuumiza mwanae huyo, Sabrina. “Vile ulivyokuwa
ukisema yeye ni fungu la kukosa.” “Halafu
nilikukataza mama. Sijui kama uliacha! Hata mimi alinilalamikia na kusema
ilibidi mpaka aende akaombewe ili kutoa hilo jina kwenye maisha yake.”
Seba kaka yao akaingilia. “Mimi nilishaacha. Kama
anashindwa kusamehe ni yeye tu.” Mama mtu akazungumza kwa jazba.
“Hapana mama. Naomba katika hili kama mnamtaka Sabrina arudi kwenye
maisha yenu, mjishushe. Ameondoka zaidi ya miezi minne sasa, na wala
haonekaniki kutaka kurudi nyumbani, bado anamalalamiko na nyinyi. Ameniambia
kwa ukali kabisa, amechoka kutukanwa na kunyanyaswa. Wote tumekuwa tukidharau alichokisoma,
lakini ndio kinampa mume! Tena huyo kijana anaonekana anampenda na kumthamini sana
Sabrina.” Kimya.
“Binafsi nimejisikia vibaya sana mbele ya huyo kijana. Anatufahamu
sisi wote mpaka Simon, lakini mimi kama dada yake Sabrina, simfahamu kabisa
wakati anasema amekuwa na Sabrina kwa miaka mitano! Hakika nimejisikia vibaya
na aibu. Hata yeye amejua Sabrina ni mtoto kwenye familia ambayo yupo mpweke.
Anasema amechelewa kuoa kwa kuwa alikuwa akimsubiria Sabrina. Anasema anaoa
mwanamke anayemfahamu na kumpenda. Sasa kazi kwenu. Mnaweza kuwa wageni kwenye
harusi ya mtoto wenu au walengwa. Mimi nimefikisha ujumbe, mtoto wenu anaolewa
na mtu maarufu sana hapa nchini. Mjipange.” Sabina
akawaaga na kukata simu.
Wazazi
hao wawili wakabaki kimya kila mmoja akiwaza lake. Wamdhaniae ndiye, siye. “Sabrina!”
Wote ikawa haiwaingii akilini. “Msindai!” Bado haikuwa ikileta maana.
Kwa jinsi wanavyomuelewa Sabrina, lilikuwa jambo ambalo haliwezekani. Heri
ingekuwa Sabina! Sabina anakutana na wasomi wengi. Anasafiri nchi mbali mbali.
Anahudhuria mikutano ya wakubwa. Yaani Sabina ndiye angestahili kuolewa na watu
kama kina Msindai, lakini si Sabrina!
Kwa Kina
Msindai.
J |
ackson huyu,
ni mtoto wa mama haswa. Kiziwanda ambaye kabla hajaimaliza siku yake, basi
lazima amalize na mama yake pia. Hajawahi kukua kwake. Swala lakuuliza kama
amekula au amekumbuka kunywa maji siku hiyo lilikuwa jambo la kawaida sana.
Jumbe katikati ya siku akiambiwa na mama yake, ‘Jua kali
sana huko nje, kunywa maji sasa hivi kabla hujasahau.’ lilikuwa jambo la
kawaida. Kupigiwa simu kwa video ili amuone alivyopendeza siku hiyo kazini,
huku akimtaka arekebishe tai hivi au vile, lilikuwa jambo la kawaida sana tu. Hata
kazini walishamzoea kumsikia mama Msindai kwa njia ya simu akizungumza na huyo
mwanae. Jack mziwanda wa mama Msindai.
Akampigia
simu mama yake. “Nilikuwa nakuwaza sasa hivi.
Nimekununulia soksi nzuri sana, nimesahau kukupa juzi ulipokuja nyumbani.
Kwanza weka video nikuone.” “Nisikilize kwanza mama.” “Umepata mchumba?”
Akamtania asijue kama safari hii amepatia. “Ndiyo.”
Jinsi Jack alivyojibu, mama yake akajua ni kweli sio utani. Akanyamaza. “Mama, umenisikia?” “Usinitanie Jackson!” Jack akaanza
kucheka. “Kweli mama. Nataka kumuoa Sabrina.” “Wewe si
ulisema Sabrina amekwambia uendelee na maisha yako haji tena Singida!?”
Sabrina akashituka mpaka akakaa akiwa ametoa macho.
“Nipo naye hapa?” “Kwa nini alikataa kwa mara nyingine tena na kwa
nini sasa hivi amekubali?” Likawa swali zito na
la kumshitua zaidi Sabrina. Akaishiwa nguvu kabisa. “Jackson!?”
Wakamsikia mama yake akiita, tena si kwa utani. “Nakusikiliza
mama.” “Maana kama kumbukumbu zangu bado zipo sawa ni kama miezi minne tu
imepita, alipokwambia hatakuja Singida, uendelee na maisha yako. Au naongopa?”
“Ni kweli.” Jack akajibu akisikika kuishiwa nguvu. “Sasa kipi kimebadilika!?” Mama huyo, aliyeshika
wadhifa wa juu mpaka kuwa waziri, ameongoza madaktari bingwa wa nchi nzima,
muelewa mambo, akataka majibu ya kueleweka akilinda kiziwanda chake. Sabrina
hakujua kama Jackson ndio anazungumza na mama yake kila kitu! Na yeye akahisi
mwili unakufa ganzi, akasimama na kuondoka hapo kabisa kama kuwapa nafasi Jack
na mama yake.
~~~~~~~~~~~~~~~~~
Kila kazi, inamalipo yake. Kile
pando, lina mavuno yake.
Nini kitaendelea?
Mizani ya
Tino Ililemea kwake, akatoa muhanga mtoto na Sabrina. Sasa safari hii Jackson
Msindai. Atahimili joto ya jiwe?
Kila Baraka Ina Changamoto
zake na ni Ngazi ya Kupanda Maishani.
Wenye nguvu wanahimili, wanapanda kwa machozi na kuvuna
kwa shangwe. Wadhaifu huishia katikati wakiyumbishwa.
Simulizi ndio Inaendelea.
Usikose kufuatilia Mapenzi, Uzazi, Siasa, Ya nyuma na Yajayo mbeleni…
0 Comments:
Post a Comment