Naomi Simulizi |+1 205 767 8163 |naomisimulizi@gmail.com Makosa! – SEHEMU YA 7 - Naomi Simulizi

Makosa! – SEHEMU YA 7

 Kwa Sabrina.

H

uku kwa Sabrina mrembo hana habari! Anafurahia uhuru akijua akitoka hapo anarudi kwenye hoteli ya kitalii, iliyojaa na wazungu. Raha tu. Muda wa chakula ulipofika, akaagiza chips yai, virigisi na Fanta orange. Vikaletwa. Akaanza kula kwa raha zote. Akaendelea kusukwa hana habari yupo Tino ambaye ahemi bila yeye. Akala, akamaliza. Akaendelea kusukwa. Akaanza kusikiliza sasa yaliyojiri mtaani. Matajiri kwa masikini. Kinadada aliosikia hapo habari zao ni warembo na mashuhuri nchini, habari zao alizisikia nakuzijua siku hiyo. Akakumbukia enzi yupo jijini, alisikia mengi kwenye masaluni. Miaka mitatu akafungiwa kwao, kusuka kwa jirani, asante ndio malipo au pesa kidogo. Hana habari, akanogewa hapo. Kuja kumaliza ni saa 12 jioni. Ni kweli alipendeza hata yeye alijikubali. Ikabidi awape na ya soda kama shukurani. Akaondoka.

~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~

Wawili hao waligawana kadi za kufungulia chumba. Akachomoa yake, akiwa amejawa furaha, akajua Tino akimuona, atabaki ‘Waw!’  Asijue hali mbaya mwenzie aliyokuwa nayo tokea asubuhi wanaachana. Akachomeka kadi mlangoni, mlango ukafunguka, akaingia na mfuko uliojaa matunda aliyopitia soko la Mwenge njiani kurudi hotelini. Akasukuma mlango akaingia na mizigo yake, Tino amelala kwenye kochi. “Nimepata na matunda yako Tino.” Akaingia na kwenda kuweka kila kitu mezani akashangaa kimya. Akahisi amelala. Akamsogelea kwa kunyata, akamkuta amejilaza tu, lakini hajalala macho kwenye tv.

“Vipi Tino?” Kimya. Sabrina akakaa. “Mbona huniangalii! Kuna nini!?” “Sijabadilika Sabrina, mimi ni yuleyule Tino uliyemuacha mdomo umepinda, wakati mwingine nikizungumza mate yanatoka.” Sabrina akashangaa hayo yote yanatoka wapi! Akatulia kidogo akaona aulize tena labda atageuka. “Mambo yalikwenda vizuri pale polisi nilipokuacha?” Akauliza tena kwa upendo. “Na kweli uliniacha. Na baada ya kuniacha pale sikuona tena sababu. Nahangaika kwa ajili ya nini? Hebu niangalie hivi nilivyo. Hata nikipata ile nyumba yote na pesa yote ile nikiachwa peke yangu itanisaidia nini mlemavu, watu wananionea kinyaa!” Sabrina akavuta pumzi. Tino alikuwa akiongea anatetemeka.

Tino aliyemshusha kituo cha polisi alijawa furaha, siye huyu waliyekutana naye hapo. “Umekula chakula cha mchana?” “Acha kujisumbua na mimi. Hata nikifa leo nani anahasara! Sina mama wala baba. Ndugu na marafiki walinitelekeza, wewe  ni shahidi. Hata nikifa, kwa kutokula nani anapata hasara? Niache tu peke yangu hata nikifa na njaa ni sawa tu na itakuwa heri kwa Lela ataweza kupata ile nyumba alee watoto wake pale.” Sabrina akawa amepata jibu lake.

Akasimama na kwenda kumimina uji kwenye bakuli kubwa, akaupasha moto palepale chumbani kwenye microwave, akaonja, akaona upo sawa. Akachukua na taulo saizi ya kati na dogo kabisa, akaenda kuvuta stuli mbele yake akakaa. “Ninachokuomba ni ufungue tu mdomo, na kumeza, mimi nitauweka huo uji mdomoni.” “Itasaidia nini wakati hata wewe unanionea shida hata kunibusu tu!” Akainama na kumbusu kwa nguvu mdomoni. Akaona hajakwepa. Akaweka bakuli pembeni, akarudi kumkalia kabisa mapajani, akamkumbatia kwa nguvu akambusu kama mara tatu mfululizo kwenye midomo kisha akaanza kumbusu shavuni mpaka masikioni. “Samahani nimechelewa kurudi Tino.” Akambusu tena mara mbili. Akambusu tena na tena. Tino ametulia.

“Naomba usikasirike Tino. Nilikuwa saluni muda wote, nikaona nikakununulie na matunda. Samahani kama umenisubiria muda mrefu. Pole.” “Kwa nini ulikuwa hupokei simu zangu.” Akili ndio ikamrudia Sabrina juu ya simu. Akaruka pale akakimbilia simu yake ndani ya pochi. Kufungua pochi, hamna simu. “Simu yenyewe hata sijui ilipo Tino! Ile simu hakuna wakunipigia mpaka mimi ndio nipige, ndio maana unaona si mpenzi sana wa simu. Ngoja nikaiangalie kwenye gari pengine niliiacha huko.” “Itasaidia nini sasa?” Akauliza, lakini safari hii akisikika ametulia. “Acha niende nikaifuate ili niwe nayo tu.” “Kwa hiyo unaniacha tena!?” Akauliza kwa kushangaa sana. “Siku nzima umeniacha Sabrina. Hujali nipo wapi! Wala nafanya nini! Umeniacha pale polisi na kunitelekeza moja kwa moja! Hivi unajua ni masaa mangapi tokea uniache?” Sabrina akabaki ameduaa.

“Hata kuwa na wasiwasi na mimi! Imekuwa ni kama uliyetua mzigo, ukaondoka moja kwa moja! Sijui wengine tumeumbiwa mkosi gani? Kwa nini imekuwa hakuna watu wanao tuhitaji na kutufikiria? Inakuwa rahisi tu kutelekezwa!  Kweli unaondoka Sabrina, unaniacha kwenye hali kama hii hujali hata ninaendeleaje! Unajua wazi nakuhitaji, na siwezi kufanya chochote bila wewe na hilo nimelirudia kwako zaidi ya mara ninazoweza kukumbuka! Leo unaniacha barabarani tu, hujali! Kama ningeanguka na kufa?” Sabrina akaumia sana.

Akajikuta machozi yakimtoka. Tino hakukosea. Ni kweli ni kama alimtelekeza. Akaumia sana moyoni na kujichukia. Kwa muda wote aliokuwa saluni hakuwaza juu ya Tino hata kidogo, akajisahau kabisa. Sabrina akajichukia kutoka moyoni, akajiambia hana tofauti na wote waliomtelekeza Tino. Akajirusha kitandani akajifunika na mto akaendelea kulia. Alilia mpaka akamsikia Tino amepanda kitandani na kulala pembeni yake.

“Nilijua umeniacha Sabrina!” “Nimekosa Tino. Nisamehe, nilipitiwa nikijua utakuwa busy na mambo ya polisi na mwanasheria wako, sikutaka kuwaingilia. Lakini unajua siwezi kukukimbia Tino.” “Nitajuaje Sabrina na leo umenisahau kabisa?”  Sabrina akazidi kuumia, akalia kwa uchungu sana. “Naomba nisamehe Tino, nimekusahau. Nimekosa.” “Basi Sabrina. Yameisha.”  Akakaa. “Naomba nikuhakikishie haitakaa ikatokea tena Tino, nisamehe. Nakuhakikishia siwezi kukutelekeza.” “Kweli Sabrina?” “Niende wapi Tino!?” “Sijui Sabrina, hebu niangalie nilivyo. Natembea nikiwa mfu!” Sabrina akazidi kuumia.

“Kwangu wewe si mfu Tino. Nakujali ndio maana nipo na wewe. Ni leo tu. Nisamehe tafadhali.” Akamsogeza kwa ule mkono wenye nguvu akarudisha busu kwa kituo. Sabrina akamkumbatia kwa nguvu huku akinyonywa midomo yake. Hakuna jinsi Sabrina angeeleza hiyo raha yake mtu akamuelewa. Alimkumbatiwa vizuri, akajaa kifuani. Wakapena mabusu zaidi ya dakika 6, Sabrina akajitoa. “Ulifanikiwa lakini?” Sabrina akauliza kwa upendo akionyesha kujali. “Nilishindwa Sabrina.” “Kwa nini tena!?” Sabrina akauliza kwa mshangao maana ni kama kila kitu kati yake na mwanasheria wake kilikuwa kikienda vizuri tu.

“Nilijua umenikimbia Sabrina. Kila kitu kikakosa maana. Nikajiambia kama ni mimi tu, ninahaja gani ya kupambana na mali zote hizo wakati najua nitakufa tu.” Sabrina hakutegemea kabisa kusikia hivyo kutoka kwa Tino, ikazidi kumuumiza. “Lakini tuliagana vizuri Tino, na tukakubaliana utanikuta hapa hotelini! Sema nilibadili staili ya nywele ndio maana ikachukua muda mrefu. Siwezi kukukimbia Tino. Naomba hilo liingie  moyoni kwako na uniamini. Najua umeshasalitiwa sana, lakini kumbuka Sabrina atasimama na wewe daima.” “Kule kutokukubali nikubusu jana nako ikawa shida, Sabrina. Nimeshinda nikijidharau kabisa. Nikajiuliza nilifikiria nini na jinsi ulivyochezea uchafu wangu wote hivyo! Unawezaje kunitizama mimi kama mwanaume!” Sabrina hakutegemea kama hayo ndiyo yalikuwa yakiendelea kichwani mwake.

“Naogopa kuchanganya mapenzi na kazi Tino! Mimi ni mfanyakazi wako tu.” “Kazi gani Sabrina? Wapi na nani umemuona anafanya aina hii ya kazi? Mbona najihisi kama huko tulishapita zamani sana!” “Mimi sikujua Tino, halafu nakuona kama bado upo katikati ya matatizo ya ndoa yako, sitaki na mimi niingilie kati.” Tino akasimama kwa hasira. “Lela anafanikiwa kunipokonya kila kitu changu hapa duniani. Hata haki yakupendwa!” Sabrina akamkimbilia.

“Naomba tuzungumze Tino, tafadhali.” “Nazungumza nini tena? Au unataka kuniambia nini wakati umeshanikataa?” “Naomba utulie Tino, bado unahasira. Naomba utulie kwanza.” “Unafikiri sijatulia mimi ni muhuni tu? Kwa taarifa yako tu Sabrina, muulize hata dada yako, sijawahi kuwa na mahusiano nje ya Lela tokea nimemuoa. Japokuwa amekuwa akinitenda vibaya, sikuwahi kutokuwa muaminifu kwake. Kiukweli hata sasa Lela si mke wangu. Wewe unajua hilo, na kila mtu anajua hilo ila unazungumza hivyo kama njia yakunikataa tu.” “Kama ningekukataa ningekubusu kwa muda mrefu hivyo Tino!? Na ninazungumzia kutulia, kukaa chini tuzungumze mimi na wewe. Tafadhali tulia Tino. Nimekosea leo, hata mimi nimeumia nahisi zaidi ya ulivyoumia wewe. Unafikiri nilikusudia kukuumiza?” “Sijui Sabrina!”

“Ukijibu hivyo unaniumiza Tino. Mpaka sasa hujasoma moyo wangu tu!? Unataka nifanye nini kukuthibitishia nakuthamini na kukujali? Leo nimekosa, nakuahidi nitajifunza kutokana na kosa la leo, sitarudia Tino. Itabidi nijifunze kutokana na wewe. Watu wote waliokuwa wakinizunguka sio watu wa mawasiliano! Hata Emma alikuwa anataka yeye ndio anipigie sio jumbe za kila wakati au simu mara kwa mara. Sijui hayo maisha ya kujuliana hali kila wakati. Sijabahatika. Ila sasa hivi kwa kuwa nimekuelewa, nitabadilika. Tafadhali naomba unisamehe Tino, na usinihukumu kwa hiki nilichofanya leo.” Tino akamsogelea.

“Nahisi nilipaniki Sabrina. Ile tu umenishusha pale nikakupigia, halafu hukupokea!” “Simu niliacha sijui kwenye gari au hapa ndani na nafikiri haina sauti. Lakini unajua nisingeacha kupokea simu zako Tino. Nakujali sana.” “Basi Sabrina. Nafikiri pia nilishapatwa na hamu na wewe. Nilikaribia kuchanganyikiwa.” Sabrina akamuhurumia. “Tino jamani!” “Nikikwambia nakuhitaji na ninaingiwa hofu bila wewe, naomba usinipuuze ukafikiri ni maneno ya kukupamba. Ni kweli naingiwa hofu.” “Basi nitajitahidi tuwe wote pamoja. Njoo ukae ule kwanza halafu tujipange upya.” Akamshika mkono mpaka pale kwenye kochi.

“Uji utakuwa umepoa Tino. Subiri nikaupashe.” “Nakutaka wewe Sabrina. Nataka kunyonya hiyo midomo yako mpaka nafsi yangu itulie. Nikalie kama ulivyonikalia mwanzoni.” “Kula kwanza Tino.” “Hapana. Akili yangu imechanganyikiwa, kukuweka hapa kifuani kwangu pekee kutanituliza.” Sabrina akarudia kumkalia miguu pembeni na pembeni kwenye mapaja ya Tino. “Niambie kama umenisamehe kwanza. Najua sikufanya vizuri. Nimejisikia vibaya, sitakusahahu tena Tino wangu. Sawa?” “Nashukuru. Amini nakuhitaji Sabrina. Kila kitu kinapoteza maana kama haupo. Halafu nahisi nilifanya haraka. Sipo tayari kutoka huko ulimwenguni. Kunatisha Sabrina!” “Nakuahidi tutakuwa wote Tino. Sitakuacha tena.” Akambusu midomoni.

Sabrina akahisi anamfungua nywele alizokuwa amezifunga zote nyuma. Taratibu huku akimbusu mpaka akafanikiwa kufungua kabisa nywele zote, akamuachia midomo na kumvuta mbele kidogo. “Umependeza Sabrina!” “Nimejichukia Tino! Na hizo nywele ndio zaidi. Naona zimeniponza.” Sabrina akaongea kwa kulalamika. “Hapana. Ni mimi ndiye nilipaniki, haikuwa mbaya hivyo. Ni kweli niliingiwa na hofu ya ajabu sana. Nikajihisi ulimwengu wote umeniangukia mimi, siwezi hata kujisaidia. Nilichofanya nikuendelea kukupigia na kukimbilia hapa ndani.” “Pole Tino, sasa ulimwambia nini yule mwanasheria?” Hapo ndio akili zikamrudia Tino.

Akamsimulia kila kitu Sabrina, akamuacha ametoa macho. “Nilikwambia ilikuwa mbaya Sabrina, umeamini sasa?” “Uwii! Itabidi hii simu niwe nabeba mpaka chooni. Tino! Tafadhali mpigie sasa hivi uzungumze naye.” “Namwambia nini?” “Anza kwa kumuomba msamaha, na umwambie upo tayari akusindikize tena. Muonyeshe bado unahitaji msaada wake.” Sabrina akasimama.

~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~

“Usiondoke basi!” “Napasha uji moto Tino! Hapo sehemu ya microwave tu. Naomba piga simu.” Akaondoka na bakuli, anafika kwenye microwave anashangaa Tino naye amefika hapo na simu yake, akapanda juu ya kiukuta kama meza ya pale jikoni, akamvuta Sabrina karibu akawa yeye amekaa, Sabrina amesimama, amempa mgongo anaangalia microwave inavyopasha uji. Akampapasa hapo ndipo akapiga simu. Sabrina akamlalia mapajani.

Max akashangaa Tino huyu siye wa asubuhi. Akawa ametulia sana na kuomba radhi. “Nahisi nilipaniki kaka, nilijua Sabrina amenikimbia.” Sabrina akashituka sana akamwangalia akiwa ametoa macho. “Sabrina ndiye aliyenitoa kwenye umauti, gizani na kuniweka mwangani. Sijawahi kutoka popote bila yeye. Sasa aliponiacha pale kituoni, nahisi niliingiwa na hofu ya ajabu. Nikijijua nimekuwa mlemavu, maisha hayaeleweki halafu na haya mambo ya Lela, nikajua ameingiwa na hofu amenikimbia. Naomba nisamehe kaka. Nilikosea.” Max mbele ya pesa, hana kipingamizi hata kidogo. Huyo Tino na Lela walimnufaisha kupita kiasi kwa hizo kesi zao za madai yasiyoisha kila kukicha. Hasira haiwezi kumtenga na pesa yao.

Akasikika akicheka. “Sasa ulimpata?” “Alirudi kaka. Unajua tuliagana kabisa kuwa anakwenda kutengeneza nywele, hata hakuwa na simu. Nilijipanikisha tu.” Tino akasikika ametulia kama mwanadamu kweli na heshima juu. “Pole sana Tino. Najua sasa hivi itakuwa ngumu kuamini tena. Lakini nipo na wewe si sababu ya pesa. Nataka kukusaidia. Nahisi na mimi nimejisikia vibaya kukuacha muda wote huo ukiteseka wakati nakumbuka ulikuwa na mimi hata kipindi kile mambo yangu yapo vibaya! Ukanisaidia ada za watoto, bila kunidai. Ukawafanya watoto wangu kama wako! Kisha nikaruhusu Lela aniingie kichwani! Ninachotaka kukuhakikishia ni kuwa, nataka kukusaidia tu, upate haki yako.” “Nakushukuru kaka. Asante.” “Lakini tunakimbizana na muda, wakati wote Lela amekuwa mbelembele, usipoangalia atatuchezea hata katika hili.” “Naomba kama anayo nafasi, turudi polisi sasa hivi baada ya kula Tino. Bado ni mapema.” Sabrina akaingilia. Max akasikia. “Sio wazo baya kabisa. Tumuwahi kabla hajatuwahi.” Wakakubaliana.

“Naomba ule kwanza Tino ndipo twende.” “Nilitaka kufanya mapenzi na wewe Sabrina. Naona kama itanituliza. Au haupo tayari? Nitaelewa tu. Najua sipo kama wanaume wengine, na kwa kuwa ulinikuta kwenye ile hali, inakuwa ngumu kujisikia ninachojisikia.” Sabrina akajua kazi atakuwa nayo. “Naelewa.” Akajilalamisha tena. “Unaelewa pia kuwa nafurahia jinsi unavyonifanyia ukinibusu? Mikono yako inakopita, na jinsi unavyonyonya midomo yangu.” Akamuona anacheka. “Kumbe unafurahia!?” “Sana tu. Na ninataka uanze kujifikiria tofauti na vile Lela alivyokuwa akikwambia muda wote ulipokuwa mgonjwa. Imekuathiri Tino. Kwa namna moja amefanikiwa kukuingia kichwani na kukuharibu akili. Anza kufungua mdomo ule wakati nakwambia.” Akafungua kweli mdomo na kuanza kumlisha.

“Lela alihakikisha anaanza kukumaliza akili, akaja kiuchumi ndipo anapanga kifo chako. Usikubali maneno yake yaliyojaa wivu, chuki dhidi yako, ufitini, na kila aina ya ubaya yakaishi ndani yako. Mimi nililijua hilo siku ya kwanza nawaona nyinyi wawili. Nimeishi na wewe nikajua wewe ni zaidi na hivyo unavyoonekana hapo sasa hivi, japo hata hivyo ulivyo sasa hivi wewe mwenyewe hujioni.” “Kwani nikoje?” Akauliza Tino.

“Zaidi ya hivyo unavyojifikiria upo Tino. Na ndivyo Lela alivyotaka ujione.” “Wewe unanionaje?” “Wewe umeona mimi naishi na nikikuchukulia wewe kama nani?” “Unataka nikwambie ukweli?” Akauliza Tino huku akicheka. “Na useme ukweli Tino, sio udanganye.” Akamuwekea tena uji mdomoni, huku wakicheka. “Najua unanijali sana. Tokea umenikuta mchafu. Hata siku ya kwanza kabisa unataka kunisafisha, umetaka ruhusa yakunifanyia kila kitu, kitu ambacho kilinivutia sana. Sio kama wale wengine waliokuwa wakiletwa na Lela. Walikuwa wakinisukuma na kuniambia maneno mabaya sana huku wakinihudumia.” “Pole Tino.” “Asante, lakini walifanya kile walichoelekezwa na Lela.” Sabrina akampa tena uji.

“Lakini wewe ukanishangaza. Uliambiwa uondoke, na usifungue kile chumba. Lakini nikashangaa ukarudi. Nikiwa sijakuongelesha chochote wala hujui kama naweza kuzungumza, ukatafuta jinsi yakuwasilina na mimi. Ukaanza kunilisha huku ukihakikisha sina maumivu wakati wote. Nilikuwa kwenye baridi Sabrina, kule kuja na kuanza kunifunika mpaka kunivalisha soksi ikawa nafuu kubwa sana. Kweli ulinitunza au unanitunza kwa heshima kubwa sana na kwa upendo wa hali ya juu na ndio maana nakwambia haupo hapa kama mfanyakazi, unafanya zaidi ya mfanyakazi.” “Naomba malizia uji.” Akamalizia uji wote.

“Kwa hiyo wewe hujioni kama mtu unayevutia? Kuwa ule uzuri wote uliisha sababu ulikuwa mgonjwa? Na kama alivyokwambia Lela, hutakaa ukarudia Tino yule wazamani. Umeamini hivyo?” “Kwa sehemu ninaamini hivyo Sabrina.” “Basi nina habari mbaya kwako Tino. Unachoamini wewe na mkeo Lela, sicho.” “Usimuite mke wangu, unataka kuninyima nini?” Sabrina akacheka sana.

“Basi nataka ujue, anayo kuaminisha ni kwa ajili yake yeye mwenyewe kujifariji huko alikokimbilia ni kwema kuliko alikokuacha.” Hapo akaanza kumgusa Tino. “Na ili kujiaminisha na kupata amani katika hilo akataka na wewe uamini hivyo na uanze kuishi hivyo ili watu wamuamini na kuona anachofanya nisahihi.” Sabrina akamfuta mdomo. “Niambie ukweli Tino, Lela atatoa sababu gani ulimwengu ukaelewa anavyozunguka mtaani na huyo mwanaume kama si kuaminisha watu wewe hufai?” Sabrina akauliza. Tino kimya. “Nilazima aaminishe watu wawe upande wake na kumuhurumia yupo katika hali ngumu, na yeye ni binadamu anahitaji mtu. Sasa na wewe ukianza kuishi hivyo kama mtu mnyonge, unajiita mgonjwa, unaishi kama mlemavu, utakuwa umemsaidia sana Lela kwenye uovu wake. Usikubali Tino. Wewe bado ni Tino yuleyule.” Tino akacheka kidogo.

“Kweli Tino. Japo sikuwahi kukuona zamani, lakini hivyo ulivyo tu unavutia kwa mwanamke yeyote anayevutiwa na wanaume weupe.” “Wewe huvutiwi?” “Najua wapo wanawake wasiopenda wanaume weupe. Nishawaona. Lakini Tino wewe bado unavutia sana. Upo bado na uwezo kifedha na unazo nguvu. Namaanisha nguvu za mwili na akili. Usiishi kama uliyefilisika na mnyonge. Kwa mara ya kwanza muonyeshe Lela wewe ndio incharge. Wewe ndio mwenye mali akakukuta nazo. Muonyeshe nyumba ni yako, ulimkaribisha. Muonyeshe kumuoa hukukosea ila yeye kukuacha ndio alikosea, mfanye ajute. Ukijifanya unajuta sasa hivi kumuoa Lela, utajirudisha nyuma na kuthibitishia watu huna maamuzi sahihi.” Tino akakunja ndita na mikono kifuani.

“Lela ni mzuri, wala si uongo. Hata kama alikuwa na madhaifu yake, onyesha ulijua angebadilika kwa mapenzi uliyompa ila yeye ndio ameshindwa kutulia kwenye ndoa nzuri na mwanaume mwenye kila kitu ambaye wanawake wengi wanaomba Mungu mwanaume kama wewe.” “Na wewe je?” “Sasa mimi niombe nini wakati nishakupata!?” Sabrina alimfanya Tino acheke sana. “Kwa hiyo ushanipata?” “Oooh yeah! Na wala sina mpango wakukuacha wala kukurudisha kwa Lela.” Tino alicheka mpaka akashuka pale juu.

 

Penzi Zito la Kwanza kati ya

Tino&Sabrina.

“Sabrina!” “Tino! Acha utani wewe! Mimi nilikuwa sipigiwi simu ya kutafutwa, leo unachananyikiwa kwa kunikosa masaa, halafu nikuache! Acha utani kabisa! Kama haitoshi, unataka mapenzi na mimi? Ni hivyo nimekuwa na siku ndefu saluni, nimeshikwa shikwa na watu tofauti tofautii naona si sawa kwako kunishika nikiwa hivi. Na...” Tino akamvamia na kumtoa ile gauni. “Tino!” “Sijali Sabrina. Nakuhitaji.” Kuja kutoa sidiria, akamuona ameduaa. Sabrina akacheka. Hata Emma hakuwahi kutosheka na hicho kifua. Ni moja ya vitu vichache alivyovipenda mwilini mwake. Alijaliwa matiti mazuri, yaliyojaa vizuri na chuchu nzuri.

“Mimi naona swala la polisi tuliarishe.” Sabrina alicheka mpaka akajifunika na sahani. “Hapo unaharibu.” Tino akampokonya zile sahani na kuanza kunyonya midomo yake mkono wake wa kushoto kifuani kwa Sabrina. “Twende kwenye kochi nikupe yote kwa pamoja.” Tino akawa anamfuata huku anavua nguo kwa haraka. “Kaa.” Sabrina akamuamuru, kwa haraka sana akakaa akiwa mtupu. Sabrina akaanza kumkalia taratibu Tino akigugumia kwa raha kama Sabrina aliyekuwa akitoa milio wakati midomo ya Tino ilipotua kwenye matiti yake.

Sabrina akagundua Tino sio mfanyaji mapenzi kwa pupa, taratibu alianza kujinyanyua na kujirudisha huku akimsikilizia Tino kila mahali. Alifurahia ufanywaji mapenzi ule. Tino naye akatulia hapo kifuani kama mtoto mwenye njaa, mwishowe akamgeuza. Wakaona kwenye kochi hapafai, wakashuka chini. Walifanya mapenzi taratibu kila mmoja akiwa amejawa hamu na mwenzie, mpaka wakamaliza.

“Wewe umepona Tino. Huna ugonjwa popote.” Tino alicheka sana, na safari hii hata sauti yake ilisikika kufurahia. “Mkono upi ndio hauna nguvu tena?” “Huu!” Tino akaonyeshea wakulia huku akicheka. “Mimi naona unakupa tu likizo kwenye kuandika, lakini kwenye mambo mengine!” “Hauna tatizo?” Akauliza Tino. “Hata kidogo.” Sabrina aliongea huku akihema kwa furaha. “Lakini Sabrina mashine yako si mchezo wewe mtoto! Sasa hivi najua kwa nini Emma anahesabu.” Sabrina alicheka mpaka akajificha uso kwake yeye mwenyewe.

“Ni nini kunipagawisha hivyo! Upo vizuri Sabrina. Zaidi ya ....” Akabaki akivuta kumbukumbu, Sabrina akimsikiliza kule alipojificha uso. “Mmmh! Nimelala na wanawake, lakini Sabrina! Wewe watofauti!” Sabrina akajisikia vizuri sana kusifiwa na mwanaume kama Tino. Huyo Tino asijue Sabrina mtoto wa Pwani. Kwao mtoto wa kike kuchezwa nilazima. Hata Sabina mwenyewe na shule yake kichwani, alichezwa. Alipovunja ungo alichezwa kimila kabisa, kwenye mji wa bibi yake, Bagamoyo. Na baada ya siku za kuwekwa ndani kuisha, walitolewa yeye na mabinti wengine wa umri mmoja waliowekwa ndani kwa sherehe za kimila kabisa, kuwa wameshakuwa wakubwa na wamepata mafunzo kama watoto wa kike.

Swala la mwanamke kumridhisha mwanamme kitandani halikuwa la kusikia juujuu, ila kuliishi kama mila na desturi ya mwanamke kwenye jamii yao. Utaalamu wa kitandani amekua tokea mtoto akiona kizazi hadi kizazi kutoka kwenye jamii ya watu wa kwao, wakiwekeza katika hilo. Jinsi ya kutunza uke na kuutumia ipasavyo wakati wa mapenzi, alijua ipasavyo kwakuwa alifundishwa na ndio mazungumzo ya watu wa kwao kama jamii nyingine walivyowekeza kwenye tamaduni zao wanazoamini zinafaa kwa watu wa kwao. Sabrina alijua kuvitumia viungo vyake, Emma mwenyewe alisalimu amri kitandani kwa Sabrina, mpaka akawa akimfuata Dodoma kama Sabrina akishindwa kwenda kwake Dar. Akaridhishwa na Sabrina ila tamaa ya muonekano wa Kasandra na roho yake mbaya vikamponza.

Hapo Tino amelala kwa kuridhishwa kwa namna yake. “Kweli nimeamini mapenzi ni sanaa! Kila mtu anao utaalamu wake. Mama nimekukubali.” Sabrina akazidi kucheka kwani alimfanyia makusudi ili kumpagawisha tu. Tino akadhani amebanwa na mdomo kumbe utundu wa Sabrina. “Nakushukuru Sabrina.” “Karibu na mimi nashukuru kwa kuwa mstaarabu kwenye mapenzi. Lakini naomba tujiandae tukakutane na yule mwanasheria. Atatusubiri sana pale kituoni.” “Mbona kama hapa ndio tumeanza!” “Kiasi Tino. Tuwe na kiasi. Usiku wote ni wetu mimi na wewe bila mwingiliano. Twende tuwahi kuja kurudi. “Naomba basi nikumbatie nipate busu la kunitoa hapa.” Sabrina akacheka na kumpandia pale alipojilaza kapetini wakaanza romance ya nguvu, Sabrina akifurahia hapo juu ya mwili wa Tino, akimpapasa nywele za kifua ambazo zilishamtoa mate tangia siku ya kwanza kuziona. Wakajisahau, mchezo wa pili wa nguvu usio na papara, Tino akauanzisha. Akamnung’unisha Sabrina vilivyo pale sakafuni mpaka hali ya uanaume ikamjaa ndani yake. Kwa mara ya pili kwake ila ya kwanza kwa Sabrina aliyekuwa amekusudia kumfurahisha yeye tu walipoanza ndipo akamfikisha kwa vishindo vyote. Tino akajisikia vizuri kwamba na yeye amemtendea haki. Wakakimbilia bafuni, kuoga haraka na kuwahi kituo cha polisi. 

Ukishika, Shikamana.

W

alimkuta Max akisubiri kwenye gari. “Sikutaka kuwasumbua.” “Nashukuru kaka.” “Acha nishuke nikutane na kiumbe aliyemudu kukuridhisha kwa kiasi hiki.” Tino na Sabrina wakaanza kucheka. “Mbona mimi nipo hivihivi tokea zamani!” Akapinga Tino. “Zamani zile hata mke wangu alikuwa akikwambia wewe mtoto mzuri sana, ila umepungukiwa tabasamu?” Walicheka, mpaka Sabrina akageuka nyuma. “Au nimeharibu? Ukute ulijisifia kwa Sabrina kuwa wewe ulikuwa na maisha ya furaha sana mpaka ulipougua?” Wawili hao wakacheka.

“Sabrina, huyu ni kaka yangu wa muda mrefu sana. Watoto wake walinizoea mpaka wakadhani ni ndugu kabisa. Anaitwa Max. Ndio mwanasheria mashuhuri sana hapa mjini.” “Acha kunipamba kwa Sabrina, halafu baadaye aje anione hovyo!” Max akapinga huku akimgeukia Sabrina.  “Hujambo Sabrina?” “Sijambo shikamoo.” Sabrina akasalimia na kumpa mkono. Max alionekana ni kaka mtumzima hata kwa Tino. “Naona mtoto mdogo lakini mambo yako makubwa! Unaweza kutuliza bahari!” Sabrina akacheka sana na aibu akimwangalia Tino huku ameshikwa mkono na Max.

Aliachia hizo nywele alizokuwa amesukwa. Hata hakuvaa hereni. Alivaa sendozi alizozinunua mchana alipokuwa saluni. Na kigauni kifupi kilichochanua kiunoni. Urefu juu ya magoti. Akaonekana vizuri, akafanania na utajiri wa Tino. Ukichanganya na uzuri wa Tino, ukatosha kumfunika Sabrina. “Nikushukuru kwa kumukoa Tino. Wengine tuliishia njiani.” “Ni Mungu kaka yangu, wala si mimi.” “Mungu anatumia watu. Wengine tulikataa, wewe ukasimama kushinda vipingamizi vyote. Kwa hiyo hizo shukurani lazima uzipokee tu, ni zako.” Akasisitiza Max. “Nashukuru. Na asante kwako pia kumsaidia Tino kimawazo. Nilikuwa nikiwasikiliza jana.” “Leo ilikuwa habari nyingine kabisa. Naona Tino bila wewe tena hakuna kinachofanyika. Badili mitindo ya nywele ambayo haitakuweka muda mrefu saluni.” Sabrina akazidi kucheka. “Nitakuwa nikienda naye mpaka saluni.” “Naona hilo ndilo la muhimu.” Tino alibaki tu akicheka huku akimtizama Sabrina.

Wakazungumza na kutaka kumsikia Tino atakachoeleza hapo polisi. Akamrekebisha kwa hili na lile mpaka Tino akaelewa. “Mimi naomba niwasubiri hapa nje, mtanik...” Akaona Tino anabadilika sura. Sabrina akabadili kwa haraka. “Au ulitaka na mimi niingie humo ndani?” “Sijui Sabrina. Lakini ni kama uliniahidi hutaniacha tena!” Sabrina akamwangalia Max, Max akabaki akiwatizama. Akamvuta Tino pembeni. “Tulizungumza nini Tino jamani!?” “Mimi sielewi tena.” “Naomba tulia halafu niangalie Tino. Najua unaelewa na unakumbuka makubaliano yetu.” “Nahisi...” “Niangalie Tino. Ukitaka tubadili tulivyokubaliana, sawa. Nitakwenda na wewe. Lakini kumbuka tulikubaliana mimi nisijihusishe na mambo yako na Lela.” Max akabaki kimya akiwasikiliza wakiongea kwa sauti ya chini.

“Ukisema hivyo ndio unanichanganya kabisa!” “Vipi tena?” Sabrina akamuuliza kwa upendo tu. “Hivyo unavyosema mambo yangu. Kama vile wewe unajitoa!” “Nipo hapa na wewe Tino. Na ukitaka tuongozane mpaka ndani, pia nitafanya hivyo. Sitakuacha. Naomba usipaniki. Tulia uniambie ni nini unataka.” Akamuona anajishika kichwani. “Tino?” “Sijui tena.” “Basi mimi naona kama ni sawa kwa kaka Max, tuongozane tu.” “Sijui Sabrina. Najihisi kama nachang...” “Naomba usikiri hivyo. Huchanganyikiwi Tino. Upo sawa kabisa.” Akamshika mkono na kumgeukia Max.

“Samahani kaka yangu. Lakini tulikubaliana haya mambo mimi nisijiingize ndio maana hata asubuhi hukunikuta hapa.” “Usiwe na wasiwasi Sabrina. Ni mimi tu ndiye nitajua kama upo hapa. Na hata kama ukionekana hapa, ni Lela mwenyewe alikuachia Tino na akakupa baraka zake uwe unamuendesha popote pale. Na nikutoe tu wasiwasi katika hili, huna jinsi ukawa rafiki wa Lela kama wewe si hela.” Sabrina akacheka kidogo. “Nakwambia ukweli. Akiamua kukuchukia, hakuna jinsi akakukosea sababu. Kama si kwa hili, basi ni kwa jingine. Na ninavyowaona nyinyi wawili, nashauri mjipange tu.” Sabrina akainama.

“Acha kumtisha bwana!” “Tino! Usimfiche Sabrina hata kidogo. Atakuja kukulaumu na kukuchukia sana baadaye. Namuona anakupenda. Tena sana tu. Si ni kweli Sabrina?” Sabrina akainama bila kujibu. “Nilijua tu. Kwa kukuangalia tu hivi, nimejua unampenda Tino. Sasa jua Lela huwa hataki kushindwa, na anazitaka pesa za Tino kwa namna yeyote ile. Kule ulikomtoa Tino kwake sio kitu kizuri. Sisi tulio mtelekeza Tino ndio wema kwake kuliko wewe. Kwa hiyo kama unamkwepa Lela, jua umechelewa. Ushamkorofisha zamani sana. Msaidie tu mwenzio aishie pazuri au umuuguze kwenye mazingira nafuu sio unauguza bila pesa! Sijui kama unanielewa?” Sabrina akatingisha kichwa kukubali.

“Nilihangaika na Lela kuhakikisha anapata pesa nikijua zitamsaidia kumtunza mwenzie, nikaishia kuambiwa amehama nyumba, analala mahotelini. Napambana walipiwe pesa za matibabu, kumbe anazitumia na mwanaume wake! Sasa maadamu wewe unatimiza lengo. Tena nakuona wewe upo tayari hata kumsaidia mwenzio hata kwenye shida, basi  ipo njia rahisi ya kuuguza. Ukiwa na pesa lakini pia mbali na Lela. Atawasumbua sana Lela kama akijua hamjajipanga. Lazima mumdhibiti haswa. Labda kama unampango wa kukimbia baada ya muda fulani.” Tino akamwangalia Sabrina aliyekuwa ameshituka kidogo baada ya kusikia hivyo.

“Au upo kwa muda tu?” Max akauliza swali la moja kwa moja. “Da Lela aliniomba nikae kwa miezi...” “Tafadhali usimzungumzie Lela.” Tino akamkatisha Sabrina kwa hasira. “Lela aliongea mengi sana, na ni wewe peke yako ulibaki na mimi mpaka sasa. Sasa kama unataka kuanza kuzungumzia na tuishi kwa makubalinao ya Lela, nafikiri umebakisha kama mwezi mmoja na siku chache sana uniache. Kwa maana nyingine haya yote tunayofanya sasa hivi hayana maana, na...” Sabrina akamshika mkono. “Tino!” “Hapana Sabrina. Ni lini utaongea moyo wako na si kile alichokwambia Lela!?” “Na hilo ni la msingi sana Sabrina. Ukikaa tu njia panda, ujue Lela atakusumbua sana. Lela ni mkorofi haswa, anataka mtu jasiri atakayeweza kusimama mbele yake akijua ni nini anafanya.” Max akaongeza nguvu hapo, akijua kwa wakati ule, pesa ya Tino hataipata bila huyo Sabrina. Sabrina akitulia, kichwa cha Tino nacho kitatulia, atapata kazi kwa Tino.

Miezi michache ametoka kumfanyia kazi Lela. Akapigania madai ya Tino. Akalipwa pesa nzuri za matibabu, Lela akamlipa cha kwake, sasa hivi anataka tena kazi kwa Tino akijua atanufaika. Lazima kumuweka sawa Sabrina ili asimpeperushie ndege wake! Akaona aongeze nguvu.

“Huyu Tino, huyu, usimuone hivi. Anaajira ya kueleweka. Analipwa pesa nyingi si kwa kuwa yupo mzuri wa sura, ni kwa kuwa anacho kipaji chakuzaliwa. Amekwenda shule, anaheshimika mpaka nje ya nchi kwa kazi yake. Lakini amechezewa na Lela, msichana ambaye sidhani hata kama alimaliza kidato cha nne. Akisimama hapa, akifungua mdomo ni kama mwanasheria mzoefu sana. Akizungumzia maswala ya pesa, utafikiri ni muhasibu mwenye CPA. Akizungumzia ugonjwa, jinsi ya kuutibu, utafikiri ni daktari aliye specialize kwenye huo ugonjwa, lakini mwisho wa yote ni pesa tu. Alianza kumsumbua Tino tokea hajaingia kwenye haya matatizo. Sisi watu wa karibu na Tino tulikuwa tukilijua hilo. Mke wangu hamtaki Lela nyumbani kwetu. Kwa kuwa anamuumiza Tino bila sababu. Akawa anasema badala ya kuwaona pale nyumbani kwetu, huyu na Lela, ni heri kama namtaka Tino, awe anafika pale peke yake sio na Lela ili wasimuumize roho. Ilikuwa inaumiza mpaka huwezi kuwatizama wakiwa pamoja.” Max akaendelea kumpanga Sabrina.

“Ni mbabe bila sababu. Anaweza akabadilisha mazingira ya amani yakawa tafarani msielewe imekuje, halafu kwa mwanaume kama Tino! Ni hivyo huwezi kumwambia mtu mwenye ndoa yake muache mwenza wake. Ninachotaka uelewe na  nilazima ujue ni nini unataka na unajiingiza kwenye kitu gani.” “Ni hivyo kwa kuwa Tino alinikatisha. Nilitaka kukwambia makubaliano tuliyokuwa nayo mwanzoni. Lakini nipo mpaka sasa, na nimemuhakikishia Tino kuwa nitakuwa naye mpaka yeye mwenyewe aseme vinginevyo.” “Sasa…..” “Subiri kwanza Tino. Naomba kuzungumza na Sabrina.” Max akamkatisha na kurudisha macho kwa Sabrina.

“Ninavyomuona Tino, maisha yameshamuathiri kwa asilimia fulani. Amejawa hofu. Samahani Tino.” Max akaomba msamaha na kuendelea. “Ninavyomwangalia na kumsikiliza, ameweza kupata nafuu ya mwili lakini kiakili Lela amefanikiwa kumuingia. Na hii sio kazi ya mara moja. Kama nilivyokwambia tokea mwanzo, Lela alikuwa kooni kwa Tino, akitawala ndoa yao kwa mabavu. Unachokiona kwa Tino sasa hivi, ni kazi ya muda mrefu tu. Na Tino amepitia maisha fulani hivi yasiyo ya mstari kama wengi wetu, tena tokea mtoto mdogo au tokea mama yake afariki. Namfahamu kwa karibu sana. Mbali na baba yake aliyemwamini akiwa anataka kufungwa kifungo cha maisha kwa kosa la kusingiziwa la ubakaji, akahangaika hapo mpaka ukamuokoa kwenye mikono ya Lela, hajawahi kutulia. Baba yake hayupo, umebaki wewe. Amejenga imani kwako. Yupo hivi unavyomuona ni kwa ajili yako. Ni kama umempa tumaini kuwa anaweza kuishi tena. Sasa kabla hamjakwenda mbali, naomba kujua msimamo wako Sabrina.” Sabrina akamwangalia Tino.

“Sijui kama umenielewa?” Max akamuuliza. “Naelewa.” Sabrina akajibu taratibu tu. “Maana kuwa njia panda. Au kuwa hapa kwa muda, hii vita hutaiweza. Na nikwambie kabisa, juhudi zako zote zitakuwa bure, utamrudisha Tino kule ulikomtoa, tena kwa jinsi ninavyomuona, utamrudisha kwa haraka sana. Mwenzio anakutegemea sana.” “Sipo na Tino kwa kubahatisha au kwa ajili ya Lela, kaka yangu. Mimi ndiye nilimchagua Tino akiwa hata hazungumzi. Nipo na Tino kwa kupenda na kumjali sana. Nilichohofia kujihusisha na haya mambo ya T...” Sabrina akakumbuka Tino hataki aseme hivyo, akabadilisha.

“Labda niseme kama ukishauri na ukasema ni sawa mimi kujihusisha, nita..” “Hunielewi Sabrina. Hilo nitalijibu nikijua msimamo wako. Kujihusisha na Tino, ni kujihusisha na kila kitu chake. Nauliza hivi kutaka uhakika kwa kuwa tumemuachia sana Lela mpaka akamuumiza Tino kupita kiasi. Japokuwa leo asubuhi huyu Tino amenitukana sana, lakini nilishajiapia kusimama na Tino, sitamuacha tena peke yake. Ndio maana nataka kujua na wewe unasimama wapi?”  “Mimi nakuahidi sitamuumiza Tino. Nitakuwa naye katika shida na raha. Nitasimama naye popote pale ambapo najua haitamdhuru yeye Tino. Nampenda Tino.” Hapo Sabrina akamalizia kwa upendo na sauti ya kujali. Max akaridhika, kwa kuwa alijua kazi mpaka hapo anayo. Shida ilikuwa Sabrina kuwa upande wa Tino kwa wakati huo, Tino atulie, apate kazi yenye pesa nzuri.

“Hilo ndilo nilitaka kulisikia kutoka kwako. Maana nakuhakikishia tu, Lela anakuja. Na safari hii atakuja kama faru aliyejeruhiwa. Kwa kujua unachotaka kama zamani. Japokuwa alikukatisha tamaa na kukukataza usimsaidie Tino, ukapambana mpaka yupo hapa, hiyo pekee itakusaidia kuendelea na kuwa na Tino kama utamuhitaji. Upweke wa Tino, ndio alitumia Lela kama silaha yake. Alijua Tino yupo peke yake. Hana mama mkwe, wala wifi wa kumkera. Kwa hiyo alifanya atakayo kwa Tino. Sasa akikutana na wewe, ukaonekana unamtaka Tino kama Tino, hapo utampunguza makali.” “Namtaka Tino.” Sabrina akaongea kwa upole na msisitizo. Max akacheka. “Haya twendeni ndani.” Akamshika mkono Tino wakaongozana mpaka ndani. Tino akiwa ametulia kabisa sio kama asubuhi.

Waliandikisha ripoti hapo polisi. Tino akajieleza vizuri kama alivyofundishwa na Max mwanasheria wake, Sabrina akiwa amemshika mkono. Akaeleza hofu ya kuuwawa na Lela pamoja na mwanaume wake. Akaomba apewe restrain order. Asimfikie wala kufika tena nyumbani kwake mpaka watakapomalizana mahakamani. Yaani mahakama itakapowaamulia baada ya talaka. Na akaomba asiwasiliane na yeye kabisa, ila kwa kupitia mwanasheria wake. Polisi mmoja wa wale waliowakuta hapo mapokezi baada ya kumsikiliza Tino kwa kina akaandikisha kila kitu. Wengine wakamuhurumia hapo, wakaongea machache, akapewa nakala yake ambayo alimkabidhi mwanasheria wake. Wakatoka.

“Nashukuru kaka Max kumsaidia Tino.” Max akacheka. “Naona ndio maana Tino anachanganyikiwa.” Wakacheka. “Kwa nini?” Sabrina akauliza huku akiendelea kucheka. “Ushikwaji huo, sidhani kama mdogo wangu aliupata kwa miaka mingi sana!” Sabrina akazidi kucheka akaangalia jinsi alivyomshika Tino, akamuachia. “Unaonekana ni mdogo, lakini umejawa hekima Sabrina. Nimekupenda tayari.” Wakazidi kucheka. “Asante.” “Sasa mapema sana kabla hajaamka kutoka usingizini, na tarehe 15 siku ya mshahara kufika, acha nimuwahi na nyaraka zake.” “Nasikia amezima simu. Ujumbe aliomuandikia Sabrina, unaonekana haujafika mpaka leo. Utampataje kaka?” Tino akatilia mashaka.

“Unafikiri ni shida kumpata Lela! Sauti yake inasikika kila mahali. Hata akinunua pochi mpya ni tangazo! Najua baa zake zote anazopenda kunywa na wenzake.” “Nasikia ni mgonjwa. Hata baa haendi.” Tino akaongeza akionyesha wasiwasi. “Tino, nenda kapumzike. Jifikirie afya yako. Mkono huo upone, uendelee na kazi. Lela sio mtu wakushindwa kupatikana. Napajua mpaka ofisini kwa mwanaume wake anayeishi naye.” Tino akashangaa. “Kila mtu anajua Tino. Jamaa mwenyewe ameajiriwa kwenye ofisi za clearing and forwading pale mjini. Kwa hiyo ujumbe na talaka yake itamfikia Lela vizuri na mapema sana. Usiwe na wasiwasi. Wewe kama utabadili namba ya simu popote ulipo, nijulishe. Lakini kila nitakachompa Lela na kuzungumza naye, na wewe nitakuwa nakwambia na kukutumia kopi zako. Kila nyaraka nitakayoandaa, nitahakikisha na wewe unayo ili tuwe sehemu moja. Ukihitajika mahakamani,…”  Akanyamaza na kumgeukia Sabrina. “Hakikisha anakuja mahakamani akiwa ametulia.” “Nitafanya hivyo.” Sabrina akakubali na tabasamu usoni.

“Nikuulize kitu kaka yangu?” Tino na Max wakamgeukia Sabrina. “Naendesha gari nikiwa na lesini iliyokwisha muda wake. Unafahamiana na mtu kule sehemu ya leseni ya magari ambaye atanisaidia kupata leseni kesho? Sitaki tuje tusimamishwe na trafiki barabarani.” “Wengi mno. Subiri sasahivi nikukabidhishe kwa mtu.” Hapo hapo akampigia mtu simu. Wakataniana kidogo, kisha akamwambia anamtuma mtu kesho asubuhi anaomba msaada wake. Kirahisi sana akakubali. Akampa Sabrina namba yake, wakaagana na kuondoka.

~~~~~~~~~~~~~~~~~~~

Sabrina katikati ya mapambano ya kumtoa Lela, asiyekubali kushindwa, pichani.

Inavyoonekana Lela na mwanaume wake wamejipanga kupata pesa ya mwisho ya Tino. Lakini yupo kimya na tetesi ya ujauzito unaomsumbua, aliopata nje ya ndoa zinaenea.

Max mcheza kotekote ilimradi pesa iingie mfukoni kwake, safari hii yupo upande wa Tino na hajawahi kushindwa kesi. Ameshampata Sabrina upande wa Tino, tumaini la kumshinda Lela lipo.

 Je, kwenye vita hiyo, nani atabaki juu nani chini?

Usikose muendelezo, Simulizi ndio inaanza.

CONVERSATION

0 Comments:

Post a Comment